Magazetini Novemba 5, 2015


[update] Kuapishwa kwa Magufuli kuwa Rais wa Tanzania na Samia Suluhu Hassan, Makamu


Overview: Mgawanyo wa Viti Maalum Bungeni 2015


Vyama vitatu kati ya 22 vya siasa vilivyoshiriki kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, ndivyo vyenye uhakika wa kupata wabunge wa viti maalumu ambao majina yao yatatangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kesho.

Vyama vya CCM, Chadema na CUF, vinatarajiwa kupata wabunge hao kutokana na jumla ya kura za wabunge majimboni, kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 78 (1) kinachoelekeza kuwa chama kilichofikisha asilimia 5 ya kura zote halali za wabunge, ndiyo kitakachopendekeza majina ya wabunge wa viti maalumu.

Wabunge wa viti maalumu wanaotarajiwa kupatikana ni 112, sawa na asilimia 40 ya wabunge 264 wa majimbo, ambao watajumuika na 10 wa kuteuliwa na Rais, watano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Spika (ikiwa atachaguliwa kutoka nje ya wabunge) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge wa Chadema, John Mrema alisema jana kuwa pamoja na kuwa majimbo mengine hayajafanya uchaguzi, chama hicho kilichopata wabunge 34 hadi sasa, kinaweza kupata wabunge 52 wa viti maalumu.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya alisema wanatarajia kupata wabunge wa viti maalumu 12, licha ya kushinda majimbo 35, kwa kuwa wabunge wengi walioshinda ni wa majimbo ya upande wa Zanzibar.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajabu Luhavi alisema wamefanya majumuisho ya kura za chama hicho, wamepata asilimia 73 ya kura, hivyo wanatarajia kuwa watapata wabunge wa viti maalumu wengi kuliko vyama vingine.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhan Kailima alisema wanaendelea na kazi ya uchambuzi wa fomu za wanawake zilizowasilishwa na vyama mbalimbali vya siasa, ili kuwapata wabunge wa viti maalumu ambao majina yao yatatolewa baada ya kazi hiyo kukamilishwa.

“Tangu Septemba 25, vyama vyote vya siasa vilituletea majina ya wanawake wanaotarajia kupata ubunge wa viti maalumu, tunaendelea kuchambua fomu zao ili tuhakiki sifa walizopendekezwa na vyama vyao kwa idadi inayotakiwa kabla ya kuwatangaza,” alisema Kailima.

Alisema orodha ya majina ya wagombea iliyowasilishwa kwa Tume na kila chama, ndiyo itakayotumiwa na NEC.

Samatta among the top 10 for the 2015 CAF African Player of the Year


Tanzanian and TP Mazembe club soccer player, Mbwana Samatta has entered the list of 10 players who are vying for the prize of  the African Player of the Year (Based in Africa) 2015.

The winner of the award is determined by votes and coaches with technical directors of the member countries of African football (CAF).

The names African Player of the Year (Based in Africa) nominees are:
 1. Abdeladim Khadrouf (Morocco & Moghreb Tetouan)
 2. Baghdad Bounedjah ( Algeria & Etoile du Sahel)
 3. Felipe Ovono (Equatorial Guinea & Orlando Pirates)
 4. Kermit Erasmus (South Africa & Orlando Pirates)
 5. Mbwana Aly Samatta (Tanzania & TP Mazembe)
 6. Mohamed Meftah ( Algeria & USM Alger)
 7. Mudather Eltaib Ibrahim ‘Karika’ (Sudan & El Hilal)
 8. Robert Kidiaba Muteba ( DR Congo & TP Mazembe)
 9. Roger AssalĂ© (Cote d’Ivoire & TP Mazembe)
 10. Zineddine Ferhat (Algeria & USM Alger)
The winner will be decided by votes of the Coaches or Technical Directors of the National Associations affiliated to CAF and the awards gala will be held on Thursday, 7 January 2016 in Abuja, Nigeria.Kituo cha redio chafungwa kwa kutangaza tamko la Maalim Seif Oktoba 26

KADHIA ya ufutwaji uchaguzi wa Zanzibar ikiwa haijapatiwa ufumbuzi, kumekuwa na hatua za ukandamizaji wa uhuru wa habari hapa Zanzibar na tayari madhara yametokea.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilichukua hatua katili tarehe 26 Oktoba 2015, ilipoamuru kufungwa kwa kituo kipya cha redio cha Swahiba FM kwa maelezo kuwa kimevunja sheria.

Mkurugenzi wa kituo hicho, Kassim Suleiman ameiambia MwanaHALISI Online, kwamba kituo hicho kilifungwa kwa uonevu kwa sababu “hata utaratibu wa kisheria haukufuatwa.”

Kwa mujibu wa Sheria ya Utangazaji ya Zanzibar, amesema hatua kama hiyo huchukuliwa baada ya mmiliki wa kituo chenyewe kufahamishwa na kuwa amepewa nafasi rasmi ya kujitetea baada ya kujulishwa kosa linalodaiwa kuwa limefanywa na kituo.

Kassim ambaye aliwahi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Sauti ya Tanzania Zanzibar (STZ) kabla ya kubadilishwa na kuwa Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC), alisema amelalamika rasmi kwa barua kwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar (ZBC).

Kosa lililotajwa kuwa kituo hicho kimefanya ni kutangaza tamko la Maalim Seif Shariff Hamad la Oktoba 26 la kwamba alikuwa anaonesha kuwa na kura nyingi na kutaka Tume ya Uchaguzi itangaze matokeo bila ya kuchelewa.

Taarifa za ndani ya Tume ya Utangazaji zinasema uamuzi huo wa kufunga kituo cha Swahiba FM, kinachoendeshwa na kampuni inayomilikiwa na Chama cha Wananchi (CUF), umechukuliwa bila ya Bodi ya Tume kujua.

Kisheria uamuzi wowote kama huo utachukuliwa baada ya Bodi kujadili tuhuma na kutoa uamuzi wake. Mjumbe mmoja wa Bodi hiyo ameithibitishia MwanaHALISI Online, kuwa hawakukaa kujadili suala hilo.

Juzi askari wa Jeshi la Polisi walivamia maeneo mbalimbali ya mji wa Zanzibar na kukamata wauza magazeti, na kukamata wafanyakazi wa duka la vitabu na machapisho la BMC kwa kuwa lilikuwa likitoa nakala za gazeti la MwanaHALISI la Jumatatu baada ya gazeti hilo kutoonekana mitaani muda mfupi lipobainika.

Job: Project Director (COP), ARISE II - Tanzania

Organization: Winrock International
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 30 Nov 2015

Maelezo mafupi kumhusu mhubiri T.B. Joshua

Mhe. Edward Lowassa akimkaribisha mgeni wake, muhubiri wa Kimataifa kutoka nchini Nigeria, T. B. Joshua, wakati alipomtembelea nyumbani kwake, Masaki Jijini Dar es Salaam, Novemba 4, 2015. (picha: Othman Michuzi)
Maelezo kwa mujibu wa tovuti ya John Kitime (johnkitime.co.tz)

Temitope Balogun Joshua (T.B. Joshua) alizaliwa tarehe 12 Juni 1963, katika kijiji kidogo cha Arigidi kilichoko Akoko, Jimbo la Ondo, Nigeria. Inasemekana mama yake alikaa na mimba kwa miezi 15, kabla Temitope hajazaliwa. 

Katika kabila lake kulikuweko na hadithi ya zaidi ya miaka 100 ambayo ilitabiri kuwa kuna mtoto atazaliwa katika familia masikini, ambaye Mungu atamtumia sana, na wengi kule kwao huamini kuwa Temitope ndie aliyetajwa katika utabiri huo. Siku tatu baada ya kuzaliwa kwake, jiwe kubwa lilirushwa kutoka kwenye sehemu kulikokuwa kunapasuliwa mawe, jiwe hilo lilitoboa bati na kumkosa kosa Temitope kwa sentimita chache. Na ndipo mama yake alimpa jina la Temitope, likiwa na maana ‘Ulichonipa Mungu lazima kishukuriwe’. 

Jina analojulikana sana sasa ni T. B. Joshua. 

TB Joshua ni muhubiri mwanzilishi na kiongozi wa The Synagogue, Church of All Nations (SCOAN), hii ni taasisi ya kidini inayoendesha Emmanuel TV, Tv ambayo huonekana kote duniani ikiwa inarushwa kutoka Lagos Nigeria. TB Joshua anasemeka ni moja ya watu 50 wenye ushawishi zaidi Afrika, anajulikana sana kwenye mitandao ya Facebook ambako anawafuasi zaidi ya milioni moja laki tano, na video zake nyingi zilizomo kwenye Youtube. Kwa mujibu wa Forbes, mwaka 2011 TB Joshua alikuwa mtu wa tatu kwa utajiri nchini Nigeria. 

Wakati akiwa shule alijulikana kwa jina la Balogun Francis, alisoma shule ya St. Stephen’s Anglican Primary School ya Arigidi-Akoko, kati ya mwaka 1971 na 1977, lakini hakumaliza sekondari. Wakati yuko shule alijulikana kama “small pastor” kutokana na kupenda sana biblia, baada ya kuacha shule alifanya kazi mbalimbali ndogo ndogo, hatimae akaanzisha darasa la biblia kwa watoto, wakati huohuo akaanza kujiendeleza kwa masomo ya jioni. Hatimae akaamua kwenda kujiunga na jeshi la Nigeria, lakini kwa bahati mbaya akaachelewa treni kwenda kwenye usaili na hivyo ndoto hiyo ikaishia hapo.

Kwa maelezo yake mwenyewe anaeleza jinsi alivyokabithiwa upako wake, “ Nilikuwa katika hali ya kuzimia kwa siku tatu mfululizo, nikaona mkono ukielekeza Biblia kwenye moyo wangu, na Biblia ikaingia kwenye moyo wangu na moyo wangu wa zamani ukachanganyika na Biblia. Ufahamu uliponijia nikawaona Mitume na Manabii wa zamani wako na mtu ambaye sikuweza kuona kichwa chake kwa sababu alikuwa mrefu sana amefika mpaka mbinguni. Nikaamini kuwa alikuwa ndie Bwana wetu Yesu Kristo, nami nikajiona nimo katika hawa Manabii na Mitume wa zamani. 

Nikauona mkono wa yule mtu mrefu sikuweza kuona uso wake maana ulikuwa na mwanga mkali sana sikuweza kabisa kuangalia uso wake. Lakini Mitume wengine niliweza kuwaona. Mitume Peter na Paul, Manabii Moses, Eliya na wengine, kwani majina yao yalikuwa yameandikwa kwa herufi kubwa vifuani mwao. Nikasikia sauti inasema, “Mimi ni Mungu wako, nakupa upako nenda kafanye kazi ya baba yako wa mbinguni.” 

Wakati huohuo yule mtu mrefu akanipa Msalaba na Biblia iliyokuwa kubwa kuliko ile iliyoingia moyoni mwangu. Akaniahidi kuwa kila nitakapo tumia muda wake na jina lake nitapata Msalaba mkubwa zaidi, nikienda kinyume na mambo yatakuwa kinyume. Nikasikia sauti ya yule mtu mrefu ambaye sikuwa naweza kuona kichwa chake ikasema,’ Mimi ndie Bwana wako, niliyekuwa na ambaye ndie, mimi ni Yesu Kristo ninaetoa amri kwa mitume na manabii wote. Sauti ile ikasema tena ‘Nitakuonyesha mambo mazuri ya ajabu na nitajionyesha kupitia mafunzo, mahubiri, miujiza, ishara, kwa ajili ya kuokoa roho za watu. Kutoka wakati huo nimekuwa napata maono kila mwaka na Msalaba mkubwa zaidi ukiwa na maana majukumu makubwa zaidi”

SCOAN ina tawi moja tu nalo liko Ghana, kwa sasa kila Jumapili kuna ibada Nigeria ambayo huhudhuriwa na kiasi cha watu 15,000 kila Jumapili. Uponyaji ni kati ya mambo mengi yanayofanywa katika kanisa la TB Joshua watu wengi wamekuwa wakisema wamepona maradhi mbalimbali kutokana na kufika kanisani hapo na kwa kutumia maji, ‘annointed water’ ambayo hutolewa na TB Joshua. 

Wakati wa tatizo la Ebola TB Joshua alisema maji hayo yanaweza kutibu ugonjwa huo na alituma chupa 4,000 za maji hayo zikiambatana na dola 50,000 kwenye serikali ya Sierra Leon. Hili lilikuja hasa baada ya maafisa afya wa Lagos walipomtembelea TB Joshua kumtaka asiwaruhusu wagonjwa Ebola kuja katika kanisa hilo kwa kuondoa uwezekanao wa kupata mlipuko wa ugonjwa huo katika jiji hilo. Wasanii wa Nollywood kama Jimmy Iyke na Camilla Mberekpe pia ni kati ya watu wengi waliowahi kupata huduma za kuondoa mapepo katika miili yao katika kanisa hilo.

Pia TB Joshua anasemekana ameweza kutabiri mambo mengi ikiwemo kifo cha Michael Jackson, milipuko ya Boston na hata matokeo ya mechi mbili za fainali za AFCON, ambapo moja mshindi alikuwa Zambia na nyingine Nigeria ilichukua ushindi. Amesha wahi kutabiri kuhusu kifo cha Rais mmoja wa Afrika na inasemekana Bingu Mutharika wa Malawi ndie aliyetabiriwa wakati huo. Pia anasemekana kutabiri kuhusu ndege ya Malaysian Airline iliyopotea baharini, miezi kadhaa kabla ya tukio hilo. 

Huyo ndiye TB Joshua ambaye alitua Tanzania jana kudhuria kuapishwa kwa Dk John Pombe Magufuli.

T.B. Joshua azungumza na viongozi wa UKAWA

Muhubiri wa Kimataifa kutoka nchini Nigeria, T. B. Joshua (shati la miraba), akizungumza jambo na wenyeji wake, aliekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA kupitia mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa na viongozi wakuu wa UKAWA, Freeman Mbowe,  James Mbatia pamoja na mwanasiasa mkongwe nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, wakati alipofika nyumbani kwa Lowassa, Masaki jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo maalum.

Lowassa na mgeni wake, Joshua alipomtembelea kwa mara nyingine nyumbani kwake, Masaki Jijini Dar es Salaam leo Novemba 4, 2015.


Zimbabwe President, Robert Mugabe arrives in TanzaniaWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe (katikati chini) akimsubiria Rais wa Zimbabwe Mhe. Robert Mugabe (katikati juu kwenye ngazi) alipokuwa akiteremka kwenye Ndege, Rais Mugabe amewasili nchini kwaajili ya kuhudhuria Sherehe za uapisho wa Rais Mteule Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli zitakazofanyika hapo kesho katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

SMZ kufikisha mahakani ZEC 'waliovuruga kura' za Uchaguzi Mkuu 2015


CCM yamteua Omary Abdallah Kigoda kugombea Ubunge Handeni Mjini


Gazeti la Mwananchi: Makala ya Prof. Lipumba kuhusu ZEC na Zanzibar 2015

 • Makala iliyonukuliwa hapa, imeandikwa na Ibrahim Haruna Lipumba na kuchapishwa kwanza na gazeti la MWANANCHI

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwamo Zanzibar ilifanya Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, 2015. Kwa upande wa Visiwani, Wazanzibari walipiga kura kumchagua diwani, mwakilishi, Rais wa Zanzibar, mbunge wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kutumia Daftari la Wapigakura la ZEC.

Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) imetumia matokeo ya kura za Rais katika majimbo ya Zanzibar kujumlisha na matokeo ya majimbo ya Bara na hatimaye kumtangaza Dk John Magufuli kuwa mshindi wa kiti cha Rais katika Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano. Kwa uamuzi huo wa kuchukua matokeo ya majimbo ya Zanzibar yaliyotumia Daftari la Wapigakura la ZEC na kupiga kura kwenye vituo vilivyoandaliwa na ZEC, Tume ya Uchaguzi ya Taifa inatambua kuwa uchaguzi uliofanyika Zanzibar chini ya usimamizi wa ZEC ni halali na matokeo yake ni halali.

Oktoba 28, siku tatu baada ya uchaguzi, Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha alitangaza kuwa uchaguzi wa Zanzibar umefutwa. Alipokuwa anatangaza alikuwa peke yake. Makamu Mwenyekiti hakuwepo. Mkurugenzi wa ZEC hakuwepo. Wajumbe wengine wa Tume hawakuwepo. Wajumbe wa ZEC walikuwa Bwawani wakimsubiri Mwenyekiti wao. Walijaribu kuendelea na kazi ya kuhakiki matokeo chini ya uongozi wa Makamu Mwenyekiti. Hawakuweza kuendelea na kazi hiyo baada ya Makamu Mwenyekiti kuondolewa na vyombo vya dola.

Sababu ambazo Mwenyekiti ametoa za kufuta uchaguzi ni pamoja na eti makamishna wa uchaguzi katika Tume hiyo walidundana kutokana na tofauti zao. Makamishna walikuwa wanapendelea vyama vyao. Katika vituo vingine, hasa Pemba, kura zilizopigwa zilikuwa zaidi ya zilizosajiliwa. Masanduku ya kupigia kura hayakupewa ulinzi wa kutosha na mawakala pamoja na maofisa wa uchaguzi. Mawakala wa vyama walifukuzwa katika vituo kadhaa. Vijana walivamia vituo vya kupigia kura wakiwa na lengo la kuzua ghasia na kadhalika.

Sababu za Mwenyekiti hazina mashiko. Malalamiko haya yalipaswa kutolewa na mawakala wa vyama mapema. Vituo vya kupigia kura vilikuwa na ulinzi wa kutosha wa vyombo vya dola. Watazamaji wa ndani na nje walisifia namna upigaji wa kura Zanzibar ulivyokuwa wa amani na utulivu.

Jecha alieleza kwamba, “Kwa kuzingatia hayo na mengine mengi ambayo sijayaeleza, Mimi Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, nimeridhika kwamba uchaguzi huu haukuwa wa haki na kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria na taratibu za uchaguzi. Hivyo kwa uwezo nilionao natangaza rasmi uchaguzi huu na matokeo yake yote yamefutwa na kwamba kuna haja ya kurudia uchaguzi huu.” Mwenyekiti Jecha hakuvitaja vifungu vya Katiba na sheria vinavyompa mamlaka ya kufuta uchaguzi.

Sura ya tisa ya Katiba ya Zanzibar inaelezea pamoja na mambo mengine uundwaji, mamlaka na taratibu za uamuzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar. Hakuna kifungu chochote cha Katiba kinachoipa tume au mwenyekiti wake maamlaka ya kufuta uchaguzi. Katiba inaeleza bayana kuwa uamuzi wa masuala yote unafanywa na tume kwa pamoja. Kifungu cha 119(10) kinaeleza kuwa “Kiwango cha mikutano ya Tume ya Uchaguzi ni Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti na wajumbe wanne na kila uamuzi wa tume ni lazima uungwe mkono na wajumbe walio wengi.” Mwenyekiti Jecha hakueleza kikao gani cha Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kilichokaa na kufikia uamuzi aliotangaza. Ukweli ni kwamba Jecha amevunja Katiba ya Zanzibar kwa kutoa uamuzi mzito bila kufuata taratibu zilizowekwa na Katiba ya Zanzibar. Uamuzi wake ni batili na hauna nguvu ya kisheria. Katiba na sheria ya Zanzibar hazijampa mamlaka mwenyekiti na hata tume yote kufuta uchaguzi. Kufanya hivyo ni kuvunja Katiba ya Zanzibar.

Inaelekea mwenyekiti amepewa shinikizo na ndiyo maana hakuwashirikisha wajumbe wengine wa ZEC. Bila shaka waliomshinikiza Mwenyekiti wa ZEC kuvunja Katiba watawashinikiza wajumbe wengine wa ZEC kuunga mkono uvunjaji wa Katiba uliofanywa na mwenyekiti wao.

Athari za kufuta uchaguzi ni kuleta vurugu za kisiasa na maafa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Kwa kuwa matokeo ya kura za Zanzibar kwa uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano hayaathiri ushindi wa mgombea wa CCM, matokeo hayo yamekubaliwa. Matokeo ya kura za uchaguzi wa Rais wa Zanzibar uliofanyika katika mazingira yaleyale na kutumia Daftari la Wapigakura la ZEC yanakataliwa kwa sababu mgombea wa CCM ameshindwa. Mwenyekiti wa ZEC ameshinikizwa kufuta uchaguzi wote wa Zanzibar.

Ni wazi wananchi wengi wa Zanzibar hawawezi kukubali kurudia uchaguzi kwa sababu wenye vyombo vya dola wameamua lazima CCM ishinde ndiyo matokeo ya uchaguzi yakubaliwe. CCM inawaeleza Wazanzibari mabadiliko ya Serikali hayawezi kuletwa na vikaratasi vya kura. Mapinduzi daima maana yake lazima CCM itawale Wazanzibari wakitaka au wasitake. CCM inawaeleza Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kama wanataka mabadiliko aslani hawatayapata kupitia visanduku vya kura. Watafute njia nyingine. Hili ni jambo la hatari.

Nilidhani CCM imejifunza tangu matukio ya 2001 baada ya uchaguzi wa 2000, uchaguzi wa majimbo 16 ulifutwa na kurudiwa.

CUF ilipotoa taarifa ya kufanya maandamano ya amani nchi nzima kudai tume huru ya uchaguzi, Katiba Mpya yenye misingi ya demokrasia, utawala bora na kurudiwa kwa uchaguzi wote wa Zanzibar kama ilivyopendekezwa na watazamaji wa uchaguzi wa ndani na wa nje, mimi binafsi nilikamatwa nikapigwa na kuvunjwa mkono na kutupwa jela. Dhahama hiyo iliwakuta wanachama na viongozi wengine wa CUF. Wananchi wa Zanzibar walipojaribu kuandamana Januari 27, zaidi ya watu 60 waliuawa na kwa mara ya kwanza Watanzania zaidi ya 2000 walikimbia nchi yao kwenda Kenya kunusuru maisha yao. Watanzania tusikubali wanaoishinikiza ZEC kuturudisha huko.

Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano, Dk John Magufuli ataapishwa Novemba 5, 2015 na ndiye atakayekuwa Amiri Jeshi Mkuu. Rais Jakaya Kikwete hatamtendea haki Rais Magufuli kumwachia mgogoro wa Zanzibar ambao anaweza kuutatua.

Uchaguzi umefanyika Zanzibar na kwa kuzingatia matokeo kwenye vituo vyote vya wapigakura yaliyotiwa saini na wasimamizi wa vituo na mawakala wa vyama, mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ameshinda uchaguzi huo. Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ikamilishe uhakiki wa matokeo na kumtangaza mshindi.

Tangu mwaka 1995 sera ya CUF ni kuunda serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar. Katiba ya Zanzibar ya 2010 imeingiza serikali ya umoja wa kitaifa kuwa sharti la kikatiba. CCM watakuwa sehemu ya serikali ya umoja wa kitaifa. Nina uhakika kwa uzalendo wa Kizanzibari wa Maalim Seif, ataunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayowaunganisha Wazanzibari.

Propaganda kubwa dhidi ya CUF ni kwamba ikipewa fursa ya kuongoza Zanzibar, itavunja Muungano. Msimamo rasmi wa CUF ni mfumo wa muungano wa shirikisho lenye serikali tatu ya Zanzibar, Tanganyika na Muungano kama uliopendekezwa na Tume ya Jaji Warioba. Huu ndiyo msimamo wa CUF tangu mwaka 1995 wakati wa uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi. Msimamo huu ulifanana na mapendekezo ya Tume ya Jaji Nyalali. CUF inaheshimu sheria mama ya Jamhuri ya Muungano ambayo ni Makubaliano ya Muungano.

Tume ya Jaji Warioba ilitoa uhuru kwa Watanzania kutoa maoni kuhusu Katiba wanayoitaka. Mjadala huu ulitoa mapendekezo mengi likiwamo la Muungano wa mkataba. Baada ya kuchambua mapendekezo yote, Tume ya Jaji Warioba iliandaa Rasimu ya Katiba yenye mfumo wa Muungano wa serikali tatu. Chama cha CUF na Katibu Mkuu wake waliunga mkono mapendekezo ya Tume ya Jaji Warioba na ndiyo sababu ya kuanzisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) katika Bunge Maalumu la Katiba. Wazanzibari wengi wanaoishi Tanzania Bara wanaunga mkono CUF, lakini pia wanaelewa umuhimu na faida za Muungano. CUF haitavunja muungano bali itauimarisha kwa kutumia njia za demokrasia na sheria kutatua kero za Muungano.

Kufuta uchaguzi wa Zanzibar ni kuwanyima Wazanzibari haki ya kuchagua viongozi wanaowataka. Nikuwaeleza hawawezi kupata mabadiliko kupitia visanduku vya kura. Watafute njia nyingine. Wanaowanyima Wazanzibari haki ya kuchagua viongozi wao kwa utaratibu wa kupiga kura ndiyo wanaoandaa mazingira ya kuvunja Muungano. Rais Kikwete na Rais Ali Mohammed Shein malizeni tatizo msiliingize taifa kwenye balaa na kumuachia Rais mteule mgogoro utakaomzuiwa kusimamia ajenda ya maendeleo ya nchi yetu.

Mwandishi wa makala haya, Profesa Ibrahim Lipumba alikuwa Mwenyekiti wa CUF.

Uchaguzi Mkuu 2015: Orodha ya Wabunge wateule, vyama na majimbo yao


Majina na Jumla ya Wabunge wote wa Bunge la 11 na Majimbo watokayo

1 Dk Charles Tizeba- Buchosa CCM


2 Nimrod Mkono- Butiama CCM


3 Omar Badwel- Chilonwa CCM


4 Kanyasu John- Geita Mjini CCM


5 Pudensiana Kikwembe- Kavuu CCM


6 Sixtus Mapunda- Mbinga Mjini CCM


7 Hassan Masala- Nachingwea CCM


8 Abdallah Chikota- Nanyamba CCM


9 Richard Mbogo- Nsimbo CCM


10 Ester Matiko- Tarime Mjini CHADEMA


11 Mwakajoka Frank- Tunduma CHADEMA


12 Joshua Nassari- Arumeru Magharibi CHADEMA


13 Dk Shukuru Kawambwa- Bagamoyo CCM


14 Andrew Chenge- Bariadi Magharibi CCM


15 Oscar Mukasa- Biharamulo Magharibi CCM


16 Wilfred Lwakatare- Bukoba Mjini CHADEMA


17 Jasson Rwikiza- Bukoba Vijijini CCM


18 Dotto Biteko- Bukombe CCM


19 Eshter Bulaya- Bunda Mjini CHADEMA


20 Raphael Chegeni- Busega CCM


21 Atupele Mwakibete Busekelo- Rungwe Mashariki CCM


22 Bilango Samson- Buyungu CHADEMA


23 Ridhiwani Kikwete- Chalinze CCM


24 Anthony Mavunde- Dodoma Mjini CCM


25 Freeman Mbowe- Hai CHADEMA


26 Mboni Mhita- Handeni CCM


27 Musa Ntimizi- Igalula CCM


28 Dk Dalaly Kafumu- Igunga CCM


29 Musa Hassan Zungu- Ilala CCM


30 Janeth Mbene- Ileje CCM


31 Anjelina Mabula- Ilemela CCM


32 Mchungaji Peter Msigwa- Iringa Mjini CHADEMA


33 William Lukuvi- Isimani CCM


34 Njalu Daud Silanga Itilima- Bariadi Mashariki Mkoa CCM


35 Jumanne Kishimba- Kahama Mjini CCM


36 Josephat Kandege- Kalambo CCM


37 Godfrey Mgimwa- Kalenga CCM


38 Innocent Bashangwa- Karagwe CCM


39 Silvestry Koka- Kibaha Mjini CCM


40 John Mnyika -Kibamba CHADEMA


41 Ally Seif Ungando- Kibiti CCM


42 Hasna Mwilima- Kigoma Kusini CCM


43 Kigua Omari- Kilindi CCM


44 Vinance Mwamoto- Kilolo CCM


45 Peter Lijualikali- Kilombero CHADEMA


46 Vedasto Edger- Kilwa Kaskazini CUF


47 Saidi Bungara- Kilwa Kusini CUF


48 Luhaga Mpina- Kisesa CCM


49 Suleman Nchambi- Kishapu CCM


50 Emmanuel Papian- Kiteto CCM


51 Edwin Sanda- Kondoa Mjini CCM


52 Stephen Ngonyani- Korogwe Vijijini CCM


53 Mary Chatanda- Korogwe Mjini CCM


54 Shanif Mansoor- Kwimba CCM


55 Dk Harrison- Mwakyembe Kyela CCM


56 Innocent Bilakwate- Kyerwa CCM


57 Zubery Kuchauka- Liwale CUF


58 Onesmo ole Nangole- Longido CHADEMA


59 Victor Mwambalaswa- Lupa CCM


60 Cosato Chumi -Mafinga Mjini CCM


61 Boniventura Destery- Magu CCM


62 Dk Norman Sigala- Makete CCM


63 Seif Gulamali- Manonga CCM


64 Mashimba Ndaki- Maswa Magharibi CCM


65 Stanslaus Nyongo- Maswa Mashariki CCM


66 Mangungu Ali- Mbagala CCM


67 Aroon Mulla- Mbarali CCM


68 Joseph Mbilinyi- Mbeya Mjini CHADEMA


69 Augustino Masele- Mbogwe CCM


70 Zacharia Paul Isaay- Mbulu CCM


71 Hassan Hassan- Babali Mchinga CUF


72 Salum Khamis- Meatu CCM


73 Joseph Haule- Mikumi CHADEMA


74 Charles Kitwanga- Misungwi CCM


75 Dustan Kitandula- Mkinga CCM


76 Abdallah Ulega- Mkuranga CCM


77 Rashidi Shangaz- Mlalo CCM


78 Susana Kiwanga- Mlimba CHADEMA


79 Julius Kalanga- Monduli CHADEMA


80 Mgumba Omari- Morogoro KusiniMashariki CCM


81 Anthony Komu- Moshi Vijijini CHADEMA


82 George Lubeleje- Mpwapwa CCM


83 Ezekiel Maige- Msalala CCM


84 Nape Nnauye- Mtama CCM


85 Livingstone- Lusinde Mtera CCM


86 Hawa Ghasia- Mtwara Vijijini CCM


87 Mahamoud Mgimwa- Mufindi Kaskazini CCM


88 Mendrad Kigola- Mufindi Kusini CCM


89 Atashasta Nditiye- Muhambwe CCM


90 Rajab Adadi- Muheza CCM


91 Charles Mwijage- Muleba Kaskazini CCM


92 Pro Anna Tibaijuka- Muleba Kusini CCM


93 Vedastus Mathayo- Musoma Mjini CCM


94 Prof Sospeter Muhongo- Musoma Vijijini CCM


95 Prof Jumanne Maghembe- Mwanga CCM


96 Kangi Lugola- Mwibara CCM


97 Dua Nkuruma- Nanyumbu CCM


98 Cesil Mwambe- Ndanda CHADEMA


99 George Mkuchika - Newala Mjini CCM


100 Alex Rafael Gashaza- Ngara CCM


101 Joram Hongoli Njombe Kaskazini CCM


102 Ally Mohamedi- Nkasi Kaskazini CCM


103 Desderius Mipata- Nkasi Kusini CCM


104 Dk Diodorus Kamala- Nkenge CCM


105 Stanslaus Mabula- Nyamagana CCM


106 Hussein Kassu- Nyangwale CCM


107 Hussein Bashe- Nzega Mjini CCM


108 Jumaa Aweso- Pangani CCM


109 Jenista Mhagama- Peramiho CCM


110 Joseph Selasini - Rombo CHADEMA


111 Mohamed Mchengerwa- Rufiji CCM


112 Saul Amon Rungwe -Magharibi CCM


113 Dk Mathayo David- Same Magharibi CCM


114 Naghenjwa Kaboyoka- Same Mashariki CHADEMA


115 William Ngereja- Sengerema CCM


116 Steven Masele- Shinyanga Mjini CCM


117 Joseph Kakunda- Sikonge CCM


118 Tundu Lissu- Singida Mashariki CHADEMA


119 Ahmed Salum- Solwa CCM


120 Leonidas Gama- Songea Mjini CCM


121 Aeshi Hilaly- Sumbawanga Mjini CCM


122 Richard Ndasa- Sumve CCM


123 Almas Maige- Tabora Kaskazini CCM


124 Emmanuel Mwakasaka- Tabora Mjini CCM


125 Abdallah Mtolea- Temeke CUF


126 Ramo Makani- Tunduru Kaskazini CCM


127 Daimu Mpakate -Tunduru Kusini CCM


128 Saed Kubenea- Ubungo CHADEMA


129 Joseph Mkundi- Ukerewe CHADEMA


130 Waitara Mwita- Ukonga CHADEMA


131 Magreth Sitta- Urambo Mashariki CCM


132 James Mbatia -Vunjo NCCR-Mageuzi


133 Japhet Hasunga- Vwawa CCM


134 Gipson Ole Meseyeki- Arumeru Magharibi CHADEMA


135 Joshua Nassari -Arumeru Mashariki CHADEMA


136 Pauline Gekul -Babati Mjini CHADEMA


137 Jitu Vrajlal Son -Babati Vijijini CCM


138 Albert Obama- Buhingwe CCM


139 January Makamba- Bumbuli CCM


140 Boniphace Mwita -Bunda Vijijini CCM


141 Lolesia Bukwimba- Busanda CCM


142 Dr Merdad Kalemani -Chananja Chato CCM


143 Juma Nkamia -Chemba CCM


144 Ahmed Shabiby -Gairo CCM


145 Joseph Musukuma- Geita Vijijini CCM


146 Mary Nagu -Hanang CCM


147 Magdalena Sakaya- Kaliua CUF


148 Willy Qambalo- Karatu CHADEMA


149 Daniel Nsanzugwanko- Kasulu Mjini CCM


150 Holle Vuma- Kasulu Vijijini CCM


151 Hamoud Jumaa- Kibaha Vijijini CCM


152 George Simbachawene- Kibakwe CCM


153 Peter Serukamba- Kigoma Kaskazini CCM


154 Zitto Kabwe -Kigoma Mjini ACT


155 Bawasili Mbaraka- Kilosa Kati CCM


156 Suleiman Jaffo- Kisarawe CCM


157 Dk Ashatu Kijaji -KONDOA VIJINI CCM


158 Job Ndugai -Kongwa CCM


159 Hassan Seleman -Lindi Urban CCM


160 Kitwana Dau- Mafia CCM


161 Dk Haji Mponda -Malinyi CCM


162 Manase Njeza -Mbeya Vijijini CCM


163 Martin Msuha- Mbinga Rural CCM


164 Pascal Haonga- Mbozi CHADEMA


165 Flatey Gregory Massay -Mbulu Vijijini CCM


166 Mhandisi Kamwele- Mlele CCM


167 David Silinde-Momba CHADEMA


168 Mbena Joseph- Morogoro Kusini CCM


169 AbdulaAziz Abood- Morogoro Mjini CCM


170 Jaffar Michael -Moshi Mjini CHADEMA


171 Sebastian Kapufi -Mpanda Mjini CCM


172 Moshi Kakoso- Mpanda vijijini CCM


173 Maftaah Nachuma -Mtwara Mjini CUF


174 Suleiman Saddiq Murad -Mvomero CCM


175 Rashid Akbal -Newala Vijijini CCM


176 William Ole Nasha -Ngorongoro CCM


177 Edward Mwalongo -Njombe Urban CCM


178 Dr Khamis Kigwangalla- Nzega Vijijini CCM


179 Lameck Airo- Rorya CCM


180 Kassim Majaliwa- Ruangwa CCM


181 Marwa Ryoba- Serengeti CHADEMA


182 Dk Godwin Mollel -Siha CHADEMA


183 James Ole Millya -Simanjiro CHADEMA


184 Philipo Mulugo- Songwe CCM


185 Ahmad Katani -Tandahimba CUF


186 Mussa Mbarouk -Tanga Mjini CUF


187 John Heche- Tarime Vijijini CHADEMA


BUNGE LA KUMI NA MOJA (2015-2020)


1. Idadi ya Majimbo ni - 264.


Majimbo 258 tayari yameshapata Wabunge kama ifuatavyo:


CCM wabunge - 182


CUF - 39


CHADEMA - 35


ACT - 1


NCCR - 1


2. Baraza la Wawakilishi - 5


3. Uteuzi wa Raisi - 10


4. Mwanasheria Mkuu - 1


5. Spika wa Bunge kama hatakuwa Mbunge - 1
6. Viti Maalumu


(i) CCM - 63


(ii) CHADEMA - 43


(iii) CUF - 7


(iv) NCCR - 0


(v) ACT - 0
7. Majimbo yafuatayo hayajapata Wabunge kutokana na sababu mbalimbali na uchaguzi utarudiwa.


(a) Lushoto


(b) Ulanga Mashariki


(c) Ludewa


(d) Masasi


(e) Handeni Mjini


(f) Arusha Mjini


(g) Lulindi


(h) Kijitoupele


HIVYO BASI;
Jumla ya Wabunge wote wa Bunge la Kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watakuwa (396) kwa mgawanyo ufuatao;


1. CCM - 245


2. CHADEMA - 78


3. CUF - 46


4. ACT - 1


5. NCCR - 1


6. Uteuzi wa Rais - 10


7. Mwanasheria Mkuu - 1


8 . Wawakilishi - 5


9. Spika - 1


10. Majimbo yaliyosalia 8

Waraka wa mwanaCCM aliyewania Ubunge Mbeya Mjini, Shitambala

Kwanza napenda kutoa shukurani kwa Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia sote kumaliza kampeni na uchaguzi kwa usalama na amani bila kuibuka kwa vurugu za aina yoyote. Na hiii ilikuwa kauli mbiu yangu amani na usalama ndo msingi wa maendeleo ya nchi na jimbo letu.

Pili natoa shukurani kwa chama cha MapinduzI kwa kuniteua kupeperusha bendera ya chama changu katika uchaguzi mkuu kugombea ubunge jimbo la Mbeya mjini ambao ulihitimishwa Oktoba 25.

Pia nawashukuru wanahabari kwa msaada wao katika kuujuza umma wa Mbeya mambo yaliyokuwa yakijiri kwenye kampeni zetu tulizokuwa tukizifanya kwenye kata zote 36, nilifanikiwa kufanya jumla ya mikutano 56 na zaidi ndani na nje na niliweza kukutana na wananchi wengi maeneo mbalimbali niliyofanya kampeni na kusikiliza kero zao.

Nachukua fursa hii pia kuwashukuru wagombea wenzangu wote wa ndani ya chama wapatao 15 kwa kushirikiana nami katika Kampeni hizo. Shukrani za pekee zimwendee Charles Mwakipesile aliyekuwa Meneja wangu.

Pamoja na mimi kuteuliwa na chama bado wagombea wenzangu katika chama walijitahidi kuniunga mkono na kunisapoti kwa hali na mali wapo walioacha shughuli zao na kuzunguka nami kwenye kampeni zote jitihada zao zimeonekana, nawashukuru sana.

Navishukuru kipekee vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi kubwa, ngumu na nzuri waliyoifanya na kulifanya jiji letu la Mbeya kuwa salama hadi leo. Nawashukuru sana.

Nilijitahidi kufanya kampeni za kistaarabu, kwa kutumia uwezo wangu wote pamoja na matukio mbalimbali ya kejeli yaliyokuwa yakitolewa na wapinzani wetu, nilichukulia kama ndio siasa kwani kila mmoja alikuwa anatafuta kiti cha Ubunge wa Jiji la Mbeya kwa namna yake lengo letu lilikuwa moja kusukuma maendeleo ya Jiji letu.

Mwenzangu wa chadema ameibuka na kura nyingi zaidi ya wengine tuliogombea naye na kutangazwa kuwa mbunge mteule wa jiji la Mbeya. Haya ni maamuzi ya wana Mbeya wengi zaidi ya wale waliotaka niwe mbunge wao. Nampongeza Sugu kwa ushindi huo na pia ninamtakia kila laheri katika muda wake wa uongozI. Pamoja na dosari zilizojitokeza kwenye uchaguzi huu lakini nimekubaliana na matokeo, tuweke mambo ya itikadi pembeni tusimame pamoja tuijenge Mbeya yetu.

Kwa bahati mbaya sana nimeshindwa katika uchaguzi huu nikiwa nimekusanya takribani kura 50,000 inawezekana wakati bado haujafika wa mimi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya, nimefarijika kwa wale walionipa kura na hata wale ambao hawakunichagua, Nawashukuru wananchi wote.

Najua walionichagua walinielewa, walinikubali,walihitaji niwawakilishe. Nasema nitawawakilisha na sitowatupa. Yale niliyoyasema yatatimia juu yao kwa namna moja ama nyingine kadri Mungu atakavyojalia. Sitawaacha wala kuwaangusha. Nawaomba wasijione wameshindwa na wasikate tamaa. Nipo nao pamoja. Ahadi nilizotoa wakati wa kampeni nitazitekeleza kwa kadri ambavyo Mungu atanijaalia.

Nipo na wanajamii hapa hapa Mbeya, shughuli zangu na biashara zangu zipo hapa Mbeya nitaendelea kuwa na wana Mbeya kwa hali na mali tukiendelea kulijenga Jiji letu la Mbeya.
Naahidi nitaendelea kushirikiana na wananchi wa jimbo la Mbeya kwa hali na mali nikifuatilia na kutekeleza ahadi zilizoahidiwa na Rais mteule Dkt.John Pombe Magufuli, pamoja na kwamba sikuchaguliwa kuwa Mbunge wa jimbo la Mbeya.Kwa niaba ya walionipigia kura nitafanya kazi.

Ndugu wanahabari nilijiwekea vipaumbele wakati wa kampeni zangu pamoja na ahadi kwa wananchi wa jimbo la Mbeya katika baadhi ya maeneo niliahidi mambo mbalimbali kama vile ujenzi wa zahanati kata ya Iyunga, Igawilo, Ilemi na Nsoho. Shule kata ya Iziwa, na zinginezo, usafiri wa daladala pembezoni, maji na umeme. Pia kutafuta waalimu wazuri kwa ajili ya shule zetu. Bila kusahau pembejeo kwa wakati. Nitashirikiana na wananchi katika kutekeleza ahadi zangu.
Pia zipo ahadi nilizoahidiwa na Rais wangu mteule ambaye ni muadilifu na mchapakazi nitamkumbusha ikiwemo km 10 za barabara Jiji la Mbeya na mengineyo ambayo nimeahidi kuyatekeleza mwenyewe kwa wapiga kura wakati wa kampeni. 

Ndugu zangu wanahabari, naamini mlikuwa mkitafakari kukaa kwangu kimya baada ya kumalizika kwa uchaguzi huu wengi walitegemea ningeweza kupinga matokeo, kufanya hivyo kungesababisha kuchelewesha mahitaji ya wakazi wa jiji la Mbeya ambao wanahitaji huduma yangu na ahadi nilizotoa kwa wengi waliojitokeza kuniunga mkono, nawaahidi sitawaangusha.

Mwisho lakini si kwa umuhimu napenda kuwasisitiza wakazi wa Jiji la Mbeya kuendelea kushikamana kwa ajili ya kuliendeleza jiji letu, tuepuke vishawishi na kujiingiza katika mambo ya uvunjifu wa amani na utulivu.

Amani ya Mbeya ikitoweka hakuna biashara inayoweza kufanywa wala hakuna shughuli zozote za maendeleo ambazo zinaweza kufanywa,vijana wajikite kwenye ujasiriamali watafute riziki yao halali kwa kuwa Mbeya yenye amani na salama kwa Maendeleo yetu linawezekana.

Ahsanteni
Capt. Sambwee Shitambala (MNEC-CCM, Mbeya)

Mapumziko ya kesho hayawahusu Kidato cha Nne

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Dk. Charles Msonde amesema pamoja na kesho kutangazwa kuwa ni siku ya mapumziko, Mitihani ya Kitaifa ya kuhitibu Kidato cha Nne itaendelea kama ratiba inavyoelekeza, hivyo wanafunzi wasikose kuhudhuria mashuleni.

Kauli ya Katibu Mtendaji wa NECTA inafafanua taarifa baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuitangaza kesho, Alhamisi, Novemba 5, mwaka huu, 2015, kuwa sikukuu na siku ya mapumziko.

Rais Kikwete amefanya uamuzi huo, ili kuwawezesha Watanzania kushiriki katika sherehe za kuhitimisha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne na kuingizwa madarakani Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wito wa UKAWA kwa umma: Msihudhurie kuapishwa Magufuli

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Freeman Mbowe amesema kuwa hawatashiriki shughuli ya kuapishwa kwa Dk. John Pombe Magufuli inayotarajiwa kufanyika Alhamis, Novemba 5, 2015.

Kauli hiyo ya Mwenyekiti Mbowe aliyoitoa leo, imekuja wakati kukiwa bado kuna sintofahamu kubwa miongoni mwa Watanzania kuhusu mchakato wa uchaguzi hususan upigaji kura, ukusanyaji na ujumlishaji wa matokeo ulivyofanyika hasa katika nafasi ya urais.

"Hatutahudhuria shughuli hiyo ya kumwapisha Magufuli. Tumekubaliana wote kwenye UKAWA, ndani ya CHADEMA, viongozi wetu, wabunge wetu wote hawatahudhuria uapishwaji wala sherehe.

"Tumetoa wito kwa wananchi wote, Watanzania wote, wapenda mabadiliko na wapenda haki wote kwa ujumla kutohudhuria shughuli hiyo," amesema Mwenyekiti Mbowe.

Mwenyekiti Mbowe amesisitiza kuwa UKAWA, wapenda mabadiliko wote na Watanzania wapenda haki hawakubaliani na wanapinga mchakato wa uchaguzi hususan matokeo ya urais ambayo, kwa mujibu wa Katiba ya Nchi aliyosema ni mbovu, yakishatangazwa hakuna haki ya kuyapinga katika mahakama yoyote ile.

"Tunataka nchi na dunia nzima ijue wazi kuwa hatukubaliani na mchakato wa uchaguzi hasa matokeo ya urais ambayo kwa mujibu wa Katiba yetu mbovu, Mwenyekiti wa Tume akishatangaza hakuna mahali pa kuyapinga."

"Matokeo ya ubunge au udiwani yanaweza kupingwa mahakamani, lakini kwa matokeo ya urais Katiba yetu mbovu inawafunga mikono na miguu Watanzania wote ambao wangependa waone haki imetendeka katika nafasi hiyo," amesema Mwenyekiti Mbowe.

"Watawala wamechezea haki ya Watanzania kupiga kura. Kura zimehesabiwa kama karatasi za kawaida tu. Hujuma dhidi ya matokeo ya wagombea wetu imehujumiwa waziwazi. Safari hii hujuma hazikuwa kificho tena. Kila mtu amejionea matokeo yaliyokuwa na Jaji Lubuva si yale ambaye yalikuwa yamebandikwa vituoni. Hayakuwa na uhalisia na matokeo yaliyokusanywa na mawakala. Uchaguzi umefanywa kama ni jambo lisilokuwa na maana yoyote. Hiyo ni hatari sana kwa taifa lolote linalotaka kukuza demokrasia kama mojawapo ya nguzo za maendeleo. Hatuwezi kukubali kufika huko," amesema Mbowe.

Aidha, Mwenyekiti Mbowe ameongeza kusema kuwa vyama vinavyounda UKAWA vimeitisha kikao cha Wabunge wateule wote wa vyama hivyo ambao watakutana Alhamis, saa 4 asubuhi, jijini Dar es Salaam.

Imetolewa leo Jumatano Novemba 3, 2015 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano

Taarifa kuhusu viongozi wa ng'ambo watakaoshuhudia Magufuli akiapishwa

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: [email protected]
Barua pepe: [email protected]
Tovuti : www.foreign.go.tz
Nukushi: 255-22-2116600

20 KIVUKONI FRONT,
P.O. BOX 9000,
11466 DAR ES SALAAM,
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Taarifa kuhusu Viongozi kutoka nje ya nchi watakaohudhuria Sherehe za Kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano


Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli ataapishwa rasmi kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 05 Novemba, 2015.

Sherehe hizo ambazo zitafanyika katika Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es Salaam zitahudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa na Kikanda na Wawakilishi mbalimbali kutoka nje ya nchi.

Miongoni mwa Marais watakaohudhuria sherehe hizo ni pamoja na Mhe. Robert Mugabe, Rais wa Zimbabwe, Mhe.Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Uganda, Mhe. Paul Kagame, Rais wa Rwanda, Mhe. Jacob Zuma, Rais wa Afrika Kusini.

Wengine ni Mhe. Joseph Kabila, Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mhe.Uhuru Kenyatta, Rais wa Kenya, Mhe. Filipe Nyusi, Rais wa Msumbiji na Mhe. Edgar Lungu, Rais wa Zambia.

Malawi itawakilishwa na Makamu wa Rais, Mhe. Saulos Chilima huku Namibia ikiwakilishwa na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah. Aidha, Serikali ya China itawakilishwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Tawala.

Vilevile nchi nyingine ambazo zimethibitisha kushiriki na zitawakilishwa na kati ya Makamu wa Rais,Waziri Mkuu, Spika au Balozi ni pamoja na Burundi, Comoro, Angola, Botswana, Lesotho, Madagascar na Mauritius.

Nyingine ni Norway, Oman, Sudan Kusini, Sweden, Umoja wa Falme za Kiarabu, Marekani, Uingereza, Shelisheli, Swaziland, Algeria, Misri, Benin, Denmark, Ethiopia, Finland, Ufaransa, Ghana, India, Japan, Kuwait, Uholanzi na Nigeria.

Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa na Kikanda waliothibitisha kushiriki au kutuma wawakilishi wao ni pamoja na Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC); Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Ulaya (EU), Jumuiya ya Ukanda wa Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR).

-Mwisho-
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam

03 Oktoba, 2015

Salam za pongezi kwa Magufuli kutoka kwa Rais Kikwete, Kagame, Abdelaziz

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Salamu za pongezi kwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli zimeanza kumiminika nchini, za kwanza zikiwa zimetumwa na Rais wa Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu ya Saharawi Mheshimiwa Mohammed Abdelaziz.

Katika salamu zake kwa Rais Mteule Magufuli, Rais wa Rwanda Mheshimiwa Kagame amesema: “Kufuatia kuchaguliwa kwako kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, napenda kukutumia Mheshimiwa salamu za dhati, pongezi na heri nyingi kwa niaba yangu mwenyewe, Serikali yangu na wananchi wa Rwanda.”

“Napenda pia kutumia nafasi hii kukuhakikishia msimamo wetu wa kudumisha na kuimarisha uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati ya mataifa yetu mawili na watu wake.”

Naye Rais Abdelaziz amemwambia Rais Mteule Magufuli: “Kwa niaba ya wananchi wa Saharawi na Serikali ya Kidemokrasia ya Kiarabu ya Saharawi, napenda kukupongeza sana kwa kuchaguliwa kwako kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nakutakia mafanikio makubwa katika kutekeleza majukumu ya nafasi yako hiyo.”

Ameongeza: “Sisi tuna uhakika kuwa chini ya uongozi wako wa busara, Tanzania itaendelea kusonga mbele na kupata maendeleo na ustawi mkubwa zaidi.”

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
4 Novemba, 2015.

Serikali yazungumzia taarifa inayosambaa kuhusu Rais Mstaafu MkapaMkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene amekanusha taarifa za uzushi zinazosambazwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii kuhusu kifo cha Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa.

Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Bw. Mwambene amesema kuwa Mhe. Rais Mkapa ni mzima na mwenye afya nzuri anaendelea na shughuli zake kila siku kama kawaida.
“Mhe. Rais Benjamin William Mkapa ni mzima hajafariki, wala haumwi na si jambo jema kumzushia tukio hilo kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria na nawasihi msiendelee kusambaza ujumbe huo” 
Aidha, katika mkutano huo Mwambene aliwashukuru wahariri, waandishi wa vyombo vyote vya habari na mitandao ya kijamii kwa ujumla kwa kuonyesha moyo wa uzalendo katika kipindi chote ambacho Taifa limekuwa katika mchakato wa uchaguzi na mpaka sasa ambapo serikali inaendelea na maandalizi ya sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Awamu ya Tano, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Mwambene amesema mpaka sasa maandalizi ya sherehe hizo yanaendelea vizuri, zaidi ya Marais 15 kutoka nchi mbalimbali wamealikwa baadhi wameshawasili nchini na wengine wanaendelea kuwasili.

Sherehe za kuapishwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya Tano zitafanyika kesho tarehe Novemba, 5 mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru.
 • Taarifa ya Georgina Misama-MAELEZO

Taarifa: Kesho ni siku ya mapumziko Tanzania

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameamua na ameitangaza kesho, Alhamisi, Novemba 5, mwaka huu, 2015, kuwa Sikukuu na siku ya mapumziko.

Rais Kikwete amefanya uamuzi huo, ili kuwawezesha Watanzania kushiriki katika sherehe za kuhitimisha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne na kuingizwa madarakani Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam leo Jumatano, Novemba 4, 2015 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Yohana Sefue, Rais Kikwete ametoa uamuzi huo kwa mujibu wa mamlaka aliyo nayo chini ya Kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
4 Novemba, 2015

Rais Kikwete siku ya mwisho ofisini


Akiondoka...

Rais Kikwete, Maalim Seif wazungumza


Rais Jakaya Kikwete ateta na makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad kuhusu hali ya kisiasa Visiwani leo asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Wakiwa na furaha..........baada ya mazungumzo yao leo Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais Jakaya Kikwete leo asubuhi mefanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Shariff Seif Hamad kuhusu hali ya kisiasa Visiwani humo, walipokutana Ikulu jijini Dar es Salaam.


Kipindi cha Jukwaa Langu - Novemba 2, 2015

Kipindi hiki hukujia kila Jumatatu, kujadili mambo mbalimbali yaihusuyo Tanzania.
Wiki hii, tumeangalia zaidi kuhusu mustakabali wa Tanzania baada ya Uchaguzi Mkuu 2015.