Notice to SUA Students: English Language Proficiency Screen Test

Source: suanet.ac.tz

Maalim Seif awaasa: Msichokozeke!

Katibu Mkuu wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza akiwahutubia viongozi wa Wilaya, Majimbo na Matawi huko Ngoma Hazingwa Chakechake Pemba
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amewataka Wazanzibari kutokubali kuchokozeka wakati huu baada ya hali iliyojitokeza nchini. Alisema wapo watu lazima watafanya vitimbi kwa tama ya kuvuruga amani ya nchi lakini amewataka wananchi kuwa na subra na kuwaacha wenye vitimbi hivyo kuendelea na vitimbi vyao huku wakisubiri.

Maalim Seif alisema hayo alipokuwa akihutubia katika mkutano ulioandaliwa kwa ajili ya viongozi wa Wilaya, Majimbo na Matawi kisiwani Pemba uliofanyika katika ofisi za uchaguzi za CUF Pemba zilizopo Ngoma Hazingwa, Chakechake.

Alisema hakuna haja ya kupoteza muda na kuendeleza propaganda zisizokuwa na msingi kinachopaswa kufanyika hivi sasa ni Tume ya Uchaguzi Zanzibar kumalizia kazi yake na kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa Oktoba 25.

“Wache wapoteze muda wataniapisha tu, na wajue muda wangu wa Urais utaanza siku nitakapo apishwa kwa mujibu wa Katiba”, alisema.

Aidha amewataka wananchi kisiwani Pemba watembee kifua mbele kwa sababu ni suala la muda tu kabla hajatangazwa kuwa mshindi wa Urais wa Zanzibar na kuapishwa kuwa Rais wa awamu ya nane.

Alisema wanachofanya viongozi wa CCM hivi sasa ni kuchelewesha muda tu, lakini kwa kuwa wananchi wa Zanzibar wamemchagua yeye kuwa Rais na Dunia nzima inafahamu hilo, hatimaye watamwita wenyewe na kumuapisha kuwa Rais wa Zanzibar.

“Wananchi wa Pemba kuleni mshibe, laleni bila ya hofu na tembeeni kifua mbele, hawana njia lazima watakubali maamuzi ya wananchi wa Zanzibar walionichagua niwe Rais wao”, alisema Maalim Seif.

Alieleza kuwa Chama cha Wananchi CUF kupitia Baraza Kuu la Uongozi tayari kimeamua kwamba hakuna suala la uchaguzi wa Zanzibar kurejewa kwa sababu wananchi wameshafanya maamuzi ya kidemokrasia katika uchaguzi uliokuwa wa huru na haki.

Katibu Mkuu huyo wa CUF ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar alisema jambo linalowatia kiwewe CCM na kutoa visingizio kuhusiana na kura za Pemba ni kutokana na fedha nyingi walizotumia kwa tamaa ya kupata majimbo kadhaa.

Alisema kwamba CCM wamesahau kuwa miaka yote hawapati majimbo kisiwani Pemba na hivyo si ajabu katika uchaguzi wa mwaka huu kukosa viti vyote vya Ubunge, Uwakilishi na Udiwani.

Maalim Seif alisema hata huyo mgombea Urais wa Zanzibar kupitia ADC, Hamad Rashid Mohammed ambaye alitegemewa na CCM kupunguza kura za Maalim Seif kisiwani Pemba hakufua dafu na yeye mwenyewe (Hamad Rashid) aliambulia kura 495 tu.

“Viongozi wa CCM maskini walimdanganya sana Dk. Shein kuwa watapata viti Pemba na kura za kutosha za Rais, wametumia fedha nyingi katika uchaguzi huu, lakini walisahau hali halisi ya Pemba na sasa wanahangaika”, alisema Katibu Mkuu wa CUF.

Alieleza kuwa zipo taarifa kuwa kiasi cha shilingi milioni 70 zilitumiwa na CCM katika jimbo moja tu la Mtambwe, jimbo ambalo katika chaguzi zote zilizofanyika chama hicho hakijawahi kupata kura zaidi ya asilimia tano.

Maalim Seif aliwapongeza mawakala wa CUF katika majimbo yote 54 ya Zanzibar kwa namna walivyo jidhatiti kulinda kura za chama chao na hatimaye kukiwezesha kupata ushindi mkubwa ambao haujapata kutokea Zanzibar.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui alisema uchaguzi mkuu uliofanyika kisiwani Pemba mwaka huu ni mfano mzuri wa uchaguzi uliokuwa huru na wa haki katika nchi nzima.

Alisema kuwa wale wanaodai kuwa kura zimezidi kisiwani humo ni waongo wanaotapa tapa kwasababu kuna watu waliojiandikishwa zaidi ya 20, 000 hawakupiga kura na waliojitokeza kwenda kupiga kura ni 119,000.

Mazrui alisema CCM wamepatwa na maumivu makubwa kisiwani Pemba kutokana na matumizi makubwa ya fedha waliyoyafanya kwa tamaa ya kupata majimbo manne, lakini wananchi wa Pemba hawakuona sababu ya kukichagua chama hicho.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui akiwahutubia viongozi wa Wilaya, Majimbo na Matawi kisiwani Pemba
Khamis Haji wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais (OMKR)

Kauli ya EU, Marekani kuhusu Sheria ya Uhalifu wa Kimtandao na ukiukwaji haki za binadamu Tanzania

Mwanamkakati wa Lowassa akamatwa

Bashir Awale
Bashir Awale
Mwanamkakati wa aliyekuwa mgombea wa urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bashir Awale, amekamatwa na kuwekwa ndani katika Kituo cha Polisi cha Kati.

Habari zilizopatikana jana kutoka ndani ya timu ya kampeni ya mgombea wa CHADEMA, Edward Lowassa, zinasema kuwa Awale alikamatwa juzi jioni kwenye maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Taarifa zaidi zinasema kuwa Awale alisimamamishwa na askari, ambao walimchukua kwenye gari lao huku wakilitelekeza gari lake kwenye maeneo hayo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, aliliambia Nipashe atalizungumzia suala hilo leo pamoja na mambo mengine.

“Nimewaagiza vijana wangu waniandalie taarifa juu ya suala hilo. Nitalizungumzia jambo hilo kesho (leo) pamoja na mambo na mengine,” alieleza Kamishna Kova, ambaye hakutaka kuingia kwa undani wakati alipohojiwa na gazeti hili kuhusiana na suala hilo.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili unaonyesha kwamba kukamatwa kwa Awale kunahusishwa na masuala ya Uchaguzi Mkuu uliomalizika hivi karibuni kutokana na ukaribu wake na Lowassa.

Lowassa alishindwa kwenye uchaguzi wa urais baada ya kushika nafasi ya pili kwa kupata kura 6,072, 848 sawa na asilimia 39.97 wakati mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli aliibuka mshindi kwa kupata kura 8,882,935 sawa na asilimia 58.46.

Awale alikuwa miongoni mwa viongozi waandamizi kwenye timu ya kampeni ya Lowassa tangu wakati alipokuwa mwanachama wa CCM.

Lowassa alipoachana na CCM na kujiunga na CHADEMA, Julai 28 mwaka huu, Awale alikuwa miongoni mwa watu waliofuatana naye.

Awale alikuwa miongoni mwa watu waliofuatana Lowassa siku anatambulishwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, baada ya kujiunga rasmi na chama hicho.

Kabla ya kuingia kwenye masuala ya siasa, Awale alikuwa Ofisa Mkuu Mtendaji wa Benki ya Stanbic nchini Tanzania kabla ya kuachia ngazi mwaka 2013.

Aliiongoza benki ya Stanbic kuanzia mwaka 2006, lakini kabla ya hapo alikuwa akifanya kazi katika Benki ya Citibank.
Tangu alipoachana na Stanbic, Awale alikuwa miongoni mwa wanamkakati waandamizi wa Lowassa tangu alipokuwa akiwania kugombea urais kwa tiketi ya CCM.

Lowassa alipokatwa jina lake CCM na kujiunga na CHADEMA, Awale alikuwamo kwenye timu ya kampeni akiwa miongoni mwa viongozi waandamizi.

Pamoja na kuwemo kwenye timu ya kampeni, pia ni anachukuliwa kama miongoni mwa wasaidizi na washauri muhimu wa Lowassa.

Kukamatwa kwa Awale kunakuja baada ya hivi karibuni vijana wanane waliokuwa wakisaidia kazi ya kujumlisha kura za Lowassa kwenye kituo cha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UJAWA) kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kujumlisha matokeo ya kura za urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu.Jeshi la polisi linamshikilia mwanaharakati wa Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Bashir Awale Ally ambaye pia anadaiwa kuwa meneja wa kampeni wa aliyekuwa Mgombea Urais Kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Edward Lowasa kwa madai ya kuibuka Utata juu ya Uraia wake baada ya kukutwa na hati ya kusafiria inayomtambulisha kuwa Raia wa Kenya huku akishiriki katika kampeni kinyume na katiba ya nchi.

Kamishna wa Polisi Kanda maalum DSM CP Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari amesema mtuhumiwa huyo alitiwa mbaroni Novemba 9 katika eneo la Mikocheni anakoishi na baada ya kupekuliwa alikutwa na nyaraka mbali mbali ikiwemo cheti vya kuzaliwa namba D.063711 Chenye jina la Bashir Abdi Ally kinachoonyesha alizaliwa katika hospitali ya dodoma Jumali 11.1969 huku pia nyaraka nyingine zikionyesha akiomba uraia wa Tanzania Idara ya Uhamiaji.

Kamishna Kova amesema kutokana na Utata huo Bashir anachunguzwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji na ikibainika kuwapo kwa makosa ya jinai, atafikishwa katika vyombo vya sheria kujibu mashtaka yanayomkabili.

Aidha katika kupambana na matukio ya Uhalifu Jeshi hilo limefanikiwa kuwatia mbaroni majambazi 7 pamoja na bastora 6 na bunduki aina ya SMG zikiwa na jumla ya risasi 61 ambazo zilikuwa zikitumika katika matukio mbali mbali ya unyang'anji.

Amesema Majambazi hao wamekamatwa katika msako maalum unaoendeshwa na jeshi hilo hasa katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka ambapo uzoefu unaonyesha kuwa matukio ya ujambazi wa kutumia silaha huongezeka.
 • via ChannelTEN

Membe ataka rungu la Rais Magufuli la kufuta safari lifikie mashirika

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amempongeza Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwa kupiga marufuku safari za nje ya nchi, akisema mawaziri na watendaji wa Serikali walikuwa wakigongana angani na ndege utadhani Tanzania ilikuwa ikiwaka moto.

Mbunge huyo wa zamani wa Mtama alisema uamuzi huo utaokoa fedha nyingi za Serikali na kumtaka Rais kushusha rungu hilo hadi kwenye mashirika.

Wakati Membe akieleza hayo, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alisema kila safari ya nje ina gharama yake na kila safari itakayofutwa zitapatikana fedha kusaidia masuala mengine ya maendeleo katika jamii.

Juzi, Dk Magufuli alipiga marufuku safari za nje ya nchi kwa watendaji na kwamba shughuli ambazo wangekwenda kuzifanya, kuanzia sasa zitahitaji kibali kutoka kwake au zitafanywa na mabalozi wa Tanzania walioko katika nchi husika.

Jana Membe alisema: 
"...Tulikuwa tunagongana huko hewani utadhani huku nyumbani kunaungua moto. Tunapobaki huku ndani tunaokoa hela nyingi na nina hakika (Dk Magufuli) ataingilia hata kwenye mashirika. Kuna wakuu wao wanasafiri kila siku, nina hakika wataguswa katika hili. Lazima kuziokoa pesa za kufanyia shughuli nyingine mimi naunga mkono mia moja kwa mia hili?
Alisema kitendo cha Rais Magufuli kufuta safari za nje hakina maana kwamba uhusiano wa Tanzania na nchi hizo unakufa. 
"Hajakataza wageni, wafanyabiashara wa dunia wala wawekezaji kuja Tanzania, hata wawekezaji hawawezi kukataa kuja Tanzania waache gesi, dhahabu, almasi au tanzanite.?
Alisema wapo watu wanaodhani kuwa kauli ya Rais Magufuli itamhusu hadi Waziri wa Mambo ya Nje,
"... atakwenda nje maana ukishamuita waziri wa mambo ya nje lazima aende nje. Dk Magufuli hawezi kusema hivyo. Hutasikia amekatazwa maana ndiyo wizara yenyewe na inashughulika na dunia."
Alisema kauli hiyo pia haina maana kwamba Wizara ya Mambo ya Nje imefutwa kwa kuwa balozi za Tanzania zilizopo nje zipo chini ya wizara hiyo.

Aondoka UVCCM baada ya kuteuliwa Mbunge - Viti Maalumu, CHADEMA

[video] Buying a used car: How to inspect (exterior, mechanical, interior), road test and paperwork

This six part used vehicle buying guide by Speedkar99 covers the following:-

 1. Exterior inspection
 2. Mechanical Inspection
 3. Interior Inspection
 4. Road Test
 5. aperwork & Procedures
 6. After Buy


Job opportunity for Tanzanian Pharmaceutical technicians

Introduction
The Mtwara Medical Training Centre (Mtwara COTC) is a Public Health Training Institution established by the Ministry of Health and Social Welfare in 1983. The MMTC envisions becoming a centre of excellence in production of competent healthcare professionals, quality research and provision of consultancy to the governmental and nongovernmental organizations in health related matters. The MMTC through its various certificate and diploma courses, delivers and promotes high quality and competitive teaching and learning, research and innovation, and public service in Clinical Medicine, Health Management, Community Health and Pharmaceutical Sciences for enhanced value addition to people, while emphasizing entrepreneurship with a view to promoting better health for all in Tanzania.  

1. Employment opportunities
The MMTC invites applications from suitably qualified Tanzanians to be considered for immediate employment to fill the following vacant posts:

a). School of Pharmaceutical Sciences
            4 positions - Tutors

b). Qualifications and Experience:
·       Applicants must possess an Ordinary Diploma in Pharmaceutical Sciences from an Institution recognized by the Ministry of Health and Social Welfare and National Council for Technical Education (NACTE).
·       S/he must also be registered by the Pharmacy Council of Tanzania.  
·       Three years working experience working in a teaching institution is an added advantage

c). Main duties and responsibilities include;
·        Carries out seminars, tutorials and practicals for certificate students
·        Assists in research, consultancy and public service;
·        Sets, invigilates and marks certificate examinations;
·        Supervises projects and practical training for certificate students;
·        Conducts research and publishes results;
·        Participates in relevant workshops and conferences;
·        Performs any other relevant duties assigned by one’s superior

2. TERMS OF SERVICE:
Full-time


3. REMUNERATION
Attractive package will be offered to the right candidate commensurate with his/her qualifications and experience.

4. MODE OF APPLICATION
Interested candidates should apply in confidence to the undersigned enclosing:
i.       Detailed CV
ii.     Photocopy of relevant certificates and transcripts.
iii.   Names and Addresses of two referees.
iv.   Mode of communication, e.g. Telephone, fax, email, etc.

The Principal,
Mtwara Medical Training Centre,
P.O. Box 86,
MTWARA

NOTE:
Only shortlisted candidates will be contacted for interview.

5. DEADLINE
Two weeks from the date of first appearance of this advertisement.

11th November, 2015

Uzinduzi wa Diwani ya Mageuzi ya Mashairi / Poetry Anthology by Prof. K.K. Kahigi

Salamu kutoka Soma,

Ndugu, Jamaa na Rafiki wa Maarifa, Usomaji na Maendeleo tunapenda kukukaribisha kwenye Uzinduzi wa Diwani ya Mageuzi ya Mashairi ya Prof. Kulikoyela. K. Kahigi.

Uzinduzi utafanyika siku ya Jumamosi - 14/11/2015, nao uzinduzi utafanyikia MKAHAWA WA VITABU - SOMA BOOK CAFE, 53 Mlingotini Close, Regent Estate.

Shughuli itaanza saa 9:00 alasiri mpaka saa 10:30 jioni. Uzinduzi utakolezwa na Utambaji/ Ughani wa Mashairi kutoka katika Diwani itakayozinduliwa.

Kwa mawasiliano zaidi
Mulokozi: 0756-795674
Jasper: 0712-568699

Greetings from Soma,

Dear Esteemed Friend of SOMA, noticing your devotion and passion for knowledge and development, Soma would like to invite you to the launch of a book - POETRY ANTHOLOGY - by Prof. Kulikoyela Kahigi.

The launching shall be held and hosted at Soma Book Cafe, 53 Mlingotini Close, Regent Estate on Saturday - 14/11/2015.

The event shall commence at 1500hrs - 1630hrs. The event shall include the recital of some of the poems in the anthology.

ADDRESS: Mlingotini Close, Plot Number 53 Regent Street - Mikocheni A, Dar es SalaamDIRECTIONS: Soma Book Cafe's Google Map
PHONE: 0673014071WEBSITE: http://www.somabookcafe.com/
FACEBOOK: https://www.facebook.com/groups/365507850907/
TWITTER: https://twitter.com/SomaMkahawani

Wito wa ACT-Wazalendo na maoni ya Ilyas na Kabugumila kuhusu mkwamo wa kisiasa Zanzibar

Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha ACT -Wazalendo, Samson Mwigamba katikati ni aliyekuwa mgombea wa Urais wa chama cha ACT-Wazalendo,Anna Mgwira na kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. (picha:Avila Kakingo)
Kwenye ukurasa wake wa Facebook, Mbunge mteule wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) aliandika hivi jana Novemba 10, 2015:
Suala la Zanzibar lisidharauliwe kabisa. Matokeo yatangazwe na mshindi aapishwe. Hatuwezi kutazama tu Katiba inakanyagwa. Vinginevyo Maalim Seif apate Jaji amwapishe na aunde Serikali mara moja na kuanza kuwatumikia Wazanzibari, Serikali ya Umoja wa kitaifa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar (link)
I have studied Zanzibar case and concluded ( S.28(1)(2) that whoever is calling himself or herself, NOW, a Zanzibar President is committing a treasonous offence liable to death penalty, once found guilty by the court of law (link)
Omar Ilyas akaeleza:
Kuhusu uhaini rejea hapa kaka Zitto Kabwe
SMZ Vs. Machano Khamis Ali & Others
Criminal Case No 8 of 2000
Kissanga J.A,
Rugakingira J.A
Ramadhani J.A
Treason cannot be commited against the Revolutionary Government of Zanzibar
Asimwe Kabugumila akasema:
Hacheni kujichanganya 28 (1) (e) inaipa nguvu Su sect 2 ya Sec 28.
So Mh Zito Ana argument nzuri, huwezi kuendelea kuwa Rais Wa Zanzibar baada ya Tarehe uliokula kiapo kupita. Kwa Mujibu Wa Subsection 2
Hapo nimetoka tafsiri yangu kama Mwanasheria.
Nadhani Mahakama ingekuja mapema kutusaidia kwenye hili.
I am tired
Leo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, uongozi wa ACT-Wazalendo umetoa taarifa iliyoripotiwa na "Globu ya Jamii" ifuatavyo: 
CHAMA Chama cha ACT Wazalendo kimemwomba Rais wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli ahakikishe Tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) itangaze matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu ili walioshinda watangazwe na waapishwe kwaajili ya kuanza kazi katika serikali ya Zanzibar ikiwa mpaka sasa Zanzibar haina Serikali.
Zitto amesema kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) hakuwa na mamlaka yoyote ile katika tume hiyo ya kukufuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar kwani tume inawajumbe wake yeye peke yake hana mamlaka hayo.
Pia zitto amesema kuwa chama chake kitafanya kazi kwaajili ya masrahi ya wananchi ya sasa na yabaadae, pia amesema kuwa chama chake hakitashiriki katika kugombea nafasi ya spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Video kutoka vyombo mbalimbali vya habari

TTCL yakanusha madai ya TEWUTA

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi akizungumza na vyombo vya habari Makao Makuu ya TTCL jijini Dar es Salaam kujibu madai ya TEWUTA. 
KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imepinga madai yaliyotolewa na Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Huduma za Mtandao wa Mawasiliano Tanzania (TEWUTA) jana dhidi ya Menejimenti na Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL na kufafanua kuwa madai hayo si ya kweli zaidi ya upotoshaji wenye nia ovu ya kufanikisha malengo binafsi na kutaka kuikwamisha jitihada za TTCL katika maendeleo.

Ratiba ya NEC ya uchaguzi wa Wabunge kwa maeneo ulimoahirishwa


Ratiba ya NEC ya uchaguzi wa madiwani kwa maeneo ulimoahirishwa


Waliochukua fomu CCM Lumumba za kuwania Uspika wa Bunge la Jamhuri


Aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta akisaini kitabu cha wageni kabla ya kuchukua fomu za kuwania uspika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mbele ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni, Ndugu Mohamed Seif Khatib

Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Karagwe Gosbert Blandes akikabidhiwa fomu za kuwania nafasi ya Uspika wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni, Ndugu Mohamed Seif Khatib

George Nangale akipitia fomu ya kuwania nafasi ya uspika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya kukabidhiwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni, Ndugu Mohamed Seif Khatib katika ofisi ndogo za CCM Lumumba.
Banda Sonoko akikabidhiwa fomu za kuwania nafasi ya Uspika wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni, Ndugu Mohamed Seif Khatib
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni, Ndugu Mohamed Seif Khatib akimkabidhi fomu Ndugu Simon G. Rubugu
Hawa ndio waliojitokeza mpaka sasa kuchukua fomu Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba:
 1. Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta
 2. Aliyekuwa mbunge wa Karagwe, Gosbert Blandes
 3. Leonce Mulenda
 4. George Nangale 
 5. Profesa Costa Mahalu
 6. Muzamil Kalokola
 7. Banda Sonoko
 8. Simon Rubugu

Taarifa ya Kamishna Mkuu TRA kuhusu makusanyo ya kodi


TAARIFA YA MAKUSANYO YA KODI

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya jumla ya shilingi trililion 3.77kuanzia mwezi Julai hadi Oktoba 2015 ambayo ni sawa na asilimia 97.6. ya lengo la makusanyo ya sh trilioni 3.87 ikiwa ni jitihada za TRA kutekeleza mkakati wa serikali ambao unaitaka kukusanya Ths trililioni 12.3 kwa mwaka wa fedha 2015/2016.

Kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa TRA Rished Bade, mwezi Julai TRA ilikusanya kiasi cha shilingi bilioni 849,582.9ambacho ni asilimia 99.4 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 854,922.9.

Mwezi Agosti TRA ilikusanya kiasi cha shilingi bilioni 890,536.7 ambacho ni asilimia 101.5 ya lengo la kukusanya shilingi biilioni 876,974.2 ambapo mwezi Septemba jumla ya shilingi trilioni 1,067,888.3 zilikusanywa ikiwa ni asilima 91.7 ya lengo trilioni 1,163,999.4 kwa mwezi mwezi Oktoba TRA iilkusanya shilingi bilioni 970,089.6 ikiwa ni asilima 99.3 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 976,441,5.

Taarifa ya mwenendo wa makusanyo ilipitishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya TRA katika kikao
cha bodi kilichofanyika jana tarehe 10 Novemba 2015 katika ofisi za makao makuu ya TRA” amesema Bw. Bade.

Mafanikio katika makusanyo haya yametokana na mikakati madhubuti iliyowekwa na mamlaka
baada ya kusaini mkataba na Waziri wa Fedha ambapo Kamishna Mkuu alisaini mkataba na kila Mkuu wa Idara na wakuu wa Idara kusaini mikataba na wafanyakazi walioko chini yao ili kila mfanyakazi kuwajibika ipasavyo.

Wito wa TRA ni kwa mfanyabiashara na wadau wote wa kodi kutimiza wajibu wao wa
kulipa kodi kwa hiari ili kuchangia pato la taifa.

Sambamba na hilo TRA imepokea kwa furaha sana wito wa Mheshimiwa Rais John Pombe
Magufuli wa kuhimiza ukusanyaji wa mapato bila woga na bila kumwonea mtu.

Pamoja Tunajenga Taifa Letu
Rished Bade
KAMISHNA MKUU

Mfumo wa utendaji TANAPA wabadilishwa

Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Bw. Allan Kijazi akikabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya uongozi kutoka mfumo wa kiraia kwenda jeshi-usu kwa Mhifadhi Mussa Mandia katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi
Shirika la Hifadhi za Taifa limeanza rasmi kutumia mfumo wa jeshi usu kutoka ule wa kiraia katika utendaji kazi wake ikiwa ni hatua mojawapo ya kuongeza ufanisi katika shughuli za uhifadhi.
Jumla ya wahifadhi 40 walihitimu mafunzo ya Awamu ya kwanza ya kubadili mfumo wa utendaji kazi kutoka ule wa kiraia kwenda wa jeshi usu kwa kwa viongozi maafisa wa ngazi ya kati “Transformation Leadership Course for Middle Cadre Wardens” yaliyofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi hivi karibuni.

Mfumo wa utendaji kazi kwa kijeshi-usu utalisadia shirika kuimarisha nidhamu ili kuboresha utendaji kazi hasa katika nyakati hizi ambapo changamoto kuu ya ujangili unaotumia silaha za aina mbalimbali za moto hasa za kivita inazidi kushika kasi.

Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Bw. Allan Kijazi akikabidhi zawadi ya kuhitimu mafunzo ya uongozi kutoka mfumo wa kiraia kwenda jeshi-usu kwa Mhifadhi Prisca Lyimo katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Faustine Masalu akiongea wakati wa hafla ya ufungaji wa mafuzo ya kutoka mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa wa jeshi-usu.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Faustine Masalu akiongea wakati wa hafla ya ufungaji wa mafuzo ya kutoka mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa wa jeshi-usu.

Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Bw. Allan Kijazi akiongea wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo kubadili mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa wa jeshi-usu.

Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Bw. Allan Kijazi akifungua mafunzo ya awamu ya pili mafunzo kubadili mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa wa jeshi-usu.

Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Bw. Allan Kijazi akikagua gwaride maalum la wahitimu huku akiongozwa na Kamanda wa Gwaride hilo Mhifadhi Kelvin Nkulila.

Gwaride la wahitimu wa mafunzo kubadili mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa wa jeshi-usu likitoa heshima mbele ya mgeni rasmi.

Gwaride la wahitimu wa mafunzo kubadili mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa wa jeshi-usu likitoa heshima mbele ya mgeni rasmi.

Wahifadhi waliohitimu mafunzo kubadili mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa wa jeshi-usu wakiwa katika picha ya pamoja.

Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa TANAPA Bi. Witness Shoo akiwa na Wahifadhi wa kike waliohitimu mafunzo ya kubadili mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa wa jeshi-usu.

Taarifa: Mashine ya MRI Muhimbili yatengemaaDaktari akimpatia huduma mgonjwa kwa kutumia mashine ya MRI ambayo ilikuwa mbovu kwa muda mrefu ila imetengamaa mara baada ya Rais John Magufuli kufanya ziara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuagiza matengenezo ya haraka yafanyike.

Madaktari wakifuatilia kwa makini jinsi mashine ya MRI inavyofanyakazi mapema hii leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo

Viongozi, Mashehe "wa Uamsho" wanaotuhumiwa ugaidi wafikishwa mahakamani


Viongozi na Masheikh 22 wa kundi la Uamsho linaoongozwa na Sheikh Farid Hadi Pamoja na Sheikh Abdallah Mselem ambao wanatuhumiwa kwa ugaidi leo wamefikishwa katika mahakama ya rufaa chini ya ulinzi mkali wa vikosi mbali mbali vya jeshi la polisi kwa ajili ya kupinga kusudio la serikali la kukataa rufaa dhidi yao.

Kesi hiyo kwa zaidi ya miaka miwili imekuwa ikiendelea katika mahakama ya kisutu jijini dsm ambapo mawakili wa upande wa washtakiwa wamekuwa wakitaka ifutwe kwa kuwa mahakama ya hakimu mkazi wa kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya ugaidi.

Akizungumza baada ya kumalizika kusikilizwa kwa kesi hiyo wakili wa watuhumiwa hao 22 Juma Nassor amesema wamekwenda kuweka pingamizi katika Mahakama ya Rufaa baada ya mawakili wa serikali kuwasilisha maombi ya kukata rufaa dhidi ya mahakama kuu ambayo ilitamka kuwa mahakama ya kisutu ambayo inasikiliza kesi ya Masheikh hao ina mamlaka ya kisheria ya kutamka kuwa mashitaka wanayotuhumiwa Sheikh Faridi na wenzake kuwa ni halali au la.

Hata hivyo kwa upande wa mawakili wa serikali hawakuridhika na hatua hiyo na kupeleka pingamizi ikiwemo kuwahishwa kwa pingamizi kwa upande wa washtakiwa chini majaji watatu wa mahakama hiyo ambao walisikiliza hoja za pande zote mbili ambazo watazitolea uamuzi pindi shauri hilo litakapoitishwa tena.

Wakati kesi hiyo ikiwa inaendelea nje ya mahakama ulinzi mkali wa vikosi vya jeshi la polisi, magereza, pamoja na askari kanzu walitanda kila kona huku magari ya maji ya kuwasha yakiwa yameegeshwa pembeni. Wananchi waliojaribu kupita katika eneo hilo pia walikuwa wakizuiwa.

Ndugu jamaa na marafiki waliofika katika eneo hilo walionekana wakipaza sauti na kutamka maneno kadhaa wakati watuhumiwa hao wakipandishwa katika basi la magereza kurudishwa rumande na hivi ndivyo ilivyokuwa.
 • via ChannelTEN

Download new song by JanB - My LifeUnaweza kuidownload Ngoma yangu mpya iitwayo My Life, imetoka rasmi jana, download kupitia link hii My life | Mkito.com

Naombeni sana muweze ku-share katika kurasa na tovuti /blog zenu pamoja nakutumia katika play list zenu redioni na kumbi za starehe.