Job: Administrative and Logistics Coordinator - Tanzania, Médecins du Monde

Organization: Médecins du Monde
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 28 Jan 2016

Job: Palladium International is seeking Climate Change Experts in Southern & Eastern Africa

Organization: Palladium International
Closing date: 08 Nov 2015

Job: Development and Planning Associate - ICAP

Organization: International Center for AIDS Care and Treatment Programs
Country: United States of America
Closing date: 30 Nov 2015

Internship position for a Junior Analyst

Organization: INTEGRITY
Country: United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland
Closing date: 13 Nov 2015

Job: Deputy Programme Managers - Response and Resilience Team, Oxfam GB

Organization: Oxfam GB
Closing date: 05 Nov 2015
Deputy Programme Managers (Response and Resilience Team)

Job: Camp Manager - Tanzania, Danish Refugee Council

Organization: Danish Refugee Council
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 13 Nov 2015

Job: Knowledge Management and M&E Specialist, Tanzania

Organization: Palladium International
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 05 Nov 2015

Job: Health & Nutrition Specialist, Zanzibar - UNICEF Temporary Appointment

Organization: UN Children's Fund
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 13 Nov 2015

Mwingine mahakamani kwa kusambaza ujumbe kumhusu Mkuu wa Majeshi

George Aloyce Kimaryo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kusambaza taarifa zauongo kupitia katika kundi la Adios la mtandao wa WhatsApp kuwa Mwanafunzi wa Chuo cha DIT, Benedict Angello Ngonyani amejitokeza kwa mara ya pili mahakamani na kuishangaza kwa kumtaka Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange ajitokeze na kukanusha kuwa amelishwa sumu.

Wakili wa Serikali Jacquline Nyantori akishirikiana na Wakili Mwandamizi wa TCRA, Johannes Kalungula walidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa Oktoba 13,2015 katika mtandao huo wa kijamii mshtakiwa huyo alisambaza taarifa hiyo kinyume na kifungu cha 16 cha sheria ya Mtandao namba 14 ya 2015.

Baada ya kusomewa shitaka hilo, mshtakiwa huyo alikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika na Hakimu Simba aliiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 3, 2015 kwa ajili ya kutajwa na kufikiria juu ya maombi ya dhamana.

Mwanafunzi huyo wa Chuo cha DIT, Benedict Angello Ngonyani yeye anakabiliwa na kesi ya kusambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa WhatsApp na Facebook kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange amelishwa sumu.

Tangu afikishwe mahakamani hapo kwa mara ya kwanza siku 14 zilizopita leo yaani jana ndiyo alipanda kwa mara ya pili kizimbani mbele ya Hakimu Respicius Mwijage ambapo Wakili Nyantori alidai kuwa kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wake bado haujakamilika.

Nyantori alidai katika kesi hiyo, kuwa kesi hiyo inahusisha mtandao bado wanakusanya taarifa ambazo ni za muhimu kupitia mfumo huo.

Hata hivyo wakili wa kujitegemea, Mnyela Abdallah alijitokeza mahakamani hapo na kujitambulisha kuwa yeye atakuwa wakili wa mshtakiwa huyo atakayemtetea kwenye kesi hiyo na akajulishwa kuwa mteja wake amewekewa zuio la dhamana na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Hakimu Mwijage aliuambia upande wa mashtaka kuwa uliweka zuio hilo la dhamana na kutoa sababu ndani ya siku hizo 14 na kuwaambia kuwa sasa kuna umuhimu wa kulijadili dhamana ya mshtakiwa huyo na kitu ambacho kinapelekea andelee kuzuiwa kwa dhamana yake maana lazima kuwepo na sababu hivyo aliwataka Novemba 3,2015 kesi itakapotajwa kwa ajili ya kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la, waeleze sababu.

Ngonyani amekuwa ni mshitakiwa wa kwanza kufikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka kupitia sheria hiyo mpya ya mtandao ambayo inazuia mtu yoyote kusambaza ama kuchapisha data, taarifa za uongo, uzushi na zile ambazo hazijathibitishwa ama hazina chanzo pamoja na picha za matusi katika mitandao ya kijamii.

Katika kesi hiyo, Ngonyani anadaiwa kuwa Septemba 25,2015, jijini Dar es Salaam, alisambaza taarifa za uongo kupitia mitandao ya WhatsApp na Facebook kuwa Jenerali Mwamunyange amelishwa sumu na kwamba amepelekwa Nairobi Kenya kwa matibabu wakati akijua taarifa hizo zilikuwa na lengo la kupotosha umma.

Mbali na kesi hiyo, Mshtakiwa Raia wa China, Royce Lee na raia wa Pakistani Iqbal Wasif na Mohamed Jamil wamepandishwa kizimbani mahakamani hapo wakikabiliwa na kesi tofauti za kuingiza mitambo ya kielektroniki ya mawasiliano nchini bila ya kuwa na leseni kutoka TCRA, wakaisimika na kutoa huduma za simu za Kimataifa kinyume cha sheria na kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya zaidi ya Sh 500 milioni.
  • Taarifa ya Mwene Said via blogu ya Michuzi

Magufuli ampasha Rais Kikwete naye amwambia "Sema"


Kucheza gani huku na sare za Chama?

Kule wengine walilalamikiwa 'kugawiwa viroba' huku nako hawa, watizame mwenyewe... https://youtu.be/OM0EQyXZN58

Opportunity! UK changes restrictions on nurse recruitment from overseas

UK Government announces temporary changes to restrictions on nurse recruitment from outside European Economic Area to ensure safe staffing levels across the NHS

Nurses will be added to the government’s shortage occupation list on an interim basis. This means that nurses from outside the EEA that apply to work in the UK will have their applications for nursing posts prioritised. The independent Migration Advisory Committee will review the change and present further evidence to the government by February 2016.

The move is designed to ease pressure on the NHS at a time when the government is introducing tough new controls on costly agency spending. It will help the NHS improve continuity of care for patients, invest in the frontline and maintain safe staffing levels.

Health Secretary Jeremy Hunt said:
Safe staffing across all our hospitals and care homes is a crucial priority. The temporary changes announced today will ensure the NHS has the nurses it needs to deliver the highest standards of care without having to rely on rip-off staffing agencies that cost the taxpayer billions of pounds a year.
We are also recruiting more home-grown nurses than ever to deliver a truly seven day NHS. There are already more than 8,000 additional nurses on our wards since 2010 and we are investing in our future workforce with a record 50,000 nurses currently in training.
The government is recruiting more home-grown nurses by significantly increasing training places, promoting return to practice programmes and improving retention of existing staff.

Health Education England has already increased nurse training places by 14% over the last 2 years and is forecasting that more than 23,000 additional nurses will be in place by 2019. A campaign is also being run to get experienced nurses who’ve left the profession back to work to co-ordinate plans across the health and care sector to improve the retention of nurses.

See Home Office letter and statement from the Migration Advisory Service on nurse shortages

Source: https://www.gov.uk/government/news/restrictions-on-nurse-recruitment-from-overseas-changed

Thanks for this tip via Twitter:


Hotuba ya Edward Lowassa kupitia Tv 23.10.2015


Ndugu watanzania wenzangu.

Imebaki siku moja tu kabla hatujapiga kura katika Uchaguzi Mkuu hapo tarehe 25 mwezi huu.

Is it a 'goodluck' to have Jonathan as Commonwealth Chief Observer?

Former Nigerian president, Goodluck Jonathan (right) congratulates his February elections challenger and successor, General Muhammadu Buhari (left) after announcement of results.

IS IT A “GOODLUCK” TO HAVE JONATHAN AS COMMONWEALTH CHIEF OBSERVER?


The ‘accidental’ president

Having started out humbly as a zoology professor, Jonathan ‘accidentally’ switched to politics to become Deputy then full Governor of Balyesa State, then Vice-President who would eventually inherit the throne in 2010 after the death of President Y’aradua.

Jonathan the ‘peace maker’

Although the job of Nigerian president in itself is a great achievement, we would somehow agree that Jonathan’s footprints would not necessarily be visible in his presidency of the most populous and arguably the most strongest economy in Africa rather in setting a rare precedent in the continent that an incumbent desperately seeking extension of his rule can indeed concede defeat, relinquish power peacefully and become a “Godfather” of democracy.

Switching to his current mandate as the Commonwealth Secretariat Chief Observer to Tanzania general elections, I am of an opinion that Jonathan’s role is pivotal and should not be confined to a mere observer who would just oversee the process and report back to NEC rather his role should extend to utilizing his diplomatic genius to counsel main candidates to accept outcome of polls.

Despite having distinct political and democratic history, as non-industrial countries in Sub-Saharan Africa, Nigeria and Tanzania have indeed a lot to compare in that they both pursue multiparty political systems.

Ethno-religious politics

As is the rest of Africa, Nigeria is renowned for its trademark Muslim North- Christian South political culture that have polarized a country, also known for its ethnic divide. Indeed, Jonathan’s and Buhari’s divided electorate is a typical example.

In Tanzania, we have recently witnessed some key presidential aspirants seeking votes on religious and ethnic lines too, hoping to benefit from a polarized electorate.

Security factor

We are all witnesses to the security tension brought about by the Boko Haram insurgency in Northern Nigeria around the time of elections, reaching its climax with abduction of 200 Chibok girls, pushing the polls for further six weeks. In Tanzania, security tension around Sunday elections has already been elevated by quest to guard votes outside 200-meter parameter from polling stations, a catalyst for clashes between/among party supporters and/ or security forces.

Moreover, there is a lingering security uncertainty in various potential hotspots which are traditionally violent for instance Arusha, Mbeya - Tunduma, Mwanza and Zanzibar, to mention a few.

Oil and gas factor

Like Nigeria, Tanzania elections are set on top of a stiff but covert battle for access to ‘gas billions’ in Southern Tanzania. While Nigerian elections were seen as a rare opportunity for any elected leader to have an upper hand in production sharing agreements with international oil companies (IOCs), Tanzania elections suggest that the new leader will be influential in the newly found gas wealth, set to start flowing in the second half of his first 5-year tenure (2019 or so). Foreseeing this glory, already some local business tycoons and business networks are siding with some candidates to ensure they win State House and state coffers by hook or crook.

Untested electoral technologies - BVR

Faced with a challenge of democratizing electoral systems, both Nigeria and Tanzania used Biometric Voters Register in an attempt to make voters roll more inclusive, transparent and credible despite being . If Nigeria could make it, I believe the best efforts employed by the National Electoral Commission (NEC)

in adding almost 3 Million voters in the register deserves an applause, although much has to be done to ensure electoral bodies become more independent, ending ‘unhealthy’ perception that they protect the incumbent regimes.

Pre-electoral pledge for peaceful elections

There is a lot to learn from former Nigerian president Abdisalam Aboubakar’s approach in forging a pre-election deal which compelled Jonathan and Buhari to accept outcome of elections. Whether that was a gentleman agreement or a legally binding one, at least it shows it can really work. Similarly, presidential contenders in Tanzania should sign such deals in future so as to impose a social and moral guilt on them.

NEC has played a more or less similar role at campaign level by engaging all parties to signing an MoU guaranteeing respect for electoral regulations and code of conduct. To some extent that has worked although key to it is for opposition parties to ensure they uphold democratic standards to the end by urging supporters to leave polling stations after voting.

How important is Jonathan to Tanzania

In his address to members of diplomatic corps earlier in the week, Jonathan praised Tanzania for not only upholding peace and tranquility, but also for being the symbol of democracy and stability, often exporting the rare commodity to the rest of the continent.

Indeed, his words should be an eye opener in seeing that as Tanzanians, we should not be complacent about peace but prove the world wrong in that we can emerge from these complex situations united.

Way forward

Commonwealth is no stranger to brokering peace deals in the region, Zanzibar Muafaka Accord in early 2000s is the best example. As an exemplary African statesman, a diplomatic genius and now Head of Commonwealth Election Observation Mission, Goodluck Jonathan should employ preventive measures to counsel our presidential contenders especially opposition parties to accept the outcome of elections even if it means conceding defeat. Urging supporters to go back home after voting will help avoid a catalyst for violence, prevent a potential trigger for a post-election conflict and help a seemingly divided country to rise above and move on.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania

By Victor Mlunde

The author is a Dar es Salaam - based Governance and Development Consultant with expertise in Elections, Democracy, Energy Governance and Conflict Resolution in the Great Lakes region. He can be easily reached through +255 714 289428 or [email protected]

Job: Program Associate, MSH

Organization: Management Sciences for Health
Country: United States of America
Closing date: 31 Dec 2015

BBC in Tanzania: What do Hip Hop and politics have in common?


From opposition's coalition to massive young people's involvement, this year's Tanzanian election has been described as quite exciting. But the wave of transition of artists into politics has very much seasoned the polls process.

What exactly has inspired their switch? 

BBC's Zuhura Yunus went to find out as she reports in the video.

Now you can pre-order BlackBerry's Priv: Android phone with slide out physical keyboard

BlackBerry's official online store has posted a pre-order page for the Priv, a high-end QWERTY slider phone -- the company's first full Android device -- at $699. 


Serikali yasaini mkataba na Ashok Leyland wa kununua magari ya ulinzi, usalama

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima (kulia), Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kutengeneza Magari ya ASHOK LEYLAND ya nchini India, Bhimasena Rau wakisaini Mkataba wa ununuzi wa magari kwa ajili ya matumizi ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambavyo ni Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, jijini Dar es Salaam.
Serikali ya Tanzania imeingia Mkataba wa ununuzi wa magari kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini na Kampuni ya Motorrama (T) LTD ambayo ni Wakala wa Magari aina ya ASHOK LEYLAND kutoka nchini India.

Mkataba huo umesaniwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima pamoja na Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo ya Utengenezaji wa magari, Bhimasena Rau ukishuhudiwa na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada mkataba huo kusainiwa, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja aliishukuru Serikali kwa msaada huo ambao utasaidia kutatua tatizo la uhaba wa magari katika Jeshi la Magereza.

“Utekelezaji wa mpango huu katika Jeshi la Magereza utakuwa na manufaa makubwa kwani utapunguza tatizo la uhaba wa magari kwa ajili ya shughuli za uendeshaji na utawala pamoja na utekelezaji wa jukumu la kuwasafirisha Mahabusu kwenda mahakamani na kurudi magerezani,” alisema Minja.

Lengo kubwa la ununuzi wa Magari hayo unalenga kuboresha huduma za usafiri pamoja na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama hapa nchini.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima (kulia), Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kutengeneza Magari ya ASHOK LEYLAND ya nchini India, Bhimasena Rau wakipongezana baada ya kusaini Mkataba wa ununuzi wa magari kwa ajili ya matumizi ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambavyo ni Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima (watatu kushoto), akitoa neno la shukrani baada ya kusaini mkataba wa ununuzi wa magari ya Kampuni ya ASHOK LEYLAND ya nchini India. Magari hayo ni kwa ajili ya matumizi ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Jumanne Sagini, wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wapili kulia) akipokea Mkataba wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Watumishi wa Jeshi la Magereza kutoka kwa Makamu wa Rais wa Kampuni ya Ujenzi ya Poly Technologies ya nchini China. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja. Halfa hiyo ilifanyika katika Ukumbi mdogo wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima (katikati aliyevaa tai), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wakumi kulia), Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, Jumanne Sagini (wanane kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Viongozi wa Kampuni ya Kutengeneza Magari ya ASHOK LEYLAND ya nchini India.
  • Picha zote na maelezo: Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Taarifa ya Bayi/TOC ya kumpongeza na kumshukuru Rais KikwetePONGEZI/SHUKRANI ZA TOC KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA KUENDELEZA MICHEZO KATIKA MIAKA 10 YA UONGOZI WAKE


Napenda kuchukua nafasi hii kuushukuru uongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kwa kuandaa hafla ya kutoa tuzo kwa wanamichezo 10 bora waliofanya vizuri kwa kuiletea heshima nchi yetu katika miaka 10 ya uongozi wa mwanamichezo mwenzetu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pamoja na kutoa tuzo kwa Wanamichezo bora waliofanya vizuri miaka 10 iliyopita, vile vile TASWA ilimtunuku tuzo Mhe Jakaya Mrisho Kikwete kwa mchango wako katika michezo.

Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa akimpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuendeleza michezo katika kipindi chake chote cha uongozi wake wa miaka 10.
Mhe. Rais, wakati anazungumza na wanamichezo waliokusanyika katika ukumbi wa Mlimani hapo tarehe 12/10/2015 alisononeka kwa wanamichezo wa Tanzania kutofanya vizuri wakati wa miaka 10 ya uongozi wake pamoja na kuleta walimu katika baadhi ya vyama vya michezo.

Mafanikio hata katika maisha ya kawaida ni mapambano hali kadhalika hata kupata mafanikio katika michezo ni mapambano. Katika miaka ya 70-80 michezo ilikuwa ridhaa, lakini kuanzia miaka ya 90 hadi sasa michezo imekuwa biashara na ajira kubwa kwa wanamichezo.

Kwa mfumo huo wa michezo kuwa biashara na ajira kila moja angefikiria kwamba tungepaswa kuwa na wanamichezo wengi kwa hiari yao kuchangamkia mazoezi ya hali ya juu ili nao waweze kuwa wawakilishi wazuri wa nchi yetu na kujipatia zawadi nono za fedha, lakini badala yake hali inazidi kuwa mbaya.

Hali hii inawezekana vile vile imesababishwa na hali ya ukata wa vyama vya michezo ambao hawana uwezo wa kutafuta vipaji huko walipo hasa Vijijini, Wilayani na Mikoani.

Katika miaka ya 70-80, Vyama vyetu vilikuwa vinapata ruzuku kutoka Serikalini kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT), ruzuku ambayo ilikuwa inawasaidia kuendesha ofisi na kuandaa Mashindano kama ya Taifa ambayo wanamichezo wengi wanakusanyika na vyama husika kufanya uteuzi wa wachezaji bora wenye vipaji ambao huwaendeleza.

Huo mfumo kwa sasa haupo kutokana na hali inayotamkwa na vyama vya michezo kama ukata na Serikali (BMT) kutokuwa na fedha.

Katika risala yake wakati wa tuzo kwa wanamichezo bora, Mhe. Rais alikiri bila kuwekeza tusitegemee kupata mafanikio, lakini nani awekeze, kwa haraka kwa tulio na uelewa mdogo ni Serikali ndiyo iwekeze kama nchi zingine duniani inavyofanya.

Mhe. Rais amefanya mengi kuinua michezo wakati wa uongozi wake. Naomba nitaje chache:

1. WALIMU WA MICHEZO KUTOKA NJE


Aliweza kuwalipa mishahara walimu wa michezo kama mpira wa miguu, netiboli, ngumi na riadha (pamoja na walimu wa riadha kutokuwa wa viwango) kupitia mpango wa ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba. Kila mmoja wetu aliona jitihada zake, na nakiri kwamba kwa namna moja au nyingine, vyama/mashirikisho ya michezo hawakutekeleza wajibu wao kutokana na hali ya ukata.

Hata wanamichezo wetu hawakutambua na kuona michezo kama ajira.
Mhe. Rais anakiri mafanikio yana gharama, bila nchi kuwekeza hafikirii kama tutakuwa na mwelekeo mwema hasa kwa vijana wetu kufanya vizuri katika medani ya Kimataifa. Nchi nyingi zinazofanya vizuri katika michezo ya kimataifa kwa asilimia kubwa wamewekeza katika michezo. Pamoja na WHVUM kutengewa bajeti ndogo ya michezo, bado suala la kuwekeza haliwezi kukwepeka kwa hali ya sasa ya michezo duniani.

2. MICHEZO YA UMITASHUMTA/UMISSETA


Tutakukumbuka hasa pale Mhe Jakaya aliporejesha michezo ya Umitashumta na Umisseta mwaka 2007 baada ya kusimama kwa zaidi ya miaka 9.

Binafsi naamini kilichotufikisha hapa tulipo leo ni pamoja na kutofundishwa kwa elimu ya viungo (PE) sambamba na kutokuwepo walimu wa masomo hayo kwenye shule zetu na kusimama kwa michezo hiyo na Michezo ya Majeshi (BAMATA).

Michezo ya Umitashumta/Umisseta ndiyo ilikuwa kiwanda cha kuandaa wachezaji ambapo wanapofanya vizuri hupata ajira katika taasisi za Serikali (JWTZ, Polisi, Magereza, Jeshi la Kujenga Taifa) lakini kwa sasa imekuwa tofauti kwani taasisi hizo haziajiri kama ilivyo huko nyuma kutokana na kutofanyika Michezo ya Majeshi (BAMATA) ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa.

Ni zaidi ya miaka 8 tangu aliporejesha michezo ya Umitashumta/Umisseta kwa nia na madhumuni ya kupata vipaji vitakavyoendelezwa na kuwa na nafasi nzuri ya kutuwakilisha Kimataifa.

Imekuwa vigumu kuendeleza vipaji vinavyoonekana katika michezo hiyo kwani hakuna maandalizi yaliyofanywa kuwaendeleza baada ya michezo hiyo kumalizika. Hata wale wanaomaliza masomo yao katika ngazi husika hawapati ajira kutokana na taasisi za Serikali nilizotaja kutokuwa na ajira rasmi kama ilivyo zamani. Mpaka sasa ni shule chache za binafsi na taasisi zimekuwa na mpango wa kuwasajili katika shule zao wanafunzi wazuri wenye vipaji na baadhi yao kutoa elimu bure (Scholarships) na kuwaendeleza katika baadhi ya michezo:

a.Shule ya Sekondari ya Alliance, Mwanza (Mpira wa Miguu na Riadha).

b.Shule za Filbert Bayi, Mkuza, Kibaha Mkoa wa Pwani (Riadha na Netiboli)

c.Shule ya Sekondari ya Lord Baden Powel, Bagamoyo (Mpira wa Miguu kwa Wanaume na Wanawake, Mpira wa Kikapu, Mpira wa Wavu na Riadha).

d.Shule ya Sekondari ya Winning Spirit, Arusha (Riadha)

e.Shule ya Sekondari ya Makongo, Dar Es Salaam (Mpira wa Miguu, Netiboli Kikapu na Wavu).

Naomba niishauri Serikali (Wizara ya Elimu na Tamisemi) kuunda Kanda ili kila baada ya michezo ya Umitashumta na Umisseta wanamichezo wenye vipaji wawekwe katika shule zilizo katika Kanda zitakazoundwa wakiendelea na masomo hali kadhalika na kucheza kwa Wizara husika kupeleka wataalamu (coaches) katika Kanda husika. Kama hilo haliwezekani, basi shule binafsi na taasisi zisaidiwe ili ziweze kuimarisha zaidi mipango waliyonayo ya kuendeleza michezo

Bila kuwa na utaratibu na mipango mahsusi, michezo ya Umitashumta na Umisseta, itakuwa kama tamasha tu.

3. UWANJA WA TAIFA


Hakuna ubishi kwa ushiriki wake katika ujenzi wa uwanja wa Taifa wakati wa uongozi wa Rais wa awamu ya tatu Mhe. Benjamin William Mkapa akiwa kama Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mpaka alipochaguliwa kuwa Rais wa awamu ya nne na kumalizia kazi za ujenzi zilizobaki.

Uwanja wetu ni mzuri sana, lakini matumizi yake kwa mchezo wa riadha yamekuwa nadra sana kutokana na gharama kubwa ambayo wakati mwingine Riadha Tanzania inashindwa kuchangia hasa inapotaka kufanya michezo ya Taifa ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka.

4. MAFANIKIO YA MICHEZO WAKATI WA UONGOZI WAKO


Mhe. Jakaya wakati wa uongozi wake wa miaka 10 kulikuwa na mafanikio ambayo hayaridhishi kwa nchi kama Tanzania yenye watu zaidi ya Milion 45, lakini kutokana na hali halisi niliyotaja hapo juu naomba nitaje mafanikio hayo kama ifuatavyo:

Samson Ramadhani
Samson Ramadhani 
1.Samson Ramadhani NYONYI, (Riadha):”Marathon”>Dhahabu: Michezo ya Jumuiya ya Madola, Melbourne, Australia 2006.
Fabian Joseph.
Fabian Joseph


2.Fabian Joseph NAASI, (Riadha): Mita 10000>Shaba: Michezo ya Jumuiya ya Modola, Melbourne, Australia 2006.

3.Martin Sulle, (Riadha) Km 21.1>Medali ya Fedha>Michezo ya Afrika, Algiers, Algeria, 2007.

4.Timu ya Netiboli, (Netiboli)>Medali ya Fedha>Michezo ya Afrika, Maputo, Msumbiji, 2011.

5.Timu ya Netiboli (Netiboli)>Kushinda Kombe la Mataifa 6, Singapore, 2012.

6.Timu ya Netiboli (Netiboli>Nafasi ya Pili, Mashindano ya Africa, Dar Es Salaam, 2012.


7.Timu ya Mpira wa Miguu watoto wa Mitaani (Street Children World Cup)>Dhahabu, Mashindano Kombe la Dunia, Rio de Jeneiro, Brazil, 2014.

8.Timu ya Mpira wa Miguu-Vijana chini ya Miaka 15>Medali ya Fedha> Michezo ya Vijana Afrika, Gaborone, Botswana, 2014.

5. SHUGHULI ZA TOC


Wakati wa uongozi wake wa miaka 10 kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kamati ya Olimpiki Tanzania imeweza kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo kwa vyama vya michezo, baadhi ya hizo shughuli zilikuwa ni kuendesha mafunzo ya ufundi kwa walimu wa michezo kutoka Vyama/Mashirikisho ya michezo wanachama wa TOC kwa kuleta Wakufunzi kutoka nje ya nchi hali kadhalika na Mafunzo ya Utawala na Uongozi wa Michezo kwa viongozi wa Vyama/Mashirikisho ya Mikoa na Taifa kwa nyakati tofauti.

Kwa ujumla Walimu 523 (448/75) na viongozi 380 (304/76) waliweza kupata elimu ya kufundisha wachezaji kwa madaraja tofauti na uongozi na utawala bora.
(Orodha Nyongeza “A” na “B”imeambatanishwa).

HITIMISHO

Kwa niaba ya Kamati ya Olimpiki Tanzania na kwa niaba yangu napenda nichukue nafasi hii kumshukuru Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kutoa posho za kujikimu, mavazi ya taifa, vifaa vya mazoezi na mashindano timu zetu za Taifa zilizowahi kushiriki Michezo ya Jumuiya ya Madola (Melbourne, Australia 2006, New Delhi, India 2010 na Glasgow, Scotland 2014) na Olimpiki (Beijing, China 2008, London, Uingereza 2012).

Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitamshukuru Mhe. Bernard Camillius Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa ushirikiano na WHVUM kuwatafutia mazoezi ya nje (China, Ethiopia, Uturuki na New Zealand) kwa kutumia mpango wa Diplomasia ya Michezo (Sports Diplomacy) wanamichezo wetu kabla ya Michezo ya Jumuiya ya Madola, yaliyofanyika Glasgow, Scotland mwaka jana (2014).

Akiwa kama mwanamichezo nambari moja hata baada ya kustaafu bado wanamichezo wenzako tutahitaji ushauri wake katika maendeleo ya michezo katika
nchi yetu.

Mwisho kabisa natoa wito kwa wanamichezo wote kujitokeza na kutumia haki yao ya Kikatiba hapo Jumapili tarehe 25/10/2015 kupiga kura kuchagua mafiga matatu (Diwani, Mbunge na Rais) kwa kipindi cha miaka 5 (2015-2020) ijayo.

Nawatakia Wanamichezo wote kila la kheri katika mchakato mzima na tulinde amani tuliyonayo.

Filbert Bayi,

KATIBU MKUU.

Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, Filbert Bayi (kushoto) akizungumza kabla ya kuwakabidhi hati wachezaji watatu wa Tanzania waliodhaminiwa na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki kupiga kambi Eldoret nchini Kenya. kutoka kulia ni Fabian Joseph, Fabian Nelson na Bazil John.
Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi akisaini moja ya hati za kuwadhamini wanariadha watatu wa Tanzania kupiga kambi Eldoret, Kenya huku Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania, Suleuman Nyambui akishuhudia. Kushoto ni Rais wa TOC, Gulam Rashid.

Taarifa ya THBUB: Pongezi kwa mwenendo wa kampeni za kisiasa na angalizo

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Kitalu Na. 8, Mtaa wa Luthuli
S.L.P 2643, DAR ES SALAAM
Simu: +255 22 2135747/8; 2137125; 2135222
Faksi: +255 22 2111281
Barua Pepe: [email protected]
Tovuti: www.chragg.go.tz


Oktoba 23, 2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
 

Tamko la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria kwa ajili ya Uchaguzi Huru, wa Haki na Amani


TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imekuwa ikifuatilia kwa karibu matamshi mbalimbali ya wanasiasa, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa Serikali, Tume ya Uchaguzi, na Jeshi la Polisi kuhusu nini kifanyike baada ya kupiga kura siku ya uchaguzi mkuu, Oktoba 25, 2015. Matamshi haya yamesababisha mkanganyiko na malumbano miongoni mwa viongozi na wananchi pia.

THBUB inapenda kusema kwamba, licha ya changamoto kadhaa zilizojitokeza katika baadhi ya maeneo, wakati wa kampeni za uchaguzi, kwa ujumla kampeni za uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani zimefanyika nchi nzima kwa amani na utulivu. Ni wajibu wetu sote kudumisha amani katika nchi yetu muda wote, wakati wa uchaguzi na baada ya kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu.

Tume (THBUB) inawashukuru na kuwapongeza wananchi kwa jinsi walivyoonyesha utulivu wakati wa mikutano mikubwa ya kampeni, ambayo imekuwa ikivuta maelfu ya wananchi.

Tume (THBUB) inatoa pongezi kwa Jeshi la Polisi kwa ulinzi ambao umekuwepo katika mikutano hiyo. Aidha, inavipongeza vyombo vya habari kwa kazi nzuri ya kuwapasha wananchi habari mbalimbali za uchaguzi.

Tume (THBUB) inatambua na kupongeza jitihada zinazofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kwa maandalizi ya uchaguzi.

Tume (THBUB) inapenda kutahadharisha kwamba malumbano haya ambayo yanaendelea hayaonyeshi dalili nzuri, pamoja na jitihada za wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini kuhubiri umuhimu wa uchaguzi wa amani. Malumbano haya yasipotafutiwa ufumbuzi wa haraka, kwa kutumia busara na kuzingatia sheria, haki za binadamu, na misingi ya utawala bora, kuna dalili kubwa ya kuwepo vurugu, uvunjifu wa sheria na amani, kwani pande zote hizi zimeendeleza malumbano na kushikilia misimamo yao.

Tume (THBUB) inaonya kwamba vurugu zinaweza kutokea, ama kwa makusudi, au kwa bahati mbaya, iwapo wananchi na wafuasi wa vyama vya siasa watashikilia misimamo yao, ama watagoma na kukaidi amri ya Polisi. Lolote katika hayo likitokea, kuna uwezekano mkubwa wa kuvurugika kwa uchaguzi, na haki za binadamu zitaathirika.

Vile vile, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imesikitishwa na matamshi yanayoashiria kutoiamini Tume ya Uchaguzi, na hata tuhuma za uwezekano wa wizi wa kura. Pia kumekuwa na matamshi ya kuwataka wananchi walinde kura, jambo ambalo halina msingi wowote wa sheria.

Ni vyema ifahamike kuwa, wajibu wa ulinzi wa kura upo kisheria, na ni wajibu ambao wamepewa mawakala wa vyama vya siasa na wagombea, ama wagombea wenyewe, wanaoruhusiwa kuwa ndani ya vituo, wakisaidiana na wasimamizi wa Tume ya Uchaguzi na Jeshi la Polisi kuhakikisha kwamba taratibu zote zinazosimamia upigaji kura zimefuatwa.

Kwa mujibu wa Vifungu vya 48(2) na 49 vya Kanuni za Uchaguzi (Urais na Ubunge) za mwaka 2010, Tanzania Bara, vyama vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi vinatakiwa kuteua mawakala wao wa uchaguzi kwa kila kituo, jambo ambalo Tume (THBUB) inaamini limefanyika. Mawakala wanatakiwa kula kiapo cha uaminifu.

Vifungu vya 59 na 60 vya Kanuni za Uchaguzi vinaeleza jinsi wakala wa chama au mgombea, atakavyoshiriki katika taratibu za kuhesabu kura, na jinsi malalamiko yatakavyo shughulikiwa na Msimamizi wa Uchaguzi.

Vifungu vya 61 hadi 66 vya kanuni hizo vinaeleza utaratibu wa kujumlisha kura za wagombea, na kutangazwa matokeo. Kanuni zinazungumzia pia uhusika wa mawakala katika hatua zote. Mawakala watapewa nakala za fomu mbalimbali husika, zikiwemo zenye malalamiko yaliyowasilishwa, na matokeo. Utaratibu huu wa sheria ndiyo unaotoa ulinzi mahususi wa kura.

Tume (THBUB) inawataka mawakala wafanye kazi zao kwa uadilifu na weledi. Mawakala wasiende kwenye vituo wakiwa na nia potofu (bad faith/malafide) ya kuharibu zoezi la kupiga kura. Tume (THBUB) inalisema hili kwa kuwa imebaini kuwepo matamshi yanayoonyesha hisia za kutoiamini Tume ya Uchaguzi. Tume (THBUB) inasisitiza umuhimu wa kuiamini na kuipa ushirikiano Tume ya Uchaguzi ili itekeleze majukumu yake bila ya kuingiliwa ama kubezwa.

Kwa hiyo Tume (THBUB) inapenda kutamka kwamba mlinzi mkuu wa kura ni wakala wa chama cha siasa, mgombea, na siyo mpiga kura au mwananchi wa kawaida ambaye hajapewa majukumu hayo kwa mujibu wa sheria.

Tume (THBUB) inatahadharisha kuwa ni vyema kila mdau wa uchaguzi atimize majukumu yake kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi. Jeshi la Polisi liendelee kutumia weledi katika kutoa ulinzi siku ya uchaguzi, kama lilivyofanya wakati wa kampeni za uchaguzi ambapo tulishuhudia mikutano mikubwa ikimalizika kwa usalama.

Kwa maana hiyo wananchi wanawajibu mkubwa wa kuwa watulivu wakati wa zoezi zima la uchaguzi kuanzia kupiga kura na kusubiri matokeo kwa amani.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inaamini kuwa utawala wa sheria lazima uheshimiwe na kila mtu, vikiwemo vyombo vya dola na mamlaka za Serikali.

Hivyo basi Tume (THBUB) inatamka:
  1. Viongozi wa vyama vya siasa na wagombea waepuke lugha zinazoweza kusababisha hofu, vurugu na uvunjifu wa amani.
  2. Inazishauri Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Tume ya Uchaguzi Zanzibar, na Jeshi la Polisi kuzingatia sheria na kudumisha misingi ya utawala bora, mambo ambayo ndiyo msingi wa kulinda haki za binadamu.
  3. Aidha, THBUB inawataka wananchi kupiga kura kwa amani na kuheshimu sheria zinazoongoza zoezi zima la uchaguzi.
  4. Vyama vya siasa vihakikishe kuwa Mawakala wao wanafanya kazi zao kwa uadilifu na wahakikishe kuwa wanatambua wajibu wao na wanazingatia taratibu za uchaguzi.
  5. Jeshi la Polisi litoe ulinzi mahsusi, bila vitisho, ili kuhakikisha kwamba zoezi la kupiga kura linafanyika kwa amani na kwa kuzingatia haki za binadamu na misingi ya utawala bora.
  6. Viongozi wa vyama vya siasa na wafuasi wao wawe wavumilivu na wajiepushe na matamshi au matendo yanayo weza kusababisha uvunjifu wa sheria, haki za binadamu, misingi ya utawala bora na kusababisha vurugu na kutoweka kwa amani.
  7. Tume ya Uchaguzi na Wasimamizi wa uchaguzi, na mawakala wa vyama wahakikishe kuwa zoezi zima la kupiga kura, kuhesabu kura, kubandika na kutangaza matokeo linafanyika kama sheria inavyotamka.
Tume ya Haki za Binadamu itaendelea kufanya ufuatiliaji wa mchakato wa uchaguzi nchini kote ili kuimarisha ulinzi wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora.

Tume inawataka wananchi watakaobaini uvunjifu wowote wa haki za binadamu, au uvunjifu wa sheria ya uchaguzi, kuzijulisha mamlaka husika zinazosimamia zoezi la uchaguzi.
Aidha, wanaweza kutoa taarifa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kupitia ujumbe mfupi wa simu ya kiganjani (SMS) kwenda Na. 0754 460 259.

Ujumbe lazima uanze na neno 'TAARIFA' au ' RIPOTI' kisha andika taarifa yenyewe. Namba hii inapokea ujumbe mfupi tu. Kwa taarifa zaidi piga Na. +255 22 2135747-8.

Kauli mbiu ya THBUB katika kuelekea Uchaguzi Mkuu ni “Watanzania wote tufanye Uchaguzi Mkuu kwa utulivu ili uwe Huru, wa Haki, na Amani.”

Imetolewa na:

(SIGNED)
Bahame Tom Nyanduga
Mwenyekiti
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Oktoba 23, 2015

Maamuzi wa mahakama kuhusu shauri la "meta 200" baada ya kupiga kura


Taarifa ya familia ya Mtikila kuhusu "siri nzito ya kifo cha Mch. Christopher"

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA SIRI NZITO YA KIFO CHA MCHUNGAJI CHRISTOPHER REUBEN MTIKILA

Ndugu Wana-Habari,

Kabla sijawaeleza kilichonilazimisha kuwaomba kuongea nanyinyi, kwanza niwarudishe nyuma kama miaka saba iliyopita, ndipo maisha ya Baba, Mchungaji, Mwenyekiti na mume wangu, Mchungaji Christopher Reuben Mtikila yalipoanzwa kuwindwa:-

MAUWAJI YA MHESHIMIWA CHACHA ZAKAYO WANGWE

Mara tu baada ya kifo cha mbunge huyo, mchungaji Mtikila alitoa ripoti maalumu juu ya mauaji yake ambayo ilimjengea uadui kati ya baadhi ya vyama vya siasa pamoja na wafanyabiashara wakubwa ambao hadi leo ni wapinzani wa serikali hapa nchini. Mchungaji Mtikila hadi anafikwa na mauti aliendelea kupata upinzani wa aina hiyo hiyo kwa sababu mchungaji Mtikila aliendelea kudai haki ya marehemu Chacha Zakayo Wangwe.

MAUAJI YA BULIGI

Hii ilimwongezea uadui baada ya kusema/kuandika ukweli juu ya watutsi wa nchi jirani kuvamia nchi yetu kwa mtindo wa kujifanya wafugaji wasio hama. L.I.F. ilibaini uharamia huo kuwa hawakuwa wafugaji bali walikuwa askari wa Jeshi la Rwanda waliokuwa na mpango wa kutumika na Chama kimoja cha siasa hapa nchini ili kuleta mapigano yatakayo zaa mapinduzi. Jambo hili lilisababisha Rais wa Rwanda, Paulo Kagame kutamka hadharani kuwa angemkamata Mwenyekiti wa chama chetu cha DP kwa lengo la kumuua na Serikali yetu inajua hilo. Mara baada ya ripoti hiyo kutolewa na Mchungaji Mtikila "operation Kimbunga" ilizaliwa na kuponya nchi yetu; lakini chuki na uadui uliendelea dhidi ya Mchungaji Mtikila.

MCHAKATO WA URAIS NDANI YA CCM

Ikumbukwe kuwa mara baada ya mchakato wa kutafuta mgombea urais kwa tiketi ya CCM kuanza DP ilitoa ripoti iliyowahusu wagombea sita wa CCM waliotumia mapesa mengi na kuanza kampeni kabla ya muda na kusisitiza kuwa Lowasa ni mtu asiefaa kuwa Rais wa nchi yetu. Na baada ya kuhama CCM, Mwenyekiti wetu aliendelea kutoa tahadhari hadharani jinsi Lowasa asivyofaa kuwa Rais wa nchi yetu hivyo likaendeleza uadui wake na Chama.

VITISHO KUANZA

Mchungaji Mtikila alipata nafasi ya kuongea katika kipindi kinachorushwa na STAR TV cha asubuhi "TUONGEE" ndipo alipoanza kupata vitisho toka kwa watu mbali mbali wengine kupitia kwenye simu wengine uso kwa uso.

Kipindi cha kwanza kilirushwa tarehe 25/9/2015 na kufuatwa na cha tarehe 27/9/2015. Alipotoka studio hiyo asubuhi ya tarehe 27/9/2015 ndipo watu waliodai wametumwa na Mhe. Edward Ngoyai Lowasa na Mhe Frederick Sumaye walimuomba wampe nusu bilioni na apewe maovu ya mgombea urais wa CCM ili afunike alivyowamaliza wao. Mchungaji Mtikila aliwapuuzia mbali wale wajumbe waliyotumwa kwni aliawaambia kuwa yeye siyo malaya wa kuuza utu wake kwa tende na haluwa. Yakumbukwe kuwa mahojiano kwenye hivyo vipindi viwili kwenye STAR TV hayakuwa yanatetea mtu au chama yalikuwa yanatetea Taifa letu lipate Rais anayefaa. Kwa hiyo basi wale waliochukizwa na mahojiano hayo ni wale amabo hawakubaliani na mawaidha ya Mchungaji Mikila aliyokuwa anawatahadharisha watanzania juu ya Mh. Lowasa kuwa hatari kwa usalama wa taifa letu kama atakuwa Rais wa nchi yetu. Hao watu ndiyo waliopanga mpango mzima wa mauaji ya Mh. Mtikila ambaye ni mume wangu. Wakati yuko Bunda mjini watu wasiofahamika walimfuatafuata na tarehe 26/9/2015 gari lake lilifukuzwa na gari usiku wakati alipokuwa anatoka Bunda kwenda Mwanza kufanya mahojiano ya tarehe 27/9/2015 na Star Tv.

MPANGO WA MAUAJI HALISI

Mchungaji Mtikila alitafutiwa gari na Victor James Manyahi ambayo ilikuwa na madereva wawili. Mchungaji madereva hakuwajua. Hata mimi madereva hao sikuwajua wala sikuwaona. Walikodiwa kutoka wapi sijui, wala sijui wanafanana vipi. Na wala sijui Victor Manyahi alikodi gari hilo kwa nani na makubaliano yepi sijui. Kwa hivyo basi, kwenye gari aliyosafiri nayo Mchungaji Mtikila kulikuwamo madereva wawili na Mgaya Patrick (tunayemfahamu). Wakati wanakwenda gari lilipata ajali Makambako.

Wakati wanarudi wakapata “ajali” Msolwa Mchungaji akapatwa na mauti peke yake. Ajali ilikuwa mbaya sana IKAUWA MTU MMOJA AMBAYE NI MCHUNGAJI MTIKILA NA HAKUKUWA MAJELUHI HATA MMOJA. Cha ajabu kwangu n kuwa mtu ambaye alikuwa ni mlinzi wa kujitolea (body guard) Mgaya Patrick sijawahi kumuona usoni mwangu kabla na hata baada ya mazishi kuja kuniambia kilichotokea eneo la ajali. Pamoja na juhudi zangu zote za kumpigia simu mara kadhaa aje anijuze Mgaya Patrick hajatokea hadi sasa ndugu zangu wanahabari ninapoongea nanyi.
Lakini si kwamba huyu mtu hayupo, yupo lakini sijaonana naye, kwa nini sijui. Je ndugu zangu wanahabari nimuweke Mgaya Patrick kwenye fungu gani?

Ndugu Wana-Habari, baada ya kuwaelezea yote hapo juu nakuja kwenye suala nililowaomba nikutane nanyi ili niongee mbele yenu kuwa sikubaliani na uchunguzi kuwa Mchungaji Christopher Reuben Mtikila amekufa kwa ajali. Sikubaliani na kazi ya Polisi kuwa wamefunga file lao kutokana na Post-mortem report kuwa mauti yaliotokana na ajali. Nafuta kabisa taarifa iliyotoka katika gazeti la Nipashe chini ya kichwa cha habari kuwa “FAMILIA YAFUNGUKA KIFO CHA MTIKILA”-ilitolewa mapema mno. Kila mwanafamilia alikuwa hajawa tayari kutoa kauli yoyote. Kwa niaba ya Chama na familia ya Mchungaji Christopher Reuben Mtikila naomba tusaidiwe yafuatayo kusudi haki ya mpendwa wetu ionekane inatendeka:-

Kwa sababu mtandao umeanza kuficha ukweli ili kulinda wauaji; tunaomba Mheshimiwa Rais aingilie utata wa kifo cha Mheshimiwa Mchungaji Christopher Reuben Mtikila kwa kuunda tume ya uchunguzi isiyohusisha polisi.Tunaiomba mamlaka ya mawasiliano yaani Tanzania Communications Regulatory Authority, TCRA itusaidie yafuatayo:-

(a) Mtu aliyeweka picha kwanza alfajiri kuonyesha mauti ya Mhe Mchungaji Mtikila alikuwa wapi? Kwenye tukio? Au ni hao wauaji walikuwa wanatoa taarifa kwa waajiri wao kuwa wamekamilisha kazi!

(b) Mtu aliyeweka picha ya Dr. Jean-Bosco Ngendahimana kwenye mtandao kuwa ndiye anahusika na mauti ya Mhe. Mch. Mtikila na kumusingizia kuwa amekamatwa na polisi akiwa anajiandaa kukimbia;

(c) Wote wanaoendelea kumhusisha Dr. Jean-Bosco Ngendahimana na mauaji ya Mhe. Mchungaji Mtikila, tuwafahamu ili watueleze vizuri.

Ukweli na haki ni vya Mungu hakuna anayeweza kuviua au kuvizuia.

Tunategemea Mungu atawatumia watendaji wa Serikali/nchi yetu wenye nia njema, na makusudi yaliyonyooka kwa ajili ya nchi yetu ili Mhe. Mchungaji Mtikila apewe haki dhidi ya wauaji wake.

Asanteni,

Georgia C . Mtikila,
KM DP/Msemaji-Familia