Kingunge katika mkutano wa UKAWA Arusha


In pictures: Kenya - Tanzania Business Forum, October 6, 2015


Executive Director of Tanzania Investment Centre Ms. Juliet Kairuki welcomes the President of Republic of Kenya H.E. Uhuru Kenyatta to the Forum

TANESCO yazima mtambo, Simbachawene aomba radhi; Rais Kikwete awasili Msumbiji kuaga

Taarifa hizo na nyinginezo zinasikika katika pleya iliyopachikwa hapo chini.[video] Mechi nzima ya soka kati ya Tanzania na Malawi
[video] Waelekezana jinsi ya kukunja karatasi ya kura ili ya CHADEMA isiangukie CCMPhD and MSc Partial scholarships

Background 

Tanzania Livestock Research Institute (TALIRI) in collaboration with Sokoine University of Agriculture (SUA) is implementing a project funded by the Bill and Melinda Gates Foundation. The project “African Chicken Genetic Gain” (ACGG) intends to test genetically improved and adapted chickens strains both on-station and in five Tanzania agro-ecological zones. 

The project will work to achieve all of the following: 

Data-driven and culturally relevant understanding of the types of chickens poor farmers, especially women prefers 
  • A productive multi-country network of public-private partnerships for long-term chicken genetic improvement that employs modern tools to drive accelerated genetic gains and to deliver more productive, farmer-preferred breeds 
  • Smallholders access to their preferred more productive breeds 
  • Evidence that adoption of the improved chicken genotypes indeed leads to significantly increased production, productivity, income, and household consumption of animal-source foods among smallholders 
  • Evidence of increased empowerment of women smallholder farmers in chicken value chains 
Within this project, exciting PhD and MSc positions are available for Tanzania nationals at Sokoine University of Agriculture. The candidate should be registered at Sokoine University of Agriculture in Morogoro (http://www.suanet.ac.tz/). 

Required competences 
  • Master a degree in socio or natural sciences and honor degree in similar disciplines for PhD and MSc respectively 
  • Candidates must satisfy SUA admission requirements for MSc or PhD studies. 
  • Candidates must have identified a supervisory Professor (for PhD) who must have agreed to the research proposal written by the applicant.  Excellent skills in oral and written communications (English) 
  • Great interest in working with an interdisciplinary and international team 
  • Willingness to travel and work in the field for extended periods 
What the research project offers: 

As part of its human capacity building component, the project is offering up to ten (10) MSc and seven (5) PhD scholarships at Sokoine university for a period of 4 years (2016-2019). Female candidates are highly encouraged to apply. 

Note that scholarships will only support research costs (on station, field expenses and travel allowances). The prospective candidate is expected to seek for additional funding from other sources to cover for the university fee, tuition fees, travel costs, stipend and insurance. 

Formal inquiries should be directed to Dr. Mbaga S.H : Sokoine University of Agriculture: Mobile +255 784 521 628: E-mail; [email protected] yahoo.com; [email protected] 

For further information about the project visit: www.africacgg.net

Mwl. Kissima - Elimu inayozingatia uwezo: Maana na misingi yake mikuu

Matumizi ya TEHAMA ni moja ya njenzo muhimu ya kufanikisha Elimu inayozingatia uwezo mashuleni. Kupitia TEHAMA, wanafunzi wanaweza kujisomea popote na kwa wakati wao huku wakishirikiana na wenzao popote pale walipo. Picha kutoka HakiElimu
Kama nilivyotangulia kuandika katika makala iliyotangualia, ni takribani miaka kumi na ushei tangu elimu inayozingatia uwezo ilipoanza kutumika rasmi nchini Tanzania. Katika kipindi hiki, hakujakuwa na mafanikio ya kuridhisha sana katika ngazi zote za elimu.

Wanafunzi wengi wanamaliza elimu ya msingi bila kujua kusoma wala kuandika, wanafunzi wengi wanamaliza shule za sekondari wakiwa wamepata madara yasiyoridhisha. Vile vile, vijana wa vyuo vikuu wanamaliza vyuo bila kuwa na stadi stahiki za kukabiliana na changamoto za kukosekana kwa ajira n.k.

Elimu inayozingatia uwezo ilitazamiwa kuwa ingeweza kukabiliana vyema na changamoto hizi za kufeli kwa wanafunzi pamoja na suala la ajira hususani kwa vijana wanaomaliza vyuo vikuu. Lakini, swali la kujiuliza ni kuwa, mfumo huu wa elimu kwa takribani miaka kumi ya uwepo wake, umetendewa haki au tuishie kusema kuwa siyo muafaka kwa mazingira yetu? Walimu wanaufahamu wa kutosha wa elimu hii? Je, ni kweli fikra za walimu na wanafunzi katika ufundishaji na ujifunzaji zinaongozwa na misingi ya mfumo huu?

Tafiti mbalimbali zilizoangalia matumizi sahihi ya elimu inayozingatia uwezo zinaonesha kuwa mfumo huu bado haujatumika ipasavyo mashuleni na hata vyuoni. Mambo kadhaa yameoneshwa kuwa yanahitajika kufanyiwa kazi. Suala la kwanza ni elimu kuhusu mfumo huu wa ufundishaji na ujifunzaji. Suala la pili ni uboreshaji wa mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji. Lengo la Makala haya ni kujaribu kutatua changamoto ya kwanza, hii ya ufahamu kuhusu elimu inayozingatia uwezo. Nitajadili kuhusu maana pana ya elimu hii na misingi yake mikuu mitatu.

Elimu inayozingatia Uwezo (Competency Based Education) ni nini?

Elimu Inayozingatia Uwezo ni mfumo wa elimu usiozingatia muda ambao mwanafunzi anapaswa kuutumia kujifunza kama kigezo cha kuwa amehitimu masomo bali hujikita kwenye maendeleo ya mwanafunzi kitaaluma kwa kuangalia kama mwanafunzi husika amefikia malengo ya ujifunzaji yaliyokusudiwa au bado hajayafikia.

Hii ina maana kwamba, muda siyo kigezo cha kumfanya mwanafunzi ahame ngazi moja ya elimu kwenda nyingine au kuhama mada moja kwenda nyingine. Kigezo kikubwa ni kama mwanafunzi amefikia lengo la kujifunza lililokusudiwa. Kama bado, ataendelea kujifunza hadi atakapofanikiwa.

Kwa mfano, wanafunzi wanaojifunza kusoma na kuandika darasa la kwanza, hawataondoka darasa hilo hadi watakapoweza kusoma na kuandika, hata wakijifunza kwa zaidi ya mwaka mmoja. Wale wanaoweza kusoma na kuandika, wataendelea na ngazi nyingine, hata kama mwaka haujaisha. Huu ndio mfumo wa elimu inayozingatia uwezo kuliko umri au muda alioutumia mwanafunzi kujifunza.

Bahati mbaya, walimu wengi mbali na kuwa dhana hii bado ni ngeni kwao, lakini pia, ni dhahiri kuwa, kwa mfumo maarufu wa kusoma kwa kuzingatia muda, utekelezaji wa mfumo huu bado una changamoto kubwa ya kuweza kutekelezwa ipasavyo hapa Tanzania.

Mfumo huu wa elimu una misingi mikuu mitatu. Msingi wa kwanza ni kuwa, mwanafunzi ndiye kiini cha ujifunzaji.

Katika msingi huu, ujifunzaji unamlenga mwanafunzi mmoja mmoja (learner-centric). Mwanafunzi anapewa fursa ya kujifunza kwa wakati wake, popote alipo na wakati huo akishirikiana na wenzake kwenye kufikia malengo yake ya ujifunzaji. Mwanafunzi mmoja akifikia malengo yake ya ujifunzaji, haimaanishi kuwa ni lazima kwa wakati huo, wanafunzi wengine wanapaswa pia wawe wamefikia malengo ya ujifunzaji yaliyokusudiwa. Kila mwanafunzi hujifunza kwa wakati wake kulingana na uwezo wake.

Msingi wa pili wa elimu inayozingatia Uwezo ni ujifunzaji unaozingatia matokeo.

Hii ni aina ya ujifunzaji ambayo hujikita zaidi kwenye kuhakikisha mwanafunzi amefanikiwa kupata kile kilichokusudiwa kwenye kujifunza. Siyo kuwa mwanafunzi ameelewa kwa kiasi gani, bali ameelewa au hajaelewa, amefikia lengo au hajafikia lengo. Mwanafunzi hataruhusiwa kuendelea na ngazi nyingine hadi pale kutakapokuwa na ushahidi usio wa mashaka kuwa, alichopaswa kujifunza amekielewa kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa.

Kwa hiyo, katika mfumo huu, jambo la kwanza kabisa linaloshauriwa ni kuhakikisha malengo mahsusi ya ujifunzaji yanaainishwa kwa ufahasaha na kwa umakini. Pia, kuhakikisha kuwa kuna vigezo madhubuti vya kuonesha kama mwanafunzi amefikia malengo au bado hajayafikia. Hii ni pamoja na kuwa na njia muafaka za upimaji na utoaji wa tathmini ya ufikiwaji wa malengo yaliyokusudiwa kwa wanafunzi.

Msingi wa tatu wa elimu inayozingatia uwezo ni ujifunzaji unaozingatia mahitaji maalum ya mwanafunzi.

Misingi huu una maana kuwa, kila mwanafunzi ana mahitaji yake ya msingi ili kujifunza kwa tija. Wanafunzi wanatofautiana mitazamo, uwezo wa kiakili, uwezo wa wazazi kifedha na hata tamaduni. Kwa hiyo, mazingira ya ujifunzaji ya mwanafunzi mmoja mmoja ni lazima yaboreshwe na kubadilishwa ili yaendane na mahitaji ya mwanafunzi husika (customized learning). Nyezo za kujifunzia, mbinu na mazingira yanapaswa kuendana na matakwa ya mwanafunzi mwenyewe. Hata kile anachopaswa kukisoma, kinapaswa kiendane na matarajio, malengo na machaguo ya mwanafunzi mwenyewe.

Ukweli ni kuwa, misingi hii ya elimu inayozingatia uwezo bado ni migumu sana kuitekeleza katika mazingira ya Tanzania. Angalao msingi mmoja tu wa mwanafunzi kuwa kiini cha ujifunzaji ndio unaotekelezwa. Hata hivyo, ni kwa kiasi kidogo sana.

Ili kufikia vyema malengo ya kumfanya mwanafunzi kuwa kiini cha ujifunzaji wake, moja ya nyenzo muhimu sana ni matumizi ya TEHAMA kwenye ufundishaji na ujifunzaji. Tanzania bado tupo nyuma sana. Vitabu havitoshelezi, shule nyingi hazina miundombinu rafiki kama ya umeme na kadhalika. Hali hii bado inapelekea wanafunzi kutumia fursa chache zinazopatikana mahali Fulani tu kuhakikisha wanajifunza, muda wa kuhitimu ukifika, wote watahitimu, walioshindwa kufika malengo yao na wale waliofikia malengo yao ya kujifunza. Na hapa, dahana ya usawa katika kujifunza inakuwa imepotea.

Hata hivyo, hadi sasa, kuna juhudi kubwa nchini Tanzania zimeshafanyika na zinazoendelea kufanyika kuhakikisha wanafunzi wanafikiwa walipo katika kupata elimu kupitia TEHAMA. Baadhi ya makampuni binafsi na taasisi za serikali kama vile Ubongo Kids, Edmodo (Chuo Kiuu cha Dodoma), elimu popote (Uhuru One) na wengine wengi wameshafanya kazi nzuri ya kuhakikisha elimu inapatika popote alipo anayependa kujifunza.

Albert Kissima
via Mwangaza blog

Waishusha bendera ya CHADEMA Moshi Mjini mchana kweupe pe!


"Wazee" CHADEMA wazungumzia uamuzi wa Mzee Kingunge


Rais Kikwete asherehekea kutimiza miaka 65 ya kuzaliwaKeki iliyoandaliwa kwa ajili ya sherehe za miaka 65 ya kuzaliwa kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete na miaka 55 ya kuzaliwa mdogo wake Yusufu Mrisho Kikwete jana jioni jijini Dar es salaam. Rais Kikwete na mdogo wake walisherehekea siku zao za kuzaliwa kwa kukata na kula keki na wajukuu wao na wa jamaa, ndugu na marafiki waliowaalikwa kwenye sherehe hii fupi iliyojaa furaha na bashasha.

Taarifa ya NIPASHE kuhusu "Siri ya mgao wa umeme"


Wakati watu mbalimbali wakiwamo wanasiasa wakilishutumu Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kutokana na hali mbaya ya kukatika ovyo kwa umeme, imebainika kuwa chanzo cha tatizo hilo ni uzalishaji duni wa nishati hiyo katika mabwawa na vyanzo vingine vyote vinavyotegemewa na shirika hilo.

Kadhalika, imeelezwa kuwa maamuzi mbalimbali ya kisiasa ndiyo yanayochangia kwa kiasi kikubwa kuwapo kwa mgawo wa umeme na kusababisha kero kwa watumiaji wake huku pia shughuli za kiuchumi zikiathiriwa kwa kiasi kikubwa.

Nipashe inatambua kuwa kabla ya kuwapo kwa mitambo mipya ya kuzalisha umeme itokanayo na utekelezaji wa miradi mbalimbali, Taifa lilikuwa likitegemea vyanzo vikuu vitatu vya nishati hiyo, ambavyo kwa ujumla wake vilikuwa na uwezo wa kuzalisha Megawati 1,226. Vyanzo hivyo vitatu ni umeme utokanao na maji uliokuwa ukichangia asilimia 45.8 kwa kutoa Megawati 561; Megawati 435, sawa na asilimia 35.9 kutoka umeme wa gesi na chanzo kingine ni cha mafuta, chenye Megawati 230 (asilimia 18.8) ya umeme wote unaozalishwa nchini.

Katika taarifa yake kwa umma ambayo Nipashe inayo nakala yake, Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco inaeleza kwa kina juu ya hali halisi ya upatikanaji wa umeme nchini, ikisema kuwa inafanya hivyo kwa nia ya kuondoa minong’ono, uzushi na kuwapo kwa taarifa nyingi za kubuni, hasa kwenye mitandao ya kijamii.

Taarifa hiyo inafichua ukweli kuwa kwa ujumla, uzalishaji wa nishati hiyo katika mabwawa yote nchini ni wa kiwango cha chini ya asilimia 20, huku hali ikiwa mbaya zaidi katika Bwawa la Mtera ambalo hivi sasa halizalishi kabisa. Kadhalika, hali siyo nzuri katika vyanzo vingine vya kuzalisha umeme vya gesi na mafuta.

UMEME WA MAJI

Inaelezwa kuwa hivi sasa, mabwawa karibu yote yanayotegemewa kuzalisha umeme wa maji yamekuwa hayazalishi ipasavyo kwa sababu ya kukosekana kwa maji na kwamba, baadhi ya mabwawa hayo hivi sasa yanaelekea kukauka.

Kwa ujumla wake, taarifa hiyo inaonyesha kuwa kiwango cha juu cha uzalishaji wa umeme kinachotarajiwa kutokana na mabwawa sita ya Mtera, Kidatu, Pangani, Nyumba ya Mungu, Hale na Kihansi ni Megawati 561.

Hata hivyo, hadi kufikia Oktoba 4, mwaka huu, uzalishaji wa umeme katika mabwawa hayo yote ulikuwa ni Megawati 105 (asilimia 18.7) ya kiwango kinachotarajiwa.

“Kwa lugha sahihi, uzalishaji umeme katika mabwawa ya maji umeshuka kwa 81.3%,” inasema sehemu ya taarifa hiyo ya Mkurugenzi wa Tanesco.

Taarifa inafafanua kwa kina hali ya uzalishaji katika kila bwawa, ikieleza kuwa Mtera lenye uwezo wa kuzalisha Megawati 80, hivi sasa halizalishi kabisa kutokana na maji yake kupungua hadi kiwango cha mwisho kinachotakiwa kuzalisha nishati hiyo.

Bwawa la Kidatu linaloongoza kwa kuzalisha umeme mwingi kulinganisha na mengine wa Megawati 204, hivi sasa limepungukiwa maji kiasi cha kuzalisha Megawati 27 tu (asilimia 13.2) ya uwezo wake wa juu.

Katika Bwawa la Kihansi lenye uwezo wa juu wa kuzalisha Megawati 180, uzalishaji wake hivi sasa umeshuka hadi Megawati 51.5 (asilimia 28.6) tu ya uwezo wake.

Upungufu wa maji umelikumba pia Bwawa la Nyumba ya Mungu lenye uwezo wa juu wa kuzalisha Megawati 8, lakini bado linazalisha Megawati 5.5 tu (asilimia 68.8) ya uwezo wake wa juu; Bwawa la Hale lenye uwezo wa kuzalisha Megawati 21 hivi sasa linazalisha Megawati 4 (asilimia 19) na maporomoko ya maji ya Pangani (New Pangani Falls) yenye uwezo wa kuzalisha Megawati 68, yameathiriwa na kupungua kwa kiwango cha maji hadi kuzalisha Megawati 17 tu (asilimia 25).

UMEME WA GESI

Baada ya kuporomoka kwa kiwaango cha uzalishaji wa umeme utokanao na chanzo cha maji, ilitarajiwa kuwa vyanzo vingine kama uzalishaji wa nishati hiyo unaotegemea gesi kuokoa jahazi.

Hata hivyo, taarifa inafichua kuwa hadi sasa, Tanesco inashindwa kupata ahueni inayotarajiwa kutoka katika chanzo hiki kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni hatua ya wazalishaji wa gesi ya Songosongo inayotoa umeme huo, kampuni ya Pan Africa, kushindwa kutoa kiwango kinachotakiwa cha Megawati 340 kilichokuwa kikizalishwa awali na sasa kuzalisha Megawati 260 tu (asilimia 76.5).

Tanesco wanaeleza katika taarifa yao kuwa hivi sasa, wazalishaji hao wa umeme wa gesi (Pan Africa), wamewaambia kuwa wanaboresha visima vyao na kazi hiyo ikikamilika uzalishaji utaongezeka.

“Japo ukarabati huo utatuhakikishia gesi zaidi baadaye, lakini wakati huu wa matengenezo panakuwa na uhaba wa gesi kutoka Songosongo,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

UMEME WA MAFUTA

Taarifa ya Tanesco inafichua vilevile ukweli mchungu kuwa uzalishaji wa umeme kwa mitambo ya mafuta umeshuka pia, kutoka kiasi cha Megawati 230 kilichokuwa kikipatikana awali hadi kufikia Megawati 190 (asilimia 82.6). Hata hivyo, haielezwi ni kwa nini uzalishaji wa umeme wa mafuta umeshuka kwa kiwango hicho.

UZALISHAJI BOMBA JIPYA LA GESI

Inaelezwa katika tarifa ya Tanesco kuwa zipo jitihada kadhaa zinazofanywa kuhakikisha kuwa bomba jipya la gesi lililowashwa linazalisha umeme kwa kiwango kinachotarajiwa. Inaelezwa kuwa hivi sasa mitambo ya kuzalisha umeme kwa gesi ya bomba jipya iliyowashwa ni Megawati 90 na mwingine wa Megawati 35.

Taarifa inafafanua zaidi kuwa mitambo mingine inayotarajiwa kuongeza uzalishaji wa umeme ndani ya wiki moja hadi mbili ni Symbion (Megawati 20), Ubungo II (Megawati 35), Songas (Megawati 20) na Kinyerezi Megawati 70.

Inaelezwa mwisho wa siku, matarajio ni kuona kuwa uzalishaji wa mitambo mipya ikiwamo miwili ya Kinyerezi inaihakikishia Tanesco Megawati 305 zaidi ya umeme unaopatikana sasa na ndipo kutakapokuwa na uhakika wa kueleza kuwa tatizo la umeme nchini limemalizika.

Kadhalika, taarifa ya Tanesco inaeleza sababu za kutoa taarifa zenye matumaini ambazo nyingine zimetofautiana na uhalisia.

“Ni muhimu pia Watanzania watuelewe kwamba kila kitu hakiko katika uwezo wetu. Hii ni kwa sababu baadhi ya mitambo ya kuzalisha umeme na pia mifumo ya gesi siyo ya kwetu na inamilikiwa na watu wengine.

Hivyo taarifa tulizokuwa tunazipokea kutoka kwa makampuni haya ndizo tumekuwa tukiwapatia wateja wetu na bahati mbaya baadhi yake hazikuwa kama tulivyokuwa tumeelezwa,” sehemu ya taarifa ya Tanesco inaeleza.

Mbali na mitambo ya Tanesco, umeme unaopatikana kwa sasa unatoka kwa kampuni za Songas, Symbion, Aggreko na IPTL huku mfumo wa gesi unahusisha kampuni za Pan Africa Energy, TPDC na M&P.

WASOMI WAZUNGUMZIA TATIZO LA UMEME

Dk. Donath Olomi wa Chuo cha Uongozi na Ujasiriamali, anasema matatizo ya umeme yaliyopo sasa ni matokeo ya usimamizi mbovu, hasa kwenye suala la mikataba kwani haiko wazi.

Alisema kuna athari kubwa katika mgawo huo na ushahidi ni Tanesco kupata hasara ya Sh. milioni 500 kwa siku kutokana na kukosa mapato. Pia, alisema athari nyingine ni kwa wenye viwanda ambao sasa hujiendesha kwa gharama kubwa kwa kutumia majenereta huku viwanda vingine vikilazimika kusimamisha uzalishaji.

Alisema njia mojawapo ya kuondokana na matatizo ya kupatikana kwa umeme wa uhakika ni kuipunguzia Tanesco baadhi ya majukumu iliyo nayo sasa.

Makamu Mkuu mstaafu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Profesa Tolly Mbwete, alisema Tanesco inatakiwa kutoa maelezo ya kina kuhusiana na tatizo la kukatika kwa umeme.

“Walisema kuna mitambo ya gesi inatengenezwa na imemalizika... sasa inakuwaje kuna mgawo na ni kwa nini wanakaa kimya hadi wanasiasa wanaliingilia,” alisema Profesa Mbwete.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Prosper Ngowi, alisema kukosekana kwa umeme wa uhakika nchini kutaleta madhara makubwa kiuchumi ikiwa ni pamoja na kutovutia wawekezaji wa uhakika wa ndani na nje ya nchi.
Alisema hata sasa wawekezaji wengi wamekuwa wakilalamikia kukosekana kwa nishati yenye uhakika na hivyo, suala hilo linapaswa kutafutiwa suluhisho la kudumu.

Mkurugenzi wa Sera na Ushawishi wa Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI), Hussein Kamota, alisema ni wazi kwamba kuna hasara kubwa imepatikana kwa wanachama wao na kwamba, wanafanya tathmini na taarifa yao wataitoa kwa umma kesho.

Kibanda atoa tamko kuhusu taarifa na magazeti feki ya Rai, Mtanzania


Kampuni ya New Habari (2006) Ltd inayochapisha magazeti ya MTANZANIA, RAI, Bingwa Dimba na The African, imelaani vikali, uzushi, uongo na upotoshaji wa hali ya juu unaofanywa na watu wasio na nia njema na kampuni
hiyo.

Jana watu hao wasio na nia njema na kampuni hiyo, hasa magazeti ya MTANZANIA na RAI, walitengeneza mfano wa magazeti hayo kisha kuyaweka kwenye mitandao ya kijamii, yakiwa na taarifa mbalimbali za uongo na uzushi.

Akizungumzia hali hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda, alisema ameshtushwa na hatua hiyo, lakini ni vema wasomaji na wafuatiliaji wa magazeti ya MTANZANIA na RAI, wakapuuza magazeti yanayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, kwani watu wanaofanya hivyo wamelenga kuyachafua kwa masilahi yao binafsi.

Kibanda alisema watu hao wenye nia ovu na magazeti hayo, juzi walitengeneza mfano wa gazeti la RAI likiwa na kichwa cha habari kisemacho “Gwajima: Nina imani na Lowassa katika kutimiza ndoto zangu” na jana wametengeneza MTANZANIA na kulisambaza kwenye mitandao ya kijamii likiwa na kichwa habari “Lowassa, Kagame wahusishwa kifo cha Mch. Mtikila”.

“Tumeshtushwa na hatua hii ya kurudia uovu wao, tulipoona kwa mara ya kwanza wametengeneza gazeti feki la RAI ambalo lina sura inayofanana na gazeti letu halisi na kuliweka kwenye mtandao ili kuwaaminisha watu kuwa gazeti linaloenda sokoni ndiyo lile ambalo lilikuwa na habari ambazo ni potofu, zenye mwelekeo wa uchochezi, tulipuuza. Hata hivyo, wahusika wa uovu ule wa awali tuliwabaini.

“Watu hawa wamerudia tena, sasa niseme inatosha, napenda kuwaambia wasomaji wa gazeti la MTANZANIA ambalo huchapishwa kila siku na RAI kila Alhamisi ya wiki kuwa, gazeti lililowekwa kwenye mitandao ya kijamii si gazeti halisi la RAI wala habari zile hazijawahi kuandikwa na RAI hata mara moja.

“Na hata ukizisoma habari zilizomo kwenye gazeti linalosambazwa mtandaoni zimetawaliwa na dhamira ya kulipaka matope gazeti halisi la RAI, wahariri na waandishi wake kwa malengo ambayo hatujayajua.

“Katika uchunguzi wetu tuliofanya baada ya gazeti feki kuwekwa mitandaoni kwa mara kwanza, tuliona kazi hiyo haramu inafanywa katika chumba kimoja cha habari ambacho watendaji na wahariri wake wana mrengo fulani wa kihabari. Tulikaa kimya wakati ule wa kwanza kwa maana tuliamini wangejifunza kutokana na upuuzi wao.

“Lakini baada ya kuona wamerudia, tumeona kuna wajibu wa kuwajulisha wasomaji wetu ambao baadhi wanaingia kwenye mitandao ya kijamii kabla ya kusoma magazeti, kwamba kile ambacho wanakiona kwenye mitandao si magazeti halisi ya MTANZANIA na RAI.

“Kutokana na hali hiyo, tunaangalia namna bora ya kuwasiliana na mamlaka husika za kiserikali ili kupata njia sahihi ya kuwashughulikia hawa wanaokiuka sheria ya mitandao,” alisema. 

Kibanda amewataka watu hao wenye nia ovu na Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, kuachana na mikakati yao hiyo miovu kwani haitawasaidia kufanikisha malengo yao dhalimu.
Ifuatayo ni moja ya habari zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii...

HII NDIYO HABARI ILIYOFANYA MTANZANIA LISIUZWE LEO 👇🏻👇🏻

UKAGUZI maalumu uliofanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kwa mwaka wa fedha 2014/15 umeibua ufisadi mkubwa katika wizara, idara, wakala za serikali, halmashauri, taasisi na mashirika ya umma.

Katika ukaguzi huo, Wizara ya Ujenzi imegundulika kuwa imefanya malipo hewa ya Sh milioni 951.7 yaliyolipwa kwa
makandarasi kwa kazi ambayo haikufanywa, huku Wizara ya Maliasili ikiwa na malipo hewa ya zaidi ya Sh milioni 156 kupitia Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).

Wizara ya Ujenzi inayoongozwa na mgombea urais wa CCM Dk. John Magufuli pia imesababisha hasara ya Sh bilioni 124.8 ambazo ni malimbikizo ya riba iliyozalishwa kutokana na kucheleweshwa malipo ya wakandarasi yenye thamani ya Sh trilioni 5.3.

Katika ukaguzi huo wa PPRA, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) ni miongoni mwa taasisi 17 zilizofanya vibaya katika ununuzi na kuwa na viashiria vya rushwa katika baadhi ya miradi.

Kutokana na ufisadi huo, PPRA imependekeza taasisi zilizohusika na malipo hayo zirejeshe fedha hizo kutoka kwa wazabuni waliolipwa na kuwachukulia hatua za nidhamu watumishi waliohusika na malipo hayo.

Akiwasilisha ripoti ya ukaguzi huo jana, Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Balozi Matern Lumbanga, alisema ukaguzi huo ulihusisha taasisi 80 zikijumuisha wizara, idara zinazojitegemea, wakala za serikali, halmashauri za Serikali za mitaa, taasisi na mashirika ya umma. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mikataba 5,206 yenye thamani ya Sh bilioni 214.6 ilikaguliwa ambako kazi za kandarasi zilikuwa mikataba 345, bidhaa mikataba 1,112, huduma za ushauri wa utaalamu 34, huduma zisizo za ushauri wa utaalamu 1,041, ununuzi yenye thamani ndogo 2,671 pamoja na matumizi ya utaalamu wa ndani mikataba mitatu.

Balozi Lumbanga alisema taasisi 35 zilifanyiwa ukaguzi kupima kama thamani bora ya fedha ilipatikana kwenye miradi 186 yenye thamani ya Sh bilioni 296.

“Ukaguzi huo ulibaini ucheleweshaji mkubwa wa malipo kwa wakandarasi hususan kwenye miradi ya ujenzi wa barabara na miradi ya maji katika Serikali za Mitaa.

Sababu kubwa ni kutokana na ucheleweshaji wa utoaji fedha zilizotengwa kwa ajili ya miradi husika.“Ikumbukwe
kwamba malimbikizo ya riba yataendelea kuongezeka hadi hapo malipo yatakapofanyika.

Unapochelewesha malipo ya wakandarasi halafu yanazaa riba maana yake Taifa linabebeshwa mizigo ambayo haistahili,” alisema.

“Kati ya miradi 186 iliyokaguliwa, miradi 35 yenye thamani ya Sh bilioni 58.2 ilipata wastani usioridhisha wa chini ya asilimia 50.

“Hii ni ishara kwamba malengo yaliyokusudiwa kwenye miradi hiyo kwa kiasi kikubwa hayatafikiwa na thamani bora ya fedha inaweza isipatikane.

“Miradi 55 yenye thamani ya Sh bilioni 81.26 ilipata wastani wa kuridhisha wa zaidi ya asilimia 75 wakati miradi 96 yenye thamani ya Sh trilion 2.8 ilipata wastani wa kati ya asilimia 50 na 75,” alisema Balozi Lumbanga.

Alizitaja taasisi 17 zilizofanya vibaya na alama zilizopata kwenye mabano kuwa ni NEC (38), TRL (51), Tume ya Ajira (53), Kituo cha Uwekezaji (51), Shirika la Madini la Taifa-Stamico (56), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (60), Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (56), Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda (42), Halmashauri ya Wilaya ya Karatu (49), Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi (50) na Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo (57).

Nyingine ni Halmashauri za Kigoma (52), Misungwi (55), Iramba (52), Nanyumbu (60), Kyela (60) na Mamlaka ya Majisafi na Maji taka Lindi (60). “Taasisi hizi zilishakaguliwa miaka iliyopita na kupewa mapendekezo ya namna ya kuboresha ununuzi wao kwa mujibu wa sheria lakini zimeendelea kuyapuuza mapendekezo hayo na kuendelea kufanya vibaya,”alisema.

 Malipo hewa

Balozi Lumbanga alisema taasisi tisa zilibainika kufanya malipo hewa kwenye miradi yenye thamani ya Sh bilioni 6.4.

“Ukaguzi umebaini malipo ya ziada ya Sh milioni 951.7 yalilipwa kwa wakandarasi kwa kazi hewa, kiasi hiki ni sawa na asilimia 15 ya thamani ya miradi yote ya kazi za ujenzi iliyokaguliwa,” alisema. Mwenyekiti huyo alizitaja taasisi zilizohusika na malipo hewa kwenye mabano kuwa ni Shirika la Hifadhi za Taifa – Tanapa (Sh milioni 156.3), TRL (Sh milioni 473.6), Halmashauri ya Kigoma (Sh milioni 11.1), Halmashauri ya Kibondo (Sh milioni 64.9), Halmashauri ya Jiji la Mwanza (Sh milioni 69.6), Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi (Sh milioni 55.6),

Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Sh milioni 25.42), Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe (Sh milioni 93.09)
na Halmashauri ya Wilaya ya Kyela (Sh milioni 2.08).

Pia alisema ulifanyika uhakiki wa malipo hewa yaliyobainishwa kwenye ukaguzi wa mwaka 2013/14 na kubaini malipo hewa ya Sh milioni 377. Kuhusu ucheleweshaji wa malipo, alisema mikataba 301 ya Wakala wa Barabara (Tanroads), yenye thamani ya Sh trilioni 5.3 ilicheleweshewa malipo na hivyo kuwa na malimbikizo ya riba ya Sh bilioni 124.8 hadi kufikia Juni mwaka huu.

 Rushwa kwenye ununuzi

Kulingana na PPRA, taasisi inapopata asilimia 20 au zaidi katika viashiria vya rushwa ni dalili ya kuwapo vitendo vya rushwa kwenye ununuzi au miradi husika. Kulingana na ripoti hiyo, katika miradi yote 186 iliyokaguliwa, miradi 27 ilibainika kuwa na viashiria vya rushwa kwa zaidi ya asilimia 20 na tayari Taasisi ya Kuzuia ya Kupambana na Rushwa (Takukuru) imearifiwa ichukue hatua zaidi.

Taasisi tisa zilizobainika kuwa na viashiria vya rushwa ni NEC (asilimia 29), TRL (22), Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (21), Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda (22), Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo (24), Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma (28), Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi (20), Halmashauri ya Wilaya ya Karatu (31) na Agricultural Input Trust Fund (28).

Alipotakiwa kutoa ufafanuzi ni miradi ipi iliyokuwa na viashiria vya rushwa katika NEC, Ofisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Dk. Laurent Shirima alisema: “Huwezi kutoa taarifa za uchunguzi wowote unaoendelea hadi uwe umekamilika.

“Hatuwezi kutoa taarifa zozote kwa sababu kwa mazingira ya sasa hivi kuna vitu ambavyo huwezi kuvifanya…vinaweza kuwa na madhara au athari kwa jamii”.

Hatua zilizochukuliwa

Balozi Lumbanga alisema maofisa masuuli na wakuu wa vitengo wa taasisi 17 zilizofanya vibaya na zilizotekeleza miradi 35 chini ya wastani wa kuridhisha, watawajibika kujieleza mbele ya bodi hiyo kwa nini wasichukuliwe hatua za nidhamu na sheria.

“Mamlaka itachukua hatua ya kuwafungia wakandarasi na wataalamu washauri waliohusika na malipo hewa. Taasisi zote zilizobainika kuwa na viashiria vya rushwa zitawasilishwa Takukuru kwa uchunguzi zaidi.

“Tutapeleka timu ya wataalamu kuhakiki malipo hewa ya wakandarasi kwa kazi ambazo hazikufanywa,” alisema.
Pia alizitaka taasisi 53 zilizopata wastani chini ya asilimia 75 kuwasilisha PPRA mahitaji yao ya mafunzo kuhusu Sheria ya Ununuzi na Kanuni zake.

PPRA pia imezifungia kampuni saba na wakurugenzi wake kushiriki zabuni za umma kutokana na kukiuka mikataba waliyoingia na vitendo vya udanganyifu. Kati ya kampuni hizo, sita zimefungiwa kwa miaka waliyoingia na vitendo vya udanganyifu. Kati ya kampuni hizo, sita zimefungiwa kwa miaka miwili na moja imefungiwa kumi kuwasilisha dhamana za zabuni za kughushi wakati wa michakato ya zabuni

Licha ya TLP kuwa na mgombea Urais, Mrema amwombea kura MagufuliHii ni moja ya sura ya hali halisi ya siasa za uchaguzi wa viongozi inavyoendelea nchini Tanzania kwa wakati huu, ambapo Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema ambaye anatetea kiti chake cha Ubunge kwa jimbo la Vunjo, leo alijotokeza kwenye msafara wa mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM), John Magufuli na kudai kuwa anamuunga mkono, licha ya chama chake, TLP kuwa na mgombea katika nafasi hiyo, Macmillan Lyimo.

Mrema amewataka wananchi wa jimbo la Vunjo kumpa kura za Urais Magufuli lakini kura zote za ubunge wampatie yeye.

Mrema anakabiliwa na upinzani mkali jimboni Vunjo kwani atapambana na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia ambaye anawakilisha umoja wa vyama vinavyounda UKAWA (NCCR, CHADEMA, CUF na NLD) na hivyo kumuweka kwenye wakati mgumu wa kutetea ubunge wake.

Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), ambaye pia ni Mgombea ubunge Jimbo la Vunjo, Augustino Mrema aliposimama kwa mudakuwasalimia wananchi Njia Panda ya Himo, mkoani Kilimanjaro. Mrema alimpigia debe Dk Magufuli kwa kuwataka watanzania wampigie kura nyingi za ndiyo ili awe rais
Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akiwa na furaha wakati Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), ambaye pia ni Mgombea ubunge Jimbo la Vunjo, Augustino Mrema akimuombea kura kwa wananchi aliposimama kwa muda kuwasalimia wananchi Njia Panda ya Himo, mkoani KilimanjaroMrema akitoa heshima baada ya kumuona Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli eneo la Njia ya Panda ya Himo.


Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akiwa na Mgombea ubunge Jimbo la Vunjo kupitia CCM, Innocent Shirima wakiwapungia mikono wananchi walipokuwa wakiwasili kwenye mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Polisi wa Himo, Jimbo la Vunjo, mkoani Kilimanjaro


Wananchi wa Rombo wakimshangilia Dk Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa kampeni mjini Tarakea, Rombo


Dk Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Rombo, Samora mjini Tarakea


Wananchi wakishangilia baada ya kumuona Dk Magufuli alipowasili kwenye Uwanja wa Polisi Mjini Himo, Jimbo la Vunjo


Dk Magufuli akijinadi katika mkutano wa kampeni mjini Vunjo ambapo ameaomba wananchi kumpigia kura ili awafanyie kazi


Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Vunjo, Innocent Shirima mjini Himo


Mgombea ubunge Jimbo la Vunjo kupitia CCM, Innocent Shirima, akikana mbele ya wananchi na Dk Magufuli uvumi uliozagaa kwamba anataka kuihama CCM kwenda Ukawa wakati wa mkutano wa kampeni katika mji wa Himo.Dk Magufuli akionesha kadi ya mwanachama wa NCCR-Mageuzi aliyeamua kuhamia ccm katika mkutano ulioffanyika mjini Himo, Jimbo la Vunjo.


Wananchi wa Njia Panda ya Himo, Jimbo la Himo, wakishangilia baada kumuona Dk Magufuli.


Wafanyabishara ndogondogo wanaofanya biashara kando kando ya barabara jimbo la Vunjo wakaishangilia baada ya kuwaeleza viongozi wa serikali kuacha kuwatoza ushuru.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo akiwaelekeza wananchi jinsi ya kuipigia kura CCM, ambayo katika karatasi la kupigia kura ipo nafasi ya tatu.


Wnanchi wwilayani Mwanga wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni mjini Mwanga


Wananchi wakisikiliza wakati Dk Magufuli akihutubia mjini Mwanga


Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Mwanga kupitia CCM, Profesa Jumanne Maghembe


Wananchi wa Kisiwani Jimbo la Same Mashariki wakishangilia baada ya kumuona Dk Magufuli


Dk Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango katika mkutano uliofanyika Ndungu


Wananchi wakishangilia wakati Dk Magufuli akitoa ahadi mbalimbali katika mkutano uliofanyika katika Mji wa Ndungu, Same Mashariki


Dk Magufuli akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi Anne Kilango


Wananchi wakishangilia wakati Dk Magufuli akijinadi kwao mjini Same


Moja ya vionjo katika mkutano wa kampeni mjini Same


Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi katika mkutano wa kampeni mjini Same. 

Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne, 2005/2006 hadi 2014/2015Tumeshirikishwa na Evarist Chahali

Kwa muhtasari: Miaka 53 ya mafanikio ya kujivunia
Tumeshirikishwa na Evarist Chahali