21 job opportunities at the Tanzania Minerals Audit Agency (TMAA)

Job opportunities at TRA for Tanzanians

The Tanzania Revenue Authority (TRA) was established under The Tanzania Revenue Authority Act (Revised Edition of 2006). The Authority is a semi-autonomous agency of the Government of Tanzania responsible for the administration of the Central Government taxes as well as several non-tax revenues.

The functions of TRA include among others, assessing, collecting and accounting for all Central Government Revenue; Administering effectively and efficiently all the revenue laws of the Central Government; Advising the Government on all matters related to fiscal policy; Promoting voluntary tax compliance; Improving the quality of services to the tax payers; Counteracting fraud and other forms of tax evasion and Producing trade statistics and publications.

TRA’s ambition is to become an efficient, customer-focused and people-centred organization comparable with its counterparts in the emerging economies. To achieve this, the Authority is basically guided by three strategic themes namely Convenience; Compliance and Continual Improvement.

TRA is seeking to recruit dynamic, strategic, experienced and qualified Tanzanians with strong credentials to fill positions in Customs and Excise and Human Resource and Administration Departments. Applications are therefore invited from suitably qualified Tanzanians for the following positions.

Miaka 53 ya Mafanikio: Awamu ya Tatu - Mkapa (1995 - 2005)


Balozi Mwapachu: Najivua uanachama wa CCM

Balozi Mwapachu Juma Volter
Balozi Mwapachu

TAMKO RASMI LA BALOZI JUMA V. MWAPACHU

NAJIVUA UANACHAMA WA CCM

Ndugu zangu,

Kesho ni siku muhimu katika kalenda ya Taifa letu. Tunamkumbuka marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyetutoka miaka 16 iliyopita. Nadhani ni siku mwafaka kwangu kufanya maamuzi magumu katika maisha yangu ambayo yanahusu uanasiasa wangu. Mimi ni mwanachama wa CCM tangu mwaka 1967 wakati nilipojiunga na TANU Youth League. Nimepata fursa ya kuwa kiongozi ndani ya Chama hiki. Lakini kuanzia kesho mimi si mwanachama wa CCM tena. Natoa maelezo yafuatayo:

Kwa kipindi chapata mwezi na nusu hivi sasa mmekuwa mkisoma makala zangu kuhusu msimamo na mwelekeo wangu katika masuala ya siasa za hapa nchini hususan kuhusu uchaguzi mkuu na mstakabali wa demokrasia nchini mwetu. Nyote mnatambua kwamba kuanzia mchakato wa kumpata mgombe wa Urais ndani ya CCM kule Dodoma, ambako nilipiga kambi, sijayumba katika msimamo wangu kwamba Edward Ngoyai Lowassa ndiye chaguo langu katika kampeni za kumpata Rais mpya wa Taifa letu.

Chaguo langu si ndoto wala mlipuko wa mapenzi juu ya Lowassa. Nimemfahamu Lowassa tangu miaka ya 90 nikiwa cadre wa Chama cha Mapinduzi kwa mahusisho katika majukumu ya Kichama. Lowassa amejaaliwa nuru na uwezo wa kuongoza na wa kupendwa na watu. Ni msikivu pamoja na kwamba ni kiongozi asiyependa ukiritimba na utovu wa nidhamu, iwe kwa upande wa watumishi au wananchi wenyewe. Kubwa kwake ni ucha Mungu wake ambao unamsaidia sana katika uongozi unaojali na kuheshimu utu, ukweli na uwazi. Wanaodhani au kutaharuki kwamba eti anaweza au ana hulka ya kulipiza kisasi kwa jambo lolote lile ni waongo; wanajilinda.

Lowassa ni chaguo la wengi na CCM, katika busara yake ya kumuengua katika mchakato wa kumpata mgombea wa Urais, kimedhihirisha kutokuwa Chama kinachoendeshwa kwa misingi ya demokrasia. Dalili za Chama hiki kupoteza lengo la kuwa Chama cha watu, na kuwa cha viongozi wachache zilianza siku nyingi na hasa katika kipindi cha uongozi wa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. CCM kimebadilika na kuwa Chama cha makundi na migawanyiko yakupambana, si kwa malengo ya itikadi na ujenzi wa Chama, bali ya kumalizana na kutaka kufukuzana.

Lowassa angeweza kufukuzwa miaka mingi tu iliyopita! Aliweza kushinda vita hivyo kutokana na kupendwa na wengi ndani ya CCM. Hivyo, kujitoa kwake uanachama wa CCM hivi karibuni ni sahihi kabisa kwasababu CCM si Chama tena cha watu. Kimetekwa. Na mimi nakubaliana na msimamo wa Lowassa na hao waliyofuata kutoka nadani ya CCM.

Niliwahi kuandika makala katika ukurasa huu nikimnukuu mshairi mmoja wa Uingereza aliyeandika kwamba, ‘there comes a time when the door opens and allows the future in’. Mlango huo sasa umefunguka usoni mwangu na huu uamuzi wangu maana yake ni kukubali kwamba wakati mpya umewadia; ni wakati wa mabadiliko. Kuendelea kujihisi kwamba ningali mwana CCM wa kadi ni kukubali kujidanganya mwenyewe. Si sawa. Kama marehemu Baba wa Taifa alivyowahi kusema, ‘CCM si mama yangu’.

Hivyo ndugu zangu, kuanzia kesho mimi si mwana CCM tena. Nitarejesha rasmi kadi yangu kupitia ofisi ya CCM ya kata yangu Mikocheni, Dar-es-Salaam. Kwa sasa sijaamua kujiunga na Chama kingine.

Mwenyezi Mungu anilinde.

UPDATE - Oktoba 15, 2015Balozi Mwapachu (kulia) akikabidhi kadi yake ya uanachama wa CCM kwa Katibu wa Siasa na Uenezi CCM, mtaa wa Mikocheni A, Sudi Odemba.Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kada wa CCM, Balozi Juma Mwapachu leo amerudisha kadi ya uanachama katika ofisi za CCM Kata ya Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Amesema anajiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kwamba baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 atatangaza chama anachojiunga miongoni mwa Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF na NLD vinavyounda umoja huo.

Mwapachu amesema haoni sababu ya kutaja chama hicho sasa kwa vile lililo muhimu kwao hivi sasa ni umoja miongoni wanamabadiliko si kujipambanua katika imani ya chama cha siasa hakuwezi kuwa na tija kwa umoja huo.

Amesema Lowassa anakwenda kuwa Rais wa Wanaukawa wote, hivyo watu wote wanaoamini katika mabadiliko ndani ya vyama hivyo wanapaswa kuwa wamoja kwa kuuwezesha umoja huo kuibuka na ushindi.

Akizungumza baada ya zoezi hilo, Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM mtaa wa Mikocheni A, Sudi Odemba amesema chama chake hakitapata madhara yoyote kutokana na hatua ya Balozi Mwapachu kijiengua na kutangaza kujiunga Ukawa.

Amesema Mwapachu hakuwa mwanachama aliyejitoa kukisaidia chama katika siku za karibuni na kwamba hajawahi kushiriki mikakati thabiti ya kukipatia CCM ushindi katika ngazi ya mtaa japo chama hicho kiliweza kuibuka na ushindi wa kishindo.

Jumanne wiki hii, Balozi Mwapachu alitangaza kujitoa CCM akikituhumu kukiuka misingi ya kidemokrasia wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais Julai mwaka huu ambapo Dk John Magufuli alichaguliwa huku mgombea anayeamini kuwa na maono ya kiuongozi kwa Tanzania ijayo, Edward Lowassa akikatwa.

Tamko la Mwanasheria kuhusu kutekwa mgombea Ubunge, Joel Nanauka

TAMKO KUHUSU UTEKWAJI NYARA WA MGOMBEA MBUNGE JIMBO LA MTWARA MJINI KUPITIA CHADEMA Ndugu JOEL ARTHUR NANAUKA
http://2.bp.blogspot.com/-7DHom55RgeI/Vdwf2pwUQSI/AAAAAAAAEyQ/GHxftyGY46c/s1600/122.jpg
Ndugu wanahabari, wananchi wa jimbo la Mtwara Mjini na watanzania kwa ujumla: ninaitwa Raymond Mwakasitu. Ni mwanasheria na mshauri wa Ndugu Joel Arthur Nanauka ambaye ni Mgombea ubunge Jimbo la Mtwara Mjini kupitia CHADEMA. Nimeamua kutoa tamko rasmi kwa niaba ya mteja wangu, ambaye siku chache zilizopita alipatwa na tukio la kinyama, baya, na la udhalilishaji wa utu wake.
Utangulizi
Naomba nianze tamko langu kwa utangulizi mfupi juu ya kilichotokea bila kuingilia taratibu za kiuchunguzi ambazo ninaamini zinaendelea chini ya Jeshi la Polisi. Mteja wangu, Ndugu Nanauka, alipatwa na tukio ambalo kwa mazingira ya kutokea kwake, maelezo yake, na hali aliyokutwa nayo, tunaamini kwamba alitekwa kwa lengo ya kuutishia maisha na uhai wake. Ndugu Nanauka alitekwa nyara siku ya tarehe 5/10/2015, kuteswa, na  kutelekezwa baada ya masaa kama 36 na watu wasiojulikana.

Siku ya tukio, mteja wangu, baada ya shughuli za kampeni, alielekea nyumbani majira ya saa kumi na mbili jioni kwa ajili ya mapumziko. Majira ya saa kumi na mbili na nusu, Ndugu Nanauka aliaga kwa meneja wake wa kampeni (Bi Anna Deo), kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu (SMS), akimtaarifu kwamba anakwenda kuonana na mtu ambaye amekua akihitaji kuonana nae kwa muda wa kama wiki mbili hivi bila mafanikio kutokana na ugumu wa ratiba zake.
Hata hivyo, masaa yalizidi kwenda pasipo mteja wangu kurudi nyumbani jambo lililoleta mashaka na hivyo kutaka kujua kulikoni. Alipotafutwa kwa njia ya simu yake ya mkononi haikua inapatikana hewani na hiki kikaleta mashaka zaidi. Meneja wake wa kampeni alinitaarifu kuhusu kutoonekana kwake majira ya kuelekea saa nne usiku. Taratibu za kisheria zinahitaji taarifa zitolewe kituo cha Polisi yanapokua yamepita masaa 24 tangu mtu inayehisiwa kapotea, alipoonekana kwa mara ya mwisho. Hivyo basi, nilishauri waendelee kuvuta subira kidogo kabla ya kutoa taarifa. Hata hivyo, kwa kutambua nafasi ya mteja wangu kama mgombea ubunge na ukweli kwamba hakua  na kawaida ya kutoka nyumbani usiku au kwenda mahali bila taarifa, niliwashauri waende kutoa taarifa kituo cha polisi ilipofika majira ya saa sita usiku. Mteja wangu amekua akizingatia tahadhari zote za kiusalama hivyo asingeweza kwenda mahali pasipo taarifa sahihi, tena akiwa mwenyewe, na simu yake ikiwa imezimwa.
Mteja wangu alitafutwa usiku ule wa Jumatatu ya tarehe 5 na siku iliyofuata bila mafanikio. Siku ya Jumatano tarehe 7/10/2015 majira ya saa kumi na mbili asubuhi  alipatikana akiwa ametelekezwa kwenye kituo cha afya kiitwacho Bursa Clinic pale Mtwara mjini. Ndugu Nanauka alikua taabani, hajitambui, amechafuka, shati lake limechanika na akiwa hana nguvu kabisa. Alipatiwa huduma ya kwanza kwenye kituo hicho na baadaye kuhamishiwa hospitali ya mkoa ya Ligula. Kutokana na hali aliyokua nayo, na ukweli kwamba usalama wa afya yake haukufahamika, ilionekana ni vema akapatiwa matibabu na vipimo vya hali ya juu zaidi ili kunusuru maisha yake. Hivyo basi, alihamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipopetibia kwa siku kadhaa. Tukio hili ni la kinyama, la kudhalilisha na limeleta masikitiko na hamaki kubwa kwa ndugu za mteja wangu na wana mtwara kwa ujumla wao.

Hali iliyokuwepo kabla ya Kutekwa kwa Ndugu Nanauka
Siku chache kabla ya tukio nililolieleza hapo juu, mteja wangu, familia yake, na hata baadhi ya watu walio katika timu yake ya kampeni, walipata vitisho vilivyoonesha kwamba kuna njama zilizokua zinafanywa dhidi yake. Kwa mfano, watu kadhaa walio karibu na mteja wangu walipokea simu za vitisho dhidi ya uhai wao. Pia walitishwa kwamba mali zao zingeharibiwa. Mzazi wa mteja wangu (Mzee Nanauka) alitishiwa kwamba nyumba yake  ingechomwa moto.

Kama vile haitoshi, nakumbuka siku ya tarehe 3 meneja wa kampeni za Joel (Bi Anna Deo) alinitaarifu kwamba alipokea simu ya vitisho toka kwa mtu aliyemtaja kwa jina na nilimshauri atoe taarifa kituo cha polisi. Bi Anna alitoa taarifa na upelelezi ulifanyika na mhusika huyo alikamatwa na jeshi la Polisi. Nimeeleza haya yote ili tuone picha halisi ya tukio zima lililompata mteja wangu. Mazingira haya yanaonesha kila dalili kwamba alitekwa nyara kama mwendelezo wa mfululizo wa vitisho alivyokua kavipata dhidi ya usalama wake.

Mwenendo wa Uchunguzi wa tukio
Nimekua nikifuatilia mwenendo na taarifa ya upelelzi/uchunguzi wa tukio zima ili nikiamini kwamba wale waliohusika na unyama na udhalilishaji huu wanafikishwa mbele za haki kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.  Taarifa za mwanzo zilizotolewa na jeshi la polisi, akiwemo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe, zimenukiliwa zikisema polisi wanachunguza tukio ili kubaini kama kuna ukweli. Kauli za polisi zinaoenesha kwamba tayari wana mashaka na uhalisia wa tukio la kutekwa kwa Ndugu Nanauka kutokana na maelezo kwamba kumekuwepo na tetesi zinazoonyesha huenda tukio hilo lilipangwa kutokana na mazingira ya kutoweka kwake hadi kupatikana akiwa katelekezwa kituo cha afya.

Nikiwa kama mwanasheria, maelezo haya ya jeshi la polisi yamenishangaza kwani nilitegemea polisi wafanye kazi yao kikamilifu na kuthibitisha kilichotokea badala ya kuanza kueleza hisia na tetesi za tukio. Uhai na usalama wa Ndugu Nanauka (kama ilivyo kwa mtanzania yoyote yule) ni jambo la kupewa uzito na umuhimu unaostahili. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (ibara ya 14) inaweka wazi kwamba, “kila mtu ana haki ya kuishi na kupata kwa jamii hifadhi ya maisha yake kwa mujibu wa sheria”.
Maelezo ya polisi na kile ambacho kimeandikwa baadhi ya vyombo na mitandao ya kijamii, yanatoa picha kwamba mteja wangu anahusika na kutekwa kwake. Jambo hili limeibua maswali mengi kwa wananchi wa Mtwara na umma kwa ujumla kujiuliza inawezekanaje mtu akafanya njama za kutekwa kwake na kufanyiwa unyama kuhatarisha maisha yake. Ninasikitika kwamba taarifa hii ya awali ya jeshi la Polisi, imepelekea watu wengi kuamini kwamba mteja wangu hakutekwa bali kafanya ujanja wa  kujiteka ili kujitafutia umaarufu wa kisiasa.
Kama vile haitoshi, baadhi ya vyombo vya habari vimekua vikiripoti tukio hili kwa mwelekeo huohuo ambao ni wa kupotosha na kudhalilisha huku ukisababisha maumivu ya kihisia kwa mteja wangu, familia yake na wananchi walioguswa na tukio hili. Vyombo vya habari vinapotoa taarifa yenye kuleta maswali au inayoonyesha kuegemea upande mmoja (hasa kwa tukio lenye utata kama hili), kuna uwezekano mkubwa wa kuleta machafuko au migongano isiyo ya lazima katika jamii hasa kipindi hiki cha kulekea uchaguzi mkuu ambapo kuna hali ya taharuki (tension) katika jamii. Taarifa hizi zenye kuonesha mkanganyiko wa tukio zinatolewa na jeshi la polisi na vyombo vya habari, bila kuzingatia kwamba mteja wangu na walio karibu naye, walishapata vitisho dhidi ya usalama wao na taarifa zilishatolewa polisi na kupelekea mmoja wa wahusika kukamatwa. Nilitegemea msingi huo wa taarifa za awali, utumike kuharakisha na kurahisisha uchunguzi wa tukio hili badala ya kuanza kulielezea kwa hisia kwamba hakuna ukweli katika tunachoamini kilichompta mteja wangu.  

Tukio la Kutekwa na Uhusiano wake na Uchaguzi:
Siku moja baada ya Ndugu Nanauka kupatikana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara alinukuliwa kupitia taarifa ya habari ya saa mbili usiku katika kituo cha ITV akisema kwamba, kuna utata katika tukio lililompata mteja wangu. Katika maelezo yake, alisema kwamba, kuna maelezo kwamba mteja wangu alishatangaza kujitoa kugombea ubunge Mtwara. Kama vile haitoshi, alisema kwamba mteja wangu, alitangaza kumuunga mkono mgombea wa CUF siku mgombea wa urais kupitia UKAWA (Mh Lowasa) aliopofika Mtwara. Maelezo haya yanashangaza na yanaibua maswali:
 • Nani aliyemtaarifu kamanda wa polisi kwamba mteja wangu alisema anamuunga mkono mgombea wa CUF?
 • Pili, Na kama aliambiwa, alitafuta uthibitisho wa alichoambiwa?
 • Tatu, hata kama mteja wangu alitangaza hivyo au la, hicho kinausikaje na usalama wake na uchunguzi wa kutafuta ukweli kuhusu kilichompata?

Ukweli ni upi?
 • Jimbo la Mtwara Mjini kama yalivyo baadhi ya majimbo mengine Tanzania bara, umoja wa vyama vinavyounda UKAWA, vilishindwa kuafikiana ni chama gani shiriki kisimamishe  mgombea kutokana na sababu kadha wa kadha. Hivyo, hadi mteja wangu anapatwa na tukio la kutekwa, vyama vya CUF, NCCR na CHADEMA vilikua na wagombea katika jimbo hili tofauti na maeneo mengine ambapo wamesimamisha mgombea mmoja.
 • Hata hivyo mteja wangu, tofauti na wagombea wenzake, na kwa kuheshimu makubaliano ya vyama husika, na kwa kuelewa kwamba viongozi wa juu wa UKAWA walikua bado wanaendelea na mazungumzo ya kutafuta muafaka; hajawahi kufanya kampeni kama mbunge na badala yake amekua akiwasaidia kampeni wagombea wa udiwani katika jimbo hilo.
 • Baada ya kuona muda unasogea sana bila muafaka na ukweli kwamba uchaguzi unakaribi sana; ukichanganya na hali ya kisiasa ilivyokua na kwa kauli zisizo na staha za wagombea wenzake, hakutamani kuona umoja wao unashindwa katika jimbo hili kwa kukosa muafaka. Kwa nia njema kabisa, aliamua kutangaza kujitoa kwenye kinyang'anyiro hicho ili kunusuru UKAWA. Hii ilikua ni siku kama nne kabla ya kutekwa kwake.
 • Hata hivyo, chama chake (CHADEMA) kupitia viongozi wake wa Mtwara na kwa maagizo ya uongozi wa Taifa, baada ya kauli yake, kilimtaka kuendelea na kampeni kwani walikubaliana na wenzao kwamba majimbo waliyokosa muafaka kila chama kiendelee kusimamisha mgombea wake. Hivyo hakua na sababu ya kujitoa. Pia wananchi wengi wa Mtwara walionesha kutokukubaliana naye na walinukuliwa kwenye vyombo vya habari wakilalamika na kumtaka arudi wenye uchaguzi kwani wao ndio watakaofanya maamuzi.
 • Siku mteja wangu alipotekwa, ndio siku alikokua amerudi rasmi kwenye kampeni kama alivyoagizwa na chama chake na kwa kutii matakwa ya wananchi wa Mtwara.
 • Siku ambayo mgombea Urais wa UKAWA alipofika Mtwara, kulikua na mikutano ya ndani kati ya wagombea wote watatu pamoja na viongozi wa UKAWA waliotoka makao makuu kutafuta mwafaka. Hata hivyo, mwafaka haukupatikana na mgombea Urais hakutoa kauli ya mwisho ya nani ni mgombea ubunge wa Mtwara bali aliwaita jukwaani wagombea wote watatu. Mteja wangu hakutangaza katika kikao cha ndani wala katika mkutano wa kampeni kwamba anamuunga mgombea mwingine mkono. Alichokisema na ambacho amekua akikisema siku zote kabla hata ya kuchukua fomu ni kwamba, yeye atakua tayari kumuunga mkono mgombea yeyote atakayeteuliwa na UKAWA iwapo haitakua ni yeye. Kauli iliyotolewa na polisi kwamba alitangaza kumuunga mkono mgombea mwenzake wa CUF siku Mh Lowasa alipokwenda Mtwara, sio ya kweli na ni ya upotoshaji. Tunajiuliza, nini malengo ya kauli hii katika mazingira ya kutekwa kwa mteja wangu?

Hivyo basi, nawasihi Jeshi la Polisi Mtwara, kuchukulia tukio la kutekwa mteja wangu kwa umuhimu na uzito wake na lione wajibu wa kufuatilia na kuchunguza kwa umakini mkubwa ili kupata ukweli. Jeshi la polisi zichukulie taarifa zozote zinazoashiria kutokuwepo kwa usalama wa raia, akiwemo mteja wangu. Mteja wangu, akiwa kama mgombea ubunge, anastahili kupatiwa ulinzi dhidi ya chochote kile kinachohatarisha maisha na uhuru wake. Kitendo alichofanyiwa, kimepelekea mteja wangu kujiona hayupo salama na hivyo kumuweka katika wakati mgumu kisiasa na hata maisha yake ya kawaida kama raia mwema wa nchi yake.

Ukweli ni kwamba, Ndugu Nanauka hakujiteka bali alitekwa na watu waliokua na dhamira ovu dhidi yake.  Walilenga kumwathiri, kumwondolea ujasiri na kumpotezea imani kwa wapiga kura wa Mtwara ili aonekane ni kiongozi asiyeaminika. Taarifa nyingine yoyote ile, ina lengo la kupotosha ukweli wa tukio hili na kulifanya lionekane halina uzito, ni la kizushi na kupuuzwa. Jambo hili lina lengo la kushusha hadhi na heshima yake katika jamii kama kiongozi wa kisiasa. Kwa wanaomfahamu mteja wangu, wanatambua kwamba ni mtu mwaminifu na mwadilifu katika jamii. Amefanya kazi nyingi na amekua kiongozi maeneo mengi kwa uaminifu mkubwa usiotiliwa shaka. Hana haja yoyote ya kujitengenezea tukio la kutekwa ili kujiongezea umaarufu wa kisiasa au kutafuta huruma ya mtu yeyote yule. Pamoja na mambo mengine,mteja wangu, kupitia taasisi yake, amesaidia kusomesha vijana wa Mtwara zaidi ya mia tatu tangu mwaka 2008. Uongozi anaoutafuta kama mbunge, una lengo la kuendeleza dhamira na nia yake njema ya kuwatumikia wananchi wa Mtwara na watanzania kwa ujumla wao, na sio vinginevyo.
Hitimisho:
 • Kama mwanasheria wa Ndugu Nanauka, ninalaani vikali kitendo alichofanyiwa mteja wangu na ninawasihi Jeshi la polisi litimize wajibu wao na kuwachukulia hatua wahusika. Hali kadhalika, ninaliomba jeshi la polisi Mtwara, litoe taarifa kamili na ya kueleweka kuhusyu mteja wangu na kuuambia umma nini kilitokea.
 • Pili, ninalaani vikali taarifa zozote zinazosambazwa juu ya mteja wangu kwamba alipanga kutekwa kwake kwa sababu za kisiasa. Wanaosambaza habari hizi, ni watu wasio na huruma wala utu kwa kushindwa kuthamini usalama na uhai wa mteja wangu
 • Kwa kua afya ya mteja wangu inazidi kuimarika, ni matarajio yangu kwamba ataendelea na kampeni za ubunge siku chache zijazo kama atakavyoshauriwa na watabibu. Hivyo niwatoe hofu na shaka wananchi wa Mtwara Mjini juu ya ushiriki wake katika uchaguzi. Mgombea wao bado anashiriki uchaguzi huu na ataendelea na kampeni hadi dakika ya mwisho. Ikimpendeza Mungu, atashinda na atawaongoza katika kujiletea maendeleo ya jimbo lao.

Kwa niaba ya mteja wangu, familia yake, na wananchi wenye mapenzi mema, tunamshukuru Mungu kwamba hali ya afya ya Ndugu Nanauka inaendelea vema, imeimarika na Mungu ameuhifadhi uhali wake ambao ni wazi ulikua kwenye hatari ya kupotea. Ninawashukuru wote waliompa msaada wa hali na mali pamoja na watabibu waliomsaidia kwa utaaalamu wao kuhakikisha anapona.

Mungu awabariki

Raymond Mwakasitu   
Mshauri na Mwanasheria wa Ndugu Joel Nanauka

Tarehe 13/ 10/ 2015

Miaka 53 ya Mafaniko: Awamu ya Pili - Mwinyi (1985 - 1995)


Wagombea Ubunge wa CHADEMA wanusurika kifo ajalini


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kahama kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh James Lembeli na Joyce Mukya wamenusurika kifo mara baada ya gari waliokuwa wakitumia kusafiria kutoka Simanjiro kuelekea Arusha, kupata ajali na kupinduka.

Picha: Massawe

Tanzania, Uganda zasaini MoU kutekeleza usafirishaji mafuta ghafi

Kutoka Kushoto - Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Nishati na Madini (Uganda), Dkt. Fred Kabagambe Kaliisa na Meneja Mkuu wa Total E&P Uganda, Ndg. Adewale Fayemi wakipongezana baada ya kutia saini Hati ya Makubaliano (MoU) baina ya Serikali ya Uganda na Tanzania juu ya utekelezaji wa mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda (Kabaale) mpaka bandari ya Tanga (Tanzania). 

SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA (TPDC)

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Uganda, TPDC na Total E&P Uganda wametia saini Hati ya Makubaliano juu ya utekelezaji wa mradi wa kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda kupitia Tanzania.

Hati hii ya Makubaliano inafungua fursa kwa Serikali hizi mbili kufanya kazi kwa pamoja kuangalia uwezekano wa kuendeleza mradi wa kusafirisha mafuta ghafi kutoka Kabaale Uganda kupitia Tanzania mpaka bandari ya Tanga. Makubaliano haya pia yanatambua faida zaidi zitakazopatikana kwa Tanzania na Uganda ambazo ni zaidi ya utekelezaji wa mradi huu. Vilevile makubaliano haya yanatoa muongozo kwa pande zote zinazohusika kuendelea kufanya kazi kwa pamoja kuboresha tafiti zilizo kwisha fanyika juu ya njia ya Tanga.

Akiongea baada ya kusaini hati hiyo, Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava alisema “Tanzania na Uganda wana historia ndefu ya ushirikiano na mradi huu utazidi kuboresha ushirika kati ya nchi hizi”. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio aliongeza kuwa, TPDC ina uzoefu wa muda mrefu katika ujenzi, uendeshaji na utunzaji wa bomba na hivyo uzoefu huu utasaidia sana katika utekelezaji wa mradi huu. Wiki hii, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alifungua rasmi mradi wa bomba la gesi la kilometa 542 kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam unaomilikiwa na kuendeshwa na TPDC.

Imetolewa na;

Mkurugenzi Mtendaji,
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania,
S.L.P 2774,
Dar-es-Salaam.
Tanzania
www.tpdc-tz.com

Mbio za Kombe la Dunia 2018: Tanzania na Algeria kuchuana Novemba 14 jijini Dar

Mchezo wa hatua ya pili kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia ziakazofanyika mwaka 2018 nchini Urusi kati ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Algeria (The Fox Desert) utafanyika tarehe 14 Novemba, 2015 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Taifa Stars inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager itacheza mchezo huo dhidi ya Mbweha wa Jangwani siku ya Jumamosi Novemba 14, na mchezo wa marudiano kuchezwa siku tatu baadae Algeria 17 Novemba, 2015.

Kikosi cha Stars chini ya Kocha Mkuu Charles Mkwasa kimefanikiwa kusonga hatua ya pili ya michuano hiyo baada ya kuiondosha Malawi (The Flames) kwa jumla ya mabao 2-1, nyumbani ikishinda 2-0, na kufungwa 1 – 0 jijini Blantyre.

Tanzia! Mkuu wa Mkoa aliyekuwa likizo ya ugonjwa

Paschal Kulwa Mabiti, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu, amefariki dunia kwa ugonjwa wa saratani.

Taarifa imetolewa na mkuu wa mkoa wa Simiyu, Elaston Mbwilo.

Mkuu huyo wa Mkoa ambaye alikuwa katika likizo ya ugonjwa alifariki nyumbani kwake Dar es Salaam na mwili wake unatarajiwa kuzikwa kesho kutwa.

Mtangazaji redio amwua Polisi wakigombea penzi la Mwanafunzi

AskariPolisi wa mjini Babati, Mkoa wa Manyara ameuawa kwa kuchomwa kisu na mtangazaji mmoja wa redio kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Baadhi ya wakazi wa Babati walisema jana kuwa wanaume hao walikuwa wakimgombea mwanafunzi wa kidato cha pili walipokuwa baa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Christopher Fuime alimtaja aliyeuawa kuwa ni Rashid Haruna (30) mwenyeji wa Mkoa wa Njombe. Kamanda Fuime alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 5.30 usiku eneo la Kitalu X.

Alisema Polisi wanamshikilia mwanafunzi huyo wakati uchunguzi zaidi kuhusu mauaji hayo ukiendelea. Kamanda Fuime alisema baada ya mtangazaji huyo kumchoma kisu askari huyo alikimbilia sehemu za Dareda.

“Kabla ya kifo chake alichomwa kisu mara 15 sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwamo mikononi, mgongoni, ubavuni na eneo la moyo,” alisema Fuime.

Kamanda Fuime alisema mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda wilayani Makete Mkoa wa Njombe kwa maziko.

Awali askari ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema siku ya tukio polisi huyo alimkuta msichana baa akiwa analumbana na mtangazaji. Alisema msichana huyo alimuomba askari ambaye ni mpenzi wake amsaidie kwani anang’ang’aniwa na mtu asiyempenda.

Taarifa ya Wizara leo Oktoba 13 kuhusu Mahujaji

Taarifa zaidi kuhusu Mahujaji kutoka Tanzania waliofariki na kujeruhiwa huko Saudi Arabia

Mahujaji wengine wanane kutoka Tanzania ambao walikuwa hawaonekani tokea ajali ya kukanyagana kwa mahujaji ilipotokea Makkah nchini Saudi Arabia tarehe 24 Septemba 2015 wametambuliwa kuwa, ni miongoni mwa mahujaji waliofariki dunia. Kutambuliwa kwa mahujaji hao kunafanya idadi ya mahujaji wa Tanzania walipoteza maisha katika ajali hiyo kufikia ishirini (20). 

Majina kamili ya mahujaji hao na vikundi vilivyowasafirisha kwenda Makkah katika mabano ni Hamida Llyas Ibrahim (Khidmat Islamiya), Farida Khamis Mahinda (Ahlu Daawa), Archelaus Anatory Rutayulungwa (Khidmat Islamiya) na Said Abdulhabib Ferej (Ahlu Daawa).

Wengine ni Awadh Saleh Magram (Khidmat Islamiya), Salama Rajab Mwamba (Khidmat Islamiya), Nuru Omar Karama (Ahlu Daawa) na Saida Awaadh Ali (Ahlu Daawa).

Serikali ya Saudi Arabia inaendelea kutoa taarifa zaidi za mahujaji waliofariki dunia au kujeruhiwa katika ajali hiyo na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa itaendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu wahanga wa ajali hiyo kadri itakapokuwa inazipokea.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam

13 Oktoba, 2015

Maelezo ya Wizara kuhusu umiliki wa mitambo ya kuzalisha umeme

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TAARIFA KWA UMMA

Hivi karibuni zimeibuka taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zikimnukuu Waziri wa Nishati na Madini, George B. Simbachawene akisema kuwa mitambo yote ya uzalishaji umeme nchini inamilikiwa na Kampuni binafsi.

Tunapenda kuutaarifu Umma kuwa taarifa hizi ni za uongo kwani Waziri Simbachawene hajawahi kutoa tamko la kuwa mitambo ya kuzalisha Umeme yote nchini ni ya kampuni binafsi bali alichosema ni kuwa, baadhi ya mitambo ni ya kampuni binafsi na mingine inamilikiwa na Serikali.
Mitambo inayomilikiwa na Serikali ni:-
 1. Kinyerezi I (Gesi) yenye uwezo wa MW 150 ambapo MW 35 zimewashwa leo 12 Oktoba 2015;
 2. Ubungo I (Gesi) yenye uwezo wa MW 102 ambayo kwa sasa inazalisha MW 85;
 3. Ubungo II (Gesi) yenye uwezo wa MW 105 ambayo kwa sasa inazalisha MW 70;
 4. Tegeta (Gesi) yenye uwezo wa MW 42 ambayo kwa sasa inazalisha MW 42;
 5. Nyakato (Mafuta) yenye uwezo wa MW 60 ambayo kwa sasa inazalisha MW 42;
 6. Kidatu (Maji) yenye uwezo wa MW 204 ambayo kwa sasa inazalisha MW 27;
 7. Kihansi (Maji) yenye uwezo wa MW 180 ambayo kwa sasa inazalisha MW 45;
 8. Pangani (Maji) yenye uwezo wa MW 68 ambayo kwa sasa inazalisha MW 17;
 9. Nyumba ya Mungu (Maji) yenye uwezo wa MW 8 ambayo kwa sasa inazalisha MW 5;
 10. Hale (Maji) yenye uwezi wa MW 21 ambayo kwa sasa inazalisha MW 4; na
 11. Mtera (Maji) yenye uwezo wa MW 80 ambapo mitambo yake imezimwa (MW-0);
Kwa hiyo, Jumla ya kiasi cha umeme kinachopatikana katika mitambo hiyo kwa sasa ni Megawati 337 kati ya Megawati 870 zinazotakiwa kuzalishwa.

Mitambo inayomilikiwa na watu binafsi ni:-
 1. IPTL (Mafuta) yenye uwezo wa MW100 ambayo kwa sasa inazalisha MW 80;
 2. Aggreko (Mafuta) yenye uwezo wa MW 70 ambayo kwa sasa inazalisha MW 70;
 3. SONGAS(Gesi) yenye uwezo wa MW180 ambayo kwa sasa inazalisha MW 158; na
 4. Symbion (Gesi) yenye uwezo wa MW 112 ambayo kwa sasa inazalisha MW 74.
Hivyo mitambo hii ya watu binafsi inazalisha umeme wa kiasi cha Megawati 382 kati ya Megawati 462 zinazohitajika.

Ieleweke kuwa Serikali inajitahidi kuiwasha mitambo hiyo yote inayomilikiwa na Serikali na Binafsi ili izibe pengo la umeme wa maji ambao umepungua kutoka MW 561 hadi MW 88. Ili nchi isiwe na mgawo wa umeme zinahitajika MW 1332 ambapo kwa sasa kiasi cha umeme kinachopatikana ni Megawati 719.

Awali tulikuwa na upungufu wa megawati takribani 450 lakini tumefanya juhudi za kuwasha mitambo mbali mbali tangu wiki iliyopita na sasa upungufu uliobaki ni kati ya MW 200 na 250.

Serikali kupitia TANESCO inatoa rai kwa Watanzania kuendelea kuvumilia kipindi hiki cha mpito kwani inajitahidi kwa hali na mali kuwasha mitambo iliyobaki ya gesi ya Kinyerezi yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 150 hivyo hadi ifikapo tarehe 20 Oktoba, 2015 hali ya upatikanaji wa umeme itaanza kutengemaa.

Asanteni na poleni kwa usumbufu unaojitokeza.

Imetolewa na;

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Mahojiano na DC Paul Makonda katika Jukwaa LanguKipindi hiki ambacho kinakujia kila Jumatatu, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu Uchaguzi Mku wa Tanzania 2015.

Katika sehemu hii ya kipindi cha wiki hii, utasikia mahojiano yetu na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe Paul Makonda juu ya Matembezi ya Amani yaliyoandaliwa na Ofisi yake na kufanyika wilayani humo

Pia wasikilizaji walipata fursa kumuuliza maswali na hata kutoa maoni yao juu ya kinachoendelea huko

KARIBU.