Taarifa ya NEC ya mchanganuo wa kiumri wa wabunge waliogombea na kushinda katika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2015. Mbunge kijana zaidi ana miaka 21 na mbunge mzee kuliko zaidi ana miaka 72.

Wabunge wenye umri wa miaka kati ya
  • 21 na 35 wako 47
  • 36 hadi 50 wako112
  • 51 na zaidi wako 92

Taarifa ya Polisi Mbeya: Wachina wakamatwa na pembe 11 za faruTAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAREHE 07.11.2015.


JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA RAIA WANNE WA NCHINI CHINA WAKIWA NA PEMBE 11 ZINAZODHANIWA ZA FARU.

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE RAIA WA CHINA WAKIWA NA PEMBE 11 ZINAZODHANIWA ZA FARU. RAIA HAO WALIFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. XIAO SHAODAN (29) AKIWA NA PASSPORT NAMBA G.29624553 ILIYOTOLEWA NCHINI CHINA 2. CHEN JIANLIN (33) AKIWA NA PASSPORT NAMBA E.09800855 ILIYOTOLEWA NCHINI CHINA 3. SONG LEI (30) AKIWA NA PASSPORT NAMBA G.52064944 ILIYOTOLEWA NCHINI CHINA NA 4. HU LIANG (30) WOTE WAKAZI WA BLANTYRE NCHINI MALAWI.

WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 06.11.2015 MAJIRA YA SAA 08:30 ASUBUHI HUKO MPAKANI KASUMULU KATIKA WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA BAADA YA ASKARI POLISI NA WADAU WENGINE WA USALAMA WALIOKUWEPO MPAKANI HAPO KULITILIA MASHAKA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.103 DER AINA YA TOYOTA HILUX RANGI YA DHAHABU LILILOKUWA LIKITOKEA NCHI MALAWI KUINGIA TANZANIA LIKIWA NA RAIA HAO.


KUTOKANA NA MASHAKA HAYO, MAAFISA HAO WALIFANYA UPEKUZI NDANI YA GARI HILO NA CHINI YA CHASES YA GARI HILO NA NDIPO WALIGUNDUA KUWA GARI HILO LILIKUWA LIMEJENGEWA BOKSI NA BAADA YA KUFUNGUA BOKSI HILO LA BATI KULIPATIKANA PEMBE 11 ZA MNYAMA PORI FARU.

AIDHA ASKARI POLISI WALIENDELEA NA UPEKUZI KATIKA GARI HILO NA KUKUTA MALI MBALIMBALI ZIKIWEMO:- SIMU MOJA AINA YA SAMSUNG, IPAD MOJA, PESA YA MALAWI KWACHA 1,600/=, TSHS.234,000/=, USD DOLLAR 1,700/=, NOTI 22 @ TSHS 100 = 2,200, NOTI 51 @ TSHS 51 = 2,550, USD 33 @ TSHS. 50 = 1,650, USD NOTI 9 @ TSHS 100 = USD 900, MALAWI KWACHA 18,760 NA CERTIFICATE OF HEALTH EXAMINATION MOJA, SIMU MBILI ZA KICHINA AMBAZO MAJINA YAKE NA AINA HAIKUFAHAMIKA MAPEMA NA SIMU MOJA AINA YA HUAWEI, SIMU MOJA AINA YA SAMSUNG, IPHONE APPLE TANO, SIMU MOJA TARDROVER, NOKIA MOJA NA SMT MOJA.

UPELELEZI KUHUSIANA NA TUKIO HILI UNAENDELEA NA PINDI UTAKAPOKAMILIKA WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA PEMBE ZA FARU/PEMBE ZA NDOVU KWANI NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU AU MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA PEMBE ZA FARU/NDOVU KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.

Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Rekodi pekee za uongozi wa kisiasa wa Agustine Lyatonga Mrema

Ujumbe huu uliotumwa na mdau wa wavuti.com, unasema kuwa hadi Oktoba 2015...

(1) AGUSTINE LYATONGA MREMA ndiye mbunge pekee aliyewahi kuwa mbunge katika majimbo matatu tofauti hapa Tanzania?
1. MOSHI VIJIJINI 2. TEMEKE 3. VUNJO.

(2) AGUSTINE LYATONGA MREMA ndiye Mtanzania pekee aliyewahi kuwa mbunge kupitia vyama vitatu tofauti?
1. 1980 - 1995 MOSHI VIJIJINI (CCM), 2. 1996 - 1998 TEMEKE (NCCR- MAGEUZI), 3. 2010 - 2015 VUNJO (TLP).

(3) AGUSTINE LYATONGA MREMA amewahi kuwa mwanachama wa vyama vitatu vya siasa nchini 1. CCM (1977 - 1995), 2. NCCR - MAGEUZI (1995 - 2000), 3. TLP (2000 - 2015).

(4) Majimbo yote ambayo AGUSTINE LYATONGA MREMA amewahi kuwa mbunge yameongozwa na vyama vitatu tofauti tu,
1. MOSHI VIJIJINI (CCM, NCCR - MAGEUZI na CHADEMA), 2. TEMEKE (CCM, NCCR - MAGEUZI, na CUF), 3. VUNJO (NCCR - MAGEUZI, TLP na CCM).

5. AGUSTINE LYATONGA MREMA amegombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA mara TATU (3). 1995, 2000 na 2005.

(6) AGUSTINE LYATONGA MREMA ndiye Mtanzania pekee aliyewahi kuwa naibu waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, cheo ambacho hakitambuliki kikatiba wala kisheria Tanzania wakati akiwa waziri wa mambo ya ndani.

(7) AGUSTINE LYATONGA MREMA ndiye mwanzilishi wa polisi jamii (SUNGU SUNGU) Tanzania.

8) AUGUSTINE LYATONGA MREMA, Ndiye mwanasiasa pekee alieweza mnadi Raisi wa chama tofauti na chama chake huku chama chake kikiwa kina mgombea wa nafasi ya Uraisi (Alimnadi Kikwete 2010 na Pia alimnadi Magufuli 2015.

Je, kipi ambacho bado hajafanya?

Watu 4 wa familia moja kizimbani Kisutu kwa taarifa walizosambaza kupitia WhatsApp

Habari ya kipekee: T.B. Joshua na Lowassa wakipata chakula Kilimanjaro Hotel

Msomaji wa wavuti.com ametutumia ujumbe ufuatao....


TB Joshua Pamoja na Lowassa


Jana, nikaona Mchungaji T.B. Joshua katika Hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es Salaam baada ya mlo na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania  na mgombea Urais wa Tanzania kupitia upinzani, Edward Lowassa.

Nje ya mambo mengi waliyojadili, kimya kimya nikasikiliza alisikika T.B. Joshua akisema kitu kama hiki kwa Lowassa: 

"Mara nyingi, Mungu anazungumzia baraka na mafanikio kupitia maumivu na tamaa. Waziri wa zamani Mkuu, kile kilichotokea ni kwa kujiandaa kwa ajili ya siku zijazo. Tunajifunza kutii kwa njia tunayokabiliana nayo. Ninamaanisha, hata kwa kuteseka."

Hapa ni picha ya kipekee na kipande cha video nimechukua:TB Joshua with Lowassa


Last night, I spotted Pastor T.B. Joshua at The Kilimanjaro Hotel in Dar es Salaam having a meal with Tanzania’s Former Prime Minister and opposition leader Edward Lowassa.

Out of the many things they discussed, I faintly overheard T.B. Joshua saying something like this to Mr Lowassa:

"Many times, God speaks blessing and breakthrough through pain and disappointment. My dear Former Prime Minister, what happened is to prepare you for the future. We learn obedience by the things we face. I mean, by what we suffer."

------- END ------


Erick J Mazyala commented the following via Facebook
May God Almighty continue to bless man of God for making yourself available for the nobel calling! How can you man of God manage to maintain humbleness with the level of Holy anointing that you have!? Those call themself men of God in Tanzania have something to learn if they pay attention in the name of Jesus! Mr hon. Edward Lowasa, regardless of the outcome of the election, u've archieved greatly, spending time with his great man of God is more than enough one may long for! God is fixing you, us Tanzanian and our land right now in Jesus Christ ' s name!


Barua "kali" ya Shigongo kwa CCM na Watanzania woteNdugu zangu. Watanzania wenzangu,

Kwanza kabisa nawapongezeni kwa amani na utulivu mliouonyesha katika mchakato wote wa Uchaguzi Mkuu ambao ulimalizika salama na hatimaye jana Rais wa Awamu wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli aliapishwa mbele ya macho yangu na ya Watanzania wengine wengi.

Hakika tumeuthibitishia ulimwengu kwamba, sisi Watanzania ni tofauti na wao, tunao uwezo wa kuvuka kwenye nyakati ngumu lakini bado tukabaki wamoja tukiishi pamoja kwa upendo kama ndugu, msingi uliojengwa na wazee wetu wa mwanzo ambao kuubomoa si kazi rahisi, kwa hili nawapongeza Watanzania wote na ninamwomba Mungu awasaidie wenzetu wa Zanzibar waweze kufikia muafaka utakaoleta utulivu wa taifa zima.

Baada ya kusema hayo niendeleze barua yangu niliyoianza wiki iliyopita kwa Chama Cha Mapinduzi na Watanzania wote, hilo ndilo dhumuni la barua hii, kuendeleza pale nilipokomea! Leo nataka kuongea baadhi ya mambo niliyoyaona kama udhaifu mkubwa kwa Chama Cha Mapinduzi kwenye mchakato mzima uliohitimishwa Oktoba 25, 2015 kwa wananchi kupiga kura. Naomba nianze na suala zima la moyo wa kujitolea katika chama, ndugu zangu hili ni jambo la kusikitisha mno katika Chama Cha Mapinduzi, nina imani wengi wamelishuhudia! Moyo wa kujitolea ndani ya Chama Cha Mapinduzi umekufa kabisa, kama haujafa basi upo chumba cha huduma kwa wagonjwa mahututi (ICU), kila kitu ndani ya chama hiki kikubwa kimekuwa POSHO, POSHO, POSHO! Bila posho ndani ya Chama Cha Mapinduzi hakuna kinachofanyika, moyo wa kujitolea ambao waasisi wa chama hiki waliupandikiza wakati wa kutafuta uhuru umekufa.

Wakati katika muungano wa vyama vya upinzani, vijana walikuwa wamehamasika, wakifanya kazi kwa kujitolea, lengo lao likiwa ni moja tu; kuing’oa CCM madarakani, mimi nilishuhudia wanaCCM, wengine viongozi kabisa wamekaa chini bila kufanya chochote wakisema “Tufanye nini sasa hakuna posho?”

Kwangu mimi hii ilikuwa ni aibu, mwanaCCM anashindwa kuondoka nyumbani kwake na kwenda kuhamasisha nyumba kwa nyumba akishawishi wapiga kura eti hawajaletewa fedha kutoka wilayani au makao makuu, bila posho ndani ya CCM hakuna kinachofanyika, jambo hili inabidi lishughulikiwe, moyo wa kujitolea na uzalendo kwa chama ni lazima ufufuliwe, hii ni kazi ya Mwenyekiti wa CCM. Inawezakanaje vijana wa 4U Movement (marafiki wa Lowassa) waliojiunga nchi nzima eti wafanye kazi kubwa za kututisha kuliko jumuia za Chama Cha Mapinduzi kama ya wazazi, UWT na vijana ambazo zina mitandao mpaka vijijini kabisa? 4U Movement wanawezaje kufanya kazi kubwa ya kutetemesha kama jumuiya zetu hizi zina moyo wa kujitolea? Jibu ni moja tu hapa, moyo huo umekufa sababu ya posho, vijana wetu hawafanyi chochote mpaka wapewe posho na chama au mgombea.

Simaanishi kwamba watu wote katika jumuiya hizi hawakufanya kazi, lakini hata wewe msomaji kama ni mwanachama wa CCM, unaelewa kabisa ninachokizungumzia hapa ni nini na iko sababu kubwa sana ya kufufua moyo wa uzalendo na kujitolea ndani ya chama hiki badala ya kuacha jambo hilo lifanywe na vyama vya upinzani. Jambo jingine ni UNAFIKI na HUJUMA ndani ya chama, hakika tabia hizi mbili zimekiathiri sana Chama Cha Mapinduzi kwenye uchaguzi huu. Nasema bila kupindisha, zimepunguza mno kura za chama hiki. Kuna unafiki mno ndani ya CCM, watu sio wa kweli, wanavaa shati la kijani mchana lakini wanavaa ngwanda la khaki usiku! Hii ni aibu, wengine ni viongozi wa chama ngazi za wilaya, walishindwa hata kumuombea kura mgombea urais wa chama chao kwa sababu walishajiunganisha na kambi ya pili.

Hawa ndiyo walioendesha hujuma kukikwamisha chama kisipate ushindi lakini ashinde mtu waliyemtaka hata kama ni wa chama pinzani, tukubali tukatae, jambo hili lipo na ni lazima lishughulikiwe haraka iwezekanavyo kwa usalama na ustawi wa chama, kuendelea kuwafumbia macho watu wa aina hii itakigharimu chama kwenye uchaguzi utakaofuata. Inawezekanaje kiongozi wa chama akapelekewa kofia na tisheti za Chama Cha Mapinduzi halafu akaacha kuzigawa wakati anazo stoo? Inawezekanaje akapewa posho za mabalozi halafu akaamua kutowagawia au kukata nusu ya kiwango alichopewa? Wakati akifayafanya haya anajua kabisa kwamba kambi ya pili ya upinzani inagawa tisheti na kofia zake na kubandika bendera kila mahali jimboni. Je, hii si hujuma?

Ndugu zangu,

Niongelee mikakati, tumejitahidi sana kupambana kwenye uchaguzi huu, naomba niwasifu watu waliokuwa kwenye kitengo cha teknohama (IT) wamefanya kazi kubwa mno kupambana na vijana wa 4U Movement, kampeni za safari hii ziliendeshwa kisasa na zilikuwa na nguvu kubwa sana kwenye mitandao ya kijamii, kazi kubwa imefanywa na vijana wetu. Lakini jambo lililonisikitisha ni kwa nini tulikuwa mara nyingi tunakuwa wafuasi, badala ya kuwa viongozi kwenye mikakati? Mfano Ukawa wakibandika bendera zao nyingi mitaani ndiyo na sisi tunafuata nyuma yao, kwa nini hatukuwa watu wa kwanza na Ukawa wakafuata nyuma? Naamini sana kwenye msemo wa Steve Jobs usemao “Be a leader, not a follower!” daima uwe kiongozi siyo mfuasi. Ilifika mahali ikaanza kuonekana kama timu ya Ukawa ilikuwa na watu hatari katika mikakati kuliko sisi, jambo ambalo kwangu mimi halikunifurahisha na ninadhani halikuwafurahisha wengi, kuna jambo la kujifunza hapa, siku zote tuwapo katika mapambano tusiwe watu wa kusitasita, bali tuwe watu wa kuchukua hatua za kutekeleza mawazo yetu mara moja.

Ndugu zangu,

Sitaweza kumaliza barua hii bila kukikumbusha Chama Cha Mapinduzi juu ya kubadilisha taswira yake kwa jamii, kisitishe mara moja tafsiri ya kwamba ni chama cha matajiri na kurejea kwenye chama cha wakulima na wafanyakazi ili kila Mtanzania mwenye sifa aweze kujitokeza na atakapofanya hivyo na watu wanamkubali, apewe nafasi ya kutumikia nchi yake, asilazimishwe tu mtu kugombea hata kama hakubaliki, sababu tu ni mkongwe katika chama au ni waziri, hili limeigharimu CCM majimbo mengi safari hii, kosa hili halitakiwi kuendelea kutendwa. Katika hili ni mpango mzima wa kutayarisha viongozi wa kesho, waliopo leo ni lazima wataondoka, nafasi zao zitachukuliwa na akina nani? Lazima kuwe na ‘succession plan’ ya kwamba kizazi hiki kikiondoka, kitaingia hiki! Nionavyo mimi jambo hili halifanyiki na kama linafanyika basi si kwa kiwango kisichotarajiwa.

Lazima kuwe na “First in, first out!” yaani wa kwanza kuingia awe wa kwanza kutoka ili kupisha wengine, ningefurahi na nitafurahi sana kuona vijana wengi wanachukua nafasi za waliotangulia katika chama chetu ili kuingiza mawazo ya kizazi cha sasa, badala ya chama chetu kuendelea kutafsiriwa kama chama cha wazee kama ilivyo leo. Yapo mengi nitakayoyaongea kwa kirefu kwenye kitabu nitakachotoa cha kuirekebisha CCM kwa lengo la kuijenga si kuibomoa, bado chama hiki ni chama chenye nguvu na kinaaminiwa na watu wengi, tukikiacha kiende kama kinavyokwenda sasa mwisho wa siku watu watakuja kupoteza imani nacho na kitakufa kama vilivyokufa vyama vingine vilivyoleta uhuru katika nchi nyingine Afrika, jambo hili sipendi litokee ndiyo maana nitaandika kitabu hicho.

Baada ya kusema haya, nimalizie barua yangu kwa kumpongeza Dk. John Pombe Joseph Magufuli kuapishwa kuwa rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nimtakie utendaji mwema wa kazi katika kuhakikisha anazitimiza ahadi alizotoa, Watanzania wanatarajia kutoka kwake; huduma bora za afya, upatikanaji wa maji safi na salama, elimu bora kwa kila Mtanzania, kutokomeza ufisadi,Tanzania yenye viwanda, miundombinu bora, amani na umoja wao kuendelea kuwepo.

Haya na mengine mengi yakifanyika, Watanzania wakafaidi utajiri ambao Mungu amewapa, naomba nimhakikishie mheshimiwa rais ya kwamba miaka mitano ijayo atachaguliwa tena, lakini hayo yasipofanyika, NINA MASHAKA.

Ahsanteni.

Wasalaam,

Eric Shigongo James

Rais Magufuli afuta safari zote za watumishi wa Serikali kwenda ng'amboRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo asubuhi katika Ikulu ya Dar es Salaam amefanya kikao na Makatibu wakuu, Manaibu Makatibu wakuu, Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kutoa uelekeo wa Serikali anayoitaka mara baada ya kuapishwa.

“Nataka Serikali iendelee kwa nguvu zote na katika kutekeleza dhana ya ‘HAPA KAZI TU’ na viongozi kuzingatia na kukumbuka ahadi nilizotoa ili zianze kuonekana na kufanyiwa kazi mara moja” Rais Magufuli amesema.

Katika Kikao chake, Rais ametoa mwongozo na kusisitizia kuwa ni lazima kila mtendaji Serikalini kuuzingatia, kufuata sheria na taratibu ili taifa lisonge mbele kwa ufanisi zaidi.

Katika kikao hicho Rais ameelekeza mambo kadhaa ambayo watendaji hao wanapaswa kuyasimamia, kuyawekea mikakati na kuyapanga vizuri ili atakapo teua Baraza lake la Mawaziri mambo hayo yawe tayari ili Mawaziri watakaoteuliwa waweze kuyasimamia bila kukosa.
Mambo hayo muhimu ni kama ifuatavyo:

Kuanzia mwezi Januari mwaka 2016, wanafunzi wote wanaoanza shule watasoma bure bila kulipa ada, Katika jambo hili, Rais amewataka watendaji kuanza kuliwekea mikakati tayari kwa utekelezaji
Suala la mikopo ya wanafunzi nalo lifanyiwe kazi na mipango yake ikamilike kwa ajili ya utekelezaji mzuri zaidi.

Amefuta safari zote za nje ya nchi kuanzia leo hadi hapo atakapolitolea suala hilo maamuzi mengine na kueleza kuwa shughuli zote zinazotakiwa kufanywa nje ya nchi zifanywe na kusimamiwa na mabalozi wa Tanzania wanaowakilisha nchi huko nje.

Pengine patokee jambo la dharura sana na hata hilo lazima kibali kitolewe na Rais au Katibu Mkuu Kiongozi. Badala yake Rais amewataka watendaji hao kufanya zaidi ziara za kwenda vijijini ili kuzijua na kutatua kero za wananchi wa Tanzania.

Katika Kikao hicho, Rais amemtaka Kamishna wa TRA, Ndugu Rished Bade kusimamia kwa makini zoezi la ukusanyaji wa mapato nchini na kuhakikisha kero ndogo ndogo kwa wananchi lianze kutekelezwa kama alivyo ahidi kwa kufanyiwa kazi mapema zaidi.

Rais ameitaka TRA kukusanya mapato hayo kutoka kwa wafanya biashara wakubwa zaidi na wale wanaokwepa kodi bila kuogopa mtu wala taasisi yoyote hapa Tanzania na kusisitiza kuwa katika Serikali hii wa kutoa maamuzi vinginevyo zaidi ya haya ni yeye Rais ama Makamu wake.

Rais Magufuli pia ameagiza usimamizi katika suala la manunuzi ambalo limekuwa likitumika vibaya na kuwa mwanya wa kuibia Serikali kwa watu kuongeza bei ya vitu hata kama ni vya bei ndogo kabisa katika jamii.

“Ikitokea suala hilo likagundulika kwa watu kuongeza bei ya vitu, watendaji watawajibishwa mara moja”. Rais amesema, na kuwataka watendaji hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo na kuzingatia maadili mema ya kazi.

………………………MWISHO……………………
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

7 Novemba, 2015


Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bwana Rished Bade na Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono na Katibu Mkuu Utumishi Mhe HAB Mkwizu na Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Mcheche Masaju na Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Watendaji Wakuu serikalini leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kukutana nao na kupanga mikakati ya kuendesha serikali kwa weledi, nidhamu na moyo wa kupenda kazi.

Picha: Ikulu