Mrema kwenda mahakamani kupinga Ubunge wa Mbatia


Uchaguzi Mkuu Tanzania 2015 haukuwa huru wala wa haki - Dk Semakafu, ULINGO


Mafuriko ya maji ya mvua yaua wawili Mwanza
Watu wawili wamefariki dunia kutokana na mafuriko ya mvua kubwa iliyonyesha kwa saa kadhaa leo jijini Mwanza, akiwamo mwanafunzi wa kidato cha nne aliyesombwa na maji wakati akiwahi kufanya mitihani ya mwisho lakini mwili wake haujapatikana mpaka sasa.

Mvua hiyo iliyoanza kunyesha saa 12 asubuhi, ilikatika saa 4:30 asubuhi na kusababisha baadhi ya barabara kuziba kutokana na maji kuporomoka kutoka milimani.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo, amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo ingawa hadi wakati anatoa taarifa hizo, mwili mwanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya sekondari Nyamanoro, ulikuwa haujapatikana.

“Mvua kubwa ilinyesha kwa masaa manne katika maeneo mbalimbali ya jiji iliyosababisha maporomoko kutoka milimani na kusababisha watu kukosa sehemu ya kupita hasa eneo la Kirumba ambako mwendesha bodaboda namba MC861 AHK aliyewapakiza wanafunzi wawili wa kidato cha nne, kusombwa na maji na dereva huyo kufariki lakini wanafunzi wakiokolewa,” alisema Mkumbo.

Kamanda Mkumbo amemtaja mwanafunzi wa shule ya sekondari Nyamanoro ambaye mwili wake haujapatikana ni, Zainabu Shabani (18) aliyekuwa na wenzake wawili waliokuwa wakivuka daraja llilopo maeneo ya Nyamanoro wilaya ya Ilemela.

“Wenzake walifanikiwa kuvuka daraja salama, lakini Zainabu hakumaliza safari yake na kusombwa na maji mpaka na sasa hajulikani kama amekufa ama yupo hai kutokana na mwili wake kutoonekana,” alisema.

Mkumbo aliwataka wananchi kuacha tabia ya kuvuka mitaro na maeneo yaliyojaa maji pindi wanapoona mvua kubwa inanyesha ili kuepuka vifo na mataizo yanayoweza kuepukika. [via Pamoja Pure blog]


Picha via WhatsApp
Picha via WhatsAppMvua yasababisha uharibifu SumbawangaPolisi Shinyanga, Singida, Dar, Pwani, Morogoro yazuia kuandamana Novemba 3

Nakala kutoka Malunde1 blog
Katibu wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini, George Kitalama amesema hawajapata taarifa wala maelekezo yoyote kuhusu kuzuiwa kwa maandamano yao na wanaendelea kujiandaa na wanachama wao kwa maandamano kama walivyopewa maagizo na viongozi wao wa Kitaifa.

Amesema kesho tarehe 03.11.2015, watafanya maandamano ya amani kuanzia ofisi za CHADEMA Wilaya kisha kuzunguka mji mzima wa Shinyanga kuanzia saa tatu asubuhi kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Taifa, NEC.

Amesema kwamba ni maandamano ya nchi nzima.

Polisi Singida yapiga marufuku maandamano Novemba 3


JESHI la polisi Mkoani Singida limepiga marufuku maandamano yaliyopangwa na vyama vya siasa vilivyosimamisha mgombea wa Urais chini ya mwavuli wa UKAWA, kufanyika Novemba 03, mwaka huu kwa nchi nzima kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na Tume ya uchaguzi nchini (NEC).

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake, Kamanda wa polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa polisi (ACP) Thobias Sedoyeka amesema pamoja na kupinga matokeo hayo yaliyotangazwa na NEC, vyama hivyo vinaitaka pia mamlaka husika kumtangaza mgombea wao katika Uchaguzi, Edward Lowasa wakiamini kuwa ndiye mshindi wa kiti cha Urais.


Polisi Kanda ya Pwani (Pwani, Dar es Salaam, Morogoro) yapiga marufuku maandamano Novemba 3
KK ya Halmashauri Kuu CCM yafuta walioteuliwa kuwania Ubunge Handeni Mjini

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM iliyokutana leo, Novemba 02, 2015 chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete imejadili kwa kina mapendekezo ya wana CCM walioomba ridhaa ya kugombea ubunge katika jimbo la Handeni Mjini.

Kamati Kuu imetengua mapendekezo ya awali na kuagiza kurejewa kwa mchakato wa kura za maoni kwa wana-CCM wawili walioongoza kura za maoni za awali.

Wana-CCM hao watakaopigiwa kura za maoni tena kesho Novemba 03, 2015 ni pamoja na Omari Abdallah Kigoda na Hamis Hamad Mnondwa.

Aidha Kamati Kuu imeteua wajumbe watatu kusimamia zoezi hilo ambao ni Dk. Maua Daftari, Dk.Emmanuel Nchimbi na Alhaji Abdallah Bulembo.

Rais Kikwete ateua Katibu Tawala mkoa wa Lindi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Ramadhan Kaswa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi kuanzia Oktoba  30, mwaka huu, 2015.

          Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Kaswa alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa Msaidizi, Mkoa waTanga.
Imetolewana:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.


2 Novemba, 2015

Picha kutoka kwenye ibada ya marehemu Gren Judica Moshi iliyofanyika Washington DCNdugu, jamaa na marafiki mbalimbali, jana (Novemba mosi 2015) walijumuika na wanafamilia katika misa na kusherehekea maisha ya Mama Gren Judica Moshi iliyofanyika hapa Washington DC.

Taarifa ya TMA ya hali ya hewa na mvua za vuli 2015


[picha] Fasheni na burudani katika utambulisho wa kipindi kipya cha Tv cha Kiswahili Marekani

Mwanzilishi wa Jambo Tv Show, Steven Mghaza (katikati) akizungumza na Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi waTanzania nchini Marekani Swahiba Mndeme na baadhi ya waliohudhuria uzinduzi huo
Jumamosi, Oktoba 31, Swahili Media Network LLC kwa ushirikiano na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapa Washington DC walitambulisha kipindi kipya cha Televisheni cha Kiswahili JAMBO TV SHOW kitakachoonekana kwenye kituo cha Televisheni cha DCTV hapa Marekani.

Taarifa ya kutaka uongozi wa Halmashauri Kilombero kuondoka madarakani