Maelezo mafupi ya Julius K. Nyerere kuhusu "shabaha zetu 2 baada ya uhuru"


Unaweza kutizama clips nyingine kumhusu hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye YouTube chaneli ya Associated Press Archive na British MovietoneMjadala katika kipindi cha Jukwaa Langu Nov 23, 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk John Magufuli akizindua Bunge la XI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk John Magufuli akizindua Bunge la XI 
Kipindi hiki hukujia kila Jumatatu kuanzia saa 11 jioni kwa saa za Marekani ya Mashariki kuijadili Tanzania ya sasa na ile tuitakayo.

Katika kipindi hiki tumejadili (mbali na mambo mengine) muelekeo wa serikali ya Tanzania baada ya kuzinduliwa kwa Bunge la 11.

Mjadala huu ambao ulifuata habari kutoka kwenye magazeti mbalimbali, umehusisha wadau kutoka Marekani, Canda na India.

Karibu.

Unaweza kutusikiliza kupitia tovuti zetu www.kwanzaproduction.com na www.vijimamboradio.com

Waziri Mkuu ataka maelezo kesho saa nne ya kwa nini mabasi yaendayo haraka hayajaanza kazi


Maelezo kuhusu kifo cha Alphonce Mawazo kilivyotokeaNOVEMBA 24, 2015
Mambo 10 aliyojifunza kocha Amani kutoka kwa Edward Lowassa

Napenda sana kujifunza kupitia watu ninaokutana nao au ninaowasoma katika maandiko mbalimbali. Na kupitia watu wengi ninaojifunza kutoka kwao, kuna wachache ambao nawaita “MY VIRTUAL MENTORS” yaani washauri wangu wa mbali. Hawa ni watu ambao wanakuwa wamefanya mambo makubwa sana kutokana na vipimo vyangu na napenda na mimi kuweza kufikia pale walipofikia wao.

Katika orodha yangu ya virtual mentors kuna watu wengi walioishi zama tofauti na wengine bado wanaishi. Na pia wapo watu wa mataifa mbalimbali duniani. Mmoja wa watu walioingia kwenye orodha yangu hii kwa siku za hivi karibuni ni aliyekuwa mgombea wa uraisi wa Tanzania Edward Ngoyai Lowassa.

Katika kipindi chote cha kampeni, mpaka kufika uchaguzi na baadaye kutangazwa kwa matokeo, kuna mambo mengi sana niliyojifunza kwa mentor wangu huyu. Na hata maisha yake kabla ya uchaguzi huu kuna mengi pia ya kuweza kujifunza.

Hapa nakushirikisha mambo kumi muhimu niliyojifunza kutoka kwa Lowassa, huenda na wewe ukaweza kuyafanyia kazi na maisha yako yakawa bora zaidi. Kumbuka hivi ni vigezo nilivyoweka mwenyewe kwa hiyo inaweza isionekane ni kitu kikubwa kwako. Karibu tujifunze kupitia mentor wangu huyu...

1. Unapokitaka kitu, jitoe hasa.

Lowassa alikuwa na ndoto za kuwa raisi wa Tanzania, na alijitoa kweli kupigania ndoto yake hiyo. Hakukubali kitu chochote kimzuie yeye kufikia ndoto yake hiyo kubwa. Ndio maana hata baada ya kutopitishwa na chama cha mapinduzi aliangalia njia nyingine anayoweza kutumia na hatimaye akaweza kugombea kupitia chama cha upinzani.

Ili uweze kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako, unahitaji kujitoa hasa, unahitaji kuangalia kila njia unayoweza kutumia ili kufikia lengo lako. Hata kama njia moja uliyokuwa unategemea imefungwa, basi angalia njia yoyote mbadala unayoweza kutumia. Na kama umejitoa kweli ni lazima utapara njia mbadala. Jitoe na pigania kile unachotaka, hakuna kitu rahisi.

2. Watu wengi hawatakuelewa.

Katika safari yako ya mafanikio, safari ya kufikia kile unachotaka, watu wengi hawatakuelewa. Kwa sababu wewe umejitoa kweli na hukubali kitu chochote kikuzuie kupata kile ambacho unakitaka, watu wengi watasema una tamaa, una uchu na mengine mengi. Wengi wanatumia maneno kama haya kwa njia hasi, kama vile kutaka kitu kwa moyo sana ni dhambi kubwa.

Kutokana na Lowassa kutaka sana nafasi ya urais na kuhakikisha anajitoa kweli, wengi waliona ana tamaa na uchu wa madaraka. Wengi walisema ni mtu hatari kwa sababu akipata nchi anaweza kufanya mambo yasiyotegemewa. Lakini hili linatokana na wengi kutokuelewa jitihada zinazohitajika ili upate kile unachokipata.

Unapochagua njia hii ya mafanikio, na kujitoa kwa kila ulichonacho, wengi hawatakuelewa, ila hili lisikuzuie, endelea kusonga mbele.

3. Kuanguka sio mwisho wa safari.

Katika safari yako ya mafanikio, katika maisha yako, kuna maeneo mengi ambapo utaanguka. Na haijalishi utaanguka vibaya kiasi gani, kama bado upo hai basi sio mwisho wa safari. 

Lowassa alianguka sana kwenye safari yake ya kisiasa. Kuanzia alipojiuzulu kutokana na kasha ya Richmond mwaka 2008. Pamoja na kuanguka huku kutokana na kasha kubwa, hakutaka hii iwe ni kikwazo kwake, badala yake aliendelea kujijenga ili kutimiza ndoto yake yakuwa raisi wa nchi yake.
Hata wewe unapochagua safari hii ya mafanikio, safari ya kuwa na maisha bora, safari ya kufanya kazi au biashara yako kwa ubora, ni lazima utaanguka. Lakini kuanguka huku kusikufanye uachane na ndoto yako kubwa uliyonayo. Hata kitokee kitu gani, ni lazima safari yako iendelee.

4. Marafiki. (sehemu ya kwanza)

Tangu zamani imekuwa ikijulikana kwamba rafiki wa karibu sana wa Lowassa ni Kikwete. Na hata baada ya kujiuzulu, kuna kauli ilikuwa inasikika mara kwa mara kutoka kwa wawili hawa kwamba wao ni marafiki na hawakukutana barabarani. Yaani wao ni marafiki wa ndani sana na wametoka mbali sana. Hivyo kama rafiki, Lowasa alitegemea msaada mkubwa wa yeye kufikia ndoto yake kutoka kwa rafiki yake. Lakini mwishowe tulimsikia Lowasa akitoa kauli za kuonesha kutelekezwa na rafiki yake huyu mkubwa.

Kikubwa cha kujifunza hapa ni kwamba unaweza kuwana rafiki ambaye mmetoka mbali sana na mkawa mmekubaliana kusaidiana, lakini ikafika kipindi rafiki yako huyu akaacha kuwa na wewe. Hivyo jua ni jinsi gani utakavyoweza kuendelea kutimiza ndoto yako hata kama rafiki unayemtegemea ataacha kukusaidia. Ndoto yako isifike mwisho kwa sababu rafiki yako uliyemtegemea sana hayupo tena na wewe. Muhimu zaidi ni usimfanye mtu yeyote kuwa na madhara makubwa sana kwenye maisha yako kwa kuwepo au kutokuwepo kwake. 

5. Unachotegemea hakitatokea.

Wakati Lowassa anaondoka CCM na kwenda CHADEMA alitegemea angeondoka na watu wengi sana. Alitegemea angeondoka na wabunge wasiopungua 50, mawaziri na wanachama wasiopungua milioni moja. Lakini hili sio lililotokea, japo kuna wengi waliomfuata, lakini sio kwa idadi ile ambayo alitegemea.

Katika safari yako ya maisha na mafanikio, kuna mambo mengi sana ambayo utapanga na utategemea. Lakini sio mambo yote yatakayotokea kama utakavyopanga. Hivyo jiandae kwa hili na jua ni hatua gani utakayochukua kama mambo hayataenda kama ulivyopanga. Kwa kujiandaa hivi itakuwezesha kukabiliana na changamoto utakayokutana nayo.

6. Kukazana na kile unachotaka, kuachana na kelele.

Kuna neno la kiingereza linaitwa FOCUS, maana yake ni kuweka nguvu zako zote kwenye kile ambacho unakitaka, na kuachana na kelele nyingine zozote. Lowassa aliweza kufanya hivi kwa kupelekea nguvu zake kwenye kuutaka uraisi. Na kwa kufanya hivyo alikazana kulenga yale ambayo yatampatia kura na sio kujibizana na watu. Katika kampeni za uraisi, tuliona wengi wakimkashifu, wengi wakimtukana, na wakitegemea atajibu mapigo lakini yeye hakufanya hivyo, aliendelea na juhudi zake za kuupata uraisi.

Unahitaji FOCUS sana kwenye safari yako ya mafanikio kama unataka kuyafikia kweli. Hii ni kwa sababu chochote utakachofanya au utakachopanga kufanya, kuna wengi watakupinga, kuna wengi watakukatisha tamaa na kuna wengine wengi watataka kukurudisha nyuma. Sasa kama wewe utaamua kupambana na watu hawa, utapoteza muda wako bure. Badala yake wewe waache wafanye hayo yanayowafurahia, ila wewe kazana kufikia ndoto yako kwa kuwajibu wanaokupinga, bali utaifikia kwa kuifanyia kazi.

Acha mara moja kujaribu kumjibu kila anayekupinga. Acha mara moja kupambana na kila anayekurudisha nyuma. Peleka nguvu zako kwenye kufikia kile unachotaka.

7. Elimu, elimu, elimu.

Kitu kimoja ambacho Lowassa alisema angekitilia mkazo kama angechaguliwa kuwa raisi ni ELIMU. Ni kweli kabisa ya kwamba elimu ndio msingi muhimu sana kwenye maendeleo ya mtu mmoja mmoja na hata taifa kwa ujumla. Ukosefu wa elimu bora unatugharimu sana kama taifa. Na ni wakati sasa umefika tutengeneze mfumo mpya wa elimu utakaoendana na matakwa yetu.
Tumeona mfumo tulionao ukizalisha waajiriwa wengi kuliko nafasi zilizopo. Na hii inaendelea kuleta shida kubwa kwa wengi.

Na pia elimu sio ile rasmi tu, kuna elimu kubwa ambayo wewe unatakiwa uipate ili uweze kufikia mafanikio yako. unahitaji kufanya kile unachofanya kwa utaalamu mkubwa na hata kwa utofauti na wanavyofanya wengine. Yote haya utaweza kama utaweka kipaumbele chako cha kwanza kuwa elimu.

Usikubali siku ipite hujajifunza kitu chochote kipya kuhusiana na kazi au biashara unayofanya, kujifunza kutakusaidia sana kufikia mafanikio makubwa.

8. Marafiki. (sehemu ya pili)

Kuna marafiki ambao wapo na wewe wakiwa na ajenda zao. Na wengi wanaangalia ni jinsi gani wao wananufaika na wewe. Hivyo wakiona kuna nafasi za kunufaika watakuwa na wewe pamoja, wakiona hakuna nafasi hiyo wataachana na wewe.

Lowassa alikuwa na marafiki wengi alipokuwa CCM, na aliamini ni watu wake wa karibu sana na wangekuwa tayari kwenda naye popote atakapokwenda. Lakini wengi hawakuweza kwenda naye, kwa sababu yale maslahi waliyokuwa wanaona watapata mwanzo, hawakuyaona tena.
Jua kuna watu wa aina hii kwenye maisha yako, na wasikuumize kichwa pale ambapo wataondoka kutokana na kuona maslahi yao hayapo tena.

9. Kuendelea kuwa na moyo wa ushindi.

Hata baada ya kushindwa uraisi, Lowassa ameendelea kuwa na moyo wa ushindi. Na moja ya kauli aliyotoa baada ya kushindwa ni kwamba; I might have lost a battle, but not a war. Akimaanisha kwamba amepoteza pambano moja, ila hajashindwa vita nzima.

Huu ni moyo unaohitaji kuwa nao kama kweli unataka kufikia mafanikio makubwa. Kwa sababu kwenye safari yako hii utapoteza mapambano mengi sana. Lakini kama hutakata tamaa lazima utashinda vita.

10. Kujali maslahi mapana ya taifa.

Baada ya kupiga kura na kura zikaanza kuhesabiwa, matokeo yalipoanza kutangazwa, watu wengi walishtushwa na kusikitishwa na matokeo yaliyokuwa yanatolewa. Wengi walisema Lowassa aliibiwa kura na mwenyewe alidhibitisha hili. Baada ya hili wananchi wengi walikuwa na hasira na walikuwa wanataka kusikia neno moja tu kutoka kwa Lowassa kwamba wafanye nini. Lakini kwa busara kubwa Lowassa hakutaka kusababisha machafuko kwenye nchi, kitu ambacho angeweza kufanya kama angewasisitiza wafuasi wake kudai ushindi wao. Lowassa alijali maslahi mapana ya taifa.

Naamini kuna mambo ambayo umejifunza na utayafanyia kazi. Lengo kubwa hapa ni wewe kuweza kuchukua hatua na kuboresha maisha yako. hakuna kinachoshindikana pale unapoamua kweli ni nini unataka.

Nakutakia kila la kheri katika utekelezaji wa haya uliyojifunza.

Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
[email protected]
0717396253
AMKA CONSULTANTS

Job: Project associate - Marketplace for nutritious foods (1 year contract)

Organization: Global Alliance for Improved Nutrition
Country: Kenya
Closing date: 13 Dec 2015
The Project Associate - Marketplace for Nutritious Foods will support the implementation of the Marketplace for Nutritious Foods in Kenya by ensuring timely delivery of project activities. He/she will also provide general support to the GAIN country office as required.
The Project Associate will be responsible among other things to maintain the Marketplace visibility plan, identify new opportunities for raising visibility around the Marketplace and increasing Community of Practice (CoP) membership. He/she will also be responsible to design and oversee GAIN/Marketplace presence in local events, such as agribusiness fairs and trade shows. Furthermore, in collaboration with the GAIN communications team and the Project Manager, Marketplace for Nutritious Foods, the Project Associate will achieve outreach for GAIN and the Marketplace by providing information, stories, press releases, etc. to the media and design Marketplace promotional materials.
The ideal candidate will have solid experience in planning and organizing events and training workshops. He/she will also have relevant experience in working with different stakeholders such as business, government and donors; and experience in working in social media, documentation and resource mobilization. Finally, he/she will have ideally a good understanding of the agribusiness landscape in Kenya.

How to apply:
Please follow this link:

Job: Programme Manager - Oxfam, Kigoma

Organization: Oxfam
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 25 Nov 2015

Call for Experts: East Africa - Gender/Youth, Climate Change/Environment, Natural Resources Management

Organization: Land O'Lakes
Closing date: 23 Jan 2016

Call for Technical Experts - East Africa

Organization: Land O'Lakes
Closing date: 23 Jan 2016

Call for Experts: East Africa - Finance, Operations, and Grants Management

Organization: Land O'Lakes
Closing date: 23 Jan 2016

Job: Senior Adviser, EGAT

Organization: Crown Agents USA
Country: United States of America
Closing date: 24 Dec 2015

UNICEF consultancy to conduct State budget analysis of key social sectors w/ equity and children

Organization: UN Children's Fund
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 30 Nov 2015

Bodi ya Sukari yapewa siku 7 kutatua tatizo soko la miwa ya wakulima wadogo Kilombero

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bibi Sophia Kaduma ameiagiza Bodi ya Sukari Tanzania kushughulikia mara moja madai ya wakulima wadogo wa miwa (out-growers) katika Kiwanda cha Sukari cha Kilombero kilichopo Mkoani Morogoro yaliotokana na miwa yao kutonunuliwa na kiwanda.

Katika agizo hilo, Katibu Mkuu Bibi Sophia Kaduma ameiagiza Bodi ya Sukari Tanzania kukuta na Uongozi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero na ule wa wakulima wadogo wa miwa ili kupata ufumbuzi wa kudumu kuhusu soko la miwa wanayozalisha.

Aidha, Katibu Mkuu ametoa muda wa siku saba kwa Bodi ya Sukari Tanzania iwe imetekeleza na kutoa taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo.

Agizo hilo limekuja kufuatia Serikali kupata taarifa kuwa Uongozi wa Kiwanda hicho umeshindwa kununua miwa ya wakulima hao licha ya makubaliano yao ya awali ya kuzalisha miwa na kukiuzia kiwanda kwa ajili ya kuzalisha sukari. Wakulima wamedai kuwa miwa hiyo, inakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16.

Bodi ya Sukari Tanzania imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Sukari Na. 26 ya mwaka 2001 kama ilivyorekebishwa mwaka 2009 na Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Mazao Na. 20 ya mwaka 2009 (Crop Laws (Miscellaneous Amendments) Act).

Bodi ya Sukari Tanzania inajukumu pamoja na mambo mengine, kusimamia na kuratibu kilimo cha miwa na biashara ya sukari nchini, kusajili wakulima, wazalishaji wa sukari na wafanyabiashara wa sukari.

Aidha, Bodi ya Sukari ina dhamana ya kuhakikisha uwepo wa ushindani wa haki kwenye soko la miwa na biashara ya sukari nchini.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika
Kilimo Complex,
1 Mtaa wa Kilimo 15471
DAR ES SALAAM.

TEMESA yatamka: Serikali itanunua vivuko vipya

Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko kutoka Wakala wa Huduma za Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Dar es Salaam kuhusu mpango wa Serikali kununua kivuko kipya kwa ajili ya wakazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Zamaradi Kawawa.

Na Frank Mvungi

Serikali ya Awamu ya V imepanga kutumia takribani shilingi bilioni sita kununulia kivuko kipya kitakachotumika kutoa huduma kwa wananchi katika eneo la Feri hadi Kigamboni, Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle amesema ununuzi huo umelenga kuboresha huduma za usafiri wa vivuko kote nchini.

Akizungumzia kivuko kitakachonunuliwa kwa ajili ya jiji la Dar es Salaam, Maselle amesema kuwa kitakuwa na uwezo wa kubeba tani 170 na kitakuwa na injini 4 hali itakayoongeza tija katika kuwahudumia wananchi.

“Serikali imepanga kununua vivuko vitatu vipya ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuondoa kabisa tatizo la vivuko hapa nchini ”alisisitiza Maselle”

Maselle amesema kuwa vivuko viko katika hali nzuri na mpango wa Serikali kwa sasa ni kuvifanyia matengenezo ya mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma yenye ubora unaotakiwa.

Pia Masele amebainisha kuwa Serikali itatumia zaidi ya bilioni 3 kujenga kivuko kipya cha Pangani ambapo kazi ya ujenzi wake itaanza wakati wowote kwa kuwa taratibu zote za maandalizi zimeshakamilika.

Maselle anabainisha kuwa wamejipanga kuwapa wananchi taarifa kwa wakati kulingana na hali ya vivuko na hatua zinazochukuliwa ikiwemo kufanya ukarabati ili kuepusha usumbufu.

TEMESA inasimamia na kuendesha vivuko vyote vya Serikali nchini ambapo kwa sasa kuna jumla ya vivuko 28 vinavyofanya kazi.

TEMESA ilianzishwa kwa sheria ya wakala Na. 3 ya mwaka 1997 ambayo inalenga katika utekelezaji wa Serikali wa kuboresha huduma kwa umma katika Wizara za Serikali na Taasisi zake. TEMESA Ilianza rasmi mwezi Juni 2006 baada ya tangazo la Serikali Na. 254 La tarehe 26/08/2005 ambapo Wakala huo unatoa huduma katika Nyanja za Uhandisi Mitambo,Umeme,Electroniki na uendeshaji wa Vivuko.

Agizo la Waziri Mkuu: Kila Mkurugenzi awe na nakala ya hotuba ya Rais atimize yaliyomo katika eneo lake


WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amewataka wakurugenzi wa vitengo na wakuu wa taasisi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) wapate nakala ya hansard ya hotuba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuzindua Bunge la 11, waisome na kufanyia kazi maeneo yote aliyoyaainisha.

“Katibu Mkuu hakikisha umepata hansard ya hotuba ya Mheshimiwa Rais wakati akizindua Bunge na uhakikishe kila mkurugenzi ana nakala na kila mmoja wenu lazima ahakikishe anafanyia maeneo ambayo Mheshimiwa Rais ameyaainisha. Ni lazima tuelewane ni nini tunapaswa tufanye,” alisema.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Novemba 24, 2015) wakati akizungumza na wakuu wa taasisi, wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) kwenye mkutano uliofanyika ofisi ndogo ya TAMISEMI, barabara ya Kivukoni, jijini Dar es Salaam.

“Ninatamani kuona mabadiliko ya utendaji kazi Serikalini katika kipindi kifupi. Natamani kila mmoja asiridhike na uzembe unaofanywa huku chini. Ni nyote ni wataalamu, kwa hiyo mnapaswa kudhirisha elimu yenu na ujuzi mlionao,” aliwasisitizia Wakurugenzi hao.

Alisema kila mkurugenzi na mkuu wa taasisi anapaswa kuongeza usimamizi na ufuatiliaji wa kazi kwenye sekta yake kwani hilo litasaidia kukidhi matarajio ya Watanzania ya kuona mabadiliko ya utendaji kazi kwenye Serikali ya Awamu ya Tano. “Ninyi wakurugenzi siyo desk officers bali ni field officers. Nataka muweke utaratibu wa kwenda vijijini mkasimamie watu wenu, pia mhimize uadilifu, uaminifu na weledi wa kazi,” alisisitiza.

“Mambo ninayotaka mhimize watendaji waliopo chini yenu ni pamoja na haya yafuatayo: muda wa kuripoti kazini uzingatiwe, muda wa kukaa kazini uzingatiwe, utokaji kazini kwenda kwenye chai na chakula cha mchana udhibitiwe, na mipango na malengo ya kazi kwa siku ni lazima yafikiwe,” alisema.

“Tunataka kujua mtumishi amefanya nini tangu alipoingia ofisini. Suala siyo kukaa tu ofisini, kwani kuna mtu anakaa ofisini, hajaenda hata kunywa chai lakini ukiuliza amefanya nini hupati jibu la kueleweka. Sisi kama vongozi wao ni lazima tujue wanafanya kazi gani wanapokuwa maofisini,” alisisitiza.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa ameitisha kikao ofisini kwake kesho saa 4 asubuhi akitaka kupatiwa taarifa ni kwa nini mradi wa mabasi yaendayo kasi (DART) haujaanza kazi hadi sasa. “Kesho saa 4 asubuhi Katibu Mkuu, Mkurugenzi Mkuu DART na watendaji wako mje ofisini. Nataka kupata maelezo ni kwa nini mabasi hayajaanza kazi hadi leo, je ni lini yataanza kazi, je ni nani anakwamisha. Na hata kama ni sheria, ni kwa nini tusiziharmonise ili kuondoa hivyo vikwazo,?” alihoji Waziri Mkuu.

“Ninataka kupata haya maelezo kwa sababu Watanzania na hasa wana-Dar es salaam, wamesubiri kwa muda kuona mradi ukianza kazi ili uondoe kero ya usafiri. Wao wanajua anayehusika ni TAMISEMI,” aliongeza.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na watumishi na viongozi wa TAMISEMI, Katibu Mkuu wa OWM-TAMISEMI, Bw. Jumanne Sagini alimweleza baadhi ya mafanikio na changamoto ambazo wizara hiyo imekabiliana nazo katika utendaji wake wa kazi.

Kuhusu ujenzi wa vyumba vya maabara kwa ajili ya kuimarisha ufundishaji wa masomo ya sayansi, Bw. Sagini alisema vyumba hivyo vimeongezeka kutoka 247 mwaka 2005/2006 na kufikia 6,161 mwaka 2014/2015. Pia alisema vyumba 4,228 viko kwenye hatua za kukamilika ujenzi wake.

Kuhusu utengaji wa madirisha ya kuhudumia makundi yenye msamaha kama wazee na watu wenye ulemavu hospitalini na kwenye vituo vya afya, Katibu Mkuu alisema nayo yameongezeka kutoka madirisha 5,074 mwaka 2010 na kufikia 7,903 mwaka 2014/2015 sawa na ongezeko la asilimia 55.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM

JUMANNE, NOVEMBA 24, 2015.

Tenga ang'atuka, CECAFA yampata Mwenyekiti mpya

L-R: Sirelkhatim Gaffar; Leodegar Tenga
L-R: Sirelkhatim Gaffar; Leodegar Tenga 
HATIMAYE Mutasim Sirelkhatim Gaffar wa Sudan, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), baada ya kupata kura sita kati ya 10 katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika jana mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Katika uchaguzi huo, Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Leodegar Tenga, alijitoa dakika za mwisho kutetea nafasi yake baada ya kuliongoza baraza hilo katika vipindi viwili.

Katika uchaguzi huo, mgombea mwingine ambaye ni bosi wa zamani wa Shirikisho la Soka nchini Uganda (FUFA), Lawrence Mulindwa, alibwagwa vibaya baada ya kupata kura mbili.

Mulindwa alichaguliwa kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya CECAFA Novemba 2013 na pia alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CECAFA Februari 2014.

Wagombea wengine ambao waliwania nafasi ya uenyekiti ni Vincent Nzamwita (Rwanda), alipata kura moja wakati Juneid Bashar Tilmo wa Ethiopia alipata kura moja.

Tenga ambaye alikuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuanzia mwaka 2014- 2013, alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa CECAFA tangu mwaka 2007, alipochukua nafasi ya Dennis Obua kutoka nchini Uganda.

Goodluck Jonathan's talk about Tanzania general election 2015