Lowassa awakagua waliookolewa mgodini baada ya siku 41Mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA Edward Lowassa leo ametoa shilingi milioni mbili kwa wahanga waliookolewa katika mgodi wa Nyangalata wanaopatiwa matibabu katika hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga.

Majaaliwa ya Mungu: Nisaidie yasinikute ya Awamu ya IV


Tunaanza kuwapima wanafunzi kwa mtihani wa darasa la pili - NECTA


BARAZA la Taifa la Mitihani (NECTA) limesema ili kutekeleza sera ya elimu ya mwaka 2014, watoto wataanza kukariri darasa kuanzia wakiwa darasa la pili.

Alisema hatua hiyo itachukuliwa endapo watashindwa mtihani wa kujipima ambao utaanza rasmi mwakani kwa wanafunzi wa ngazi hiyo ya elimu.

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipozungumza na gazeti hili.

Alisema kufanyika kwa mitihani hiyo kunakwenda sambamba na kuipa hadhi mitihani ya kupima wanafunzi katikati ya masomo ya darasa la nne na kidato cha pili ambayo kwa sasa itakuwa chini ya baraza hilo tofauti na ilivyokuwa awali.

Dk. Msonde alisema kwa upande wa mitihani ya darasa la pili, matokeo ya mitihani hiyo itasaidia kuwatenga wanafunzi hao kwenye makundi matatu ambayo walimu watatakiwa kuyafanyia kazi kuhakikisha watoto hao wakiendelea na madarasa ya juu watafanya vizuri.

Alisema kwa kuwaandaa watoto kwa mitihani hiyo, anaamini mpaka wakiwa wanamaliza darasa la saba hakuna ambaye atakuwa hajapata stadi za kusoma na kuandika kama ilivyo kwa sasa ambako baadhi uhitimu elimu ya msingi wakiwa hawajui kusoma na kuandika.

“Kwa kuanza kuwapima wakiwa darasa la pili watakuwa wanaangalia kwenye stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu huku mitihani mingine kama ile ya darasa la nne ikipandishwa hadhi na kuwa chini ya baraza.

“Tunaamini suala la watoo kumaliza darasa la saba baadhi wakiwa hawajui kusoma na kuandika litaisha,” alisema.

Alisema mipango ya sera hiyo ikikamilika, mtihani wa darasa la saba ambao hivi sasa ni wa kuhitimu elimu ya msingi, utakuwa wa kupima kama ulivyo ule wa darasa la nne kwa sababu elimu ya msingi mwisho itakuwa kidato cha nne.

“Siwezi kusema ni lini hili litaanza kwa sababu utekelezaji wa sera ni mchakato, lazima kwanza madarasa ya sekondari yaongezwe.

“Mitaala ibadilike kama hivi sasa ambavyo ya darasa la kwanza na la pili imebadilika na ndiyo kwanza tunaanza kuwapima wanafunzi kwa mtihani huo wa darasa la pili.

“Faida nyingine ya mtihani huo na ule wa darasa la nne ni kuhakikisha mpaka mtoto anafika darasa la saba, wale watakaopata alama 100 chini ya 250 ambao kwa sasa ndiyo ufaulu wawe wameongezeka,” alisema Dk. Msonde.

Alisema ili kuona namna bora ya kuanza kufanya mtihani huo mwakani, leo watoto wa darasa la pili kutoka shule 66 zilizo kwenye mikoa 11 watafanya mtihani huo ikiwa ni sehemu ya majaribio.

Alisema kwenye mikoa hiyo zimechaguliwa wilaya ambazo zimetoa shule moja ya kijijini, moja ya mjini na nyingine ya mchepuo wa Kiingereza.

Mahakama yaridhia: Mattaka na wenzake wana kesi ya kujibu kuhusu ATCL

David Mattaka
David Mattaka
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imesema aliyekuwa Mkurugenzi wa zamani wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka na wenzake, wana kesi ya kujibu.

Mattaka na wenzake wanakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kutangaza zabuni ya ununuzi wa magari 26 yaliyochakaa na kuisababishia Serikali hasara ya Dola 143,442.75 za Marekani.

Aidha, mahakama hiyo imesema kesi hiyo itaanza kusikiliza ushahidi wa upande wa utetezi Desemba 10 na 11, mwaka huu.

Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Emmilius Mchauru, baada ya kusikiliza mashahidi 13 wa upande wa Jamhuri dhidi ya washtakiwa.

Alisema washtakiwa hao wana haki ya kujitetea kupitia njia tatu.

“Washtakiwa mnaweza kuamua kujitetea kwa njia ya kiapo, bila kiapo ama kukaa kimya kuiachia mahakama kutoa hukumu,” alisema Hakimu Mchauru wakati akisoma uamuzi huo.

Hata hivyo, washtakiwa hao kwa nyakati tofauti walidai watajitetea kwa njia ya kiapo.

Upande wa utetezi ukiongozwa na Peter Swai na Alex Mgongolwa, ulidai kuwa katika ushahidi wao wa utetezi, wanatarajia kuita mashahidi saba wakiwamo washtakiwa.

Mbali na Mattaka, washtakiwa wengine ni Kaimu Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha, Elisaph Ikomba na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Ndani, William Haji, wa shirika hilo.

Katika kesi hiyo ya matumizi mabaya ya madaraka, Mattaka na wenzake Elisaph Ikomba na William Haji wanadaiwa pamoja na mambo mengine, wakiwa waajiriwa wa ATCL na wenzao ambao hawajulikani kati ya Machi na Julai, mwaka 2007, walikula njama ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Dola 143,442.75 za Marekani.

Maelezo ya Mtatiro kuhusu kesi ya kupinga ushindi wa CCM Segerea

TAARIFA MAALUM,

"HATUTAFUNGUA KESI KUPINGA USHINDI WA CCM HAPA SEGEREA"


Napenda kutoa taarifa hii rasmi na ya awali kwa wananchi wa Segerea na watanzania wote ambao walipigana kufa na kupona ili kuhakikisha UKAWA tunashinda madiwani, mbunge na kuongoza kura za Rais hapa jimboni. Kwa bahati mbaya tulifanikiwa kushinda madiwani wote, kuongoza kura za Rais lakini tukashindwa kwenye Ubunge.

Baada ya jimbo letu kwenda CCM nilishauriwa nisisaini kukubali matokeo na nikatekeleza ushauri huo, lengo lilikuwa ni kuwapa muda wanasheria wetu na mawakili waweze kushauri ikiwa kuna kesi ya kufungua kupinga ushindi wa CCM.

Baada ya mashauriano ya wiki kadhaa yaliyohusisha mawakili na wataalam wa sheria wa ngazi mbalimbali, tumejiridhisha na kushauriwa kwamba hatutakuwa na kesi ya kufungua, na kwamba tukiifungua kwa kulazimisha au "kwa kusukumwa na upepo wa wananchi" tutashindwa mahakamani mapema.

Wanasiasa wengi hukimbilia mahakamani wanaposhindwa uchaguzi si kwa sababu wana kesi zenye ushahidi wenye mashiko, bali huogopa maneno na tuhuma wanazoweza kupewa kuwa "wamenunuliwa na wagombea wa CCM", mimi kwa bahati nzuri sijakumbwa na upepo huo na natambua wananchi wa Segerea wananiamini kiasi cha kutosha.

Baada ya wiki moja kutoka sasa, ntatoa taarifa rasmi na ya kina juu ya hoja na sababu zilizopelekea wanasheria na mawakili wetu washauri tusihangaike kufungua kesi na kupoteza muda wa matumaini ya wananchi.

Mtatiro Julius,
Segerea.
(via Facebook)

Maandamano ya Wazanzibari hadi Ikulu nchini Marekani


Maelezo Mbunge wa Singida ya kukataa posho na maelekezo ya pa kuipelekaAgizo la Rais Magufuli kuhusu sherehe za maadhimisho ya uhuru wa taifa

Kwa mujibu wa Sheria ya Sikukuu za Kitaifa (The Public Holidays Act, Cap 35) pamoja na Sheria zingine zinazompa mamlaka Rais kutangaza siku yoyote kuwa sikukuu au mapumziko, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameamua kuwa maadhimisho ya Sherehe za Uhuru na Jamhuri zitakazofanyika tarehe 9 Desemba, 2015, yatumike kwa kufanya kazi.

Kwamba maadhimisho ya Uhuru ya mwaka huu (2015) yatatumika kama kichocheo cha kujenga tabia ya kufanya kazi (Uhuru na Kazi) katika Taifa letu. Mheshimiwa Rais ameelekeza Watanzania wote siku hiyo waitumie kwa kufanya kazi mbalimbali kama vile, mashambani, maofisini, sokoni, viwandani na usafi wa miji yao katika kutimiza dhana ya Uhuru na Kazi kwa vitendo.

Aidha, kwa kuwa Sherehe za Uhuru na Jamhuri huendana na Maandalizi mbalimbali ambayo yanatumia fedha, kwa kuzingatia kuwa siku hiyo itaadhimishwa kwa kufanya kazi, fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe hiyo sasa zitumike kwa shughuli zingine za kijamii ikiwa ni pamoja na kupambana na maradhi hasa kipindupindu, kununulia dawa za hospitali, vitanda vya hospitali n.k. kadri kamati za maandalizi zitakavyoamua.

Ieleweke kuwa sherehe za Uhuru na Jamhuri ni muhimu katika kuadhimisha kumbukumbu ya uhuru wa nchi yetu. Hivyo, sherehe hizi zitaendelea kuadhimishwa kila mwaka kama kawaida kuanzia mwaka 2016.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Waziri Mkuu aanza kwa kutaka mpango-kazi kutoka kila idara

Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakipokea shada la maua kutoka kwa Immaculata Warqaso wa Ofisi ya Waziri baada ya kuwasili kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam leo Novemba 22, 2015 wakitoka Dodoma kwa gari.Wapili kulia ni Katibu Mkuuwa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt Florens Turuka. (Picha: Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amewataka wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu watambue jukumu walilonalo la kuwahudumia wananchi kutokana na majukumu ya ofisi hiyo ambayo yanagusa maisha ya kila siku ya Watanzania.

“Ofisi ya Waziri Mkuu ni kubwa na pana sana na inahusika na shughuli za kila siku za Watanzania. Kwa hiyo tuna kazi kubwa ya kukidhi matarajio yao,” alisema.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Novemba 23, 2015) wakati akizungumza na wakuu wa taasisi, wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye mkutano uliofanyika ofisini kwake, Magogoni, jijini Dar es Salaam. Leo ndiyo ameripoti kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa Ijumaa iliyopita kwenye Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.

Pamoja na kazi nyingine tunayo majukumu makubwa ambayo ni udhibiti, usimamizi na ufuatiliaji wa masuala mbalimbali humu Serikalini. Ninataraji kupata mpango kazi kutoka kwa Mkuu wa kila idara na kila taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Nitakwenda pia ofisi za TAMISEMI ili kuweka vipaumbele vyetu sawa,” alisema.

Aliwataka watumishi hao wawe tayari kutekeleza kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ ambayo imekuwa ikisisitizwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili kuweza kumudu kasi ya utendaji kazi Serikali ambayo anaihimiza hivi sasa.

Alisema ana imani kuwa watumishi hao watampa ushirikiano kama ambavyo walikuwa wakiutoa kwa mtangulizi wake, Mhe. Mizengo Pinda ambaye amestaafu hivi karibuni.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM

JUMATATU, NOVEMBA 23, 2015.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea shada la maua kutoka kwa kaimu Mkurugenzi wa Utawala wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Savera Kazaura (kulia) Baada ya kuwasili ofisini kwake Novemba 23, 2015. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt, Florence Turuka. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akitia saini kitabu baada ya kuingia ofisini kwake , Magogoni jijini Dar es salaam, Novemba 23, 2015. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florence Tiruka.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa wakati alipozungumza nao katika mkutano wa kujitambulisha , Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa wakati alipozungumza nao katika mkutano wa kujitambulisha , Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akimsikiliza Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florence Turuka ambaye alitoa taarifa ya jumla kuhusu Ofisi ya Waziri Mkuu baada ya Waziri Mkuu kuwasili Ofisini na kujitambulisha kwa watumishi wa Ofisi yake Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu katika mkutano wa kujitambulisha alioufanya baada tu ya kuwasili ofisni Novemba 23, 2015. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florence Turuka wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu baada ya kuzungumza nao katika mkutano wa kujitambulisha alioufanya baada ya kuwasili ofisini kwake Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt Florence Turuka baada ya kuwasili Ofisini Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florence Turuka wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu baada ya kuzungumza nao katika mkutano wa kujitambulisha alioufanya baada ya kuwasili ofisini kwake Novemba 23, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Kitimtim cha Wabunge kuhusu posho na fedha za magari yao


Wakati Serikali ikihaha kutafuta fedha kwa ajili ya kuendeshea shughuli zake, wabunge wameingia kwenye mvutano na ofisi ya Bunge kuhusu fedha ambazo watunga sheria hao wanastahili kupewa kwa ajili ya kununulia magari yao.

Mwaka 2010, wabunge walilipwa Sh90 milioni kwa ajili ya ununuzi wa magari hayo aina ya Toyota Land Cruiser (hardtop), ambayo ni vitendea kazi vyao. Wabunge hutakiwa kulipa nusu ya fedha hizo wkati nyingine ni mchango wa Serikali.

Lakini wakati gharama za maisha zikipanda huku thamani ya Shilingi ikiporomoka kulinganisha na Dola ya Marekani na hivyo kusababisha bidhaa kupanda bei, wabunge wamekataa kulipwa kiasi hicho cha fedha mwaka huu na badala yake wanataka walipwe kulingana na bei ya sokoni ya magari aina hiyo.

Kwa mujibu wa habari ambazo Mwananchi imezipata, wabunge wanataka walipwe Sh130 milioni ambazo wanasema ni bei ya magari hayo kwa sasa baada ya kupanda bei.

Wakizungumza na Mwananchi kwa sharti la kutotajwa majina, baadhi ya wabunge walisema mara baada ya kujisajili bungeni kwa ajili ya uzinduzi wa Bunge la Kumi na Moja, katibu wa chombo hicho, Dk Thomas Kashililah alifanya kikao na wabunge wote ili kuwapa taratibu lakini pia kuwafahamisha stahili wanazopaswa kupata kama wabunge.
“Katibu alitujulisha kuwa tunapaswa kulipwa kiasi cha Sh300,000 kwa siku za posho, lakini pia tutapewa Sh90 milioni kwa ajili ya mkopo wa gari ambao nusu hutolewa na ofisi ya Bunge na kiasi kilichobaki tunapaswa kulipa wenyewe,” alisema mmoja wa wabunge hao.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, suala hilo liliibua mjadala na kusababisha wabunge kuhoji iweje kiwango hicho kitumike katika Bunge la Kumi na Moja, miaka mitano baada ya wabunge wa Bunge la 10 kupewa kiasi hicho.

Mbunge mmoja alisema:
“Unajua magari tunayotakiwa kununua ni Toyota Land Cruiser Hardtop, na ukweli sasa thamani ya magari hayo imepanda sana huwezi kuifananisha na mwaka 2010 wakati wa Bunge la 10” 
Wabunge hao walitaka walipwe kiasi cha Sh130 milioni kwa madai kuwa ndiyo bei ya sokoni ya magari aina hiyo.

Mbunge wa viti maalumu (CHADEMA), Anatropia Theonest alikanusha habari hizo akisema hawajakataa fedha hizo, lakini walisema thamani ya Dola imepanda hivyo kusababisha thamani ya magari hayo kupanda pia.
“Hakuna asiyejua kwamba thamani ya Dola imepanda na kwa kawaida kila Bunge kunakuwa na ongezeko la Sh30 milioni. Mfano Bunge la Tisa walipewa Sh60milioni la 10 wakapewa Sh90milioni, hivyo ilipaswa sasa iwe Sh 120mililioni ili kuendana na soko,” 
Alisema baada ya mazunguzo hayo ofisi ya Bunge iliahidi kulifanyia utafiti suala hilo na kwamba ingewajibu.

Mbunge wa Singida Magharibi (CCM), Elibariki Kingu alisema wabunge wanapaswa kufahamu wapo kwa ajili ya wananchi na si kujilimbikizia mali.
“Kwa mfano mimi siwezi kuchukua fedha za posho kwa ajili ya kikao. Nimepanga kumuandikia barua Spika juu ya uamuzi wangu. Mshahara wangu unanitosha kabisa” 
alisema Kingu ambaye awali alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga kabla ya kutolewa katika nafasi hiyo na kugeukia ubunge.


Akizungumzia sakata hilo, katibu wa Bunge alisema masharti na vigezo vilivyotumika mwaka 2010, ndivyo vinavyoendelea kutumika katika Bunge hili, na hivyo hakuna kilichobadilika.

Dk Kashililah alisema fedha za magari hayo hutolewa na Wizara ya Fedha kama mkopo na wabunge wataulipia huku kiasi kingine wakipewa kama ruzuku ya kununulia magari.

Hata hivyo hakutaka kuzungumzia kiwango halisi cha fedha zinazotolewa kwa wabunge hao.

Awali naibu katibu wa Bunge, John Joel alisema jukumu la ununuzi wa magari ya wabunge, lipo chini ya Serikali na siyo ofisi yake hivyo ni bora wangeulizwa wenye jukumu hilo.
“Tunachofamu sisi mbunge anatakiwa apewe vitendea kazi likiwemo gari, lakini wanaohusika na hilo ni Serikali”
“Sisi huwa tunawahudumia jimbo allowance (posho) kwa ajili ya kuhudumia ofisi ya mbunge na kununua mafuta ya gari” 
alisema Joel bila kutaja kiwango cha posho hiyo.

Alisema ofisi ya Bunge hushauriana na Serikali namna ya kutoa huduma kwa wabunge na kwamba kwa jinsi anavyofahamu, mpaka jana watunga sheria hao walikuwa hawajapewa fedha yoyote ya kununua magari kwa awamu hii, hivyo wanasubiri utaratibu.

Wakati Joel akisema Serikali ndiyo inahusika, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue aliurudisha mpira kwenye ofisi hiyo ya Bunge, akisema uongozi wa chombo hicho ndio uulizwe.

Katika kukusanya fedha za kuwezesha kutekeleza mipango ya Serikali na ahadi alizotoa wakati wa kampeni, Rais John Maguguli alitangaza hatua mbalimbali za kudhibiti matumizi, na akawaeleza wabunge mwishoni mwa wiki kuwa hataweza kufanikiwa iwapo hatapata ushirikiano wao.

Katika kuonyesha kuwa anatoa kauli thabiti, Dk Magufuli aliagiza fedha ambazo zilichangwa na taasisi mbalimbali za fedha kwa ajili ya hafla za kuwapongeza wabunge, zielekezwe kwenye ununuzi wa vifaa tiba kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Tayari Rais ameshafuta safari za nje isipokuwa kwa kibali cha Ikulu baada ya mtu anayetaka kusafiri kutimiza masharti kadhaa, likiwamo linalomtaka aeleze faida ya safari yake na kama iwapo hatasafiri, nchi itaathirika vipi.

Kilichosababisha ajali ya ndege aliyoabiri Filikunjombe


Uchunguzi wa awali kuhusu ajali ya chopa iliyogharimu maisha ya aliyekuwa mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wenzake watatu, unaonyesha ilitokana na hitilafu ya injini.

Mchunguzi Mkuu wa Ajali za Ndege wa Wizara ya Uchukuzi, Omar Mhina aliiambia Mwananchi kuwa:
“Katika uchunguzi wa awali, tulichukua injini na kugundua kuwa ilipata hitilafu. Hiyo ndiyo lugha ya kwanza tunayoweza kusema wakati tukisubiri uchunguzi mwingine,\”
Mhina alisema wameshaichukua injini kutoka pori hilo la Selous na kwamba wanatarajia kuipeleka kwa watengenezaji wake kwa ajili ya kufunguliwa na kujua kiini cha kufeli kwa injini hiyo.

Alisema waliwasiliana na wamiliki wa chopa hiyo nchini Kenya, lakini hawajapata ushirikiano wa kuridhisha mpaka sasa. Lakini Mwananchi ilizungumza na opereta mkuu wa chopa hiyo wa Kenya, na rubani wa kampuni ya Sun Drew, Kapteni Charles Wachira ambaye alisema TCAA hawajawasiliana na Mamlaka ya Anga ya Kenya (KCAA) kwa ajili ya uchunguzi wa ajali hiyo.
“Mimi ni kapteni wa ndege lakini siwezi kufanya lolote kama sijapata baraka kutoka TCAA na KCAA. Wao ndio walitakiwa wawasiliane kwanza kabla ya sisi Sun Drew kuchukua hatua zozote, ni suala baina ya serikali na serikali”
Kapteni huyo amesema akipata ruhusa kutoka KCAA atakuja nchini kwa ajili ya uchunguzi wa chanzo cha ajali ya chopa hiyo.

Kauli ya Musyoka

Kalonzo alisema kampuni yake imeshampa baraka zote, Kapteni Wachira ili kushirikiana na Tanzania kubaini chanzo cha ajali hiyo na kwamba kilichochelewesha ujio huo ni kusubiri kumalizika kwa shughuli za uchaguzi zilizokuwa zikifanyika Tanzania. Kalonzo alisema walituma mwakilishi ambaye ni mjumbe wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Peter Mathuki kupeleka salamu za rambirambi na kuhudhuria msiba wa Kapteni Silaa.
“Ni lazima tushiriki katika hili kwa sababu ni pigo kubwa kwetu na kwa serikali yenu. Tayari Kapteni Wachira amekuja huko ili kushirikiana na Mamlaka ya Anga ya Tanzania”

Mafuta

Chanzo kingine cha ajali hiyo kilichoelezwa na timu hiyo ni madumu matano ya mafuta ya ndege yaliyokuwa yamepakiwa ndani.
“Walikuwa wamebeba hayo madumu yenye mafuta ya akiba kwa kuwa walikuwa wametokea Ludewa ambako hakuna mafuta; unajua chopa hazikai na mafuta kwa muda mrefu ndiyo maana walibeba mafuta ya akiba”
Kadhalika chanzo hicho kimesema viti vya ndege vilionekana kuanguka na kuvunjika na watu waliokuwamo walivunjika uti wa mgongo na miguu. Hata kama wasingeungua, wangepoteza maisha kutokana na madhara ya kuanguka kwake.

Ripoti ya BEA

Ripoti ya awali ya Kitengo cha uchunguzi wa ajali za ndege cha Serikali ya Ufaransa (BEA) iliyochapishwa kwenye tovuti yake imeeleza kuwa chopa hiyo ilionekana ikianguka kutoka angani, ikiwa tayari haina nguvu na ikifuka moshi. Kadhalika chopa hiyo ilionekana kwa muda mrefu ikiruka umbali wa chini na baada ya kuanguka, ililipuka.

Turbomeca


Mkuu wa kitengo cha wanafizikia wa kampuni ya Turbomeca iliyotengeneza injini ya ndege hiyo, Delpgine Robelin alikataa kutoa maelezo akisema kuwa ni ya siri. “Hii ni siri kubwa. Hakuna taarifa zozote zinazoweza kutolewa,” inasema barua pepe ya Robelin akijibu barua pepe ya Mwananchi iliyoomba kupata ripoti ya awali ya uchunguzi wa ajali hiyo.

Mawasiliano

Uchunguzi umebaini pia Kapteni Silaa hakuwasiliana na kitengo cha usalama wa anga na mawasiliano ya ndege cha TCAA

Kuhusu tatizo la chopa. Mhina amesema Kapteni Silaa aliwasiliana na kitengo hicho wakati ndege ipo ardhini, ikipaa na ilipofika juu, lakini baada ya hapo hakukuwa na mawasiliano yoyote.

“Kabla hajaruhusiwa kwenda eneo jingine la anga (area control route) ndipo alipokata mawasiliano na hakuwasiliana hata na ndege nyingine kueleza kama ana tatizo,” alisema.

“Kwa kawaida chopa zinatakiwa kuwasiliana zikiwa angani, lakini hakuna chopa yoyote iliyotoa taarifa kama waliwasiliana na Kapteni Silaa,” alisema Mhina na kuongeza: “Iwapo chopa ina matatizo ya injini, kuna namna ambayo marubaini wanaweza kudhibiti ili kusitokee madhara, lakini haijulikani kwa nini Kapteni Silaa alishindwa kudhibiti hali hiyo.”

Shahidi

Mhina alisema kwamba mmoja wa mashuhuda aliiambia timu ya wachunguzi kwamba alianza kuona chopa hiyo ikifuka moshi wakati iko hewani. “Lakini haikuwa ikiungua, hapana, ilifuka moshi hadi ilipoanguka ndipo ikawaka.”

Novartis launches new anti-malarial formulation for Africa

MEDIA RELEASE


Novartis launches new anti-malarial formulation and reaffirms commitment to achieve quality healthcare for Africa

Mwongozo wa masharti kwa watumishi wa umma wanaotaka kusafiri nje ya nchi

Ofisi ya Rais imesambaza mwongozo unaoweka masharti ambayo watumishi wa umma wanaotaka kusafiri nje ya nchi watatakiwa kutimiza ili wapewe kibali, ikiwa ni mkakati wa kutekeleza agizo la Rais John Magufuli la kudhibiti safari holela za nje.

Rais alitoa agizo hilo baada ya kikao baina yake na makatibu wa wizara kilichofanyika Ikulu siku chache baada ya kuapishwa, akisema ofisi yake ndiyo itakayotoa kibali kwa watumishi ambao wana safari za nje.

Kwa mujibu wa waraka huo, sharti la kwanza linalotakiwa kuzingatiwa na watumishi hao ni kuomba kibali kwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Pili, kwa mujibu wa mwongozo huo, maombi yawasilishwe kwa msajili wa hazina kabla ya kwenda kwa katibu ili aweze kujenga hoja kwa kuzingatia umuhimu wake na tija itakayopatikana kutokana na safari hiyo.

Tatu, mtendaji mkuu wa shirika au taasisi lipime maombi ya safari husika ili kuona kama yana tija na yana umuhimu wa kuombewa kibali kwa katibu mkuu kiongozi, kabla ya kuwasilishwa kwa msajili wa hazina, kwa mujibu wa mwongozo huo.

Nne, lina vipengele vitano ambavyo vinatakiwa kuzingatiwa wakati wa kuwasilisha hoja ya safari.

Kipengele cha kwanza ni chanzo cha safari husika, cha pili ni faida yake, tatu kwa nini ni muhimu kwa safari hiyo kufanyika na isipofanyika itaathiri vipi.

Kipengele cha nne kinachambua gharama za safari, kikiweka masharti yanayomtaka mwombaji aainishe gharama ya tiketi ya ndege, posho za safari husika, mlipaji wa gharama za safari na uwezo wa taasisi kifedha.

Kipengele cha tano cha sharti la nne kinamtaka mwombaji aeleze manufaa ya safari hiyo kwa taasisi na Taifa kama imewahi kufanyika huko nyuma.

Akizungumzia hilo, Balozi Sefue alisema ni kweli ofisi ya Rais ilituma taarifa ya kupiga marufuku safari za nje na kinachofanywa na ofisi za umma ni taratibu za safari hizo zisizoepukika.

Alisema tangu Rais Magufuli apige marufuku safari za nje, ofisi hiyo imesambaza agizo hilo katika ofisi za umma kuwa ni marufuku mtumishi wa umma kusafiri isipokuwa kwa kibali, kiwe cha Rais au cha Katibu Mkuu Kiongozi.

Alisema miongozo ya safari hizo inazitaka ofisi za umma kuhakikisha kuwa ombi la kila anayetaka kusafiri, lichujwe na kuhakikisha safari yake haiepukiki.
“Ofisi inapoleta maombi kwetu ijiridhishe kuwa haiepukiki. Maombi mengi yataishia kwenye ofisi zao, ikija kwetu inatakiwa ionyeshe wazi kuwa haiepukiki na tukipima vigezo vyake na kuona haviridhishi, tunaweza kuikataa vile vile” 
Alisema miongozo iliyobandikwa katika ofisi za umma kuhusu safari za nje ni taratibu ambazo zinafuatwa na taasisi baada ya agizo hilo kutoka ofisi ya Rais.

Ofisi za umma zilipokea barua kutoka kwa msajili wa hazina, yenye kumbukumbu namba CEA.111/372/01 iliyowasilishwa Novemba 12 mwaka huu ikielekeza kuwa Rais Magufuli ametoa zuio la jumla la safari za nje ya nchi katika utumishi wote wa umma na mihimili yake.

Zuio hilo linayagusa mashirika na taasisi zote za umma. Barua hiyo ya msajili ilieleza kuwa zuio hilo litadumu hadi pale itakavyoelekezwa vinginevyo.

Habari za kuwapo kwa agizo hilo zilithibipitishwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala, ambaye alikiri kupokea maelekezo kutoka kwa msajili wa hazina.
via Mwananchi

NORAD scholarships for Tanzanians for PhD in Energy and Petroleum

EnPe – NORAD´s SCHOLARSHIPS FOR PhD STUDIES IN ENERGY AND PETROLEUM SECTOR AT THE NORWEGIAN UNIVERSITY OF SCIENCE AND TECHNOLOGY (NTNU) 

ANTHEI (Angolan Norwegian Tanzanian Higher Education Initiative) Project 2016 – 2019 

Background 

Since 2011 the University of Dar es Salaam (UDSM) the Norwegian University of Science and Technology (NTNU) of Norway and the University of Agostinho Netto (UAN) in Angola have been collaborating under the ANTHEI project to train professionals in petroleum engineering and petroleum geosciences at masters level. Already three batches of a total of 28 Tanzanian students have been enrolled in phase one of the programme. 

In phase two of the programme, 9 students were enrolled for Masters and a batch of 3 students will be granted scholarships next year (2016) to undertake a three year full-time PhD study in Petroleum Engineering and Petroleum Geosciences at NTNU. The scholarship covers subsistence allowance (stipend), travel to and fro, tuition, insurance and stationeries. 

PhD in Petroleum Engineering and Applied Geophysics 

The PhD programmes are taught in English. The programmes focus on the following areas: 
  1. Exploration and production of oil and gas 
  2. Methods of increasing oil recovery 
  3. Development of subsea production solutions for greater water depths 
  4. Seismic surveillance of reservoirs 
A candidate can specialize in: drilling technology, petroleum production, reservoir technology, petroleum geology or petroleum geophysics. 

For general information about the PhD programme in Petroleum Engineering and Petroleum Geosciences please follow the link https://www.ntnu.edu/studies/phpetr 

Eligibility 
  1. Applicant should have a background in the mentioned areas of specialisation at MSc level; 
  2. Applicant must have obtained a GPA of 3.8 or above at undergraduate level or its equivalent and a GPA of 4.0 or above for Masters degree by coursework or PASS for Masters degree by thesis or their equivalent,; 
  3. The Masters degrees must have been obtained within the past 5 years; 
  4. Qualified females will be given priority. 
Application 

Each application must be accompanied by transcripts, certificates, CV and a concept note of not more than two pages addressing a research topic of interest. 

Please submit your application in electronic form by 3rd December 2015 to 

EnPe Project Coordinator, 
Department of Chemical and Mining Engineering 
College of Engineering and Technology (CoET), 
UDSM P. O. Box 35131, 
Dar es Salaam 

Tel: +255 222 410 368 
Fax: +255 222 410 114

Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Kanda ya Kaskazini


Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili kanda ya Kaskazini na Meneja Miradi wa Shirika lisilo la kiserikali la NAFGEM, Honorata Nasuwa akizungumza na wanahabari(hawako pichani ) juu ya uzinduzi huo, kushoto kwake ni Afisa Ushawishi na utetezi (KWIECO) na mratibu wa maadhimisho hayo kanda, Hilary Tesha.

Picha za misa ya kumkumbuka Nyamiti Lusinde - Baltimore, MarylandPicha ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde ikiwa kanisani siku ya Jumapili Novemba 22, 2015 siku ilikofanyika misa takatifu ya kumbukumbu na kuhudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akiwa ameongozana na mkewe pamoja na mwanae. 

Nyamiti alikuwa mfanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani alipatwa na mauti alipokua likizo Tanzania katika hospitali ya Kariuki alipokua amekwenda kwa matibabu baada ya kuugua ghafla alipokua huko na baadae kuaga Dunia Novemba 17, 2015.