Orodha ya wadaiwa sugu wa kodi ya majengo katika manispaa ya Kinondoni

HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI.

TAARIFA KWA UMMA

ORODHA YA WADAIWA SUGU WA KODI YA MAJENGO NDANI YA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI


Jina la mdaiwa na tarakimu ya kiasi cha fedha anachodaiwa

1 Local Government Pension Fund 331,400,000.00
2 IMTU UNIVERSITY Mbezi Beach A 320,000,000
3 Land Mark 126,773,280
4 Basic Element Ltd mikocheni 103,604,000
5 21st Century Packaging Ltd 90,865,256.00
6 Wellworth Hotel and Lodge Ltd 51,000,000.00
7 Continental Services Ltd 48,991,090.00
8 Uzibora Tanzania Ltd 39,441,952.00
9 Hope Shopping Centre 33,696,000.00
10 Mahando Enterprises Ltd 42,099,838.00
11 Sky properties Ltd 19,918,080.00
12 The Orchard inn Ltd Royale 137,800,000.00
13. NavitejBains Masaki, plot no.1403, Block 1 61,200,000.00
0777400000
14. GulamDewji Oysterbay, house no. MSN/OBY/301 8,618,400.00
0754600000
15 Rostam Aziz 2,925,000.00
16. George Madafa 5,988,875.00
17 Amverton Tower Plot1127, masaki 8,170,052.00
18 D.K.R. Towers 39,757,910.00
19 Winstone N. Mogohile Oysterbay,House MSN/OBY/3 22,121,708.00 0754784472, 0755327438
20. Thomas Masawe 36,334,958.00
21. RukiaSimbakalia 64,842,381.00
22 Synergy Lounge Grill 5,400,000.00
23. Nirvana PropertiesLtd Masaki Plot no. 463 15,000,000.00
24. Avic International Ltd and Majogo 36,000,000.00
25. Tazama pipe line Plot no. 379, block 1Masaki 6,750,000.00
26. Tan House 72,754,200.00
27. Bahari Beach Hotel Kunduchi, Mtongani 96,307,864.00
0779905078
28. Jangwani Sea Breeze 55,500,000.00
29. Erick Shigongo Bonde la Mpunga,plot no.776, Msasani Beach
27,000,000.00
0754290167
30 TCRA 42,212,624.00
0754997991
31. Oilcom 22,212,624.00
32. NIT 22,162,688.00
0712004929
33. Repoa 4,136,612.00
34. AbigalKaugwa 71,463,178.00
35. Paradigms 5,000,000.00
36. University of Dar es Salaam- Kijitonyama 45,824,649.00
37. FatemaGhadiyalShabir 25,600,000.00
38. Kwanza International 11,025,360.00
39. ShashikantBatuklal Plot 303 Msasani 14,000,000.00
40. Gregory Mutungi Plot 1079 masaki 4,500,000.00
41. Frank Karage Plot 408 block 1 masaki 2,682,720.00
42. RostamAzizi Plot no. 42, Oysterbay 2,925,000.00
43 Daniel NziraYona Plot no. 439, Block 1 Masaki 6,000,002.00
44. Kid time nursery School masaki 2,181,720.00
45. Joseph Leon Simbakalia 1,468,128.00
46 MO HA NS Plot no. 1796, block 4, masaki 3,363,750.00
47. The Oyster appartment Masaki, house .MSN/MSK/16 20,000,000.00
48. Melisa Katara Masaki, plot no. 1003, block 2 4,050,000.00
49. Steven James Mbwana Masaki, plot 309 10,125,000.00
50. BasiliPesambiliMramba Masaki, Plot no. 281 742,500.00
51. Village Walk Masaki, Plot no.435 16,200,000.00
0789333396
52. Al-irshaad Nursery and Primary School Masaki, Plot no. 1357 12,000,002.00
0775550555
53. Hitesh Hasmukhlal Shah Masaki, Plot no.1787 887,870.00
0754288441
54. Jitu Patel Masaki 1,200,000.00
55. Tanzania Postal Corporations 16,621,130.00
56. NavitejBains Masaki 9,120,000.00
57. George Madafa Oysterbay, House no. MSN/OBY/281 5,988,875.00 0784761555
58. Institute of Finance Management Oyster bay-Haillesellasierd 3440,123.00
59 The Royale Orchard inn Ltd Masaki, Kaolest 7,880,000.00
60. NHC 305,426,886.00
61. International Baptist church Makumbusho-Sokoni street 1,320,084.00

Imetolewa na:
ENG.MUSSA NATTY
MKURUGENZI
MANISPAA YA KINONDONI

Easy cellphone hacks: A stand/holder with eye glass or cardboard or paper clip or cassette tape; A cover from balloonFAO analysis of price incentives for cashew nuts in Tanzania 2005–2013

previewThis technical note aims to measure, analyse and interpret price incentives for cashew nuts in the United Republic of Tanzania over the period 2005-2013. 

The results and recommendations presented in this analysis of price incentives can be used by stakeholders involved in policy-making for the food and agriculture sector. 

They can also serve as input for evidence-based policy dialogue at the national, regional or international level.

UNICEF Tanzania Situation Report - Burundi Response, 25 November 2015

previewHIGHLIGHTS
 • The rains that started in October continued this month causing several challenges:
 • increasing the risk of cholera and malaria;
 • flooding latrines, tents and temporary shelters; and
 • slowing down transport of refugees, aid workers, and supplies.
Situation Overview & Humanitarian Needs Throughout November the flow of refugees from Burundi has not subsided with 2986 new refugees arriving in Tanzania since end October for a total of 113,341 new arrivals since May. Although the average in November comes to 100 arrivals per day the real numbers swing from nearly zero to over 400 per day – a pattern that is not steady or predictable. As the situation in Burundi remains a concern UNICEF is working closely with partners and stakeholders on a new action plan in case of accelerated influx of asylum seekers. The main assumptions are that: (1) the old camp, Nyaragusu, could not accommodate new arrivals as it is already overcrowded with many flood prone areas; (2) newly opened Nduta camp and soon to open Mtendeli camp could take on up to 58,000 new arrivals (though with very limited services and needing some weeks to prepare for this) and (3) border entry points and way stations need to be upgraded to prepared for up to 1000 asylum seekers per day.

New arrivals are moved straight to the Nduta camp, which is slowing down the relocation of refugees from the flood prone areas of Nyaragusu camp. The longer that refugees remain in temporary mass shelters in Nyaragusu camp the more they are at risk from the current rains that are inundating latrines, mass shelters and temporary schools in low lying areas. The third camp, Mtendeli, is still being prepared for new arrivals. Humanitarian agencies must spread resources on several fronts to ensure that services are delivered and to be ready for new influxes at any point and at any time. The rainy season has further complicated this process raising the risk of disease outbreaks and hindering logistics.

Serikali: Tunawapima mabalozi wetu - Balozi umeleta watalii au kuhamasisha wawekezaji wangapi?

Mabalozi kutokuwa na utaalamu

Uwezo wa mabalozi kushiriki kikamilifu kwenye masuala ya kitaalamu pia ni moja ya mambo yanayoonekana kuwa kikwazo kwa agizo la Rais Magufuli kuzuia safari za nje.

Lakini Balozi Sefue alisema matukio yanayohusu masuala ya kitaalamu kama kilimo, mazingira, afya, madini na mawasiliano ambayo yanahitaji watendaji waliobobea kwenye fani hizo, yatawekewa utaratibu licha ya kuwa changamoto kwa mabalozi.

“Kila ubalozi una wataalamu wa masuala mbalimbali ambao wanaweza kutoa mchango unaostahili kwa lolote linaloweza kuhitajika,” alisema.

“Si rahisi kukosa mtu mwenye uwezo wa kumsaidia balozi kutekeleza majukumu yake kiasi cha kuhitaji mtu mwingine kutoka nyumbani. Lakini likijitokeza hilo, tutatuma mwakilishi.”

Akizungumzia suala hilo, Balozi Mulamula alisema mapema mwezi huu kuwa utekelezaji huo utachukua muda kidogo kutokana na balozi nyingi kukosa fedha na watalaamu.

Suala la fedha kwenye balozi za Tanzania limekuwa kilio kikubwa kila wakati wa Bunge la Bajeti na mwaka huu suala hilo liliibuka kwenye hotuba ya kambi ya upinzani iliyosema kiasi cha Sh30 bilioni ziloizotengwa kwa wizara hiyo hazikutosha kuwawezesha mabalozi kufanya kazi yao kwa ufanisi.

Suala la weledi pia lilizungumzwa kwenye hotuba ya kambi ya upinzani ya mwaka 2014/15 ikisema uteuzi holela wa mabalozi usiozingatia sifa, unalikosesha Taifa fursa nyingi za kiuchumi kwa kuwa wengi hawana ufahamu wa fursa zilizoko kwenye nchi wanazokwenda.

Lakini mapema mwezi huu, Balozi Mulamula alisema suala hilo sasa litaangaliwa kwa jicho la karibu zaidi, hasa uteuzi wa mabalozi.

Alisema watatoa mwongozo ambao utawataka wawakilishi hao wasibweteke katika utendaji wao kwa kuwa kuna mpango wa kuanzisha utaratibu wa kupima matokeo ya utendaji wao kwa kila baada ya kipindi kitakachoelekezwa.

“Kwa sasa tutakuwa tunawapima mabalozi wetu kwa malengo tuliyokubaliana nao ambayo yanaweza kuwa ya mwaka au zaidi.

Tutakuwa tunamuuliza balozi umeweza kuleta watalii au kuwahamasisha wawekezaji wangapi nchini?” alisema.

“Hii ni kwa sababu zamani tulikuwa tunakwenda kienyeji lakini kwa sasa hapa kazi tu.”

Vifurushi vyote kutoka Posta vitakaguliwa tena kiwanja cha ndege kabla ya kupakiwa kwenda ng'ambo

Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, Mhandisi, Thomas Haule, (katikati), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa uwanja huo leo Ijumaa Novemba 27, 2015. 


UONGOZI wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere unaomilikiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, TAA, umetangaza leo Ijumaa Novemba 27, 2015 kuwa kuanzia sasa vifurushi na mizigo mingine yote ya Shirika la Posta Tanzania, itakaguliwa kwa mara ya pili kama mizigo mingine yoyote kabla ya kupakiwa ndani ya ndege.

Uamuzi huo umetangazwa na Mkurugenzi wa Uwanja huo, (JNIA), Injinia Thomas Haule, wakati akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa VIP ulioko uwanjani hapo.Alisema, uamuzi huo ni baada ya Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege, TAA, kutoa maonyo kadhaa, kwa Shirika la Posta, kuimarisha ukaguzi wa vifurushi na mizigo itokayo Posta kwa vile imekuwa ikikamatwa na mizigo ambayo ni tofauti na iliyokusudiwa.

Alitaja mizigo hiyo kuwa ni pamoja nabangi, na kwamba, Uholanzi wamekuwa wakilalamika mara kadhaa kuwa wamekuwa wakikamata vifurushi vya Posta vikiwa na mizigo iliyoharamishwa.
"Sisi Kama Mamlaka, wajibu wetu mkubwa ni kuzuia kitu au vitu vyovyote vinavyoweza kuhatarisha usalama wa abiria wawapo ndani ya ndege au ndege yenyewe haviingii ndani ya ndege." Alianza kwa kusema Injinia Haule na kuongeza kuwa, vitu vingine kama madawa ya kulevya, pembe za ndovu, na vingine vingi, , vinashughulikiwa na mamlaka nyingine ambazo zina maafisa wake hapa JNIA wakishirikiana na maafisa wetu.

Hata hivyo makosa yafanywayo na idara Fulani ya serikali yenye afisa wake hapa JNIA, ni wazi kwamba watakaonyooshewankidole ni TAA, alisema na kubainisha kuwa Mamlaka haitavumilia tena uzembe utakaofanywa na taasisi nyingine ya serikali katika kuhakikisha zinatekeleza wajibu wake ipasavyo.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, JNIA
 • Imenukuliwa k utoka K-Vis Media

ha ha haa, katuni! Next... Anayefuatia...


[video] "Dili limebumbuluka!" Wizi wa magogo ya Tanzania kutumia mpaka wa Zambia
Serikali imesema vita dhidi ya biashara haramu ya magogo itazidishwa ili kuokoa rasilimali muhimu za misitu Tanzania. Biashara hiyo ni kinyume na Sheria ya Misitu ya mwaka 2002 inayozuia kusafirisha magogo yasiyoongezwa thamani kwenda nje ya nchi.

Akiongea na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Adelhelm Meru alisema kamwe biashara hiyo haitakubalika kuendelezwa na watu wasio waaminifu kwa taifa lao. 

“Tutapambana nao mpaka tabia hii ikome,” alisema wakati wa kukamatwa kwa kontena 31 zilizokuwa na magogo ya miti aina ya mitiki katika bandari ya Dar es Salaam. 

Aliwataka raia wema kutoa taarifa pale wanaposikia uhalifu kama huo ukitendeka hapa nchini na kusisitiza kuwa vyombo vinavyohusika viko makini kuzuia tabia hiyo. 

Magogo hayo yenye thamani ya Tshs Milioni 300 yalikamatwa baada ya wizara hiyo kupatiwa habari kuwa kuna makontena yenye magogo bandarini yanasafirishwa kwenda nje ya nchi. Alisema kontena hizo za futi 40 zilijazwa magogo yaliyodaiwa kutoka nchini Zambia. 

Akifafanua zaidi alisema pamoja na kuwepo kwa madai kuwa mzigo huo unatoka Zambia hapakuwepo nyaraka halali inayoonyesha umetoka kweli nchi hiyo jirani. 

Naibu Balozi wa Zambia nchini, Bi. Elizabeth Phiri alikuwepo bandarini hapo kushuhudia tukio hilo. Nakala ya nyaraka zilizopatikana kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA) kitengo cha bandari ya Dar es Salaam zinaonyesha kuwa magogo hayo yalisafirishwa kutoka Zambia. Hata hivyo balozi huyo mdogo alipoangalia nyaraka hizo na kuomba kupatiwa nakala halisi aziangalie aliambiwa zimebaki mpakani, Tunduma. 

Maafisa wa TRA waliokuwepo katika eneo la tukio walitakiwa kufuatilia nyaraka halali za kuruhusu magogo kuingia Tanzania. 

“Ikithibitika vinginevyo ni lazima mtandao huu utokomezwe,” alisema Dkt. Meru.
Alisema kama hakutakuwa na nyaraka halali, serikali kupitia wizara hiyo itawashughulikia kisheria maofisa walioshiriki kufanya uharibifu huo. 

“Ni lazima watanzania watambue kuwa hizi ni rasirimali za nchi, serikali haitakubali zifanyiwe uharibifu na baadhi ya watu wachache,” alisema. 

Alisema watashirikiana na vyombo vyote ikiwemo TRA, uhamiaji na vingine kukomesha tabia hizo. Balozi Phiri alisema panatakiwa kufanyika uchunguzi ili kujua yalikotoka magogo hayo.
“Siwezi kusema lolote juu ya uhalali wa magogo haya kutoka nchini kwangu, tusubiri uchunguzi,” alisema na kuongeza kuwa hata Zambia hairuhusu biashara ya magogo. Alisema vita hivyo vinapaswa kupiganwa kwa ushirikiano wa nchi majirani.
Naibu Balozi wa Zambia nchini, Bi. Elizabeth Phiri (katikati) akielezea jambo waandishi wa habari na maafisa wengine katika bandari ya Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ambapo kontena 31 zilizojaa magogo ya miti aina ya mitiki yalikamatwa. Awali ilielezwa kuwa mzigo huo ulitoka nchini Zambia; uchunguzi unaendelea kuthibitisha hilo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Adelhelm Meru.


Majibu ya Katibu Mkuu Kiongozi kuhusu maswali ya vitanda vya Muhimbili "iliwezekanaje haraka"; "kanuni za manunuzi"


Video ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alipofanya ziara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ya kufuatilia agizo la Rais.

Pamoja na mengine, amejibu kuhusu maswali yanayoulizwa ikiwa kanuni za manunuzi zilifuatwa, kwa nini iliwezekana kutimiza agizo la Rais Magufuli haraka na kama vitanda na vifaa vilikuwepo ilindikana vipi kutimiza siku za nyuma na pia ameeleza ni lini uamuzi wa kupeleka vitanda hospitalini ulifanywa na Ikulu.

Mkuu wa Wilaya afunga mpaka wa Gosebe, Tarime


Mkuu wa Wilaya asweka ndani Hakimu na M/Kiti kwa kudhulumu shamba la familia


Mwenyekiti wa ulinzi na usalama Babati, Manyara, Chrispin Meela amemweka chini ya ulinzi Mwenyekiti wa Kitongoji na kuagiza jeshi la polisi kumkamata na kumsaka pia kumkamata Hakimu wa mahakama ya mwanzo ya Bashnet kwa tuhuma za kufanya njama na kudhulumu shamba la familia lililokuwa katika mgogoro. Pia ameiagiza TAKUKURU kuwafungulia mashitaka watuhumiwa.

[video] Alichokisema Makamu II wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi


Video ya mazungumzo ya watumishi wa Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC) na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi kama yalivyowekwa mtandaoni na Cathbert Kajuna (via YouTube) siku ya Alhamisi, Novemba 26, 2015.

Job opportunity at SUA for a Webmaster

Sokoine University of Agriculture 

VACANCY 

Applications are invited from suitably qualified Tanzanians to fill the following vacant positions at Sokoine University of Agriculture at the Centre for Information and Communication Technology, under the funding of Innovative Agricultural Research Initiative (iAGRI) project. 

POSITION: WEBMASTER (Senior Computer Programmer III) 

Sokoine University of Agriculture (SUA) in Morogoro, Tanzania, is seeking a full-time developer/webmaster to redevelop and maintain SUA’s website. The Web Developer/Administrator will provide technical and management expertise to a team that is responsible for delivering a new website for SUA. The Web Developer will manage the design process, maintenance and share ownership of the delivery and success of the new site. 

The Web Developer will lead the functional and technical design, development, testing, integration, and training for ongoing support of the SUA website. He or she will work with the Centre for ICT to direct aspects of the development lifecycle. The primary responsibility of this position is to clearly define, manage and maintain priorities. The developer will work closely with the fellow staffs of the Centre for ICT to implement a website that fulfills the needs of the university while using technology appropriate for the area and available 2 resources. A large component of this project will be to provide training to SUA staff on website design, planning and maintenance. 

The successful candidate will be responsible for:

(a) Defining and implementing technical direction for the website; 
(b) Selecting and implementing a CMS software solution including, but not limited to, template creation, security and approval levels, WYSIWYG content editor, versioning, content scheduling, etc. 
(c) Performing and reviewing systems analysis, design, programming, testing, debugging, and documentation for all projects; 
(d) Providing technical and user training and manuals to SUA staff; 
(e) Leading process improvement; 
(f) Providing technical leadership to team and department members, leading through example, mentoring/ influencing others and effectively working with peers, team members, and other departments; 
(g) Creating mechanisms to enable members of staff to create and maintain online profiles; 
(h) Creating templates for content storage; 
(i) Implementing website archiving strategies. 

Knowledge, Skills, and Abilities

(a) Creative, dynamic, and forward thinking individual; 
(b) Innovative - able to identify new opportunities and make them happen; 
(c) Experience, managing websites, including management of design and developer staff; 
(d) Extensive Web User Interface Design (UI), Debugging and Cross-Browser Compatible Development Experience; 
(e) Knowledge of online Security Principles; 
(f) Knowledge of automatic backup and mirroring; 
(g) Intermediate or expert knowledge of HTML5, CSS, PHP, Javascript, jQuery, XML,CSS, SOAP and RESTful APIs implementation; 
(h) Knowledge of web multimedia technologies a plus; 
(i) Analytical capabilities to measure performance and weigh tradeoffs; 
(j) Problem solving and project management skills, with ability to balance competing project and resource demands; 
(k) Comfort with cross-cultural interaction across language barriers; 
(l) Team player who can work independently. 
(m) Ensuring that all design elements, templates and finished solutions work within a variety of browser types and screen settings; 

Required Qualifications/Experience 

(a) Degree or Advanced Diploma in Computer Science/Engineering, Information Technology, Web Development or related field and/or equivalent work experience. Masters is a plus; 
(b) Experience managing the development of a complex website; 
(c) At least 2 years of experience related to the Webmaster position; 
(d) Experience with open source content management systems like Joomla, Drupal or WordPress; 
(e) Experience in coaching, training and mentoring staff; 
(f) Excellent verbal and written communication skills; 
(g) English language fluency required; 

How to Apply 

Qualified candidates should send their applications by 18th December 2015. To apply for either opportunity, please send a cover letter referencing the position you are applying for, CV or resume, and at least two samples/links of your previous website related work to: 

Deputy Vice Chancellor (Administration and Finance) 
Sokoine University of Agriculture 
P. O. Box 3000 
Morogoro 
Tanzania 

A copy of the application dossier must be sent by email to: [email protected] 

Job opportunity at SUA for an Online Communications Specialist

Sokoine University of Agriculture 

VACANCY 

Applications are invited from suitably qualified Tanzanians to fill the following vacant positions at Sokoine University of Agriculture at the Centre for Information and Communication Technology, under the funding of Innovative Agricultural Research Initiative (iAGRI) project. 

POSITION: Online Communications Specialist (Public Relation Officer II) 

Sokoine University of Agriculture (SUA) in Morogoro, Tanzania, is seeking a full-time Online Communications Specialist. An Online Communications Specialist or Web Designer is responsible for the written and visual communication aspects a new website for SUA. The Online Communications Specialist will manage the creation of content, design the user interface, edit content and ensure a positive customer experience. This includes overall navigation flow, layout of specific pages, and the knowledge and use of the website. 

The successful candidate will be responsible for: 

(a) Training, organizing, and supporting SUA staff as they create and edit web content; 
(b) Collecting and preparing content for the website; 
(c) Ensuring content on the SUA website communicates clearly, effectively, and consistently; 
(d) Designing a maintenance mechanism for all pages on the SUA web site; 
(e) Providing technical and user training and manuals to SUA staff; 
(f) Working with the university-wide website committee on style and approach for the project; 
(g) Providing design elements, comps, templates, and finished solutions; 
(h) Testing new content before move to production; 
(i) Creating and maintaining metadata and other inputs in the system to optimize search engine results; 
(j) Performing image manipulation tasks such as creating thumbnails, image resize, file format conversion and simple image edits; 
(k) Creating and maintaining multimedia, including photo galleries, slideshows, and videos embedded in Web pages; 
(l) Improving the website information architecture to provide easier navigation and accessibility of the site to stakeholders; 
(m) Participating in efforts to improve quality of SUA web pages as required. 

Knowledge, Skills, and Abilities 

(a) Online communications specialist; 
(b) Superior English writing, editing, and proofreading skills 
(c) Creative, dynamic and forward thinking individual; 
(d) Innovative - able to identify new opportunities and make them happen; 
(e) Experience managing websites, including management of design and developer staff; 
(f) Comfort with cross-cultural interaction across language barriers; 
(g) Team player who can work independently; 
(h) Ability to prioritize, multi-task, and work with minimal supervision in a team environment; 
(i) Strong organization skills with emphasis on being conscientious and detail-oriented; 
(j) Excellent computer skills and proficiency with image editing, desktop publishing, word processing, spreadsheet, and presentation software; 
(k) Conversant in web basics; 
(l) Knowledge of multimedia/creative: e.g., interactive/web content, digital graphics/optimization. 

Required Qualifications/Experience 

(a) Advanced diploma or Degree in Communications or related field and/or a satisfactory combination of experience and training which demonstrates ability to perform the duties above. Bachelors preferred; 
(b) Minimum 2 years as a web content specialist, preferably in a university setting or similar environment, with content development and maintenance responsibilities; 
(c) Excellent oral and written communication skills; 
(d) Experience editing various types of web content ranging from general text content to specialized digital content; 
(e) Graphics experience with image editing and desktop publishing software required; 
(f) Experience in coaching, training and mentoring staff; 
(g) Working knowledge of software such as operating systems, desktop publishing, word processing, and presentation software, as well as experience with social networking websites; 
(h) Experience with WordPress, Drupal, Joomla or other open source CMS, including template development and customization; 
(i) English language fluency is required. 

How to Apply 

Qualified candidates should send their applications by 18th December 2015. To apply for either opportunity, please send a cover letter referencing the position you are applying for, CV or resume, and at least two samples/links of your previous website related work to: 

Deputy Vice Chancellor (Administration and Finance) 
Sokoine University of Agriculture 
P. O. Box 3000 
Morogoro 
Tanzania 

A copy of the application dossier must be sent by email to: [email protected] 

Kutimiza agizo la Rais: Maelekezo ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje kwa Balozi zote

Kufuatia maagizo ya Mhe. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoyatoa hivi karibuni ya kusitisha safari za nje kwa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imeanza kutekeleza maagizo hayo kwa kutoa maelekezo mahsusi kwa Balozi zake nje.

Wizara imezielekeza Balozi zote zilizopo maeneo mbalimbali duniani kujipanga ili kushiriki kikamilifu katika kuiwakilisha Serikali kwenye mikutano yote ya kimataifa na kikanda inayofanyika katika maeneo yao ya uwakilishi. Tanzania inazo Balozi 35; Balozi Ndogo tatu; Vituo viwili vya Biashara; na Konseli za Heshima 17 katika nchi mbalimbali. Hizi zote zitahusika katika kuendeleza utekelezaji wa Diplomasia yetu ya Uchumi na uwakilishi wa maslahi ya nchi yetu.

Aidha, hadi sasa Mikutano ambayo tayari imefanyika na Balozi zetu kuwakilisha ni pamoja na Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) unaoendelea nchini Malta na Mkutano wa Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Habari wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika nchini Lesotho.

Aidha, Wizara inatoa wito kwa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali kuwasilisha mapema taarifa za mikutano inayohusu sekta zao ili kutoa fursa kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuzifanyia kazi kwa wakati ili kuhakikisha ushiriki wa Tanzania unakuwa wenye tija kwa taifa.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inaungana na wadau wengine kumpongeza Mhe. Rais Magufuli kwa hatua anazozichukua za kuleta ufanisi mkubwa wa kazi na kubana matumizi ili kuiwezesha Serikali kuwahudumia wananchi kikamilifu.

Imetolewa na:
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
27 Novemba, 2015

Makamu II wa Rais Zanzibar afafanua alichosema RFI kuhusu kurudiwa Uchaguzi Mkuu

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema mazungumzo yanayowashirikisha viongozi wa vyama viwili vya siasa CCM na CUF yanaendelea na hakuna makubaliano yaliyofikiwa hadi sasa ya kurudiwa kwa uchaguzi mkuu uliofutwa wa Oktoba 25.

Kauli hiyo imetolewa na makamu wa pili wa rais balozi Seif Ali Iddi wakati akitoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya taarifa za vyombo vya habari zilizotolewa ambazo zimepotosha ukweli wa mazungumzo hayo.

Akifafanua zaidi balozi alisema mazungumzo yanayowashirikisha viongozi wa pande mbili za vyama vya siasa vya CCM na CUF yanaendelea hadi sasa na taarifa kamili ya makubaliano yaliyofikiwa yatatolewa kwa wananchi.

Alisema hadi sasa hakuna makubaliano yaliyofikiwa ya pande mbili hizo kuhusu suala la kurudiwa kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 ambao ulifutwa na tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) baada ya kujitokeza kwa kasoro mbali mbali za ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi.

Hivi karibuni balozi Seif alifanya mahojiano na idhaa ya kiswahili ya Redio ya Ufaransa (RFI) ambapo alisema mazungumzo yanayowahusisha viongozi wa vyama vya siasa vya CCM na CUF hayajafikia makubaliano ya kurudiwa kwa uchaguzi.
'Nilichosema mimi ni kwamba mazungumzo yanayoendelea ya vyama vya siasa bado hayajafikia makubaliano ikiwemo suala la kurudiwa kwa uchaguzi mkuu... lakini nilisema kwamba chama cha Mapinduzi kipo tayari kurudia uchaguzi kama itakubaliwa kufanya hivyo,'
Vyama vikuu vya CCM na CUF vimekuwa na msimamo tofauti katika suala la uchaguzi mkuu wa Oktoba uliofutwa na Tume ya uchaguzi ambapo msimamo wa CCM ni kurudiwa kwa uchaguzi huo kutokana na kasoro zake.

Hata hivyo hadi sasa chama cha wananchi CUF kimesisitiza kwamba hakipo tayari kurudiwa kwa uchaguzi huo kwa mujibu wa taarifa za naibu katibu mkuu wa CUF Nassor Ahmed Mazrui.

Kutimiza agizo la Rais: Bunge litarekebisha Sheria ili kuondoa ajira za kudumu Serikalini

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litafanyia mabadiliko makubwa sheria za utumishi wa umma kwa kuondoa ajira za kudumu serikalini, ili kuwezesha mabadiliko yaliyokusudiwa na Rais Dk. John Magufuli.

Katika mabadiliko hayo, mfumo sasa wa ajira za serikali kuwa za kudumu utabadilishwa na badala yake, kudumu kwa ajira ya mfanyakazi kutategemea juhudi na bidii yake kazini, ili kuondoa uzembe uliodumu miaka nenda miaka rudi, katika sekta ya umma.

Akizungumza katika mahoajino binafsi na gazeti la Raia Mwema, mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, alisema baadhi ya sheria za kazi zinawafanya baadhi ya watumishi wa umma kuwa wazembe.

“Kwa mfano katika serikali ya sasa mfanyakazi mzembe kabisa kabisa hata waziri kumfukuza kazi hawezi. Hata Katibu Mkuu hawezi mpaka afuate mlolongo mrefu na hatua nyingi sana, yaani kazi ni guarantee (uhakika) katika nchi yetu ni permanent and pensionable (ya kudumu na ina pensheni). Sheria za namna hiyo lazima ziondoke,” alisema Spika Ndugai .

“Katika nchi ambazo zinaendelea kwa haraka moja ya jambo ambalo huna uhakika nalo ni ajira, ukifanya vizuri unayo ajira yako ukiboronga unaondoka saa hiyo hiyo na wakati huo huo, sasa sheria za namna hiyo ni lazima zibadilishwe ili watu wachape kazi. Wawe wakijua kabisa kwamba nipo kwa sababu nachapa kazi akileta uzembe kazini kwaheri,”aliongeza.

Aliongeza kuwa mabadiliko mengine ambayo Rais Magufuli atayaleta ni pamoja na ile sheria ya ununuzi na sheria nyingine ambazo ni za hovyo hovyo, zinazoifanya serikali isifanye vizuri. Kwa mujibu wa Ndugai, Bunge litahakikisha sheria hizo zibadilishwa haraka.

“Huo ndiyo ushirikiano wetu tutakaompa lakini pia tutachangia vizuri katika mipango na bajeti zinazokuja tutazitengeneza vizuri zaidi kwa kupunguza fedha zote za ulaji ulaji, hii ya kila mwaka mapazia, kuweka makochi, kuweka makapeti na kompyuta kila mwaka na ofisi ni zile zile watu wale wale, bajeti ilikuwa imejaa ununuzi wa magari vilainishi lazima tukate kote huko,” alisema.

Akizungumzia hatua hiyo, Rais wa Shirikisho la Vyama wa Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Gratian Mukoba, alisema hawezi kuunga mkono au kukataa hoja hiyo mpaka atakapoona hoja yenyewe na maelezo yake.

“Kwa kawaida muswada wa sheria huanzia kwanza kwa wadau, wakituletea tutaona, siyo kila kitu ni kibaya, sheria zinapotungwa zinakuwa na sababu kwa nini zimetungwa. Unaweza ukawa na maelezo mazuri tukajadili utekelezaji wake, tutaamua,” alisema.

Alipoulizwa kuhusu mwenendo wa baadhi ya watumishi wa umma kufanya kazi kwa mazoea na kama sheria hiyo inaweza kutibu tatizo hilo, alikiri kuwepo kwa hali hiyo miongoni mwa watumishi wa umma lakini akatahadharisha kwamba tiba yake siyo kuondoa ajira za kudumu.

“Ziko sababu nyingi zinazosababisha baadhi ya wafanyakazi kuwa wazembe, siyo ajira ya kudumu peke yake. Kama kwenye nchi yenu mmeamua kubaguana kwa malipo, mmoja analipwa mara 30 ya mwingine, huyo anayelipwa kidogo hawezi kuwa na morali ya kazi, atanyong’onyea.

“Yule anayepata mara 30 ataathiriwa utendaji wake na hawa wenye kidogo kwa sababu ni wengi, kwa sababu watajifanya (wanaolipwa kidogo) na serikali itajifanya inalipa lakini kumbe kinacholipwa hakitoshelezi chochote,” alisema Mukoba.

Aliogeza kwamba miaka ya 1970 na 1980 watu walikuwa na uhakika wa ajira za kudumu lakini walikuwa wanachapa kazi kwa bidii kwa kuwa kulikuwa na uwiano wa haki kwenye malipo ya mishahara, tofauti na sasa, akishauri pia suala la kushuka kwa morali ya kazi miongoni mwa watumishi wa umma lifanyiwe utafiti makini na si kulikurupukia.
 • via Raia Mwema

Taarifa ya CUF kuhusu kauli ya CCM kuwa vyama vimeridhia kurudiwa Uchaguzi Mkuu Zanzibar

KWA VYOMBO VYA HABARI

Tumepokea taarifa kwamba Balozi Seif Ali Iddi amehojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Radio France International (RFI) na kusema kwamba eti viongozi wa CCM na CUF WAMEKUBALIANA UCHAGUZI ZANZIBAR URUDIWE, na kinachojadiliwa hivi sasa ni NANI ASIMAMIE UCHAGUZI WA MAREJEO kwa sababu ZEC ya JECHA INAONEKANA KUTOAMINIKA.

Tunapenda kuwawekea wazi Wazanzibari wote kwamba taarifa hizo hazina ukweli wowote, ni za uzushi na wazipuuze.

Msimamo wa CUF na Maalim Seif Sharif Hamad uko pale pale kwamba HAKUNA KURUDIWA UCHAGUZI na kwamba MSHINDI HALALI WA UCHAGUZI WA TAREHE 25 OKTOBA, 2015 ATANGAZWE NA KUAPISHWA.

Kauli za Balozi Seif Ali Iddi ni za kutapatapa zianzolenga kuwatuliza wana-CCM ambao wanaonekana kukata tamaa baada ya kushindwa vibaya na CUF kwenye uchaguzi mkuu wa Rais wa Zanzibar, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Wabunge na Madiwani uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015.

Kwenye uchaguzi mkuu wa Urais wa Zanzibar, mgombea wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, alimbwaga vibaya mgombea wa CCM, Dk. Ali Mohamed Shein, kwa zaidi ya kura 25,000.

Balozi Seif Ali Iddi mwenyewe akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya CCM anatuhumiwa na wana-CCM kushindwa kazi na kukisababishia chama chao kushindwa vibaya kuliko wakati wowote katika historia ya chaguzi za Zanzibar.

Lakini kama hilo halitoshi, wana-CCM wanamtuhumu Balozi Seif na wajumbe wengine wa Kamati ya Kampeni aliyokuwa akiiongoza kusimamia matumizi mabaya ya kiasi kikubwa cha fedha za kampeni za Chama hicho ambazo sehemu kubwa walimdanganya mgombea wao, Dk. Ali Mohamed Shein, kwamba zimetumika kuleta ushindi wa CCM kisiwani Pemba lakini kumbe ziliishia katika mifuko ya watu binafsi.

Haistaajabishi kwamba sasa Balozi Seif Ali Iddi ameamua kuja na njia ya kutoa taarifa za udanganyifu ili kujinusuru na mzigo wa tuhuma za kushindwa kazi na kusimamia matumizi mabaya ya fedha za kampeni kutoka kwa CCM wenzake.

CUF tunamtaka Balozi Seif Ali Iddi awache kudanganya umma na badala yake awajibu CCM wenzake kwa nini amekitia chama hicho aibu na fedheha kubwa ya kupata kipigo kibaya katika uchaguzi kilichopelekea CCM kupoteza majimbo tisa (9) kisiwani Unguja na Dk. Ali Mohamed Shein kushindwa uchaguzi wa Urais wa Zanzibar kwa zaidi ya kura 25,000 huku wakidai kutumia mamilioni ya fedha ambazo hawana maelezo zimetumika vipi.

CUF tunawataka Wazanzibari kutobabaishwa na kauli za kushindwa kazi za Balozi Seif Ali Iddi na watulie wakijua kuwa ufumbuzi wa haki wa uchaguzi mkuu utapatikana kwa kutangaza matokeo ya kura kwa majimbo yaliyobakia na hatimaye mshindi kutangazwa na kuapishwa.

HAKI SAWA KWA WOTE
ISMAIL JUSSA
MKURUGENZI WA MAWASILIANO - CUF
26 NOVEMBA, 2015

Kauli ya Serikali kuhusu taarifa za Hazina kuachwa tupuSerikali imekanusha taarifa zinazosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Rais mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete alikomba fedha kutoka Hazina na kuiacha Serikali bila fungu lolote.

Hayo yamesemwa jijini Dare es Salaam na Kamishina wa Bajeti kutoka Wizara ya Fedha Bwa. John Cheyo huku akiwataka wananchi kupuuza habari hiyo kwani hazina ukweli wowote.
“Hazina inazo pesa za kutosha na tunajivunia kufanya uchaguzi wa mwaka huu, kununua mashine za BVR kwa kutumia pesa za watanzania bila kutegemea msaada wowote kutoka nje ya nchi na kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu mwaka huu”
Pia aliongeza kuwa serikali imeendelea kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa bomba la gesi ambalo limekamilika hivi karibuni, vinu vya kuchakata gesi na ujenzi wa barabara nchini.

Aliendelea kusema kwamba mfumo wa serikali wa bajeti unaiwezesha serikali kupanga vipaumbele vya matumizi kulingana na bajeti ilivyopangwa ambapo fedha zinazokusanywa kupitia mfuko mkuu wa serikali ndizo hutumika.

Bajeti iliyoidhinishwa na Bunge kwa kipindi cha 2015-2016 ni shilingi trilioni 22.5 na bajeti hiyo inatengenezewa mpango wa makusanyo na matumizi kwa kulipia mishahara ya wafanyakazi na miradi mbalimbali iliyoidhinishwa.

Pia katika matumizi mengine bajeti hiyo inalipia chakula cha wanafunzi, mikopo ya wanafunzi elimu ya juu, ununuzi wa dawa na vifaa tiba na chakula cha hifadhi ya taifa.
 • Jovina Bujulu - Maelezo

[video, update] Kamisha 'alivyojieleza' mbele ya Waziri Mkuu alipofanya ziara ya kushitukiza TRA

[video] Kamishna wa TRA...


Barua kwa watumishi wa ummaNawasalimuni nyote katika jina la nchi yetu nzuri Tanzania,

Jina ambalo huko nyuma sote tuliliimba “Tazama ramani utaona nchi nzuri, yenye mito na mabonde mengi ya nafaka…nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzaniaaa!”

Hakika wimbo huu vijana wengi siku hizi wanashindwa kuuimba, kwa nini? Uzuri wa taifa lao haupo tena, umepotezwa na baadhi yenu watumishi wa umma wasio na uadilifu.

Sio siri vijana wetu kwa muda mrefu wameshindwa kujivunia taifa lao, wameshindwa kuongea mbele za watu kwa sauti kubwa kwamba wao ni Watanzania, uzuri wa taifa lao na sifa nzuri ya nchi yao imeharibiwa na vitendo kama ufisadi uliokithiri ambao umesababisha wachache katika taifa kunufaika huku wengi wakiteseka.

Ndugu zangu watumishi wa umma,

Ni kwa kupitia jina la nchi hii ndiyo leo nawaandikieni, kuwakumbusha juu ya wajibu wenu ambao kwa muda mrefu sana umekuwa hautimizwi ipasavyo!

Kwanza kabisa niseme wazi kwamba nayafahamu mateso yenu, nayafahamu mahangaiko yenu ya maisha magumu, ambayo wakati mwingine yamefanya uaminifu wenu kutikiswa.

Pamoja na hayo yote nasema hakuna jambo hata moja linalohalalisha kwenu ninyi kupoteza vigezo vitano muhimu vya utumishi wa umma ambavyo ni;
 1. UADILIFU
 2. UAMINIFU
 3. KUSEMA KWELI DAIMA
 4. UZALENDO NA DHAMIRA
 5. HOFU YA MUNGU.
Yeyote kati yenu aliyehalalisha kuondoka kwa vitu vitano nilivyovitaja hapo juu kwa sababu ya aidha kipato kidogo anachokipata serikalini, akavunjika moyo na kuacha kuwatumikia wananchi, ama akachagua kuendeleza rushwa na kukosa uzalendo, huyu hatufai kuwa mtumishi wa umma. Kwa muda mrefu mmekuwa mkilalamikiwa, mkinung’unikiwa na wananchi kwa sababu ya utendaji mbovu unaosababishwa na kukosekana kwa mambo matano niliyoyataja hapo juu, kwa kweli ilionekana kana kwamba uadilifu katika taifa hili hauwezekani tena, vivyo hivyo uaminifu, kusema kweli, uzalendo na hofu ya Mungu vilitoweka.

Uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, 2015 na kumwingiza madarakani rais ambaye hawezi kumaliza hotuba yake bila kusema “TUNAMTANGULIZA MUNGU MBELE” Dk. John Pombe Joseph Magufuli umerejesha tena imani ya Watanzania kwamba, kumbe utumishi wa umma uliotukuka unawezekana, yote haya yamefanyika ndani ya siku chini ya arobaini tangu aingie madarakani!

Kwa matendo yake hayo, nimesikia kwa masikio yangu watu waliompinga Rais Dk. Magufuli wakati wa kampeni wakijuta na kusema: “Laiti ningejua ningempa kura yangu!” haya yanatokea ndani ya siku chini ya hamsini tangu rais huyu aingie madarakani, upepo umebadilika, utumishi wa umma uliowekwa madarakani na watu kwa ajili ya watu kumbe unawezekana. Ule msemo wa wazungu usemao “Once you shake the top, you have shaken the bottom” yaani ukishatikisa juu, tayari utakuwa umetikisa na chini, sasa umedhihirika kwamba ni kweli. Tanzania inakimbia mbio, kuanzia serikalini mpaka kwenye sekta binafsi, adui uvivu ameanza kupotea kwa sababu tu raia aliyeingia madarakani sio mvivu.

Kwa mara ya kwanza maishani mwangu nimeanza kusikiliza taarifa za habari na kusikia habari za kamatakamata, fukuzafukuza, kila kona ya nchi. kila kiongozi, kila mtendaji sasa anajaribu kutimiza wajibu wake, yote haya kwa sababu amebadilishwa mtu mmoja tu juu ambaye kauli mbio yake ni “HAPA KAZI TU!”

Ndugu zangu Watumishi wa Umma,

Nawaandikieni barua hii kuwakumbusha kwamba ile kauli yenu ya kusema “huu ni moto wa mabua” naomba muiache, anayesema hivyo hamfahamu vizuri rais wetu, kwa wanaomfahamu hawawezi hata siku moja kutoa kauli hiyo, haigizi, haya ndiyo maisha yake, ni kama mapafu ambavyo kazi yake ni kupumua,ndiyo ilivyo kwa Rais Dk. John Pombe Magufuli.

Ndugu zangu,

Nawasihi mfanye kazi, timizeni wajibu wenu mliopangiwa kwa faida ya taifa hili, ambaye hatayasikia maneno haya, hakika ajiandae kukumbuka ninachokisema kwani mfumo utamtema! Ni wakati wa kuchapa kazi, si wa kuchati kwenye mitandao ya jamii saa ya kazi. Tukifanya jambo hili kwa pamoja, ninawahakikishieni taifa letu litasonga mbele kutoka hapa tulipo kwenda tunakotakiwa kwenda, rais wetu ni MUADILIFU, ndivyo itakavyokuwa kwa Makamu wake wa Rais Samia
Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, serikali nzima na hatimaye vijijini, vivyo hivyo katika uchapakazi, kama rais wetu si mvivu, wavivu wote watang’oka, watake wasitake.

Matarajio yangu ni kwamba kama watumishi wa umma mtatimiza vyema wajibu wenu, mtafanya kazi kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo wa hali ya juu, lazima kipato cha taifa letu kitaongezeka na maisha yenu yataboreshwa na rais huyu huyu tuliyemweka madarakani. Lakini niwasihi msipoteze hali yenu ya kujiamini kwa kusema “Rais ni mkali mno” matokeo yake mkawa ni watu wa kutekeleza mambo kwa nidhamu ya woga, taifa la watu wenye aina hii ya nidhamu, ambao hutekeleza mambo yao kwa kutaka tu kumfurahisha mkuu huwa halisongi mbele, matokeo yake huzaa hata uonevu kwa sababu tu mtu alikuwa anataka aonekane anafanya kazi.

Sidhani rais wetu ni mtu wa aina hii, bali ni mtu anayependa kufanya kazi na watu wanaojiamini na wachapakazi na atakuwa tayari kujenga jamii ya watu wenye kujiamini si wanaotetemeka ovyo kila wanapokutana naye wakimpa ushauri anaopenda kuusikia, si ule anaotakiwa kuusikia hata kama hautamfurahisha.

Nimeyasema haya kwa sababu msipokuwa makini wale mlioko madarakani, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi nk. Mtajikuta mkionea watu au kuwatoa watu sadaka kwa sababu tu mnataka kumfurahisha mkuu au muonekane mnafanya kazi na baadaye kupanda vyeo kwa gharama za maisha ya watu wengine.

Sitaki kusema mengi siku ya leo, kwa haya machache niliyoyasema nawatakieni utendaji mwema wa kazi katika Awamu hii ya tano ya HAPA KAZI TU! Tendeni kazi zenu kwa kujiamini na uadilifu wa hali ya juu, nawahikikisheni awamu hii ya tano itabadilisha maisha yenu, kama anavyosema mwenyewe Rais Magufuli, tumuombee kwa Mungu atimize ndoto yake yakutufikisha kwenye nchi ya ahadi.

Ahsanteni.
NUKUU
WASALAAM
Eric Shigongo James