Orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili wa mahojiano TBS

Shirika la Viwango Tanzania linapenda kuwatangazia waombaji wa nafasi za kazi zilizotangazwa 25.5.2015 katika kada zifuatazo kuwa usaili wa mahojiano utafanyika tarehe 19 Novemba 2015 hadi tarehe 27 Novemba 2015 katika ofisi za TBS Makao Makuu, Ubungo Dar es Salaam.

Matarajio na matamanio ya Watanzania


Ni unafuu wa kimaisha kwa walalahoi na si faraja ya kuona baadhi ya wachache wakiwajibishwa.

Wakati mwingine utendaji wa mtu unaweza kuwa ni uwakilishi wa ukweli wa mawazo yako yakiwakilisha jamii ya watu wa aina fulani, aidha kitabaka, kijinsia au hata kiimani.

Kiongozi yoyote yule, anapotoa mahamuzi fulani na kulifuatilia ili kutatua tatizo ambalo kwa namna moja au nyingine linaigusa jamii moja kwa moja au kwa njia mbadala, basi wananchi wanaoguswa na jambo ilo aidha watakuwa wanayaangalia maamuzi hayo kwa jicho la bashasha au mashaka, na hii ni kulingana na hali halisi ya jamii hiyo kihistoria na hapo ndipo kunaweza kuzua maswali mengi vichwani mwa wadadisi wa mambo mbalimbali ya kijamii na kisiasa.

Viongozi wetu wanapaswa kuwa makini sana kwa kila hatua wanayochukuwa kwenye maamuzi yao ili yale ambayo yaliwahi kutokea uko nyuma yasijirudie tena.

Unaweza kujiuliza nakusudia nini kwa utangulizi huo. Kwa kuendelea kunisoma unaweza kuelewa kusudio langu ni nini.

Hii nchi imepata uhuru wake mwaka Desemba 1961, mpaka ikifika Desemba 9 2015 ni miaka 54 tangia tujitawale. Tanzania ni nchi iliyopitia kwenye hali na maazimio balimbali ya kisiasa na kiuchumi.

Haya Maazimio yalikuwa mengi tu, moja katika Maazimio ni lile la Arusha. Azimio ambalo lilitoa azimio la kutaifisha Mashamba na Mashirika na Makampuni ya watu binafsi na kuyafanya kuwa ni mali ya Taifa (umma). (sina uhakika hapa kama kweli zilikuja kuwa mali za umma au za viongozi wachache). Mambo hayo yalijiri mwaka sitini na saba (1967) na tukaipa jina - Azimio la Arusha.

Hawakuishia hapo fikra zao sahihi zikapelekea azimio lingine la madaraka mikoani hii ilikuwa mwaka1971... (siyasa hii ilikuja baadae kuuwa co-operatives zote zilizo anzishwa na wananchi, usiniulize tafadhali ilikuwaje kuwaje... sitaki udaku).

Tanganyika ilipotaifisha, mashamba, Mabenki na baadhi ya mashirika... Ilionekana kuwa ni jambo jema na litawainua mpaka makabwela, lakini tukasahau kuwa hayo makampuni na hayo mashamba tuliyoyanyang'anya wenyewe ndio hao hao walioshika soko la ulimwengu wa bidhaa mbali mbali, na ndio hao hao wenye kutengeneza hizo mashine za viwandani....!

Hayo makampuni na hayo mashirika pamoja na mashamba tuliotaifisha, tukawapa ndugu jamaa na marafiki zetu, ili waziendeleze matokeo yake kila mtu anayajuwa... Hakuna hata mmoja aliyesimamishwa mbele ya wananchi kuulizwa kulikoni?

Zikatumika akiba zilizoko, zilipokwisha basi tukabaki tunatizamana tu. Tukaambiwa tufunge mikanda miezi kumi na nane (18), na kweli tukaifunga nikanda mpaka viuno vikawa kama nyigu. Matokeo yake yakatushinda tukaamua kuwarudishia walewale tulio wanyang'anya...!

Nadiriki kusema kuwa hii nchi ni ya wachache sana, ni wale wenye uwezo wa kuuza na kununua, wenye uwezo wa kupata matibabu, wenye uwezo wa kula na kusaza, wenye uwezo wa kutobanana kwenye madaladala na si kwa wale waishio uko vijijini, ambako kwao kuwaona viongozi ni mpaka kipindi cha kampeni.

Wazalendo wale ambao enzi zile walijulikana kama Makabwela, yaani watu wa kipato cha chini, leo hii tunajulikana kwa jina la Walala Hoi, na haswa wanaoishi mikoani wanaweza zaidi kuona kile ninacho kizungumza... Si ajabu uko mikoani na haswa ukitembea siku ya soko au gulio ukamwona dalali akiuza kitanda cha kamba... karne hii.

Miaka ile ya themanini Tanzania iliingia kwenye nngwe nyingine, tilishuhudia aliyekuwa waziri mkuu Marehemu Edward Moringe Sokoine, akitoa maagizo ya kuwafilisi wale wote waliokuwa wakionekana kuwa wana hujumu uchumi wa nchi hii. Walalahoi tukafarijika kiasi kwa kuona sasa hali zetu zitakuwa bora zaidi ya jana.

Matokeo yake yakawa ni kinyume na matarajio yetu. Nchi ikaingia kwenye kizaa zaa kingine kwa wafanyabashara wengi wakajikuta wamepoteza biashara na mali zao, kuanzia majumba, Magari na hata mashamba. Tukajikuta kwa mara nyingine tena nchi haina bidhaa muhimu, kama vile Unga wa Mahindi, Ngano, Sukari, Mchele, sabuni, Mafuta ya kula na ya taa, hizi zote tukaziita bidhaa adimu.

Serikali ilipoona kuwa hali si nzuri, tukaanzishiwa maduka ya kaya, yaani kila familia ilikuwa na resheni yake ya kununua bidhaa kulingana na idadi ya watu wa kwenye familia husika. Mtu alikuwa haruhusiwi kununua bidhaa ambazo tukiziita adimu zaidi ya kiwango kilichopangwa.

Lakini yanini kujikumbusha hayo yote, si wazee wetu walituambia kuwa yaliopita si ndwele tugange ya jayo...? Ah wakati mwingine kukumbuka yaliopita, kunaweza kusaidia tusijikwae pale tulipojikwaa na kudondoka kwa mara ya pili. Kwa sababu aliyeumwa na nyoka akiguswa na unyasi ushtuka, tena anaweza kupiga yowe likawashtua wengi.

Watanzania tulishaumwa na nyoka, na madhara yake bado yapo mpaka hivi leo tunauguza donda. Japokuwa hali inavyo onekana sasa kama vile kuna dalili za furaha na matumaini labda hali inaweza kuwa nzuri kwa jinsi rais Magufuri na timu yake wanavyozikabiri kero chache katika nyingi ambazo wananchi wengi wanaamini zikiondoka basi tunaweza kuwa na nafuu ya kimaisha.

Wakati mwingine ni unafuu wa kisaikolojia tu, kwa kuona kuna watu wanawajibishwa kulingana na utendaji wao kuwa si wa kuridhisha.

Watanzania tuna matatizo mengi yanayotukabili, matatizo ambayo kila kukicha yanaongezeka na kukosa utatuzi yakinifu. Uduma nyingi zimekuwa hazipatikani mpaka kwa kujuana au kwa kutoa rushwa. Japokuwa tunajuwa kuwa rushwa ni uchafu na kama vile mwili mchafu usababisha harufu mbaya na kuwakera walio jilani nawe, hivyo hivyo uduma mbaya za kijamii zinazo ambatana na utowaji wa hongo ukera na kuathiri jamii ya Watanzania kwa kiwango kikubwa sana.

Hali inavyokwenda si kwamba sote tutakuwa matajiri au wenye uwezo kama hao walio na uwezo kifedha, lah! Tunacho tarajia ni kuona kuwa uduma za kijamii kama vile Hospitali, Usafiri, Elimu na hata upatikanaji wa uduma za maji safi na umeme bila kusahau chakula, mavazi na malazi, nakadharika vinapatikana na vikiwa katika hali bora zikiwakilishwa kwa utendaji mzuri na kila mwanachi awe na uwezo wa kuvipata na kunufaika navyo.

Hatutaki kufarijiwa kisaikolojia, kwa kuona tu baadhi ya wafanyabiashara au kwa baadhi ya wahusika wa uduma za kijamii wakiwajibishwa tu, bali tunataka kuona tunapata unafuu wa maisha na kila raiya akajivunia kuwa Mtanzania.

Kwanini nimekumbushia miaka ile ya vita vya wahujumu uchumi na madhira yake kwa jamii ya walalahoi. Lengo langu haswa ni kuitahadharisha serikali, hisije kurudia kosa kama lile tena. Serikali inapaswa kuyaendea haya mambo kwa namna ambayo mlalahoi hato athirika na kujikuta yupo hoi kuliko mika 30 iliyopita.

Wafanyabiashara, baadhi ya viongozi wa kisiasa na wale walio na madaraka, wanaweza kuwa ni wenye kuchukia hali inavyokwenda hivi sasa, kiasi wakaamua kwa namna moja au nyingine kuikomoa serikali aidha kwa kupunguza uwagizaji wa baadhi ya bidhaa na kusababisha mfumuko wa bei au wakaamua tu kupandisha bei za bidhaa ili kuziba lile pengo ambalo lipo wazi la ukwepaji wa kodi na wakati mwingine wakaamua tu kufanya njama na hujuma ili serkali ya awamu hii ya tano isifikie malengo yake.

Kwa miaka yote hamsini ya uhuru, tulikuwa tunaambia kuwa ili nchi iendelee tunaitaji mambo manne, Ardhi, Watu, Siyasa safi na Uongozi bora.
Kiukweli hivi vyote tunavyo, kinachotakiwa tu ni jinsi gani tunaweza kuvitumia ili kutuwezesha kufika kule tunakotaka kufika.

[video] Orodha ya majina yaliyotajwa na TRA ya kampuni na watu waliokwepa ushuru wa kontena


Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) jana ilitaja majina ya kampuni 43 na wamiliki wa makontena 329 ambayo yalipitishwa bandarini bila kulipiwa ushuru, na kufichuliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wiki iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Dk. Philip Mpango alisema Mamlaka hiyo iliagizwa na Waziri Mkuu Majaliwa kuchukua hatua mara moja kwa kufuatilia na kubaini wamiliki wa Bandari Kavu (ICD) zilizohusika katika kashfa hiyo.

Alisema mbali na hilo walitakiwa kuwatambua wamiliki wa makontena hayo, bidhaa zilizokuwemo, kuwalipisha wahusika kodi iliyokwepwa pamoja na kuwachukulia hatua watumishi waliohusika na upotevu huo.

Dk. Mpango aliyataja majina ya makampuni na watu binafsi na idadi ya makontena waliyopitisha bila kulipit ushuru (katika mabado) kuwa ni:-
 1. Lotai Steel Tanzania Ltd (100)
 2. Tuff Tryes Centre Company Ltd (58)
 3. Binslum Tyres Company Ltd (33)
 4. Tifo Global Mart Tanzania Company Limited (30)
 5. IPS Roofing Company Limited (20)
 6. Rushywheel Tyre Centre Co Ltd (12)
 7. Kiungani Trading Co Ltd (10)
 8. Homing International Limited (9)
 9. Red East Building Materials Company Ltd (7)
 10. Tybat Trading Co Limited (5)
 11. Zing Ent Ltd (4)
 12. Juma Kassem Abdul (3)
 13. Salum Link Tyres (3)
 14. Ally Masoud Dama (2)
 15. CLA Tokyo Limited (2)
 16. Farid Abdullah Salem (2)
 17. Salum Continental Co Ltd (2)
 18. Zuleha Abbas Ali (2)
 19. Issa Ali Salim (2)
 20. Snow Leopard Building (2) 
 21. Abdulaziz Mohamed Ally
 22. Ahmed Saleh Tawred 
 23. Ali Amer 
 24. Ally Alhamdany 
 25. Awadhi Salim Saleh 
 26. Faheed Abdallah Said 
 27. Hani Said 
 28. Hassan Hussein Suleyman 
 29. Hamud Suleiman Enterprise 
 30. Kamil Hussein Ali 
 31. Libas Fashion 
 32. Nassir Salehe Mazrui 
 33. Ngiloi Ulomi Enterprises Co Ltd 
 34. Omar Hussein Badaway 
 35. Said Ahmad Hamdan 
 36. Said Ahmed Said 
 37. Salumu Peculiar Tyres 
 38. Sapato N. Kyando 
 39. Simbo Yonah Kimaro 
 40. Strauss International Co. Ltd 
 41. Swaleh Mohamed Swaleh
Alisema kwa ujumla, makampuni hayo yalipitisha makontena 329 ambayo yaliondolewa kinyume cha taratibu kutoka ICD ya Azam inayomilikiwa na Said Salim Bakhresa And Company Limited.

Dk. Mpango alisema bidhaa zilizokuwemo ndani ya makontena hayo ni pamoja na matairi ya magari, samani mbalimbali, betri za magari, vifaa vya ujenzi, nguo na bidhaa zingine mchanganyiko.

Taarifa ya PPF kwa Wastaafu kwenda kuchukua vitambulisho

Shukurani kwa Wasamaria wema waliomchangia dada Mwambepo sasa yupo "Magufuli Ward" MOI

Deo Kakuru akiwa na dada Joyce ndani ya FastJet wakitoka Mbeya keuelekea Dar es Salaam 
Ndugu Wasamaria wema,

Tunapenda kutumia fursa hii kuwapa updates kuhusu dada Joyce Mwambepo, mkaazi wa Sinde jijini Mbeya mwenye umri wa miaka 27 ambaye anaishi na bibi yake mwenye umri wa miaka 80 pamoja na mwanaye mwenye umri wa miaka 4.

Kwa bahati mbaya mwezi April mwaka jana dada huyu alipata ajali ya kugongwa na gari ambalo dereva wake hakusimama kumsaidia. Ila kwa msaada wa wasamaria wema alipelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya ambako inasemekana alikaa kwa miezi mitatu bila kupata matibabu kwa kukosa fedha. Katika uchunguzi wa awali ilibainika kuwa Joyce amevunjika miguu yote miwili, hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako pia baada ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa Mbeya baada ya kukosa pesa za matibabu.

Baada ya mwanahabari Deo Kakuru wa Mbeya kumgundua na kufanya juhudi za kutoa taarifa za dada Joyce katika mitandao mbalimbali, wasamaria wengi wa ndani na nje ya nchi wakaguswa na kuchangia. Mungu mkubwa, kiasi kilichopatikana (kiasi cha 3.2m/-) kimewezesha dada Joyce kupelekwa Dar es salaam toka Mbeya kwa ndege ya Fast Jet Alhamisi iliyopita na moja kwa moja kupelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kupokelewa katika kitengo cha MOI na kupatiwa kitanda katika wodi mpya ijulikanayo kama Wodi ya Magufuli, ghorofa ya tatu chumba namba mbili.

Cha kufurahisha ni kwamba Joyce aliweza kukaa kwenye kiti cha kusukumwa na hata kwenye ndege aliketi kama kawaida, zoezi ambalo hata yeye anasema limemsaidia kwani kwa mara ya kwanza hivi sasa ganzi miguuni inapotea taratibu na ukimgusa anahisi mguso tofauti na ilivyokuwa awali.

Daktari bingwa ameshaonana naye na kumpa matumaini ya kupona, hasa sehemu ya chini ya uti wa mgongo wake ambao inasemekana una matatizo yaliyopelekea kubana mishipa ya fahamu na kufanya miguu ipooze. Zoezi linalosubiriwa kwa sasa ni kupatiwa vipimo vya MRI ili kubaini kiufasaha tatizo lake na hatimaye kupatiwa matibabu. Zoezi hili linatarajiwa kufanyika wakati wowote kuanzia sasa.

Mpiganaji Deo Kakuru amesharejea Mbeya na kijiti cha kumwangalia dada Joyce amekabidhiwa Ankal ambaye anaomba Wasamaria wema waendelee kumuombea na kumsaidia kwa hali na mali dada huyu ambaye ni yatima.

Kwa bahati njema Ankal alikutana na kuongea na Msamaria mwingine aitwaye Mama Rozi ambaye anamuuguza mama yake mzazi aliyelazwa wodi moja na dada Joyce. Msamaria huyu amekubali kumsaidia dada Joyce kwa chakula na pia kumsaidia usafi maana hapo kitandani hawezi kuondoka.

Mungu kweli ni mkubwa. Dada Joyce anatabasamu na kuongea vizuri tu. Anatoa shukurani sana kwa wote waliomsaidia na wanaoendelea kumsaidia. Anasema hana cha kuwalipa ila kusema ASANTE SANA na anamwomba Mola Muumba awazidishie pale patapopungua. Ameomba anayeweza kumtembelea atafurahi sana maana hana ndugu hapa Dar es salaam.Pia anawashukuru sana madaktari waliomhudumia vyema katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya ambao amesema hatowasahau kwa msaada wao.

Ankal amejitolea kuendelea kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce. Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email [email protected] ama whatsapp namba+255 754 271266 kwa jina la Ankal au mratibu-mwenza Deo Kakuru Msimu +255769 512 420. Pia unaweza kuwasiliana moja kwa moja na dada Joyce kwa namba.
Mpiganaji Deo Kkuru akiwa na dada Joyce mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam

Msamaria mwema Mama Rozi akimhudumia dada Joyce akiwa kitandani kwake Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha mifupa cha MOI katika wodi ijulikanayo kama Wodi ya Magufuli ghorofa ya tatu

Wakwepa kodi wanavyoshughulikiwa


Maoni na Uoni Wangu Kisiasa:

Baada ya uchaguzi kwisha na Rais kukabidhiwa rasmi jukumu la kuongoza nchi, Rais Magufuri ameonyesha vile utendaji wake wa kazi kivitendo na tumeshuhudia jitihada zake katika kurekebisha baadhi ya wizara idara mbalimbali za serikali.

Wanao mfahamu John Pombe Magufuri, haswa wale ambao walibahatika kufanya naye kazi hawaoni ajabu katika utendaji wake wa kazi. Kabla ya kuwa Rais wa Tanzania, Magufuri alishakuwa waziri na kufanyakazi kwenye wizara kadhaa na matokeo yake wengi wameyaona na wameyafurahia.

Rais Magufuri tangia kwenye kampeni zake, kauli mbiu yake ilikuwa ni "Hapa Kazi tu" ikimaanisha kuwa serikali atakayo iongoza yeye itawajibika kusimamia kwa kila hali kile ambacho yeye anakiamini kuwa kitasaidia Watanzania katika kujikwamua kiuchumi.

Tumeshuhudia kwa masiku machache tu tangia alipoapishwa rasmi kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, jinsi anavyo yaendea mambo kwa mwendo kasi ya kuwabana wakwepa kodi za serikali na kuwabana watu ambao wanahujumu uchumi kisawasawa kwa lengo la kurejesha pesa zinazoibwa kwenye kodi na kuondoa matumizi yasio ya lazima kwenye wizara na maofisi ya serikali. Kwa kweli ni jambo zuri sana, ila inapaswa pia kuangalia upande wa pili.

Hapa ninacho hofia si uko serikalini la hasha, bali upande wa wafanyibiashara waletao bidhaa aidha mikoani au nje ya nchi, kwa maana athari itakayo patikana kwenye bei ya bidhaa ambazo waletaji wake ndio hao wanaobanwa kikamilifu ili walipe kodi inayo husika.

Bidhaa nyingi ambazo zimelipwa kodi ndogo zina uwezekano wa kuuzwa kwa bei ya chini, na zile ambazo zimelipiwa kodi kamilifu kuna uwezekano wa kuuzwa ghali na ili ndio linaweza kutokea na kusababisha mfumuko wa bei kwa walaji.

Nahofia kuna uwezekano kwa serikali kurudi miaka thelathini nyuma kipindi ambacho serikali ndio walikuwa wapangaji wa bei za bidhaa na si kama hivi sasa wafanyibiashara wanajipangia bei au wanategemea soko la bidhaa lipo vipi...!

Vilevile anapaswa kuwa makini sana na mtandao wa viongozi mafisadi, kwa sababu ndio wanaolengwa, nao wanaweza kutengeneza uadui na kupanga njama za kuhujumu jitihada zake, kwa kukwamisha baadhi ya mambo.

Hali inaweza kuwa mbaya bidhaa zikakosekana kisha ulanguzi na maduka bubu kama zilivyokuwa store bubu za bia enzi ya Nyerere zikarejea tena...!

Ninacho kiona mimi kwa Rais wetu huyu ni jitihada zake kurejesha heshima kwenye kila wizara na hata watakapochaguliwa mawaziri wakute kila wizara zipo safi kiasi chake na hata atakayeshika uwaziri au ukatibu wa wizara husika ajuwe kuwa kinachotakiwa ni utendaji ulio tukuka na si uzembe uzembe kama ilivyokuwa uko nyuma.

Umakini ni muhimu anatakiwa awatumie wasomi mbalimbali kulingana na jambo husika kama vile mambo ya uchumi na fedha, elimu na teknolojia, nakadhalika. Tena akiona mtu anafaa hata kama yupo upande wa upinzani si vibaya kumuweka mahali akapatengeneza vizuri kwa manufaa ya nchi na watanzania kwa ujumla.