Picha za halfa mchapalo kusherehekea kuapishwa Rais Magufuli


Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwasili kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Alhamisi usiku kwa ajili ya mchapalo maalum ulioandaliwa na Rais wa awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli kusherehekea kupishwa kwake

ha ha haa! Katuni za baada ya Uchaguzi Mkuu...Picha za dhifa ya kitaifa ya kumkaribisha Rais Magufuli makazini Ikulu


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na wanausalama alipowasili Ikulu mara baada ya Kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais Kikwete aaga kwa kuwapunguzia wafungwa adhabu


Wakati wa kuaga na kukabidhi madaraka ya serikali kwa rais mpya wa serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, rais wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete amewapunguzia wafungwa wote moja ya sita (1/6) ya vifungo vyao.

Hii ni zaidi ya punguzo la kawaida linalotolewa chini ya kifungu 49 (1) cha sheria ya Magereza sura ya 58 ispokuwa wafungwa walioorodheshwa katika ibara ya pili (i-xix).

Msamaha huo ni kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya ibara ya 45 (1) (d) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ilifahamika Magufuli ni Rais pale Kahama: Alibadilishiwa gari na ‘kukalishwa’ kiti cha nyuma

HADI saa nne za asubuhi ya Oktoba 26 mwaka huu, mgombea wa ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, alikuwa anatumia “mifumo na muundo wa kiprotokali” ya chama hicho tawala.

Lakini mfumo huo wa kiprotokali ulibadilika ghafla wakati msafara wake ulipowasili mjini Kahama, mkoani Shinyanga, ukitokea wilayani Chato ambako mgombea huyo alikwenda kupiga kura yake Oktoba 25, Jumapili iliyopita.

Kwa kawaida wakati wa kampeni Dk. Magufuli alitumia gari la CCM na wakati wote alikaa kiti cha mbele na kuhudumiwa kiulinzi na maofisa wa CCM wakisadiwa pia na maofisa protokali wa chama hicho.

Dk. Magufuli na timu yake ya kampeni waliamua kutumia usafiri wa barabara kurudi jijini Dar es Salaam akitokea Chato badala ya usafiri wa ndege uliozoeleka kwa viongozi wengi wa Tanzania.
Msafara huo uliwasili Kahama majira ya nne asubuhi na kusimama katika hoteli moja iliyoko pembezoni mwa barabara kuu ya Kahama-Shinyanga, kwa lengo la ‘kuchimba’ dawa.

Baada ya mapumziko hayo mafupi yaliyochukua dakika 10 hivi Raia Mwema lilishuhudia maofisa wa CCM na wale wa Idara ya Usalama wakijadiliana na kabla msafara kuendelea, Dk. Magufuli alibadilishiwa gari na ‘kukalishwa’ kiti cha nyuma, hali iliyoashiria kuwa kuna mabadiliko katika mfumo wa kiprotokali.

Aidha mfumo wa kuendesha magari ulibadilika, kwa tahadhari huku gari la mgombea huyo likiwekwa kati na kuhakikisha kuwa hakuna gari au kitu chochote kitakachohatarisha usalama wake na ule wa msafara mzima.

Wakati viongozi wa mikoa husika ambako msafara ulipita kuanzia Geita, Shinyanga, Tabora na Singida, walitokeza kumpokea wakiongozwa na makamanda wa polisi wa mikoa hiyo.

Moja wa maofisa wa juu wa CCM aliliambia Raia Mwema kuwa wamefikia uamuzi wa kubadilisha mfumo huo na kumkabidhi Dk. Magufuli kwa timu maalumu ya maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa, baada ya kupokea maelekezo kutoka ngazi juu.

“Tumepokea maelekezo kutoka juu tubadilishe utaratibu na sisi ni wajibu kutekeleza amri,” alieleza ofisa huyo bila ya kufafanua zaidi.

“Kuna kila dalili kuwa kwa taarifa za matokeo ya awali, ushindi kwa CCM unanukia na tumeongoza katika baadhi ya mikoa na majimbo hivyo jukumu la ulinzi sasa tunaliacha kwa timu maalumu ya watu wa Idara,” alieleza ofisa mwingine.

Msafara wa Dk. Magufuli ulipumzika juzi, Jumatatu, mjini Dodoma na uliendelea na safari ya kurudi Dar es Salaam kwa njia hiyo hiyo ya barabara, kusubiri matokeo ya mwisho ya uchaguzi huo wa kihistoria nchini.

Samuel Sitta aeleza uamuzi wa kuwania Uspika wa Bunge la JMT 2015


[video] "Mada Moto" - Wanasheria wachambua Katiba ya Zanzibar na Uchaguzi


Mtendeni, Zanzibar: Maalim Seif azungumzia msimamo wa CUF


Presentation about greenhouse - Mhadhara wa kilimo cha shamba-kitalu


Beach Party ya kujipongeza kwa wote waliofanikisha ushindi wa "Tingatinga"


[update] Rais John Pombe Magufuli ateua Mwanasheria Mkuu wa Serikali

UPDATE: Picha za uapisho...


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimina na Makamu wake, Mama Samia Suluhu Hassan, wakati aliwapowasili kwenye Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam, leo asubuhi Okt. 6, 2015 kwa ajili ya kumwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, aliyemteua jana Novemba 5, 2015 mara tu baada ya kuapishwa rasmi. Kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande. Picha na OMR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli (wa tatu kushoto) akiwa na Makamu wake, Mama Samia Suluhu Hassan (wa pili kushoto) Spika wa Bunge Mstaafu, Anne Makinda (kushoto) Jaji Mkuu wa Serikali, Othman Chande (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, baada ya kuapishwa leo wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akimwapisha George Masaju, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali,wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan,(kushoto) akizungumza jambo na Jaji Mkuu wa Serikali, Othman Chande (katikati) wakati wa hafla fupi ya kumwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya ndigu jamaa na marafiki na watumishi wa Serikali waliohudhuria hafla hiyo ya kuapishwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.George Mcheche Masaju
George Mcheche Masaju
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk John Pombe Magufuli amemteua Bwana George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amesema Rais Magufuli ameyafanya uteuzi huo katika siku yake ya kwanza ya kuingia ofisini Ikulu jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo.

Itakumbukwa kuwa, Ijumaa, Januari 2, 2015 huu Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alimteua Masaju kushika wadhifa huo kwa mara ya kwanza baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwanasheria wa Serikali, George Werema.

Mwanasheria Mkuu huyo ataapishwa kesho Ijumaa Novemba 6, 2015, Ikulu, Dar es Salaam.

Masaju alipata kuwa mshauri wa Sheria wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na baade kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Katia hatua Nyingine, Rais Dk John Pombe Magugufuli ameitisha Bunge la 11 ambapo wabunge watakutana mjini Dodoma Novemba 17 na Novemba 19 atapeleka jina la Waziri Mkuu ambaye atamteua kwa ajili ya kuidhinishwa na Bunge hilo.
  • via Father Kidevu blog

Jeff aachia "Mama Afrika" unaotangaza utalii Tanzania

Jeff Maximum
Jeff Maximum
Mwanamuziki aliyewahi ishi nchini Tanzania na pia mwenye asili ya Congo ambaye anafanya kazi zake nchini Marekani na Dubai, Jeff Maximum tayari ameshaachia video ya wimbo wake mpya uitwao “Mama Afrika” ambao umetayarishwa Bagamoyo Nchini Tanzania hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Jeff anaweka wazi kuwa, kuwa video hiyo iliyoachiwa Novemba 2 mwaka huu, tayari imeshaanza kuonekana katika vituo mbalimbali vya televisheni Bara la Afrika ikiwemo nchini, pia katika nchi za Nigeria, Afrika Kusini, Kongo, Ghana, Kenya na kwingineko.

Pia video hiyo inaonekana katika vituo vya televisheni vya nchini Uingereza, Dubai, Amerika na kwingineko huku ikitangaza utalii wa Tanzania kwa asilimia kubwa.

Jeff anaweka wazi kuwa, aliamua kuitayarishia video hiyo nchini Tanzania kwa kuwa ni kati ya nchi nyingi anazozipenda zaidi Barani Afrika.

Na kuongeza kuwa, video hiyo imetengenezwa na mwongozaji anayechipukia kutoka Tanzania Hanscana (Wanene Films), huku audio yake ikiwa imetayarishwa katika studio yake iliyopo nchini Dubai (One Vision Records).

Tazama video hiyo hapa.