Taarifa nzima ya habari ya usiku ChannelTEN Desemba 3, 2015Haya! Tembo 7,500 kati ya 12,000 "waliopotea" warejea


Job: Africa Regional HIV/AIDS Advisor

Organization: Global Health Fellows Program
Country: United States of America
Closing date: 16 Dec 2015

AG azungumzia 'kuchelewa' Baraza la Mawaziri 2015 na Malalamiko ya likizo kufutwa


Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju amezungumzia suala la wakuu wa mikoa kutoa matamko ya kusitisha likizo za watumishi wa umma kwa kuwataka wafanye kazi tu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalum na kituo cha runinga cha Azam, Masaju amesema amekuwa akisikia kupitia vyombo vya habari kuhusu taarifa za kuwepo matamko hayo kutoka kwa baadhi ya wakuu wa mikoa.

Amesema kuwa hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria na kwamba sheria na katiba ya nchi lazima ifuatwe na watu wote nchini bila kujali cheo cha mtu aliyetoa matamko hayo.

Masaju amesema kuwa hajawahi kupokea malalamiko yoyote ofisini kwake kutokana na matamko hayo ambayo amekuwa akiyasikia kwenye vyombo vya habari pekee .

Katika mahojiano hayo,Masaju alikataa kueleza moja kwa moja kama uamuzi huo unaochukuliwa na baadhi ya wakuu wa mkoa ni kosa kisheria.

“Mimi sio Jaji wa kusema kuwa waliosema hivyo wamevunja sheria, lakini nataka kusema kuwa sisi sote tunaongozwa na sheria na katiba ambavyo lazima vifuatwe.” Alisema Masaju.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla wametangaza kusitisha likizo kwa watumishi katika mikoa hiyo kwa sababu za kuwataka wafanye kazi tu!

Rais Magufuli azungumza na Makamu II wa SMZ, Balozi Iddi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kulia akifurahia jambo na makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Joseph Magufuli kulia akizungumza na makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Joseph Magufuli kulia akiagana na makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kufanya nae mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam.

Jinsi ya kuripoti ikiwa umetozwa nauli isiyo sahihi


Je, UMETOZWA NAULI KUBWA KWENYE BASI KULIKO UMBALI UNAOKWENDA?

Fanya yafuatayo:
  1. Bishia nauli uliyotozwa kuwa si halali. mfano kama unakokwenda ni Dar-Mafinga, nauli inapaswa kuwa 20,000 wewe ukatozwa Dar - Njombe 25,000, bishia. Kondakta akikataa lipa, ingia kwenye gari.
  2. Atakupa tiketi imeandikwa Dar - Mafinga 25,000 au atakupa tiketi imeandikwa Dar-Njombe 30,000. Pokea
  3. Ipige picha hiyo tiketi, au iscan kisha itume kwenda nambari 0682 887722(kwa whatsapp, telegram au wechat) ukielezea kuwa umetozwa nauli kubwa kuliko umbali wa safari au umepandishwa bus ordinary wakati wewe ulitozwa nauli ya luxury. Na kwamba kondakta amekataa kukuandikia tiketi ya unakokwenda badala yake akakuandikia tiketi inayoonesha kituo ambacho basi linaishia. Au Tuma ujumbe au piga simu kwenda 0800 110 019 au 0800 110 020 (bure). Namba hizi tumia hata pale gari inapokatisha ruti au kuwatelekeza njiani baada ya kuharibika.
  4. Basi litasimamishwa kituo cha mbele, utarudishiwa nauli yako. Kama limekamatwa na askari polisi basi dereva au kondakta atarudisha nauli na 30,000 itamhusu. Akikamatwa na SUMATRA basi atarudisha nauli na faini ya sh.250,000 itamhusu.
SAMBAZA UJUMBE HUU KADIRI UWEZAVYO, MUELIMISHE MWENZIO

Imetolewa na
RSA TANZANIA
USALAMA BARABARANI JUKUMU LETU SOTE

The Guardian, The Citizen divulge bigwigs named in $14bn Stanbic bribery claimsHardly two days after the 14bn/- controversial payments by Stanbic came to the fore, Treasury Permanent Secretary Dr Servacius Likwelile who was among  the top officials who signed the fee letter in 2012, yesterday came out  strongly, saying there was no loss of public money.

Dr Likwelile’s defence, which also echoed by Central Bank’s governor Professor Benno Ndulu comes at the time of the further revelation of more  prominent names that were involved in brokering the deal.

Reacting to The Guardian, which contacted him to get his side of the story,  the Treasury PS said, “It is important to be clear on this: there is no  loss of USD 600 million, it’s about irregularities in the exercise by the  bank officials that has attracted the penalty and thus the award of USD 7 million to the government,” Dr Likwelile said.

The Guardian understand that the UK’s investigators didn’t claim that the Tanzanian government lost money in this transaction, but revealed that bribery might have been through a local front company to influence key decisions makers within the treasury.

According to Serious Fraud Office documentary evidence presented to British Judge, Brian Leveson the questionable payments paid to Harry Kitilya and Dr Fratern Mboya of Enterprise Growth Market Advisors Limited of Dar es Salaam might have also benefitted top officials in the finance ministry who brokered the $600 million(Sh1.3 trillion) transaction.

It’s understood that after the sudden death of former Finance Minister Dr William Mgimwa, President Kikwete appointed Madam Saada Mkuya to replace him. But, at that time, the payments to the mysterious company have already been done.

According to the evidence Dr Likwelile was amongst top ministry officials who were actively involved in the controversial deal and final cut of USD 6 million as consultancy fees paid to EGMA in 2013. The deal kicked off in April 2012 but was finalised in March 2013.

“When the letter of proposal for the transaction was first submitted in February 2012, "Minister A" was the GOT Minister of Finance. In May 2012 Minister A was among a number of ministers dismissed from the government in respect of corruption allegations,” the SFO document reads in part.

Who is being referred here as Minister A was in actual sense Mustafa Mkullo was the minister for Finance until May 2012, when former President Kikwete reshuffled his cabinet and appointed the late Dr Mgimwa as the new Finance boss.

The SFO document further pointed out that Mkullo had wanted to conclud the deal as fast as possible prior to his departure in May 2012 but could not manage which then meant that his successor, Dr Mgimwa took over the role as key Treasury architect backed by another top official and later on Dr Likwelile.

Sugarcoating and pushing the whole deal from Stanbic Bank was Miss Tanzania 1996 Shose Senare then working as Head of Corporate and Investment Banking backed by her Managing Director, Bashar Awale who started with minister and Likwelile but later ended with Mgimwa and Likwelile.

Senare was so powerful that in 2012, she was included on the official delegation of the government going for an International Monetary Fund and World Bank meeting in Washington.

“During April 2012 SS (Senare) attended a spring IMF meeting as part of the GOT's delegation. There she met Harry Kitilya in his GOT capacity as "Commissioner for Tax". In reporting back to colleagues she explained that Kitilya had introduced her to two Governors of other African central banks (both ex-commissioners themselves) proclaiming that we (i.e. the bank) specialize in raising funds for governments and how good the Bank was,” the SFO document which is a result of interrogating all the key actors except Senare who resigned from her position to escape the questioning in 2013.

Senare’s masterly so impressed his local boss, Awale and London based Florian Von Hartig who was Standard Bank's Head of Global Debt Capital Markets that at one point in time, she was named as running a one man show.

Senare was instrumental in reviving the deal which started in 2011 but nearly collapsed because there was no offer of a fee for consultancy to public officials.”A further letter of proposal dated 20th February 2012 was sent to the Ministry of Finance. This joint Standard Bank and Stanbic Tanzania proposal outlined a now $550 million sovereign private placement but the bank fee remained as per the October 2011 proposal at 1.4 percent,” the SFO document said.

In his 25th February 2012 reply to Bashir Awale from the minister it indicated that the government was "willing to participate in the deal". The letter invited BA to immediate discussions with the MOF technical staff with a hope of concluding the deal by April 2012, the SFO said.
Awale was deported last month by the government after he was accused of  hiring international hackers in order to temper with the general election  tallying process—the charges he vehemently denied.

“By email on the same day, Shose Senare announced to Florian Von Hartig and others that the proposal had been accepted by the minister and continued: both Bashir and I have been lobbying both yesterday and full day today to win this mandate. Please note that in this proposal Standard Bank Group will not be putting any balance sheet nor are we taking any risk, we pocket 1.4 percent arrangement fees being USD 7,700,000 (over 15bn/-).

Contacted to comment on the saga, Bank of Tanzania Governor, Prof Benno Ndulu also maintained that so far the government has lost no money because of the London’s court ruling which offered a USD 7 million (15bn/-) compensation.

Prof Ndulu was particularly asked by this paper to respond to measures taken by the Central Bank so far to reign in Stanbic Bank Tanzania Limited which has been embroiled in two major corruption scandals this year.

“Regulatory actions related to Tegeta Escrow will be reported in the government’s implementation report of Bunge resolutions. On the matter related to private placement in London, it is BoT’s regulatory action that SFO relied upon for its prosecution, SFO has interacted with BoT on this matter,” Prof Ndulu said.
------------- THE END --------------

A meeting in the US between the then Tanzania Revenue Authority (TRA) boss Harry Kitilya and socialite Shose Sinare began the events that would lead to the Sh12 billion bribery scandal now at the centre of a government investigation, it has emerged.

Mr Kitilya met Ms Sinare, who was a senior employee at Stanbic Bank ,during a spring meeting of the International Monetary Fund (IMF) in Washington in April 2012, and has a conversation on government financing.

The two later took their chitchat to a serious level, playing key roles in securing a $600 million foreign loan for the government and opening a can of worms over mega corruption in the country.

After the Washington meeting in which both attended as part of a government delegation, Ms Sinare boasted to fellow staff that Mr Kitilya introduced her to two African central bank governors who were formerly tax chiefs and implored for her “good” bank consider the business of raising funds for the government.

Details in the London case that has exposed how the 2013 government loan was used to create the Sh12 billion bribery conduit, paint a picture of wheeler-dealing among public and private corporate executives to siphon billions of shillings of taxpayers’ money for personal benefit.

In the documents, Ms Sinare says Mr Kitilya’s company, Enterprise Growth Markets Advisors (EGMA), the firm that was paid the Sh12 billion bribe in the loan transaction, facilitated behind-the-scene talks to secure the deal.

In one of her documents explaining the role of EGMA in an internal investigation, Ms Sinare who was Acting Head of Corporate and Investment Banking at Stanbic, claimed Mr Kitilya and his company did intervene to stop a cabinet meeting on February 27 and also “obtained the AG’s (Attorney General) opinion in good time.”

She does not say why the cabinet meeting had to be stopped but the details paint a picture in which Stanbic Managing Director Bashir Awale and herself were engrossed in lobbying with cabinet ministers and other senior civil servants to bag the agreement as lead players in sourcing for the government loan.

UK’s Serious Fraud Organisation (SFO) which carried out the corruption investigation involving Stanbic and its main unity, Standard Bank’s role, reveals a link between individuals who were central to the deal and how they may have influenced it.

The back and forth negotiations run from February 2012 to March 8 when the government finally received the $600 million (Over Sh1.2 trillion). Other than the former TRA chief who played a camouflage role as EGMA co-principal, the negotiations were handled at either stage by former finance minister Mustafa Mkulo, his successor William Mgimwa, retired finance Permanent Secretary Ramadhan Khijja, the current PS in the same docket, Dr Servacius Likwelile, and other senior treasury officials.

One of the puzzles in the investigation was to establish when and how EGMA came into the picture despite the fact that Standard Bank was kept in the dark over its role in the negotiations that eventually raised the cost of the loan agent fees by a staggering Sh12 billion.

Other than the Washington meeting between, Mr Kitilya and Ms Sinare, the Stanbic MD is also shown as enjoying a personal relation with the former TRA chief since 2008. Information shows that Mr Awale was the referee for Mr Kitilya in a Havard University course seven years ago. Investigators also found that his contact was high priority.

Mr Kitilya’s co-principal in EGMA, Fratern Mboya, is shown at one time approaching a Standard Bank subsidiary with a proposal for a business opportunity, believed to have been the role it played for Stanbic despite insiders in the bank labelling his firm “a one man show without experts.”

Mr Mboya’s CV that was filed with Mr Awale in the middle of the negotiations, give Dr Likwelile as his referee as well. He formerly served as the Director General of the Capital Markets and Securities Authority (CMSA). Dr Likwelile was mentioned by Ms Sinare as “the key person in this transaction.”

According to the details, Mr Mkulo gave the go-ahead for the negotiations when the deal was first floated by Mr Awale in 2012 but would soon be fired from the docket in a cabinet reshuffle in May of the same year. Mr Mkulo had in 2011 overseen another $250 million loan deal for the government by Standard Bank of South Africa and Stanbic.

Dramatic turn of events are detailed when Dr Mgimwa is appointed as finance minister to replace Mr Mkulo. Details show most of the negotiations that followed involved him and Dr Likwelile and some technical staff at the ministry of finance.

In show of high wheeler-dealing, Ms Sinare is quoted severally indicating how she had “cleared the air” with potentially set-back queries raised by the government negotiating team. When Mr Mkulo was sacked, she wrote to their London headquarters thus; “despite no letter of mandate signed, our deal is intact, with support of the technical team and civil servants.”

A few week after meeting Dr Mgimwa in May 2013, the deceased minister’s son, Godfrey Mgimwa was expressly hired as graduate trainee at Stanbic bank. He was placed directly under Ms Sinare.

According to the documents, the younger Mgimwa, was sent to Mr Awale by his father with an introductory letter which then saw him interviewed alone by the bank’s CEO and hired him two months later. The SFO point to this move as a possible inducement for the minister to consider the deal fronted by Stanbic.

The newly recruited Mgimwa would actually play a minor role at some point, first acting as a go between the bank and the ministry of finance, delivering confidential documents on the deal.

On October 12, 2012, Mr Mgimwa who is now the MP for Kalenga, is said to have organized a meeting on Tokyo, Japan, between his father and the representatives of Standard Bank who were pushing for hard to bag deal.

At all the stages however that the Standard Bank UK members met the Tanzanian minister, there was no mention of the EGMA role and that they were kept in the dark throughout by Mr Awale and Ms Sinare. The two always described the fees paid to EGMA as being payment for “facilitation and arrangement.”

Yesterday, the younger Mgimwa who would later quit his bank job for a detour to London before he returned to run for politics in the same constituency his father represented, denied any role in the negotiations for the loan deal when he worked at Stanbic bank. He declined further inquiries on the SFO record. “With due respect, there is nothing for me to comment about,” he said in an SMS reply.

Contacted, Dr Likwelile said he would not comment as an investigation had been ordered by the Chief Secretary. “You heard the Chief Secretary on this issue, Investigations are onging….facts will be made clear when the investigation is concluded,” said Dr Likwelile.


[audio] Kauli ya Januari Makamba kuhusu kumkejeli Rais Magufuli


Shukurani: Blogu ya GSengo


Uchunguzi wa NIPASHE kuhusu "mashangingi" yanavyofilisi

2010-2011_Lexus_LX_570_(URJ201R_MY10)_Sports_Luxury_wagon_(2011-04-22)

Utitiri wa magari aina ya VX-V8 na mengine ya aina hiyo maarufu kama ‘mashangingi’ huigharimu serikali mabilioni ya fedha kila mwaka na hiyo ndiyo sababu kubwa iliyomlazimu Rais Dk. John Magufuli kutangaza kuwa atadhibiti matumizi yake, imefahamika.

Uchunguzi uliofanywa na Nipashe kwa kuhusisha taarifa kutoka vyanzo mbalimbali umebaini kuwa idadi ya mashangingi iliyopo serikalini yaweza kuwa takriban 2,778.

Kwa makadirio ya Nipashe, vyombo hivyo vya usafiri kwa maafisa wa juu wa serikali hugharimu taifa takribani Sh. trilioni 1.18 kwa ajili ya manunuzi peke yake huku kiasi kingine cha wastani wa Sh. bilioni 125.01 kikitumika kwa uendeshaji wake kwa mwaka.

Aidha, kiasi hicho cha makadirio ya fedha za kununulia mashangingi 2,778 peke yake (Sh. trilioni 1.18) ni sawa na misamaha yote ya kodi iliyotolewa nchini katika mwaka wa fedha wa 2013/14.

Kwa mwaka, kulingana na ripoti ya kamati ya Bajeti ya Bunge misamaha ya kodi nchini ilifikia kiwango cha juu cha Sh. trillion 1.18 kwa mwaka wa fedha wa 2013/14, sawa na asilimia 4.3 ya pato la taifa.

Kadhalika, jumla ya makadirio ya gharama za manunuzi na uendeshaji kwa mashangingi 2,778, yaani Sh. trilioni 1.31 ni sawa na asilimia 5.8 ya bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016 ya Sh. trilioni 22.4, kama ilivyowasilishwa bungeni Juni, 2015 na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum.

Katika uchunguzi wake, Nipashe imekadiria gharama ya mashangingi kwa kuchukulia kuwa mawaziri, naibu mawaziri, wakurugenzi wa idara na wakuu mbalimbali wa vitengo wizarani, wakuu wa mikoa; wakuu wa wilaya na makatibu tawala wa mikoa na wilaya ni miongoni mwa wale wanaoyatumia. Wengine waliokadiriwa kutumia mashangingi hayo, kwa mujibu wa uchunguzi wa Nipashe, ni pamoja na mameya wa manispaa, wakurugenzi wa majiji na baadhi ya wakurugenzi wa wilaya na pia wakuu wa taasisi na mashirika ya umma kama Shirika la Umeme (Tanesco).

Akizungumza katika hotuba yake wakati akizindua bunge Novemba 20, 2015, Rais Magufuli alisema wazi kuwa serikali yake ya awamu ya tano itahakikisha kuwa inadhibiti matumizi ya magari ya kifahari kwa viongozi na watumishi wake waandamizi ili kuokoa matumizi makubwa ya fedha ambayo vinginevyo yangesaidia kuboreshwa kwa huduma za kijamii na kuwaondolea Watanzania baadhi ya kero zinazowakabili.

“Serikali ya awamu ya tano, itasimamia kwa karibu na kudhibiti ununuzi wa magari ya gharama kwa ajili ya viongozi na watumishi waandamizi wa Serikali. Kwa sababu unakuta mtu ni Injinia, unatakiwa uende ukakague barabara badala ya kuwa na pick-up, unataka kununua V-8. Sasa ni lazima tubadilishe huo mwenendo,” alisema Magufuli.

IDADI YA MASHANGINGI

Katika uchunguzi wake, Nipashe haikufanikiwa kupata takwimu rasmi za serikali kuhusiana na idadi ya mashangingi. Jitihada za kufuatilia katika Wizara ya Ujenzi ambako awali iliaminika kuwa ndiko takwimu za mashangingi zaweza kupatikana ziligonga mwamba baada ya mwandishi kuelezwa kuwa hivi sasa kila wizara husimamia yenyewe magari yake na ya taasisi zilizo chini yake.

Hata hivyo, uchunguzi binafsi wa Nipashe umebaini kuwa kwa nchi nzima, serikali kupitia wizara na taasisi au mashirika yake ya umma yakadiriwa kuwa na mashangingi 2,778.

Katika uchunguzi huo, Nipashe iliangalia muundo wa baadhi ya wizara na kuchukulia kuwa kila mkuu wa idara na kitengo hustahili kuwa na shangingi.

Katika uchunguzi huo, imebainika kuwa baadhi ya wizara zina viongozi wengi wanaotajwa kutumia mashangingi kutokana na upana wa shughuli zake kulinganisha na nyingine. Kwa mfano, muundo wa Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano waonyesha kuwa kuna Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, wakurugenzi 11 wa idara/vitengo na wakuu wa seksheni 12.

Kwa sababu hiyo, Nipashe imekadiria kuwa wastani wa mashangingi yaliyopo kulingana na idadi ya wakuu hao yafikia 27, hapo achilia mbali wasaidizi wa wakurugenzi na wakuu wa vitengo ambao kama wakitumia mashangingi, wakichanganywa wanakuwa zaidi ya 50. Wizara ya Fedha yaonyesha kuwa kwa mpangilio kama huo, kuna watu takriban 52 wanaotumia mashangingi huku wizara nyingine zenye muundo usiokuwa mpana sana zikiwa na watu walau 10 wanaostahili magari hayo, baadhi wakiwa ni mawaziri, makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu, wakurugenzi wa idara za rasilimali watu na utawala, wakurugenzi wa idara za fedha na wakurugenzi wa idara za mawasiliano.

Kwa sababu hiyo, Nipashe imekadiria kuwa kwa wastani, walau kila wizara ina mashangingi 10. Kwa sababu hiyo, kwa wizara zote 30, maana yake hadi sasa kuna jumla ya mashangingi 300 yanayotumiwa na vigogo katika wizara hizo.

Kadhalika, kwa mujibu wa Msajili wa Hazina, Lawrance Mafuru, hivi sasa idadi ya taasisi na mashirika ya umma ni 220. Nipashe inakadiria kuwa wakuu wa taasisi zote, wasaidizi wao pamoja na wakuu wa idara kama za utawala na fedha hutumia pia mashangingi aina ya VX-V8.

Hivyo, ikiwa kila taasisi au shirika la umma lina wastani wa viongozi 10 wanaotumia mashangingi, maana yake, kwa ujumla taasisi na mashirika yote ya umma nchini yana mashangingi 2,200. Makadirio hayo ni mbali na ukweli kuwa zipo taasisi na mashirika makubwa ya umma kama Shirika la Umeme (Tanesco) lenye mtandao mpana zaidi wa huduma zake nchi nzima na hivyo kuwa na viongozi wengi wanaostahili kutumia mashangingi, wakiwamo mkurugenzi mkuu, msaidizi wake, wakuu wa idara za fedha, utawala, mhasibu mkuu, idara za usambazaji, uzalishaji, masoko, mawasiliano na pia mameneja wa shirika hilo katika kanda na mikoa yote nchini.

Aidha, Nipashe imekadiria kuwa yapo mashangingi walau 62 yanayotumiwa na wakuu wa mikoa yote 31 nchini na makatibu tawala wa mikoa yao. Kadhalika, inakadiriwa kuwa yapo mashangingi 133 yanayotumiwa na wakuu wa wilaya na vile vile magari kama hayo walau 83 yakadiriwa kutumiwa na nusu ya idadi ya wakurugenzi wa halmashauri 166 zilizopo nchini pamoja na mameya wa manispaa, mameya wa majiji matano yaliyopo nchini na baadhi ya wenyeviti wa halmashauri za miji. Idadi hii yakadiriwa nusu kwa vile Nipashe imehakikishiwa kuwa siyo wakurugenzi wote wa halmashauri hutumia mashangingi.

Kutokana na makadirio hayo, ndipo Nipashe ilipopata makadirio ya jumla ya mashangingi yanayotumiwa na viongozi wa serikali nchini kote kuwa ni 2,778.

AINA YA MASHANGINGI

Kwa mujibu wa mtandao wa moja ya kampuni zinazoshughulikia mashangingi, ukubwa wa injini ya Land Cruiser VX ni CC 4,608 (LC 200 Petrol). Ulaji wake wa mafuta huwa ni lita moja kwa kilomita 4 hadi 5, kutegemeana na uendeshaji wa dereva na hali ya barabara. Tanki lake la mafuta lina uwezo wa kuchukua lita 138, likiwa na vyumba viwili ambavyo kimoja kikubwa huchukua lita 93 na kingine lita 45.

Mbali na magari aina hayo, yapo ya matoleo mengine kadhaa yenye sifa zinazotofautiana na mengine. Baadhi, yakiwamo aina ya LC 200 VX High Diesel ambayo hutumia dizeli na ulaji wake mafuta watajwa kuwa ni lita moja kwa kilomita nane kutegemeana na uendeshaji wa dereva kwani huweza pia kutembea umbali mfupi zaidi.

Chanzo kimoja kiliiambia Nipashe kuwa mashangingi aina ya LC 200 Petrol na mengineyo yanayotumia lita moja kutembea umbali wa kilomita 4 na tano hula mafuta zaidi kwa sababu yana mfumo wa mafuta wa kielektroniki na pia huwa na huduma mbalimbali zinazotumia mafuta na umeme maradufu kama vitoa hewa ya joto (heater) na viyoyozi.

“Magari haya yana viti vya watu nane, masofa yake ni ya ngozi na kwa kweli, ukipanda ndani yake ni raha tupu. Ni imara lakini yanastarehesha vile vile na ndiyo maana viongozi na watu wenye uwezo mkubwa kifedha hupenda kuwa nayo,” chanzo kimoja kiliiambia Nipashe.

Kulingana na takwimu ambazo Nipashe imezikusanya kutoka vyanzo mbalimbali, wastani wa gari jipya aina ya Land Cruiser VX-V8 hununuliwa kwa kiasi cha dola za Marekani 200,000, sawa na Sh. milioni 423. 31 kwa mujibu wa viwango vya ubadilishaji fedha vya jana kwa kikokotozi cha mtandao wa Oanda.

Chanzo kimeiambia Nipashe kuwa yapo pia mashangingi yanayouzwa kwa Sh. milioni 245,000, lakini kwa vile bei za vitu vya serikali huambatana na ‘cha juu’, mara zote ununuaji wa magari hayo huigharimu serikali mabilioni ya fedha kwani bei zake huwa tofauti na zile wanazouziwa watu au taasisi zisizokuwa za serikali.

Jambo hilo la kuongezwa bei katika manunuzi ya serikali, hata Rais Magufuli alilizungumzia wakati wa hotuba yake bungeni Ijumaa ya Novemba 20, 2015.

Kwa sababu hiyo, ikiwa kila gari miongoni mwa mashangingi 2,778 yaliyokadiriwa na uchunguzi wa Nipashe yatanunuliwa kwa mkupuo kwa Sh. milioni 423, maana yake magari hayo huligharimu taifa fedha hizo kiasi cha Sh. trilioni 1. 18.

GHARAMA ZA UENDESHAJI, VIPURI

Uchunguzi uliofanywa na Nipashe katika baadhi ya gereji jijini Dar es Salaam umebaini kuwa shangingi moja lisilokuwa la serikali hufanyiwa matengenezo ya kawaida (service) kwa gharama ya wastani wa Sh. 400,000 kila baada ya kilomita 5,000 au kila baada ya miezi mitatu. Gharama hizi huhusisha mahitaji kadhaa yakiwamo ya ununuzi wa lita 11 za mafuta ya kulainisha injini yaitwayo ‘engine oil’ kwa Sh.10,000 kwa kila lita moja; mafuta ya kulainisha yaitwayo ‘oil filter Sh. 15,000, ‘pre-filter’ Sh. 10,000, air filter Sh. 30,000, grease kilo moja Sh. 10,000 na vitu vingine kadhaa. Kadhalika, gharama hizi (Sh. 400,000) huhusisha pia malipo ya ufundi.

Hata hivyo, yaelezwa kuwa ‘service’ kwa mashangingi ya serikali huwa ghali zaidi huku gharama zikitajwa kuwa jumla yake huwa ni kati ya Sh. milioni moja milioni 3.5 kulingana na aina ya shangingi. Nipashe imechukulia wastani wa gharama hizi kuwa ni Sh. milioni 2.25 kwa kila gari.

Kwa sababu hiyo, wastani wa gharama za ‘service’ moja kwa mashangingi 2,778 ya serikali ni Sh. bilioni 6.25. Na kama service hizi zitafanyika mara nne kwa mwaka, maana yake gharama za jumla zinazobebwa na serikali kwa mashangingi yote ni takriban Sh. bilioni 25.

Kadhalika, yaelezwa kuwa miongoni mwa sifa za mashangingi ni uimara wa vipuri vyake. Hata hivyo, inapotokea vimeharibika kwa namna yoyote ile, gharama zake huwa kubwa, hasa kwa mashangingi hayo ya serikali.

Kwa mfano, yaelezwa kuwa tairi zikiharibika au kubadilishwa baada ya kutembea umbali wa kilomita 50,000, bei yake huwa ni Sh. milioni 4; taa kubwa zikiharibika huuzwa Sh. milioni 7 (kwa zote mbili); nozzle zipo nane na kila moja huuzwa Sh. milioni 1.5, hivyo kwa zote ni Sh. milioni 12 na brakepads (breki) Sh. 650,000 kwa wateja wa kawaida huku kwa mashangingi ya serikali zikitajwa kufikia hadi Sh. milioni 3.5 pindi zinapobadilishwa.

Kwa sababu hiyo, gharama za kawaida za kubadilisha vipuri hivyo kwa shangingi moja kila inapobidi kufanya hivyo ni Sh. milioni 26.5, sawa na Sh. bilioni 73.65 kwa mashangingi yote 2,778.

Kuhusiana na mafuta, chanzo kimeiambia Nipashe kuwa viongozi wa serikali wanaotumia magari hayo huwa na mgawo maalum kulingana na nafasi zao.

Uchunguzi umebaini kuwa kwa kawaida, wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya, Mikoa, makatibu tawala wa mikoa, wakurugenzi wa wizara, makatibu wakuu na naibu waziri na mawaziri hupata mgawo wa lita 10 za mafuta kwa matumizi ya kawaida ya kila siku, sawa na lita 280 kwa mwezi. Hata hivyo, kiwango hiki huongezeka pindi panapokuwa na safari maalum za kikazi nje ya kituo cha kazi.

Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya mmoja wa zamani, watumiaji wengi wa mashangingi hutumia mafuta zaidi ya kiwango kilichowekwa cha kati ya lita 280 hadi 300 kwa mwezi. Badala yake, wapo ambao hutumia hata zaidi ya lita 500 kwa mwezi kutokana na sababu mbalimbali, zikiwamo ziara za nje ya maeneo yao ya kazi.

Kadhalika, imeelezwa kuwa mashangingi yaliyopo maeneo ya mijini kama Dar es Salaam hutumia mafuta mengi pia kwa sababu madereva wengi hubaki na magari hayo huku wakikaa maeneo ya mbali na wanapoishi mabosi wao, mfano ni pale dereva anayeishi Mbagala kulazimika kusafiri umbali mrefu kila uchao kumfuata bosi wake aishiye Tegeta na kumpeleka ofisini Posta kabla ya kumrejesha Tegeta na kisha naye kurejea nyumbani kwake Mbagala.

Aidha, imeelezwa kuwa bosi anapokwenda nje ya mkoa kikazi, mfano kutoka Dar es Salaam kwenda Arusha, dereva hutangulia na gari tupu huku mkuu akisafiri kwa ndege na hivyo kazi kubwa inayofanyika ni kwenda kumpokea bosi uwanjani na kumpeleka tena uwanjani siku ya kusafiri tena.

Kadhalika, wapo vigogo pia wanaotumia magari hayo kwa matumizi ya nyumbani kama kwenda kununulia bidhaa sokoni na hapo matumizi ya mafuta huongezeka zaidi.

“Mgawo wa mafuta upo, lakini wakuu wengi hawaufuati kwa sababu matumizi ni makubwa… matokeo yake ni mzigo mkubwa wa gharama kwa serikali,” chanzo kingine kimeongeza.

Nipashe imechukulia kuwa kwa wastani, kila shangingi hutumia mafuta kiasi cha lita 400 kwa mwezi. Hivyo, kwa mashangingi 2,778, maana yake jumla ya mafuta ni lita 1,111,200 kwa mwezi, ambazo zikipigiwa hesabu ya bei elekezi ya petroli jijini Dar es Salaam iliyotolewa jana na Ewura ya lita moja kwa Sh. 1,977, maana yake serikali hugharimia kuendesha mashangingi hayo kwa Sh. bilioni 2.20 kwa mwezi, sawa na Sh. bilioni 26.36 kwa mwaka.
Hivyo, wastani wa gharama za jumla kwa mwaka za mafuta, matengenezo ya kawaida na kununua vipuri pindi inapobidi kufanya hivyo kwa mwaka ni Sh. bilioni 125.01.

KUONDOLEWA KWENYE MZUNGUKO

Nipashe imeelezwa kuwa licha ya kununuliwa kwa bei ya juu, mashangingi huanza kuondolewa katika matumizi ya serikali kutegemeana na taratibu za taasisi na wizara husika, hasa kwa kuangalia jinsi yanavyopungua thamani. Baadhi huyaondoa baada ya matumizi yake kufikia asilimia 50, wengine asilimia 60 na zipo taasisi zinazoyatumia kwa muda mrefu zaidi kabla ya kuyapiga mnada.

MASHANGINGI YALIIBUKA LINI?

Uchunguzi wa Nipashe umebaini kuwa kwa kiasi kikubwa, neno ‘shangingi’ kwa maana ya magari aina ya Toyota Land Cruiser yanayotumiwa na viongozi wa umma lilianza kuibuka baada ya uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995 wakati wabunge walipoanza kupewa magari aina hiyo kwa ajili ya kuwarahisishia usafiri, hasa kutokana na hoja kuwa magari hayo huhimili pia misukosuko kwenye barabara duni zisizokuwa na lami, hasa kwenye maeneo ya vijijini.

Waziri Mkuu Mstaafu katika serikali ya awamu ya nne, Mizengo Pinda, aliwahi kusema bungeni mwaka 2012 kuwa serikali imedhamiria kudhibiti matumizi ya magari hayo ili kubana matumizi. Hata hivyo, jambo hilo halikufanikiwa kwa asilimia mia moja kwani vigogo wengi waliendelea kuyatumia.

TRILIONI 1.31/- ZAWEZA KUFANYA NINI?

Uchunguzi wa Nipashe umebaini kuwa fedha kiasi cha Sh. trilioni 1.31 zinazokadiriwa kuwa gharama za kununulia mashangingi ya serikali 2,778 na kuyahudumia kwa mwaka moja zaweza kufanya mambo mengi ya maendeleo kwa taifa, ikiwamo kuwapa mikopo wanafunzi wote wa elimu ya juu nchini, kujenga maelfu ya zahanati, kuchimba visima katika kila kijiji nchini na pia kumaliza tatizo la madawati nchini.

MIKOPO KWA KINA MAMA

Uchunguzi uliofanywa na Nipashe umebaini kuwa kina mama wengi wanaojihusisha na shughuli za biashara ndogo ndogo huhitaji mikopo ya kuanzia Sh. 50,000 hadi Sh. 500,000 tu ili kufanikisha biashara zao.
Kwa sababu hiyo, kama fedha za kununulia mashangingi aina ya VX-V8 na kuyahudumia kwa mwaka (Sh. trilioni 1.31) zingetumika kuwakopesha wajasiriamali wanawake, maana yake wanufaika wangekuwa kina mama milioni 2. 62 ambao kila mmoja angepata Sh. 500,000.

MAABARA ZA SEKONDARI

Mkuu wa Shule ya Sekondari Tandika, Hussein Mpungusi, aliwahi kukaririwa Aprili 20, 2015, akisema kuwa wao walikamilisha ujenzi wa maabara mojawapo shuleni kwao kwa Sh. milioni 58.2. Kwa sababu hiyo, kama makadirio ya fedha za kununulia mashangingi na kuyahudumia kwa mwaka (Sh. trilioni 1.31) zingeelekezwa katika ujenzi wa maabara kama ya Sekondari ya Tandika, maana yake zingepatikana maabara takriban 22,509.

MADAWATI

Akizungumza na Nipashe hivi karibuni, Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu, alisema wastani wa bei ya dawati moja linalokaliwa na wanafunzi watatu wa shule ya msingi katika jimbo lake ni Sh. 15,000. Kwa sababu hiyo, fedha za kununua mashangingi 2,778 na kuyahudumia kwa mwaka (Sh. trilioni 1.31) zingetosha kununua madawati milioni 13.1 ya kiwango sawa kama ya Jimbo la Singida Magharibi na kumaliza tatizo hilo nchini kote na mengine yakabaki kwa kukosa wanafunzi wa kuyatumia.

ZAHANATI

Akizungumza na Nipashe Septemba 16 mwaka huu, Mbunge wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga, January Makamba, alisema kuwa katika jimbo lake, wamekamilisha ujenzi wa zahanati za vijiji kadhaa kwa wastani wa Sh. milioni 80 kwa kila moja. Kwa sababu hiyo, kama fedha za makadirio ya ununuzi wa mashangingi na huduma zake kwa mwaka (Sh. trilioni 1.31) zingetumika kujenga zahanati za kiwango cha Jimbo la Bumbuli, maana yake taifa lingepata zahanati mpya 16,375.

VISIMA VYA MAJI SAFI

Aidha, kwa mujibu wa Kingu (Mbunge wa Singida Magharibi), gharama ya kuchimba kisima cha maji safi kwenye jimbo lake huwa ni wastani wa Sh. milioni 15. Kwa sababu hiyo, wastani wa gharama za serikali kununua mashangingi na kuyahudumia kwa mwaka (Sh. trilioni 1.31) zingetumika kuchimba visima vya kiwango sawa na vile vya Jimbo la Singida Magharibi, maana yake vingepatikana visima 87,333 na hivyo kila kijiji nchini kingepata mgawo wa visima vinne kwani kwa mujibu wa Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), nchi nzima ina vijiji 19,200.

MAGARI YA KUBEBEA WAGONJWA

Mwaka jana, Agosti 28, kulikuwa na taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa kampuni ya Biolands International ilikabidhi msaada wa gari la kubebea wagonjwa (ambulance) aina ya Nissan Patrol kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela lenye thamani ya takriban Sh. milioni 76. Kwa sababu hiyo, ikiwa fedha za gharama za mashangingi (Sh. trilioni 1.31) zingetumika kununulia magari ya kiwango kama walilopata msaada Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, maana yake taifa lingepata magari mapya ya kubebea wagonjwa takriban 17,237 na hivyo kumaliza tatizo la ukosefu wa magari hayo katika vituo vya afya na hospitali nyingi nchini.

MIKOPO WANAFUNZI ELIMU YA JUU

Katika uchunguzi wake, Nipashe imebaini kuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa shahada ya uhandisi wa madini katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anayepata mkopo wa asilimia 100 hulipwa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) jumla ya Sh. 4,219,500 kwa mwaka. Mchanganuo wa mkopo huo kwa mwaka wote wa masomo ni Sh. 2,099,500 kwa ajili ya chakula na malazi, Sh. 200,000 ya vifaa, Sh. 620,000 kwa ajili ya mafunzo ya vitendo, ada Sh. milioni 1.3.

Kwa sababu hiyo, ikiwa makadirio ya fedha za ununuaji mashangingi na kuyahudumia kwa mwaka (Sh. trilioni 1.31) zingetumika kuwakopesha wanafunzi wa elimu ya juu kama wa mwaka wa kwanza wa shahada ya uhandisi wa madini wanaolipwa asilimia 100, maana yake wanafunzi wangekuwa wanafunzi 310,463. Ikumbukwe kwa mujibu wa Tume ya Vyuo Vikuu, wanafunzi wote nchini hawazidi 300,000.

VIPIMO CT-SCAN

Vyanzo mbalimbali vya Nipashe vinaeleza kuwa kipimo maarufu cha CT-Scan, aina ya Phillips huuzwa kwa wastani wa Sh. milioni 600 hadi bilioni moja. Hivyo, kama fedha za makadirio ya gharama za ununuaji mashangingi na kuyahudumia walau kwa mwaka mmoja (Sh. trilioni 1.31) zingetumika kununua mashine hizo za bei ya Sh. bilioni moja , maana yake zingepatikana CT-Scan 1,310 na kufungwa katika hospitali zote za rufaa nchini na nyingine nyingi zikabaki kwa hospitali za wilaya, vituo vya afya na zahanati katika kila kijiji.

BARABARA ZA LAMI

Vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa wastani wa kujenga barabara ya lami ya umbali wa kilomita moja ni Sh. bilioni moja. Kwa sababu hiyo, kama fedha za makadirio ya gharama za kununua mashangingi ya serikali 2,778 na kuyahudumia kwa mwaka mmoja zingeelekezwa katika ujenzi wa barabara, maana yake taifa lingepata barabara mpya ya urefu wa kilomita 1,300, takriban sawa na kutoka Dar es Salaam hadi Bukoba, ambako kwa mujibu wa kikokotozi cha umbali cha mtandao wa Distancefrom, umbali wake wa ardhini ni kilomita 1,376.

via NIPASHE

Kauli za Kitillya, Mgimwa, Ndulu, Hosea kuhusu kesi iliyoibuliwa na SFO

Harry Kitillya Kitilya
Harry Kitilya
Kamishna Mkuu wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitillya, ambaye anadaiwa kuhusika katika kashfa ya ununuzi wa dhamana ya serikali (hati fungani) zenye thamani ya trilioni 1.2, amefunguka kuhusiana na tuhuma hizo akisema kuwa muda muafaka ukifika ataeleza kila kitu.

Kitillya ambaye ni Mwenyekiti wa kampuni ya Egma iliyokuwa wakala wa ununuzi wa dhamana ya serikali wenzake, inadaiwa kuingiziwa Dola za Kimarekani milioni sita. Fedha hizo wanadaiwa kuzipata baada ya kujiongezea asilimia moja badala ya asilimia 1.4 na kuwa asilimia 2.4.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu, Kitillya alieleza kwa kifupi kuwa kwa sasa hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa lipo katika uchunguzi.
Alisema muda mwafaka ukifika atalitolea maelezo suala hilo kwa kirefu, ingawa hakutaja lini atafanya hivyo.

“Kwa sasa sina comment (maoni) yoyote kwa kuwa suala hilo lipo katika uchunguzi, lakini muda ukifika nitalizungumzia,” alisema Kitillya na kukata simu.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Huduma kwa Walipa kodi wa TRA, Richard Kayombo, alisema kwa sasa hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa lipo katika uchunguzi.

Kayombo alisema kama fedha hizo zitarudishwa na serikali ya Uingereza na kukiwa na uwezekano wa TRA kuchukua kodi, watatekeleza mara moja.

Benno Ndulu
Benno Ndulu
KAULI YA GAVANA

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu, alisema kwa sasa BoT haiwezi kuchukua hatua yoyote kwa kuwa ilishafanya kazi yake awali ya ukaguzi na kugundua ubadhirifu huo.

Alisema baada ya kugundua ndipo Taasisi ya Uchunguzi wa Makosa Makubwa ya Ufisadi ya Uingereza (SFO) nayo ikapata taarifa.

Alipoulizwa ni hatua gani BoT kwa sasa wanazichukua dhidi ya benki ya Stanbic Tanzania kuhusika mara kwa mara katika kashfa za fedha nchini ikiwamo kupitisha fedha za mgawo kwa watu walionufaika na kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow, Profesa Ndulu alisema hatua za kisheria haziwezi kuchukuliwa kwa benki husika bali kwa waliotenda kitendo hicho.

“SFO wao walipa taarfa kutoka kwetu mara baada ya kugundua, hata Oktoba 1, mwaka huu walituomba tuwapatie ripoti yetu katika kwa ajili ya kesi na tukawapa,” alisema Ndulu.

Edward Hosea
Edward Hosea
HOSEA: MASHTAKA YAIVA

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dk. Edward Hosea, alisema taasisi yake ilishaanza uchunguzi wa suala hilo muda mrefu.

Alisema hivi sasa uchunguzi wa suala hilo umefikia hatua ya mashtaka ambayo kiutaratibu inatakiwa kufanyika baada ya kuwa na ushahidi usio na mashaka juu ya suala hilo.

Hata hivyo, Dk. Hosea aliliambia gazeti hili kuwa suala hilo linapaswa kufanyika kwa kwa umakini kwa kuzingatia kuwa linahusisha benki za kimataifa.

Godfrey Mgimwa
Godfrey Mgimwa
MGIMWA ATOA MAELEZO

Awali kulikuwapo na taarifa kuwa mtoto wa aliyekuwa Waziri wa Fedha mwaka 2012/13, hayati Dk. William Mgimwa, Godfrey Mgimwa alitumwa na benki ya Stanbic akiwa kama mwajiriwa kwenda wizara ya fedha kupeleka nyaraka za dokezo la mkopo huo lililoonyesha kuwa riba yote ya asilimia 2.4 na kulitekeleza.

Akizungumza na Nipashe Mgimwa, ambaye ni Mbunge wa Kalenga, alikiri kuwa mwaka huo alikuwa mwajiriwa wa benki hiyo, lakini hakuhusika katika kupeleka dokezo lolote kwa baba yake (waziri wa fedha).

“Kama nilikuwa mfanyakazi wa kawaida wa Stanbic kipindi hicho, nisingepewa document (nyaraka) nzito kama hiyo kumpelekea waziri wa fedha hata kama alikuwa ni baba yangu,” alisema Mgimwa jana.

Jumatatu wiki hii, Mahakama ya London, Uingereza ilibaini ufisadi wa Sh. trilioni 1.3 zilizotokana na mkopo uliotolewa na benki ya Standard ya Uingereza kwa serikali ya Tanzania.

Mahakama hiyo iliamuru serikali ya Tanzania irejeshewe Dola za Marekani milioni saba, baada ya kubainika kuwapo kwa udanganyifu huo.

Baada ya kesi hiyo kufunguliwa kwenye mahakama hiyo na SFO, ilibainika kwamba asilimia moja ya mkopo huo ambayo ni Dola milioni sita zililipwa kwa Egma ambayo inamilikiwa na Kitillya, ambaye kwa wakati huo alikuwa Kamishna Mkuu wa TRA.

Mmiliki mwingine wa kampuni hiyo ni Gasper Njuu na aliyekuwa Ofisa Mtendaji wa Soko la Mitaji ya Umma Tanzania, Dk. Fratern Mboya, ambaye kwa sasa ni marehemu.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, juzi alitoa taarifa ya serikali kuhusiana na sakata hilo na kusema kuwa baada ya uchunguzi kufanyika ilibainika kwamba Benki ya Uingereza iliitaka Tanzania ilipe mkopo huo na riba ya asilimia 1.4, lakini Stanbic Tanzania ilidanganya na kusema ulipwe asilimia 2.4 na asilimia moja ambayo ni nyongeza wakalipwa Egma.

NAMNA ILIVYOBAINIKA

Mwaka 2013 BoT ilikagua Benki ya Stanbic na kubaini kuwapo kwa malipo yasiyokuwa ya kawaida yaliyofanywa kwa kampuni ya Egma, ambayo yalikuwa kinyume cha taratibu za kibenki.

Fedha hizo Dola milioni sita ziliingizwa kweye akaunti ya Egma na ndani ya siku kumi fedha hizo zilitolewa na mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo marehemu Mboya.

Baada ya BoT kufanya ukaguzi huo walitoa taarifa kwa serikali ya Uingereza kupitia SFO ambayo ilianzisha uchunguzi ambao ulisababisha kesi kufunguliwa.

Hata hivyo Benki ya Standard Group ambayo ni benki mama ya Stanbic Tanzania, imekiri makosa hayo na kukubali kulipa faini ya Dola milioni 25.2 (Sh. bilioni 54) kwa kosa hilo.

Comments by Alex Kakala regarding the $6 million bribery scandal

Let us not beat around the bush.

1. Standard Chartered Bank has been involved in so many scandals in the country, it is time to to show our resolve that this is not a banana country to this British bank, and cancel its licence via STAMBIC. The have been involved in also mot each and every financial , corruption scandal in the country involving or connected to international businesses, especially those tied to UK, yet you have al these UK leaders calling Africans government bunches of corrupt without taking responsibility of their country being the leader. British bank corruption is stinking every where from USA to UK , EU etc. Till to date ESCROW a/c money paid by STAMBIC died silently no action has been taken against the bank. That means poor Tanzania citizen sweating blood have continuously been feeding these corrupt international financial banks though fraudulent schemes in cahoots with government leaders through corrupt private companies.

2. BOT has never convinced majority of Tanzania citizen of its denials of being involved in all financial scandals within its armpit. EASCROW a/c, now this case, and many others in fact previous BOT governor stole the money from BOT and escaped to foreign countries. There is no way BOT can be pypassed with huge transactions invoving foreign deals without the itself BOT satisfying that the deals are clean That means BOT governor should be taken to task and be sacked straight away, while investigation is on going.

3. Ministry of finance of which TRA, BOT are part of its ministry departments, those leaders including ministers at the time must be apprehended.

4. Time to take stern actions against private companies involved in corruption scandal, as for now, every one is focused on government departments and government leaders but private companies CEOs and their staffs are left out of the hook, no it is completely wrong, they must be arrested and prosecuted, jailed, fined , ill gotten wealth confiscated. Look at how the government continue to pay the rogue businessman Harbinder Singh  millions of USD per month by exorbitantly charging poor Tanzania electricity tp feed the cheating mafia type individual after bribing his way through corrupt judges, finance ministry including BOT. The parliament recommended IPTL/PAP contract with TANESCO be terminated immediately and TANESCO take over the plants, till today after one year nothing has been done, instead the government continue to pay the company for unlawful ownership and business transactions.

5) The government is foolishly enough to pay such huge amount to corrupt mafia, and he is using the same money to damp into our gas production and selling back the gas to the government, means he is hitting our nation and poor people twice, yet we sit there and smile! All these people should be arrested, prosecuted and jailed , and all stolen money including assets should be confiscated.
If USA can fine those corrupt banks and companies such as BP billions of usd when they commit offence, why country like Tanzania should be scared or for whatever reason fail to take action when more serious crimes are committed by local and foreign companies, including banks in the country?
Unless Tanzania government tackle these monster corrupt cases which denied the nation millions to billions usd for social and economic development for the people, there is no way the country can succeed in taming corruption and realizing the real change.

"Wachagga wapewa magari ya kwenda kuhiji"

MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), imeanza kutoa leseni za muda mfupi kwa kuongeza idadi ya mabasi katika njia ya Dar es Salaam hadi Arusha.

Hatua hiyo ya Sumatra imekuja ili kukabiliana na ongezeko kubwa la mahitaji ya huduma za usafiri kwenda maeneo mbalimbali nchini, ambapo watu wengi wanataraji kufanya safari kwenda makwao kwa ajili ya sikukuu za mwisho wa mwaka.

Akizungumza jana kuhusu hatua hiyo, Meneja Mawasiliano wa Sumatra, David Mziray, alisema Sumatra imetoa leseni kwa mabasi matano ambayo yalianza kutoa huduma za usafiri kuanzia Desemba moja na leseni hizo zitakoma Januari 30, mwakani.

Mziray aliyataja mabasi ambayo hadi sasa yameshapewa leseni za muda kwa ajili ya kupunguza kero hiyo ya usafiri kwa njia ya Dar es Salaam-Arusha na ambayo tayari yameshaanza kutoa huduma hiyo ni yenye namba za usajili T431BYX, T473CCC, T694 ALX, T924DFR na T922 DFR.

Aidha, alisema mabasi mengine 10 yanataraji kuanza kutoa huduma kuanzia Desemba 7, mwaka huu katika njia tofauti za Dar-Mbeya, Dar –Songea, Dar- Mwanza na Dar -Mtwara, huku bado wakikaribisha wasafirishaji wengine kujitokeza kuomba njia wanazodhani zina uhitaji wa nyongeza ya usafiri.

“Mamlaka inawakumbusha wamiliki wa mabasi wanaotaka kubadili njia kuomba leseni za muda mfupi kwa lengo la kutoa huduma ya usafiri kwa mikoa yenye upungufu wa huduma ya usafiri katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka,” alisema Mziray.

Pia aliwakumbusha abiria kupanga safari zao mapema na walipe viwango vya nauli vilivyoidhinishwa na mamlaka hiyo, huku akitoa tahadhari pia kwa wamiliki wa mabasi kutovunja sheria kwa kuingiza mabasi yao katika njia mpya bila leseni hizo kwani kufanya hivyo ni uvunjaji wa sheria.

“Wapo wamiliki wanaovunja sheria kwa kuingiza mabasi yao katika njia ambazo hawana leseni na bila ukaguzi wa mabasi yao… Kabla ya kupatiwa leseni kuna ukaguzi hufanyika na hiyo ni faida kwa mmiliki wa gari,” alisema Mziray.

[audio] Prof. Lipumba asema kwa ufupi aliyoteta na Rais Magufuli

Katuni kuhusu "alimserema ya jeshi la watu watatu" Tanzania...

Kuhusu hoteli iliyopo juu ya bomba la TAZAMA...


Katibu Mkuu ofisi ya Waziri mkuu (TAMISEMI) Jumanne Sagini ametoa siku 14 kwa Afisa Ardhi, Mhandisi wa Majengo na Afisa Mipango Miji wa manispaa ya Morogoro za kuandika maelezo ya ni kwa nini wasifukuzwe kazi kutokana na kufanya kazi chini ya kiwango na kukiuka maadili ya utumishi wa umma.

Agizo hilo limetolewa baada ya watendaji hao wa serikali kutumia vibaya mamlaka waliyopewa na serikali ikiwemo kuruhusu ujenzi wa hoteli ya Flomi iliyopo eneo la Msamvu, katika eneo ambalo wanajua limepita bomba la mafuta la Tanzania na Zambia (TAZAMA).

Pia, kwa kushindwa kuzuia ujenzi wa holela katika maeneo yasiyo rasmi licha ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi.
Waziri Mkuu Majaliwa azungumza na Makamu II wa Rais wa SMZ, Balozi Iddi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi baada ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 3, 2015. (Picha kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu)Wizara yaahidi wazazi, walezi kuapata ada alekezi kwa shule binafsi Desemba 15

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imewataka wazazi na walezi wenye wanafunzi wanaotegemea kuanza masomo au kuendelea na masomo katika shule binafsi mapema Januari mwezi ujao, kuvuta subira hadi Desemba 15, mwaka huu serikali itakapotoa maelekezo mbalimbali ikiwemo suala la ada elekezi.

Akizungumzia hatua zinazofanywa hivi sasa na serikali kuhusu ada elekezi kwa shule binafsi, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Sifuni Mchome, alisema timu mbili hivi sasa zinafanya kazi ya uchambuzi wa michanganuo ya ada kwenye shule hizo, na baada ya muda mfupi uamuzi utatolewa.

“Hili sasa tumeliundia timu mbili za kufanya uchambuzi wa masuala ya ada katika shule za msingi na sekondari binafsi, ili kuwa na ada ekelezi kwenye utozaji wa ada kuanzia Januari mwakani,” alisema Profesa Mchome.

Aidha, alisisitiza kuwa katika mchakato huo, na kwa muda uliopo hivi sasa hadi Januari ni kipindi kifupi, hivyo inawezekana ada elekezi zikaanza kutumika kwa baadhi ya shule za msingi binafsi, kama eneo la majaribio.

Aliongeza kuwa Tanzania ina shule za msingi 17,000, zikiwamo za binafsi karibu 1,000 na zile za serikali 16,000 na kwamba iwapo wataanza na ada elekezi kwa shule hizo binafsi, wanaweza kuona utekelezaji wake.

Kwa upande wa shule za sekondari, Profesa Mchome alisema ziko zaidi ya shule 4,700 na kati ya hizo shule binafsi ni karibu 1,400 huku za serikali zikiwa 3,300 na kwamba mchakato wa ada elekezi kwa shule hizo binafsi unaendelea pia.

“Timu yetu inaendelea kufanya kazi kwenye mchakato katika shule za sekondari binafsi, zina wadau wengi kwa vile ni nyingi pia, hivyo hatuwezi kutoa maekelezo ya harakaharaka bila kuangalia utekelezaji wake kwa kina,” alifafanua Katibu Mkuu.

Alisisitiza kuwa kwa kuanzia, serikali ilifuta michango yote kwa shule zote nchini na kwamba hatua hiyo inazihusu pia shule binafsi na kuzitaka kutotumia ujanja wa kuingiza michango hiyo kwenye ada kwa madai ya kupandisha ada kwa mwaka ujao wa masomo.

Bei mpya ya ankara za maji Dar

Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam,(DAWASCO), limeanza rasmi kutumia bei zake mpya za ankara ya maji, ikiwa ni siku chache tu baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa huduma ya Nishati na Maji (EWURA) kupitisha mapendekezo ya kupandisha gharama hizo zilizotolewa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) ili kusaidia kuboresha huduma ya majisafi na salama jijini Dar es salaam, Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.

Gharama hizo mpya ambazo zimeanza rasmi kutumika Desemba 01, zimepanda kutoka kiasi cha shilingi 1098 kwa unit 1 ya ujazo wa maji ambayo ni sawa na lita 1000, hadi kufikia shilingi 1663 ambazo ni sawa na ongezeko la asilimia 51%.

Ilielezwa kuwa kupitishwa kwa mapendekezo hayo kutaongeza uwezo wa DAWASCO kufanya maboresho ya huduma za Maji na kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo kwa wateja na kuwafanya wateja hao kuwa na uhakika wa huduma hiyo kwa kukamilisha miradi mbalimbali mikubwa ya Maji ambayo tayari ipo katika hatua zake za mwisho.

Wakizungumzia gharama hizo mpya za maji wakazi wa jijini Dar es Salaam, wametoa maoni yao kuhusu ongezeko hilo jipya la bei za maji, ambapo wengi wao wameonesha kuridhika na bei hiyo mpya lakini wameiomba DAWASCO kuhakikisha inawapatia huduma hiyo kulingana na mahitaji yao huku ikiendana na gharama iliyoongezwa.

“Sisi hatuna shida kabisa na hiyo bei, tunachotaka ni maji, DAWASCO wahakikishe wananchi tunapata huduma hiyo bila usumbufu wowote, sio mnaongeza bei halafu maji yenyewe hatupati, hapo hatutakubali kabisa” alisema Bi. Penieli Tenga mkazi wa Mwananyamala.

Mkazi mwingine wa Kinondoni bi. Agnes Mbwana ameonesha kuridhika na gharama hizo japokuwa hapo awali hakuwa na taarifa za ongezeko hilo la maji, mkazi huyo ameiomba DAWASCO kutoa taarifa mapema ili wanapopata bili zao wasishangazwe na kiasi cha bili kilicholetwa.

Kwa upande wa DAWASCO, Kaimu Meneja Uhusiano Bi Everlasting Lyaro alisema bei hiyo mpya imeanza kutumika rasmi desemba mosi na wanaendelea kuwaelimisha wananchi wa maeneo mbalimbali juu ya ongezeko hilo ili kuepuka usumbufu wakati wa ulipaji wa bili.

“tumeanza bei mpya rasmi ya Maji juzi (01/12/2015) kwa sh 1663 kwa unit moja ya Maji ambayo ni sawa na lita za ujazo 1000. Tulishawaandaa wateja wetu kuipokea bei hiyo kwa kuwaelimisha na pia kupitia njia za mawasiliano za shirika kama vile Tovuti, Magazeti na hata ujumbe mfupi wa simu ya Mkononi ili wajue kiasi cha maji watakachochajiwa kwa mwezi huu wa disemba” alisema Lyaro.

Mnamo Mwezi novemba 2015, mamlaka ya udhibiti wa huduma ya Maji na Nishati (EWURA) ilipitisha bei pendekezi ya maji kwa watumia Maji wa Jiji la Dar es Salaam kama ilivyoombwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitka Dar es Salaam (DAWASA) kutoka sh 1098 hadi Tsh 1663 kiwa ni ongezeko la ziaid ya asilimia 50 ya bei ya awali.
  • via Michuzi blog

Hatutakuwa na TANESCO katika uzalishaji wa umeme bali usafirishaji tu

Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Mhandisi, Hosea Mbise akizungumza katika mkutano wa tatu wa wawekezaji na wadau wa nishati ya umeme ujulikanao kwa jina la Powering Africa uliodhaminiwa na kampuni ya Wind East Africa.
WAKATI Serikali ikibainisha kuliondoa Shirika la umeme nchini (TANESCO) katika uzalishaji wa umeme, kampuni ya kuzalisha umeme wa upepo (Wind East Africa) imesema itaanza uzalishaji wa nishati hiyo mwishoni mwa mwaka ujao.

Wakizungumza katika mkutano wa kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya umeme, Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Mhandisi, Hosea Mbise na Mwanzilishi na Mkurugenzi wa wa kampuni ya Wind East Africa, Rashid Shamte walieleza mkakati uliopo katika kuboresha sekta ya umeme nchini ambapo baada ya muda, Tanesco itakuwa na kazi ya usafirishaji tu huku kazi ya uzalishaji ikifanywa na kampuni kama Wind EA.

Mbise alisema kuwa alisema uzalishaji wa umeme unahitaji uwekezaji wa hali ya juu ikiwamo kutoa fursa kwa kampuni mbalimbali kuanza kuzalisha umeme kwa manufaa ya Taifa.

Kwa mujibu wa Mbise, hatua za awali za kuliondoa shirika hilo la umeme nchini kuwa mzalishaji wa nishati hiyo umeanza na ifikapo 2022, Shirika hilo halitajihusisha na uzalishaji wa umeme zaidi ya kazi ya usafirishaji tu.

"Kwa utaratibu huu, Tanesco sasa itaondoshwa katika mchakato wa kuzalisha umeme na kubaki kuwa msambazaji, hatua tayari zimeanza kwa kuangalia madeni yaliyopo Tanesco na jinsi ya kuyafuta sanjari na kuwachukua watumishi wa Tanesco.

"Ifikapo 2022 hatutakuwa na Tanesco katika uzalishaji wa umeme bali umeme utazalishwa na kampuni mbalimbali na mkakati uliopo ni kwamba hadi kufikia 2030, asilimia 70 ya Watanzania wawe wamefikiwa na huduma ya umeme," alisema Mbise.

Kwa upande wake, Shamte alieleza kuwa mradi wa umeme wa upepo wa Singida kwa sasa upo katika maandalizi ya kina kuanza na mwaka ujao watakamilisha taratibu mbalimbali kwa mujibu wa sheria za uwekezaji.

Shamte alisema kuwa mradi huo ambao utazalisha 100 Mega Watts mbali ya kutatua tatizo la umeme, utaufanya mkoa wa Singida kubadilika kwa kupata maendeleo makubwa kiuchumi, biashara na hata kijamii.

Alisema kuwa mkataba mikataba ya kumalizia uwekezaji wamradi huo itasainiwa mwanzoni mwa mwezi ujao (Januari 2017).

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa kampuni ya Wind East Africa, John Chagama alisema, mradi wa umeme wa upepo utakapokamilika utawanufaisha Watanzania hasa wakazi wa Singida ambako mradi huo unaanzishwa.

"Kwanza utasaidia kutoa ajira kwa wakazi wa Singida, lakini pia utawanufaisha Watanzania hasa wa kipato cha chini kwani umeme utakuwa wa gharama nafuu," alisema.

Chagama alisema kuwa umeme wa upepo ni mradi wa kudumu na utawafanya watanzania kupunguza gharama za maisha kwani bei ya umeme itashuka.


Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa kampuni ya Wind East Africa John Chaggama akifafanua jambo kuhusiana na uwekezaji wao wa Umeme wa Upepo uliopo mkoani Singida. Chaggama alisema mradi huo utatatua tatizo la nishati hiyo hapa nchini mara utakapoanza rasmi uzalishaji mwishoni mwa mwaka 2017.

Wadau na wawekezaji mbali mbali wa nishati ya umeme wakimsikiliza Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Mhandisi, Hosea Mbise hayupo pichani wakati wa ufunguzi wa mkutano wa tatu wa wawekezaji na wadau wa nishati ya umeme ujulikanao kwa jina la Powering Africa uliodhaminiwa na kampuni ya Wind East Africa.

Taarifa ya ziara ya ghafla bandarini na TRL aliyoifanya leo Waziri Mkuu Majaliwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimwonyesha Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es salaam, Bw. Abel Mhanga (kulia) orodha ya makontena 2,431 yaliyopitia kwenye banda ya Dar es salaam bila kulipiwa kodi wakati alipofanya ziara kwenye bandari hiyo Desemba 3, 2015.


WAZIRI MKUU ATINGA TENA BANDARINI NA TRL

*Akuta makontena 2,431 yametoka bila kulipiwa ushuru
*Ataka majina yaletwe ofisini leo saa 11 jioni
*Atoa wiki wiki moja kwa mfumo wa malipo kubadilishwa
*Akagua mabehewa, awaweka kiporo TRL

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara nyingine ya kushtukiza bandarini na kukagua mfumo wa upokeaji na utoaji mizigo na utozaji wa malipo baada ya kupewa taarifa kwamba kuna makontena 2,431 yametolewa bila kulipiwa ushuru.

Waziri Mkuu alisema kwa mujibu wa taarifa ya ukaguzi wa bandari ya kuanzia Machi hadi Septemba 2014, makontena hayo yalipita bila kulipiwa kodi kupitia bandari kavu nne (ICDs) ambazo ni JEFAG, DICD, PMM na AZAM.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ni watumishi 10 tu ambao wamesimamishwa kazi kutokana na makosa hayo. “Mmeamua kuwasimamisha kazi watu wadogo na kuwaacha wakubwa wanaendelea na kazi. Hatuwezi kuendelea kuikosesha Serikali mapato namna hii,” alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu amemtaka Kaimu Meneja wa Bandari, Bw. Hebel Mhanga amletee ofisini majina ya watumishi wote waliohusika na ukwepaji kodi huo ifikapo leo saa 11 jioni. Pia amempa Meneja huyo wiki moja kuhakikisha kuwa mamlaka hiyo inabadilisha mfumo wa utozaji malipo kutoka kwenye billing system na badala yake kuweka mfumo wa malipo wa kielektroniki (e-payment).

Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Desemba 3, 2015), wakati akikagua idara mbalimbali za mamlaka ya bandari na kuona ukaguzi wa mizigo unavyofanyika kwa kutumia scanners. Akiwa kwenye chumba cha scanner mojawapo, Waziri Mkuu alikuta manifest moja ikisema kontena limejaa diapers lakini picha ya kwenye kompyuta ya scanner ilionyesha kuwa ndani ya kontena hilo kuna vitu kama vifaa vya umeme.

Kwa mujibu wa Kaimu Meneja Bandari upande wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Ben Usaje ambaye pia ni msimamizi wa kitengo cha scanner, inapobainika taarifa kama hiyo inapaswa itumwe kwa wenye ICDs ili wafanye ukaguzi kwa kulifungua kontena ili kuhakikisha mali zilizomo ndizo zilizoandikishwa kwenye manifest.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa amefanya ziara ya kushtukiza kwenye ofisi za Shirika la Reli (TRL) na kukagua mabehewa yaliyokuwepo kisha akazungumza na baadhi ya wafanyakazi waliokuwepo kwenye stesheni hiyo ambako alibaini madudu kwenye malipo ya mishahara na makato ya michango ya wafanyakazi.

Akizungumza na Mkurugenzi Mkuu TRL, Mhandisi Elias Mshana, Waziri Mkuu alisema amefika kwenye shirika hilo ili kujifunza utendaji wao kazi lakini anazo taarifa za wao kupewa fedha na Serikali kiasi cha sh. bilioni 13.5/- ili waendeleze miundombinu ya reli lakini hawakufanya hivyo. “Nia ya kuwapa fedha hizo ilikuwa ni kuboresha miradi ili muweze kujiendesha kibiashara lakini nyie mkaamua kujilipa wenyewe,” alisema.

“Ninazo taarifa kuwa baada ya hapo, mlikopa sh. bilioni 3 kutoka benki ya TIB ili kuendesha miradi ya shirika lakini badala ya kufanya miradi, fedha hizo mkaamua nazo kujilipa mishahara. Sasa sijui mnarudishaje huo mkopo wakati hakuna mradi wowote uliofanyika,” alihoji bila kupata majibu.

Alipoulizwa wafanyakazi wana matatizo gani hapo TRL, Katibu wa TRAWU, Bw. Boaz Nyakeke alisema wanadai malimbikizo ya makato yao kwenye mifuko ya pensheni, malimbikizo ya makato kwenye SACCOS na malimbikizo ya kuanzia Julai – Novemba 2014.

Waziri Mkuu kwa upande wake alimtaka Mhandisi Mshana asimamie uboreshaji huduma za usafiri wa treni katika Jiji la Dar es Salaam ili hata mabasi ya mwendo kasi yatakapoanza wananchi waweze kuwa na uhuru wa kuchagua aina ya usafiri wautakao.

“Tunataka kujenga yadi kubwa nje ya mji ili watu wenye magari wawe wanayaacha huko na kutumia usafiri wa treni au DART kuja mjini kama njia mojawapo ya kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam,” alisema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
ALHAMISI, DESEMBA 3, 2015.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua bandari ya Dar es salaam Desemba 3, 2015 ambako alikwenda kupata ukweli kuhusu makontena 2,431 yaliyopitia kwenye bandari hiyo bila kulipiwa kodi ya serikali.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mfumo wa kukagua makontena bandarini kwa kutumia scanner huku akipata maelzo kutoka kwa Ofisa wa forodha, January Shauri wakati alipotembelea bandari ya Dar es Salaam Desemba 3, 2015 kutaka kujua ukweli wa tuhuma za makontena 2,431 yaliyopita bandarini hapo bila kulipiwa kodi ya serikali.

Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu utoaji bili za kulipia kodi za serikali kwa watumiaji wa bandari ya Dar es salaam kutoka kwa ofisa mwandamizi wa masuala ya fedha, Bw. Sartho Mbuya wakati alipotembelea bandari hiyo Desemba 3, 2015 kutaka kujua ukweli wa tuhuma za makontena 2,431 yaliyopita bandarini hapo bila kulipiwa kodi za serikali.


Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini TRL wakati alipotembelea stesheni ya Dar es Salaam kukagua uendeshaji wa Shirika hilo Desemba 3, 2015.

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akitembelea steheni ya reli ya Dar es Salaam Desemba 3, 2015.
Agizo la Wizara kwa umma kuhusu kuvamia maeneo ya ardhi kuvizia fidia


Wawili wasimamishwa kortini kwa njama za kumuua Mwenyekiti NEC na familia yake

WATU wawili wakiwemo Mwanasheria na Mwalimu, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka ya kula njama za kumuua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva na familia yake.

Washitakiwa hao, Mwalimu Samwel Gikaro (30) na Mwanasheria Angela Mbonde (32) walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba.

Wakili wa Serikali, Hellen Moshi alidai kati ya Oktoba 23 na Novemba 16, mwaka huu katika maeneo tofauti Dar es Salaam na maeneo mengine nchini, washitakiwa na wengine ambao hawajafika mahakamani, walikula njama za kumuua Jaji Lubuva na familia yake.

Washitakiwa walikana mashitaka na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo unaendelea na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa. Wakili wa upande wa utetezi, Moses Kaluwa ambaye alifika mahakamani hapo kwa niaba ya Wakili Peter Kibatala, aliiomba mahakama itoe dhamana kwa washitakiwa kwa kuwa mashitaka yanayowakabili yana dhamana.

Wakili Moshi alidai Jamhuri inatambua mashitaka hayo yana dhamana kisheria, lakini inaomba dhamana izuiliwe kwa muda hadi watakapoona inafaa kwa sababu ya asili ya kosa, washitakiwa hawawezi kuwa nje wakati upelelezi unaendelea.

Hata hivyo, Wakili Kaluwa alidai sababu zilizotolewa na upande wa jamhuri hazina msingi kisheria, suala la msingi ni mashitaka yanayowakabili kuwa na dhamana na washitakiwa wapo tayari kutimiza masharti yatakayotolewa na mahakama.

Hakimu Simba alisema pamoja na mashitaka hayo kuwa na dhamana kisheria, kutokana na kosa pamoja na hatua ya upelelezi, mahakama imekubali hoja za upande wa jamhuri hivyo washitakiwa watakuwa rumande. Kesi itatajwa tena Desemba 15, mwaka huu.

[Hotuba] Agizo la Rais Magufuli katika mkutano na wadau wa sekta binafsi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wadau wa Sekta Binafsi na kuwaahidi kuwapa ushirikiano mkubwa kwani anatambua mchango wao katika ukuaji wa uchumi na kuwasihi kuwa wazalendo katika suala la utoaji kodi ili kulipeleka taifa katika nchi yenye uchumi wa Kati Ikulu leo Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amewapa siku saba kuanzia tarehe 03/12/2015 wafanyabiashara wote ambao waliingiza mizigo yao bila kulipa kodi wakalipe kwani baada ya hapo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Hayo yamesemwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam na Mheshimiwa Rais katika mkutano wake na wadau wa sekta binafsi alipoamua kufanya mazungumzo nao pamoja na kuwasikiliza maoni yao ikiwa ni sehemu ya ahadi zake katika kipindi cha kampeni za kuomba kura za kiti cha Urais,lengo likiwa ni kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta binafsi.

Mheshimiwa Rais aliendelea kusema kuwa katika kipindi hichi cha miaka mitano amedhamiria kuijenga nchi na watu wasimuelewe vibaya kwa maamuzi anayofanya kwani ni kwania njema ya kuleta maendeleo na siyo ujeuri.

“Tutaangalia namna ya kupunguza utitiri wa ushuru katika bidhaa mbalimbali,mfano katika kipindi cha kampeni niligundua katika Mkoa wa Kagera na Kilimanjaro wanakolima zao la Kahawa,wamekuwa wakitozwa tozo 26 kwa zao hilo na hiyo imechangia kusababisha wafanyabiashara wa zao hilo kufanya biashara haramu ya kupeleka zao hilo kwa magendo kuuza katika nchi jirani”,alisema Mheshiwa Rais Dkt. Magufuli.

Pamoja na hayo Mheshimiwa Dkt.Magufuli amewaahidi wadau wasekta binafsi ushirikiano mkubwa kwani anatambua mchango wao katika kukuza uchumi na pia amewataka wadau hao kuwa wazalendo na kuliacha kukwepa kulipa kodi ili tuweze kujenga taifa lenye maendeleo makubwa ya kiuchumi.

Mheshimiwa Rais Dkt.Magufuli ameendelea kusema kuwa kama kutakuwa na mfayabiashara yeyote atakayetaka kuwekeza na akakwamishwa na mtu aliyechini ya uteuzi wake basi mtu huyo ataondoka kwani sasa ni wakati wa wadau wa sekta binafsi kuanza kuanzisha viwanda mbalimbali vitakavyo toa ajira.

Pamoja na hayo Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli amewapa mawazo ya kibiashara wadau wa sekta binafsi kuanzisha kampuni ya kutenganisha udongo unaotoka kwenye machimbo ya madini,kuanzisha viwanda vya samaki pembezoni mwa bahari pamoja na kutengeneza samani zitokanazo na mazao ya misitu.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bw.Regnald Mengi amesema kuwa wako tayari kumpa ushirikiano mkubwa Mheshimiwa Rais katika kuhakikisha uchumi watanzania unakuwa kwa haraka na pia amemuomba mheshimiwa rais kuendelea kukemea masuala ya rushwa pamoja kusaidia kupunguza utitiri wa kodi.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Viongozi na Wawakilishi wa Umoja wa Sekta Binafsi nchini (Tanzania Private Sector Foundation - TPSF) katika ukumbi wa mkutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 3, 2015.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Viongozi na Wawakilishi wa Umoja wa Sekta Binafsi nchini (Tanzania Private Sector Foundation - TPSF) katika ukumbi wa mkutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 3, 2015.

  • Picha tumeshirkishwa na IKULU