Alichokutana nacho Mkuu wa Wilaya akikagua vyoo ShinganyaHiki choo cha ajabu kiko Shinyanga maelezo yapo chini.Leo Jumatatu Novemba 30, 2015 ambapo mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ameanza kufanya ziara kutembelea kata za manispaa hiyo ili kuangalia hali ya usafi wa mazingira kubwa zaidi ni kukagua vyoo vya wananchi ili kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu.

Call: Visiting reserch fellowships, Univ. of Cambridge Centre of African Studies

CALL FOR APPLICATIONS: VISITING RESEARCH FELLOWSHIPS 2016-17


The Centre of African Studies invites applications for two Visiting Research Fellowships from candidates in all the disciplines in the humanities and social sciences.

The aim of the Fellowships is to enable the fellows to focus on a period of research and writing in Cambridge. Preference will be given to early- to mid-career candidates with a distinguished research profile. They are expected to be permanent residents in Africa.

The appointments will take place from 1 October 2016 – 31 March 2017 and are non-renewable. Each award is worth up to £14,000; out of which travel, college accommodation, maintenance costs and medical insurance will be paid by the Centre on behalf of the fellow.

The closing date for applications is 15 January 2016

The University follows an equal opportunities policy An application package may be downloaded from our website: www.african.cam.ac.uk or contact the Centre by emailing: [email protected]

This programme is generously supported by the A. G. Leventis Foundation University of Cambridge Centre of African Studies Alison Richard Building 7 West Road Cambridge CB3 9DT United Kingdom

Senti mbili za Mwl. Mabala kwa CHADEMA

Thinking out of the box

Ningekuwa kiongozi wa CHADEMA, ningewashauri wenzangu kwamba maana ya upinzani si kupinga tu. Pamoja na kupinga mambo mengine, kama uchakachuaji wa uchaguzi wa Zanzibar na matumizi ya nguvu dhidi ya wanaCHADEMA, bado tungemshukuru Magufuli kwa kuiba sera yetu na kuanza kuitekeleza kabla hatujapata nafasi ya kufanya hivyo sisi wenyewe. Kisha tungeomba wanaCHADEMA wote tuungane naye katika mpango wa HapaMabadilikoTu katika kuhakikisha kwamba vita dhidi ya mafisadi, wakwepa kodi, wazembe, wala rushwa na wengine haiishii kwa wachache wanaofikiwa na yeye na badala yake vita iwe na Nguvu ya Umma kabla mafisadi hawajaweza kutafuta mbinu ya kuizuia.

Wananchi wanapenda kuona hatua zinachukuliwa lakini mmeona chama chake kikifurahi? Mmeona wakiandamana kumwunga mkono. Huu ni wakati muafaka kwa matumizi ya Pipozzzz Pawa katika kukomesha ufisadi wote.
Imenukuliwa kutoka kwenye ukurasa wake Facebook

British court approves landmark plea deal over Standard Bank bribery (on $6 million in bribes paid to Tanzanian officials)

The following news story is a cross-post from REUTERS, Business News. You may click here for the same, from other news sources, and read more.

LONDON | BY ESTELLE SHIRBON

A judge approved Britain's first deferred prosecution agreement (DPA), a new type of plea deal, on Monday in a case centred on $6 million in bribes paid to Tanzanian officials by the Tanzanian unit of South Africa's Standard Bank (SBKJ.J).

Under the deal with the Serious Fraud Office (SFO), the London arm of Standard Bank, which worked with the bank's Tanzanian subsidiary on a 2012-2013 transaction to raise $600 million (£399 million) for the Tanzanian government, faces penalties totalling $32.2 million after admitting to failing to prevent bribery.

Introduced into English law last year, a DPA is a court-approved deal under which a company charged with wrongdoing agrees to sanctions that can include fines and additional supervision, in return for legal proceedings being suspended.

The penalties in this case include a $16.8 million fine to be paid to the SFO, a $6 million fine plus interest of over $1 million to be paid to the government of Tanzania, and $8.4 million in disgorgement of profits.

London-based Standard Bank Plc has since changed its name to ICBC Standard Bank following the acquisition of a controlling stake by China's ICBC earlier this year.

The new DPA procedure is seen as a potentially useful tool for British law enforcers to tackle corporate wrongdoing as prosecuting companies in Britain can be very costly and complex.

"This landmark DPA will serve as a template for future agreements," Director of the SFO, David Green, said in a statement after the agreement was approved by senior High Court judge Brian Leveson at a public hearing.

Handing down his judgement after hearing a detailed account of the facts and of how the SFO had arrived at those figures, Leveson said the DPA was "fair, reasonable and proportionate" and was in the public interest.

Lawyers predicted that the DPA would be the first of many.

"There has been fairly widespread concern that the U.S.-style plea deals present a way for big companies to simply 'buy their way out of trouble'," said Barry Vitou, partner and head of Global Corporate Crime at law firm Pinsent Masons.

"The bar in the UK will, however, be set much higher. A key difference here is that judges will independently assess DPAs, and will only sign off on them if they are in the interests of justice," he said.

CASH WITHDRAWALS

The case stems from a sovereign note private placement undertaken in 2012-2013 by Stanbic Bank Tanzania Ltd and London-based Standard Bank Plc to raise $600 million for the Tanzanian government as part of its five-year development plan.

In a lengthy statement setting out the details, SFO counsel Edward Garnier told the court that Stanbic and Standard Bank had initially quoted a fee of 1.4 percent of gross proceeds raised, but matters did not progress until that went up to 2.4 percent.

Evidence showed that the additional 1 percent, worth $6 million, was paid to a "local partner", a Tanzanian company called EGMA, for supposed consultancy services.

These arrangements were made by Bashir Awale, then chief executive of Stanbic, and Shose Sinare, then the unit's head of corporate and investment banking. Awale was later sacked, while Sinare resigned.

EGMA's chairman and one of its three shareholders and directors was Harry Kitilya, then head of Tanzania's tax authority, while its managing director was Fratern Mboya, ex-CEO of Tanzania's Capital Markets and Securities Authority.

Garnier said the purpose of the $6 million was to induce government officials to show favour to Stanbic in appointing it to conduct the private placement, and to reward those whom Awale and Sinare believed had been induced to act improperly.

The money was deposited into an EGMA account in March 2013, and withdrawn by Mboya in large cash amounts within days. Garnier told the court the cash has never been traced.

The cash withdrawals raised suspicions within Stanbic Tanzania, with four employees raising concerns. After those were escalated to head office in South Africa and to London, the UK-based subsidiary reported itself to law enforcement agencies.

Standard Bank Group said in a statement it had fully cooperated with investigators from the outset.

"The group and its subsidiaries take the risk of corruption very seriously and deeply regret that this issue arose on a transaction with which they were involved," it said.

Kitilya resigned from the tax authority in December 2013, while Mboya died in July that year.

ICBC, which acquired 60 percent of London-based Standard Bank in February, had no direct interest in the bank at the time of the corrupt transaction, and had no involvement in the incident in any way.

(Editing by Susan Fenton)

Mbinu 10+1 za namna kodi inavyokwepwa bandarini Dar


Wakati Serikali ikikunjua makucha yake dhidi ya wote waliohusika katika kashfa ya kupitisha makontena 349 kwenye Bandari ya Dar es Salaam bila ya kuyalipia kodi, imefahamika kuwa idadi hiyo ya makontena ni sehemu ndogo tu ya mamia ya mizigo yanayovushwa kinyemela kila uchao na kuikosesha serikali mabilioni ya fedha.

Hata hivyo, wakati serikali ya Rais Magufuli na Waziri Mkuu wake, Kassim Majaliwa, ikiendelea kutafuta suluhu ya kudumu kuhusiana na ukwepaji kodi, imebainika kuwa kazi hiyo siyo lelemama kwani zipo njia zaidi ya tisa zinazotumiwa kukwepa kodi katika Bandari ya Dar es Salaam.
 • Mosi, ni kupitia mwanya utokanao na mfumo wa zamani wa malipo usiohusisha ule wa sasa wa kielektroniki, maarufu kama ‘E-Payment’.
Kwamba, wafanyabiashara wengi hutumia mfumo huo wa zamani unaohusisha matumizi ya karatasi zilizojazwa kwa mkono na hivyo kuwezesha ujanja wa kubadili taarifa kwa manufaa ya mitandao ya wakwepaji wa kodi.

“Tatizo lililopo ni kwamba mfumo wa E-Payment ni mpya (umeanza Julai) na umefungwa kwenye benki moja tu iliyopo ndani ya eneo la Bandari… ule wa zamani unaendelea kutumiwa na wajanja hucheza na maandishi ya kujaza kwa mkono kuhujumu mapato ya serikali,” chanzo kimeeleza.
 • Njia ya pili ya kuhujumu mapato bandarini hapo, imetajwa kuwa ni ya kushirikiana na maafisa wa benki. Hii ina uhusiano mkubwa na njia ya kwanza inayohusisha matumizi ya mfumo wa malipo wa zamani usiokuwa wa kielektroniki.
Mfanyabiashara anaweza kuandikiwa kodi sahihi anayotakiwa kulipa, lakini anashirikiana na wafanyakazi wa benki anayokwenda kuweka fedha kwa kuhakikisha kuwa baada ya kufanikiwa kuondoa kontena bandarini, maafisa wa benki husika husitisha malipo hayo kwa kuondoa fedha husika kwa madai kuwa fedha ziliingizwa kwenye akaunti husika kimakosa.

“Huwa kuna ushirikiano wa karibu kati ya maafisa wa benki na mfanyabiashara husika. Baada ya kontena kutolewa bandarini, hamisho la fedha (transaction) huondolewa katika mfumo kwa maelezo kuwa halikuwa sahihi,” chanzo kimedai, huku kikisisitiza kuwa ushirikiano huo huhusisha pia watu wa Bandari na TRA ambao mwishowe hugawana malipo kadri wanavyokubaliana.
 • Tatu, ni mwanya wa uvushaji wa makontena yenyewe yasiyolipiwa ushuru kupitia mageti maalum yanayofahamika kwa kazi hiyo, hasa geti Namba 3 ambalo chanzo kimedai ndilo linaongoza kupitisha mizigo ya ‘dili’.
“Kwa ujumla yapo mageti matano ya kupitisha bidhaa mbalimbali, baadhi yakiwa ni ya kupitihia mafuta, nafaka na magari.

"Hili Namba 3 ndiyo hutumika kupitisha makontena ya bidhaa zenye thamani kubwa na wengi wasiolipa kodi hulitumia hili,” chanzo kilieleza kabla ya kufafanua kuwa awali, hilo geti Namba 3 halikuwa na mfumo wowote wa kuangalia kama kontena husika limelipiwa au la na ndiyo maana lilikuwa likitumika zaidi kupitisha makontena yasiyolipiwa kodi.
 • Njia ya nne ya kuhujumu kodi ya mapato ni ya kuwatumia watu wanaoendesha bandari kavu (ICD’s). Inaelezwa kuwa hivi sasa kuna bandari kavu 12, ambazo kila meli inapoingia hujulikana kila mzigo husika unapelekwa kwenye bandari ipi kati ya hizo.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa kinachofanyika ni kwa baadhi ya makontena yanayotolewa bandarini ili yapelekwe bandari kavu kabla ya kukombolewa na wahusika huishia kupelekwa kwa wafanyabiashara wenye makontena na hivyo kuikosesha mapato serikali.

“Awali kwenye ICD’s kulikuwa na askari wa mmiliki wa ICD’s na siyo wa TPA… huyu alikuwa akiangalia malipo ya bosi wake tu ambayo ni gharama za kuhifadhi mzigo na hivyo TPA na TRA huambulia patupu,” chanzi kimeeleza, kikiongeza kuwa hivi sasa walau kuna nafuu kwani kwenye ICD’s kuna walinzi wa TPA lakini hilo limefanyika baada ya watu kuwa tayari wameshaiba sana.
 • Njia ya tano inayotumiwa kukwepa kodi ni ya kubadili taarifa, hasa kupitia watu wenye wajibu wa kufanya tathmini. Kwamba, badala ya mzigo kukadirwaa kodi kwa kiwango sahihi, wahusika ambao zaidi huwa ni watu wa TRA hukadiria fedha kidogo baada ya kujihakikishia kuwa nao wanapewa mgawo na wafanyabiashara.
“Hapo utakuta kontena la kodi ya milioni 80, mteja anaambiwa alipe milioni 40 tu … na wakati mwingine kiasi hicho pia hakiandikwi balki huandikwa cha chini zaidi kama milioni 5 tu…hii ni njia nyingine inayoligharimu taifa mabilioni ya fedha,” chanzo kimeeleza.
 • Njia ya sita inayofanikisha ukwepaji kodi ni mtandao mpana wa baadhi ya vigogo wa maeneo mbalimbali Bandarini na TRA, ambao hawa huhakikisha kuwa wanakuwa na timu ya vijana wao wa kazi karibu katika kila eneo ili kufanikisha mipango yao.
“Hii ndiyo njia kubwa ya hujuma. Kama utakumbuka aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, alisambaratisha baadhi ya mitandao kwa kuwagusa vigogo 27… ile ilikuwa kuvunja mtandao uliokuwapo. Hilo lilisaidia kiasi, lakini sasa ipo pia mitandao mingine ambayo uchunguzi ukifanyika utabaini kuwa mambo yameanza kurudi kama zamani,” imeelezwa.
 • Njia ya saba ya ukwepaji kodi ni kwa baadhi ya vigogo wa Bandari na TRA kuanzisha kampuni zao za uondoaji mizigo bandarini. Inaelezwa kuwa hizi hutumiwa sana kufanikisha ‘dili’ za ukwepaji kodi na ndiyo maana haishangazi kusikia kuwa kuna makontena zaidi ya 300 hayaonekani kwenye kumbukumbu za TRA.
 • Njia ya nane ya ukwepaji kodi ni kuonyesha kuwa kontena linapelekwa nje ya nchi, kwa mfano Malawi, wakati ukweli ni kwamba huishia hapahapa nchini.
“Utakuta kontena linadaiwa kupelekwa Malawi, lakini linachukuliwa na gari kukuu linaloonekana wazi kuwa haliwezi kufika hata Kibaha… njia hii pia hutumiwa sana kuikosesha serikali mapato,” chanzo kingine kilisema
 • Njia ya tisa ya ukwepaji kodi ni ucheleweshaji wa makusudi wa utoaji makontena. Kwamba, mteja anapotaka kutoa mzigo wake kwa kufuata njia halali zilizopo, huishia kuzungushwa kila uchao ili akubali kutoa rushwa na mwishowe kulipishwa kiwango pungufu cha kodi au kulipa fedha zisizoingia kabisa kwenye mikono ya TRA.
 • Njia ya kumi ni ubabaishaji unaofanyika katika kuorodhesha idadi ya makontena inayotolewa bandarini kwenda kwenye bandari kavu. Hapa, kama makontena yanayotolewa ni 12, basi huandikwa kuwa ni 10 na mengine mawili huishia kuondolewa bila ya kuwa na kumbukumbu zake kwa ajili ya kulipiwa kodi.
 • Pamoja na kuwapo kwa njia zote hizo, chanzo kimedai kuwa sababu kubwa ya kufanikiwa kwa ukwepaji kodi ni mtandao mpana unaoundwa na vigogo mbalimbali na ndiyo maana taarifa mbalimbali za wakaguzi wa ndani na wa nje katika Bandari ya Dar es Salaam huishia kubaki kwenye makabrasha bila ya kuwapo kwa utekelezaji wowote wa vitendo juu ya yale yanayopendekezwa na wataalamu.

Zoezi la bomoa bomoa lapiga hodi KahamaZoezi la bomoa bomoa linaloendelea nchini kwa kubomoa nyumba zilizojengwa kwenye maeneo ya wazi limeingia wilayani Kahama kwa hatua ya kwanza ambayo itazikumba kata za Kahama Mjini, Majengo, Nyahanga, Nyasubi na Nyihogo.

Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Kahama Anderson Msumba ambaye amesema kwa kuanza katika Kata hizo tayari viwanja 48, wamiliki wake amewataka wawasilishe ofisini kwake nyaraka za kumiliki maeneo hayo.

Msumba amesema baada ya zoezi hilo la kuwasilisha nyaraka za umiliki wa maeneo hayo zitachunguzwa upatikanaji wake na hati miliki zitapelekwa kwa Waziri mwenye dhamana kwa ajili ya kufutwa na baadaye zoezi la kubomoa litaanza kwa maeneo hayo.

Ameagiza umiliki wa maeneo ya hoteli za CDT na zahanati ya Community Health Dispensary uchunguzwe na hatua za ubomoaji ziendelee ikithibitika madai kuwa maeneo hayo ni ya wazi. Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili katika Halmashauri hiyo Joachim Henjewele, tayari kikosi chake cha ramani na mpango mji kimeanza uchunguzi kwenye eneo hilo ambalo linadaiwa kuwa ni la wazi ambalo lilikuwa miliki ya vijana kabla halijavamiwa na watuhumiwa hao.

ACT-Wazalendo yajia juu mpango wa SFO na Benki ya Standard wa kuzika tuhuma za rushwa ya trilioni 1.2/=


Taasisi ya Serious Fraud Office ya Uingereza ( SFO ) inafanya mazungumzo na Benki ya Standard Group ya Afrika ya Kusini Lakini iliyoorodheshwa katika soko la hisa ya Uingereza ( London Stock Exchange ) ili kumalizana kuhusu tuhuma za rushwa katika ununuzi wa hati fungani za Serikali ya Tanzania yenye thamani ya dola za kimarekani milioni Mia Sita ( $ 600m ). Mazungumzo hayo yanafanywa mbele ya Jaji katika mji wa London.

Ndugu wanahabari, ni jambo la kawaida kwa serikali yoyote duniani kuuza hati fungani. Mnamo mwaka 2011/2012 Serikali kupitia Wizara ya Fedha iliuza hati fungani ( Bonds ) zenye thamani ya dola za kimarekani 600 milioni ($600 million), dhamana hizo za serikali zilinunuliwa na benki ya kigeni (Stanbic) ambayo ni mali ya Standard Group ya Afrika ya Kusini, yenye makao makuu yake huko London, Uingereza.

Hata hivyo, sehemu ya fedha hizo haikuingia kwenye akaunti za Serikali ya Tanzania na pia gharama za Bond hiyo zilipaishwa kupitia wakala wa kati kati ( middle men ) na hivyo kupelekea rushwa ya takribani $60 milioni kutolewa Kwa maafisa waliothibitisha biashara hiyo.

Ndugu wanahabari, taasisi za kiuchuanguzi za nchini Uingereza, hasa ile ya kushughulikia makosa ya rushwa (Serious Fraud Office-SFO) tayari imeshafanya uchunguzi wake wa awali kwa kuhusisha pande zote zinazohusika, na wamegundua kuwepo kwa rushwa kubwa katika mchakato huo, jambo ambalo liliwafanya washauri uongozi wa benki hiyo hapa nchini kuondolewa na kurejeshwa nchini Uingereza kwa hatua zaidi. Hata hivyo SFO na Standard Group wanataka kulimaliza jambo hili Kwa mtindo wa walivyomaliza suala la radar.

Ndugu wanahabari, Chama changu cha ACT-Wazalendo, kinazitaka mamlaka za kiuchunguzi hapa nchini, kuwachukulia hatua ikiwa ni pamoja na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote waliohusika na upotevu wa $600 milioni, ambazo kwa pesa ya Tanzania ni zaidi ya shilingi 1.2 trilioni. Hicho ni kiwango kikubwa sana cha fedha, ikilinganishwa na makusanyo ya Mamlaka ya Maapato Tanzania (TRA). Tunaitaka Benki Kuu ya Tanzania, FIU Tanzania na PCCB kuweka hadharani taarifa ya chunguzi zao na kueleza ni kwanini hawajachukua hatua mpaka sasa.

Ndugu wanahabari, chama cha ACT-Wazalendo, kinaunga mkono jitihada za Rais wetu Dr John Pombe Joseph Magufuli, za kutumbua majipu, hivyo tungependa kuona Mheshimiwa Rais akichukua hatua kwenye jambo hili ambalo lina maslahi mapana ya nchi yetu, hasa ikizingatiwa na uzoefu tulionao katika masakata kama hayo yanayohusisha nchi za kigeni, mfano mmojawapo ni sakata la rada, ambalo vyombo vyetu vya uchunguzi vilisema hakukuwa na rushwa, na baadaye serikali ya Uingereza ilithibitisha pasina shaka kwamba kulikuwa na rushwa, na baadaye serikali yetu ilirudishiwa sehemu ya fedha zilizozidi kwenye manunuzi ya rada ( chenji ya rada ).

Chama cha ACT Wazalendo kinasubiri taarifa ya makubaliano ( settlement ) Kati ya SFO na Benki ya Standard Group ( Benki mama ya Stanbic ) ili kushauri zaidi hatua za kuchukua. Ikumbukwe kuwa Benki ya Stanbic ndio ilihusika na kashfa ya Tegeta Escrow na mpaka sasa haijachukuliwa hatua zozote kama ilivyoagizwa na Bunge. Benki hiyo imewaficha waliochota fedha za escrow mpaka Leo.

( imesainiwa )
Masasi, 30 Novemba 2015
Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mb
ACT-WAZALENDO

Rais Magufuli, Makamu wa Rais Suluhu, Waziri Mkuu Majaliwa wazungumza


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akiagana na Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa (kulia) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 30, 2015. Wa pili (kulia) ni Naibu Katibu wa Makamu wa Rais, Mohamed Khamis

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, (kushoto) akizungumza na Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, wakati Rais na Waziri Mkuu walipomtembelea Makamu Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 30, 2015 kwa mazungumzo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, (kushoto) akizungumza na Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, wakati Rais na Waziri Mkuu walipomtembelea Makamu Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 30, 2015 kwa mazungumzo.

Notice to Tanzania Employers regarding double pay this Independence & Republic Day


Re: 9th DECEMBER 2015 - INDEPENDENCE & REPUBLIC DAY

The above subject refers.

The Association of Tanzania Employers (ATE) would like to bring to your attention that 9th December is still a Public Holiday.

The directive by the President of the United Republic of Tanzania, H.E. Dr. John Pombe Magufuli was meant to cancel parades and other government celebrations not the Public Holiday. He announced therefore that Independence and Republic Day this year will be commemorated by making general cleanliness of the environment following rapid spread of cholera in different parts of the country which has left some people dead while others remain seriously affected.

Employers are therefore advised that, if you require your employees to work on that day, you will be obliged to pay double wages as provided for in the labour laws. Employers are urged however to give all necessary cooperation during this Independence and Republic Day to make our environment clean.

Members are advised accordingly.

Yours Sincerely,
ASSOCIATION OF TANZANIA EMPLOYERS 

[signed]
Dr Gggrey K. Mlimuka
EXECUTIVE DIRECTOR

Rais Magufuli aagiza fedha za sherehe za Uhuru zitumike barabara ya Mwenge - Morocco

Sehemu ambako utaanzia upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami kufuatia agizo la Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli la kutumia fedha shilingi bilioni nne zilizopaswa kutumika kugharamia Shamrashamra za siku ya Uhuru Desemba 9, 2015 kutumika kufanya upanuzi wa barabara hiyo. (Picha: Ikulu)

Rais Magufuli azungumza na Prof. Ibrahim H. Lipumba

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba. Profesa Lipumba amempondeza Rais kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo na pia ameipongeza hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa wakati wa kufungua Bunge la 11 mjini Dodoma 30, 2015Picha: Ikulu

Rais Magufuli azungumza na Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Korea Kusini hapa nchini Mhe. Chung IL Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015. Balozi huyo pia alitumia nafasi hiyo kumuaga Rais kwa kuwa muda wake wa kufanya kazi nchini umemalizika.Rais Magufuli azungumza na Balozi wa China nchini Tanzania

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 30, 2015. 


Picha na maelezo: Ikulu.