EBM Signature - Dress to kill! Opening soon...EBM SIGNATURE opens at Dar Free Market Mall, store number 30B on December 15, 2015.

@ebmsignature specializes in MADE IN USA women and children Clothing and Accessories. All products are of high quality and original from the United States of America.

@ebmsignature sells both in retail and wholesale. Our price is affordable. The wholesalers who purchase a package of 10 pieces receive Tsh. 50,000/- discount and those purchasing 30 pieces get Tsh. 300,000/- discount.

Follow the EBM SIGNATURE for selection of such high quality Made in USA products.

Contact us through WhatsApp +16192284381

Don't miss the opportunity to purchase Christmas clothing and accessories for your loved ones from EBM SIGNATURE. We are providing special sale for Christmas and official store launching


Job: Tanzania ACT Coordinator, Lead IP Project (Local Candidates Preferred)

Organization: Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 31 Dec 2015

Maalim Seif azugumza na Balozi wa EU na viongozi wa UKAWA

Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa pamoja na viongozi wa UKAWA baada ya kikao cha mashauriano kilichofanyika Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Na Hassan Hamad, OMKR

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amerejea kauli yake ya kutotambua kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika tarehe 25 mwezi uliopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kikao cha mashauriano na viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA, Maalim Seif amesema Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Bw Jecha Salim Jecha hana mamlaka ya kufuta uchaguzi huo, na kinachohitajika na kuendelea na mchakato wa kuhakiki kura zilizobakia na mshindi kutangazwa.

Kuhusu tamko lililotolewa na serikali juu ya kufutwa rasmi kwa uchaguzi huo kupitia tangazo lililochapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali tarehe sita mwezi huu, Maalim Seif amesema tamko hilo limekosa uhalali tangu lilipotolewa na Mwenyekiti wa ZEC.

Maalim Seif ambaye pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF amesema Chama chake hakijalizingatia tamko hilo na wala hakijadili uwezekano wa kurejewa kwa uchaguzi huo, kwa madai kuwa uchaguzi ulikamilika bila ya kuwepo malalamiko kutoka chama chochote cha siasa na wala Tume ya Uchaguzi.

Mapema akizungumza baada ya kikao hicho cha mashauriano, aliyekuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema Mhe. Edward Lowassa amesema kikao hicho kilichojadili Mkwamo wa kisiasa Zanzibar kimekwenda vizuri.

Hata hivyo amesema ufafanuzi zaidi utatolewa Jumapili ijayo ambapo viongozi hao wanakusudia kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kikao hicho Maalim Seif alifanya mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) Bw. Filberto Seregondi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kuelezea hatua zinazochukuliwa kukwamua mkwamo wa kisiasa Zanzibar.

Balozi Seregondi ambaye anamaliza muda wake wa utumishi hapa nchini,aliambatana na ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi mkuu wa Tanzania kutoka Umoja huo.

Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad alipokutana na Balozi wa EU nchini Tanzania Bw.Filberto Seregondi pamoja na ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi mkuu wa Tanzania kutoka EU huko hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam 
Picha na Salmin Said, OMKR

Ushirika wa Mama na Baba Lishe

Mratibu na Msimamizi Mkuu wa Jumuiya Ya Mama na Baba Lishe Mkoa wa Dar es Salaam, Said Said (wa pili toka kulia), akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya Maelezo kuelezea kuhusu uzinduzi wa "Ushirika wa Mama na Baba Lishe" unaotarajia kufanyika Novemba 15, 2015 katika ukumbi wa SabaSaba jijini Dar es Salaam. 

Lengo la ushirika huo ni kuunganisha kwa pamoja wadau mbalimbali, kutoa fursa kulinda haki za ajira na kuzitafutia ufumbuzi na kuondoa tatizo la ajira kupitia tasnia hii ikiwa ni kumtambua mama na baba lishe kama sehemu ya maisha ya kila mmoja wetu, kwani kila Mtanzania anaufahamu umuhimu wa mama na baba lishe. Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 50% ya Wanzania waishio mijini hupata huduma ya chakula kupitia baba na mama lishe.


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mama na Baba Lishe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Mhonzu akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idata Maleleo kuelezea kuhusu Uzinduzi wa Ushirika wa Mama na Baba Lishe unaotarajia kufanyika Novemba 15, 2015 ukumbi wa SabaSaba jijini Dar es Salaam.


Mama Lishe wakiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa idata Maleleo kuelezea kuhusu Uzinduzi wa Ushirika wa Mama na Baba Lishe unaotarajia kufanyika Novemba 15, 2015 ukumbi wa SabaSaba jijini Dar es Salaam.
Waaandishi wa habari wakufuatia mkutano huo.
 • Tumeshirikishwa taarifa hii na Cathbert Kajuna / Kajunason Blog. 

Dhana ya mabadiliko: Kama tunataka kubadili taifa hili...

Unapodai mabadiliko katika nchi, wewe kwanza umebadilika? Je unatabia ambazo zina reflect raia anayewajibika na mwema? Hili ni swali ambalo wote tunapaswa kujiuliza, tunaopenda na kuhitaji mabadiliko katika serikali yetu na katika nchi.

Kwa sababu swali hili litakuwa ndio msingi wa mabadiliko makubwa zaidi katika nchi yetu na katika jamii yetu.

Naamini mabadiliko huanza na mtu binafsi kwa kubadili mtazamo wake . Huwezi kubadili jamii yako kama mtazamo wako mwenyewe haujabadilika. Ili ubadili nchi ni lazima wewe mwenyewe ubadilike.

Changamoto ambazo zinatukabili kama taifa na katika jamii yetu zitabadilika tu kama tutabadili mtazamo wetu ambao ndio msingi wa tabia zetu na matendo yetu.

Kama hutendi haki ukiwa raia wa kawaida huwezi kutenda haki ukiwa kiongozi. Viongozi wanatoka miongoni mwetu na ili tupate viongozi bora ni lazima sisi wenywe tutambue changamoto zetu na tubadilike.

Kuna tabia ambazo ni vikwazo kwa maendeleo yetu ni lazima tuzijue na tuwe tayari kukabiliana nazo katika ngazi ya chini. Lakini kuna tabia ambazo ni vikwazo kwa mahusiano yetu nazo lazima tuzijue. Kwasababu hatuwezi kuendelea kama hatuna mashirikiano mazuri.

Tunapodai mabadiliko katika nchi ni lazima kwanza tujiangalie wenyewe. Na kuona ni vitu gani ambavyo wewe binafsi unapaswa kubadilika uwe raia bora na anayewajibika kwa taifa lake, jamii yake na familia yake lakini pia mwenye mahusiano mazuri na wengine.Halafu baadae ndio tuiangalie serikali na kuinyooshea kidole. Kisha tuiambie serikali wewe huwajibiki umeshindwa!

Maisha yako yamejaa utapeli na wizi na wewe unasema unataka mabadiliko ni yapi hayo? UNAVUTA BHANGI, UNAJIUZA NA KULA UNGA. Hufikirii kwanza unahitaji kubadilika wewe kwanza.

Angalia kwenye familia yako ni nini hakiko sawa? Angalia mahusiano yako na majirani zako badilisha huko kwanza. Alafu iambie serikali wewe serikali hufanyi kazi sawa sawa.

Katika nchi yeyote raia wana haki na wajibu. Unapaswa kutimiza wajibu wako kwanza kabla ya kudai haki. Lazima kuwe na balance ya vitu hivi viwili.

Kama tunataka kubadili taifa hili kwanza tuanze ngazi ya mtu binafsi tubadilike.

Swali la kujiuliza tunalalamika kila siku kuhusu ufisadi lakini ufisadi unaanza katika ngazi ya tabia ya mtu binafsi na mahusiano yake na wengine. Uchoyo, ubinafsi na kujiangalia mwenyewe badala ya jamii na taifa. 

Kwahiyo kama tunataka mabadiliko hii isiwe katika serikali peke yake lakini ziwe ni harakati za kubadili mtazamo wa jamii nzima. Na kujenga upya mahusiano yetu kama taifa.

There will be no significant change kama watu wenyewe kwa ujumla wake kama hawatobadilika na kama hawatojaliana kama watu wa taifa moja.
 • Imeandikwa na ShaYu

Kichupa kipya: Joh Makini ft AKA - Don't bother


Orodha ya WanaCCM waliochukua fomu za kuwania Uspika wa Bunge JMT 2015

Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini Ndugu Daniel Nswanzungwanko akionesha fomu ya kuwania uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano mara baada ya kuzichukua katika ofisi ya Oganaizesheni CCM Lumumba leo Ijumaa, Novemba 13, 2015
Idadi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaoomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Uspika na Unaibu Spika katika Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) linalotarajiwa kuanza wiki ijayo, inazidi kuongezeka na hapa ni majina 21 ya ambao wameshachukua fomu hizo, kadiri ya taarifa ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib.
 1. Aliyekuwa Naibu Spika katika Bunge la 10 na Mbunge mteule wa Kongwa, Job Ndugai
 2. Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Tulia Arkson 
 3. Aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi
 4. Aliyewahi kuwa Spika na Waziri, Samuel Sitta
 5. Mbunge mteule wa Chato, Dk Medard Kalemani
 6. Diwani wa Goba jijini Dar es Salaam, Mwakalika Watson
 7. Julius Pawatila
 8. Agnes Makune
 9. Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Abdullah Ali Hassan Mwinyi
 10. Naibu Waziri, Ritha Mlaki 
 11. Mhitimu wa chuo kikuu mwenye umri wa miaka 28, Veraikunda Urio
 12. Aliyekuwa Mbunge wa Karagwe, Gosbert Blandes 
 13. Aliywania nafasi ya Urais wa JMT kupitia CCM, Dk Kalokola Muzzamil.
 14. Mbunge wa Songea Mjini, Dk Emmanuel Nchimbi
 15. Aliyewahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge Philip Marmo
 16. Balozi wa zamani wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu
 17. Mbunge wa zamani wa Afrika Mashariki, George Nangale
 18. Simon Rubugu
 19. Banda Sonoko
 20. Leonce Mulenda
 21. Mbunge mteule wa Kasulu Mjini Daniel Nswanzungwanko
 22. Mbunge mteule wa Ilala Mussa Hassan Zungu

TANESCO nguzo yenu na transfoma hii... hatari!


Upepo mkali uliotokea maeneo ya mji wa Kilosa ukiwa umeharibu nguzo ya umeme uliosambazwa eneo la mradi wa makazi mapya, kama ilivyokutwa jana eneo hilo na mpiga picha, John Nditi (via Lukwangule Ent. blog)

Bi Makinda atangaza kung'atuka uongozi wa kisiasa na kumwosia atakayemrithi

Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam kuhusiana na kuachana na uongozi katika siasa
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania anayemaliza rasmi muda wake, Anne Makinda amejing'atua rasmi na kuachana na uongozi katika siasa kutokana na kufanya kazi za siasa kwa miaka 40.

Makinda amenukuliwa kuyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam leo kwa kusema, "Sitagombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wala sitachukua fomu ya kugombea nafasi ya Uspika wala sifikirii kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Uspika."

Aidha amesema kuwa katika awamu yake ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kulikuwa na changamoto nyingi kutokana na kuwepo na wabunge vijana.

Hata hivyo kuwa na changamoto nyingi ila amesema kuwa alilifurahia sana Bunge hilo kutokana na kuwaelewa wabunge mbalimbali tabia zao hasa wakiwa Bungeni.

Makinda amesema kuwa Spika atakayeshinda nafasi asiwe mwepesi wa kukasirika kutokana na changamoto atakazozipata Bungeni wakati wakijadilia masuala mbalimbali ya Serikali, bali awe mtulivu na akabiliane na changamoto zitakazojitokeza.

Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kuzungumza nao leo katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.
 • Avila Kakingo via Globu ya Jamii

Habari 2 za gazeti la Jamvi la Habari: Kashfa sukari ni zaidi ya escrow; Moshi mweusi CHADEMA


Watumishi 4 wa Halmashaori ya Wilaya Hai wasimamishwa kaz

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Anthony Mtaka akisalimiana na wananchi alipofanya ziara katika hosptali teule ya Machame na kuzungumza na wafanyakazi 
Na Dixon Busagaga

HALMASHAURI ya wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, imewasimamisha kazi watumishi wake wanne kwa tuhuma za kughushi hati za mishahara na kughushi nyaraka zilizofanikisha kuchukua jumla ya kiasi cha sh mil 73.4/= zikiwemo fedha za malipo ya muda wa kazi wa ziada kwa madaktari na wauguzi wa hospitali teule ya Machame.

Tuhuma hizo pia zina mtaja Mweka Hazina wa hosptali hiyo anayedaiwa kushirikiana na watumishi wa halmashauri hiyo kufanya ubadhirifu wa fedha na kwamba tayari uongozi wa hosptali hiyo iliyo chini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Kaskazini, umekwisha mfukuza kazi.

Watumishi wawili kati ya wanne wamesimamishwa kazi kutokana na tuhuma mbili tofauti, moja ikiwa ni kughushi hati za mishahara, vitambulisho na sahihi za watumishi waliostaafu na wengine kuacha kazi na kuchukua mikopo wa sh mil 35/= katika benki ya CRDB kwa majina ya watumishi walioacha kazi.
Mkuu wa wilaya ya Hai, Anthony Mtaka akizungumza na wafanyakazi wa Hosptali teule ya Machame (hawapo pichani) .

Baadhi ya iongozi wa Hosptali hiyo na viongozi wa serikali wa wilaya ya Hai.


Wafanyakazi wa Hosptali teule ya Machame. 


Mkurugenzi wa Hosptali hiyo,Dkt Saitore Laizer akizungumza katika kikao hicho.


Baadhi ya madktari wa hosptali teule ya Machame.

Baadhi ya watumishi wa Hosptali hiyo.

Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi katika hosptali ya Machame, Dkt Fredrick Muro akizungumza katika kikao hicho.

Baadhi ya wafanyakazi.

Mkuu wa wilaya akiondoka katika hosptali hyo mara baada ya kumalizika kwa kikao na watumishi .Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Thailand wachagua uongozi wao

Meza Kuu: Kutoka Kushoto ni Ndugu Maumba Mgaya, Mwenyekiti wa Jumuiya, Bi Magreth Mjindo na Ndugu Andrew Katibu.
Mnano tarehe 7/11/2015, Jumuiya ya watanzania waishio nchini Thailand ilikutana na kujadiliana mambo mbalimbali ya jinsi gani wanaweza kusaidiana katika mambo mbalimbali, TIT ilianzishwa mnano mwezi wa nne mwaka, 2015 na inahusisha watanzania mbalimbali, wanafunzi,wafanyabishara na wafanyakazi waishio na kufanya nchini Thailand. Mkutano mkuu wa Jumuiya ulifanyika katika Hoteli ya Amari Boulevard Mjini Bangkok na kuhudhuriwa na wanajumiya mbalimbali.

Pamoja na kujadiliana mambo mbalimbali kulifanyika uchaguzi wa viongozi ambapo wafuatao walichaguliwa kuwa viongozi wa jumuiya kwa kipindi cha mwaka mmoja:
 • Mwenyekiti: Bwana Maumba Mgaya
 • M/Kiti: Bw. Alois Ngonyani
 • Katibu: Bw.Andrew Wajama
 • Katibu Msaidizi: Bw. Emmanuel Mushi
 • Mhazini: Bw. Adolf Kigombola
 • Mhazini Msaidizi: Bi.Tumaini Kalindile
 • Afisa Mawasiliano: Bw. Emmanuel Nyamageni
 • Afisa Mawasiliano Msaidizi: Bw. Jordan Hossea.
Pamoja na uchaguzi kulifanyika sherehe fupi ya kumpongeza Bi Magreth Dionis Mjindo ambaye amemaliza Shahada ya uzamili ya maendeleo ya jamii na anarejea nyumbani kulitumikia Taifa.

Jumuiya inapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wadhamini wao Ndugu Florean Rwehumbiza, Dada Lucy Kileo pamoja na Ndugu Kivea Mbwana (Homeboy) kwa kusimamia uchaguzi na kufanikisha kufanyika kwa mkutano huu muhimu. Shukrani za pekee ziende kwa Kampuni ya Broadhurst Pacific, kwa kusimamia, kudhamini na kufanikisha tukio hili muhimu.

Tunapenda kuwapongeza na kuwashukuru viongozi waasisi wa jumuiya waliomaliza muda wao ambao ni ndugu Saidi Husein Kitenge Mwenyekiti wa kwanza wa jumuiya na makamu wake Ndugu Masui Vicent Munda na ndugu Antidius Muchunguzi bila kuwasahau maafisa mawasiliano wetu akiwemo ndugu Felix Mwema na Bi Diana Richard.Mungu awabariki kwa kuitumikia vema TIT.

Aidha Jumuiya inawakaribisha watanzania mbalimbali walioko nchini Thailand au wanaotarajia kuja nchini Thailand kushirikiana na jumuiya yetu.

Umoja ni nguvu

Imetolewa na Jumuiya ya Watanzania waishio nchini Thailand (TIT)

+66947230002/+66972494819


Mhazini wa Jumuiya ndugu Adolph Kigombola akisoma taarifa ya fedha.


Mkutano Mkuu ukiendelea.


Baadhi ya Watanzania waishio nchini Thailand.


Mkutanoni.


Timu ya wadhamini wakisimamia uchaguzi.


Bw. Florean akikabidhiwa keki ya kuzaliwa na Bi Lucy.


Ndugu Florean akimkabidhi Bi Magreth zawadi kwa niaba ya Jumuiya.


Wanajumuiya Wakipata Chakula cha Pamoja.


Watanzania waishio Thailand wakipata chakula cha pamoja.


Watanzania Waishio Thailand wakiwa katika picha ya pamoja.