Polisi, makampuni binafsi na vitengo vya ulinzi wazindua "WhatAapp group" maalumu kupeana taarifa

Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha (ACP) Edward Balele akifungua kikao kati ya Jeshi hilo na Taasisi za ulinzi kujadili mustakabali wa usalama ndani ya mkoa huu. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Bwalo la Polisi Jijini hapa (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

Jeshi la Polisi mkoani hapa limeazimia kushirikiana na makapuni binafsi ya ulinzi na taasisi za ulinzi kutoka UN-ICTR, UNMICT, kitengo cha ulinzi cha B.O.T pamoja na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu katika kupeana baadhi ya taarifa za uhalifu na wahalifu mara kwa mara kwa njia mtandao wa kijamii wa “WhatsApp”.

Link za kupakua fomu za Ahadi ya Uadilifu kwa Watumishi wa UmmaOfisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma imeanza rasmi kutekeleza Ahadi ya Uadilifu kwa watumishi wa Umma nchini.

Akiongea na vyombo vya habari leo, Katibu Mkuu Hab Mkwizu amesema utekelezaji huo umeanza rasmi Desemba, 2015 ambapo kila Mtumishi wa Umma ataweka saini ya kiapo kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na mazingira ya taasisi husika.

“Utaratibu wa Utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu kwa Watumishi wa Umma umetolewa kupitia waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma Na. 2 wa mwaka 2015 kuhusu utekelezaji wa Ahadi ya Uadilifu kwa viongozi, Watumishi wa Umma na sekta binafsi wa tarehe 1 Agosti, 2015.” alisema Mkwizu.

Mkwizu aliongezea kwa kusema, uanzishwaji wa Ahadi na Uadilifu ni muendelezo wa uundwaji wa vyombo vya kusimamia maadili baada ya ongezeko kubwa la ubadhirifu, utoro sehemu za kazi na kushuka kwa nidhamu katika kipindi cha miaka ya themanini na tisini.
Alivitaja vyombo vingine ambavyo vilianzishwa kusimamia ahadi na uadilifu kuwa ni Sekretariate ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Mkwizu alivitaja vipengele ambavyo mtoa ahadi anatakiwa kuvitamka ni, kuwa mzalendo wa nchi yake na kutii Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, kuhudumia Umma na watumishi wenzake kwa heshima, kutimiza wajibu wa kutoa huduma bora kwa umma, kutoa huduma bora kwa usawa kwa watu wote na kutofanya ubaguzi wa dini, siasa, kabila, udugu, ukanda, jinsia, urafiki au hali ya mtu.

Vipengele vingine ni kutumia rasilimali za Umma kwa manufaa ya Umma, kutotoa siri za Serikali au mteja kwa watu wasiohusika isipokuwa kwa maslahi ya Umma, kufanya kazi kwa nidhamu ya hali ya juu, kutoomba kushawishi, kutoa wala kupokea rushwa na kutotumia madaraka kwa manufaa binafsi ya ndugu, rafiki au jamaa.

Aidha, Mkwizu ametoa wito kwa waajiri wote kuhakikisha kuwa utekelezaji wa Ahadi na Uadilifu unakamilika ifikapo tarehe 31/12/2015 na kuwasilisha Ofisi ya Rais – UTUMISHI kabla ya tarehe 25/02/2016 na utekelezaji wake kuwa kila ifikapo Juni 30 ya kila mwaka.

Fomu za Ahadi ya Uadilifu zinapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Rais – UTUMISHI yenye anwani www.utumishi.go.tz

Au unaweza kupakua moja kwa moja kwa kubofya maneno yafuatayo yaliyokolezewa wino

Jipu langu limekaa pabaya... Meku, nikusaidieje?Rais Magufuli azungumza na Mwakilishi wa Benki ya Dunia


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli akisalimiana na mwakilishi mkazi wa Benki ya dunia Bi. Bella Bird alipomtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli akizungumza na mwakilishi mkazi wa Benki ya dunia Bi. Bella Bird Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimpa pole Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015

Picha za kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM

Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho kikwete akiongozana na Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli , Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahmana Kinana kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dar es salaam leo Desemba 7, 2015

Muhimbili yapatiwa vifaa mbalimbali ikiwemo Digital X-ray machine

Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Flora Lwakatare akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu matumizi ya mashine mpya ya X-ray ya digitali. Dk Lwakatare amesema mashine hiyo ina uwezo wa kupiga picha na kutumwa nje ya nchi kwa ajili ya ushauri wa kitaalamu zaidi. Mashine hiyo haihitaji chumba cha kusafishia picha wala dawa za kusafishia.
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepata mashine mpya na ya kisasa ya Digital X-ray ambayo wataalamu wake hawatalazimika kutumia filamu kusafisha picha kama ilivyozoeleka katika mashine za kawaida.

Mashine hiyo imegharimu Dola 200,000 za Marekani ambazo zimetolewa na serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambayo ina uwezo wa kusafirisha picha nje ya nchi ili kupata ushauri wa kitaalamu.

Akilelezea kuhusu maendeleo ya mashine ya MRI na CT-SCAN , Mkuu wa Idara ya Mionzi wa MNH, Dk Florah Lwakatare amesema matengenezo ya mashine hizo yamekamilika na kwamba hadi sasa wagonjwa 148 wamepimwa kwa kutumia mashine ya MRI , wakati wagonjwa 304 wamepimwa kwa kutumia CT-SCAN .

Katika hatua nyingine Hospitali ya Taifa Muhimbili leo imepokea msaada wa mashuka 200, vyandarua 150, Televisheni nne , Decoder 4 pamoja na Tv Stand 4.

Akikabidhi msaada huo ambao umetolewa na Kampuni ya Mr. Uk Electronics Limited ya Dar essalaam, mwakilishi wa kampuni hiyo John Solomon ametoa wito kwa jamii kuwa na moyo wakujitolea na kushirikiana na serikali katika kuboresha huduma mbalimbali za jamii ikiwemo huduma za afya.

Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Flora Lwakatare akitoa maelezo kuhusu idadi ya wagonjwa waliopata huduma ya kipimo cha CT Scan baada ya mashine hiyo kukamilika.
Pichani ni misaada ya shuka 200, neti 150 na Televisheni nne ikipokelewa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Pichani ni misaada ya shuka 200, neti 150 na Televisheni nne ikipokelewa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Taarifa ya kuvunjwa Bodi ya Bandari na utenguzi wa Katibu Mkuu - UchukuziWaziri Mkuu Mhe. Majaliwa, Kassim Majaliwa akiingia kwenye ukumbi wa mikutano tayari kwa kuzungumza na waandishi wa habari.

Mnamo tarehe 27 Novemba, 2015 nilifanya ziara ya kushitukiza Bandari ya Dar es Salaam ambapo nilifichua mwanya wa ukwepaji kodi kwa makontena 329 yaliyopitishwa bandarini kinyume cha utaratibu.

Mtakumbuka pia tarehe 4 Desemba, 2015 nilirudi tena kufanya ufuatiliaji wa hatua ya udhibiti wa upitishaji wa bidhaa mbalimbali kinyume cha utaratibu.

Ziara yangu ilinipitisha hatua zote za upitishaji mizigo ambazo pia kwa mujibu wa Taarifa ya Ukaguzi wa Ndani wa tarehe 30 Julai 2015 Mamlaka ya Bandari uligundua kuwepo kwa mianya mingi ya ukwepaji kodi ikiwemo na makotena 2387 yaliyopitiahwa kati ya Machi – Septemba 2014 kinyume cha utaratibu, vitendo hivi vinaonyesha kuwa bandari yetu hupitisha makontena mengi bila ya kulipiwa kodi na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa.

Upotevu huo unaenda sambamba na mfumo usiokidhi wa kupokelea malipo (BILLING SYSTEM) ambao unatoa mwanya mkubwa wa kupoteza mapato ya Serikali. Bandari ni eneo muhimu ambako kama panasimamiwa vizuri panaweza kukusanya fedha nyingi na kuchangia Pato la Taifa.

Serikali haitavumilia kuona watu wachache au kikundi chochote kilichojipanga kuhujumu mifumo au kuiibia Serikali kwa namna yoyote ile kwa manufaa ya wachache.

Matokeo ya ziara hizo ni haya yafuatavyo:-
1. Nimeagiza mfumo wa kupokelea malipo ubadilishwe kutoka Billing System na uwekwe mfumo wa e-payment ambao tayari ulianza kuwekwa na uwe umekamilika kufikia tarehe 11 Disemba 2015.
2. Kwa kuwa ripoti iliwataja waliohusika na upitishaji makontena hayo na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa, kuanzia muda huu nawasimamisha kazi wale wote waliohusika kupitisha makontena kinyume na utaratibu.

1. Wasimamizi wa Bandari Kavu (ICD)
(i) Happygod Naftari
(ii) Juma Zaar
(iii) Steven Naftari Mtui
(iv) Titi Ligalwike
(v) Lydia Prosper Kimaro
(vi) Mkango Alli
(vii) John Elisante
(viii) James Kimwomwa – ambaye amehamishiwa Mwanza.

2. Wafuatao ni Viongozi wa sekta zilizotoa ruhusa ya makontena kutoka ndani ya Bandari ambao hawamo kwenye ripoti ila ni wahusika wakuu.

1. Shaban Mngazija – Aliyekuwa Meneja Mapato ambaye kwa sassa amehamishiwa Makao Makuu kitengo cha Fedha.
2. Rajab Mdoe – Aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Mkuu wa Bandari Kavu (ICD) – ambaye amehamishiwa Makao Makuu kwa Naibu Mkurugenzi Co-operate Services.
3. Ibin Masoud – Kaimu Mkurugenzi wa Fedha.
4. Apolonia Mosha – Meneja Bandari Msaidizi – Fedha.
5. James Kimwomwa.

Kutokana na utendaji mbovu wa Mamlaka ya Bandari kwa muda mrefu na kwa kitendo cha kutochukua hatua kwenye vyanzo.

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amevunja Bodi yote ya Bandari na kutengua uteuzi wa wafuatao:-

1. Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari – Prof. Joseph Msambichaka.
2. Mkurugenzi Mkuu wa Bandari – Bw. Awadhi Massawe.

Ndugu Waandishi wa Habari mtakumbuka pia nilifanya ziara pia TRL ambako kwa awali nimegundua matumizi mabaya ya fedha Shilingi Bilioni 13 nje ya utaratibu ambako uchunguzi unakamilishwa.

Mheshimiwa Rais, pia ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Shaban Mwinjaka kuanzia tarehe ya leo na atapangiwa kazi nyingine.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha kwa waandishi wa habari, ripoti Bandari ya Dar es Salaam iliyobaini mianya ya ukwepaji kodi ikiwemo ya Makontena 2,387 yaliyopitishwa kati ya Machi na Septemba mwaka jana. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari, Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.Waziri Mkuu Majaliwa, Kassim Majaliwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu leo wakati alipotoa taarifa ya serikali kuhusu hatua zilizochukuliwa dhidi ya watumishi wa TPA, TRA, Wizara ya Uchukuzi na TRL. kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue.
Waziri Mkuu Majaliwa, Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wa kwa utulivua wakati akitoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari , Kalia ni Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue.

* Atengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu TPA
* Amsimamisha kazi Katibu Mkuu Uchukuzi
* Waziri Mkuu awasimamisha kazi watumishi wengine 13 wa bandari

RAIS Dkt. John Pombe Magufuli amevunja Bodi ya Mamlaka ya Bandari (TPA) na kutengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari, Prof. Joseph Msambichaka pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bandari, Bw. Awadhi Massawe.

Dkt. Magufuli pia ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaban Mwinjaka kuanzia leo (Jumatatu, Desemba 7, 2015), na kwamba atapangiwa kazi nyingine.

Akitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika leo ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hatua hizo zimechukuliwa kufuatia ziara mbili za kushtukiza alizozifanya katika mamlaka ya bandari Novemba 27 na Desemba 3, mwaka huu.

Waziri Mkuu amesema Rais Magufuli amevunja bodi hiyo na kutengua uteuzi wa viongozi hao kutokana na utendaji mbovu wa muda mrefu wa Mamlaka ya Bandari na kwa kitendo cha viongozi hao kutochukua hatua kwenye vyanzo.

Pia alisema Katibu Mkuu amesimamishwa kazi kwa sababu ya kutosimamia kwa makini mashirika mawili ya Bandari na Reli ambayo yako chini ya wizara yake ambako yeye mwenyewe alizuru Shirika la Reli (TRL) Desemba 3, 2015 na kukuta kuna ubadhirifu wa sh. bilioni 16.5/-.

“Tarehe 3 Desemba mwaka huu nilifanya ziara ya kushtukiza pale TRL nikakuta wametumia visivyo sh. bilioni 13.5/- walizopewa na Serikali. Pia nilikuta wamekopa sh. bilioni 3/- kutoka benki ya TIB lakini nazo wamezitumia nje ya utaratibu. Fedha hizi zilikuwa ni za kusaidia kuboresha miradi ya shirika lakini wao wamezitumia visivyo. Uchunguzi bado unaendelea,” alisema Waziri Mkuu.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi kuanzia leo viongozi watano wa sekta zilizotoa ruhusa ya makontena kutoka ndani ya bandari pamoja na watumishi wanane wa bandari kavu ambao walihusika na ukwepaji kwa makontena 2,387.

“Viongozi hawa hawakuwemo kwenye ripoti ya ukaguzi lakini ni wahusika wakuu. Hawa ndiyo waliotoa ruhusa ili makontena yaende kwenye ICDs. Nao ni aliyekuwa Meneja Mapato ambaye kwa sasa amehamishiwa Makao Makuu kitengo cha Fedha, Bw.  Shaban Mngazija; aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Mkuu wa Bandari Kavu (ICD) – ambaye amehamishiwa Makao Makuu kwa Naibu Mkurugenzi Co-operate Services, Bw. Rajab Mdoe; Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Bw. Ibin Masoud; na Meneja Bandari Msaidizi – Fedha, Bi. Apolonia Mosha

Pia amewasimamisha kazi wasimamizi wanane wa Bandari Kavu (ICDs) ambao ni Happygod Naftari, Juma Zaar, Steven Naftari Mtui, Titi Ligalwike, Lydia Prosper Kimaro, Mkango Alli, John Elisante na James Kimwomwa ambaye alihamishiwa Mwanza lakini kuanzia sasa anasimamishwa kazi huko huko aliko.

“Bila wao kuidhinisha hakuna kontena linaweza kutoka au kwenda kokote. Watumishi wote hao wawe chini ya ulinzi na waisaidie polisi kupata taarifa hayo makontena ni ya nani na yana thamani gani,” Waziri Mkuu alisema.

Waziri Mkuu Majaliwa aliwaeleza waandishi wa habari kwamba Desemba 3, mwaka huu aliamua kurudi tena bandarini kufuatilia na kuangalia hatua ya udhibiti wa upitishaji wa bidhaa mbalimbali kinyume cha utaratibu. “Ziara yangu ilinipitisha hatua zote za upitishaji mizigo ambazo pia kwa mujibu wa Taarifa ya Ukaguzi wa Ndani ya tarehe 30 Julai 2015, Mamlaka ya Bandari iligundulika kuwepo kwa mianya mingi ya ukwepaji kodi ikiwemo makotena 2,387 yaliyopitishwa kati ya Machi – Septemba 2014 kinyume cha utaratibu”.

“Vitendo hivi vinaonyesha kuwa bandari yetu hupitisha makontena mengi bila ya kulipiwa kodi na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa. Serikali haitavumilia kuona watu wachache au kikundi chochote kilichojipanga kuhujumu mifumo au kuiibia Serikali kwa namna yoyote ile kwa manufaa ya wachache kwani bandari ni eneo muhimu ambalo likisimamiwa vizuri, linaweza kukusanya fedha nyingi na kuchangia Pato la Taifa,” alisema.

Desemba 3, mwaka huu, Waziri Mkuu alimpa saa tatu tu Kaimu Meneja wa Bandari, Bw. Hebel Mhanga amletee ofisini majina ya watumishi wote waliohusika na ukwepaji kodi huo. Pia alimpa Meneja huyo wiki moja kuhakikisha kuwa mamlaka hiyo inabadilisha mfumo wa utozaji malipo kutoka kwenye billing systemna badala yake kuweka mfumo wa malipo wa kielektroniki (e-payment). Mwisho wa kukamilisha zoezi hilo ni Desemba 11, 2015.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATATU, DESEMBA 7, 2015.