Thinking that your way is the right way of doing things


We all do it — if we’re not worried that we’re doing things the wrong way, we seem to be sure that our way is the right way -- says Leo Babauta in his latest post "Avoid the Tendency to Think Your Way is the True Way"
  • I judge people who don’t eat as healthy as me. Especially those who eat fast food.
  • I look at people who carry lots of luggage when traveling, and think they don’t travel as well as I do with just one small backpack.
  • I judge people who don’t exercise, and think that my way of exercising is the right way to do it.
  • I have felt superior to people who smoke (even though I used to do it).
  • I sneer at people who watch popular movies, listen to pop songs, watch too much TV (even though I’ve done all of these).
  • I judge “bros,” hipsters, Internet trolls, gamers, startup culture, racists, misogynists, gluttons, people who have ads on their sites, people who drive big trucks, people who are on Facebook or Instagram too much, hoarders, people who aren’t neat or organized, people who don’t have their finances together, people who eat too much meat and cheese …
In other words, I judge everyone, in some way or another, for being different from me. And so, it seems, does everyone else. When someone doesn’t do things your way, you judge them. Your way is right. Or my way is.

This is, of course, just our natural reaction to other people who are different than us. When we stop to think about it, our way can’t possibly be the only right way. Other people just have different preferences, and the world would be boring if everyone were the same, if no one did things differently.

We want diversity. We want different ideas. We want a clash of cultures and ideas. We want to be exposed to a constant stream of differentness.

And so I urge you to pay attention to when you are thinking your way is better than someone else’s. Notice this, question it, and see if you can try to be curious about the other person’s way. How can their way be just as good as yours?

How can we drop judgment and embrace curiosity?

I’m trying this, and struggling with it, but the struggle is worth it.

Magazetini 27.20.2015


Mo Dewji Foundation yasaidia kuboresha Furahini Youth Learning Centre, Kilimanjaro

Baadhi ya vijana hao wakiwa darasani wakifurahia masomo wanayopatiwa ya kujiandaa na elimu ya sekondari katika kituo hicho cha Furahini mkoani Kilimanjaro.
TAASISI ya misaada ya Mo Dewji Foundation imekubali kufadhili mradi wa kituo cha mafunzo cha vijana cha Furahini (FYLC) wenye lengo la kuboresha upatikanaji wa elimu katika kijiji cha Kisangara mkoani Kilimanjaro.

Imeelezwa kuwa taasisi hiyo ya bilionea Mo Dewji imetoa shilingi milioni 7 kusaidia ujenzi wa miundombinu inayotakiwa na kituo hicho chenye lengo la kuboresha elimu kwa watoto wa kijiji hicho.

Baadhi ya watoto hao ni wawafanyakazi wa mashamba ya Mkonge ya MeTL yaliyopo jirani na kijiji hicho.

Ufadhili huo unaenda sambamba na sera za MeTL za urejeshaji wa faida yake kwa wananchi kama sehemu ya wajibu wake kwa jamii, wenye lengo la kuimarisha ustawi wa jamii inayochangia biashara za kampuni hiyo.

Taasisi ya Mo Dewji ambayo ndiyo inatekeleza wajibu wa kundi la makampuni ya MeTL la kurejesha faida kwa umma, kwa ufadhili huo kwa kikundi cha Furahini wametanua wigo kutoka katika shughuli mbalimbaliw alizokuwa wakufadhili mkoani Singida.

Lengo la ufadhili huo ni kuwezesha jamii yenye kipato cha chini kabisa kuweza kumudu mikiki ya elimu ili kukabili umaskini.

Toka mwaka 2000 kundi la makampuni ya MeTL imekuwa ikitanua mazingira ya urejeshaji wa faida kwa umma kutokana na shughuli zake mbalimbali. Katika kipindi cha miaka mitano taasisi ya Mo Dewji imetumia zaidi ya dola za Marekani milioni 3 kusaidia miradi mbalimbali ya jamii.
Baadhi ya vijana hao wakiwa darasani wakiendelea na masomo katika jengo la kituo hicho cha Furahini ambacho kinatarajiwa kukabaratiwa na kwa msaada wa Mo Dewji Foundation.
Tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo, shughuli mbalimbali zimedhaminiwa na kufadhiliwa. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule, uchimbaji wa visima, ugawaji wa vyandarua, usambazaji wa unga wa mahindi kwa wananchi waliokumbwa na baa la ukame kwa mwaka 2005-2006,ufadhili kwa wanafunzi wa sekondari,afya kw awale waliozidiwa kiafya, kujenga kitengo cha macho katika hospitali za mkoa,kuweka taa katika mitaa, msaada wa chakula kwa waliokumbwa na ugonjwa wa ukimwi, ununuzi wa vifaa vya michezo na vifaa vya wakulima.

Kwa mujibu wa mratibu wa kituo hicho cha Furahini (FYLC) Bw. Msuya Isiaka, wazo la kuanzishwa kwa kituo lilitokana na uzoefu wa muda mrefu wa ufundishaji katika eneo hilo la mahusiano ya jamii.

Alisema wazo la kuanzishwa kwa kituo limetokana hasa na matokeo mabaya ya mitihani kwa wanafunzi wanoasoma shule za umma katika kijiji hicho.

“Elimu imekuwa tatizo kubwa katika jamii yetu hasa katika shule za serikali ambazo mara nyingi zimejikuta hazina walimu, na kama wakiwa wamebahatika wanakuwa na mwalimu mmoja wa somo la hisabati kwa shule nzima, bila kutaja masomo mengine kama fizikia, kemia na bayolojia,” alisema Isiaka na kuongeza kwamba kuna shida kubwa ya uwajibikaji kwa wlaimu na hivyo kluleta athari mbaya kwa wanafunzi.

“Tunaamini kwamba silaha yetu kubwa ya kukabili umaskini unaozunguka katika vizazi vyetu hapa Kisangara ni kuwa na elimu bora” alisema.Kwa mujibu wa Isiaka kituo hicho kinatakiwa kuwa na maktaba kamili na chumba cha tehama.

“Kwa kuwa na miundombinu hiyo ya kujifunzia ya maktaba na tehama, wanafunzi wanakuwa katika nafasi ya kujifunza vyema na kuwa katika hali ya kukabili umaskini unaozunguka janmii yetu.” alisema.

Mratibu huyo alisema kwamba mafunzo katika kituo hicho katika masomo ya kemia,fizikia,bayolojia na hisabati yalianza Juni 2015.

Kituo cha Furahini ambacho kimejengwa katika ardhi yenye ukubwa wa nusu eka katika kijiji cha Kisangara kata ya Mtuva katika wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjarokipo umbali wa kilometa 2.5 kutoka kituo cha mabasi cha Kisangara.

Kijiji cha Kisangara ambacho kipo katika eneo kame wastani kina wakazi wa kutoka makabila mbalimbali ambayo yalifika hapo kufanyakazi katika mashamba ya mkonge.

Mkonge ndio zao kubwa la biashara ambalo linalimwa na kampuni ya MeTL ikiajiri idadi kubwa ya watu kutoka katika kijiji hicho.
Eneo la jengo hilo la kituo linavyoonekana kwa nje.
Ukame uliitafuta Kisangara kwa muda mrefu umesababisha kasi kubwa ya umaskini. Kutokana na hali hiyo watoto wameathirika zaidi kutokana na familia zao kushindwa kuwapeleka shule binafsi na kuwaacha katika shule za umma ambazo hazina ubora.

Kutokana na hali hiyo FYLC inajipanga kuhakikisha kwamba inarejesha matumaini kwa kuwawezesha wanafunzi hao kupunguza tofauti kati ya wanafunziw aosoma shule binafsi na shule za umma katika masomo.

Kituo kikiwa na wanafunzi 86 wa umri kati ya miaka 13 hadi 14 wanafundishwa kujiandaa kuingia kidtao cha kwanza kwa kufunzwa Fizikia, kemia,bayolojia,jiografia na Kiingereza.

Lengo kuu la kituo ni kuhakikisha kwamba wanawawezesha wanafunzi wanaosoma shule za umma wanakuwa na uwezo mkubwa kwa kuwapa nafasi ya kutumia maktaba na chumba cha Tehama na kuwapelekea walimu waliobobea kuwanoa wanafunzi hao na kuleta mabadiliko.

Aidha kituo kitatoa elimu ya maarifa ya afya ya uzazi kwa vijana ili kuweza kubadili maisha yao na kuondokana na tabia mbaya.


Ukarabati wa kituo hicho ukianza baada ya Mo Dewji Foundation kukipiga tafu.
Mratibu wa Furahini Youth Learning Centre, Isiaka Msuya katika zoezi la kupakia matofali kwa ajili ya ukarabati wa kituo hicho kwa msaada wa Mo Dewji Foundation.

That Trump said “Africans are lazy fools, eating, lovemaking, stealing AND will deport Kenyans, Obama included”

A story with such headlines is circulating in WhatsApp.

It has also been shared in some Nigerian, Zimbabwe and Kenyan blog/sites and discussion fora.

The original story was published by Newslo on Saturday, August 22, 2015 and got picked up by a Kenyan website on October 25th, 2015 and the rest is history.

However, the "About Us" page on Newslo is very clear about it's stories.

Here is a screen-shot...


Jukwaa Langu: Tanzania baada ya Uchaguzi 2015

Picha:: dw.com/sw

Kipindi hiki hukujia kila Jumatatu, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2015.

Leo tulizungumzia Tanzania baada ya upigaji kura uliofanyika jana Oktoba 25, 2015.Vijana wailalamikia NEC kuhusu malipo yao


Ripoti kutoka Mwanza na Shinyanga 26.10.2015


Vipande vya nondo na mapanga yanayodaiwa kuwa ni ya mgombea ubunge jimbo la Solwa mkoani Shinyanga Jeremia Mshandete wa Chadema,ni miongoni mwa silaha za jadi zilizokatwa ambazo zinadaiwa kuwa ziliandaliwa kwa ajili ya kufanya uhalifu wakati na baada ya uchaguzi mkuu 2015

Rais Kikwete ateua Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Joel Laurent kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA). Uteuzi huo ulianza Oktoba 18, mwaka huu, 2015.

Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Laurent alikuwa Katibu wa Taasisi hiyo ya TEA na ndiye amekuwa anakaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
26 Oktoba, 2015

[video] Lowassa azungumza na vyombo vya habari 26.10.2015
[video] Maalim Seif azungumza na vyombo vya habari 26.10.2015
MGOMBEA wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad ameitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutangaza matokeo ya kura ya urais visiwani humo.

Taarifa iliyoandikwa na Shirika la Utangazaji Ujerumani-DW imemnukuu Maalim Seif akisema baada ya chama chake kukusanya fomu zote za matokeo kutoka vituoni, yeye amepata kura nyingi.

“Baada ya kukusanya matokeo yote, nimepata kura 200,007 dhidi ya kura 178,363 za mgombea wa CCM anayetetea nafasi yake, Dk. Ali Mohammed Shein.”

Maalim Seif ameitika Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo halisi kama yalivyo kwenye fomu zinazotoka vituoni.