Ombi la AG la kukamatwa mali na bilionea mtuhumiwa wa dawa za kulevya latekelezwa

Akiwa mikononi mwa polisi
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju amewasilisha waraka Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam akitaka kushikiliwa na kuzuiwa kwa mali zote za mtuhumiwa wa madawa ya kulevya ‘unga, Muharami Abdallah au maarufu kwa jina la ‘Chonji’ na mkewe, Mwalibora Nyanguri kuhamisha umiliki, kupangisha au kuombea mikopo.

Maombi hayo dhidi ya Chonji na mkewe yaliwasilishwa kwa hati ya dharura mahakamani hapo Septemba 13, mwaka huu mbele ya Jaji Wilfred Dyansobela.

AG aliiomba mahakama hiyo imzuie Chonji, mawakala wake au mtu mwingine yeyote kwa niaba yake, kuhamisha umiliki wa mali, kupangisha nyumba au kuombea mikopo (ili serikali ifuatilie uhalali wa upatikanaji wa mali hizo).

Mahakama hiyo imetakiwa kutoa zuio hilo kwa nyumba sita za Chonji zilizopo maeneo ya Magomeni, Tandale Ziota na Mbezi Juu jijini Dar es Salaam.

Nyumba hizo ni namba 95280 iliyopo Kiwanja Namba 43 Kitalu O, Namba 90292 iliyopo Kiwanja Namba 66 Kitalu P, nyumba iliyopo Kiwanja Namba 68 Kitalu X, nyumba yenye Mita ya Luku Namba 43001304757 na nyumba nyingine yenye Mita ya Luku Namba 04215118664.

Mali nyingine zilizowekewa zuio na kuwa chini ya serikali ni gari aina ya Mitsubishi Canter yenye namba za usajili T 376 BYY, Toyota Verossa yenye namba za usajili T 326 BXF na mali nyingine zote zenye jina au umiliki wa Kampuni ya Mumask Investment ambayo ipo chini ya mtuhumiwa huyo.

Katika maombi hayo, AG amemwomba Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni na Ofisa Mtendaji wa Mtaa (husika) wasipitishe uhamishaji wa umiliki wa nyumba hizo na mahakama imwamuru Msajili wa Ardhi kutambua kwamba nyumba hizo zimewekewa pingamizi.

Maombi hayo kwa mara ya kwanza yalitajwa katika mahakama hiyo Novemba 12, mwaka huu ambapo mahakama iliamuru wadaiwa kuwasilisha hati kinzani Novemba 26 (leo) na AG atajibu Desemba 3, mwaka huu na maombi yatasikilizwa Desemba 4, mwaka huu.

Chonji anakabiliwa na kesi ya jinai namba 50 ya mwaka 2014 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar ambapo anatuhumiwa kujihusisha na biashara haramu ya kusafirisha madawa ya kulevya yenye thamani ya shilingi 227, 374,500. Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Mkazi, Janet Kaluyenda.

Hata hivyo, katika Mahakama ya Kisutu kesi hiyo ilitajwa jana Novemba 25. 

Mtuhumiwa huyo anapelekwa mahakamani akitokea katika Gereza la Keko jijini Dar.

Akilifungua bunge mjini Dodoma, Ijumaa iliyopita, Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ alisema amedhamiria kupambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya ambapo alisema atashughulika zaidi na vigogo (wauzaji) badala ya vidagaadagaa (watumiaji) huku akisema kazi hiyo na ile ya kupambana na mafisadi ni sawa na kutumbua jipu na kujipambanua kuwa, anataka kuwa mtumbua majipu huku akitaka kusaidiwa na idara husika za kupambana na mambo hayo!Vitendea kazi alivyokutwa navyo.Mjengo anaomiliki.


via GPL

Polisi wafutwa kazi kwa ku-chat kuhusu utendaji wa viongozi wao


Polisi mkoani Kigoma imewafukuza kazi askari wake watatu kwa kusambaza taarifa za uongo kupitia mitandao ya kijamii juu ya utendaji kazi wa baadhi ya viongozi wa jeshi hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui amesema kutokana na utaratibu wa kijeshi, askari hao walichunguzwa na mashitaka yaliendeshwa dhidi yao kwa miezi mitatu kabla ya kuchukua uamuzi huo.

Amewataja askari waliofukuzwa kazi ni Koplo Johnson, PC Justine na WP Mercy ambao pamoja na kufukuzwa kazi, wamepewa nafasi ya kukata rufaa ikiwa hawakubaliani na hukumu waliyopewa.

“Askari huwa wanaajiriwa kwa cheti lakini wanafukuzwa kwa makosa ya utovu wa nidhamu na hili linachukuliwa kwa Askari yeyote bila kujali ukubwa wa cheo chake. Ni vema wakawa makini kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria za kijeshi ili kuepuka hali ya namna hii kutokea,” amesema Mtui.

Licha ya kushindwa kufafanua makosa hayo kuwa yalimlenga Kigogo gani wa Jeshi hilo, lakini habari za uhakika zilizopatikana katika Kituo cha Polisi kati mjini Kigoma zinaweka bayana kwamba askari hao watatu walitoa lugha za kejeli kwenye mitandao ya kijamii wakidai ziara ya Mkuu wa Jeshi hilo, IGP Ernest Mangu haikuwa na tija mkoani Kigoma.

“Hawa wenzetu waliofukuzwa walikuwa wanachati (wanaandika) kwenye mitandao wakijadili kama ujio wa IGP Kigoma unaonekana kuleta tija lakini ikatokea wakubwa wakapata taarifa hiyo na ndipo hatua zimechukuliwa dhidi yao,” amesema askari mmoja aliyekataa jina lake lisitajwe.

Kamanda Mtui ametoa wito kwa askari kuzingatia maadili ya kazi katika muda wote wanapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yao na hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka maadili ya kazi.

Hata hivyo, askari wote watatu waliofukuzwa kazi wanadaiwa kukata rufaa kupinga hukumu waliyopewa.

Mkuu wa Wilaya aagiza kukamatwa Mratibu Maabara kwa wiziMkuu wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga, Hafsa Mtasiwa ameagiza kukamatwa kwa mratibu wa maabara halmasharuri ya mji anayedaiwa kujaribu kuiba vifaa vya kupimia malaria, MRDT.

Mratibu huyo, Emanuel Masondole, anatuhumiwa kuchukua boksi la vifaa hivyo kutoka halmashauri ya wilaya ya Korogwe vijijini akidai Halmashauri ya Korogwe mjini anakofanya kazi kuna upungufu wa vifaa hivyo.

Kaimu Ofisa wa dawa wa halmashauri ya wilaya ya Korogwe Vijijini, Issa Mkwawa amesema tukio hilo limetokea Novemba 11 na vifaa hivyo vimerejeshwa juzi baada ya taarifa hiyo kusambaa.

Katika maelezo yake, mtuhumiwa amesema alifanya hivyo kwa ajili ya kuweka hifadhi ya kutosha ya vifaa hivyo, isipokuwa hakueleweka kwa utetezi wake kwa kuwa alikuwa na hifadhi ya kutosha.

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya amesema ni lazima mtumishi huyo achukuliwe hatua za kinidhamu ili kukomesha wizi wa dawa unaofanyika kwenye vituo mbalimbali vya afya.
''Vifaa hivyo ni vile vinavyouzwa kwenye maduka ya dawa na vituo vya afya, tunataka kukomesha tabia hiyo ambayo inaisababishia serikali hasara," amesema Mtasiwa.

Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, boksi hilo la vifaa vya MRDT vina thamani ya zaidi ya shilingi milioni sita.

Agizo la Mkuu wa Mkoa: Marufuku kuuza, kunywa pombe muda wa kazi


Bilioni 90/= zilivyopatikana ndani ya siku 20 za Urais wa MagufuliUamuzi wa Rais Dk. John Magufuli, kubana matumizi ya serikali kwa nia ya kuelekeza nguvu katika kushughulikia kero mbalimbali zinazowakabili wananchi, umeokoa wastani wa zaidi ya Sh. bilioni 90 katika siku 20 tangu aingie madarakani.

Dk. Magufuli ambaye aliapishwa Novemba 5, 2015 kufuatia ushindi wake wa asilimia 58.46 katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, ametangaza maamuzi kadhaa ya kubana matumizi ya serikali ili kuimarisha huduma za jamii.

Miongoni mwa maamuzi aliyofanya Rais Magufuli katika siku zake hizo 20 hadi kufikia jana ni pamoja na kusitisha safari holela za nje, kupiga marufuku michango ya aina yoyote kwa wanafunzi kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne na pia kuamuru kutengenezwa mara moja kwa mashine za vipimo vya CT-Scan na MRI katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kadhalika, wiki iliyopita, Rais Magufuli alitangaza pia kufuta sherehe za Uhuru zilizotarajiwa kufanyika Desemba 9 na kutaka siku hiyo iadhimishwe kwa kufanya usafi nchi nzima ili kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu.

Uchunguzi uliofanywa na Nipashe kupitia vyanzo mbalimbali umebaini kuwa katika kipindi hicho kifupi cha siku 20, maamuzi ya Rais Magufuli yameokoa kiasi hicho kikubwa cha fedha ambacho sasa chaweza kutumika kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kuchimba visima, kujenga zahanati, kununua magari ya kubebea wagonjwa, kununua madawati na pia kuweza kujenga viwanja vya soka walau viwili vyenye hadhi kama Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

1. MICHANGO SHULE YA MSINGI

Wakati akihutubia Bunge kuelezea mapitio ya kazi za wizara yake kwa mwaka wa fedha 2013/2014, aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, alisema wanafunzi wa darasa la kwanza walioandikishwa mwaka 2014 walikuwa 1,166,497.

Aidha, uchunguzi wa Nipashe hivi karibuni ulibaini kuwa gharama walizokuwa wakilipa wazazi kama michango pindi wakipeleka watoto wao kuandikishwa darasa la kwanza zilikuwa zikitofautiana kati ya shule moja na nyingine, mfano ni katika Shule ya Msingi Mabatini iliyopo Temeke jijini Dar es Salaam iliyokuwa ikitoza michango ya jumla ya Sh.25,000, Shule ya Msingi Kwembe wilaya ya Kinondoni Sh. 67,000 huku shule nyingi za msingi kadhaa za Wilaya ya Mtwara Vijijini zikiwaandikisha darasa la kwanza kwa michango yenye thamani ya jumla ya Sh. 9,000. Hivyo, wastani wa michango hiyo kwa shule walau tatu ni takriban Sh. 35,000.

Ingawa siyo shule zote za msingi zilizoanza uandikishaji darasa la kwanza kipindi hiki, bado hesabu zinaonyesha kuwa amri ya Magufuli ya kupiga marufuku michango ya aina yoyote kwa wanafunzi kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne imesaidia kuwapunguzia wazazi mzigo wa gharama zitokanazo na michango ya uandikishaji darasa la kwanza.

Kwa ujumla, kama kila mzazi nchini angeandikisha mwanawe darasa la kwanza kwa Sh. 35,000, na kama idadi ya wanafunzi hao ni sawa nay a mwaka 2014 ambayo ni 1,166,497, maana yake kiasi cha fedha za michango kwa wanafunzi wote milioni kingekuwa ni takriban Sh. bilioni 40.83. Amri ya Magufuli imeokoa fedha hizi kwani sasa wazazi hawatalazimika kuzitoa ili kaundikisha watoto wao.

2. SHEREHE ZA UHURU

Katika moja ya makala zilizopo kwenye tovuti yake, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika (Chadema), anasema gharama za sherehe za wiki ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru, Desemba 2011, zilikuwa ni zaidi ya Sh. bilioni 50.

Gharama hizi zilikuwa kubwa zaidi kutokana na ukweli kuwa sherehe hizi zilikuwa na upekee wa aina yake kwani ilikuwa ni nusu karne baada ya uhuru wa Tanganyika. Hata hivyo, chanzo kimoja kiliiambia Nipashe kuwa gharama za kawaida za sherehe za siku ya uhuru huwa siyo chini ya bilioni 29. Hizi huwa ni pamoja na maandalizi kabambe yanayohusisha gwaride la vikosi vyote vya ulinzi na usalama, ngoma, muziki, halaiki na pia kukaribisha viongozi wa mataifa mbalimbali wa ndani na nje ya nchi. Kadhalika, jioni ya siku ya Uhuru huwa na dhifa maalum ya chakula inayoandaliwa na mkuu wa nchi.

Gharama nyingine za siku hii ya sherehe za Uhuru huwa ni fedha za kulipa posho askari wanaoshiriki kwenye gwaride, watumishi wa umma na watoto wanaoshiriki maonyesho ya halaiki, vinywaji, mafuta ya magari, ndege, vifaru, vipeperushi, mapambo na gharama nyinginezo.

Kwa sababu hiyo, uamuzi wa Rais Magufuli kufuta sherehe za mwaka huu za Uhuru siku ya Desemba 9, 2015 na kutaka siku hiyo isherehekewe kwa kila mmoja kufanya usafi wa mazingira ili kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu umeokoa fedha hizo ambazo sasa zinaweza kuelekezwa katika maeneo mengine ya maendeleo.

3. SAFARI NYINGINE ZA NJE

Katika hotuba yake wakati akilizindua Bunge Novemba 20, 2015, Dk. Magufuli alisema anafuta safari zote holela za nje kwa sababu zimekuwa zikiligharimu taifa mabilioni ya fedha ambayo yangeweza kusaidia shughuli nyingine za maendeleo kama kujenga barabara za lami za urefu wa kilomita 400, kuchimba visima vya maji safi na salama na pia kujenga zahanati au kununua dawa ili kuondoa kero wanayopata wananchi waendapo kwenye hospitali za umma.
Katika kutoa mfano, Rais Magufuli alisema kuwa katika mwaka wa fedha wa 2013/2014 na sehemu ya 2014/2015, taifa lilitumia takriban Sh. bilioni 356. Kwa sababu mwaka mmoja huwa na siku 365, maana yake wastani wa matumizi ya serikali kwa safari za nje kila uchao ni takriban Sh. milioni 975.34. Hata hivyo, hesabu hizi ni kwa makadirio kuwa fedha alizotaja Rais Magufuli zilitumika kwa kipindi cha mwaka mmoja wa kalenda.

Kwa sababu hiyo, katika siku 20 za kuwa madarakani kwa Magufuli, yaani kuanzia Novemba 5, 2015 hadi jana Novemba 25, maana yake kama siyo amri ya Magufuli, kiasi cha fedha kilichopaswa kutumiwa na taifa kwa ajili ya safari za nje za vigogo ni takriban Sh. bilioni 19. 51 (yaani siku 20 x Sh. milioni 975.34). Ukiondoa kiasi kilichohesabiwa katika safari ya Jumuiya ya Madola, yaani takriban Sh. milioni 700, maana yake fedha zinazobaki kwa ajili ya safari nyingine za nje zisizokuwa za Jumuiya ya Madola ni Sh. bilioni 18.81. Wastani wa fedha zote hizo zimeokolewa na kutokana na amri ya Magufuli hadi kufikia jana na sasa zinaweza kufanya kazi nyingine za maendeleo.

4. VIPIMO CT-SCAN MUHIMBILI

Kabla ya kuapishwa kwa Magufuli, vipimo vya CT-Scan katika Hospitali ya Taifa Muhimbili vilikuwa vimesimama kufanya kazi kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni ubovu, na pia kuwapo kwa mgogoro wa malipo baina ya hospitali hiyo na kampuni iliyokuwa zabuni ya kufanya matengenezo.

Baadhi ya taarifa zilieleza kuwa kifaa hicho kiliharibika tangu Agosti 30, 2015, hivyo kwa ujumla hadi kufikia jana (Novemba 25, 2015), tayari zilishatimia siku 85 ziliopita bure bila kifaa hicho kufanya kazi.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma za Jamii wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaeshi, CT-Scan inapofanya kazi huhudumia watu 25 hadi 40 kwa siku. Gharama wanazolipia wagonjwa huwa ni kati ya Sh. 100,000, Sh. 170,000 au Sh. 250,000, kutegemeana na kundi la malipo la mgonjwa kuwa ni wa ‘private’, ‘general’ au mwenye kadi ya Bima ya Afya.

Kwa sababu hiyo, ikiwa itachukuliwa kwamba kila mgonjwa huwa wa kujilipia binafsi (private) na hivyo kulipa Sh.250,000 ili kupata huduma ya CT-Scan, maana yake gharama zinazokosekana kwa siku kutokana na vifaa hivyo kutofanya kazi yake huwa ni Sh. 10,000,000; yaani 250,000 x 40. Jumla ya gharama hizi hadi kufikia jana ambayo ni siku ya 85 tangu kuharibika kwake ni Sh. milioni 850.

Hata hivyo, gharama hizo sasa zinaelekea kukomeshwa kwani Rais Magufuli ameingilia kati kwa kutimua Bodi ya Hospitali hiyo, kumuengua aliyekuwa akikaimu nafasi ya ukurugenzi na pia kuamuru kutengenzwa vipimo hivyo mara moja. Mafundi wameshaingia kazini na vilitarajiwa kukamilika jana.

5. HAFLA KUPONGEZA WABUNGE

Hii ni tafrija maalum iliyokuwa imeandaliwa na Bungeni mkoani Dodoma kwa nia ya kupongezana kufuatia ushindi walioupata katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, kuapishwa na mwishowe Rais Magufuli kulizindua Bunge lao la 11, Ijumaa ya Novemba 20, 2015.

Kwa kawaida, hafla za namna hii ambazo huwakutanisha wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kisha Rais kukaribishwa, huwa na mbwembwe za kila namna. Waheshimiwa wabunge hula na kunywa watakavyo huku wakiburudika kwa muziki wa ‘live’ kutoka kwa bendi maarufu za muziki wa dansi nchini.

Ili kufanikisha sherehe hizo, yaelezwa kuwa fedha kiasi cha takriban Sh. milioni 225 kilichangishwa. Hata hivyo, bahati mbaya sana kwa waheshimiwa wapya wa Bunge la 11, Rais Dk. Magufuli hakukubaliana hata kidogo na matumzi ya mamilioni yaliyochangwa. Mwishowe, badala ya kuzimwaga fedha zote hizo kwenye sherehe, akaamuru zitumike kati ya Sh. milioni 10 na Sh. milioni 15 tu, kisha kiasi chote kilichobaki cha Sh. milioni 210, kielekezwe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kitumike kununua vitanda na kuwaondolea wagonjwa adha ya kulala sakafuni.

Kufika Jumatatu, ikiwa ni siku mbili tu baada ya Magufuli kutoa agizo hilo, vitanda 300 vilinunuliwa kwa kutumia fedha hizo, pmoja na ziada ya mashuka 600. Viotu hivyo vyote vimeshafikishwa Muhimbili na wagonjwa wangali wakinufaika na uamuzi huo wa Rais Magufuli.

6. VIPIMO MRI MUHIMBILI

Kama ilivyokuwa kwa CT-Scan, mashine ya kipimo cha MRI pia iliharibika kwa takriban siku 85 hadi kufikia jana. Kwa mujibu wa Eligaeishi, wastani wa watu wanaopata huduma ya kipimo hiki kwa siku huwa ni 10 hadi 15 na gharama huanzia Sh. 160,000 kwa wagonjwa wa kundi la jumla (general), Sh. 350,000 kwa walio na kadi za Bima ya Afya na Sh. 450,000 wanaojilipia binafsi (private).

Ikiwa wahitaji wote wa huduma ya MRI ni wa kundi la private, yaani wanaojilipia Sh. 450,000, na ikiwa vipimo hivyo huhudumia idadi ya juu ya wahitaji ambayo ni watu 15, maana yake serikali ilikuwa ikipoteza takriban Sh. milioni 6.75 kila uchao au Sh.milioni 573. 75 kwa siku zote 85 hadi kufikia jana.

Hata hivyo, mzigo wa gharama zote hizo zinazotokana na ubovu wa kipimo hicho zinaelekea kukomshwa kwani kutokana na amri ya Magufuli, tayari mafundi walishaingia kazini tangu wiki iliyopita na kipimo hicho kinatarajiwa kuanza kazi leo.

7. SAFARI JUMUIYA YA MADOLA

Siku moja tu baada ya kuapishwa Novemba 5, 2015, Rais Dk. Magufuli alitoa maagizo kadhaa yakiwamo ya kuzuia safari holela za nje nchi. Alisema panapokuwa na ulazima, safari yoyote ni lazima iidhinishwe na yeye (Rais Magufuli) au Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, lengo likiwa ni kupunguza matumizi ya serikali ili fedha zinazookolewa zitumike kuboresha huduma za jamii.

Kutokana na agizo lake hilo, Rais Magufuli ameripotiwa kufyeka msafara mzito uliopaswa kuongozwa na yeye mwenyewe na vigogo wengine serikalini takriban 50 kwenda kwenye mkutano wa wakuu wa Jumuiya ya Madola unaofanyika barani Ulaya, katika kisiwa cha Malta.

Ikiwa ni sehemu mojawapo ya kubana matumizi, yaelezwa kuwa ni watu wanne tu ndiyo walioruhusiwa kwenda kwenye mkutano huo kumuwakilisha Rais Magufuli na timu yake yote iliyopaswa kuwa kisiwani humo kwa wiki nzima, ambao ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, balozi mwingine mdogo na maafisa wengine wawili wa ofisi za ubalozi huo zilizopo jijini London, Uingereza. Uamuzi huu umeokoa matumizi ya serikali yatokanayo na gharama za tiketi za ndege na posho za vigogo waliopaswa kusafiri kutoka takriban Sh. milioni 700 hadi Sh. milioni 49.9 tu.

BILIONI 90.97/- ZAWEZA KUFANYA NINI?

Kwa ujumla, wastani wa fedha zilizookolewa kutokana na maamuzi mbalimbali ya Rais Magufuli ndani ya siku 20 za kuwapo kwake madarakani, yaani Sh. bilioni 90.97, zaweza kufanya mambo mengi ya maendeleo kwa taifa.

Kwa mfano, akizungumza na Nipashe juzi, Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu, alisema wastani wa gharama za kukamilisha ujenzi wa zahanati hadi kukamilika katika jimbo lake ni Sh. milioni 50.

Kwa sababu hiyo, kama fedha hizi zikielekezwa katika kujenga zahanati za kiwango sawa na kile cha Singida Magharibi, maana yake zaweza kukamilishwa zahanati 1,819.

Wakati Uwanja wa Taifa ukikamilishwa mwaka 2009, gharama zake zilitajwa kuwa ni takriban Sh. bilioni 56. Kwa sababu hiyo, ikiwa fedha zilizookolewa na Magufuli katika siku 20 za kuwa madarakani, yaani Sh. bilioni 90.97 zingeelekezwa kujenga viwanja vya namna ya ule wa Taifa na kutumia hesabu za wakati huo, maana yake kungekuwa na uwanja mmoja uliokamilika na mwingine wa pili ungefikia katika hatua muhimu ya kuukamilisha.

Akizungumza na Nipashe, Kingu (Mbunge wa Singida Magharibi) alisema wastani wa bei ya bati moja la migongo myembamba mkoani Singida ni Sh. 15,000. Kadhalika, bei ya mfuko mmoja wa saruji ya ujazo wa Kilogram 50 huuzwa pia kwa Sh. 15,000. Kwa sababu hiyo, kama fedha hizi zilizookolewa na Rais Magufuli katika siku 20 za kuwa kwake madarakani zingeelekezwa kununua vitu hivyo kwa bei kama ya Singida, maana yake ingepatikana mifuko 6,064,667 ya saruji au mabati ya idadi kama hiyo.

Aidha, kwa mujibu wa Kingu, gharama ya kuchimba kisima cha maji safi kwenye jimbo lake huwa ni wastani wa Sh. milioni 15. Hivyo, kama fedha zilizookolewa kutokana na maamuzi ya Rais Magufuli katika siku 20 za kuwa kwake madarakani zitaelekezwa kuchimba visima vya kiwango sawa na vile vya Jimbo la Singioda Magharibi, maana yake vyaweza kupatikana visima 6,065.
  • Taarifa hii imenukuliwa kutoka kwenye gazeti la NIPASHE

Ubashiri wa gazeti la Nipashe wa Wizara 9 zilizofutwa katika Awamu ya TanoWakati kukiwa na taarifa kwamba Rais Dk. John Magufuli, anatarajia kupunguza karibu nusu ya wizara zilizokuwapo kwenye Serikali ya Awamu ya Nne, imefahamika kuwa wizara zinazolengwa ni zile zilizopo Ofisi ya Rais, Makamu wa Rais na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Chanzo kimoja kutoka serikalini kimeiambia Nipashe jana kuwa wizara hizo zitaunganishwa kwenye wizara mpya zitakazoanzishwa na Rais ambaye ameweka mkakati wa kuwa na baraza dogo la mawaziri.

Wizara zinazotajwa kufyekwa ni
  1. Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji
  2. Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Kazi Maalum
  3. Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu
  4. Wizara Ofisi ya Waziri Mkuu na Sera, Uratibu na Bunge
  5. Wizara Ofisi ya Rais, Utawala Bora
  6. Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma
  7. Wizara ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
  8. Wizara ya Nchi, Ofisi Makamu wa Rais Mazingira 
  9. Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Kadhalika, katika mabadiliko hayo, wizara nyingine zitaguswa ili kufikia malengo ya kubakia na wizara chache kutimiza dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano kubana matumizi na kuinua maisha ya Watanzania.

Chanzo hicho kimebainisha kuwa Rais Dk. Magufuli atalitangaza Baraza la Mawaziri ndani ya wiki hii ingawa bado kumekuwa na usiri wa siku halisi atakayotangaza. Juzi, chanzo kingine kiliiambia Nipashe kuwa tayari Rais Magufuli kwa kushirikiana na wasaidizi wake, ameshakamilisha sehemu kubwa ya mchakato wa kuunda baraza lake la mawaziri.

Serikali ya Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete, ilimaliza muda wake Novemba 5, mwaka huu ikiwa na wizara 30. Vile vile, alipoingia kwa mara ya kwanza mwaka 2005, Rais Kikwete alikuwa na serikali kubwa yenye mawaziri na naibu wao zaidi ya 60.

Wawili wasimamishwa kazi kwa wizi wa dawa za kituo cha afya

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga, Boniface Chambi wakiwa katika chumba cha kuhifadhia dawa walipofanya ziara ya kushitukiza katika kituo cha afya Kambarage
Picha, taarifa:  Kadama Malunde-Malunde1 blog

Novemba 26, 2015 asubuhi... Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro anafanya ziara ya kushitukiza katika kituo cha afya cha Kambarage katika manispaa ya Shinyanga ili kujionea hali halisi ya huduma zinazoendelea katika kituo hicho.

Kubwa zaidi lililomfikisha hapo asubuhi asubuhi ni kuhusu sakata la muuguzi wa kituo hicho Joseph Nkina kukamatwa na wananchi akiwa na dawa za serikali ikiwemo kopo moja la dawa aina ya paracetamol na chupa mbili za dawa ya maji aina ya Erythromycin kinyume na utaratibu. [Taarifa hiyo iliripotiwa jana hapa.]

Baada ya kukutana na uongozi wa kituo hicho na wananchi waliofanikisha kukamatwa kwa muuguzi mkunga wa kituo hicho Joseph Nkila amemwagiza mkurugenzi wa manispaa hiyo kumsimamisha kazi muuguzi huyo kuanzia leo Novemba 26,2015, ili kupisha uchunguzi wa tukio hilo.
“Nimekuja hapa kuona uhalisia wa jambo hili. Kuna ushihidi wa wazi kabisa kuwa muuguzi huyu kweli kaiba dawa za serikali,mbaya zaidi akataka kudanganya kwa kuchukua stakabadhi kutoka kwenye duka la dawa za binadamu (pharmacy), nimekutana na msimamizi wa kituo cha afya Kambarage na mfamasia anayetunza dawa na kinachoonekana hapa ni uzembe kwenye uongozi kwani dawa zinatoka bila kufuatiliwa kuwa dawa hizo zinafanya nini”“Nitamshangaa sana hakimu atayepindisha kesi hii kwani ushahidi uko wazi kabisa kutoka kwa wananchi kwamba amekuwa akijihusisha na wizi kwa muda mrefu na kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu katika kituo hiki cha afya,wananchi wananyimwa dawa,kumbe watu wachache tu wanacheza mchezo huu mchafu wa kuiba dawa,”“Kila siku wananchi wanalalamika hakuna dawa,lakini tumeangalia stoo tumekuta dawa zipo za kutosha na Shinyanga hatuna tatizo la dawa,dawa moja tu ambayo ni Antibiotic ndiyo haipo,na tumeagiza iletwe,”“Cha kusikitisha msimamizi wa kituo hiki Dkt Nassoro Yahya anasema hakuna upotevu wa dawa, huyu naye hatakiwi kuwa hapa kazi imemshinda, nimemwagiza mkurugenzi pia amsimamishe kazi kwani haiwezekani dawa zitoke kwenye kituo bila yeye kufahamu,” amesema Matiro.
Katika hatua nyingine Matiro amewashukuru na kuwapongeza wananchi waliofanikisha kumkamata muuguzi huyo na kuahidi kuwapa zawadi kwa kazi nzuri waliyofanya akiwataka wananchi wengine kuendelea kuwafichua watumishi wasiofanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi zao.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa onyo kwa muuguzi aliyekamatwa,ndugu na marafiki kuacha kutoa vitisho kwa wananchi waliokamata dawa hizo na kufanikisha juhudi za kukamatwa kwa muuguzi huyo kinyume na hapo hatua kali za kisheria zitachukulia dhidi yao. 


Hapa ni ndani ya ofisi ya mganga mkuu/msimamizi wa kituo hicho ambapo mkuu wa wilaya akiwa ameambatana na maafisa wengine wa manispaa ya Shinyanga amekutana na uongozi wa kituo hicho pamoja na wananchi waliomkamata muuguzi mkunga wa kituo hicho Joseph Nkila akituhumiwa kuiba dawa za serikali. Kulia ni Rashid Shaban akimweleza mkuu huyo wa wilaya jinsi walivyofanikisha kufichua wizi huo. Mwenye koti na suruali ya khaki ni msimamizi wa kituo hicho, Dkt Nassoro Yahya. Kaimu mganga mkuu wa manispaa ya Shinyanga Dkt Mhana Raphael (mwenye suti pichani). Wa pili kulia ni Mfamasia/mtunza dawa wa kituo hicho, Seleman Hamza.


Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akiwa katika kituo cha afya Kambarage, nyuma yake ni katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniface Chambi na kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Sande Deogratius


Mfamasia/mtunza dawa wa kituo cha afya Kambarage Seleman Hamza akizungumzia kuhusu tukio la wizi wa dawa katika kituo hicho na changamoto ya dawa katika kituo hicho ambapo alisisitiza kuwa kuna baadhi ya dawa hazipo katika kituo hicho


Dawa katika kituo cha afya Kambarage


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoka kwenye kituo cha afya Kambarage


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa maelekezo kwa kaimu mganga mkuu wa manispaa ya Shinyanga Dkt Mhana Raphael (mwenye suti), kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Sande Deogratius na mfamasia wa manispaa ya Shinyanga Emmanuel Zablon

Kenya: Wamtaka Gavana aeleze vipi katumia milioni 400/= kwa shughuli ya Magufuli
Gavana wa Jimbo la Siaya, nchini Kenya, Cornel Rasanga ameingia matatani akidaiwa kutumia Sh20 milioni za nchi hiyo (karibu Sh400 milioni) kutoka katika mfuko za Serikali kwa ajili safari ya kuhudhuria sherehe za kumwapisha Rais John Magufuli.

Dk Magufuli alipishwa Novemba 5, kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Oktoba 25.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kenya (PAC), Nicholas Gumbo amemtuhumu Rasanga kwa kutumia fedha hizo kutoka kwenye mfuko wa Serikali wa safari.

“Gavana wa Rasanga lazima awaambie wananchi wa Siaya, imekuwaje akatumia Sh20 milioni kwenda Tanzania kwa ajili ya shughuli ya Dk Magufuli?
“Sidhani kama Dk Magufuli ana uhusiano wowote na wananchi wa Kaunti ya Siaya kiasi cha Gavana kutumia fedha hizo za umma kwenda Tanzania,” alisema Gumbo.

Gumbo alisema Dk Magufuli anafahamika kuwa ni rafiki mkubwa wa kiongozi wa Cord, Raila Odinga ambaye pia alihudhuria sherehe hizo.

Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na viongozi wengine wa Afrika.

Akizungumzia tuhuma hizo, Rasanga alisema madai yalitolewa na Gumbo ambaye ni Mbunge wa Rarieda, ni uzushi na alikuwa anataka kujikweza kisiasa.

“Hii ilikuwa safari binafsi. Hatukutumia fedha za Serikali kama inavyoelezwa,” alisema alipohojiwa na gazeti la Daily Nation.

Gavana huyo alisema alikwenda kuhudhuria kuapishwa kwa Dk Magufuli kwa mwaliko binafsi wa Rais hiyo wa Tano wa Tanzania.

Hata hivyo, alisema ziara yake Tanzania itasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza ushirikiano katika Ukanda wa Ziwa Victoria.

“Ukweli ni kwamba Rais wa Tanzania aliwahi kutembelea Siaya na tulijadiliana masuala mbalimbali ikiwamo usafiri hasa katika Ziwa Victoria,” alisema Rasanga na kuongeza:
“Dk Magufuli anatokea Kanda ya Ziwa na mpango wake mkubwa ni kuimarisha bandari katika Ziwa Victoria na kuchaguliwa kwake kuwa Rais kutarahisisha zaidi utekelezaji wa mipango yake.
“Hakuna sababu ya kuingiza siasa katika safari hii. Tuko katika mipango mizuri tu ya kibiashara na Tanzania ambayo kwa sasa imeanza kupanuka.”

Mwenyekiti huyo wa PAC Kenya alisema safari hiyo ya Novemba 5, ni matumizi mabaya ya rasilimali za umma.

Hata hivyo, Naibu Gavana, Wilson Ouma alipinga madai ya Gumbo akisema alikuwa na lengo la kumharibia bosi wake.

“Ukweli Gavana Rasanga alitumia fedha zake kwenda Tanzania na uzushi wowote unatakiwa ukomeshwe,” alisema Ouma alipozungumza na Nation.

Akisisitiza, Gumbo alisema ataendelea kupambana na matumizi mabaya ya fedha za umma unaofanywa na maofisa wa Serikali kwa kutumia vyeo vyao.

Wapo wanaosubiri kuona kama ataugusa huu...


Kosa letu...?


[update] Ratiba. Uamuzi wa mahakama kuhusu maziko ya Alphonce MawazoRatiba ya shughuli ya utoaji heshima za mwisho na mazishi ya Kamanda Mawazo


Kesho Siku ya Ijumaa, Novemba 27 saa 2 asubuhi, mwili wa Mpiganaji na Kiongozi wetu Alphonce Mawazo utachukuliwa Hospitali ya Bugando kuelekea nyumbani kwa Baba yake mdogo, eneo la Nyegezi-Swea kwa ajili heshima za familia kabla ya kuelekea Viwanja vya Furahisha ambapo Viongozi waandamizi wa UKAWA, wakiongozwa wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, Mgombea Urais Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye, wabunge wa UKAWA, wataongoza maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza na vitongoji vyake kutoa heshima za mwisho kwa mpendwa wao Mawazo.

Baada ya Viwanja vya Furahisha, mwili wa Mpiganaji Mawazo utasafirishwa kuelekea Geita kwa ajili ya kuwapatia nafasi wakazi wa Mkoa wa Geita kumuaga Kiongozi wao siku ya Jumamosi, Novemba 28 kuanzia asubuhi mapema ambapo baadae mchana mwili huo utapelekwa Mji Mdogo wa Katoro, mkoani Geita, ambapo pia wananchi watapata fursa ya kumpatia heshima za mwisho na kumuaga Mawazo ambaye alikuwa ni Mgombea wao wa Ubunge wa Jimbo la Busanda.

Baada ya wakazi wa Katoro kushiriki tukio hilo, mwili wa Kamanda Mawazo utapelekwa nyumbani kwao kijijini Chikobe tayari kumhifadhi kwenye nyumba ya milele shambani kwake, siku a Jumapili, Novemba 29, baada ya familia, ndugu, jamaa na wakazi wa kijiji hicho kutoa heshima zao za mwisho.

Makene Tumaini 
Afisa Habari Chadema


Mahakama kuu kanda ya Mwanza imetoa hukumu ya kuondoa zuio la kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza la kuinyima familia ya aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kibali cha kuuaga mwili wa marehemu Alphonce Mawazo katika jiji la Mwanza.

Hukumu ya kesi hiyo iliyovuta umati mkubwa wa wakazi wa jiji la Mwanza na mikoa jirani ya kanda ya ziwa, imetolewa leo mchana na jaji Lameck Mlacha, baada ya familia ya marehemu kupitia kwa baba yake mdogo mchungaji Charles Lugiko kufungua kesi ya madai dhidi ya kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza na mwanasheria mkuu wa serikali ya kupinga marufuku ya jeshi la polisi mkoani humo kuaga mwili wa Alphonce Mawazo kwa madai kwamba jijini Mwanza kuna mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu na taarifa zao za kiitelejensia zilibaini kwamba kungetokea uvunjifu wa amani.

Akisoma hukumu hiyo iliyochukua muda wa saa moja na dakika 33, Mhe. Jaji Lameck Mlacha amesema kuwa baada ya kupitia maombi ya mapitio ya Charles Lugiko dhidi ya kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza chini ya hati ya dharura, ameona kuna utofauti mkubwa katika zuio hilo na kusema kuwa marehemu ana haki zote za kuagwa na ndugu, jamaa, marafiki na wafuasi wa chama chake na pia anayo haki ya kufanyiwa taratibu za ibada, huku akiongeza kwamba mtu asiangaliwe kwa historia yake ya nyuma bali aangaliwe sasa.

Amesema kama kamanda wa polisi alikuwa na taarifa za kiitelenjesia hakuwa na sababu ya kuweka katazo, bali alitakiwa kuwaita ndugu na viongozi wa CHADEMA na kuzungumza nao kwa ajili ya kujitetea na wala si kuwanyima haki yao ya kikatiba, kwani haki ya kisheria ilikuwa ni kuwaita wote.

Baada ya kutoa hukumu hiyo, Jaji Lameck alitoa maelekezo ya kuzingatiwa na pande zote mbili, ambapo amesema mtoa maombi ambaye ni baba mdogo wa marehemu Alphonce Mawazo, mjibu maombi wa kwanza – kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza na viongozi wa CHADEMA wakutane haraka kwa ajili ya kuweka taratibu za ibada na kuaga mwili.
Agizo la marufuku ya kutengeneza na kuchapisha kadi za sikukuu kwa gharama za serikali


Rais Magufuli afika ofisini kwa Waziri Mkuu, MajaliwaRais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa wakati alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam leo Novemba 26, 2015 na kuzungumza nae kwa takribani saa moja.

Rais John Pombe Joseph Magufuli akitia saini kitabu cha wageni wakati alipomtembelea Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa ofisini kwake jijini Dar es salaam leo Novemba 26, 2015 na kuzungumza nae kwa takribani saa moja

Rais John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa wakati alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam Novemba 26, 2015. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Report: Tanzanians say "no change" in water sector one year after Big Results Now

Only 1 out of 3 citizens have access to piped water
One year after implementation of Big Results Now in water sector, citizens report no change

26 November 2015, Dar es Salaam: 
Just over one out of three citizens (36%) has access to piped water. The majority of citizens rely on either wells (35%) or surface water (18%), which are generally less hygienic sources. The difference between urban and rural areas is significant: half of urban residents (51%) have access to piped water on their premises compared to only 11% of rural citizens. Despite the introduction of the Government’s Big Results Now, and expiry of the Millennium Development Goals, access to piped water has been static in the last year. Overall only 41% of rural residents have access to any kind of improved water source as compared to 69% of citizens in urban areas.

These findings were released by Twaweza in a research brief titled Half empty or half full? Citizens’ views on accessing clean water. The brief is based on data from Sauti za Wananchi, Africa’s first nationally representative high-frequency mobile phone survey. The findings are based on data collected from 1,852 respondents across Mainland Tanzania (Zanzibar is not covered in these results) between 9 and 26 September 2015.
Close to half (44%) of citizens spend over 30 minutes collecting water for their needs, while the government guideline recommends that citizens should not spend more than half an hour per trip to collect water. In both urban and rural areas, around one out of three citizens in both urban and rural areas cite the lack of water points as a major challenge. 
In general, citizens experience a range of issues in accessing water, with significant differences in the experiences of rural and urban communities. Rural residents emphasize the distance to water points (47%) and dirtiness of the water (40%), while urban residents are troubled by irregular supply (43%) and cost (40%).
Just over half of citizens (57%) report doing something to make their drinking water safe. The majority of these say that they boil the water (85%). Other popular alternatives are straining (69%) or letting the water stand and settle (38%), but these are not considered, by international standards, to be acceptable methods of water treatment.
Unsurprisingly, 65% of citizens see access to clean water as the major challenge facing their community. Despite two years of the Big Results Now initiative, most citizens (80%) report seeing no change in the water sector over the past two years.
In recent months there has been significant media coverage of Cholera outbreaks in the country. Cholera spreads through contaminated water, among other things. However, here the story is more optimistic as only 6% of citizens have seen or heard of someone diagnosed with Cholera in the four weeks before the survey.
Aidan Eyakuze, Executive Director of Twaweza said “The saying goes, Maji ni Uhai (Water is Life). Sadly for too many Tanzanians, water can actually be deadly. Years of data have shown us that merely increasing resources does not improve access to safe, clean water. As the new government begins its work, we have a unique opportunity to radically review our strategies in the water sector. Providing every citizen with water in a sparsely populated, large country such as Tanzania is particularly challenging. But there is no escaping the need to reach every citizen with this vital service. So, we have no choice but to think quickly and creatively to guarantee citizens’ basic right of access to clean and safe water.”

Ask Mo anything. Muulize Mo lolote.Msomaji na mdau wa mtandao wako wa habari www.modewjiblog.com unakupa nafasi wewe kumuuliza maswali/swali lolote lile Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL Group, Mohammed Dewji. 

Maswali yote yatajibiwa na kutolewa ufafanuzi wa kina. Tutakuwa na mahojiano naye karibuni.

Utaratibu wa kumuuliza maswali ni kwa kukomenti kwenye post hii kisanduku cha maoni, zingatia kanuni na sheria ikiwemo kutotumia lugha zisizo rasmi.

Pia waweza kutoa maoni yako kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ukiwemo ukurasa wa Mohammed Dewji, facebook.com/mohammeddewjitz au ukurasa wa Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL)  facebook.com/MeTLGroup/photos