Mwl. Mndeme: Rais Magufuli amelianzisha, na sisi tulitibue

Leo (9/12/2015) siku ya kukumbuka Uhuru wa nchi yetu toka kwa mkoloni wa kingereza, niliamka mapema nikikimbizana ra ratiba na nikiwaza mambo kadhaa. Nilisikitika sana baadaye kugundua kwamba nimewapeleka watoto wangu shule bila kuwaambia kwamba leo ni siku ya uhuru wa nchi yetu. 

Mwasisi wa CHADEMA, Prof. Lipumba, Spika Msekwa watia tiki uamuzi wa Rais Magufuli

Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia mwasisi wa chama hicho, Edwin Mtei, amesema kuwa uamuzi wa Rais Magufuli wa kufuta sherehe za uhuru utakuwa umeleta tija kubwa kwa taifa ambapo miaka mingi taifa limekuwa likichezea mabilioni ya shilingi bila faida kwa taifa.

Mtei alimesema kuwa sherehe hizo zilizokuwa zikifanyika kwa shamrashara ambazo zilikuwa zinagharimu fedha za walipa kodi kwa anasa za kula, kunywa na kulewa huku watanzania wakikosa huduma muhimu.

Aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ameshauri kuwa sherehe hizo zifanyeke mara moja kila baada ya miaka mitano ambapo zisihusishe matumizi mabaya ya fedha za wananchi kama zilivyokuwa za awamu iliyopita kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii.

Naye spika wa kwanza wa Bunge la Tanzania Pius Msekwa amesema kuwa kitendo hicho kinapaswa kuungwa mkono kwa kila ambaye anayeitakia mema Tanzania. Sherehe hizo zimewaunganisha waatanzania wote kwa kufanya jambo moja ambapo sherehe hizo zilikuwa zikifanyika Dar es Salaam pekee kwa gharama kubwa lakini sasa zimekuwa za nchi nzima na zenye maslahi na taifa.

[video, 9 minutes] PLO Lumumba talks Pres. Magufuli with Jeff Koinange


Australian ship seize high purity heroin worth USD $80 million off Tanzania's coast

HMAS Melbourne’s boarding party approaches a suspicious vessel suspected of smuggling narcotics off the coast of Tanzania.
Her Majesty’s Australian Ship (HMAS) Melbourne, working for the Combined Maritime Forces (CMF) in the Middle East, has made another seizure of illegal narcotics off the coast of East Africa.

The latest haul of 151 kilograms of high purity heroin has an estimated value of approximately US$80 million. It is HMAS Melbourne’s second significant drugs seizure during her current deployment, working as part of the Combined Task Force (CTF) 150, under the command of Rear Admiral Moazzam Ilyas from the Pakistan Navy. It brings the total weight of heroin seized by HMAS Melbourne during her two months with CTF 150 to more than 578 kilograms.

Following surveillance, it was suspected that a vessel situated off the coast of Tanzania might be engaged in unlawful activity and so HMAS Melbourne conducted a routine boarding of the dhow. Interviews with the dhow’s crew raised further suspicion that the vessel could be involved in the smuggling of narcotics.

Based on the information gathered, CMF approved a search of the vessel. A thorough search by HMAS Melbourne’s boarding team led to the discovery of heroin.

Members of the Ship’s Company in HMAS Melbourne inspect 151 kilograms of heroin discovered in a vessel off the Tanzanian coast.
Commanding Officer of HMAS Melbourne, Commander Bill Waters, said the smugglers had gone to considerable efforts to conceal the drugs. He said: “On first inspection there were no obvious signs of smuggling. However, our boarding teams are trained to a very high standard and with determination and diligence we were able to locate and extract the narcotics from hidden compartments within the vessel.”

Once the search was complete, the bags were moved to the flight deck of HMAS Melbourne for testing which confirmed the substance was heroin. The seized drugs were subsequently destroyed at sea and in accordance with procedures, the vessel and crew were released and allowed to continue their journey.

Rear Admiral Ilyas acknowledged the relentless efforts of HMAS Melbourne, saying that: “CTF 150 remains determined to combat the flow of funding to international terrorist organizations. This most recent seizure by HMAS Melbourne is CMF’s tenth successful narcotics seizure this year and it comes as the result of the tenacity of the ship’s command team. Locating a drug smuggling dhow in a large maritime area of over two million square miles is a real challenge.”

Commander Waters said the seizure would make a significant impact. He said: “We are not only stopping the drugs from reaching communities, we are also restricting the funding for international terrorism, which comes from the illegal trade of these types of narcotics.”

Members of the Ship’s Company in HMAS Melbourne inspect 151 kilograms of heroin discovered in a vessel off the Tanzanian coast.
News source: combinedmaritimeforces.com

Video za habari kutoka vituo mbalimbali Afrika kuhusu Rais Magufuli kufanya usafi Desemba 9

[video] ITV ilivyokwenda mguu kwa mguu na Rais Magufuli katika usafi


Kalapina amtungia wimbo huu Rais Magufuli


Matokeo ya usaili TBS uliofanyika Novemba 19 hadi 27


Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linapenda kuwatangazia waombaji kazi waliofanya usaili tarehe 19 hadi 27 Novemba 2015 kuwa wafuatao wamechaguliwa. Hivyo wanaombwa kufika TBS, Ubungo DSM siku ya Jumatano tarehe 16.12.2015 saa 3 asubuhi kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa ajira.

Tafadhali bonyeza linki ifuatayo ili uweze kuona orodha ya waliochaguliwa:

TANGAZO LA TOVUTI-MATOKEO YA USAILI DESEMBA_2015.pdf

It appears you don't have a PDF plugin for this browser. You can see the screen-shot photos of the document below or click here to download the PDF file.

Katuni za Siku ya Uhuru 2015... Kamata hii kitu.Kipande cha gazeti cha Desemba 9, 1971 ilivyoadhimishwa Siku ya Uhuru


Picha kutoka kwenye blogu ya Chambi Chchage - Udadisi

Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wafanya usafi


Balozi Liberata Mulamula, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa katika zoezi la usafi kwenye uzio wa nyumba yake maeneo ya Mbezi jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9 Disemba 2015
Nje ya uzio wa nyumba ya Balozi Simba Yahya, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa baada ya kufanyiwa usafi kwenye maeneo ya Mbweni jijini Dar es salaam katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9 Desemba 2015.

Balozi Mohammed Juma Maharage, Mkuu wa Itifaki na Mkurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akiwa kwenye zoezi la usafi kwenye gari maalum la "Rapid Deployment Unit" huko nyumbani kwake maeneo ya Makongo Juu, jijini Dar es salaam.
Mhe. Juma Khalfan Mpango, Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Kiongozi wa Mabalozi wa wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania naye akiwa kwenye zoezi la usafi nje ya ofisi za ubalozi maeneo ya Upanga jijini Dar es salaam. Usafi huo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru kufuatia maagizo ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli ambapo kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni Uhuru na Kazi. 

Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa naye akisafisha maeneo ya pembezoni mwa bararabara kuu inayopita nyumbani kwake, Migombani maeneo ya Mikochini jijini Dar es Salaam. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Mindi Kasiga akisafisha ngazi za jengo la makazi yake Garden Avenue, jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru tarehe 9 Disemba 2015. Bulaya aongoza wananchi kufanya usafi Bunda


Mbunge wa Bunda Mjini kupitia CHADEMA, Esther Bulaya ameshiriki zoezi la kufanya usafi wa wananchi wa jimbo hilo mapema asubuhi kuanzia Nyamakokoto yaliko machinjio ya kitoweo na baadaye kufanya usafi tena eneo tofauti na jimbo hiloBulaya akisafisha eneo la machijio
Bulaya akishiriki kufyeka nyasi

Wananchi walishiriki

Ndani ya soko la Mjini Bunda akiangalia eneo la dampo la soko likiwa limetolewa uchafu wote

Akikagua usafi sokoni

Ofisini baada ya kazi

Picha: Shommi Binda

Mkuku wa Majeshi afanya usafi


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange (kulia), Mkuu wa Brigedi ya Chui Brigedia Jenerali Sharif Othman (kushoto) pamoja na Maafisa na Askari wakishiriki zoezi la usafi katika kambi ya Lugalo, jijini Dar es Salaami wakati wa kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru kama alivyoagiza Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli

Zaidi ya wafungwa 2,000 wanufaika na masamaha wa Rais siku ya Uhuru 2015

Katika kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru wa Nchi yetu tarehe 9 Desemba, 2015 Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya ya Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa msamaha kwa wafungwa wafuatao:-

i) Wafungwa wote wamepunguziwa moja ya sita(1/6) ya vifungo vyao zaidi ya punguzo la kawaida linalotolewa chini ya kifungu 49(1) cha Sheria ya Magereza Sura ya 58 isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika Ibara ya 2(i-xix);

ii) Wafungwa wagonjwa wenye magonjwa kama UKIMWI, KIFUA KIKUU(TB) na SARATANI(CANCER) ambao wako kwenye "terminal stage". Wafungwa ambao wamethibitishwa na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya;

iii) Wafungwa wa wazee wenye umri wa miaka (70) au zaidi ambao umri huo umethibitishwa na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya;

iv) Wafungwa wa kike walioingia na mimba gerezani, pamoja na wale walioingia na watoto wanaonyonyesha na wasionyonya;

v) Wafungwa wenye ulemavu wa mwili na akili(Physical disability and mental disability) ambao ulemavu huo umethibitishwa na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.

Aidha, Msamaha huo wa Mheshimiwa Rais hautawahusu wafungwa wafuatao:-i) Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa;

ii) Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa na adhabu hiyo kubadilishwa kuwa kifungo cha maisha au kifungo gerezani.

iii)Wafungwa waliohukumiwa kifungo cha maisha gerezani;

iv) Wafungwa waliohukumiwa kifungo kwa makosa ya kujihusisha na usafirishaji na matumizi ya madawa ya kulevya kama vile cocaine, heroin, bhang;

v) Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kujihusisha na uombaji, upokeaji au utoaji wa rushwa;

vi) Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya unyanga'anyi na unyang'anyi wa kutumia silaha au kujaribu kutenda makosa hayo;

vii) Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kupatikana na silaha, risasi au milipuko isivyo halali;

viii) Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya shambulio la aibu, kunajisi, kubaka na kulawiti, au kujaribu kutenda makosa hayo;

ix) Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo kwa kosa la kuwapa mimba wanafunzi wa shule za msingi na Shule za Sekondari na ambao walitenda kosa hilo wakiwa na umri wa miaka kumi na nane(18) na kuendelea;

x) wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya wizi wa magari na pikipiki au kujaribu kutenda makosa hayo;

xi) Wafungwa wanaotumikia kifungo chini ya Sheria ya Bodi ya Parole(Act. No. 25/1994) na Sheria ya Huduma kwa Jamii(Act. No. 6/2002);

xii) Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo kwa makosa ya kutumia vibaya madaraka yao;

xiii) Wafungwa waliowahi kupunguziwa kifungo na Msamaha wa Mheshimiwa Rais na bado wangali wanaendelea ksehemu ya kifungo kilichobaki;

xiv) Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kwa kosa la kuzuia watoto kupata masomo;

xv) Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kwa kosa la utekaji wa watoto, kupoka ma kufanya biashara ya binadamu (Human Trafficking);

xvi) Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kwa kosa la kukutwa na viungo vya binadamu pamoja na vitendo vya mashambulizi na ukatili dhidi ya watu wenye ualbino;
xvii) Wafungwa wanaotumikia vifungo kwa makosa ya kujihusisha na usafirishaji wa nyara za Serikali na ujangili(Poachers);

xviii) Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya wizi/ubadhirifu wa fedha za Serikali;
xix) Wafungwa wanaotumikia vifungo kwa makosa ya kutoroka au kujaribu kutoroka wakiwa chini ya ulinzi halali.

Wafungwa wapatao 2,336 watanufaika na msamaha huu baada ya kupunguziwa 1/6 ya vifungo vyao ambapo 117 wataachiliwa huru na wafungwa 2,219 watanufaika na kubaki gerezani wakitumikia sehemu ya kifungo kilichobaki. Ni mategemeo ya Serikali kwamba watakaochiliwa huru watarejea tena katika jamii kushirikiana na wenzao katika ujenzi wa Taifa na kwamba watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani.

Imetolewa na kusainiwa na;
JOHN C. MINJA
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA
9 Desemba, 2015

Mtoa agizo naye alitii agizo lake: Rais Magufuli afanya usafiRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakielekea eneo la ufukwe wa Ferry kufanya usafi katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru tarehe 9 Desemba.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizoa taka katika eneo la ufukwe wa ferry jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizoa taka katika eneo la ufukwe wa ferry jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizoa taka katika eneo la ufukwe wa ferry jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizoa taka katika eneo la ufukwe wa ferry jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka taka ndani ya ndoo ya Taka katika eneo la Magogoni jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka taka ndani ya ndoo ya Taka katika eneo la Magogoni jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kulia akiwa pamoja na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakifanya usafi katika eneo la ufukwe wa ferry jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kulia akiwa pamoja na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakifanya usafi katika eneo la ufukwe wa ferry jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka taka taka kwenye dastibin wakati akifanya zoezi la kufanya usafi katika eneo la ufukwe wa Ferry jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiokota takataka katika eneo la Ferry katika zoezi la kufanya usafi nchi nzima.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wavuvi wa ferry huku akiwa ndani ya Mtumbwi. Rais Magufuli alizikiza kero zao na kuahidi kuzitatua ndani ya muda mfupi.

Rais Magufuli akifanya usafi pamoja na wavuvi wa eneo la ferry waliojitokeza kuungamkono zoezi hilo. Rais Magufuli amewataka Watanzania kuwa na Utamaduni wa kufanya Usafi kila wakati ili kuweka mazingira katika hali nzuri.

Picha: Ikulu

CCM Iringa wafanya usafi

Katibu wa CCM Wilaya ya Iringa Mjini Bw Elisha Mwampashi kushoto akiongoza wana CCM Iringa Mjini kufanya usafi leo kata ya Kihesa
Na Francis Godwin

KATIBU wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa mjini Bw Elisha Mwampashi amewaongoza wanachama wa CCM kufanya usafi katika eneo la Semtema kata ya Kihesa inayoongozwa na diwani wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) huku akiwataka wana CCM Iringa mjini kujiandaa kufika mahakamani kufuatilia mwenendo wa kasi ya kupinga matokeo ya ubunge na udiwani katika jimbo la Iringa mjini.

Akizungumza na wanachama hao wa CCM baada ya kufanya usafi na kupanda mti wa kumbukumbu katika Kituo cha Afya Ngome katibu huyo wa CCM wilaya ya Iringa mjini Bw Mwampashi alisema kuwa zoezi hilo ambalo ni agizo la Rais Dr John Magufuli kwao litaendelea kuwa endelevu ila wao wameweza kuitumia siku hiyo ya leo kama sehemu ya kuonyesha uhai wa chama na msimamo wao wa kuendelea kupinga matokeo ya ubunge na udiwani katika jimbo la Iringa mjini.

Akielezea kuhusiana na kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo Bw Mwampashi alisema CCM wilaya ya Iringa mjini imefungua kesi hizo na kupinga matokeo katika kata zote 14 ambazo Chadema walitangazwa kushinda pamoja na kupinga matokeo yaliyompa ushindi mgombea wa Chadema jimbo  hilo Mchungaji Peter Msigwa na kudai kuwa kesi hizo zinaanzwa kusikilizwa Desemba 14 mwaka huu hivyo kuwataka wana CCM kuendelea kufuatilia mwenendo wa kesi hizo na kuwa wavumilivu wakati kesi hizo zikiendelea.

Bw Mwampashi alisema kuwa ni vizuri kwa wana CCM kuendelea kufuatilia kesi hizo pasipo kujali kama ni kesi ya kata yake ama lah na kuwa kila siku kutakuwa na kesi zisizopungua tatu ambazo zitasikilizwa mahakamani hapo.

Alisema kuwa CCM imejiandaa kuwasilisha ushahidi mahakamni na kuwataka wale wote ambao ni mashahidi wa kesi hizo kujiandaa kwa kuwasilisha ushahidi wao mahakamani huku akidai kuwa mbali ya CCM kupinga matokeo ya kata 14 Mahakamani pia kwa upande wa Chadema wao wamefungua kesi mahakamani kwenye kata mbili ya Mlandege na Miyomboni Kitanzini kupinga ushindi wa CCM.

Hata hivyo alisema pamoja na kuwa kesi ya kata ya Kihesa itasikilizwa tofauti na kesi nyingine kuwa  kesi ya kupinga matokeo ya udiwani kata ya Kihesa itasikilizwa Desemba 15 mwaka huu .

Kuhusuana na zoezi hilo la usafi lililofanyika kata ya Kihesa alisema kuwa mbali ya kufanya usafi huo katika ya Kihesa CCM walitawanyika katika mitaa mbali mbali na kata mbali mbali ya jimbo la Iringa mjini ili kumuunga mkono Rais katika zoezi hilo la usafi na kutoa wito kwa wana CCM kuendelea kuwa mfano katika mitaa yao kwa kufanya usafi badala ya kusubiri siku maalum ya usafi

Kwa upande wake makada wa CCM Francis Mkokwa na aliyekuwa mgombea udiwani kata ya Kihesa Bw Kenani KIhongosi wakizungumzia siku hiyo ya Uhuru kuadhimishwa kwa kufanya usafi walisema ni maamuzi mazuri yaliyofanywa na Rais Dr Magufuli na kuwa inawezekana kwa serikali kupunguza mnatumizi yasiyo ya lazima ya sherehe kwa kugeuza maadhimisho hayo kufanya kazi za kiuchumi ama usafi kama hivyo.

Walisema kuwa anachokifanya Rais Dr Magufuli ni kuirejesha nchi katika misingi ya azimio la Arusha na wakati wa utawala wa baba wa Taifa ambayo aliitumia siku ya Uhuru kwa watu kufanya kazi na sio kufanya sherehe.

Bw Mkokwa alisema kuwa kwa nchi ilipofikia hapa ndani ya mwezi mmoja wa serikali ya CCM chini ya uongozi mzuri wa Dr Magufuli kila mmoja amekuwa shahidi kwa kuona kazi kubwa iliyofanyika na kuwa kuna haja ya watanzania kuepuka itikadi za vyama na kumsaidia Rais kuiongoza nchi hii.Mwampashi akishirikiana na wana CCM kupanda mti Kituo cha afya NgomeMwampashi akipanda mtuZoezi la upandaji mti Kituo cha afya Ngome leo likifanywa na wana CCMKatibu wa CCM Iringa Mjini Bw Mwampashi kushoto akiwa na Makada wa katikati mwenyekiti wa UVCCM Bw Kaunda na aliyekuwa Mgombea Udiwani kata ya Kihesa Bw Kenan KihongosiWatumishi wa Manispaa ya Iringa wakitoka kufanya usafi Soko kuu leoVijana wa kwaya ya vijana kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania ( KKKT) Usharika wa kanisa kuu wakifanya usafi kanisani hapoVijana KKKT wakiwa katika usafiKaunda kushoto na Mwampashi wakifanya usafi leo