Job: Children's Home & Nursery Coordinator - Tanzania

Organization: help2kids
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 18 Dec 2015

Maneno ya Dk Slaa kuhusu utendaji wa Rais Magufuli


KASI ya kupambana na ufisadi ya Rais Dk. John Magufuli, imefufua matumaini ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, kuhusu hatma ya Tanzania.

Hata hivyo Dk. Slaa amesema bila kuifumua Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) matarajio ya Watanzania yanaweza yasifikiwe.

Slaa ambaye alijizolea umaarufu mkubwa kama kiongozi anayepambana na rushwa kwa nguvu zote, ameliambia Raia Mwema mwanzoni mwa wiki hii kwamba, Tanzania kwa sasa inahitaji Rais aina ya Magufuli na kuwataka wananchi wamuunge mkono katika juhudi za kusafisha nchi.
“Nadhani unaelewa sasa niliposhikilia msimamo wangu, katika mazingira ya sasa Magufuli is the best (ni bora zaidi). Kumbuka nyuma niliwahi kusema nchi hii kwa siku za mwanzo inahitaji udikteta kurudisha kwenye mstari ulionyooka! Nimefurashi sana,” alisema Dk Slaa.

Akizungumzia baadhi ya madai ya watu kwamba kasi hii inaweza kujenga misingi ya uongozi wa kidikteta na kwamba inaweza kuwa na madhara ya moja kwa moja kwa maisha ya wananchi, alisema kwa jinsi ufisadi ulivyokita mizizi kwenye mfumo wa nchi zinahitajika hatua za namna hiyo kupambana nao.

“Aliahidi, anatekeleza sasa wanataka nini! Udhibitiwe (udikteta) na Bunge ili usipindukie mipaka, lakini tusilalamike tu,” alisema.

Dk. Slaa ambaye alikuwa mwiba kwa Serikali ya CCM, hasa katika Awamu ya Tatu, kwa kulipua aliyoyaita mabomu ya vitendo vya ufisadi wa baadhi ya viongozi na watumishi wa umma, alishauri ili kasi ya rais iweze kupata mwendelezo mzuri kwenye vita dhidi ya rushwa, ni lazima Takukuru isukwe upya.

“Pasipo kuchukua hatua ya kufumua Takukuru, sina hakika kama matarajio yatafikiwa. Naona inatakiwa hatua ya haraka kwa Takukuru,” alisema Slaa.

Wakati Slaa akipongeza hatua zinazochukuliwa na Rais Magufuli, baadhi ya wabunge wa CCM wanahofia kusema neno lolote kuhusu juhudi hizo.

“Kazi anafanya nzuri na sisi tunaipenda, lakini sasa ukiomba maoni yangu hadharani naweza kuambiwa najipendekeza kutafuta cheo na jamaa, hataki kusikia anapewa sifa za kujipendekeza,” alisema mbunge mmoja maarufu na kuongeza; “Haya masuala ya makontena tuliyasemea sana bungeni lakini tulionekana wasaliti na wapinzani, lakini kipindi hiki ukipongeza pamoja na hatua nzuri zinazochukuliwa na Rais tutaonekana tunajipendekeza ili tuteuliwe kuwa mawaziri.”

Taarifa ya habari ya usiku ChannelTEN Desemba 2, 2015

Katuni: Nyakati za mwisho... Kanyaga wese ng'wana wane waisome namba


Serikali haitafunga maduka ya dawa ya watu binafsi yaliyo nje ya mahospitaliSerikali imewahakikishia Watanzania kwamba mashine ya Magnetic Resonance Imaging (MRI) pamoja na Computerized Tomography Scan (CT-SCAN) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) hazitakwama kufanya kazi kwa kuwa imeweka utaratibu mzuri wa kuzitengeneza.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Donan Mmbando amesema serikali imezungumza na Philips na wamekubaliana kwamba mashine hizo hazitakwama na endapo litatokea tatizo la kiufundi watashughulikia mara moja.

“Mwaka ujao ni mwaka wa bajeti serikali itatenga fedha kwa ajili ya kutengeneza mashine za CT-SCAN na MRI, lakini mtambue kwamba si tu mashine hizo zinapaswa kutengenezwa bali na mashine nyingine.”amesema Dk Mmbando.

Pia, Dk Mmbando amefungua duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kueleza kwamba kufunguliwa kwa duka hilo kutasaidia wananchi kupata huduma haraka na kununua dawa kwa gharama nafuu na huduma hiyo itatolewa kwa saa 24.

Akifafanua kuhusu mashine za MRI na CT-Scan, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Mseru amesema Novemba 25, 2015 alifika fundi kutoka Afrika Kusini ambaye pia ni fundi wa MRI na kuitengeneza na kuanza kufanya kazi tangu Novemba 26 mpaka Disemba 2, mwaka huu. Wagonjwa 152 wamepimwa na kwamba wengi wagonjwa wa dharura.

Amesema hivi sasa mafundi wanafunga mashine ya Digital X-Ray iliyotolewa na serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambapo usimikaji unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa juma hili.

Akielezea utekelezaji wa agizo la wagonjwa wanaolala chini kupatiwa vitanda, Profesa Mseru amesema ili kuondoa wagonjwa wote waliolala chini, serikali kupitia MSD ilileta vitanda 300 pamoja na magodoro yake, vitanda hivyo vyote vilipelekwa kwenye Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na tayari MOI imeanza kuhamisha wagonjwa waliokuwa wamelala chini kutoka wodi za MNH walizokuwa wanazitumia, mpaka sasa wagonjwa 120 wamehamishwa.Novemba 9, mwaka huu Rais John Magufuli alifanya ziara MNH na kutoa maagizo kwamba ndani ya wiki mbili mashine ya MRI na CT-SCAN ambazo zilikuwa zimeharibika ziwe zinafanya kazi, wagonjwa waliolala chini wawe wamepata vitanda na Bohari Kuu ya Dawa (MSD) ifungue duka la dawa ndani ya hospitali ili kuondoa ukosekanaji wa dawa.

Serikali yatangaza ukomo wa kuisaidia TAZARA


Makonda azuia matumizi ya nguvu na kueleza sababu ya kushindwa kukoromea Urafiki walipe deni la wafanyakaziWanauliza namna ya kupata vitambulisho kama Katibu Mkuu Kiongozi alivyoonesha mfano

Ombeni Sefue
Ombeni Sefue
Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue ameendelea kuwasisitiza watumishi wa umma kuvaa vitambulisho (badge) vinavyowatambulisha majina yao wanapokuwa katika maeneo ya kazi.

Mhe. Balozi Sefue aliutoa mwito huo jana wakati akijibu swali la mwandishi wa habari aliyemuuliza ni sababu ya kuvaa kitambulisho chenye jina lake tofauti na siku nyingine.

Alisema mwishoni mwa mwezi wa kumi na moja alifanya ziara ya kutembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuagiza watumishi wote wa umma kuvaa vitambulisho vinavyowatambulisha majina yao.
“Nimeamua kuonyesha mfano kwa vitendo kufuatia agizo nililolitoa kwa watumishi wa Umma kwa kuvaa beji inayonitambulisha jina langu , nilisema nitakuwa wa kwanza kuvaa jina langu nimevaa. Kama mtumishi wa umma atakuwa na mashaka ajue mimi nimeshalivaa”
“Mtumishi wa umma anapomuhudumia mwananchi ni lazima ajue amehudumiwa na nani, mtumishi wa Umma akifanya kazi zake kwa kutenda haki sidhani kama ataogopa kuvaa beji inayomtambulisha jina lake hivyo basi kama nilivyoagiza watumishi wote wa Umma mvae beji zinazowatambulisha majina yenu” 
alisisitiza Mhe. Balozi Sefue  aliyefanya mkutano na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam na kutoa taarifa ya Serikali kuhusu kesi ya Serious Fraud Office (SFO) dhidi ya Standard Bank.

------- MWISHO -------

PS: Baadhi ya wafanyakazi wanauliza utaratibu wa namna ya kupata vitambulisho hivi.

Thomson Reuters and ICD launch the Islamic Finance Development Indicator

PRESS RELEASE

MSD yazindua huduma za duka la dawa hospitali ya MuhimbiliNa Dotto Mwaibale

SERIKALI imesema haiwezi kufunga maduka ya dawa binafsi yaliyopo nje ya hospitali hapa nchini na badala yake kuimarisha upatikanaji wa huduma za dawa katika duka la bohari Kuu ya Dawa (MSD) katika hospitali hizo.

Hali hiyo imefika kutokana na agizo la rais John Magufuli wakati alipofanaya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) iliyopo jijini Dar es Salaam Novemba 9 mwaka huu.

Akizungumza jijini humo wakati wa uzinduzi wa Duka la Bohari ya Dawa (MSD) hospitalini hapo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mbando alisema upatikanaji wa duka hilo hospitalini hapo kutapunguza adha za wagonjwa wanaohitaji dawa.

"Kufunguliwa kwa duka hili kutapunguza wagonjwa walikuwa wakilalamika na kutaabika ambapo kutokana na hali hiyo wakati wa ziara yake rais alitoa agizo la kuwepo kwa duka hili ndani ya hospitali,"alisema.

Alisema wateja wakuu katika duka hilo ni serikali na hospitali za serikali ambapo mgonjwa akitaka dawa huelekezwa na kupewa karatasi maalumu kwa ajili ya manunuzi ya dawa hizo dukani humo.

"Dawa zenye majina mengi zitapatikana hapa. Tutalisimamia na tutafurahi zaidi tukipata mrejesho kutoka kwa wananchi, matarajio yetu ni kupata mahitaji yote ya dawa tofauti tofauti,"alisema Dk. Mmbando.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa MSD, Laurrean Bwanakunu alisema kazi kubwa ya bohari hiyo ni kununua, kuuza na kusambaza dawa kwa serikali na kujipanga kutoa huduma hiyo katika hospitali zote za kanda.

Ofisa Udhibiti Ubora (MSD), Betia Kaema alisema hospitali za serikali zinapaswa kupeleka oda za dawa ambazo wanahitaji ili kuepusha usumbufu wa kutopatikana kwa dawa
katika duka hilo.

"Tunajidhatiti katika kutoa huduma kwa saa 24, Muhimbili watoe mahitaji yao ya dawa mapema ili kusiwe na usumbufu wa upatikanaji wa dawa,"alisema Kaema

Kaema alifafanue zaidi kuwa dawa zinazopatika katika duka hilo na za bei nafuu ukilinganisha na gharama za duka la dawa binafsi.

"Nitoe mfano mdogo tu jana alikuja mteja hapa aliandikiwa dawa na daktari aje kununua hapa...gharama ya dawa hiyo ilikuwa sh.18,000 yule mteja alishangaa kwani alikuwa akinunua katika duka la dawa binafsi sh. 48,000 hivyo aliona unafuu na umuhimu wa duka hili,"alisema.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli kwa hospitali za serikali za kanda na mikoa kuwa na duka la dawa la MSD.
Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com - simu namba 0712-727062

Taarifa rasmi kuhusu usahihi wa majina ya Waziri Mkuu

Kassim M. Majaliwa
Kassim M. Majaliwa
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anatumia majina matatu kama ifuatavyo: Kassim Majaliwa Majaliwa au Kassim M. Majaliwa.

Tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo, kumekuwa na uchanganyaji wa majina yake na hii ni kwa sababu tangu akiwa chuoni na jeshini, alikuwa akitanguliza kutaja ubini (jina la ukoo) na ndiyo maana ikawa inasomeka Majaliwa Kassim Majaliwa.

Endapo jina hilo litaanza kuandikwa na ubini, litapaswa kutenganishwa na koma kama ifuatavyo: Majaliwa, Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliteuliwa na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli Novemba 19, 2015 na kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku hiyo hiyo. Aliapishwa Novemba 20, 2015 kwenye Ikulu ndogo ya Chamwino, Dodoma.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATANO, DESEMBA 2, 2015.

EWURA yapunguza bei ya mafuta


TanzaniteOne kupunguza wafanyakazi 635


KAMPUNI ya madini ya Tanzanite One imetoa likizo ya malipo kwa wafanyakazi 635 kwa lengo la kujiweka sawa katika shughuli za uendeshaji wa kampuni hiyo. 

Wafanyakazi hao wamepewa likizo ya malipo kuanzia jana huku mchakato wa kuwaachisha kazi baadhi ya wafanyakazi ukiendelea kwa kuhusisha pande zote.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Iringa mjini, Meneja wa Kampuni hiyo, Apolinari Modest alisema kwa sasa uongozi wa kampuni hiyo tayari ulishafuata taratibu zote za kuachisha kazi wafanyakazi.

Modest alisema hakuna mfanyakazi atakayeachishwa bila ya kufuata sheria na taratibu za kazi kwani uongozi umezingatia kila kitu na kuwataka wafanyakazi kuacha kuwa na wasiwasi juu ya hilo.
Alisema mchakato wa kupunguza wafanyakazi umetokana na kampuni kushindwa kujiendesha kutokana na kukosekana kwa uzalishaji kwa muda mrefu na gharama za uendeshaji kuwa kubwa.

Alisema kwa sasa kazi ya kuchambua wafanyakazi wa kuachishwa iko katika vikao mbalimbali kwa kuhusisha uongozi wa Kampuni ya Tanzanite One, viongozi wa vyama vya wafanyakazi tawi la kiwandani hapo na uongozi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

Naye Mwanasheria wa Tanzanite One, Kisaka Mnzava alisema kuachishwa kazi kwa wafanyakazi kutafuata sheria zote za kazi na zitasimamiwa na pande zote na hakuna mfanyakazi atayeachishwa bila kufuata sheria za nchini.

Alisema kupunguzwa kazi kwa wafanyakazi sio mchakato mgeni katika kampuni hiyo kwani ulishafanyika na hakukuwa na malalamiko yoyote. Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Tawi la Tanzanite One, Daniel Hagay alikiri kuwepo kwa mchakato wa kupunguza wafanyakazi, lakini alikuwa na wasiwasi juu ya taratibu kukiukwa, hivyo kuutaka uongozi kukamilisha kwanza taratibu za kuachisha wafanyakazi ili kila mfanyakazi atayeachishwa awe na haki yake ya msingi.

Akithibitisha hilo, Mkurugenzi wa Sky Group, Faisal Shahbhai alisema kupunguzwa kwa wafanyakazi ni kutokana na gharama za uendeshaji kuwa kubwa kuliko uzalishaji hivyo kushindwa kutekeleza baadhi ya ahadi walizoahidi kabla ya kuchukua kitalu hicho C katika mgodi wa Tanzanite Mirerani wilayani Simanjiro, Manyara.

Alisema mchakato mzima wa upunguzaji wa wafanyakazi utafuata taratibu na sheria za kazi ikiwamo kushirikisha pande zote ikiwemo Stamico, mwakilishi wa serikali kama mbia na viongozi wa wafanyakazi.

Alisema Sky Group imekuwa ikifanya kazi katika mazingira magumu tangu ichukue kitalu hicho C kilichokuwa kikimilikiwa na Tanzanite One kutokana na kukosa uzalishaji kwa muda mrefu, lakini pia imekuwa na madeni makubwa ya nyuma.

[video] Wahusika waeleza kuhusu makontena 9 yaliyokamatwa Tangi Bovu