Mmarekani atamani Magufuli awe rais wao

John Pombe Magufuli in July of 2015. Khalfan Said/AP
John Pombe Magufuli (phogo:  Khalfan Said/AP)
NPR (National Public Radio) ni chombo kimojawapo kikubwa cha habari nchini Marekani.

Katazo la kuongeza ada kwa shule zisizo za serikali


Amazing! How to calm a crying baby using Dr Hamilton's technique "The Hold"Dr. Hamilton, a pediatrician in Santa Monica, CA shows how to calm a crying baby using "The Hold". This technique has been utilized by Dr. Hamilton (Dr. Bob) to quiet infants during office visits. Parents have learned it and have experienced great success at home. You can too. 

His Pacific Ocean Pediatrics is in Santa Monica pacificoceanpedriatics.com. He also leads Africa medical missions with Lighthouse Medical Missions lighthousemedicalmissions.com.

Ujumbe FWD kutoka WhatsApp: Ugonjwa wa kuhifadhi vitu... Hata kikopo cha ice cream kinaoshwa

Umasikini sio sababu ya kuwa mchafu wala utajiri siyo kuwa na kila kitu hata kama hukihitaji. 

Hebu angalia hapo nyumbani kwako! Vitu msivyovihitaji leo wala kesho, mmeweka vya nini? 

Umenunua makochi mapya, yale ya zamani mmegawana vyumbani mnaishia kurundika minguo hapo na kufuga mipanya. Godoro umenunua jipya la zamani umeviringisha juu ya kabati. Kabatini kwako kuna nguo ulivaa ukiwaona secondary mpk leo unazo eti ukumbusho au utazivaa ukipungua. 

Jikoni ndo shida iliposhika hatamu!! Mivyombo ya plastiki imepaukiana, imeyayuka na moto ipo tu eti vyombo vya watoto. Mahotpot yamekata roho imebaki kuwa sufuria we unalo tuu. Ndoo hata hazitumiki zip ozipo tu hata maua hazifai kupandia we unazogo tu huchomi, hutupi wala huzihitaji. Vyombo vya udongo vina mapengo na magego km vinang'atwaga na kila kimoja na dizaini yake havifanani coz seti imeshavunjika vunjika hivo ndo vimebaki.

Dressing table imejaa mikopo na mibox haina kazi, perfume ya mwaka 2000 unayo hapo kisa ukumbusho wa zawadi. 

Stoo yenu wenyewe ila mwaiogopa kuingia coz imejaa vitu visivyohitajika imekuwa ghetto la panya badala kuweka mnavyohitaji.

Nje ya nyumba kuna gari la urithi la babu lipogo tu hapo linafuga ndege. 

Kutupa vitu visivyohitajika hamtupi eti dhambi na kugawa hamgani coz mmeviharibu hadi mwisho mtampa nani? 

Kutwa mnapishana mahospitalini mnaumwa flu na vifua kila siku, kimoja. Kwa nini msiumwe na mnakaa dampo ? Hivi mnajua kama huu ni ugonjwa? Unaitwa hoarder disorder. Tena mnawaambukiza wanenu as wanajua kwao hata kikopo cha ice cream hakitupwagi kinaoshwa kinawekwa hapo. 

Halafu bado unaendelea kumuomba Mungu akupe, akupe uweke wapi na kwako pameshajaa?

eSchool programme for O-Level and A-Level students in Tanzania


The Twiga Holding Limited (lHt) in partnership with Alliance Services Company (ASCo.Edu) have come up with eSchool programme. This programme is designed to help O-Level and A-Level students to learn and examine themselves. This comes with a 7.8" tablet with preinstalled learning materials which comprise of syllabus eBooks and questions, also inclussive are previous NECTA exams with workout answers.

We have applications for smartphones and computers that will have online access to our materials.

The material are tailored for Tanzanian secondary and high school learning curriculum.

This are the product services:

7.8" tablet tzs 400000 or usd 200

Offline subscription on smartphones or computers tzs 50000 or usd 25

Online subscription tzs 2000 usd 1 per week

Online subscription tzs 5000 or usd 4 per month

Online subscription tzs 7000 or usd 5

Online subscription tzs 12000 or usd 7

For more information on this services and products contact as through WhatsApp +254770195185 or email: [email protected]
The shocking effects of drinking alcohol whilst pregnant


Gazeti la MTANZANIA: Mamilioni yakutwa kwenye majumba ya waajiriwa TRA

Kaimu Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Philip Mpango akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Ijumaa, Desemba 4, 2015.
SIKU chache baada ya kigogo mmoja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kubainika kumiliki nyumba 73, wafanyakazi wengine wa mamlaka hiyo wamekutwa na mamilioni ya shilingi waliyoficha majumbani mwao, limeripoti gazeti la MTANZANIA.

Taarifa kutoka ndani ya TRA zinapasha kuwa tangu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa awasimamishe kazi maofisa kadhaa wa mamlaka hiyo, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na kitengo cha uchunguzi cha mamlaka hiyo, hivi sasa wapo kwenye msako wa kubaini ukwasi wa wafanyakazi wake.

Chanzo chetu cha kuaminika kilisema kuwa juzi maofisa wa kitengo cha uchunguzi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, walifika katika eneo la Tegeta Salasala wilayani Kinondoni na kuvamia nyumba mbili za wafanyakazi wa mamlaka hiyo.

Katika nyumba hizo, wafanyakazi hao kila mmoja alikutwa na kiasi kikubwa cha fedha ndani kuliko kiwango cha mshahara anaolipwa.
“Walivamiwa wafanyakazi wawili (majina yanahifadhiwa), ambapo katika kila nyumba zilikutwa fedha nyingi. Kwa mtu wa kwanza zilikutwa Sh milioni 200 na yule wa jirani yake pia alikuwa na zaidi ya shilingi milioni 150.
“Tangu kuanza kwa msako huu wafanyakazi wengi wamekuwa hawana amani kabisa, na hata wengine wanasema wazi kama wangekuwa na uwekezaji wa nje ya nchi wangeondoka kabisa nchini,” kilisema chanzo chetu.
Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wafanyakazi hivi sasa wamelazimika kuzikimbia nyumba zao na kuishia kulala hotelini huku wakienda kazini wakiwa na hofu.

Hivi karibuni, vyombo vya habari viliripoti kuwa Kamishna wa Forodha wa TRA, Tiagi Masamaki, aliyesimamishwa kazi pamoja na vigogo wengine wa mamlaka hiyo kutokana na upotevu wa kontena 349 zenye thamani ya Sh bilioni 80, amebainika kumiliki nyumba 73.

KAULI YA KOVA

MTANZANIA ilimpomtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, alisema hawezi kuzungumzia suala la uchunguzi ulipofikia kwani suala hilo lipo ngazi za juu.

“Siwezi kuzungumzia hilo kwani kwa sasa lipo ngazi za juu kwa ajili ya uchunguzi wa kina,” alisema Kova.

EALA congratulates President Magufuli and Tanzanians

From left Hon Martin Ngoga, Hon ShyRose Bhanji, Hon Taslima Twaha and Hon Peter Mathuki outside the Parliament of Rwanda moments before the Chamber commenced.
EALA has moved a Resolution congratulating President of the United Republic of Tanzania, H.E. Dr John Pombe Joseph Magufuli following his election as the fifth President of the United Republic of Tanzania. EALA further commends the people of the United Republic of Tanzania on their commitment to peace and democracy during the General elections.

At the same time, EALA wants H.E. Dr John Pombe Joseph Magufuli to address the Assembly at the earliest opportunity.

“Aware of the credible elections held in Tanzania, we would like to seize this great opportunity to extend to His Excellency, President John Pombe Joseph Magufuli our warmest congratulations and to wish him every success at a time of great expectations in Tanzania, the East African Community and Africa in general in terms of national unity, prosperity of the people in maintaining the position as a strong champion for regional integration and democracy in Africa.

We would also like to extend our sincere congratulations to the CCM party for the renewed confidence and trust by the people of the United Republic of Tanzania to spearhead their aspirations for a great future. We commend the opposition fraternity for a well fought battle, for behaving responsibly after the defeat, keeping in mind the peace and security which are the common interest are above any other individual interest”, a section of the Resolution says.

The Resolution moved by Hon Jeremie Ngendakumana, recognizes and takes pride in the success of the United Republic of Tanzania which it avers has made history in what could be the most competitive Presidential elections ever since multiparty politics commenced.

The Assembly further appreciates the brilliance and tone of campaigns demonstrated which exemplifies maturity and vitality of democracy in Tanzania.

The general elections of October 25th, 2015 in Tanzania were the fifth since the re-introduction of the multiparty democracy in 1992 and therefore constituted another important step towards the consolidation of democracy. Since the first multiparty elections in 1995, the United Republic of Tanzania has enjoyed peaceful transfer of political power in conformity with the constitutionally established Presidential limits.

Hon Mumbi Ngaru noted that the election of Dr Magufuli as President and that of H.E. Dr Samia Suluhu, as the first woman Vice President was good show for the women of East Africa. She remarked that Tanzania had realized significant maturity in the politics.

Hon Taslima Twaha remarked that whilst the elections had produced the President of United Republic of Tanzania, the Zanzibar Elections Commission had declared the elections in Zanzibar a nullity.

“The international community has called on President Magufuli to endeavor to expeditiously end the stalemate. I propose that we add this matter on the Resolution”, Hon Twaha said. Hon Maryam Ussi said the issue of Zanzibar was work in progress.

Hon Peter Mathuki said President Magufuli had taken on to fighting corruption wholeheartedly and this in the long run would prove to be useful to the country.

Hon Dora Byamukama said H.E. Dr Magufuli had good credentials. “We should adopt the slogan of Hapa Kazi Tu (loosely translated to Time to work is now) across the entire region,” she said.

Hon Abubakar Ogle said the region needed the energy and stamina as exhibited by H.E. Dr Magufuli. This should be sustained. He said the process in Zanzibar was objective and that challenges were realized when the counting process began.

Hon Adam Kimbisa said the President had carried out civil campaigns devoid of ethnic or divisionary tactics while Hon Sara Bonaya said there were vital lessons that the rest of the region could pick up on.

Hon Martin Ngoga remarked that the historic ideology of deploying graduates and students in other regions of work and schooling was necessary towards consolidating the prevailing peace. “We must congratulate the founding father of the nation and the subsequent leaders”, he said.

The Minister for EAC, Republic of Uganda, Hon Shem Bageine remarked that the President was keen in ensuring infrastructure is maintained up to the best standards.

Council of Ministers also looks forward to his contribution when it comes to assent to Bills and the uptake of the Political Federation as well.

Yesterday however, Hon Dr Kessy Nderakindo said the elections in Zanzibar were yet to be completed. She said United Republic of Tanzania was lucky to have tolerance.

Hon Shyrose Bhanji said the Head of State had in his acceptance speech to Parliament prioritized road and rail network, revive industries and enhancement of the Dar es Salaam port. All this are measures that will enhance the integration of East Africa.

Official photos of the Prime Minister Kassim Majaliwa and wife, Mary

Majaliwa Kassim Majaliwa - Tanzania Prime Minister
Majaliwa Kassim Majaliwa - Tanzania Prime Minister 
Mary Majaliwa
Mary MajaliwaTaarifa: Sheria mpya za kutoa huduma za ziada

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Sayansi na Tekinolojia Priska Olomi (kushoto) , akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es Salaam leo, kuhusu kutungwa kwa kanuni za huduma za ziada kwa makampuni ya simu nchini zitakazo walinda watumiaji wa huduma hizo,kulia ni Mkuu wa kitengo cha Sheria wa Wizara hiyo, Veronika Sudayi. (Picha na Hassan Silayo)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KANUNI MPYA ZA HUDUMA ZA ZIADA ZA MWAKA 2015 ZA SHERIA YA MAWASILIANO YA KIELEKTRONIKI NA POSTA YA MWAKA 2010 


(THE ELECTRONIC AND POSTAL COMMUNICATION ACT 2010 (VALUE ADDED SERVICES) REGULATIONS 2015) 


Ndugu Waandishi wa Habari
1. Awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutupatia uhai na afya njema na kutuwezesha kukutana leo kupeana taarifa kuhusu Kanuni Mpya za Huduma za Ziada za Mwaka 2015 ambazo zinatokana na Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya Mwaka 2010. Napenda pia kuchukua nafasi hii kuwashukuru kwa kukubali mwito kushiriki nasi katika siku hii ya leo. Karibuni sana.

Ndugu waandishi wa Habari.
2. Sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) imeendelea kukua kwa kasi duniani na hapa nchini kwetu na imeleta mafanikio mengi katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, kisiasa na kijamii kwenye ngazi ya kitaifa na kwa mwananchi mmoja mmoja katika maisha ya kila siku kwa waishio mijini na vijijini. Idadi ya watumiaji wa huduma za mawasiliano nchini imeendelea kuongezeka kutoka line za simu za viganjani milioni 2.96 mwaka 2005 hadi kufikia milioni 32.1 mwezi Desemba 2014. Watumiaji wa mfumo wa intaneti nao wameongezeka kutoka milioni 3.56 mwaka 2008 hadi kufikia milioni 11.34 mwaka 2014.

Mafanikio haya yanathibitika nanyi mmekuwa ni mashahidi kwa kuongezeka kwa huduma za mawasiliano na huduma za ziada za matumizi ya mitandao ambapo imerahisisha kutoa na kupata huduma kwa haraka na kwa wakati; na wananchi hawalazimiki kusafiri; na kupunguza urasimu kama vile huduma za kutuma na kupokea pesa; kulipia ankara za maji, umeme, ada; ukusanyaji wa mapato; kulipia leseni; kusafirisha taarifa na data; huduma mtandao kama vile Serikali mtandao, biashara mtandao, shule mtandao na tiba mtandao.

Kwa mfano kuna ongezeko kubwa la huduma za ziada kupitia mawasiliano ya simu za kiganjani. Huduma hizo ni pamoja na miamala ya kifedha ambayo ina watumiaji wapatao 12,330,962 na ununuzi wa huduma na bidhaa kwa kutumia miamala ya kibenki. Hivi sasa, wananchi wanaweza kufanya malipo ya huduma mbalimbali wanazozitumia kupitia simu za kiganjani ambapo katika kipindi cha Julai, mwaka 2013 hadi Aprili, mwaka 2014 jumla ya miamala 972,641,605 yenye thamani inayofikia shilingi Trilioni 28.3 imefanyika. Maendeleo haya yamesaidia kuokoa muda na kupunguza msongamano sehemu za kulipia na kupata huduma hizi.

3. Aidha, mafanikio hayo yameleta changamoto mbalimbali kwenye Sekta na katika jamii yetu. Kwa leo tunazungumzia uwepo wa changamoto ya utoaji wa huduma za ziada kwa watumiaji wa huduma za ziada bila kuwa na utaratibu unaoeleweka kati ya mtoa huduma na mpokea huduma au mlaji. Baada ya kujitokeza kwa changamoto katika utoaji wa huduma za ziada, Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia ilitunga Kanuni Mpya za Huduma za Ziada za Mwaka 2015 (Value Added Services - VAS Regulation 2015).

Kanuni hizo zimetangazwa kwenye Gazeti la Serikali la tarehe 7 Mwezi Agosti mwaka huu 2015 na kupewa GN. Namba. 320. Kanuni hizo zimetokana na Sheria ya Mawasiliano ya kielektroniki na Posta ya Mwaka 2010 (The Electronic and Postal Communication Act 2010) iliyotungwa na kuridhiwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 29 Januari 2010 na badae kusainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 20 Machi 2010.

Ndugu Wananchi
4. Lengo kuu la Kanuni za VAS ni kuweka utaratibu mahususi unaoleweka wa utoaji na upokeaji wa huduma za ziada. Huduma za ziada ni huduma za mawasiliano za kielektroniki zinazotolewa kupitia mitandao zaidi ya huduma za msingi za mawasiliano. Kanuni za VAS zimeweka utaratibu kwa mlaji kujiunga na kujiondoa kupata huduma za ziada; wajibu wa mtoa huduma na mlaji wa huduma za ziada; pamoja na adhabu pindi matakwa ya kanuni yatakapokiukwa. Kimsingi kanuni hizi humlinda mlaji wa huduma za mawasiliano asipewe huduma ambazo hajaridhia kupitia huduma za ziada zinazotolewa na watoa huduma za mawasiliano.

Ndugu Waandishi wa Habari
5. Kanuni za VAS zinamtaka mtoa huduma za ziada kutoa taarifa kamili na sahihi kuhusu huduma za ziada katika lugha rahisi na ya uwazi. Lugha zinazotakiwa kutumika kwa mujibu wa Kanuni zetu Mpya ni Kiswahili na Kiingereza tu. Mtoa huduma za ziada atakuwa na wajibu ufuatao katika kutoa huduma kwa mlaji;

i. Kutoa masharti na vigezo vya huduma zote ikiwemo gharama, kwa njia ya kielektroniki na kudurufu (printed and electronic formats);

ii. Ikiwa mhusika mwingine atahusishwa katika utoaji wa huduma hiyo (third party), mlaji anapaswa kujulishwa kuhusu hitaji ama utegemezi wa huduma hizo kutoka kwa mhusika mwingine;

iii. Kuzingatia matakwa ya Kanuni za Viwango vya Huduma (Quality of Service - QoS) za Sheria ya EPOCA;

iv. Ikiwa kutakuwepo na mabadiliko katika huduma, mlaji apatiwe taarifa kamili kuhusu masharti ya uhamaji, ikiwa ni pamoja na mabadiliko katika utoaji wa huduma hizo na gharama endapo zitajitokeza;

v. Kumjulisha mlaji juu ya waranti za bidhaa zilizotolewa kwa ajili ya kutumika pamoja na huduma ikiwa ni pamoja na jinsi ya kupata waranti hizo.

Ndugu waandishi wa habari
6. Kanuni zinamtaka mtoa huduma za ziada, kuweka mfumo wa kuwezesha huduma za ziada kwa mlaji kujiunga (opt in / activation) au kujiondoa (opt out/de-activation) ambao ni rahisi na wa uwazi kwa kutumia teknolojia inayofaa ikiwemo ujumbe wa meseji (SMS), Huduma ya sauti (Interactive Voice Request – IVR), namba maalum (Unstructured Supplementary Service Data – USSD) ama mchanganyiko wa teknolojia hizi.Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania itawajibika katika kutoa namba (short code) kwa watoa huduma za ziada ili kuwezesha huduma hizo kupitia teknolojia zilizotajwa.

7. Mlaji anaweza kujiunga (opt in/activation) ili kupatiwa huduma za ziada kwa njia tajwa hapo juu. Ili kujiunga kwa njia ya SMS, mtoa huduma za ziada atatoa taarifa ya uwepo wa huduma za ziada kupitia menyu ya huduma, meseji wakati wa maulizo ya salio, ama meseji ya uthibitisho wa kuongeza salio. Ili kusajili huduma ya ziada katika namba yake, mlaji atachagua kutoka katika menyu ya huduma au kutuma ujumbe mfupi wenye chaguo la huduma anayoihitaji.

Mlaji atapokea ujumbe kutoka kwa mtoa huduma za ziada ikieleza masharti na vigezo vya huduma hiyo, ikiwemo gharama za huduma; kipindi ambacho huduma imewezeshwa; na namna ya kujiondoa katika huduma hiyo. Baada ya kuridhika na masharti na vigezo, mlaji atathibitisha ili huduma hiyo kuwezeshwa katika namba yake. Baada ya hapo, mtoa huduma za ziada atatuma ujumbe wa kuthibitisha kuwezeshwa kwa huduma iliyoombwa (activation).

8. Aidha, kwa kutumia njia ya sauti (IVR) na namba maalum (USSD), pindi mlaji atakapopiga namba ya IVR ama USSD, mlaji atapokea tangazo lililorekodiwa ama orodha ya huduma za ziada zinazopatikana pamoja na masharti na vigezo ikiwa ni pamoja na gharama na kipindi cha huduma hizo. Baada ya mlaji kuchagua kwa kubonyeza kitufe kinachohusika, atapokea uthibitisho ndani ya dakika 15 kwamba maombi ya kuwezeshwa kwa huduma yamepokelewa na yanashughulikiwa. Mlaji atapokea tangazo lililorekodiwa kwamba huduma iliyochaguliwa imewezeshwa. Ikiwa amekosea kubonyeza kitufe, mlaji atataarifiwa na orodha kurudiwa tena.

9. Kanuni zinamtaka mtoa huduma za ziada, kuweka mfumo wa kumuwezesha mlaji kujiondoa katika huduma za ziada (opt out/de-activation) ambao ni rahisi na wa uwazi kwa kutumia ujumbe wa maandishi (SMS) ama Huduma ya sauti (Interactive Voice Request – IVR). Mamlaka inawajibika kutoa namba (short code) kwa watoa huduma za ziada ili kuwezesha mlaji kujiondoa katika huduma hizo.

10. Ili kumuwezesha mlaji kujiondoa kwenye huduma za ziada kwa kutumia njia ya SMS, mlaji atatuma ujumbe mfupi wa maandishi; au kutumia njia ya sauti kwa kupiga namba ya IVR au USSD ambapo mlaji atapokea ujumbe unaomjulisha orodha ya huduma za ziada zilizowezeshwa katika namba yake na kuchagua huduma anayohitaji ili iweze kuondolewa. Mtoa huduma atatuma ujumbe wa maandishi unaohitaji mlaji athibitishe nia yake ya kutaka kujiondoa katika huduma husika. Baada ya kupokea uthibitisho wa kujiondoa kutoka kwa mlaji, mtoa huduma za ziada ataondoa huduma hiyo katika namba ya mlaji. Endapo ikitokea mlaji amekosea, mtoa huduma za ziada atatuma ujumbe mfupi wa maandishi ili kumjulisha mlaji kuhusu kosa lililopo na chaguo la kurudia zoezi husika. Baaada ya mlaji kufanikisha kujiondoa, mtoa huduma za ziada atatuma ujumbe kuthibitisha kwamba huduma iliyochaguliwa imeondolewa katika namba ya mlaji.

11. Aidha, Ili mlaji aweze kujiondoa katika huduma za ziada kwa njia ya sauti (IVR), baada ya kupiga namba ya IVR, mlaji atapata tangazo lililorekodiwa lenye orodha ya huduma za VAS zilizowezeshwa katika namba yake. Baada ya kukubaliana na masharti na vigezo, mlaji atachagua huduma ya ziada ya kuondolewa kwa kubonyeza kitufe kinachohusika na atapokea uthibitisho ndani ya sekunde sitini kwamba ombi la kujiondoa limepokewa na linafanyiwa kazi. Iwapo atakuwa amebonyeza kitufe kisichohusika, mlaji atajulishwa na orodha ya huduma za ziada itarudiwa ili zoezi hilo liweze kurudiwa. Ikiwa mlaji atakosea kwa mara nyingine simu yake itahamishiwa katika kituo cha huduma kwa mteja (call centre) cha mtoa huduma za ziada.

Ndugu waandishi wa habari
12. Katika kutoa matangazo ya promosheni ya huduma za ziada, mtoa huduma za ziada atazingatia Kanuni za Sheria ya EPOCA za kumlinda mteja (Consumer Protection) za mwaka 2011. Mtoa huduma atatangaza kwa mlaji aidha wakati wa kuuliza salio, ama kupitia meseji ya uthibitisho baada ya kuongeza salio ama katika menyu ya mtoa huduma.

Mtoa huduma za ziada hatajihusisha katika kutoa matangazo yasiyoombwa na mlaji kwa njia ya kielektroniki ila tu pale ambapo aidha mlaji ameridhia, ama mwanzoni mwa mawasiliano ataweka wazi utambulisho wa mtoa huduma za ziada (ama mhusika aliyepo kwa niaba) na madhumuni ya mawasiliano hayo; ama mawasiliano yanatoa mchanganuo wa gharama za bidhaa ama huduma ambayo inahusika katika mawasiliano.

Ndugu wananchi
13. Kwa mujibu wa Kanuni Mpya za Huduma za Ziada za Mwaka 2015, Mlaji anawajibu ufuatao;

i. Kuridhia huduma kwa kukubali masharti na vigezo vya huduma kama ilivyoelekezwa katika kanuni hizi;

ii. Baada ya kuridhia masharti na vigezo vya huduma kutoka kwa mtoa huduma za VAS, mtumiaji atabanwa na masharti na vigezo hivyo.

14. Aidha, ni vema ieleweke kuwa kwenye Kanuni ya kumi (10) ya Kanuni hizi Mpya za Huduma za Ziada Kanuni hiyo inaelekeza kuwa mtu yoyote atakayekiuka vipengele vya Kanuni hizi anatenda kosa kisheria na atawajibika kulipa faini ambayo si chini ya shilingi milioni tano ama kifungo kisichozidi miezi mitatu ama vyote kwa pamoja. Kanuni Mpya inapatikana kwenye tovuti ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia www.mst.go.tz

15. Natoa rai kwa watoa huduma za ziada kuwa waendelee kuzingatia Kanuni hizi katika kuwapatia wateja wao huduma za ziada zenye bora na viwango vinavyotakiwa na walaji kuhakikisha kuwa wanapatiwa huduma za ziada inayostahili na waliyoomba kwa kuwa teknolojia imerahisha utaratibu wa utoaji na upokeaji wa huduma za ziada.

Imetolewa na;
Prisca J. Ulomi
Msemaji
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Asanteni kwa kunisikiliza.


Taarifa ya TCRA kuhusu app zinazofuatilia maongezi ya watu WhatsApp


Makamu wa Rais, Suluhu yupo Afrika Kusini akimwakilisha Rais Magufuli mkutanoni


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Shulu Hassan, akisalimiana Mwambata wa Kijeshi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini (Defence advisor) Brig. Gen Ibrahim A. Kimario, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Olver Tambo jijini Johanesburg jana Desemba 3, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Radhia Msuya.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Shulu Hassan, akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Radhia Msuya, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Olver Tambo jijini Johannesburg jana Desemba 3, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais wa China, Xi Jinping, wakati wa Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye kitambaa cheupe) akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.Baadhi ya washiriki katika Mkutano huo kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliohudhuria ufunguzi wa mkutano huo leo jijini Johannesburg.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan (kulia) akiwa katika mazungumzo na Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi, walipokutana kwenye ufunguzi wa Mkutano huo Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye kitambaa cheupe katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wakuu wa Nchi za Afrika baada ya ufunguzi wa Mkutano huo Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Wafanyakazi wote TRA watakiwa kuorodhesha mali zao, 35 wasimamishwa kazi; Makampuni 43 matatani

Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dkt. Philip Mpango (kulia)akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa taarifa ya upatikanaji wa makontena 43 pamoja na malipo ya kodi ya Zaidi ya shilingi bilioni tano kutoka kwa wakwepa kodi,kushoto kwake ni kaimu Kamishna Mkuu wa TRA Bw.Lusekelo Mwaseba.
Na Lorietha Laurence

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kukusanya kodi ya zaidi ya shilingi bilioni tano kutoka kwa wafanyabiashara waliokuwa wamekwepa kulipa kodi.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA Dkt. Philip Mpango amesema hatua hiyo imekuja kufuatia agizo kutoka kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Kassim alipofanya ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam Novemba 27 mwaka huu .

Katika Maagizo hayo ya Mhe. Kassim aliitaka TRA kubaini wamiliki wa makontena 329 yaliyoondolewa kwenye bandari kavu kinyume na taratibu pamoja na kutaja bidhaa zilikuwemo ndani ya kontena hizo ikiwemo wakwepaji wa kodi na kuwachukulia hatua watumishi wa TRA walihusika katika mchakao huo.

Aidha Dkt. Mpango aliongeza kwa kusema mpaka sasa wamefanikiwa kubaini jumla ya kampuni 43 zilizohusika katika uigizaji wa makontena ambayo yaliondolewa katika bandari kavu kinyume na taratibu.

“Katika kontena tulizozikamata hizo tumekuta bidhaa za matairi ya magari,samani mbalimbali,betri za magari,vifaa vya ujenzi,nguo na bidhaa mchanganyiko” alisema Kamishna Mpango.

Kwa upande wa watumishi wa TRA mpaka sasa watumishi 35 wa ngazi mbalimbali wamesimamishwa kazi wakiwemo 27 waliokamatwa wiki hii katika geti namba 5 ambao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.

Pia aliendelea kufafanua kuwa uongozi wa TRA unawataka watumishi wote kuorodhesha mali zao ili kuhakiki uhalali wa mali hizo na endapo watabainika kuwa wamezipata mali hizo kinyume na sheria hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yao.

Naye Naibu Kamishna Mkuu Lusekelo Mwaseba ameeleza kuwa kwa sasa TRA inapitia kwa upya taratibu za utoaji wa leseni ili kuondoa mianya pamoja na kuweka udhibiti katika uondoshaji wa mizigo katika bandari zote, ICDs na bohari za forodha.

“Sambamba na kufuatilia taratibu hizo,TRA pia itahakikisha inawafuatalia mawakala wote wa forodha walioshiliki katika upotevu wa makontena na kuwachukulia hatua ikiwemo kuwafungia leseni na adhabu nyingine kulingana na sheria zilizowekwa” alisema Mwaseba.

Kaimu Kamishna Mkuu Mpango alitoa wito kwa wote wanaohusika na uondoshwaji wa makontena kutoka bandari kavu kinyume na taratibu kujitokeza na kulipa kiasi cha kodi yote wanayodaiwa kama ilivyoagizwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli aliaagiza kwamba wadaiwa wote walipe madeni yao ndani ya siku saba baada ya hapo watachukuliwa hatua kufuatana na mujibu wa sheria.

------------- MWISHO -----------

TAMKO LA MALI NA MADENI


Katika hatua nyingine, Kaimu Kamishna Mkuu wa mamlaka hiyo, Dk. Philip Mpango, ameibuka na kuwataka watumishi wote kuwasilisha fomu za tamko la mali na madeni yao kwa mwaka 2015 kabla ya Desemba 15.

Waraka huo umekuja siku chache baada ya Serikali kuwasimamisha kazi vigogo sita wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), akiwamo Kamishna Mkuu, Rished Bade kutokana na upotevu wa kontena 349.

Taarifa za ndani ambazo MTANZANIA imezipata, zinasema kuwa kaimu kamishna huyo, amewaandikia watumishi hao waraka akiwataka kuwasilisha fomu hizo tarehe hiyo badala ya Machi 31 mwakani.

Gazeti hili lina nakala ya waraka huo ambao umesainiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Ndani, Stella Cosmas.

Waraka huo, ulieleza kuwa agizo hilo linajumuisha pia watumishi wanaowasilisha matamko yao Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

“Tafadhali zingatieni kwamba kwa maelekezo haya tarehe ya mwisho ya kuwasilisha fomu za tamko la mali na madeni imebadilika kutoka Machi 31 mwaka 2016 na kuwa Desemba 15, mwaka huu.

“Kama kawaida, matamko yote yawasilishwe kupitia mfumo wa ARUTI isipokuwa watumishi wanaowasilisha matamko yao Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,” ilisema sehemu ya waraka huo.

Kwa mujibu wa waraka huo, mtumishi yeyote ambaye atashindwa kuwasilisha au kuwasilisha tamko lisilo sahihi, atachukuliwa hatua kali za kinidhamu kama ilivyoainishwa kwenye kanuni za utumishi za Serikali na za Mamlaka ya Mapato.

Aidha waraka huo ulieleza kuwa kwa wale watumishi wapya, wanakumbushwa kuwasilisha matamko yao ndani ya wiki mbili baada ya kuripoti kazini.

Maafisa wa TRA wafikishwa mahakamani kwa kesi ya uhujumu uchumiMshitakiwa namba moja katika kesi ya kuhujumu uchumi, Tiagi Masamaki (katikati) na washitakiwa wenzake wakitoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo mchana baada ya kusomewa mashitaka yao.

Watuhumiwa hao wakisindikizwa na maofisa wa polisi kuingia chumba cha Mahabusu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Aliyekuwa Kamishna wa Kodi na ForodhawaTRA, Tiagi Masamaki akiingia katika gari lenye namba za usajili T 442 BBL wakati alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwa kosa la uhujumu uchumi na kutoa makontena 329 bandarini bila ya kulipiwa kodi na kuisababishia Serikali hasara ya sh. bilioni 12.7. Kushoto ni mtuhumiwa mwingine Harun Mapande ambaye alikuwa Mkuu wa Mfumo wa Kompyuta TRA.
Hapa Masamaki na wenzake wakiingia ndani ya gari kuelekea gereza la Segerea.

Watuhumiwa wa kesi hiyo wakiingia ndani ya gari.

Mkuu wa Mfumo wa Kompyuta wa TRA, Harun Mapande akiwa chini ya ulinzi wa askari Polisi wakati akisubiri kupelekwa katika mahabusu ya gereza la segerea baada ya kusomewa mashtaka mawili ya uhujumu uchumi na kutoa makontena 329 bandarini bila ya kulipiwa kodi na kuisababishia Serikali hasara ya sh. bilioni 12.7. Kushoto ni mtuhumiwa mwingine Harun Mapande ambaye alikuwa Mkuu wa Mfumo wa Kompyuta TRA. 

Watuhumiwa hao waliokaa wakiwa chini ya ulinzi wa polisi.

Gari la polisi lililowabeba watuhumiwa hao likiondoka mahakamani hapo.
  • Picha kutoka kwa Dotto Mwaibale na Francis Dande