Mwl Mndeme: Nawahurumia wanetu kwa waliyojifunza katika kampeni za kisiasa 2015

Tumemaliza Kampeni, ila Nawahurumia watoto wetu kwa waliyojifunza

Mbuyu huu, kituo cha kupigia kura maeneo haya


Overview! Idadi na Takwimu za wagombea Ubunge wa majimbo 264 ya Uchaguzi Mkuu 2015

Risala ya Jaji Lubuva kuhusu kupiga kura kesho, Oktoba 25

Ufafanuzi wa NEC kwa CHADEMA kuhusu mfumo wa kujumlisha matokeo ya kura

Mkurugenzi wa TEHAMA kwenye NEC Dk Modest Kipilimba ametoa maelezo kuhusu kauli ya CHADEMA kutokuwa na imani na mfumo huo.
WHO report: Processed meats, red meats linked to cancer

(image source: foodnavigator.com - Red and processed meat consumption linked to gestational diabetes)
UK Department of Health advises people who eat more than 90 grams (cooked weight) of red and processed meat a day to cut down to 70 grams.

Why?
[Because] evidence shows that there is a link between eating red and processed meat and the risk of bowel cancer.

The Independent says that on Monday, the World Health Organisation is reportedly planning to declare that bacon, sausages and other processed meat cause cancer.

Red meat is also expected to be listed as being “probably carcinogenic to humans”.

A source told The Daily Mail that the announcements were expected to be made on Monday with processed meat put in the same category as cigarettes, alcohol and asbestos.

Again, according to NHS processed meat refers to meat that has been preserved by smoking, curing, salting or adding preservatives. This includes sausages, bacon, ham, salami and pâtés. This is What counts as red and processed meat:-
 • beef
 • lamb
 • pork
 • veal
 • venison
 • goat
It does not include:
 • turkey meat
 • duck
 • goose
 • game birds
 • chicken
 • rabbit 
How much red and processed meat should we eat? Click here and read the guidelines for adult as well as children above 5 years, from the NHS.


[video] Naibu Mwanasheria Mkuu akitamka tafsiri ya "meta 200"


Rais Kikwete ateua Makatibu Wakuu 4 wapya wa WizaraTHE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa Ijumaa, Oktoba 23, 2015, amewateua Makatibu Wakuu wanne wapya wa wizara mbalimbali.

Aidha, Rais Kikwete amewateua Naibu Makatibu Wakuu wapya watano, amewateua Makatibu Tawala wa Mikoa wawili na pia amewahamisha Naibu Makatibu Wakuu wawili.

Kwa mujibu wa uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Ndugu Hab Mkwizu kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma; Profesa Elisante Ole Gabriel kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo; Dkt. Yamungu Kayandabila kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na Mhandisi Omari Chambo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.

Aidha, kwa mujibu uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Mhandisi Paul M. Masanja kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini; Dkt. Maria Mashingo kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Ndugu Zidikheri Mgaya Mundeme kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

Wengine walioteuliwa kuwa Naibu Makatibu Wakuu ni Ndugu Tixon T. Nzunda ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Ndugu Emmanuel Kalobelo ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

Walioteuliwa kuwa Makatibu Tawala wa Mikoani Ndugu Eliakim Maswi ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara na Mhandisi Madeni Kipande ambaye anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.

Katibu Mkuu ambaye anahamishwa ni Bibi Sihaba Nkinga ambaye anakwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Wanawake, Jinsia na Watoto kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Naibu Makatibu Wakuu wanaohamishwa ni Ndugu John T. Mngodo ambaye anahamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kutoka Wizara ya Uchukuzi na Ndugu Mwamini Juma Malemi ambaye anakwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Wateuliwa hao wote wataapishwa asubuhi ya Jumamosi, Oktoba 24, 2015, Ikulu mjini Dar es Salaam.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
24 Oktoba, 2015