Kutimiza agizo la Rais: Dodoma wasafisha mji


Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge (kulia walioingia mtaroni) na watumishi wengine wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakishiriki zoezi la kusafisha mitaro ya maji ya mvua eneo la Bahi Road mapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira.


Mhandisi wa Maji wa Mkoa wa Dodoma Bazil Mwiserya akishiriki zoezi la kusafisha mitaro ya maji ya mvua eneo la Bahi Road mapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira.

Wafanyakazi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Tume ya Maendeleo ya Ushirika na Manispaa ya Dodoma wakishiriki zoezi la kusafisha mitaro ya maji ya mvua eneo la Bahi Road mapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira.

Watumishi wa Manispaa ya Dodoma wakishiriki zoezi la kufanya usafi kwa kufyeka magugu eneo la makaburi ya Bahi Road mapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira.

Wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Tume ya Maendeleo ya Ushirika wakijiorodhesha baada ya kumaliza zoezi la usafi wa mazingira mapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira, orodha hiyo itatumika kuwabaini watumishi ambao hawajashiriki zoezi la usafi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge (katikati aliyeshika koleo) akifanya majumuisho mara baada ya kumalizika kwa zoezi la watumishi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa kusafisha mitaro ya maji ya mvua eneo la Bahi Road mapema leo.

Picha: PamojaPure blog

[video] Wito wa Lowassa wakati wa maziko ya Alphonce Mawazo


Yule binti maarufu kupiga mpira danadana ajeruhiwa kikatili


UWT wamfanyia dua Rais Magufuli na kusihi wananchi wamwombee


Rais ameshateua baraza la Mawaziri isipokuwa...


Breaking News
Imefahamika! Si kwamba Mhe. Magufuli bado hajateua baraza la mawaziri ni kwamba kila anayeteuliwa anachomoa anasema mzee samahani sitaweza tafuta mwingine!
Hii ni moja ya zile habari za kipuuzi ambazo hubandikwa hapa wavuti.com kutoka WhatsApp (lighter moments - smile!)

Nakutakieni mwanzo mwema wa juma lijalo!

CWT yamshukuru "shemeji" aliyeondoka, wamwomba "shemeji" aliyekuja alipe deni lao kwa hela anazobana
Taarifa ya Azam ya kupotea makontena, kuhusishwa na TRAKumekuwa na taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa kampuni ya Bakhresa inahusika na upotevu wa makontena 349 yaliyoripotiwa hivi karibuni kuwa yametolewa bandarini bila kulipiwa ushuru. Taarifa hizo zilitolewa na Waziri Mkuu wakati wa ziara yake ya Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni.

Uchunguzi wetu umeonyesha kuwa si kweli kuwa kuna makontena yenye bidhaa zilizoingizwa na kampuni hio ama ni miongoni mwa makontena yaliyohusika katika sakata hilo. Isipokuwa kumetokea upotevu wa makontena yaliyoingizwa nchini na baadhi ya wafanyabiashara katika eneo la kuhifadhia makontena (ICD) linalomilikiwa na kampuni hiyo la Azam ICD.

Aidha imebainika kuwa kuna uchunguzi unaofanywa na mamlaka ya mapato nchini TRA, huku kukiwa na ushirikiano na uongozi wa Kampuni hiyo (SSB Group of Companies) kuhakikisha wale wote wanaohusika na upotevu huo wanachukuliwa hatua na kodi yote ya serikali inalipwa na wamiliki wote wa makontena yaliyohusika katika upotevu huo wanawajibishwa.

SSB Group of Companies
Corporate Affairs Department
November 29, 2015

Biggest hurdle that may block Magufuli's reforms and expectations of Tanzanians


President John Magufuli may be determined to implement reforms, but a slack public service machinery may prove to be the biggest hurdle to fulfilling the expectations of the majority of Tanzanians.

With a modus operandi that is unfamiliar in government circles, observers are of the view that President Magufuli has no option but to overhaul the public service machinery if he is to succeed in implementing his grand plans.

There is growing concern the country’s public service machinery is in a shambles and accountability among public servants at an all-time low.

Access to service in some public offices, hospitals, schools and other government institutions is no longer an automatic right for the citizenry.

ROT IN PUBLIC SERVICE STARTED 20 YEARS AGO

There is no quick fix for the situation, which some analysts say gradually started nearly 20 years ago, and building a vibrant public service machinery is a challenge President Magufuli must confront head-on.

“I cannot tell to what extent President Magufuli understands that the public service machinery is in disarray and whether it has the capacity to implement his plans,” says a retired permanent secretary, who spoke on condition of anonymity.

He said although the President had demonstrated great determination to change the lives of Tanzanians, any plans geared towards the realisation of his goals should go in tandem with overhauling the public service machinery.

President Magufuli outlined the priorities of his government in his speech when inaugurating the National Assembly in Dodoma last week in which he clearly sent out the message that it will not be business as usual under his leadership.

He said the time has come for Tanzanians to walk the talk and confront vices that were holding the nation back.

MAGUFULI'S INAUGURATION PROMISES

Apart from reiterating his decision to offer free education, he also promised to cut public spending, fight corruption and enhance accountability in public service.

But the former permanent secretary who spoke to The Citizen said a lot needs to be done to make Dr Magufuli’s plans a reality.

“Resources to offer free education are there, but the question should be: how are we going to curb corruption? We need a step-by--step approach to curbing and eventually eradicating corruption. Our problem is that the public service machinery to do that is no longer there,” he said.

He cited as an example the Ministry of Energy and Minerals, saying its accountability and service delivery were poorer than was the case 30 years ago.

“If you look at the systems at the Energy and Minerals ministry today you will see that we are very backward in terms of the capacity and strategies to bring about development. This explains why ministers and permanent secretaries who served in the ministry in the last ten years invariably left under a cloud of corruption allegations,” he said.

Because of ineptitude in the system, the former official said, Dr Magufuli may find himself sacking many bureaucrats in the early days of his administration.

LITTLE OR NO CAPACITY

He cautioned, however, that Dr Magufuli could be left with people with little or no capacity to put in place effective strategies.

“What will follow is that public servants will be advising him in fear, and this will worsen the situation. He (the President) must look for people who are courageous enough to tell him what he does not want to hear.”

A private consultant on leadership and public service management, Mr Jesse Mashimi, said President Magufuli could not implement his plans because the relevant institutions have been dismantled.

“The laxity you see in public service is a direct consequence of the abolishment of Ujamaa, which had its checks and balances as far as public service delivery was concerned,” he said.

According to Mr Mashimi, public service delivery had been neglected and it is place taken by personal discretions and biases rather than laid-down rules and procedures.

“New styles and systems of operation in public service only serve to support corruption. The President will need to start rebuilding our public service delivery system from scratch…he is unlikely to succeed if he doesn’t overhaul the system first.”

USE SECURITY AND INTELLIGENCE SYSTEM TO FOSTER ACCOUNTABILITY

Mr Mashimi added that the new government should start to make use of the national security and intelligence system to enhance accountability in public service.

The Secretary-General of the Trade Union Congress of Tanzania (Tucta), Mr Nicholaus Mgaya, said morale in the public service sector was “very low”.

“It is not right, in my opinion, to point an accusing finger at civil servants without addressing their plight. For Dr Magufuli to succeed in his bid to transform the sector, the welfare of the civil servants must be a top priority,” he said.

According to Mr Mgaya, there are currently two classes of civil servants.

“There are those at the top of the hierarchy, who are claiming huge allowances which account for 52 per cent of the public wage bill, and there are those at the bottom of the ladder, who are paid peanuts. These are the ones who are demoralised,” he said.

Mr Mgaya added that the Public Service Negotiating Machinery Act, 2003, among other issues, established a joint committee to review salaries annually, but the panel has never been operational.

“What we have are meetings which never reach a consensus. The small increments we occasionally see are unilaterally decided by the government,” he said.
  • Article by BERNARD JAMES

Eti shilingi imeanza visa?
Habari iliyochapishwa Juni 22, 2014 na NIPASHE kuhusu kashifa ya makontena TPA na TRA


Kama uhujumu uchumi kupitia utoroshwaji wa makontena ulioripotiwa na gazeti hili mwaka jana ungefanyiwa kazi, vigogo wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na Mamlaka ya Bandari (TPA) wasingekumbwa na kadhia ya kusimamishwa kazi.

Lakini licha ya matoleo matatu kuchapisha uozo huo kutokana na uchunguzi uliofanyika kwa weledi, mamlaka husika zilipuuza na badala yake zikakanusha ikiwa ni pamoja na kupitia matangazo yaliyolipiwa kutokana na fedha za umma.

Ingawa habari hizo hazikuzungumzia moja kwa moja makontena yote 349 yaliyotajwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, lakini mwelekeo wake ulilenga kuonyesha namna vitendo vya ukwepaji kodi kupitia utoroshwaji wa makontena, vilivyokithiri nchini hususan ni kwenye bandari hiyo.

Moja ya habari hizo ni ile ya Juni 22 mwaka jana, gazeti hili lilipoandika habari yenye kichwa Makontena yaondolewa kinyemela bandarini Dar.

Makontena yaliyobainika kwa wakati huo yalikuwa ni pamoja na yaliyotokea China na kuondolewa bandarini kinyemela.

Hatua hiyo ilifikiwa kwa maelezo kuwa makontena hayo yalikuwa ni mzigo wa kupita ukipelekwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), lengo likiwa ni kukwepa kodi.

Makontena hayo yalibainika kubaki hapa nchini na kusambazwa kwenye soko.

Wahusika katika kadhia hiyo walifanikisha kuyatoa makontena hayo kwa kutumia vibali `feki’ na wakaguzi wakaruhusu magari ya kusafirishia mizigo kubeba makontena hayo licha ya kutokuwa na vigezo vya usafirishaji.

Nipashe ilijulishwa kuwa `mchezo mchafu huo na mingine ya aina hiyo imekuwa ikifanywa mara kwa mara na baadhi ya wafanyabiashara ili wasilipe kodi kwa kushirikiana na maafisa wa TRA wanaopokea rushwa nono.

Mamlaka za TRA na TPA zilipoulizwa kuhusiana na tukio hilo walianza kwa kueleza kwamba hawakuwa na taarifa kuhusiana na suala hilo.

TPA ilikanusha na kutolea ufafanuzi tukio hilo lakini kwa kukiri kuwapo kontena lililokamatwa huko Chang’ombe.

Taarifa ya TPA ilieleza kuwa kulikuwa na jaribio la kutumia nyaraka za kughushi kuondoa kontena namba PCIU 298647-4 lililokuwa limepakiwa katika gari aina ya Scan namba T 425AAY/T318BXS.

Kwa mujibu wa TPA hatua hiyo ilifanyika kwa kutumia nyaraka za kughushi Juni Mosi mwaka jana.

TRA ilipingana na taarifa ya TPA na kueleza kuwa (TRA) ilifuatilia kontena hizo na kulikamata moja huko Chang`ombe likiwa linapakua vitenge.

Nipashe ilizungumza na TRA kuhusiana na kutolewa kwa makontena kadhaa kwa njia za udanganyifu, Afisa mmoja alisema suala hilo linafanyiwa uchunguzi ili kubaini makontena mengine yaliyotoka kwa njia za udanganyifu, lakini hatima yake haijatangazwa hadi sasa.

Julai 27 mwaka jana, Nipashe liliendeleza habari ya uchunguzi yenye kichwa, TRA yahusishwa uondoaji mizigo kinyemela bandarini.’

Vyanzo vya gazeti hili bandarini hapo vilieleza maofisa wa TRA wasiokuwa waadilifu ni wahusika wakuu wa kutengeneza nyaraka za uongo kwa kushirikiana na wafanyabiashara ili kukwepa kodi.

Miongoni mwa mbinu zilizobainika kutumiwa na maofisa wa TRA ni kubadili kampuni za utoaji mizigo ili kuvuruga ushahidi ikiwa kampuni za awali ziliwekewa vikwazo.

Makontena yaliyohusishwa katika kashfa hiyo ni pamoja zilizozuiliwa mara kadhaa bandarini hapo ili kufanya uchunguzi kutokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza.

Moja ya taarifa tulizochapisha ni kuhusu magari yanayotumika kubeba mzigo kwenda nje kulazimika kuwa na C65 na TI, miongoni mwa yaliyotumika kutorosha makontena kwa lengo la kukwepa kodi yakiwa na mihuri ya ‘seal’, hayakuwa na sifa na vigezo vya usafirishaji nje ya nchi.

Hata hivyo Nipashe ilipofuatilia suala hilo TRA, mamlaka hiyo haikutoa ushirikiano zaidi ya kujulishwa kuwa suala hilo limeshafanyiwa kazi.

Juzi, Rais John Magufuli alimsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade na maafisa watano kutokana na ubadhirifu wa makontena 349 kupitishwa kinyemela na kuisababishia serikali hasara ya Shilingi bilioni 80.

------------- MWISHO ---------------


Makontena yaondolewa kinyemela bandarini Dar es Salaam


BEATRICE SHAYO
22nd June 2014

Licha ya baadhi ya viongozi wa serikali kuisifia Mamlaka ya Bandari (TPA) kudhibiti wizi kwenye bandari ya Dar es Salaam, sifa hizo zimeyeyushwa na madai ya makontena yanaendelea kuondolewa kinyemela kwa lengo la kukwepa kodi.

Habari za uhakika kutoka bandarini zinaeleza kuwa makontena hayo yanadaiwa kuondolewa forodhani hapa kwa vibali feki ambavyo kampuni zilizoyaondoa baadhi hazijasajiliwa.

Kontena hizo zilizotokea China ziliondolewa bandarini Dar es Salaam kwa maelezo kuwa mzigo wa kupita ukielekea Kongo ili usilipiwe ushuru wakati shehena hiyo ya vitenge vya waksii ilikuwa inasambazwa jijini hapa.

Watoa taarifa walisema kontena tatu zinadaiwa kukamatwa zikifanyiwa mpango wa kuzitoa kijanja wakati nyingine mbili zilikuwa katika mchakato wa kutayarishiwa vibali vya kutoka bandarini hapo kwa njia za kitapeli.

Walioagiza mzigo huo ambao ni wafanyabiashara wakubwa waliopo jijini (majina tunayo), wamedaiwa kuwaahidi maofisa wa bandari donge nono la Sh milioni 100 ili kufanikisha uporaji huo.

Gazeti hili lilidokezwa kuwa kontena moja lilikuwa limetolewa bandarini na mengine yalinaswa mlangoni baada ya kushtukiwa kuwa kuna mchezo mchafu uliopangwa na maofisa hao wa kukwepa kodi.

KUNASWA


Kontena hilo moja lilidaiwa kukamatwa eneo la Chang’ombe likiwa linapakua vitenge vya wax wakati mitaani huku likiandikiwa taarifa na vibali vya mzigo wa kupita unaoelekea Kongo uliopitishwa kiulaini bila kutozwa ushuru.

Gazeti hili lilipata baadhi ya nyaraka zilizoidhinisha utokaji huo wa makontena mawili yenye namba PCIU2626734 na PCIU2986474 ambayo yalikamatwa baada ya kudaiwa kutumia kampuni ambayo haijasajiliwa kutolea mzigo huo.

Aidha ilielezwa kuwa kontena hizo mbili zilitumia kampuni mbili kutolea mzigo huo kinyume cha sheria za usafirishaji shehena.

Habari hizo zilieleza kuwa kampuni mbili ambazo hujihusisha na utoaji wa mizigo bandarini za Le- General Inn na nyingine ya Green Trading zinadaiwa zilitengeneza nyaraka zote za Mamlaka ya Mapato (TRA) na kupata vibali vya kuondoa mizigo bandarini (release order).

Ziliongeza kuwa kampuni ya Green Trading ambayo inasadikika imesimamishwa kwa muda baada ya kushindwa kulipa kodi za ndani ilitengeneza vibali vya TPA kwa kutumia nyaraka za TRA ‘release order’ hiyo.

Taarifa zake zilitumika kuandika vibali vyote kuanzia vile vya kuuchukua mzigo kwenye eneo yanakohifadhiwa makontena hadi kuutoa getini.

“Wakati wakitoa kontena hizo wahusika wa kampuni ya Le-General Inn walifuta jina lao kwa kulikata kwa kalamu na kuandika jina la Kampuni ya Green Trading wakati haikutakiwi kukata maandishi kwenye nyaraka hizo rasmi.

Gazeti hili lilijulishwa kuwa kwa upande wa Shirika la Meli la PIN linadaiwa kughushi nyaraka za nembo pamoja na kitambulisho na kuweka picha za wafanyakazi wa Kampuni ya Green Trading na kufanikiwa kupata kibali cha kuruhusiwa kutoa mzigo bandarini (delivery order).

Kamanda wa Kikosi cha Wanamaji cha Polisi, Mboje Kanga, alipohojiwa kuhusu tukio hilo alisema ana taarifa na kwamba uchunguzi unafanywa.

Alisema kontena hilo lenye futi 20 likiwa na namba PCIU2686474 lilikamatwa mwanzoni tarehe mosi mwezi huu saa 6 usiku likiwa na shehena ya vitenge.

"Tunaendelea na uchunguzi wetu , limezuiliwa kutoka huenda nyaraka zilizotumika si sahihi au kuna sababu nyingine," alisema Kanga.

Meneja Mawasiliano wa TPA, Janet Ruzangi, katika mahojiano na gazeti hili alisema hana taarifa na kama kuna tukio hilo wahusika ni TRA. “Hivyo suala hilo ni vizuri ukawauliza TRA maana watakuwa na taarifa wao ndiyo wakamataji sisi hatuna taarifa hizo,” alisema

KAMPUNI YA GREEN 

Frank Mushi, Meneja wa Kampuni ya Green Trading, alipohojiwa kuhusu ushiriki wa kampuni hiyo alisema : “nashangazwa na TPA kutumia kampuni yangu kutoa mzigo wa kontena wakati sheria hairuhusu”.

Alisema hadi sasa kampuni hiyo haina leseni hivyo hairuhusiwi kushughulikia shehena bandarini na nyaraka zilizotumika ziligushiwa.

TRA HAIJUI

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi TRA, Richard Kayombo, alipoulizwa kuhusu tukio hilo alisema hana taarifa.

Licha ya ahadi hiyo NIPASHE ilimfuatilia Kayombo kwa siku tatu kwa kutuma ujumbe mfupi na kuzidi kusisitiza kuwa anafuatilia.

Wahadhiri UDSM wazungumzia ya TRA; Washauri wananchi watoe taarifa za mali za wahusika


WANANCHI wamehamasishwa kujitokeza kusaidia uongozi wa Rais John Magufuli, kwa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya sheria, vinavyofanya uchunguzi kuhusu mali za maofisa na vigogo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Ushauri huo kwa wananchi umetolewa baada ya Waziri Mkuu Majaliwa Kassim, kuagiza mali za maofisa waliosimamishwa kwa upotevu wa zaidi ya Sh bilioni 80 za kodi, baada ya kupotea kwa makontena 349 yaliyopaswa kutoa mapato hayo ya Serikali.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Ally alisema hatua hiyo ni vema izingatie misingi ya haki na uwajibikaji kwa kushirikisha wananchi, kwa kuwa wanajua yanayoendelea kwa watendaji wa mamlaka hiyo.

Alisisitiza kuwa ushiriki wa wananchi ni muhimu, kwani wanajua mbinu zote wanazotumia maofisa hao katika ukwepaji kodi, makontena yanavyotoroshwa na mali walizonazo.

Ally alisema wananchi wanajua majengo makubwa wanayomiliki watendaji hao, magari na mali zingine kwa kuwa baadhi yao ni vijana wadogo waliosomeshwa na Serikali kwa kutumia fedha za umma kwa lengo la kufanya kazi, lakini wamegeuka na kudhulumu watu.

Mhadhiri huyo alishauri uchunguzi unaofanyika uwe wa kina na mapana na washiriki wote, wakiwemo watumishi wa umma na wafanyabiashara, wachukuliwe hatua kwa kuwa huo ni mtandao unaohusisha watu wengi.

Alisifu hatua hiyo ya Serikali, akisema itaongeza nidhamu na heshima kwa Serikali na kuongeza kuwa watendaji hao wasipokuwa na maelezo ya kutosha ya mali walizonazo kwa kuzingatia mshahara wao na muda waliofanya kazi, ni sahihi mali zichukuliwe kwa kuzingatia sheria. Mbali na watumishi hao, Ally alishauri na wafanyabiashara watakaobainika kushirikiana na watumishi hao, wachukuliwe hatua pia kwa kuwa nao ni wahusika.

“Hawa wafanyabiashara wakubwa wametumika kuwarubuni watumishi wa umma, nao warejeshe kodi waliyokwepa na ikiwa watabainika kuwa na kosa la jinai, wafikishwe mahakamani na kushitakiwa ikibidi na mali zao zifilisiwe,” alisema.

Majina mengine 

Naye, Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Benson Bana alitaka maofisa hao wa TRA wachunguzwe kwa kina kwani watu kama hao mali zao nyingi wanaziandika kwa majina mengine ili wasijulikane.

Alisema hatua ya Serikali kuagiza mali za maofisa hao zichunguzwe kama zinaendana na kipato cha mtumishi wa umma ni nzuri, kwani mara nyingi watu walikuwa wakilalamika kuwepo kwa watumishi wanaojitajirisha kwa kukwepa kodi. Kwa mujibu wa Profesa Bana, wafanyakazi wa TRA wanalipwa vizuri zaidi katika sekta za umma kwa lengo la kuwatosheleza, ili wasishawishike kuingia katika ukwepaji kodi utaratibu ambao ni mzuri, lakini wameshindwa kutumia vema fursa hiyo ya kuthaminiwa na Serikali.

Alitaka taasisi za udhibiti wafanye kazi zao, badala ya kusubiri Rais au Waziri Mkuu kugundua masuala mazito kama hayo, huku akitaka wananchi kusaidia kubaini mali walizonazo na kuwachukulia hatua.

Akizungumzia wafanyabiashara wanaomiliki makontena yaliyokwepa kulipa kodi, Profesa Bana alisema haitoshi kuwataka kulipa kodi, bali ni lazima baada ya kulipa, waadhibiwe kwani wao ndiyo walioharibu mifumo ya ukusanyaji kodi ya Serikali. Profesa Bana alisema baadhi ya wafanyabiashara hao, wamekuwa wakiweka mitandao inayotengeneza mifumo ya kushawishi watendaji wa Serikali, ili wakwepe kulipa kodi.

Mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na mchambuzi wa masuala ya siasa, Profesa Mwesiga Baregu alisema hatua hiyo inaonesha kusonga mbele katika mapambano ya ufisadi, lakini inatakiwa kuwa endelevu na kuacha kuwa sehemu ya matukio.

Katibu wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Nicholas Mgaya, alisema anaunga mkono maofisa hao kuchunguzwa na kutaka kuwe na mtindo wa kuchunguza mali za watendaji wote wa sehemu nyeti serikalini.

Mgaya alisema ni vema kufahamu watendaji hao, wanapata wapi fedha za kujenga majengo ya fahari, wakati hawana mkopo ili kuleta usawa kwa kupata kitu alichofanyia kazi na si nje ya utaratibu.

Aliitaka Serikali kuendelea kuchunguza taasisi na sekta nyingine za umma, kwani bado zipo sehemu nyingine zenye matatizo kama hayo. Akizungumzia wenye makontena, Mgaya alisema ni vema Serikali ifanye hesabu upya za wafanyabiashara wote wanaokwepa kodi.

Alisema ni vema wafanyabiashara wote wanaoingiza vitu kutoka nje, wafanyiwe ukaguzi wa vitu walivyoingiza kwa miaka mitano iliyopita na kodi waliyolipa na kama wanadaiwa, walipe, lakini wakishindwa mali zao ziuzwe na kufilisiwa kisheria, kwani kodi hizo zitasaidia kutoa elimu bure na kufanya nchi kuendelea kiuchumi.

KFC yazindua tawi Kariakoo


Mkurugenzi mkuu wa KFC nchini Tanzania, Louis Venter (kushoto) akikata utepe wakati wa ufunguzi wa tawi la KFC eneo la Kariakoo jijini Dar ambapo waliweza kusherekea na watoto wenye mahitaji maalumu wa shule ya msingi ya Uhuru Mchanganyiko.

Mmoja wa wahudumu hao akiwahudumia wanafunzi hao wenye mahitaji maalumu mara baada ya ufunguzi wa Mgahawa huo eneo la Kariakoo jijini Dar

Mkurugenzi Mkuu wa KFC nchini Tanzania, Luis Venter akitoa huduma kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum mara baada ya ufunguzi wa Mgahawa huo.

Wafanyakazi wa Wizara wawang'ong'a Makatibu Wakuu wao


Wakati hilo likifanyika, Ikulu jijini Dar es Salaam imesema Katibu Mkuu au mtumishi yeyote wa umma atakayeshindwa kwenda na kasi na mabadiliko ya utendaji kazi katika serikali ya awamu ya tano ajiondoe.

Tamko hilo linalotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alipohojiwa jana kwa njia ya simu kuhusu kutokuwapo kwa makatibu wakuu wa wizara kadhaa kwenye ofisini zao wiki iliyopita. Uchunguzi wa Nipashe umebaini kuwa baadhi ya ofisi za viongozi hao kufungwa kwa maelezo kwamba wapo nje ya jiji kikazi.

Hali ya viongozi hao kuhama jiji na kwenda mikoani imeleta mabadiliko ya utendaji kazi wao baada ya miaka ya nyuma kuzoeleka kutumia muda mwingi ofisini na kuacha kazi za nje kufanywa na waziri, naibu au watendaji wengine.

Baadhi ya wizara ambazo zilitembelewa na kukuta ofisi za Katibu Mkuu zikiwa zimefungwa ni Uchukuzi, TAMISEMI, Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano na Ujenzi.

Baadhi ya wafanyakazi wa wizara hizo ambao hawakutaka majina yao yatajwe, walisema mabosi wao kwa sasa inakuwa nadra kuonekana ofisini wakifanya kazi kwa kuogopa kuonekana wazembe.

Hatujawahi kuona katibu anakwenda mikoani kama ilivyo sasa, kila siku anakwenda huku na kule kuangalia miradi na kero za wananchi, alisema mmoja wa wafanyakazi wa moja ya wizara hizo.

Aidha Katibu Muktasi wa wizara moja, ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema kuwa moja sasa bosi wake yupo mikoani akikagua miradi ya serikali. Bosi harudi leo au kesho labda ukitaka kumuona njoo wiki inayokuja, alisema katibu huyo na kufunga mlango wa bosi wake kwa ufunguo.

Akitoa kauli ya serikali, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alisema kuanzia sasa katibu Mkuu na mtendaji wa serikali ambaye anafanya kazi kwa kusuasua ajiondoe mwenyewe.

Alisema tayari amefanya kikao na makatibu wote kuwaeleza suala hilo na atakayerudi nyuma hatakuwa na nafasi katika serikali ya awamu ya tano.

Jambo hilo tumekubaliana kwenye kikao, serikali ya awamu ya tano haitakuwa na utani kwa wale watakaoonekana hawaendi na kasi ya Rais, sasa wanatakiwa kuchagua kama wanataka kuendelea na nafasi zao au la, alisema Sefue na kuongeza:

Tafsiri ya kisheria kuhusiana na Mkuu wa Wilaya kusweka rumande watumishiPONGEZI HIZI KWA MAKONDA HAZIKUBALIKI!

Ndugu zangu, muda huu nimeona kwenye mitandao kadhaa watu wakifurahia hatua ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ndugu yetu Paul Makonda kutoa amri (ambayo imetekelezwa) ya kuwaweka ndani wataalam wa ardhi ambao walishindwa kufika eneo la kazi kwa wakati.

Binafsi siungi mkono kitendo cha watendaji kuchelewa maeneo ya kazi lakini zaidi ya yote siungi mkono kitendo cha mkuu wa wilaya kuwaweka ndani watendaji kwa kosa la kuchelewa kazini.


Madhara ya kuwachekea wakuu wa wilaya pale wanapotoa amri zinazokiuka haki za msingi za wafanyakazi ni makubwa mno. Huko nyuma tulizoea mambo haya kufanywa na wakuu wa wilaya enzi za Nyerere, hatutarajii hadi leo wakuu hawa kuendesha wilaya zao kwa amri.

Ni muhimu sana masuala ya kazi yaendeshwe kwa sheria na kanuni za kazi na huyo mtu anayefurahia mamlaka (haramu) ya ma DC kuweka watu ndani atakuwa na matatizo makubwa. Watu wanapaswa kuwekwa ndani kama wamefanya makosa kwa mujibu wa sheria na si kama apendavyo DC.

Tuijenge nchi yetu kimfumo zaidi kuliko ki-amri, nchi zinazoendeshwa kwa amri amri huwa hazifiki kokote, kama tutashindwa kujijenga kimfumo katika miaka hii mitano tukategemea kuendesha nchi kwa amri, matamko na mikwara - ikifika 2020 tutaulizana nini kilifanyika na sote tutabaki kusimulia matamko lukuki yaliyotolewa.

Nimalizie tena kwa kuwakumbusha kuwa "Afrika itajengwa na mifumo imara, watu imara hawawezi kuijenga Afrika maana siku moja watakufa, na kama watakufa bila kuacha mifumo imara - yale yote waliyoyafanya yatapotea haraka ".

Ndugu yetu DC, Paul Makonda, tujengeeni mfumo imara utakaofanya wafanyakazi wote kuwa kazini kwa wakati, (msijijenge ninyi) watu imara na amri lukuki!

SAKATA LA MAKONDA NA KUWAWEKA NDANI WATENDAJI WALIOCHELEWA – MTIZAMO WA KISHERIA;

Nilipo- post juu ya jambo hilo mjadala mkubwa wa wananchi umekuwa ni kutaka kujua sheria inaelekeza nini kwa mamlaka ya wakuu wa wilaya. Kwa uelewa wangu wa shahada ya kwanza ya sheria nimeona niwawekee hapa ufafanuzi wa kisheria kwa ajili ya faida yenu na mjadala mwingine tena.

SHERIA INASEMAJE?

Sheria ya Tawala za Mikoa ya mwaka 1997 (The Regional Administration Act) kwenye kifungu cha 15 (1) imeweka sharti muhimu kwa Mkuu wa Wilaya ikiwa atahitaji kutumia mamlaka ya kuamrisha mtu akamatwe, kifungu hicho kinamtaka afanye hivyo pale tu ambapo atakuwa amejihakikishia kuwa kosa lililotendwa na mhusika athari yake huwa ni kukamatwa na kushtakiwa na tena sheria imeweka masharti ya namna ya kushtaki.

JE KISHERIA DC MAKONDA ANA HAKI YA KUWAWEKA NDANI WATAALAM HAO?

Hapana, kisheria hana mamlaka hayo, Kosa walilotenda watalaam hawa wa ardhi ni la kuchelewa kwenye eneo la kazi, kosa la kuchelewa mahali kwenye majukumu ya kawaida ya kupima ardhi haliwezi kamwe kumfanya mtu ashitakiwe hadi pale ambapo kuchelewa huko kutakuwa kumesababisha madhara makubwa na yanayoweza kuthibitishwa mahakamani. Kwa hiyo kama Makonda amewaweka ndani anawajibika kwa mujibu wa sheria hii kuwapandisha kizimbani haraka kesho (Jambo ambalo atalikwepa kwani hawana kosa ambalo lina “amount to being arrested and tried” yaani “kukamatwa na kushtakiwa”).

JE, MAKONDA AKISHTAKIWA ANAWEZA KUPEWA ADHABU GANI?

Bahati nzuri, sheria hiyohiyo katika kifungu cha 15 (1) imeeleza kuwa ikiwa mkuu wa wilaya atatumia mamlaka yaliyowekwa na kifungu husika kwa maana ya kutumia madaraka yake vibaya, atakuwa ametenda kosa na anaweza kushtakiwa kwa mujibu wa kifungu cha 96 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code).

Kifungu hicho cha 96 (1) na (2) kinaeleza kuwa Mtu yeyote ambaye ameajiriwa kwenye utumishi wa umma (akiwemo Mkuu wa Wilaya) anayetenda au kuamrisha utendekaji wa jambo kwa kutumia vibaya madaraka ya kazi yake, kitendo chochote cha dhuluma ambacho kinazuia haki ya mwingine atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani anaweza kufungwa miaka mitatu jela.

JE WATAALAM HAO WA ARDHI WANAWEZA KUMSHITAKI MAKONDA?

Ndiyo, wataalam wa Ardhi waliotendewa amri hiyo wanaweza kumshitaki Paul Makonda kwa kitendo chake cha kutumia vibaya madaraka yake lakini bahati mbaya itakayowakuta ni kwamba Sheria hiyo hiyo ya Kanuni ya adhabu kwenye kifungu cha 96 (3) imeweka sharti lingine kuwa Uendeshaji wa shitaka kwa husika hautaanzishwa mpaka kitakapotolewa kibali cha Mkurugenzi wa Mashitaka (Kesi ya Nyani amekabidhiwa ngedere).

Nawatakia jioni njema sana.

Na. Julius Mtatiro

Pope Francis' speech in Uganda

People hold candles as they wait for the arrival of Pope Francis for a meeting with catechists and teachers during his visit to Munyonyo, Uganda, Friday, Nov. 27, 2015. Pope Francis is in Africa for a six-day visit that is taking him to Kenya, Uganda and the Central African Republic. (AP Photo/Andrew Medichini)

Mr President,

Pope Francis' speech in Kenya

Pope Francis addresses leaders after arriving in Nairobi Wednesday, including Kenya's President Uhuru Kenyatta. - EPA
Mr President,

Simu kwa kiongozi mmoja wa juu wa CCM...

WHERE IS CCM? (CCM IKO WAPI?)

Na. Mtatiro J,

Rafiki yangu mmoja leo amenivunja mbavu, ananiambia juzi alimpigia simu kiongozi mmoja wa juu wa CCM ambaye wakati wa kampeni alikuwa ni kati ha watu 50 muhimu waliosimamia, kupigania na kulinda ushindi wa Magufuli (achilia mbali utata wa ushindi huo, hâta hivyo kikatiba tayari Magufuli ni Rais).

Simu ile ilikuwa kutaka kujua maoni ya mwana CCM huyo nguli juu ya KASI YA UTENDAJI WA MAGUFULI na kwamba CCM inafarijika kwa kiasi gani. Jibu alilopewa mwandishi ni "NO COMMENT...", kwamba mwana CCM huyu aliyempigania Magufuli, hana maoni juu ya utendaji wa siku 22 za awali.

Kisa hiki kikanipa tafakari muhimu sana siku ya leo, kwamba mbona hatuoni matamko mazito ya taasisi na ngazi za uongozi ndani ya CCM kusifia kwa uwazi hatua za bosi wao? Mbona sioni UVCCM, UWT, lile baraza la wazee la CCM na ile Idara ya vyuo vikuu? Mbona sioni pilikapilika za CCM kama chama kujawa na furaha kubwa sana? Kuna nini?

Mara kadhaa nimeona mwana CCM mmoja mmoja akitoa katamko kake hapa Facebook kusifia utendaji wa Magufuli, sijaona CCM kama chama tena chini ya Mwenyekiti wake JK kikisimama hadharani kupongeza, kuunga mkono na kutangaza rasmi kuwa KIMBIZA KIMBIZA hii ya Magufuli ndiyo hasa chama kiliisubiri.

Niliambiwa Mwenyekiti wa CCM yuko Ethiopia, huwenda akirudi atatoa tamko zito la kuunga mkono juhudi hizi, maana yule Rais wetu mstaafu ni muungwana na mtu asiye na makuu.

Ukianza kuona CCM inapata kigugumizi kusimama hadharani kupigana upande wa Rais wake, ujue basi WANAISOMA NAMBA. Na wale wenzangu na mimi waliodhani kuwa sijui upinzani utaisoma namba, warudi walitizame hili tena, liko kinyume.

Jambo hili linanifanya nianze kuona kuwa kumbe wengi wa wana CCM na vigogo wa CCM walimpigania Magufuli abakie madarakani si kwa lengo la kuleta mabadiliko bali ilikuwa ni kwa uhakika kuwa CCM itaendelea kuwepo kwenye dola na mirija yote ya wizi na ma DEAL makubwa vitapotea.

Wana CCM wengi huwenda waliamini katika kuendelea kuongoza dola kwa lengo lile lile la kutafuna pesa, kujenga ukuu n.k. Sijui kama kati yao hâta kuna asilimia kumi walidhani kuwa mambo yatakuwa TOO SERIOUS like what it seems to be!

Kama ni kuisoma namba, basi itasomwa humo CCM ndani kwa ndani. Na ikisomwa huku nje itawahusu mafisadi na matajiri wanaoifadhili CCM usiku na mchana, ita BACK FIRE kwa CCM yenyewe.

Sisi wengine ambao hatukuwahi kuishi kwa kutegemea NETWORK za CCM wala fadhila za vyeo, mali n.k. tuna amani télé mioyoni mwetu, hofu ni kwenu ninyi wenzetu.

Mtatiro J.

Waziri Mkuu: Tumedhamiria kuwatumikia Watanzania; Serikali hii siyo ya watu wapole

Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa kanisa la Africa Inland Church wakati alipohitimisha maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo katika Dayosisi ya Pwani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere Kilwa Road jijini Dar es Salaam Novemba 29, 2015.

Waziri Mkuu Majaliwa afunga maadhimisho ya miaka 20 ya Dayosisi ya Pwani ya Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT)WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuhakikisha kila kinachokusanywa kama mapato ya nchi kinatumika kwa maslahi ya Watanzania wote na si kwa manufaa ya wachache.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumapili, Novemba 29, 2015) wakati akifunga maadhimisho ya miaka 20 ya Dayosisi ya Pwani ya Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) kwenye ukumbi wa PTA, viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Serikali imeanza kukabiliana na upotevu wa mapato ya Serikali na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima ya fedha za umma. Nia yetu ni kuhakikisha kila kinachopaswa kukusanywa kama mapato ya nchi, kikusanywe na kitumike kwa masuala ya msingi kwa ustawi wa Watanzania wote na si kwa watu wachache,” alisema.

Akifunga maadhimisho hayo kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu alisema Serikali imedhamiria kupambana na maovu yote na kuondoa kero zinazowaumiza wananchi wa kawaida. “Wako watu wanaoamini kwamba hatuwezi, nawaomba waondoe hiyo dhana. Wako watu wanaodhani kwamba kwamba utawala huu ni wa watu wapole, nao pia waondoe hiyo dhana,” alisema huku akishangiliwa na mamia ya waumini waliohudhuria sherehe hizo zilizoanza Novemba 27, 2015.
“Tunawaomba Watanzania wote mtuunge mkono kwenye vita hii na mtuwezeshe kuifanya kazi hiyo. Tunaomba waumini wote mtuombee katika sala zenu za kila siku ili tuweze kuongoza kwa haki na kuwaletea Watanzania wote maendeleo,” aliongeza.

Akinukuu kitabu cha Mithali sura ya 29 mstari wa pili, Waziri Mkuu alisema: “Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi, bali mwovu atawalapo, watu huugua. Mtuombee viongozi wenu tuwe waadilifu na wenye kutenda haki. Nasi tutaendelea kuwa waadilifu ili watu wetu wasigue,” alisema.

Aliwataka viongozi wa kanisa hilo waendelee kuisaidia Serikali katika kujenga kundi la watu wenye maadili mema ili walisaidie Taifa kuwa na watu waadilifu na hivyo kupunguza kero nyingi zinazoikabili jamii.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na waumini wa kanisa la hilo kutoka mikoa mbalimbali, Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT, Askofu Silas Kezakubi alisema Kanisa hilo litaendelea kumuombea Rais Dkt Magufuli na viongozi wenzake ili wawe na afya njema, wawe na hekima na kuahidi kwamba wataendelea kuwaweka chini ya ulinzi wa Mungu siku zote.

Alisema wao kama kanisa wanaamini kwamba Serikali ya awamu ya tano ina nia ya kuwatumikia wananchi kwa bidii na uadilifu lakini akasisitiza kuwa siri ya bidii na uadilifu inapatikana kwenye neno la Mungu.

Akisoma risala ya kanisa hilo, Askofu wa AICT Dayosisi ya Kibaha, Askofu Charles Salalah alisema kanisa halina budi kushirikiana na Serikali kwa sababu wote wanawahudumia watu walewale isipokuwa katika malengo tofauti.
Alisema kanisa hilo linahubiri maadili mema na bidii katika kazi kwa vile linaamini kuwa maendeleo hayadondoki kutoka juu wala hayaoti kama uyoga bali yanapatikana kwa watu kufanya kazi.
Akisisitiza kuhusu uadilifu, aliwataka wazazi kudumisha ndoa zao ili watoto wapate malezi mema kutoka kwa baba na mama na kwamba baba na mama wasipokaa vizuri, watoto hawawezi kuwa waadilifu.
“Wazazi tunao wajibu wa kupanda mbegu bora ya uzalendo kwa watoto wetu. Endapo tutapanda mbegu mbaya ya kuwagawa watoto wetu kwa itikadi tofauti, ni lazima tujue kuwa tutavuna tunachopanda.”

“Tukumbuke kuwa tunalo Taifa moja tu la Tanzania. Hata kama watoto wetu watakuwa na upenzi na vyama vyao, ni lazima tuwalee katika misingi ili wakue wakijua Taifa letu ni moja tu. Ndiyo maana tunaweka mkazo kwenye familia kwa sababu maadili mema yanaanzia nyumbani,” alisisitiza.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMAPILI, NOVEMBA 29, 2015.Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipohitimisha maadhimisho ya miaka 20 ya Kanisa la Africa Inland Church Dayosi ya Pwani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015


Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akiwa meza kuu na viongozi wa kanisa la Africa Inland Church wakati alipohitimisha maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo katika Dayosisi ya Pwani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015.

Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim majaliwa akiwash moja ya pikipiki tatu ili kuashiria mkaka ti wa kueneza injili wakati alipohitimisha maadhimisho ya miaka 20 ya kanisa la Africa Inland Church Dayosisi ya Pwani kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere, Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

[audio] "Tutawakomesha kwa urais, cha mtema kuni watakiona" Asante KombaKutimiza agizo la Rais: MSD yaanza kukarabati jengo la duka la dawa Muhimbili


Mafundi wakikarabati jengo ambalo Bohari ya Dawa (MSD), itafungua duka la dawa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MSD) Dar es Salaam jana kwa ajili ya kuhudumia wananchi kwa karibu zaidi vikiwemo vifaa tiba. Duka hilo linatarajiwa kufunguliwa kesho kutwa.

Na Dotto Mwaibale

BOHARI ya Dawa (MSD) imejiimarisha na kuhahikisha inatekeleza kwa wakati agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuweka maduka ya dawa katika hospitali za rufaa na kanda nchini.

Katika kutekeleza agizo hilo MSD imeanza kwa kasi kubwa ya kukarabati jengo la duka la dawa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), ambalo linatarajiwa kufunguliwa kesho.

Mwandishi wa habari hii alishuhudia jana kasi kubwa ya mafundi ujenzi wakikarabati jengo hilo ambalo awali lilikuwa likitumika kama stoo ya kuhifadhi vitu mbalimbali vya hospitali hiyo.

Akizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni kuhusu ufunguzi wa maduka hayo, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laureane Bwanakunu alisema agizo la Rais la kuitaka MSD kuanzisha duka la dawa karibu na hospitali limekuja wakati muafaka kwani kwenye mpango mkakati wa miaka sita wa MSD tayari ilikuwa na mpango wa kufungua maduka hayo kwa ajili ya kusogeza huduma karibu a wananchi.

Alisema maduka ya MSD ambayo yatafunguliwa kwenye hospitali za rufaa na kanda yatafanya kazi masaa 24 na kuuza dawa na vifaa tiba chini ya bei ya soko pia yatahudumia watu binafsi na wale waliopo kwenye taratibu za Bima ya afya kote nchini.

"Ili kudhibiti watumishi wasio waaminifu kuiba dawa MSD inafanya kazi za uagizaji, uhifadhi na usambazaji kwa kutumia mfumo wa mtandao wa E9 na tangu mwaka wa fedha uliopita tumeanza kuziwekea alama ya GOT bidhaa zetu ikiwa ni pamoja na vidonge." alisema Bwanakunu.

Alisema vidonge ambavyo tayari vimewekewa nembo ya GOT vipo 45 na wanaendelea kuwapa maelekezo wazabuni ili vyote viwekwe alama hizo..,nembo ya serikali inaonekana kwenye dawa za serikali kama Diclofenac, moxillin, iprofloxacin, Contrimoxale,paracetamol, na magnesium.

Alisema wanatarajia kuanzisha huduma ya kutoa taarifa kwa njia ya simu pale wananchi watakapoona kuna wizi wa dawa za serikali na kwamba wananchi wanaelimishwa kutoa taarifa pale wanapoona dawa za serikali mitaani.

Alisema, pamoja na serikali kuanza kupunguza deni lake linalodaiwa na MSD bado inadaiwa Sh.bilioni 53.

Fundi akitoboa ukuta sehemu litakapo fungwa beseni la kunawia katika duka hilo.

Mafundi wakiendelea na ukarabati wa jengo hilo lililopo jirani na wodi ya Kibasila linalotizamana na maegesho ya magari.

Fundi akipaka rangi ndani ya jengo hilo.

Jengo la duka hilo la MSD linavyoonekana kwa nje. Hapa mafundi wakiendelea na kazi ya ukarabati.

Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com