Uongozi mpya wa Tanzania Agricultural Organisation

Moja ya vyama muhimu katika kuleta mapinduzi ya Kilimo Nchini Tanzania ni Tanzania Agricultural Organisation (TASO). 

Pamoja na majukumu mengine, TASO ndiyo wamiliki na wasimamiaji wamaonyesho ya "nane nane" nchini Tanzania. 

Hadi sasa TASO ina viwanja vitano vya maonyesho ya nanenane kwenye kanda ya Kaskazini-Arusha, kati –Dodoma, mashariki – Morogoro, nyanda za juu – Mbeya na kusini – Lindi. Mfumo wa utendaji wa TASO umeanzia kwenye Kata, Wilaya, Mkoa, Kanda naTaifa.

Juhudi zinafanyika kuanzisha viwanja vya maonyesho kwenye kanda ya Magharibi na kanda ya ziwa katika muda mfupi ujao. Tanzania ikiwa inatumia si zaidi ya asilia 25% ya Aridhi inayofaa kulimwa, Kilimo kinabakia kuwa msingi muhimu wa kukuza uchumi na ajira Nchini Tanzania. Pia izingatiwe kuwa Tanzania ina jumla asilimia 46% ya aridhi yote ya Afrika Mashariki hivyo kuwa na fursa kubwa ya kukuza soko na kulisha nchin yingine za Afrika Mashariki na nje.

Jumamosi yaTarehe 14 Novemba 2015 mjini Dodoma, TASO ilifanya uchaguzi wa viongozi wa Taifa ambao wataongoza taasisi hii muhimu katika kukuza kilimo kwa miaka 5. Viongozi waliochaguliwa ni Engelbert Moyo – Mwenyekiti, SharifaAbebe – Makamu Mwenyekiti, Imani Kajula – Katibu Mkuu, Daudi Mwalusyamba – Katibu Mkuu Msaidizi na Michael Lupyana – Mweka Hazina.

Akizungumza baada ya kuchaguliw aMwenyekiti wa TASO Taifa Engelbert Moyo alisema ‘Huu ni mwanzo mpya wenye malengo ya kuchochea mchango wa kilimo katika uchumi, maisha ya Watanzania, weledi katika kilimo na ajira. Ni fursa adhimu kuwa na viongozi wa Taifa wenye ujuzi katika fani mbalimbali - kilimo, biashara, masoko na fedha. Naamini kuwa TASO itapiga hatua kubwa katika kuwa muda muhimu katika kutoa mchango katika sekta hii nyeti.’


Naye Katibu Mkuu wa TASO, Imani Kajula alisema ‘Kilimo ni sekta yenye kuajiri watanzania wengi, lakini imekuwa na changamoto nyingi, tunatambua kazi hii tuliyopewa ni adhimu na muhimu katika kuleta mabadiliko ya kukuza soko la mazao, ubunifu watechnojia rahisi za kilimo, upatikanaji wa habari za kilimo, uvuvi, ufugaji na masoko kwa wakulima na pia kuboresha maonesho ya nanenane kuwa jukwaa la kuchochea ukuaji wa kilimo na ajira’.

Salam za Malkia wa Uingereza, Elizabeth II kumpongeza Rais Magufuli

     RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amepokea salamu za pongezi kutoka kwa Malkia Elizabeth II wa Uingereza kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

     Katika salamu hizo Malkia wa Uingereza amemueleza Mhe. Rais Dkt. Magufuli kuwa  “Natumaini kuwa mahusiano baina ya nchi hizi mbili ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola yataendelea wakati wa utawala wako, nakutakia kheri pamoja na wananchi wa Tanzania”  amesema malkia katika salamu zake.

     Salamu pia zimetoka kwa Mfalme Akihito wa Japan ambaye amemueleza Mhe.  Rais Dkt. Magufuli “Nakutumia salamu za dhati,  mafanikio na furaha kwako Mheshimiwa Rais na watu wa nchi yako” Amesema.

     Salamu zingine kwa Mhe. Rais Dkt. Magufuli zimetoka kwa Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kiarabu  ya Saharawi, Mhe. Mohamed Abdelaziz ambaye amemtakia kheri  Mhe. Rais Dkt. Magufuli na kumueleza kuwa “Nina  imani kuwa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea vyema chini ya uongozi wako kuelekea katika kupata maendeleo  na mafanikio zaidi”.

  Amesema; na pia amekipongeza Chama Cha Mapinduzi na Watanzania kwa uchaguzi wa kidemokrasia ulioendeshwa katika mazingira ya kistaarabu chini ya usimamizi wa waangalizi kutoka kwenye kanda, bara na kimataifa na hivyo kuliletea sifa bara la Afrika.

     Mhe. Rais Dkt. Magufuli pia amepokea salamu kutoka kwa Rais wa Namibia Mhe. Hage Geingob na kumueleza Mhe. Rais Dkt. Magufuli kuwa salamu zake na zile za wananchi wa Namibia ni za dhati kwa Serikali na Watanzania kwa ujumla kwa ushindi wa kiti cha Urais.

     “Pia napenda kutoa pongezi kwa Chama Cha Mapinduzi kwa ushindi uliopatikana katika uchaguzi wa Oktoba 25, 2015”. Amesema na kuongeza kuwa  “Kwa hakika Watanzania wamezungumza na kukipa tena CCM  Mamlaka ya kuipeleka mbele Tanzania  kuelekea kwenye mafanikio zaidi”.  Ameongeza.

      Salamu zingine ni kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye amesema Tanzania kwa mara nyingine tena imedhihirisha kuwa ni nguzo ya demokrasia barani Afrika.

     Naye Rais wa Jamhuri  ya Shirikisho la Ujerumani, Joachim Gauck amemtakia Mhe. Rais Dkt. Magufuli na Watanzania kwa ujumla mafanikio  katika kuendeleza Taifa kwa ujumla.

Imetolewa na:
Premi Kibanga, 
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
16 Novemba, 2015.

Watano wakutwa hai mgodini Kahama baada ya kufukiwa na kifusi siku 41 zilizopitaKatika hali isiyokuwa ya kawaida watu 5 kati ya 6 waliyokuwa wamefunikwa na kifusi kwa siku 41 (tangu Oktoba 5, 2015) katika machimbo madogo ya mgodi wa Nyangalata wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameokolewa wakiwa hai umbali wa meta 100 baada ya ardhi. 

Wakizungumza leo na Kahama FM wakati wakiwa wamelazwa katika hospitali ya mji wa Kahama, wahanga hao wamesema hali hiyo iliwakuta katika harakati za kuwaokoa wenzao waliokuwa wamefukiwa na kifusi katika machimbo hayo. 

Wahanga hao ambao wametambuliwa kwa majina na umri ni Onyiwa Kanyimbo(55), Msafiri Gerald (38), Amos Muhangwa (25), Chacha Wambura (53) na Joseph Burule (44). Aliyefariki dunia ni Mussa Supana ambaye aliaga dunia siku 15 zilizopita na mwili wake bado unatafutwa. 

Wamesema walikuwa wakiishi kwa kunywa maji waliyoyakinga kwenye helmet zao na kula magome ya miti pamoja na mende hali iliyowasababisha kuendelea kuwa hai kwa siku 41 hadi jana jioni walipookolewa. 

Meneja wa mgodi mdogo huo Amos Mbanga amesema timu ya mafundi ilifanya utafiti na kugundua kuna sauti za watu zikiita na kuamua kupeleka uokawaji kwa kushirikiana na serikali pamoja kampuni ACACIA na kufanya uokoaji huo uliochukua saa 24. 

Afisa habari wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Massoud akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa mgodi huo ulianza kudidimia kwenda chini, Oktoba 5 mwaka huu mpaka Novemba 15 ambapo waokoaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini walifanya juhudi za kuwatafuta hadi jana walipofanikiwa kuwatoa wakiwa katika hali mbaya na kuwakimbiza hospitalini.

Naye Kaimu Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Kahama Dk. Jibai Mkama amethibitisha kuwapokea wahanga hao na kusema kwa sasa hali zao zinaendelea vizuri wakiwa bado wanapatiwa matibabu katika hosspitali hiyo.

Wizara inatoa ruzuku na mikopo kwa wachimbaji wadogo wadodo ili wafanye shughuli zao kwa usalama, hivyo wito umetokewa kwa wadau kutumia nyenzo za kisasa na kuwa makini katika shughuli za uchimbaji.

Mmoja wa wahanga hao akiwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama 


Afisa habari wa Wizara ya nishati na Madini, Badra Massoud akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO kuhusiana na watu waliopatikana wakiwa hai katika mgodi wa wachimbaji wadogo wa Nyangarata mkoanI Kahama.

Bunge la XI kuanza kesho: Spika, Naibu, Waziri Mkuu kujulikana

Bunge la Kumi na Moja la Serikali mpya ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia chini ya rais Dk Johon Magufuli limepangwa kuanza rasmi kesho mjini Ddodoma baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu nchi nzima uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

SPIKA

Bunge hilo linaloanza kesho linatarajiwa kuwa na matukio kadhaa ikiwemo upatikanaji wa Spika na Naibu wake lakini pia linatarajiwa kuthibirtisha jina la Waziri Mkuu wa Tanzania kama litakavyowasilishwa na rais Dakta John Magufuli

Huko mjini Dodoma mchakato wa kumpata Spika kwa upande wa chama tawala (CCM) ambacho ndicho chenye wabunge wengi umekuwa ukiendelea kupitia vikao mbalimbali vya chama hicho ambapo kati ya wanachama wake 22 walioomba nafasi hiyo, ni Job Ndugai aliyeteuliwa.

Ndugai ambaye alikuwa Naibu Spika katika Bunge la X ameelezea matumaini yake ya kuongoza bunge la XI kwa kuwa CCM yenye wabunge wengi inatarajia kushinda uchaguzi huo dhidi ya vyama vingine vya upinznai vitakavyosimamisha wagombea

RATIBA

Inaonesha kuwa kesho Jumanne baada ya kufunguliwa kwa kikao cha kwanza cha Bunge inaonesha kuwa kutasomwa tangazo la Rais la kuitisha Bunge, kufanyika kwa uchaguzi wa Spika na kuapishwa na baada ya tukio hilo wabunge wataanza kuapishwa shughuli itakayoenda hadi siku ya Alhamis asubuhi, na baadaye Alhamis jioni wabunge watalithibitisha jina la Waziri Mkuu, kabla ya rais Mpya hajalihutubia siku ya Ijumaa majira ya Alasiri.

Taarifa: Rais Magufuli amteua Dk Mwansasu kuwa Mbunge

Dk Tulia Ackson Mwansasu
Dk Tulia Ackson Mwansasu

Wanaotajwa kupitishwa kuwania Uspika wa Bunge JMT 2015

Mbunge wa Jimbo la Kongwa Ndugu Job Ndugai akiongea na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa NEC baada ya jina lake kupitishwa na wabunge wa CCM (picha)
Kamati ya Wabunge wote wa Chama cha Mapinduzi kwa kauli moja wamepitisha jina la mbunge wa Kongwa mkoani Dodoma Mhe. Job Ndugai kugombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma mapemalLeo.

Wagombea wengine wawili waliokuwa wamepitishwa na CCM jana, Mhe Abdullah Ali Mwinyi na Dk Tulia Ackson Mwansasu walijitoa, hivyo kupisha nafasi hiyo kwenda kwa Ndugai.

Dkt.Tulia amepisha nafasi hiyo baada ya kupokea Uteuzi kutoka kwa Rais Dk. Magufuli kwa kuteuliwa kuwa Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katibu wa Itikadi na Uenezi, CCM-Taifa, ambaye ni Mbunge mteule wa Mtama, Nape Nauye amesema kukamilika kwa uteuzi huo kunatoa nafasi kwa wabunge wote wa CCM kumfanyia kampeni Ndugai ili aweze kuchaguliwa na Wabunge wote katika mkutano wa Bunge la XI linalotarajiwa kuanza hapo kesho mjini Dodoma.

Wengine ambao inatajwa kuwa wameteuliwa na vyama vyao (katika mabano) kuwania kiti hicho ni pamoja na:-
  1. Peter Lenoard Sarungi (AFP)
  2. Hassan Kisabiya Almasi (NRA)
  3. Dkt Godfrey Raphael Malisa(CCK)
  4. Goodluck Joseph Ole Medeye (CHADEMA)
  5. Richard Shadrack Lyimo (TLP)
  6. Hashimu Spunda Rungwe(CHAUMA)
  7. Robert Alexander Kisinini (DP)


Ombi kwenu waja wema: Sh milioni 3 zinahitajika kwa tiba ya dada Mwambepo

Ndugu Wasamaria wema

Napenda kutumia fursa hii kukushirikisha habari ya kusikitisha kuhusu dada Joyce Mwambepo (pichani akiwa na mwanaye, na migu yake iliyopooza) mkaazi wa Sinde jijini Mbeya. Dada huyu mwenye umri wa miaka 27 anaishi na bibi yake mwenye umri wa miaka 80 pamoja na mwanaye mwenye umri wa miaka 4.

Kwa bahati mbaya mwezi April mwaka jana dada huyu alipata ajali ya kugongwa na gari ambayo haikusimama kumsaidia. Ila kwa msaada wa wasamaria wema alipelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya ambako inasemekana alikaa kwa miezi mitatu bila kupata matibabu.

Katika uchunguzi wa awali ilibainika kuwa Joyce amevunjika miguu yote miwili, hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako pia baada ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa Mbeya baada ya kukosa shilingi 550,000/- za vipimo na matibabu.

Hadi nakutana naye dada huyu alikuwa amelala nyumbani kwa bibi yake (pichani kushoto) ambaye ni mlezi wake tangu akiwa na miaka minne baada ya wazazi wote wawili kufariki dunia.

Hawezi kukaa wala kusimama na anajisaidia hapo hapo kitandani kwa msaada wa mwanaye na bibi yake. Inasikitisha.

Hivyo nimejitahidi kufuatialia ili kujua mahitaji halisi lakini sikufanikiwa kumpata daktari bingwa wa mifupa . Ili kumsaidia Joyce inatakiwa aanze process upya za matibabu kuanzia hapa Mbeya referral Hospital hadi Muhimbili jijini Dar es salaam.

Gharama za matibabu ni kama ifuatavyo:

1. shilingi 300,000/- za kupima CT-SCAN

2. Shilingi 250,000/- za MRI

3. Usafiri wa kutoka Mbeya-Dar kwa gari maalum la kukodi 700,000/-

4. Gharama za msaidizi ambaye ni rafiki yake 300,000/-

5. Chakula 450,000/- (Endapo watakaa hospitali mwezi mzima)

6. Gharama za matibabu (CT-SCAN&MRI ni vipimo tu) 500,000/-

7. Na mahitaji mengineyo wakiendelea kupata tiba 500,000/-

Hivyo kwa kuanzia kiasi cha shilingi 3,000,000/- (milioni tatu) kinahitajika kumpunguzia mateso dada yetu huyu. Asante sana kwa moyo wako wa kujitoa na Mungu atakubariki.

Deo Kakuru Msimu

Msamaria mwema

+255769 512 420

Wakati huo huo kwa niaba ya Michuzi Media Group, Ankal amejitolea kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce. Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email [email protected] ama whatsapp namba +255 754 271266 kwa jina la Ankal.Makala akagua hospital ya Rufaa ya Mawenzi
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Amos Makala akisalimiana na wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kutembelea idara mbalimbali hospitalini hapo.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amos Makala akitia saini katika kitabu cha wageni maara baada ya kuwasili katika hosptali ya Rufaa ya Mawenzi mkaoni Kilimanjaro.
Mganga mkuu wa mkoa wa Kilimajaro Hajati, Dkt Mtumwa Mwako akifanya utambulisho wa watumishi wa hosptali hiyo katika ukumbi mdogo wa mikutano hospitalini hapo.

Baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi ya mkoani Kilimanjaro.

Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Novatus Makunga akizungumza jambo katika kikao cha mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makala na watumishi wa Hopstali ya rufaa ya Mawenzi.

Mganga mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya Mawenzi Dkt, Bingileki Rwezaula (kushoto) akiwa na watumsihi wengine wa hospitali hiyo.


Katibu wa Hosptali ya Rufaa ya Mawenzi, Boniface Lyimo akisoma taarifa ya hospitali hiyo kwa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Amos Makala (hayupo pichani)

Baadhi ya wakuu wa vitengo mbalimbali katika hospitali ya Rufaa ya Mawenzi ,mkoani Kilimanjaro.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjar, Amos Makala akizungumza na watumishi wa Hopstali ya Rufaa ya Mawenzi mara baada ya kutembelea hosptali hiyo.

Badhi ya watumishi katika hospitali hiyo.RC Makala akizunguza na watumishi.

RC Makala akizungumza na mmoja wa wzee waliofikisha wagonjwa wao katika hospitali ya Mawenzi.

RC Makala akizungumza na mmoja wa wauguzi katika hospitali hiyo,kushoto ni mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Hajati, Dkt Mtumwa Mwako.

RC Makala akiwajulia hali wagonjwa waliofika katika hospitali hiyo kujipatia huduma ya matibabu.


Mganga Mfawidhi wa Hopstali ya Rufaa ya Mawenzi,Dkt Bingilaki Rwezaula akimuelekeza maeneo mbalimbali mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Amos Makala alipotembelea hospitalini hapo.

RC Makala akizungumza na mmoja wa wazee waliofika katika hospitali hiyo kupata matibabu.

RC Makala akitizama hali ya wagonjwa katika hospitali ya rufaa ya Mawenzi.

RC Makala akitembelea kitengo kinachoshughulika na bima ya afya.

RC Makala akizungumza jambo na mkuu wa idara ya Bima, Dkt Saganda katika hospitali hiyo.

RC Makala akizungumza na mmoja wa wagonjwa waliopo katika hospitali hiyo.

Wodi ya kina mama.

RC Makala akisalimiana na mmoja wa wauguzi wa zamu katika hospitali hiyo.

RC Makala akizungumza na mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika wodi ya kina baba.

RC Makala akizungumza na madkarai wa zamu katika hospitali ya Mawenzi.


RC Makala akimsikiliza mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika wodi ya Majeruhi katika hospitai hiyo.

RC Makala akitoa maelekezo kwa mkuu wa wilaya ya Moshi,Makunga baada ya kupata maelezo toka kwa mmoja wa wagonjwa katika hospitali hiyo namna alivyojeruhiwa.

RC Makala akitoka katika wodi ya wagonjwa wa akili hosptalini hapo.


RC Makala akiwa katika wodi ya watoto katika hospitali ya Mawenzi.RC Makala akitembelea jengo jipya la wodi ya wazazi linalojengwa katika hospitali hiyo.


RC Makala akiondoka katika hospitali ya rufaa ya Mawenzi mara baada ya kutembelea idara mbalimbali hospitalini hapo kujionea namna huduma zinavyotolewa.
  • Dixon Busagaga