Taarifa ya ZEC kuhusu shahada za kupigia kura

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar inawatangazia wananchi wote wa Zanzibar kwamba kuanzia tarehe 19/10/2015 itasitisha zoezi la uchukuaji wa shahada za kupigia kura katika afisi za Tume za Wilaya kwa Unguja na Pemba.

Tume inawataka wale wote ambao hawajachukua shahada zao katika ofisi za Tume za Wilaya kuharakisha kuchukuwa shahada zao, kwani zoezi la utoaji wa shahada hizo katika afisi za Wilaya litasitishwa ifikapo tarehe 19/10/2015, na litaendelea kufanyika Makao Makuu ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar yaliyopo Maisara kwa upande wa Unguja na ofisi ndogo ya uchaguzi ya iliyopo Chakechake Pemba hadi litakapotoka tangazo jengine.

Aidha tume inawaomba wananchi kuzingatia muda uliotolewa wa uchukuwaji wa shahada za kupigia kura katika ofisi za Wilaya kwa lengo la kuondoa usumbufu utakaoweza kujitokeza.

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar inaomba mashirikiano kwa kulifanikisha zoezi hili.

Piga kura kwa amani upate maendeleo nchini.

Ujumbe huu umeletwa kwenu na tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC).

Mzee Majuto aelezea hijja, yaliyomkuta Macca na alivyonusurika ajalini
Hatima ya kura ya Wanavyuo kwa Uchaguzi Mkuu 2015 - Kaimu Mkurugenzi wa Sheria NEC ajibu maswali


Makulilo aelezea msimamo wake kuhusu mabadiliko Tanzania 2015


Zitto atamka hataki kura za watu gani na anaomba zipi


Mgombea mmoja wa uongozi wa kisiasa "inji" hii...


Mwaliko: Mkutano wa NEC na Vyama vya Siasa


Taarifa na mwaliko wa mdahalo wa Urais Tanzania 2015

Muda: saa tano asubuhi hadi saa sita
Time: 11am to 12 noon

Tarehe: Jumatatu 12 Oktoba 1 2015
Date: Monday 12 October 2015

Mahali: Makumbusho (Imetazamana na IFM)
Place: National Museum in town (opposite IFM)

Ufafanuzi wa NEC kuhusu tuhuma za vituo hewa 20,000 vya kura


Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ndugu Kailima Ramadhani amefafanua jinsi mabavyo Tume ya taigfa ya uchaguzi ilivyo gawanya vituo vya wapiga kura kote nchini. Katika ufafanuzi huo amefafanua mambo makuu Mawili.

1. Namna ambayo siyo sahihi ya kuhesabu vituo vya wapiga KURA kama walivyo fafamua baadhi ya watu, Ambayo ni namna ya KUPOTOSHA NA NI UWONGO, na

2. Namna SAHIHI ya kuhesabu vituo kama tume ye taifa ya uchaguzi ilivyo hesabu. Nia hii inazingatia mambo yafuatayo.
i). KUTUO HAKITAZIDI WATU 450
ii). KITUO KINAWEZA KUWA NA IDADI CHINI YA WATU 450
ILI WATU WALIOJIANDIKISHA KITUO KIMOJA WASIHAMISHWE KWENDA KUJAZIA ENEO JINGINE.

Itakuwa hivi.
Endapo kuna eneo ambalo watu waliojiandikisha ni 1900 Tume ya taifa ya uchaguzi itagawanya watu kama ifuatavyo:-
450+450+450 = 1300
1900-1300 = 550
550 gawanya kwa 2 = 275

KWA HIYO MAHALI PENYE WAPIGA KURA 1900
PATAKUWA NA VITUO VITANO (5)
  1. KITUO CHA KWANZA WATU 450
  2. KITUO CHA PILI WATU 450
  3. KITUO CHA TATU WATU 450
  4. KITUO CHA NNE WATU 275
  5. KITUO CHA TANO WATU 275
JUMLA 1900

ZINGATIA

Kutokana na kuwepo kwa vituo vyenye idadi ya watu chini ya 450 kumefanya idadi ya vituo iwe kubwa.

Taarifa ya NEC kuhusu vifaa vilivyokamatwa kiwandani vikiandikisha kama BVR
Siku moja baada ya kunaswa mashine zilizosadikiwa kuwa ni za uandikishaji wapiga kura kwa njia ya kielektroniki (BVR), zilizokuwa zikiandikisha wafanyakazi wa Kiwanda cha MM Steel jijini Dar es Salaam, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeibuka na kueleza kuwa mashine hizo ni 'feki' na wala hazihusiani kwa namna yoyote na vifaa vyao.

Mkurugenzi wa NEC, Ramadhani Kailima, ndiye aliyetoa ufafanuzi huo wakati akizungumza na Nipashe jana kuhusiana na mashine hizo ambazo zilikamatwa juzi wakati zikiendelea kutumiwa kwa shughuli ya uandikishaji wa wafanyakazi wa kiwanda hicho kilichopo katika eneo la Mikocheni.

Wakati Polisi wakizikamata jana kwa ushirikiano na maofisa kadhaa wa NEC, tayari mashine hizo zinavyofanana na BVR zilishaandikisha wafanyakazi zaidi ya 100 wa Kiwanda cha MM Steel.

Akielezea zaidi kuhusiana na tukio hilo, Kailima alisema kuwa, mara baada ya kupata taarifa za kuwapo kwa mashine hizo, walienda kuzikagua na kubaini kuwa hazina uhusiano na zile za Biometric Voter Registation (BVR), zilizotumiwa na wao (NEC) kuandikisha wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25.

“Hakuna ukweli wowote kuwa zile ni mashine za BVR na tumebaini ni feki, tena ni sawa na zile zinazotumika kwenye ofisi mbalimbali kuandikisha wafanyakazi wake... hawa waliosema ni mashine za kuandikishia wapiga kura hawako sahihi... si kweli,” alisema Kailima.

Alisema endapo watu wataendelea kuwa na shaka juu ya namna NEC inavyofanya kazi kwa sababu tu ya kuona mashine kama hizo, basi wanaweza pia kukamata mashine za ofisi nyingi zikiwamo za kwenye viwanja vya ndege, hospitali na hata manispaa kama ya Kinondoni ambayo hutumia mashine kama hizo kwa shughuli zake mbalimbali.

“Mashine tulizozikuta kwenye hiyo ofisi jana (juzi) ni computer mpakato (laptop) na mashine za kuchukua alama za vidole. Hata wale wafanyakazi tulipowahoji walibainisha kuwa wanazitumia kuorodhesha wafanyakazi wao kwa ajili ya usalama wa ofisi... na tena zipo ofisi nyingi zinatumia mashine hizo,” alisema Kailima.

Kailima alitoa tahadhari kwa wataalamu wanaovishauri vyama vya siasa kuwa makini na kuacha kupotosha kwa kuwaleza mambo yasiyo na ukweli, hasa kuhusiana na NEC kwani wao wanafanya kazi zao kisayansi zaidi na hakuna fursa ya kuwapo kwa ubabaishaji wa aina yoyote.

Aliongeza kuwa hawafanyi kazi zao kwa misikumo ya kisiasa, bali huzingatia utaalamu na hivyo wanaotumiwa kwa ushauri na vyama waache kuwadanganya wanasiasa.

“Hawa wanasiasa wanadanganywa na watu wanaojiita wataalamu... mashine hizi (zilizokamatwa) hazihusiani na BVR," alisisitiza.

Akieleza zaidi juu ya hatua walizochukua baada ya tukio la juzi, Kailima alisema kuwa (jana) walifanya uchunguzi wa mashine hizo kwa kushirikiana na wawakilishi kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambao ndiyo walitoa malalamiko kwao kuhusiana na madai ya kuwapo kwa mashine kama BVR zinazotumiwa kuandikisha watu.

“Wataalamu wao (Chadema) walikuja na tukathibitisha (wote) zile ni feki na hazihusiani kabisa na mashine zetu za BVR,” alisema Kailima.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) John Mnyika, aliitaka NEC ivikabidhi vyama vya siasa nakala za daftari la kudumu la wapiga kura ili kuepukana na njama za wizi wa kura alizodai zinaweza kufanywa na chama tawala -- Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumia tukio la juzi kuhusu kukamatwa kwa vifaa vinavyofanana na mashine za BVR, Mnyika alisema suala hilo walilikabidhi kwa maofisa wa NEC na Jeshi la Polisi ambao wanalichunguza kwa kushirikiana na maofisa wa Chadema ili kubaini ukweli.

Kadhalika, Mnyika aliitaka NEC kushughulikia suala hilo haraka na kutishia kuwa wasipotoa majibu ya kina ndani ya siku tatu, atashauri wanachama wenzake kuishinikiza ifanye hivyo ili kuondoa shaka iliyopo.

Hata hivyo, Mnyika aliyasema hayo kabla ya kutolewa kwa maelezo ya Kailima kuhusiana na uchunguzi walioufanya kwa mashine hizo zilizokamatwa Mikocheni.

Juzi, Chadema walipata taarifa kutoka vyanzo vyao vyao kuwa kuna mashine zinazofanana na BVR zinaandikisha watu na hivyo wakashirikiana na Polisi na NEC kuvikamata kabla ya kwenda kuvichunguza. Meneja Mawasiliano wa MM Steel, Aboubakar Mlawa, alieleza kuwa kampuni yao imeamua kuandikisha wafanyakazi wao kwa nia ya kudhibiti usalama vitendo vya wizi, na kwamba tayari walishaandikisha wafanyakazi zaidi ya 100 kati ya 900 waliokuwa wakitarajiwa kutoka kwenye viwanda vyao saba.

Visit Website