Tanzia! Waziri Kigoda aaga dunia


[video] Last Resort Rehab: Solution to drug addiction by inducing vomit


Mada ya NEC katika Mkutano na Viongozi wa Vyama vya siasa


Hotuba ya Jaji Lubuva ya kufungua Mkutano wa NEC na Viongozi wa vyama vya siasa
HOTUBA YA UFUNGUZI YA MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KATIKA MKUTANO WA TUME NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA KATIKA UKUMBI WA NEW AFRICA HOTEL TAREHE 12/10/2015.

Viongozi wa Vyama vya Siasa,
Mheshimiwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa Ya Uchaguzi,
Waheshimiwa Makamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,
Mkurugenzi wa Uchaguzi,
Inspekta Jenerali wa Polisi,
Msajili wa Vyama vya Siasa,
Viongozi wa Serikali,
Watendaji wa Mradi wa Uimarishaji wa Demokrasia (DEP),
Watendaji wa Tume,
Waandishi wa Habari,
Mabibi na Mabwana.

Kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, napenda kuchukua nafasi hii kuwakaribisheni wote katika Mkutano huu wa kujadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ya Uchaguzi pia kupeana taarifa kuhusu maandalizi ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 25 Oktoba 2015.
Pamoja na kwamba mna majukumu mengi na ya muhimu mmetambua umuhimu wa mkutano wetu na mmekuja kuhudhuria mkutano huu kama ilivyotarajiwa. Tume imefarijika sana kukutana nanyi siku ya leo na tunawashukuru kwa moyo mliyoonyesha katika mchakato huu wa maandalizi ya Uchaguzi na wa kututhamini na kuja kuhudhuria Mkutano wetu.

Viongozi wa Vyama vya Siasa,
Pamoja na changamoto mbalimbali mnazokabiliana nazo katika kutekeleza majukumu yenu kisiasa ni ukweli ulio dhahiri, kuwa Viongozi wa Vyama vya Siasa ni Wadau muhimu wa Uchaguzi ambapo mkishirikiana kutekeleza majukumu yenu kwa ufasaha mtaleta mafanikio katika uendeshaji wa Uchaguzi.

Viongozi wa Vyama vya Siasa,
Vyama vya Siasa vina nafasi kubwa katika kuelimisha na kuhamasisha jamii, Tume inaamini kwamba ili Mpiga Kura aweze kufanya maamuzi sahihi ni muhimu kwake kupate Elimu sahihi. hivyo basi, Tume inatarajia kuona mkitumia majukwaa yenu vyema katika kuhamasishaji na kuelimishaji si tu wanachama wenu bali jamii nzima ya watanzania


Viongozi wa Vyama Vya Siasa
Kuelekea Uchaguzi Mkuu, Tume imeaandaa vituo vya kupigia kura 64,736, ambapo, Tanzania Bara ni Vituo 63, 156 na Zanzibar ni Vituo 1,580. Kila kituo kitakuwa na uwezo wa kuhudumia Wapiga Kura 450 na wasiozidi 500. Hata hivyo Kituo kinapokuwa na wapiga Kura zaidi ya 500 kinabidi kigawanywe ili viwe viwili yaani Kituo “A” na Kituo “B” na namba ya Wapiga Kura itakuwa nusu kwa nusu. Wapiga Kura wanashauriwa kwenda katika vituo walivyojiandikishia kupiga kura siku nane (8) kabla ya siku ya kupiga kura ili kuweza kujua Vituo vyao halisi vya kupigia kura. Sambamba na hilo wananchi wataweza kupata taarifa zao zilizoko kwenye kanzidata (Database) kwa kutumia simu zao za kiganjani kupitia ujumbe mfupi wa maneno ‘sms’ bila wao kulazimika kufika vituoni, namba hiyo ni *152*00# na kufuata maelekezo. Au kupitia Tovuti ya Tume ambayo ni (www.nec.go.tz)

Viongozi wa Vyama Vya Siasa,
Tume imekuwa ikifuatilia kampeni za Vyama vyenu vya Siasa, hata hivyo Tume inasikitika kuona kuwa baadhi ya Vyama vya Siasa vimekuwa vikitumia majukwaa yao vibaya. Tume kwa namna ya pekee inawaomba katika kipindi hiki kifupi kilichobaki kutumia nafasi zenu majukwaani kuelezea sera za Vyama Vyenu ili kuweza kuwasaidia wananchi kufanya maamuzi sahihi baada ya kuwa na taarifa sahihi.

Viongozi wa Vyama Vya Siasa,
Tume imekuwa ikisikia katika vyombo vya Habari malalamiko mengi kuhusu uvunjifu wa maadili ya Uchaguzi katika kipindi hiki cha kampeni, naomba nitumie nafasi hii kuwaasa viongozi wa vyama vya siasa kupeleka malalamiko yenu katika kamati za maadili na si kukimbilia katika Vyombo vya Habari kama ambavyo baadhi ya Vyama vya Siasa na Wagombea mmekuwa mkifanya.

Viongozi wa Vyama Vya Siasa
Tume inawaomba kuepuka kutoa taarifa na shutuma sisizo sahihi kuhusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi badala yake mjikite katika kufikisha taarifa zilizo sahihi na zilizokusudiwa kwa Wafuasi wenu na wananchi wote kwa jumla, na pia kuwahamasisha wananchi kujitokeza kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba 2015.

Viongozi wa Vyama Vya Siasa,
Tume imejipanga kuhakikisha kila Mpiga kura mwenye sifa za Kupiga Kura anapiga Kura yake pasipo kubughudhiwa. Ili kuhakikisha jambo hili linafanyika kwa ufanisi, Tume imetoa maelekezo kwa Makarani waongozaji vituoni kutoa upendeleo kwa watu wanaoishi na Ulemavu ili kuwasaidia waweze kupiga kura. Kwa wale wasioona Tume imeandaa kifaa maalumu cha nukta nundu ‘Tactile Ballot Folder’ ambayo itawasaidia katika upigaji kura kwa urahisi.

Viongozi wa Vyama Vya Siasa
Baadhi ya wagombea wamekuwa wakiwashawawishi Wapiga Kura wao kutoondoka katika Vituo vya Kupigia Kura baada ya kumaliza zoezi la Upigaji Kura, naomba nichukue nafasi hii kuwakumbusha kifungu cha 104 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 kinasema nanukuu
Hakuna mtu atakayefanya Mkutano siku ya kupiga kura katika au ndani ya jengo lolote ambamo upigaji kura katika Uchaguzi unaendelea, au mahali popote ndani ya eneo la mita 200 ya jengo hilo, kuvaa au kuonyesha kadi ya picha yoyote, upendeleo au nembo nyingine inayoonyesha kuunga mkono mgombea Fulani katika Uchaguzi.” mwisho wa kunukuu.

Aidha, kifungu cha 103 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 kinasema, nanukuu:
Hakuna mtu atakayeruhusiwa, katika jengo lolote ambalo upigaji kura katika Uchaguzi unaendelea, au njia yoyote inayotumiwa na umma ndani ya umbali wa mita tatu ya mlango wowote wa kuingilia katika jengo atavaa au kuonyesha au kuonyesha kadi, upendeo au nembo yoyote inayoashiria kumuunga mkono mgombea Fulani katika Uchaguzi” mwisho wa kunukuu.
Kifungu cha 5 cha Sheria ya Adhabu, Sura Na. 16 kinaeleza maana ya njia ya Umma. Nanukuu:
Public way includes any highway, market place, square, street, bridge or other way which is lawfully used by the public” mwisho wa kunukuu.

Vifungu vya Sheria zote kwa pamoja havisemi wala kutoa fursa au nafasi kwa wananchi kukusanyika, zinapiga marufuku na kukataza uvaaji wa sare, au nembo au alama za Vyama vya Siasa siku ya kupiga kura kwa umbali kati ya mita 200 na 300.

Hivyo basi ieleweke kwamba umbali huo wa mita 200 mpaka 300 sio umbali unaowaruhusu watu kukusanyika kwa kisingizio cha kulinda kura.

Hivyo niwaase Wanasiasa kuzingatia Sheria na taratibu za uendeshaji wa Uchaguzi, kuepuka lugha zozote za uchochezi zinazoweza kuleta uvunjifu wa amani na kuhatarisha maisha ya Watanzania. Aidha uzoefu unaonyesha kwamba, katika Kampeni zinazoendelea, pale ambapo wafuasi wa Vyama tofauti wanapokutana uwezekano wa kutokea vurugu ni mkubwa na sehemu nyingine vurugu zimetokea na kusababisha maafa, majeruhi na uharibifu wa mali.

Hivyo, endapo kila chama kitaamua kuwaelekeza wafuasi wake kubaki kwenye Vituo vya Kupigia Kura uwezekano wa kutokea vurugu ambazo zinaweza kupelekea kuwatisha, kuwabughudhi, kuwatia hofu na kuwasumbua Wapiga Kura ni mkubwa hivyo kuhujumu zoezi la Upigaji Kura.

Zaidi ya hayo, maelekezo yaliyotolewa chini ya kifungu cha 126 na kifungu cha 63(2) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na kifungu cha 63(2) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura 292 na kifungu2.1 cha Maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2015 yanasistiza kwamba kiongozi yeyote wa Chama cha Siasa anapaswa kuheshimu na kufuata maagizo yote ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Viongozi wa Vyama Vya Siasa
Kwa kumalizia ninapenda tena kuwashukuru wote kwa kuhudhuria Mkutano huu na Tume inaahidi kuyachukua mawazo yenu na kuyafanyia kazi yale yaliyomo ndani ya uwezo wetu ili kuweza kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwa amani na utulivu.

Baada ya kusema hayo kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, natamka kuwa Mkutano huu umefunguliwa rasmi.

Asanteni sana kwa kunisikiliza.

Today only! You have one hour to order OnePlus 2 without invite


Today, Monday, October 12, the OnePlus team has it's the first-ever OnePlus 2 open sales for one hour in four different time zones.

It means it is possible to purchase the OnePlus 2 invite-free.

If you live in North America, you still have a chance to place your order at 12:00 pm PDT​.

In India, visit the OnePlus 2 page on Amazon.in on October 13 from 8:00 am onwards and add it to your cart while supplies last.

For more information, visit the announcement at https://forums.oneplus.net


Job opportunities - Tanzania Library Services Board

Miaka 53 ya Mafanikio: Awamu ya Nne - Kikwete


Twaweza, TMF, CEO RoundTable, TAMWA waungana kwa Midahalo ya Wagombea Urais Tanzania 2015

Taarifa juu ya midahalo ya wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Oktoba 12, 2015

Kumekuwepo juhudi za asasi za kiraia na vyombo vya habari kuandaa midahalo ya wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Juhudi hizi zimefanywa kwa nyakati na namna tofauti ili kukidhi kiu ya Watanzania kuwapima wagombea hao kwa kuwauliza maswali muhimu kabla ya kuwapa ridhaa ya kuwaongoza.

Kwa sasa mashirika ya CEO Roundtable Tanzania, Tanzania Media Foundation (TMF), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), na Twaweza wameungana katika kuendeleza juhudi za kufanikisha mdahalo huu mahsusi.

Mdahalo huu utatoa fursa ya kipekee kwa wananchi kuuliza maswali muhimu kwa wale wanaoomba ridhaa yao ya kuwawakilisha na kuwaongoza. Mdahalo huu pia unawapa fursa wagombea Urais kuweka wazi ajenda zao kwa nchi yetu ili wananchi wazipime. Hivyo, tunatoa fursa kwa wananchi kuwasilisha maswali yao kwa wagombea Urais kuanzia leo hadi Ijumaa Oktoba 16. Maswali yanaweza kuwasilishwa kwa barua pepe, ujumbe mfupi wa maneno (SMS), mitandao ya kijamii au kupelekwa moja kwa moja kwenye ofisi ya asasi yoyote iliyotajwa hapo mwanzo.

Tumevialika vyama vya siasa vyenye wagombea Urais Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na wagombea ubunge wa majimbo yasiyopungua 55, kushirikisha wagombea wao wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tumevialika vyama husika kuchukua fursa hii ya kipekee na ya kihistoria kuwaonesha watanzania kuwa wako tayari kujibu moja kwa moja, maswali ya wapiga kura, na kuonesha kuwa serikali watakayounda baada ya uchaguzi itasimama bega kwa bega na wananchi.

Mpaka sasa, vyama vifuatavyo vimethibitisha ushiriki wao: Alliance for Democratic Change (ADC), Alliance for Change and Transparency - Wazalendo (ACT-Wazalendo) na Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA).

Mdahalo wa wagombea Urais umepangwa kufanyika Jumapili tarehe 18 Oktoba 2015. Tunaendelea kuwashawishi wagombea wa vyama vilivyobaki ili wathibitishe ushiriki wao kwenye tukio hili la kihistoria. Tumetuma barua rasmi kwa vyama vyote na tunawafuatilia ili wathibitishe ushiriki wao mapema iwezekanavyo.

Tutakutana na wawakilishi wa vyama vitakavyoshiriki Alhamisi tarehe 15 Oktoba 2015, ili kukubaliana sheria na kanuni za mdahalo. Tutakuwa na mkutano na wanahabari kutangaza sheria na kanuni hizo kwa wananchi siku ya Ijumaa tarehe 16 Oktoba, 2015.

--- Mwisho---

Maelezo kwa Wahariri

1.       Kuwasilisha maswali, wananchi wanaombwa watumie Twitter, Facebook au barua pepe au wawasiliane moja kwa moja na asasi mshirika yoyote, au watumie Twitter ya #Mkikimkiki, au ukurasa wa Facebook wa Mkikimkiki2015, au watume kwenye barua pepe: [email protected]

2.       Muungano huu umeanzishwa ili kuunganisha na kupanua jitihada za kuhakikisha mdahalo ya Urais unafanyika mwaka 2015. Washirika wa muungano huu ni:
·         CEO Roundtable Tanzania ni jukwaa la viongozi wa sekta binafsi Tanzania ambalo huwakutanisha kimjadala na serikali, washirika wake wa maendeleo na wadau wengine kwa lengo la kuweka mazingira mazuri zaidi kwa ajili ya kufanikiwa kibiashara na kuendeleza nchi yetu.
·         Tanzania Media Women’s Association (TAMWA) ni mtandao wa wanahabari wanawake wanaofanyakazi kuboresha maisha ya wanawake na kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu kwenye masuala ya jamii na uongozi wa kisiasa.
·         Tanzania Media Foundation (TMF) ni taasisi inayoimarisha tasnia ya habari nchini ili kuleta uwajibikaji na utawala bora kupitia uandishi wa habari za uchunguzi na zenye maslahi ya umma.
·         Twaweza inafanya kazi ya kuwezesha watoto kujifunza, wananchi kushiriki kuleta mabadiliko na serikali kuwa wazi zaidi na sikivu katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.

Twaweza, TMF, CEO RoundTable, TAMWA team up for Presidential Debates in Tanzania 2015

Statement on Presidential Debates

Monday October 12, 2015

In 2015, there have been a number of efforts and attempts by various media and civil society organisations to hold debates for candidates for the post of President of the United Republic of Tanzania. These attempts have made use of different strategies and approaches to respond to the strong desire among citizens for presidential debates.

The CEO Roundtable, Tanzania Media Foundation, Tanzania Women’s Media Association and Twaweza have come together to continue this work and ensure that presidential debates are held this year.

The debate will provide a historic opportunity for citizens to ask questions directly to those who seek to represent and govern them. The debate also provides a platform for presidential candidates to lay out their agendas for the country in an interactive environment. We call on all citizens to submit questions on the issues that matter most to them and to assess which candidate can really represent them and address their concerns. We invite citizens to submit their questions to presidential candidates by Friday 16 October. Questions can be submitted by email, SMS, on social media or directly to the offices of any of the coalition partners.

We have invited those political parties that are fielding candidates for both the Zanzibar presidency and the Union presidency, as well as fielding candidates in at least 55 constituencies across Tanzania, to participate in the debate through their official presidential candidates.

The following parties have confirmed participation so far: Alliance for Democratic Change (ADC), Alliance for Change and Transparency – Wazalendo (ACT-Wazalendo) and Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA).

We also call on all invited political parties to use this historic opportunity to show citizens that they are ready and willing to engage in a direct dialogue with the electorate and to demonstrate that their government will stand side by side with citizens.

The debate is scheduled for Sunday 18 October and preparations are ongoing. We are also continuing to reach out to the remaining parties to confirm their participation in this historic event. Thus far letters have been sent to all parties and attempts made to confirm their participation at the earliest opportunity.

We will meet party representatives on Thursday October 15 to agree the rules and regulations for the debate on Thursday 15 October. A press conference to announce these rules to citizens and observers will be held on Friday 16 October.

--- Ends---

Notes to editors

1. To submit questions, citizens are invited to post use Twitter, Facebook or email to communicate directly with any of the members of the coalition, or to use the #Mkikimkiki on Twitter, or the Mkikimkiki2015 Facebook page, or to email [email protected].

2. This coalition has come together to harmonise and expand efforts to ensure that presidential debates are held in 2015. The coalition’s members include:

a. The CEO Roundtable is a forum through which industry leaders within the Tanzanian private sector can constructively engage with government, its development partners and other stakeholders with a view to creating a more conducive environment for business to prosper and for the country to develop.

b. Tanzania Media Women’s Association is a network of female media personnel which work on improving the lives of women and ensuring their participation in community and political leadership.

c. Tanzania Media Foundation works to strengthen the media in Tanzania in order to increase accountability and improve governance, by enabling investigative and public interest journalism and facilitating critical reflection and learning.

d. Twaweza works on enabling children to learn, citizens to exercise agency and governments to be more open and responsive in Tanzania, Kenya and Uganda.

Miaka 53 ya Mafanikio: Awamu ya Kwanza - Nyerere