[video] Rais Kikwete ahutubia Bunge la KenyaMagufuli awaambia TANESCO wajiandae kuondoka ofisini baada ya uchaguziFinally Microsoft impresses with originality, ambition - The 10 important things from today's event 1. The Lumia 950: A Windows 10 Mobile flagship
 2. The Lumia 950 XL: Microsoft's really big phone
 3. The Lumia 550: it's very cheap
 4. The Display Dock: a new attempt to turn phones into PCs
 5. The Surface Pro 4: A new volley in the tablet wars
 6. The Surface Book: an actual laptop from Microsoft
 7. FACEBOOK: now a universal Windows 10 app
 8. More surface accessories
 9. The new Microsoft Band: an answer to smartwatches
 10. HoloLens development kits will cost $3,000
Find details of the ten items above at The Verge

Microsoft’s Windows 10 hardware event in 9 minutes...Akamatwa kwa kusambaza ujumbe kuwa Jen. Mwamunyange kalishwa sumu na kufa

Kijana mmoja ambaye ni mwanafunzi kutoka taasisi moja ya Elimu ya Juu amekamatwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kutunga na kusambaza ujumbe katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa Mkuu wa Majeshi hapa nchini, Jenerali Davis Mwamunyange amelishwa chakula chenye sumu na kufariki dunia.

Taarifa hizo potofu na zisizo na ukweli wowote zilitolewa Septemba 25 mwaka huu na kukanushwa na Jeshi siku chache baadaye.

Jeshi hilo limesema kijana huyo alikiri kuhusika na utunzi wa taarifa hiyo na ingawaje alipewa fursa ya kujitokeza na kuomba msamaha kwa umma, mtuhumiwa alikaidi, ndipo hatua ya kumkamata ilipofuatia.

Serikali yamshitaki M/kiti wa Walimu aliyelalamika katika kampeni za Lowassa

Siku chache baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Chato, Lucas Michael, maarufu Masai kupanda jukwaani na kuzungumza kwenye mkutano wa kampeni za mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Edward Lowassa na kuilalamikia serikali kushindwa kuwarejesha makwao walimu waliostaafu, kulipa madai ya walimu, pamoja na kutopandisha madaraja kwa wakati, serikali imemshitaki.

Katika madai yake, Michael pia alidai kusikitishwa na kitendo cha serikali ya wilaya ya Chato kuwaandama baadhi ya walimu wanaoonekana kuunga mkono vyama vya upinzani, huku wanaokiunga mkono CCM wakionekana wako sahihi, kitendo alichodai ni ukandamizwaji wa demokrasia.

Mwenyekiti huyo wa CWT alihudhuria mkutano wa kampeni za mgombea huyo wa urais alipofika wilayani Chato Septemba 19, mwaka huu, baada ya kupokea mwaliko wa CHADEMA wilayani humo akiwa kama mdau wa elimu.

Kufuatia hatua hiyo, mwenyekiti huyo wa CWT wilaya ya Chato ameshitakiwa kwenye Tume ya Utumishi wa Umma Idara ya Utumishi wa Walimu wilayani hapa, kwa madai ya kukiuka maadili na taratibu za utumishi, kanuni namba 65 (1) na kutakiwa kujieleza.

Hati ya shitaka ambayo imesainiwa na Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Frank Angus, Septemba 22, mwaka huu, inadai kuwa mwalimu huyo alitenda kosa la kujihusisha na masuala ya kisiasa, kuchukua taarifa za kiutumishi na kuzisema kwenye mkutano wa kisiasa pamoja na kutumia nafasi yake akiwa mtumishi wa Umma kumnadi mgombea urais wakati wa kampeni.

Akizungumza na Nipashe mjini hapa jana, Michael alithibitisha kupokea hati ya shitaka hilo. Hata hivyo, alisema hakuhusika kufanya kampeni za mgombea urais kupitia CHADEMA isipokuwa alisimama kuzungumzia malalamiko ya walimu wa wilaya ya Chato.

Alidai alialikwa kuhudhuria mkutano huo wa kampeni kupitia barua ya CHADEMA yenye kumbukumbu namba CHADEMA /CHT/G/M/1/015 na anaamini alitimiza wajibu wake kwa mujibu wa katiba ya CWT.

Naye Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Chato, Mange Ludomya, alisema mwalimu huyo alialikwa kwenye mkutano huo kama mwenyekiti wa CWT, ambao ni wadau wa elimu nchini kutokana na umuhimu wake, ikizingatiwa kwamba kipaumbele cha chama hicho iwapo kitapewa ridhaa ya kuongoza nchi ni elimu.

Maaskofu waruhusu misa ya Jumapili ya Uchaguzi Mkuu ifanywe Jumamosi


BAADHI ya Majimbo ya Kanisa Katoliki nchini, yametoa ruhusa maalum kwa mapadri yakiwataka kuendesha ibada zao siku ya Jumamosi ya Oktoba 24 badala ya Jumapili mwaka huu ili kutoa nafasi kwa waamini wao kushiriki Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani kwa uhuru.

Hatua hiyo inatokana na siku ya Jumapili ambayo waamini wengi wa kanisa hilo huabudu kuangukia Oktoba 25 ambayo ni siku ya Uchaguzi Mkuu.

Habari za uhakika ambazo MTANZANIA imezipata mjini Dar es Salaam jana na kuthibitishwa na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Severin Niwemugizi, zinasema kila askofu wa jimbo ana mamlaka ya kutoa maelekezo ya aina hiyo kwa waamini wake.

Askofu Niwemugizi alisema kila askofu katika jimbo lake anawajibika kufanya hivyo, kwani ni haki ya msingi ya waamini wake kupiga kura.
“Kilitrujia siku ya bwana inaanza Jumamosi jioni, kwa msingi huo wanaweza pia kuadhimisha dominika bila tatizo lolote.
“Si utaratibu wa kawaida kwa sababu kama baraza hatujakaa, lakini kila askofu anawajibika ndani ya jimbo lake, hivyo anaweza kutoa fursa hiyo. “Hata mimi katika jimbo langu la Rulenge Ngara, nimetoa kibali hicho kwa makanisa yote… kwa wanaotaka wala siwalazimishi wote,” 
Katika hatua nyingine, askofu huyo alizungumzia mwenendo wa kampeni za uchaguzi, alisema amesikitishwa na dharau na matusi yanayotolewa na wanasiasa katika majukwa ya kampeni.
“Kumekuwa na lugha chafu, hakuna anayeona kama amefanya vibaya kwa mwenzake,…. kwa mfano unamwita mwenzako oil chafu, maana yake unamdharau muumba aliyemuumba hata kama ana upungufu.
Alisema tabia hiyo ya kutoleana lugha chafu ipo siku viongozi wa dini nao wategeukiwa.

MOSHI

Habari kutoka Jimbo Katoliki la Moshi mkoani Kilimanjaro na Mbulu mkoani Manyara, zinasema kanisa hilo limetoa ruhusa maalumu kwa waamini wa majimbo hayo kusali ibada ya Jumapili Oktoba 24, ili kutoa fursa kwa waamini hao kwenda kupiga kura.

Uamuzi huo unatokana na waraka wa Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi, Mhashamu Isaac Amani uliosambazwa katika makanisa yote ya majimbo hayo.

Waraka huo wenye kumbukumbu namba PROT Na. BSH/2657/2015- VIII/B kwenda kwa mapdre, watawa na waamini walei, uliosainiwa na Askofu Aman unawahimiza waamini wake kushiriki Uchaguzi Mkuu.
“Wakati kampeni za Uchaguzi Mkuu zikiendelea, ni muhimu wananchi wafuatilie hotuba za wagombea ili hatimaye waweze kuchagua viongozi wenye sera na sifa za kuleta maendeleo ya wananchi.
“Tunaendelea kumwomba Mungu atujalie amani wakati wa kampeni, siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi wagombea na wananchi wayapokee matokeo kwa utulivu na raha ya kudumisha umoja na amani ya kitaifa.
“Kwa kuwa siku ya uchaguzi ni Dominika, nawaletea tangazo la kuboresha mazingira ya kupiga kura. Kwa waraka huu natoa kibali maalumu kwa mapadre majimboni Mbulu, Moshi kufanya ibada ya Dominika ya 30 ya mwaka huu siku ya Jumamosi Oktoba 24.
“Lengo la kibali hiki ni kuwapa wapiga kura fursa ya kupata ibada Jumamosi jioni na Jumapili asubuhi ili wakapige kura mapema. Hata Mapadre wanatakiwa kushiriki zoezi hili la kitaifa. Kwa hiyo ratiba za misa zipangiliwe maparokiani na vigangoni kwa kuzingatia kibali kilichotolewa.
“Natumia fursa hii kuwahimiza wale wote waliojiandikisha watumie haki na wajibu wa kupiga kura ili tupate viongozi wazalendo tunaowapenda. Kura yako ni muhimu katika harakati za kuwasaka viongozi, madiwani,wabunge na rais.
“Usiachie wengine wakuchagulie viongozi wakati wewe unao wajibu wa kupiga kura. Ukishapiga kura yako rudi nyumbani ukangojee matokeo,”ilisema sehemu ya waraka huo.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mhashamu Askofu Amani ambaye pia ni msimamizi wa kitume wa Jimbo Katoliki la Mbulu alisema kutoa fursa hiyo ni kuwataka waamini wake kutumia haki ya kidemokrasia ya kupata viongozi.

Alisema ratiba za misa zote za ibada zitapangwa kwa parokia zote na vigango vyote kwa mujibu wa kibali kilichotolewa na kanisa hilo.

Uamuzi huo wa kanisa unakwenda sambamba na ushauri uliowahi kutolewa siku za nyuma na Jukwaa na Katiba Tanzania (JUKATA) pamoja na wadau wengine. Wadau hao waliwahi kupendekeza kuhusu haja ya siku ya uchaguzi

Mkuu ibadilishwe ili kutoa fursa kwa waamini ya dini ya Kikristu kutumia vizuri haki yao ya kupiga kura, ili siku ya Jumapili waitumie kwa ajili ya ibada tu.

Utaratibu huo wa siku maalum ya kupiga kura ulitumiwa na nchi ya Kenya katika uchaguzi mkuu uliopita, uliomuweka madarakani Rais Uhuru Kenyatta.

Mwl. Mndeme: Mabadiliko na Uchaguzi Mkuu 2015

MABADILIKO NA UCHAGUZI MKUU WA 2015 - SEHEMU YA KWANZA
Kwenye makala iliyotangulia (isome hapa), nilieleza namna ambavyo hoja ya MABADILIKO imekua nguzo kuu wa uchaguzi wa mwaka huu.  Kwa kuwa hoja hii imekua na uzito wa kipekee na uhitaji wa MABADILIKO umeongelewa kwa undani sana, nimeona ni vema niandike kidogo kuhusu uhalisia wake na kuoainisha kile kinachoahidiwa kama MABADILIKO katika uchaguzi huu. Nimeamua kufanya hivi kwa sababu, katika kuchangamana na kuongea na watu, na kupitia mirejesho ninayopata kwa baadhi ya makala nilizoandika, nimejihakikishia kuwa watu wengi hawana kauli inayoeleweka sana kuhusu MABADILIKO kwa muktadha wa uchaguzi wa mwaka huu. Kuna wanaotamani baadhi ya vitu vitokee na ndivyo wamevibatiza kuviita MABADILIKO, na wako ambao wamekaririshwa/wamekariri kinachoitwa MABADILIKO lakini ukweli ni kwamba hawana tafsiri halisi ya MABADILIKO husika.
http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/2820412/medRes/1081287/-/10k1ebt/-/low_assa.jpghttp://taarifa.co.tz/wp-content/uploads/2015/08/MAGUFULI-1.jpg
Nashawishika kwamba, kabla ya kujikita kwenye kuyaongelea MABADILIKO yanayohubiriwa katika uchaguzi huu, ni vema kujenga msingi kwa kuangali nyuma kidogo kuona ni nini kimekua kinasema na kuendelea kuhusu MABADILIKO. Wale wafuatiliaji wa siasa na uongozi wa nchi yetu, watakubaliana nami kwamba, dhana ya MABADILIKO, pamoja na kwamba imepata nguvu sana ndani ya miezi michache iliyopita tulipoanza mchakato ya uchaguzi, imekuwepo kwa muda mrefu. Pande mbili zenye nguvu kubwa katika uchaguzi huu (UKAWA/CHADEMA na CCM), kwa namna moja au nyingine, zimejihusisha na hoja ya MABADILIKO ndani ya miaka kama mitano iliyopita. Hivyo basi, ili niweze kuoanisha ahadi hizi za MABADILIKO katika uchaguzi huu, ni vema nianze kwa kuelezea chimbuko lake ndani ya UKAWA (CHADEMA) na CCM kwa miaka mitano ya kuelekea uchaguzi huu.
1: Hoja ya MABADILIKO ndani ya CHADEMA
Ni ukweli ulio dhahiri kwamba, hoja, madai, na kelele za MABADILIKO, zimekua ni wimbo wa vyama vya upinzani karibu vyote na kwa muda mrefu wakitaka utofauti na kile ambacho kinasimamiwa au kufanywa na CCM. Vyama hivi ambavyo Ndugu Polepole anaviita vyama vya mawazo mbadala, vimekua vikihubiri MABADILIKO, ingawa vinatofautiana katika mitizamo wa mabadiliko hayao na uzito wake. Nijikite kuyatazama MABADILIKO kama ambavyo yamekua yakitafutwa na kuhubiriwa na CHADEMA.
 • Fikra za MABADILIKO ndani a CHADEMA ndizo zilipelekea kuibuka kwa kaulimbiu maarufu ya harakati za "Vuguvugu la MABADILIKO" yaani "Movement for Change" (M4C). Kaulimbiu hii wameitumia kwa miaka kadhaa kujenga ushawishi na msukumo kwa wananchi kuwaunga mkono katika harakati zao za kisiasa ili kuleta MABADILIKO ya kiutawala na kimfumo dhidi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichoongoza nchi kwa miongo karibu minne sasa.
 • CHADEMA pamoja na vyama vingine vya upinzani kama CUF, wamekua mstari wa mbele kuitaka serikali ya CCM ianzishe mchakato wa katiba mpya kama msingi wa kuleta MABADILIKO ya kweli kama taifa. Msimamo wa vyama hivi ulijikita katika ukweli kwamba, katiba iliyoko haiwezi kuleta uwanja sawa wa ushindani wa kisiasa kwani imejengwa katika kukilinda chama kinachotawala. Hali kadhalika, ina mapungufu mengine mengi ambayo yanavinyima haki vyama vya upinzani na kuwapora wananchi madaraka ambayo ni ya lazima katika mfumo wa kidemokrasia tunaoufuata kama taifa.


 • Msingi wa uundwaji wa umoja wa UKAWA, ulijikita katika kutaka MABADILIKO ya katiba yenye kuheshimu maoni ya wananchi kama yalivyooanishwa kwenye rasimu ya pili ya katiba iliyowasilishwa bungeni na tume ya Jaji Joseph Sinde Warioba.


 • CHADEMA na wabunge wake, wamekua wakisimama kidete kuonesha mapungufu na udhaifu wa CCMna serikali yake na hivyo kujenga hoja ya kutaka mabadiliko kwa chama hicho kuondoka madarakani. Pamoja na mambo mengine, wamekua mstari wa mbele kupigia kelele maswala ya rushwa, haki za binadamu na ufisadi hata kupelekea kutambulika kama chama kinachopinga ufisadi.


Udhaifu ulijitokeza CHADEMA kuhusu hoja ya MABADILIKO

Kitu ambacho CHADEMA kama chama hawakufanikiwa sana katika harakatti operesheni na operesheni mbalimbali walizokua nazo, ni kuwasaidia wananchi kuelewa dhana ya MABADILIKO kwa maana ya itikaji na sera tofauti na zile za CCM. Matokeo yake ni kwamba, kaulimbiu ya M4C ilipata umaarufu na mwitikio mkubwa kuliko uelewa wa dhana nzima ya vuguvugu iliyobebwa na kaulimbiu hii.
 • Wakati kampeni za vuguvugu la M4C linaendelea, CHADEMA walihubiri sana habari za kuupinga ufisadi serikalini hasa kupitia matukio makubwa ya rushwa na utovu wa maadili wa viongozi. Hili lilipelekea M4C au dhana ya MABADILIKO waliyokua wanayahubiri, kuonekana kama ni vita ya ufisadi pekee na ndio mana hata katika kampeni zinazoendelea, wapinzani wao wa kisiasa wanajiuliza na kuwahoji kwa nini hawaongelei tena hoja iliyowatambulisha. Kwa mtazamo wangu, ni kosa kwa chama chenye mawazo mbadala kujikita katika eneo moja tu katika nchi ambayo ina matatizo na mapungufu karibu katika kila eneo la kiutawala na kiutendaji.


Pamoja na kwamba hili linaonekana kama ni hoja chanya kwa CHADEMA (kwamba walikua na utambulisho wa kupinga ufisadi), kwa upande wangu , naona maoni haya ni kukidhalilisha chama na kukionesha hakina hoja na sera. Huenda wanaowahoji kwa nini hawaipi nguvu sana hoja ya ofisadi kama ilivyokua awali, wanafanya hivyo kuwakebehi na sio kwamba wanawatakia mema. Tafsiri yake ni kuwaambia CHADEMA hawana itikadi na sera zinazoeleweka zaidi ya ufisadi, hivyo iwapo ufisadi ukikabiliwa ipasavyo, kitakua na lingine la kusimamia. Ninapata tafsiri kwamba wapinzani wao wa kisiasa hasa CCM na ACT, wameshtuka kuwaona wanakuja na hoja zingine ambazo huenda ni nzito, zinauzika na zenye ushawishi kwa wananchi wakati wao walitaka waendelee "kuimba wimbo wao wa ufisadi" huku wao wakihubiri kwamba wanakwenda kuumaliza ufisadi.


 • Pamoja na uchafu, ubaya na uovu wa ufisadi na mafisadi na athari zake kwa nchi, bado wananchi wanataka uhakika wa mambo yanayogusa maisha yao moja kwa moja. Wanataka uhakika wa huduma za kijamii kama usafiri, afya, elimu, maji, usalama na yanayofanana na hayo. Wanataka kuona maisha yao yanaboreka na wana kipato kinachoweza kukabiliana na gharama za maisha. Nikitumia lugha ya vijana, pamoja na kwamba naweza kusema CHADEMA kilijiuza vizuri kupitia harakati dhidi ya ufisadi, "kilibugi" kwa kutokuweka wazi na mengine ya misingi kwa lugha inayoeleweka na wananchi walio wengi. Sina hakika ni wapenzi na wanachama wangapi wa CHADEMA wanaweza kwa ujasiri kabisa kuelezea dhana ya MABADILIKO ambayo chama hiki imekua ikiyahubiri kwa muda mrefu.


 • Nina ujasiri wa kusema kwamba vuguvugu la M4C lilibeba dhana ya MABADILIKO kwa ujumla sana na viongizi wake hawakufanya bidii "kuwabebesha wananchi hoja ya MABADILIKO" kwa maana ya kuoainisha masuala ya kiitikadi na kisera (tangiable elements of change). CHADEMA ilijikita katika udhaifu wa utendaji wa serikali ya CCM kama msingi wake wa kudai MABADILIKO kuliko mambo mengine ya kisera yaliyo katika katiba na miongozo yake. Nimewasiliana na watu wengi katika kuchambua mambo haya na nilipata mshtuko mkubwa kwamba wengi wa wanaoiunga mkono CHADEMA hawajawahi hata kuona katiba yake. Kama vile haitoshi wengi hawajui falsafa na itikadi za chama chao kwa mambo muhim kama itikaji za kiuchumi, itikadi za kiuongozi wa nchi, mfumo wa serikali, na mengine kama hayo. Kwa mfano, wanachama wengi hata wasomi, hawajua kwamba slogani ya "peple's power" inatokana na imani ya CHADEMA kwamba madaraka ya uongozi ya nchi lazima yawe kwa wananchi na wananchi ndio wawe na nguvu katika maamuzi badala ya kundi la watu wachache kuamua kwa niaba ya wananchi.


 • Dhana hii ya kukihubiri chama kwa kuegemea zaidi madhaifu ya serikali ya CCM badala ya kuonesha tofauti (altenative) ambayo CHADEMA inataka kuwaletea wananchi, ilidhoofisha kukubalika kwa CHADEMA hasa miongoni mwa wasomi ambao wengi walionekana kuhamasika na harakati zao. Kulikuwepo na watu wengi ndani ya CCM ambao walichoshwa na chama chao na kutamani MABADILIKO, lakini kila walipokua wanatazama siasa za CHADEMA zilizojikita katika uanaharakati dhidi ya CCM, walipata shida. Kwa kuwa walilelewa katika Chama cha Mpainduzi kilichojikita katika kuhubiri imani, sera, itikadi na msingi yake, haikua rahisi kwao kukubali kujiunga na chama ambacho hawaelewi undani wa sera na itikadi zaidii ya kujitambulisha kwa madhaifu ya CCM. Nakumbuka kuongea na baadhi ya watu ambao walijenga hoja kwamba, iwapo CCM watapambana na kufuta kabisa ufisadi, na watendaji wa serikali wakawajibika kama inavyotegemewa; CHADEMA kitakosa hoja za kusimamia kama chama mbadala.


 • Udhaifu mwingine ambayo umeleta changamoto katika dhana ya mabadiliko ni ukweli kwamba umoja wa vyama vinavyounda UKAWA, umetegemea zaidi mawazo, maamuzi na imani kwa viongozi wa vyama husika kuliko wanachama na wananchi. Ndio mana sehemu ya matokeo ya tafiti za uchaguzi zilizofanyika karibu, zinaonesha wananchi wengi wanadhani UKAWA ni chama cha siasa na wako wanaotegemea kuona mgombea wa chama hivyo kwenye karatasi ya kupigia kura. Naelewa uharaka (urgency) ambayo viongozi wa vyama hivi walikua nayo katika kuhakikisha UKAWA inapanuka kutoka kwenye utetezi wa rasimu wa katiba na kuwa fungamano la kisiasa katika kuchukua madaraka ya kuongoza nchi. Hata hivyo, bado ilitegemewa nguvu kubwa itumike kuelimisha na kuhamasisha wananchi kuuelewa UKAWA na kujua ni MABADILIKO gani umoja huo umeyabeba tofauti na kile ambacho chama kimojakimoja kilikua kimesimamia.
Naomba ieleweke kwamba, kwa madhaifu niliyooainisha, simaanishi kuwa CHADEMA haina sera, faslafa wala itikadi zinazoeleweka: hapana. Waliosoma katiba yake wanaelewa kwamba mambo haya yako wazi kabisa na yamefafanuliwa vya kutosha. Ila nisemacho ni kwamba, kumekua na mapungufu katika uenezaji wa harakati wa chama hiki katika kuwaelewesha wananchi kuijua misingi (dogma) ya chama. Kiliwekeza katika katika madhaifu ya CCM na nguvu kidogo kwenye faslafa, itikadi, imani na sema za chama zinazoeonesha mbadala katika uongozi wa nchi. Wakati mwingine, baadhi ya viongozi wake walionekana au walijitambulisha kuw amaarufu na wenye kubeba ahadi kubwa kwa wananchi kuliko ahadi za chama. Ndio mana katika uchaguzi wa 2010, CCM na hata wananchi waliotamani mabadiliko, walikua na waliona kama vile bado chama hicho hakijafikia kiwango cha kuaminika kukabidhiwa madaraka ya kuliongoza taifa. Kwa mfano, ni watu wachache sana wanaweza kuelezea itikadi ya CHADEMA inayojitambulisha kwa mfumo wa kibepari wa uhuru wa soko lenye nidhamu katika MRENGO WA KATI (Centre Party). Nini itikadi ya mrengo huu wa kiuchumi? Wananchi na wanachama wangapi wanaweza kuulezea kama vile wanavyoelezea itikadi za Ujamaa na Kujitegemea za CCM? Je unatofauti gani na mfumo unaosimamiwa na CCM na kwa nini ni bora zaidi au mbadala?
Pia, nieleweka kwamba ninachokijenga hapa, ni mazingira ya hoja ya MABADILIKO iliyokuwepo kabla ya kuanza mchakato wa uchaguzi mkuu unaonendelea. Kwa jinsi hali ya mambo ilivyo, ni wazi kwamba watu wamepata mwamko na ufahamu zaidi juu ya imani ya vyama wanavyoviunga mkono na huenda ndio mana wanayazungumzia mabadiliko kwa namna ya kipekee.
C:\Users\User\Dropbox\155 Uandishi\uchaguzi mkuu\mabadiliko\M4C.jpg C:\Users\User\Dropbox\155 Uandishi\uchaguzi mkuu\mabadiliko\lowasa2.png


2: Hoja ya MABADILIKO ndani ya  CCM
Kwa miaka kama mitano iliyopit ,ndani ya CCM, wamekua na "harakati za kukikarabati" chama chao. Harakati hizi zilianzishwa kwa msukumo wa matukio kadhaa ya kisiasa na kiungozi ya miaka ya hivi karibuni, yaliyokifanya kionekane kinapoteza mwelekeo na mvuto mbele ya wananchi. Walifanya MABADILIKO kadhaa ya kiungozi na tume/kamati maalumu zilizopewa kazi ya kushughulikia mambo kadhaa na kukishauri chama namna ya kujikarabati na kukijenga. Miongoni mwa ushauri uliopatikana, ni pamoja na dhana ya kujivua gamba ambayo ilivuma sana na kua kaulimbiu ya moja ya makundi ndani ya chama dhidi ya wale walioonekana kama ndio magamba. Tangu Katibu Mkuu wa sasa (Abrahaman Kinana) akabidhiwe madaraka aliyonayo, amefanya kazi kubwa sana akijaribu kukipa chama sura na mwenekano mpya. Ukiachilia mambo mengine, kazi aliyoifanya Kinana kwa chama chake ni kazi iliyotukuka sana na ninadhani itakumbukwa kwenye vitabu vya historia ya chama hicho kwani amekiongoza chama chake katika kipindi kigumu cha na mtikisiko mkubwa. Ameongoza harakati za aina yake katika zoezi la ukarabati ambapo pamoja na mambo mengine, yafuatayo yalijitokeza zaidi:


 • Tuliona na kusikia kwa mara ya kwanza, uongozi wa CCM (hasa katibu mkuu), "ukiipeleka puta na kuikaba koo" serikali yake kwa maana ya kuhoji utendaji wa mawaziri na viongozi wengine kwa ujuml. Bila kumumunya maneno, waliweza kuwataja walionekana wadhaifu na wazembe na hata kuwabatiza wengine kama "viongozi mizigo".


 • Tuliona bidii kubwa ya kukirudisha chama kwa wananchi kwa vitendo. Kanali huyu mstaafu  (Kinana), alitembea nchi zima na kufika karibu kila kijiji, kukagua uhai wa chama, kukijenga, na kushirikiana na wananchi katika shughuli za ujenzi wa taifa kupitia miradi mbalimbali
 • Tulishuhudia, viongozi wa chama wakiwakemea kwa uwazi wanachama na viongozi wao walionekana kukosa maadili au kwenda kinyume na taratibu za chama hasa katika rushwa na ufisadi


 • Kwa mara ya kwanza ya kipekee, CCM kiligeuka kuwa chama cha kuwasemea wananchi shida zao na kuonesha kutoridhishwa na uendeshaji wa mambo. Waliachana na kasumba ya kukisifia chama na serikali kwa kila jambo na kubainisha madhaifu yaliyohitaji kufanyiwa kati.  


 • Ingawa kwa shingo upande, CCM ilikubali kuanzisha mchakato wa kuandaa katiba mpya. kwa kuruhusu serikali yake kuunda tume na kukusanya maoni ya wananchi na hatua zilizoendelea. Hii inaonesha ni kwa jinsi gani walisikia na kukubali nguvu ya madai ya MABADILIKO toka kwa wananchi  na ni lazima wapongezwe kwa uthubutu huo.
C:\Users\User\Dropbox\155 Uandishi\uchaguzi mkuu\mabadiliko\1.jpg C:\Users\User\Dropbox\155 Uandishi\uchaguzi mkuu\mabadiliko\2.jpg C:\Users\User\Dropbox\155 Uandishi\uchaguzi mkuu\mabadiliko\kazi tu.jpg
Udhaifu wa CCM kwenye Hoja ya MABADILIKO
Hata hivyo, dhana hii ya kukikarabati chama, haikua na sura dhahiri ya MABADILIKO kwani naweza kusema ilifanyika bila mikakati ya wazi sana huku "wakilindana na kuogopana", na hivyo kutokua na mwelekeo wa ki-MABADILIKO. Kwa mfano:


 • Wakati wala rushwa na walioitwa mafisadi walikemewa na kushambuliwa kwa maneno makali ndani ya chama, bado watu hao walikua ni watu muhim na viongozi ndani ya chama. Walikua ni wajumbe wa vikao muhimu vya maamuzi ndani ya chama na wengine ni viongozi wa serikali. Unajiuliza, ni kwa nini chama kinachotaka kujikarabati kinawalea watu kinachowashutumu kwa utovu wa maadili na wasiostahili kukumbatiwa? Unajiuliza, kwa nini hakiwapeleki mahakamani kupitia serikali wanayoongoza seriakli? Unajuliza, kwa nini hakiwafukuzi uanachama wale wachafu ili kujisafisha?


 • Wako mawaziri walilaumiwa na kushambuliwa kuwa ni mizogo, lakini tumewaona watu hao hao wakifanya kazi hiyo kwa mihula yote miwili ya uongozi wa awamu ya nne.


 • Wakati chama kiko kwenye harakati zake za kujisafisha/kujikarabati, bado serikali ya chama hicho ilijikuta ikikabiliana na shutuma na vitendo vya rushwa na kifisadi vilivyopelekea mabilioni ya fedha kupotea au hasara kubwa ya mali za umma.


 • Mara nyingi, ilionekana wazi kwamba kile chama kinachoongea kupitia Katibu mkuu wake, sio msimamo na mtizamo wa wote. Mara nyingine, kilitofautiana na kauli, mwenendo, na matendo ya viongozi wa serikali. Wakati chama kinawalaumu baadhi ya watu kuwa ni wazembe na mizigo, serikali iliendelea kuwapa nafasi nyeti za uongozi na kuwatetea kwa utendaji wao


 • Yalipoibuka maswala mazito yahusuyo shutuma za rushwa, uzembe, utovu wa maadili na mengine kwa viongozi wa serikali na watumishi wa umma, na mambo hayo kufika bungeni: tulishuhudia kamati ya wabunge wa CCM (Party Caucus), ikijipanga kwa wingi wao, kukabiliana na waliokua wanashutumu na kuwalinda waliokua wanashutumiwa kwa kigezo cha "kuficha aibu na kuogopa kukivua chama nguo"


 • Wakati chama kinajisafisha, bado serikali yake ilishindwa kudhibiti mambo yanayoendana na udaifu wa kiuongozi na utendani kama vile ujangili wa wanyama pori uliokithiri; utumiaji na na biashara madawa ya kulevya kuendelea kuwa tatizo kubwa kwa nchi yetu; usalama wa wananchi na mali zao (hasa wa ngazi chini na ya kati) kuendelea kua mdogo; na mengine kama hayo


 • Wakati chama kinajikarabati, bado repoti za taaisisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi, zimetuoneshanchi yetu kama taifa linalokiuka sana haki za binadamu na kua miongoni mwa yanayoongoza kwa matendo ya kifisadi na rushwa.


 • Pale ambapo serikali ya CCM ilikubali kwa shingo upande kukubali MABADILIKO ya katiba, bado CCM yenyewe ndio iliyoongoza kutofautina na yale yaliyoonekana ni maoni ya wananchi katika rasimu ya katiba. Tuliona jinsi ambavyo CCM ilipambana kwa njia zote kuondoa mambo ambayo "yalionekana hayatakua na maslahi" kwa chama hicho na kuongeza yale ambayo kwa namna moja au nyingine "yangeendeleza mambo waliyoyazoea na kukilinda chama zaidi".


 • Pamoja na kwamba sera ya itikadi ya CCM imejikita katika siasa za Ujamaa na Kujitegemea, chama hiki kimeshindwa kuihubiri itikadi hii kwa vitendo na kwa  muda mrefu. Serikali ya CCM, kwa sehemu kubwa imekua kinyume au kusimamia sera zisizoendana na imani yenye mizizi ya ujamaa na kujitegema. Badala ya kujitegemea kiuchumi, nchi imeendelea kujiendesha kwa kutegemea hisani ya wafadhili na misaada ya kimataifa hata katika sekta nyeti kama elimu, maji, na afya. Serikali imekua ikihubiri umuhimu wa misaada na kuitafuta kwa nguvu zote, hata kuliko mahubiri ya ni kwa namna gani twaweza kujitegemea kama taifa. Tofuati kati ya wasiona nacho wa walionacho imeendelea kuwa kubwa kadiri siku zinavyoendelea. Katika hali ya kawaida, hili lingetakiwa kuwa eneo muhim la kufanyia kazi katika mchakato wa chama kurudishwa kwenye misingi na kujisafisha.
Ndio maana kwa mtazamo wangu naona kwamba, harakati za kukikarabati chama hazikua na dhamira ya kweli na haikua ajenda ya chama katika ujumla wake. Kinyume na hapo, basi inawezekana CCM haikujiandaa kukabiliana na nguvu kinzani dhidi ya ukarabati uliyodhairia kufanya na hivyo kujikuta inakua dhaifu na kujichanganya katika mipango ya kujisafisha. Au labda huenda ilikua ni Katibu Mkuu na viongozi wengine wachache ndio waliokua na dhamira njema ya kujisafisha au kuleta MABADILIKO, lakini halikua jambo lenye tija kwa chama katika ujumla wake. Kwa minajili hii, CCM hawakua na ujasiri na wasingeweza kuita mkakati huu wa kujikarabati kama MABADILIKO,kwani kimsingi hakukua na MABADILIKO ya kwa mambo yaliyokua yanasumbua wananchi kuhusu uendeshaji na utendaji wa serikali na vyombo vyake. Kujikarabati kulifanyika sambamba na mazingira ya kuogopana, kulindana, kusemana na kula pamoja (ilipobidi), kwa lengo la kukilinda chama. Hivyo naweza kuhitimisha kwa kusema kwamba kwamba, dhana ya MABADILIKO ndani ya CCM ilikua au imekua ni ya kinadharia zaidi kuliko uhalisia.
Baada ya kutoa utangulizi huu, nirudi kwenye dhana ya MABADILIKO katika uchaguzi wa mwezi huu.
 1. Ni MABADILIKO gani ambayo CCM na UKAWA vinawaahidi wananchi?
 2. Je, kinachoitwa MABADILIKO ni mbadiliko kweli?  
 3. Je, kuna tofauti gani ya MABADILIKO yanayohubiriwa kati ya UKAWA kupitia mgombea wao Mzee Lowasa na CCM kupitia mgombea wao Dr. Magufuli?
 4. Je, ni kweli kwamba ILANI za makundi haya mawili zimebeba dhana ya MABADILIKO kwa uzito uleule tunaousikia ukihubiriwa majukwaani?
Sehemu ya pili ya sehemu itakayofuata nitajaribu kujibu maswali haya na kuoainisha tofauti ya MABADILIKO ya CCM (Dr. Magufuli) na yale ya UKAWA (Mzee Lowasa). Ninashawishika kwamba, kwa kufanya hivi naweza kuwapa mwanga zaidi (angalau wachache) wale ambao bado wanatafakari dhana ya mabadiliko wanayoyataka na hivyo kufanya maamuzi sahihi katika upigaji kura
Endelea Kunisoma

Mwalimu MM anapatikana kupitia [email protected]. Pia waweza kumsoma zaidi kupitia www.mwalimumm.blogspot.com   

Taarifa ya TBS ya makampuni yaliyositishiwa matumizi ya leseni ya ubora

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linapenda kuutaarifu umma kuwa kampuni zifuatazo zimeshindwa kukidhi matakwa ya leseni ya matumizi ya alama ya ubora ya TBS, hivyo leseni zao zimesitishwa mara moja.

Kifungu cha 13(1) cha Kanuni za Udhibiti Ubora za mwaka 2009 kinamtaka Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania anapositisha leseni ya kutumia alama ya ubora kutangaza hatua hiyo angalau gazeti moja linalosambazwa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, kwa mujibu wa kifungu cha 13(2) cha Kanuni za Udhibiti Ubora ya mwaka 2009, kampuni ambazo leseni zao za kutumia alama ya ubora zimesitishwa, zitaacha mara moja kuweka alama ya ubora ya TBS katika bidhaa zao.

Tunapenda kuuarifu umma kuwa TBS haitatoa dhamana ya ubora wa bidhaa zinazotengenezwa na kampuni hizi.

Kwa yeyote atakayebaini matumizi ya nembo ya ubora kwa kampuni tajwa hapa chini tafadhali toa taarifa TBS.

Orodha ya kampuni ambazo leseni zao za kutumia alama ya ubora zimesitishwa ni kama ifuatavyo:-

Tafadhali bonyeza linki ifuatayo hapo chini kwa maelezo zaidi:

KUSITISHWA_KWA_MATUMIZI_YA_LESENI_YA_UBORA_.pdf

TBS: Suspension of standard mark licences and tested product certificates

Tanzania Bureau of Standards (TBS) wishes to inform the general public that the following companies have failed to meet the requirements of license to use the TBS standard’s mark of quality and tested product certificates thus their licenses are hereby being suspended with effect from the date of this notice.

Regulation 13(1) of the Standards (Certification) Regulations, Government Notification No. 406 of 2009 requires the Director General upon cancellation of license to cause to be published at least in one Newspaper published or circulated in the United Republic of Tanzania.

Upon cancellation of license, companies concerned shall forthwith cease to apply the ‘TBS’ quality mark on the said product pursuant to regulation 13(2) of the same Certification Regulations.

Members of the public are hereby informed that TBS NO LONGER guarantee the quality of the products manufactured by these companies.

Whoever comes across such products in the market belonging to the listed companies below, bearing TBS mark, please notify TBS immediately.

The list of companies whose standard mark licenses have been suspended and the products in question is as follows;

Kindly click the link below for more details:

LIST_FOR_PUBLIC_NOTICE_LICENCSE_CERTIFICATE_SUSPENDED_SEPT_2015.pdf

Hatimaye Lowassa ahani msiba wa Mzee Peter Kisumo


Mgombea Urais Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA, Mh. Edward Lowassa, akisaini kitabu cha maombolezo, wakati alipofika kuhani msiba wa aliewahi kuwa mwanasiasa mkongwe nchini, marehemu Mzee Peter Kisumo, alipokwenda kuhani msiba nyumbani kwa familia ya Kisumo, Usangi, wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro, Oktoba 6, 2015.

Lowassa akiweka shada la maua katika kaburi la Mzee Kisumo.Lowassa akisalimiana na kaka wa marehemu, Mzee Daniel Mchangila. Kulia ni Mama Mdogo wa Marehemu Mzee Kisumo, Bi. Nashati Mbawa.
Picha: Othman Michuzi.

Maelezo ya Polisi ya mfumo na namna ya kulipa faini za barabarani kielektroniki

Mfumo wa ulipaji faini za papo kwa hapo kielekitroniki unafanyakazi kama ifuatavyo:
Dereva aliyetenda kosa akikamatwa na kutakiwa kulipa faini kwa njia ya kielektroniki, askari ataingiza kwenye mashine taarifa za namba ya usajili wa gari, nambari ya leseni ya dereva, eneo kosa lilipofanyika, kosa lililofanyika na kisha askari atatoa tiketi ya kielektroniki kumpa dereva aliyetenda kosa.

Tiketi hiyo pamoja na kuwa na namba ya kumbukumbu ya malipo pia itakuwa na maelekezo kwa dereva yanayosema: Unatakiwa kulipa faini ya kosa ulilotenda kupitia mitandao ya simu ya tigo pesa, M-pesa, Airtel Money, Maxi malipo au kupitia kadi yako ya benki (ATM Card za NMB na UMOJA SWITCH). Unatakiwa kulipa faini yako ndani ya siku saba. Baada ya siku saba utatozwa ziada ya 25%, baada ya siku kumi na nne na kuendelea utatozwa ziada ya 50% ya tozo la awali na itakuwa ikiongezeka kadiri unavyochelewa kulipa. Kwa wale watakaokamatwa wakati wa oparesheni watafikishwa mahakamani ambapo mbali na kulipa malimbikizo ya tozo watatozwa faini ya TZS 50,000/= au kifungo cha miezi miwili jela.

Ili kulipia kwa njia ya mitandao ya simu namba maalum ya Polisi (USSD Code) itakayotumika ni *152*75#. Namba hii pamoja na kutumika katika kulipia tozo pia unaweza kuangalia iwapo gari lako linadaiwa tozo la notification lililolimbikizwa.

Baada ya kutolewa tiketi hiyo dereva husika atatakiwa kulipa faini yake kwa njia hizo zilizotajwa kisha kuiwasiliha kwa askari mwenye mashine namba ya kumbukumbu ya malipo aliyoipata kupitia mtandao husika. Namba hiyo ya kumbukumbu itaingizwa kwenye mashine ya kutolea tiketi ambapo itatolewa risiti ya malipo kisha kukabidhiwa kwa dereva husika.

Ieleweke kwamba, ulipaji huu wa tozo kielektroniki hauna tofauti na ule unaotumika katika kulipia umeme wa LUKU au ada za Magari zinazotozwa kwa njia ya mtandao na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Ili kurahisisha zoezi hili la ulipaji faini kwa njia ya kielektroniki, madereva watatakiwa kutembea na leseni zao halisi za udereva vinginevyo watalazimika kupelekwa vituoni kwa ajili ya kupata taarifa zao za leseni kutoka katika computer za mfumo wa leseni za udereva jambo ambalo linaweza kuwapotezea muda.

Aidha ieleweke kwamba dereva anapoandikiwa faini ya kielekroniki akichelewa kulipa katika muda aliopewa, Jeshi la Polisi litakuwa likiendesha oparesheni mara kwa mara kwa kuyamulika magari yote yanayodaiwa faini kwa kutumia mtambo maalum wa kutambua namba za usajili wa magari yanayodaiwa (Automatic Number Plate Recognition System). Watakaokamatwa katika oparesheni hizi kwa kukwepa kulipa faini, mbali na kutakiwa kulipa faini aliyolimbikiza awali pia atafikishwa mahakamani kwa mujibu wa sharia.

ENDESHA SALAMA - OKOA MAISHA.

Imetolewa na:

MOHAMMED R.MPINGA – DCP,
KAMANDA WA POLISI,
KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI (T)

Wanavijiji 4 Hanang' wapokea hati za umiliki wa kimila wa ardhiWenyekiti wa vijiji vinne vya wilaya ya Hanang’ wamepokea hati za hakimiliki za kimila za ardhi ya vijiji vyao baada ya kuwa vimepimwa na wao kupewa mafunzo ya matumizi bora ya ardhi kwa ufadhili uliotolewa na shirika la Oxfam kupitia shirika la Ujamaa Community Resource Team - UCRT.

Vijiji hivyo vya Mureru, Ming'enyi, Dirma na Gehando vimekabidhiwa hati hizo na katibu tawala wa Wilaya ya Hanang’ John Gabriel aliyemuwakilisha mkuu wa wilaya hiyo katika hafla fupi iliyofanyika katika kijiji cha Mureru na kuhudhuriwa na wakazi zaidi ya 100 kutoka katika vijiji hivyo vinne.

Akiongea kwa niaba ya wenyeviti wa vijiji hivyo vinne, Mbisha Gicharoda ambaye ni mwenyekiti wa kijiji cha Ming’enyi aliyashukuru mashirika ya Oxfam na UCRT kwa kuwapatia elimu ya matumizi bora ya ardhi na kuwasaidia kupata hati za hakimiliki za ardhi ya vijiji. "Sisi kama wafugaji tulikua hatujui thamani ya ardhi yetu, sasa tumeamka na kujua haki zetu na manufaa ya kuwa na cheti cha umiliki wa ardhi", aliongezea.

Aidha mwenyekiti huyo alisema vijiji vyao kupata hati za hakimiliki za ardhi itawasaidia kuwa na eneo la pamoja la malisho na itawasaidia kuwa na nguvu zaidi ya kuilinda ardhi yao na kuisimamia vyema hali ambayo itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi.

Katika hatua nyingine, afisa ardhi wa wilaya ya Hanang' Bi Eveline Mirai aliyashukuru mashirika ya Oxfam na UCRT kwa kuwasaidia wakina mama wajane nao kupata hati za hakimiliki za maeneo yao iliyoenda sambamba na kusaidia vijiji hivyo vinne kupata hati za vijiji.

Eveline alitoa wito kwa wananchi kuheshimu mipaka inayowekwa kisheria kwa sababu mipaka hiyo inawekwa kwa gharama na wananchi wenyewe wanakuwa wameikubali. “Mtakapoheshimu mipaka, hatutakua na migogoro ya ardhi” na akawataka wananchi wenye maeneo yao kuhakikisha wanapata hati za hakimiliki za maeneo yao ili wayamiliki kisheria.

Naye meneja wa program ya ufugaji kutoka Oxfam Laurent Wambura aliwapongeza wakazi wa vijiji hivyo vinne pamoja na wananchi mmoja mmoja ambao nao walipokea hati zao siku hiyo. "Ukilinda maeneo ya wafugaji maana yake ni kwamba umewahakikishia maisha yao, tunapenda kuona haki za wafugaji zinapatikana" aliongezea.

Wambura aliishukuru serikali hususani Halmashauri ya wilaya ya Hanang’ kwa ushirikiano mkubwa ambao wameutoa kufanikisha zoezi hili na akatumia fursa hiyo kutoa wito kwa serikali kushirikisha mashirika na wadau mbalimbali wa maendeleo wakati wa ugawaji wa maeneo ya ardhi za vijiji kwani wanapogawa vijiji wakati mchakato wa upimaji unaendelea ni hasara kwa mashirika hayo kwani aidha yanalazimika kuanza kazi upya au kushindwa kwa sababu tayari fedha zinakuwa zimetumika na tatizo kwa wananchi linakuwa halijatatuliwa.

Naye Makko Sinandei Mratibu wa Miradi wa shirika la UCRT alisema wamekutana na changamoto za migogoro ya mipaka katika vijiji ambayo inazuia kushindwa kupima mipaka katika vijiji husika.

Changamoto nyingine ni pamoja na udhaifu katika uongozi wa serikali ya vijiji ambazo huchelewesha mipango lakini pia kuchelewa kupata ripoti ya matumizi ya ardhi kutoka wizarani nayo ni changamoto.

Naye Mgeni rasmi wa hafla hizo katibu tawala wa Wilaya ya Hanang’ John Gabriel aliyemuwakilisha mkuu wa wilaya hiyo, alipozungumza kabla ya kukabidhi rasmi vyeti hivyo alizitaja faida za kumiliki ardhi kisheria kuwa ni pamoja na ardhi ile huwezi kupokonywa na mtu kirahisi, utajua mipaka ya eneo lako ambayo huwezi kuingiliwa na mtu na vilevile inaweza kuwa rasilimali baadaye ukapata fedha kukuwezesha kufanya vitu vingine zaidi.

Akitolea mfano, John alisema "Mara nyingi wakina mama huwa wanakosa haki yao pale mume anapofariki, huwa ananyanganywa mali yote ikiwa ni pamoja na ardhi wakati anaachiwa watoto awatunze, lakini wanapokuwa na hati za hakimiliki hakuna mtu anayeweza kuwapokonya kirahisi."


Mzee wa heshima akielezea historia ya umiliki wa ardhi miaka ya nyuma ukilinganisha na sasa.Wanakijiji wakifuatilia tukio la makabidhiano ya hati za hakimiliki za kimila za vijiji vya Mureru, Ming'enyi, Dirma na Gehando vilivyopo wilayani Hanang’.Makko Sinandei Mratibu wa Miradi wa shirika la UCRT alisema wamekutana na changamoto za migogoro ya mipaka katika vijiji ambayo inazuia kushindwa kupima mipaka katika vijiji husikaBaadhi ya akina mama wa Kijiji hicho wakifuatilia tukioEveline Mirai, afisa ardhi wa wilaya ya Hanang' alitoa wito kwa wananchi kuheshimu mipaka inayowekwa kisheria kwa sababu mipaka hiyo inawekwa kwa gharama na wananchi wenyewe wanakuwa wameikubali.Laurent Wambura Meneja wa program ya ufugaji kutoka Oxfam aliwapongeza wakazi wa vijiji hivyo vinne pamoja na wananchi mmoja mmoja ambao nao walipokea hati zao siku hiyo.Mkutano ukiwa unaendelea huku wanakijiji wakifuatiliaMmoja wa wanakijiji akiongea wakati wa Shughuli hiyo ya kukabidhi hatiMgeni rasmi wa hafla hizo katibu tawala wa Wilaya ya Hanang’ John Gabriel akizungumza kabla ya kukabidhi rasmi vyeti.


Mwenyekiti wa kijiji cha Mreru James Gejaru akipokea hati ya hakimiliki ya ardhi ya kimila ya kijiji chake.Kaimu Mwenyekiti wa kijiji cha Dirma Agustino Majawa akipokea hati ya hakimiliki ya ardhi ya kimila ya kijiji chakeMwanakijiji akipokea hati ya hakimiliki ya ardhi yakeMwanakijiji akipokea hati ya hakimiliki ya ardhi yake

Wananchi na viongozi wa Serikali ya kijiji wakipitia kwa makini hati za hakimiliki za kimila za ardhi.

Sherehe zilipambwa na ngoma ya wa-Barbaig