Lipumba: Kikwete usimwongezee Magufuli matatizo yaliyopo yanamtoshaMwenyekiti wa zamani wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amemwomba Rais Jakaya Kikwete kuiamuru Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC ) kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa uliofanyika Zanzibar ili kuipusha nchi kuingia katika machafuko.

Jumatano iliyopita, Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha alifuta matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu akisema uchaguzi ulikuwa na kasoro nyingi.

Akizungumza leo kwa mara ya kwanza na waandishi wa habari tangu alipojiuzulu, Agosti 6, mwaka huu, Lipumba alisema amelazimika kutoa ushauri baada ya kuona hatari iliyo mbele kama wananchi wa Zanzibar watanyang’anywa haki yao.

“Ijumaa ijayo Dk John Magufuli ataapishwa kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Tanzania, Kikwete usimwongezee Magufuli matatizo yaliyopo yanamtosha, ” alisema.

Lipumba ambaye alipokelewa na wafuasi zaidi ya 100 kwenye ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni, alisema Kikwete ahakikishe kabla hajamaliza muda wake wanaiamuru ZEC kuendelea kutangaza matokeo na kuwatangaza washindi wa uchaguzi huo.

[video] Maalim Seif: "Sitowazuia"


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za CUF Mtendeni kuhusiana na maendeleo ya “mkwamo” wa kisiasa Zanzibar. (Picha na Salmin Said, OMKR)
Na: Hassan Hamad (OMKR)

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema jitihada za kuutafutia ufumbuzi mkwamo wa kisiasa Zanzibar uliotokana na tamko la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Bw. Jecha Salim Jecha baada ya kutangaza kufuta uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015, zinaendelea vizuri.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CUF Mtendeni mjini Zanzibar, Maalim Seif ambaye pia ni mgombea Urais kupitia Chama hicho amesema ana matumaini kuwa suala hilo litapatiwa ufumbuzi wa haki unaoheshimu maamuzi ya wapiga wa Zanzibar waliyoyafanya tarehe 25 mwezi uliopita.

Amefahamisha kuwa jitihada hizo zimekuwa zikifanywa na taasisi mbali mbali za ndani na nje ya nchi zikiwemo Umoja wa Mataifa pamoja na nchi kadhaa ambazo ni marafiki wa Tanzania zikiwemo zilizoleta waangalizi wa kimataifa katika uchaguzi huo.

Amesema jitihada pia zimekuwa zikifanywa na viongozi wakuu wastaafu, viongozi wa dini na Msajili wa vyama vya siasa Tanzania Jaji Francis Mutungi.

Ameeleza kuwa Chama Cha Wananchi CUF kimetiwa moyo na imani kutokana na jitihada hizo, na kwamba ufumbuzi wa haki wa suala hilo utapatikana katika kipindi kifupi kijacho.

Maalim Seif ametumia fursa hiyo kuwataka Wazanzibari waendelee kubaki watulivu na kuitunza amani ya nchi, na kuwaaachia viongozi wao kulifanyia kazi suala hilo kwa kushirikiana na watu mashuhuri pamoja na Taasisi za kitaifa na kimataifa.

Amewaomba wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kufanya juhudi kuhakikisha Zanzibar inabaki katika hali ya amani na utulivu, na kutokubali kutumiwa na wanasiasa kufanikisha mbinu chafu ambazo zinaleta taharuki na hofu miongoni mwa raia.

Maalim Seif amewahakikishia viongozi na wanachama wa CCM na Wazanzibari wote kwamba iwapo atatangazwa mshindi wa uchaguzi huo hakutokuwa na ulipizaji wa kisasi, na kwamba atafanya kazi kwa ushirikiano chini ya muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa maslahi ya Zanzibar.Kauli ya SMZ: Rais aliyepo madarakani hivi sasa ataendeleaOthman Khamis Ame, OMPR

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewahakikishia Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwamba Rais aliyepo madarakani hivi sasa ataendelea kushika madaraka ya Urais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi mpaka pale utaratibu wa Kikatiba na Kisheria wa kumpata Rais utakapokamilika.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akitoa Taarifa ya Serikali akisisitiza Taarifa ya awali ya Serikali iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuhusiana na kauli za kupotosha zinazotolewa na baadhi ya Viongozi wa vyama vya Kisiasa kuhusu uhalali wa kuendelea kuwepo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyopo madarakani pamoja na Serikali yake.

Balozi Seif aliwaomba Wananchi wazipuuze kauli za upotoshaji zinazotolewa zikiashiria zaidi uvunjifu wa amani na kuwataka waendee kuwa watulivu na kudumisha amani iliyopo Nchini.

Alisema Kifungu cha 28 Mbili {a} cha Katiba ambacho kimekuwa kikitumika katika kutoa tafrisi potofu kwa Wananchi kwamba Rais aliyopo madarakani atamaliza muda wake wa miaka mitano kuanzia Tarehe ambayo alipokula kiapo cha uaminifu na kiapo cha kuwa Rais.

Balozi Seif alieleza kwamba ni dhahiri kwamba dhamira ya kifungu hicho cha Katiba ilikuwa kuweka bayana kuwa kama uchaguzi Mkuu utafanyika na msindi wa kiti chja Urais atatangazwa rasmi na Tumen ys Uchaguzi, hivyo muda wake wa kuendelea Mtu kuwa Rais ungemalizika kwa kufuatana na masharti ya Kifungu hicho.

Alifafanua kwa kuwa Tume ya Uchaguzi haikumtangaza mshindi wa kiti cha nafasi ya Urais ni dhahiri masharti ya kifungu hicho hayataweza kusimama na hivyo masharti ya Kifungu cha 28 {1} {a} cha Katiba kitakuwa na nguvu za Kikatiba kumpa uwezo wa Rais aliyopo madarakani kuendelea na madaraka ya Urais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Alisema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi anapatikana kwa mujibu wa masharti ya Kifungu cha 27 cha Katiba ambacho Rais anachaguliwa kufuatana na Katiba Hiyo na kwa mujibu wa Sheria yoyote itakayotungwa na Baraza la Wawakilishi hukusu Uchaguzi wa Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Balozi Seif alifahamisha kuwa ili Rais wa Zanzibar apatikane kwa mujibu wa Katiba na sheria ya Uchaguzi nambari 11 ya Mwaka 1984, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar inapaswa kuendesha uchaguzi na hatimae kumtangaza mshindi wa nafasi ya Urais ambae atashika madaraka hayo pale ambapo atakuwa ameapishwa rasmi kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Katiba ya Zanzibar.

Alisema Kifungu cha 28 {1} {a} cha Katiba kinaweka utaratibu kuhusu muda wa kuendelea kuwa kuwa Rais, na kwamba kwa kufuatana na kifungu hicho, mtu aliyechaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ataendelea na dhamana hiyo mpaka pale ambapo Rais anayefuata ale kiapo cha kuwa Rais.

Alieleza kwamba kwa msingi huo wa Kikatiba ni vyema Wananchi wakafahamu na kuelewa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braza la Mapinduzi ataendelea kuwepo madarakani mkapa pale Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar itakapomtangaza mshindi wa kiti cha Urais na Rais Mteule atashika madaraka hayo baada ya kuapishwa rasmi kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Katiba.


Stori ya kugusa

Leo ningependa niwahadithie hii stori ya kugusa sana. Siku moja jamaa alikuwa akipita njiani kuelekea mjini. Alipofika njiani akamkuta paka amelala barabarani, akahisi labda kaumizwa, akaingiwa na huruma hivyo kuanza kumsogelea. Alipomfikia, akamgusa kujua kama amekufa au yupo hai. Alipomgusa, paka hakushtuka. Akamgusa tena, akamgusa tena, tena na tena...
Kama nilivyowaambia mwanzo kwamba hii stori ni ya kugusa.
Siyo wakati wote wavuti.com inaweka 'stori siriaz' tu, bali hata hizi 'silly' zisizo na maana wala mantiki yoyote ila pengine kusababisha sura itabasamu kwa baadhi yetu, kama tunavyotumiwa na wasomaji wengine kupitia WhatsApp.

Jumapili Njema na Juma jema linaloanza kesho!

Wabunge wateule watakiwa kuanza kujisajili katika Ofisi za BungeTafrija ya UKAWA ya shukurani - Lowassa: "Safari ndiyo imeanza"


Aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CHADEMA, Edward Lowassa amesema awamu ya pili ya safari yake ya kuelekea Ikulu ndio kwanza imeanza na kuwataka watu wote wanaomuunga mkono kutokata tamaa.

Lowassa, ambaye ameshika nafasi ya pili katika mbio za urais wa Jamhuri ya Muungano akiweka rekodi ya kukusanya kura milioni 6.07 ambayo ni rekodi kwa mgombea wa upinzani, alitoa kauli hiyo jana mchana katika hafla ya chakula cha mchana ya kuishukuru timu yake ya kampeni iliyofanyika Kawe, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wakuu wa vyama vinavyounda UkKAWA, wanahabari na familia yake.

“Nimefarijika sana, asanteni kwa msaada mlionipa, sina cha kuwalipa,” alisema waziri huyo mkuu wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne aliyeihama CCM na kujiunga na CHADEMAmwezi Julai.

“Ukweli ni kwamba kila mmoja alifanya kazi yake. Tujiandae kwa awamu ya pili na safari ndiyo imeanza,” alisema na kushangiliwa.

“Unaweza kuchelewesha bahati ya mtu, lakini hauwezi kuiondoa,” aliongeza.

Hata hivyo, Lowassa hakueleza awamu ya pili itahusisha mambo gani.

Tangu kumalizika kwa uchaguzi huo, Lowassa amezungumza na vyombo vya habari mara mbili, mara ya mwisho akieleza jinsi alivyowasilisha pingamizi lenye hoja tatu kuhusu mwenendo wa uchaguzi kwa mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva ambalo liligonga mwamba.

Katika tamko lake, Lowassa alikuwa akipinga matokeo ya kura za urais yaliyokuwa yakitangazwa na NEC akidai kuwa si halisi na kuitaka isitishe kutangaza, lakini tume hiyo haikueleza lolote na badala yake iliendelea kutangaza matokeo ya majimbo na baadaye mshindi wa urais.

Mambo hayo matatu yaliyowasilishwa NEC ni kupunguzwa kwa kura zake, kuongezewa kura kwa mgombea wa CCM na kutangazwa matokeo batili kwa wagombea wa UKAWA.

Lowassa aliyeanza kwa kuwatambulisha watu wake wa karibu waliomshauri masuala muhimu na nyeti katika kampeni, akiwemo Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, alizungumza kwa kifupi, akitoa mfano wa jinsi majeshi ya ukombozi wa nchi mbalimbali barani Afrika yalivyorudi nyuma kujipanga baada ya kushindwa.

Muda mfupi kabla ya Lowassa kueleza hayo, mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe aliufananisha Uchaguzi Mkuu na vita, akisema kulikuwa na njama za makusudi za kuhakikisha Lowassa hapati ushindi.

Alisema wagombea ubunge kutoka vyama vinavyounda UKAWA vya NCCR-Mageuzi, CHADEMA, NLD na CUF, waliibiwa kura na ushindi kupewa wagombea wa CCM.

Mbowe alisema kwa kuwa hawawezi kupinga matokeo ya urais mahakamani, watafungua kesi za kupinga matokeo ya ubunge.

“Tunachofanya, tunarudi nyuma, tunajipanga kukata rufaa kupinga matokeo katika majimbo zaidi ya 30,” alisema Mbowe.

“Wagombea wetu waliokuwa wabishi na kupigana kwelikweli walitangazwa washindi, lakini kuna majimbo ambayo wagombea wetu waliporwa ushindi waziwazi kabisa. Kwa kuwa ubunge unapingwa mahakamani tutafanya hivyo,” alisema Mbowe.

Miongoni mwa majimbo ambayo matokeo yake yalikuwa na ubishi ni Nyamagana, ambako mbunge maarufu wa CHADEMA, Ezekiah Wenje alishindwa na mgombea wa CCM, Stanslaus Mabula baada ya mvutano uliochukua muda mrefu. Pia mbunge wa NCCR Mageuzi, David Kafulila wa Kigoma Kusini aliangushwa baada ya matokeo kuibua mzozo mkali uliosababisha polisi kuingilia kati.

Mbowe pia alisema kuwa wanahamishia nguvu Zanzibar kuungana na mgombea urais kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad kudai haki yake.

Mbowe alisema kitendo cha kufutwa kwa uchaguzi huo kina mkanganyiko mkubwa na kusisitiza kuwa kuanzia wiki ijayo UKAWA itapiga kambi kwenye visiwa hivyo kuhakikisha haki inatendeka.

Baadhi ya viongozi wa UKAWA waliohudhuria hafla hiyo ni makamu mwenyekiti wa CHADEMA –Bara, Profesa Abdallah Safari, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi na Mbunge mteule wa Vunjo, James Mbatia na Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Salum Mwalimu.
  • [Mwananchi]

Wapandwa jazba katika uwanja wa CCM, Mkwakwani


Kura "zilizopigwa" zenye mhuri wa NEC zaokotwa Njoro, Moshi


Siku ya maruhani "Halloween Day" na Zanzibar iliyosibiwa "haunted house"

Wana maruhani wakiwa katika kwaride. (Photo Jefferson Siegel/New York daily news)
Jana ililkuwa ni "Siku ya Maruhani" nchini Marekani. Siku hii ijulikanayo kama "Halloween" husherehekewa kila tarehe 31 Oktoba, na ina historia ndefu.

Statement by the Scholars of Zanzibar regarding 2015 General Elections


Statement by State House regarding claims by CUF on situation in Zanzibar

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz               

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
     STATE HOUSE,
             1 BARACK OBAMA ROAD,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

STATE HOUSE STATEMENT
The State House has learnt, with regret, claims by the Secretary General of the Civic United Front (CUF) and its Presidential candidate in this year’s General Elections in Zanzibar, Honorable Seif Shariff Hamad, that he has been ignored and his request for an appointment with President Jakaya Mrisho Kikwete, to discuss the political situation in Zanzibar, turned down.
The State House would like to categorically deny that it has received any request from Honorable Hamad for him to meet President Kikwete since voting day in Zanzibar on Sunday and subsequent nullification of the election process in Zanzibar by the Zanzibar Electoral Commission (ZEC) Chairman Jecha Salim Jecha on Tuesday.
What President Kikwete has received, are complaints by CUF about some actions from some sections of the Police Force in Zanzibar and a request for him to facilitate a conversation between Honorable Hamad and the Chief of the Armed Forces (CDF) General Davis Mwamunyange.
Subsequently, President Kikwete, who is also Commander-in–Chief, has instructed the Inspector-General of Police Ernest Mangu to investigate these claims by CUF and report back to him. Accordingly, he has also instructed his office to facilitate a conversation between General Mwamunyange and CUF officials.
The State House would like to confirm that President Kikwete is as concerned about the political and security situation in Zanzibar as every Tanzanian is, and has been working tirelessly and consulting widely over the last few days to find amicable and peaceful resolution to the situation in Zanzibar.
While the matter remains firmly in the hands of an independent electoral body in Zanzibar, President Kikwete would like to express his readiness to do whatever is in his powers to regularize the situation in Zanzibar.
ISSUED BY THE DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
STATE HOUSE
DAR ES SALAAM.
31, OCTOBER, 2015

Picha za ibada ya kumbukumbu ya marehemu Godfrey Mngodo, Marekani


Pr. Mwakabonga akiongoza ibada ya kumbukumbu ya marehemu Godfrey Mbiu Mngodo iliyofanyika siku ya Jumamosi Octoba 31, 2015 Columbus, Ohio nchini Marekani na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wakiwemo wafanyakazi wa kituo cha utangazaji Sauti ya Amerika idhaa ya Kiswahili (VOA). Marehemu Godfrey Mbiu Mngodo aliaga Dunia Tarehe 11 Septemba, 2015 Dar es Salaam na kuzikwa Tanga. Godfrey Mbiu Mngodo amefanya kazi katika sehemu mbalimbali kama Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD), Voice of America, wizarani na kituo cha Channel Ten ameacha watoto 10 na wajukuu 14. PICHA NA KWANZA PRODUCTION/VIJIMAMBO

Mmoja ya mtoto wa marehemu Michael Mngodo akiwa na mwanae Alvin wakifuatilia ibada ya kumbukumbu ya mpendwa baba yake marehemu Godfrey Mbiu Mngodo iliyofanyika siku ya Jumamosi Octoba 31, 2015 Columbus, Ohio nchini Marekani.

Familia ya Mngodo ikifuatilia Ibada.

Pr. Mwakaboma akifanya maombi kwa wanafamilia.

Michael Mngodo akisoma wasifu wa mpendwa baba yake. Kulia ni mtoto wake Alvin.

Ndugu, jamaa na marafiki wakifuatilia ibada. Kwa picha zaidi bofya bofya hapa.