Yasemavyo magazeti 26.10.2015 siku moja baada ya kupiga kura

Katuni kuhusu kupiga kura za Uchaguzi Mkuu Tanzania 2015
Akaunti rasmi za Mawasiliano ya Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC)

Tovuti: www.nec.go.tz

Facebook: facebook.com/TumeyaTaifayaUchaguziTanzania

Twitter: twitter.com/TumeYaUchaguzi

Youtube: youtube.com/channel/UCTA5ilGDEjAju3RbWhSORvw

Audio: hulkshare.com/TUME_YA_TAIFA_YA_UCHAGUZI

Blog: tumeyataifayauchaguzi.blogspot.com

Redio: myradiostream.com/FocusRadioTz

Kuhakiki mpiga kura: voters.nec.go.tz:8081/vote 

SMS: +255(0)772 55 55 53

Mgombea Udiwani kupitia NCCR-Mageuzi akamatwa

Mgombea Udiwani wa Kagondo kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, Anatory Amani anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kuvamia wasimamizi wa kituo cha kupigia kura na kuwanyang'anya vitabu.

Imeelezwa katika taarifa ya habari StarTv kuwa Amani alifanya hivyo baada ya kupokea ujumbe wa simu unaomtaarifu kuwa vitabu hivyo vimenyofolewa baadhi ya karatasi.

Polisi wamethibitisha kumkamata mtuhumiwa na kusema kuwa atafikishwa kortini hapo kesho.

Taarifa ya TCRA kuhusu utangazaji matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2015

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu utangazaji wa matokeo ya Uchaguzi Mkuu kwa vyombo vya utangazaji kwa mujibu wa Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015.

Kanuni hizi zipo kwa mujibu wa Sheria kama ilivyotolewa na Gazeti la Serikali la Tarehe 26 Juni, 2015.

Kanuni hizi zinalenga kuweka utaratibu mzuri wa kutangaza shughuli za kampeni na uchaguzi mkuu kuwa wa amani na utulivu.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inapenda kuwakumbusha kuwa ni marufuku kwa vituo vyote vya utangazaji kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu bila kupata taarifa sahihi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa utaratibu waliojiwekea.

Vilevile, vituo vyote vya utangazaji vinapaswa kuzigatia Sheria na Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015.

Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015, Na. 16 (1) na 16(2) inaelekeza kama ifuatavyo:-
16(1) kwamba kila mtoa huduma za maudhui atakuwa na wajibu wa kuuarifu umma juu ya matokeo ya uchaguzi, kadiri yanavyopatikana. uangalizi maalumu ufanyike kuhakikisha usahihi wa matokeo yote yanayotangazwa.
16(2) Mtoa huduma za maudhui hatatangaza maoni ambayo yanaweza kuchochea vurugu au kuhamasisha chuki kwa misingi ya mbari, kabila, jinsia, dini au Imani za kisiasa na ambayo yanajenga uchochezi wa kusababisha madhara.
Hivyo basi, vituo vya utangazaji vinatakiwa kufuata kikamilifu Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015 na kwamba vituo vya utangazaji vitawajibika na matokeo ya maudhui ya matangazo ambayo hayatozingatia Kanuni.

Mamlaka inatoa wito kwa vituo vya utangazaji kutumia weledi katika maamuzi ya kihariri kuchanganua kipi kinafaa kutangazwa na uangalizi maalumu ufanyike kuhakikisha kuna usahihi katika kutangaza matokeo yote yatakayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAREHE 25/10/2015

Tetesi na ripoti ya kura bandia zilizokamatwa

Mtuhumiwa huyu anaripotiwa kukamatwa huko mkoani Arusha

Video hii ni ya ripoti ya tukio moja huko Kagera
Taarifa ya CCM ya leo ya tathmini ya upigaji kura

Mkurugenzi NEC azungumzia hitilafu katika vituo vya kupigia kura 25.10.2015Baadhi ya viongozi na wananchi waliopiga kura leo 25.10.2015

Kasoro zilizoripotiwa katika baadhi ya vituo vya kupigia kura 25.10.2015
Huku Arusha, mgombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha TLP Macmillan Lyimo alishindwa kwa muda kutekeleza haki yake ya msingi na ya kikatiba ya kupiga kura leo baada ya kukosekana kwa fomu namba 19 inayomruhusu kupiga kura kwa kuwa hayupo kituo chake cha kupigia kura cha Dar es Salaam alikojiandikisha na kupangiwa kupiga kura awali, kwa kuwa sasa yupo jijini Arusha. Mgombea hata hivyo alifanikiwa baadaye kupiga kura.


Huko Bariadi Faustine Fabian anaripotia gazeti la Mwananchi kuwa wakati zoezi la upigaji kura likiendelea nchi nzima wakazi wa kata ya Matongo, jimbo la Bariadi, mkoani Simiyu wameshindwa kupiga kura kwa nafasi ya udiwani kwa kile kinachodaiwa uhaba wa karatasi za kupigia kura.

Akiongea na waandishi wa habari Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo Abdallah Malela amesema kukosekana kwa karatasi ndicho chanzo cha uchaguzi kwa ngazi ya udiwani kusitishwa katika eneo hilo.

Alisema kuwa kata hiyo ina jumla ya wapiga kura 7500, na vituo 17 lakini karatasi ambazo zimetoka Tume ya ucHaguzi zilikuwa 3400 tu, huku zaidi ya wapigakura 4100 wakikosa karatasi hizo za kupigia kura.

“Baada ya kuona hali hiyo niliwasiliana na viongozi wa tume kutoa taarifa ambao waliamua kuhairisha zoezi kwa nafasi ya udiwani tu, mpaka tena itakapotangazwa na tume,” alsiema Malela.

Kwa upande wa rais na mbunge, zoezi liliendelea kama kawaida kwa kuwa karatasi hizo zililetwa za kutosha.

Kwa upande wa Jimbo la Itilima Mkoani hapa Msimamizi wa uchaguzi Alphonce Aloyce alisema zoezi lilienda salama licha ya mihuri kukwama ingawa tatizo hilo lilipatiwa ufumbuzi mapema.