Miujiza yetu! Shule ina Mwalimu mmoja; Anafundisha STD I hadi VII wanafunzi 279


Japo Tanzania ina mengi mazuri ya kustaajabia, pia na vituko na viroja vya kuona na kuamini!

Shule ya Msingi Luhoza iliyopo katika kijiji cha Ngaiti wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro ina mwalimu mmoja anayefundisha wanafunzi 279 kuanzia darasa la kwanza hadi la saba, huku wananchi wasio na taaluma ya ualimu wakilazimika kuingia darasani kufundisha.

Mbowe atamka jibu la Dk Slaa alipoulizwa Lowassa akiwa Rais yeye awe nani...


Serikali yasema madai ya Walimu ya sh bilioni 29/- yanahakikiwa na Mkaguzi


Afande Sele azungumzia kilichomkwamisha kuzindua kampeni zake za Ubunge


Mtangazaji wa ChannelTEN aliyepata ajali anaomba msaada akatibiwe


Aliyekuwa mfanyakazi wa Africa Media Group Limited - AMGL inayomiliki vituo vya televisheni vya Channel Ten, DTV, CTN, C2C na kituo cha radio cha Magic Fm, bw. Meshack Nzowah ambaye alipata ajali hivi karibuni anaomba msaada wa matibabu nje ya nchi kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye ajali hiyo.

Meshack Nzowah ambaye kwa sasa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili anatakiwa kusafirishwa kwenda India kwa ajili ya matibabu haraka iwezekanavyo, ambapo kiasi cha shilingi milioni 30 zinahitajika.

Kwa mujibu wa kaka wa Meshack, bw. Masoud Suleiman Nzowah tayari Meshack amepatiwa huduma kadhaa akiwa Muhimbili hospitali ikiwemo kufanyiwa upasuaji wa jicho lakini kwa mujibu wa madaktari, anatakiwa matibabu zaidi ya kichwa.

Kwa yeyote atakayeguswa na kutaka kumsaidia Meshack Nzowah anaweza kuweka mchango wake kupitia akaunti namba 2011 000 9584 NMB HOUSE - yenye jina MASOUD NZOWAH ama anaweza kutuma mchango wake kwa tigo pesa kwenye simu namba 0715 30 41 85 au 0713 461627.

Watuhumiwa wa makosa ya mtandao wafikishwa mahakamani


Serikali leo imemfikisha mahakamani bwana Bernedict Angelo Ngonyani kwa tuhuma za kutumia mtandao wa Facebook na WhatsApp kueneza taarifa za uongo kuwa mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange amelazwa Nairobi kwa madai ya kulishwa chakula chenye sumu.

Akizungumza kwenye eneo la mahakama ya kisutu jijini Dar es Salaam ambako mtuhumiwa huyo alifikishwa kwa ajili ya kusomewa mashitaka, wakili mkuu wa serikali Joanes Karungura amesema, mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo kwa kuvunja kifungu namba 16 cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao ya mwaka 2015.

Sheria hiyo ijulikanyo kwa lugha ya Kiingereza, Tanzania Cybercrime Act 2015, inakataza kusambaza ujumbe, taarifa au data za uongo au zisizothibitishwa kwa njia ya mtandao.

Ngonyani ambaye amenyimwa dhamana kutokana na aina ya kosa alilofanya la kuvunja sheria ya mtandao ya mwaka 2015 alikamatwa Septemba 25 mwaka huu kwa ushirikiano wa mamlaka ya mawasiliano nchini, Jeshi la Polisi na vyombo vya ulinzi na usalama.

Wakati huo huo serikali imewafikisha watuhumiwa watano katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, mmoja raia wa Afrika ya Kusini, mmoja raia wa China na watatu kutoka Pakstani, kwa kosa la kuiba kwa njia ya kimtandao wizi wenye thamani ya karibu shilingi billion moja, fedha za Kitanzania.

Mhandisi wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini, TCRA anasema watuhumiwa hao walikutwa na laini zaidi ya mia moja zenye usajili bandia ambazo walikuwa wanazitumia kufanya biashara ya kupiga simu Kimataifa kinyume cha sheria.Mtuhumiwa wa makosa ya mtandao Benedict Angelo Ngonyani (24) (wa kwanza kulia) anayetuhumiwa kusambaza taarifa za uongo zinazomhusu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, akiwa katika mahakama ya hakimu mkazi ya Kisutu akisubiri kusomewa mashitaka. 

Wengine ni watuhumiwa wa wizi kwa kutumia mitandao ya simu (fraud and use of telecommunication network) Ally Hamze (53) raia wa Afrika Kusini (wa pili kulia), Huang Kun Bing (26) Raia wa China (wa tatu kulia) Irfan Mirza Baig (46) (wa kwanza kushoto) Hefeez Irfan (32) (wa pili kushoto) na Mirza Rizwan Baig (41) (wa tatu kushoto) wote watatu raia wa Pakistani wakiwa katika Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu wakisubiri kusomewa mashitaka ya wizi kwa kutumia mitandao ya simu (fraud and use of telecommunication network).

Kesi zote zimeahirishwa hadi Oktoba 23 na watuhumiwa wote wamepelekwa rumande huku uchunguzi ukiendelea.

Burudani ya sanaa ya kucheza na baiskeli


Wakamatwa na vifaa wakiandikisha kiwandani kwa mtindo BVR


Hofu ilitanda jana katika kiwanda cha MM Steel cha jijini Dar es Salaam, baada ya kuwapo kwa taarifa kuwa mashine ya kusajili wapiga kura kwa mfumo wa elektroniki (BVR) inatumika kuandikisha wafanyakazi katika kiwanda hicho.

Kutokana na hofu hiyo, baadhi ya maofisa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakiongozwa na Mwanasheria wa chama hicho, John Mallya, Polisi na Tume Taifa ya Uchaguzi (Nec), walifika kiwandani humo na kufanya upekuzi ikiwamo kuondoka na baadhi ya vifaa vilivyokuwa vinatumika.

Baada ya kukubaliana pande zote, vifaa hivyo ambavyo ni vya kuchukua alama za mikono, macho, scanner na kompyuta mpakato, vilichukuliwa na Polisi ili baadaye vikakabidhiwe Nec.

Polisi, Chadema na Tume, walielezwa na Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo, Abubakari Mlawa, kuwa kampuni hiyo imeamua kuandikisha wafanyakazi wake kutokana na kukithiri kwa vitendo vya wizi katika viwanda saba walivyonavyo na kushindwa kuwatambua wafanyakazi.

“Tunaendesha zoezi la kuweka ‘data base’ kwa ajili ya wafanyakazi wetu wote kwa maana ya kupiga picha na kuandika taarifa zake zote; amezaliwa wapi, amesoma wapi na ameanza kazi lini, wakati tunaendelea na zoezi letu walikuja watu wakajitambulisha kuwa ni polisi wakawaweka chini ya ulinzi watu wanaofanya zoezi hilo. Tulipowauliza ni kina nani, walisema wanatoka Chadema na wamepewa taarifa kuwa tunatoa vitambulisho vya kupigiakura,” alisema na kuongeza:

"Ili tujiridhishe, tuliamua kuwaita Nec na polisi kuthibitisha wamechukua mashine kwenda kujiridhisha. Tunafanya zoezi hili wiki nzima na tumeandikisha wafanyakazi zaidi ya 100 na tuna zaidi ya wafanyakazi 900.”

Hata hivyo, wakati anahojiwa na Polisi na Chadema kama kifaa cha alama za vidole wametoa wapi, Meneja huyo alisema walitoa zabuni kwa kampuni ambayo hakuitaja na alipotakiwa kuitaja hakufanya hivyo.

Afisa wa ICT wa Nec, Amosi Madaha, akizungumza mara baada ya kufika na kulinganisha mashine ya alama za vidole ya Nec na yao, alisema ni mapema sana kueleza kama vifaa hivyo ni sehemu ya vifaa vya BVR hadi watakapokwenda kuvichunguza zaidi.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango wa Nec, Salvisius Mkwera, alisema walipata taarifa kuna uandikishaji wa wapigakura unafanyika ndani ya kiwanda hicho na walipofika walikuta baadhi ya vifaa ambavyo ni ngumu kusema.

“Tulichokiona ni baadhi ya vifaa ambavyo vinafanana na vifaa vya Tume, lakini hatuwezi kuhakikisha kama ni vyetu au siyo, tulichokubaliana na polisi ni kuchukua vifaa hivyo vifanyiwe uchunguzi zaidi tujiridhishe na vifaa tulivyonavyo,” alisema.

Alitaja kifaa kinachofanana na cha Nec kuwa ni `finger print machine,' lakini wamechukua na vifaa vingine kama kompyuta mpakato na scanner.

Alisema pia wataingia kwenye data base ya kampuni hiyo ili kujiridhisha na taarifa zilizoingizwa.

Alisema pia wamechukua orodha ya wafanyakazi waliorodheshwa kwenye karatasi ili kuangalia kwenye daftari la kudumu la wapigakura kama kuna uwiano wowote.

“Tutatoa taarifa mapema na kwa wakati ili kuondoa wingu lililotanda kwa sasa, tunataka pande zote zijiridhishe hivyo tutafanya kwa uwazi kueleza kama hizi ni mashine zetu,” alisema.

Baadhi ya wafanyakazi ambao hawakutaka kutajwa majina yao, walisema wameshtushwa na uandikishaji huyo kwa kuwa unafanana na BVR hasa kwenye uchukuaji wa alama na kuamua kutoa taarifa.

Taarifa ya Wizara leo Oktoba 9 kuhusu Mahujaji

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Taarifa zaidi ya Mahujaji kutoka Tanzania huko Saudi Arabia

Idadi ya mahujaji wa Tanzania waliopoteza maisha katika tukio la kukanyagana lililotokea eneo la Mina, Makkah tarehe 24 Septemba, 2015 imeongezeka kutoka 11 na kufikia 12 hadi sasa. 

Idadi hiyo imeongezeka kufuatia Bi. Aluiya Sharrif Saleh Abdallah kugundulika kuwa ni miongoni mwa mahujaji waliofariki dunia katika tukio hilo. Bi. Abdallah alienda Makkah kufanya ibada ya hijjah kupitia kikundi cha TCDO.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
09 Oktoba, 2015

Kampeni za Ubunge zasimama Arusha Mjini baada ya mgombea kufariki

KAMPENI za wagombea Ubunge jimbo la Arusha Mjini zimesimama kutokana na kifo cha mgombea Ubunge wa chama cha ACT-Wazalendo, Estomih Mallah aliyefariki usiku wa kuamkia leo Oktoba 9, 2015 katika hospitali ya KCMC iliyopo wilaya ya Moshi, Kilimanjaro, baada ya kuugua ghafla ugonjwa wa shinikizo la juu la damu.

Akithibitisha kupokea taarifa za kifo cha mgombea huyo, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Juma Idd ambaye pia ni msimamizi mkuu wa uchaguzi katika jimbo hilo amesema kuwa kampeni ambazo zitaendelea ni za urais na udiwani, lakini wabunge watasubiri mpaka hapo tume ya uchaguzi itakapopanga upya ratiba.

“Kweli mgombea amefariki na nimepata taarifa za kifo hiki leo saa 12:00 asubuhi, kutoka kwa katibu wa chama anachotoka marehemu ACT-Wazalendo, Eliamam Motivo,” amesema.

Katibu wa Jimbo la Arusha wa Chama cha ACT-Wazalendo, Eliaman Motivo amesema amepokea kwa masikitiko makubwa msiba wa mgombea wao na Mshauri Mkuu wa Chama chao kwa mkoa wa Arusha.

“Mzee alikuwa haumwi lakini kwenye mkutano wa mgombea urais wa chama chetu Oktoba 6, alipanda jukwaani na baada yakushuka alisema hajisikii vizuri na kesho yake ambayo Oktoba 7 alikwenda hospitali ya St. Thomas na alipatiwa matibabu ila hali yake iliendelea kuwa mbaya na tuliamua kumwamishia hospitali ya KCMC na usiku wa kuamkia leo saa saba usiku alifariki,” amesema.

Motivo alisema chama hicho kimesimamisha kampeni zote, kwa siku tatu ili kuomboleza msiba huo.

Mwaka 2010, Mallah alishinda kiti cha Udiwani wa Kata ya Kimandolu kupitia CHADEMA. Mapema mwaka 2011, Mallah na madiwani wengine watatu wa CHADEMA -- John Bayo (Elerai), Reuben Ngowi (Themi) na Charles Mpanda (Kaloleni) walivuliwa uanachama wao katika mgogoro baina ya CCM na CHADEMA kuhusiana na kilichodaiwa kuwa uchaguzi batili wa Meya wa Jiji.

Baadaye Mallah alijiunga na ACT-Wazalendo ambapo alipata nafasi ya kuwakilisha chama hicho katika kinyang’anyiro cha Ubunge wa Arusha Mjini katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe Oktoba 25 mwaka huu, na kupambana na Mbunge anayemaliza muda wake MP Godbless Lema (CHADEMA).

Mallah ni mgombea wa tatu wa Ubunge kufariki baada ya CHADEMA kumpoteza Mohamedi Mtoi Kanyawana katika ajali ya gari hapo Septemba 12 akitokea katika kampeni za kuwania kiti cha ubunge wa jimbo la Lushoto.

Septemba 24, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi), Celina Kombani ambaye pia alikuwa mgombea ubunge jimbo la Ulanga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) aliaga dunia nchini India alikokuwa anapatiwa matibabu.

Kama ilivyo kwa maeneo mengine, sheria itafuata mkondo wake na uchaguzi wa ubunge jimbo la Arusha mjini utaahirishwa hadi tarehe itakayotajwa rasmi na Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC), ili kutoa nafasi kwa chama cha ACT-Wazalendo kuteua mgombea mwingine.

Job opportunity as Sikika - Program Officer – Public Financial Management

        Join us in advocating for quality health services for all Tanzanians          Sikika-Logo

Introduction
Sikika is a non-governmental organization that advocates for quality health services for all Tanzanians. The organization works to ensure equitable and affordable quality health care services through social accountability monitoring of health systems at all government levels. For more information about Sikika please visit us at www.sikika.or.tz.
Sikika seeks to recruit Program Officer-Public Financial Management for its Dar es Salaam Office with immediate effect:
Job Title: Program Officer – Public Financial Management (1 post)
Reporting to: Head of Department

Responsibilities:
Independently perform analysis and produce outputs for advocacy in the following areas:
  • Fiscal policy, legal, and regulatory framework for public financial management, in particular with regard to transparency and accountability.
  • Annual government budgets including revenues, expenditures, and budget deficits, in particular with regard to equity and efficiency.
  • Regular technical performance reports, financial performance reports, and audit reports.
  • Assessment of PFM system through PEFA framework.
  • Act as liaison with various stakeholders that are involved in the public financial management reform process at local, national and international level.
  • Assist in the preparation of Sikika’s annual work plans, budgets, and reports.
  • Advise and support other colleagues on public financial management issues.
Qualifications:
(a) University degree or equivalent qualification in the following, or related, fields: Economics, Public Policy, Public Administration or Business Administration, Controlling or Accounting (master’s level will be added advantage. (b) At least 3 years of experience in relevant field of work (c) Proven ability to manage projects and achieve results (d) Fully proficient in oral and written English (fluency in Kiswahili is highly desirable) (e) Computer skills

If you think you are suitable for this job, we encourage you to send:
a) A one-page cover letter explaining why you believe that your competencies and experiences are suitable for this job
b) An updated CV that includes your contact details and names and contacts of 3 references
Remuneration:
An attractive remuneration package will be offered to successful candidates.

Send your application to: The Human Resources and Administration Manager at Sikika, by e-mail only: [email protected]. Please note, only shortlisted candidates will be contacted.

Application Deadline:  20Th October 2015