Gazeti larejea kile kisa cha mtego wa panya kwa kufananisha mgombea Urais mmoja Marekani

Na kisa hiki sijaona sababu ya kukifasiri kutoka kwenye lugha ya Kiingereza, ila nimekumbuka Mwenyekiti wa Kijiji cha Mjengwa aliwahi kuisimulia hadithi ya kisa hicho kwa ufasaha, nainukuu ilivyo...

Ndugu zangu,

Mengine tuandikayo tulishayaandika zamani. Tunayarudia maana yanayotokea sasa ishara zake tulishaziona, isipokuwa, tu mahodari sana wa kupuuzia.

Nimepata kuandika ( Raia Mwema) juu ya nilichokiona Jumapili moja nilipokuwa nikipita mitaa ya Kariakoo. Pale kona ya Mtaa wa Nyamwezi na Narung’ombe nikamkuta kijana na mkokoteni wake. Alikuwa akiuza filamu na CD za kidini.
Kijana yule alikuwa akionyesha pia mkanda wa video. Mzungumzaji kwenye mkanda huo alikuwa akihubiri chuki. Ni kuanzia nilipoanza kumsikiliza hadi nilipoondoka mahali hapo.

Na watu, hususan vijana, waliuzunguka mkokoteni ule kusikiliza chuki ile ya kidini iliyokuwa ikipandikizwa. Ndipo tulipofikia. Kwamba mijini si tu kuna wanaouza sumu za panya na mende. Bali siku hizi kuna wanaosambaza bure, ’sumu za kijamii.’

Vyombo vinavyohusika vimebaki vikiwaangalia wenye kupandikiza mbegu hizi za chuki.Kosa kubwa tulifanyalo, ni kudhani yanayotokea Kariakoo au Unguja hayatuhusu wa Kinondoni, Iringa au Mwanza.

Nimepata kusimulia kisa cha mtego wa panya uliosababisha madhara hata kwa wasio panya.

Panya kwenye nyumba aliubaini mtego wa panya uliowekwa na mwenye nyumba uvunguni mwa kitanda. Panya yule akamwendea jogoo wa mwenye nyumba. Akamwambia: “Ewe jogoo, kuna mtego umewekwa uvunguni mwa kitanda. Tusaidiane namna ya kuutegua kabla haujatudhuru wote."

Jogoo akajibu: "Ondoka zako, mie mtego wa panya unanihusu nini wakati sina kawaida ya kufika uvunguni mwa kitanda?" Panya yule akaenda hadi kwa mbuzi wa mwenye nyumba. Akamwambia: "Ewe mbuzi mwema, unajua kuna mtego wa panya uvunguni mwa kitanda cha mwenye nyumba. Tusaidiane mawazo ya kuutegua kabla haujatudhuru sote."

Mbuzi akajibu: "Hivi tangu lini ukaniona nikiingia chumbani kwa mwenye nyumba? Mtego huo wa panya haunihusu mie mbuzi." Panya akaenda hadi kwa ng'ombe wa mwenye nyumba. Akamwambia: "Ewe ng'ombe wa Bwana, kuna mtego wa panya umewekwa uvunguni mwa kitanda. Tusaidiane mawazo namna ya kuutegua kabla haujatuletea madhara."

Ng'ombe akajibu akionyesha mshangao! "Sijapata kusikia jambo la ajabu kama hilo. Yaani, mie ng'ombe nidhurike na mtego wa panya ulio uvunguni mwa kitanda! Hilo halinihusu."

Basi, ikatokea siku moja, nyoka akaingia chumbani kwa mwenye nyumba. Katika kutambaa kwake uvunguni mwa kitanda, mkia wa nyoka ukanasa mtegoni. Kishindo kilisikika. Mwenye nyumba alikwenda kwa furaha akiamini hatimaye panya aliyekuwa akimsumbua sasa amenaswa. Hapana, ni nyoka aliyenaswa mkia. Na ni mwenye hasira pia. Akamng'ata mguu. Sumu kali akamwachia. Mwenye nyumba akafa.

Jirani wakafika msibani. Siku ya kwanza watu walikuwa wachache. Wakahitaji kitoweo. Akakamatwa jogoo wa mwenye nyumba. Jogoo akachinjwa. Siku ya pili watu wakaongezeka. Kilihitajika kitoweo pia. Akakamatwa mbuzi wa mwenye nyumba. Mbuzi akachinjwa. Na siku ya maziko watu wakawa wengi zaidi. Akakamatwa ng'ombe wa mwenye nyumba. Naye akachinjwa!

Ni jogoo, mbuzi na ng'ombe wa mwenye nyumba walioamini kuwa madhara ya mtego ule wa panya yasingewahusu wao. Walikosea. Panya alikuwa sahihi, na wala mtego haukumdhuru panya! Kuna cha kujifunza kutoka kwenye kisa hiki. Nahitimisha.

Maggid Mjengwa,
0788 111 765
mjengwablog.co.tz

Kauli za baadhi ya Mawaziri wateule wa baraza la Rais Magufuli


SAA chache baada ya kutangazwa kwa Baraza jipya la Mawaziri na Rais Dk. John Magufuli, MTANZANIA iliwatafuta baadhi ya mawaziri na kuzungumza nao kuhusu uteuzi wao.

BALOZI MAHIGA

Kwa upande wake, Waziri mteule wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga, alisema: “Siwezi kuongea jambo lolote kwa sababu hata rais wangu hatujazungumza…nawaomba muwe na subira.

“Nikimaliza kuongea na rais, hata ninyi watu wa media (vyombo vya habari), nitakuwa na jambo la kuwaambia, nakushukuru ndugu mwandishi,” alisema Balozi Mahiga.

KITWANGA

Waziri mteule wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, alisema amefurahishwa na uteuzi huo, ambapo aliahidi kuhakikisha anasimamia ulinzi wa wananchi na mali zao.

“Sipendi kuzungumza sana kuhusu namna ambavyo nitatekeleza majukumu yangu kama Waziri wa Mambo ya Ndani, ila napenda kutoa salamu kwa wahalifu wote kuwa tutapambana nao kwa nguvu zote,” alisema.

ANGELINA MABULA

Naibu Waziri mteule wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, alisema amejipanga kukabiliana na changamoto zilizopo katika wizara hiyo.

Akizungumza kwa njia ya simu, Mabula ambaye ni mbunge wa Ilemela, alisema wizara hiyo ina changamoto nyingi.

Alisema kuwa amepokea kwa furaha uteuzi huo na kumpongeza Rais Magufuli kutokana na kuwa na imani kubwa naye na kuahidi kuwatumikia Watanzania kwa nguvu zake zote.

“Nafahamu ugumu wa Wizara ya Ardhi, kuna kero ambazo zimekuwa zinawakabili Watanzania hasa masikini, kuna migogoro ya wakulima na wafugaji, nitahakikisha namsaidia rais kukabiliana na changamoto hizi kwa nguvu zote.

“Nimejiandaa kutumika kwa ajili ya Watanzania, nina uzoefu wa kutosha, hivyo natoa rai kwa watumishi wa wizara hiyo kutoa ushirikiano wao kwetu na kamwe hatutasita kuchukua hatua kwa wale ambao watashindwa kwenda na kasi ya Serikali ya awamu ya tano,” alisema.

MANYANYA

Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya, alisema alipatwa na mshangao kusikia ameteuliwa kushika wadhifa huo.

“Nakiri wazi kuwa nimepatwa na mshangao mkubwa, nilikuwa sifikiri hata siku moja kwamba nitateuliwa kushika nafasi kama hii.

“Nawashukuru waliokaa chini na kuona nafaa, kwa sababu taifa hili lina watu wengi mno jamani. Namshukuru Mungu, wananchi wa jimbo langu, mkuu wa wilaya na viongozi wa halmashauri yangu (Nyasa) waliosimamia uchaguzi nikawa mbunge.

“Kumbe walikuwa na maono ya mbali… eeh Mungu wangu asante na awabariki wote,” alisema.

Alipoulizwa kama anaweza kwenda na kaulimbiu ya Rais Magufuli ya ‘Hapa Kazi Tu’, Mhandisi Manyanya alisema yuko tayari kuwatumikia Watanzania.

“Nipo tayari kwenda na kasi hii, unajua kaulimbiu hii inatuhamasisha mno kuchapa kazi, inatupa nguvu ya kuondokana na utendaji kazi wa mazoea, huu ndiyo moto wa kutimiza majukumu yangu.

UMMY MWALIMU

Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema amepokea uteuzi huo kwa heshima kubwa na unyenyekevu.

“Nimepokea uteuzi uliofanywa na Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa heshima na unyenyekevu mkubwa. Nipo tayari kukabiliana na changamoto zinazoambatana na kazi hii ya Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto,” alisema Ummy.

MAVUNDE

Naibu Waziri mteule wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde, alisema anahisi ana deni kubwa kwa taifa kutokana na uteuzi wake.

“Najisikia deni kubwa la kuwatetea wananchi kwa uadilifu na uaminifu mkubwa ili kumsadia Rais Magufuli. Nitawatumikia wananchi na Watanzania kwa uzalendo uliotukuka hasa kuhakikisha Tanzania inapiga hatua kimaendeleo,” alisema.

SIMBACHAWANE

Akizungumzia uteuzi wake, Waziri mteule wa TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene, alisema hana maoni yoyote ila kwake ni kazi tu.

“Maoni yangu ni hapa kazi tu, sina maoni yoyote zaidi ya hayo,” alisema Simbachawene.

ASHATU

Naibu Waziri mteule wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji, alisema hawezi kuzungumzia kitu ambacho hakijui.

“Nipo kijijini sana na ‘network’ siyo nzuri sana, siwezi kuongea lolote, naweza nikawa najibu vitu ambavyo sivielewi, nitafute baadae,” alisema Dk. Kijaji.RAIS wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, ametangaza Baraza la Mawaziri na kumteua Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo.

Awali kabla ya uteuzi wa jana wa Serikali ya Awamu ya Tano, wizara hiyo ilikuwa chini ya mbunge wa kuteuliwa Dk. Fenella Mukangara na Naibu Waziri wake Juma Nkamia ambaye ni Mbunge wa Chemba.

Akitangaza baraza hilo jana jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema kutakuwa na jumla ya mawaziri 19 ndani ya wizara 18 ambapo baadhi hazitakuwa na Manaibu Waziri lengo likiwa ni kuwa na baraza dogo ili kupunguza gharama.

Nape ambaye pia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kabla ya kuteuliwa kuwa waziri aliwahi kufanya mahojiano na MTANZANIA na kuwatoa hofu Watanzania wanaopenda michezo akiwataka wawe na imani na Rais wa Awamu ya Tano, akiamini ataweza kuinua michezo nchini tofauti na wanavyofikiria.

“Nawapa mfano, Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, hakuwahi kuwa mwanamichezo wala kuwahi kukanyaga uwanjani, ila ametuachia alama ya uwanja,” alisema.

Nape pia katika mazungumzo hayo na gazeti hili, hakusita kuzungumzia matokeo mabovu ya soka hivi karibuni ambapo alisema hayo yamesababishwa na kutowekeza katika soka badala yake tunatengeneza timu kiujanja ujanja.

“Tukitaka matokeo makubwa inatubidi tufanye uwekezaji ili tufanye vizuri, tusifanye vitu kirahisi Serikali lazima iwekeze lakini badala ya kuwekeza tunaanzisha vitu kirahisi Azam B, Yanga B na Simba B, ndio maana tunakutana na wachezaji wenye umri mkubwa lazima tukubali kuwekeza,” alisema Nape.

Alieleza kuwa kuna wakati yalifanyika makosa makubwa ambapo Waziri wa Elimu, Joseph Mungai, alifuta michezo shuleni jambo ambalo lilichangia kuua michezo kabisa lakini sasa michezo inatakiwa kurudi.

Alisema ili kufikia mafanikio, zitungwe sheria zitakazowabana watu, sheria zitakazoongeza maslahi ya wachezaji.

Nape pia alitaka zitungwe sheria za michezo ambazo zitasaidia kuwabana wanamichezo ambao wanatumia vilevi kama pombe na dawa za kulevya.

Hatua ya kuteuliwa kwake kuwa Waziri wa Michezo kunaweza kusaidia kupunguza machungu ya Watanzania waliokata tamaa kutokana na kufanya vibaya katika michuano mbalimbali ya kimataifa na kutekeleza hayo aliyoyaongea wakati wa mahojiano alipotembelea ofisi za New Habari (2006) Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Rai, The African, Bingwa na Dimba.

Maoni ya Watanzania kuhusu Baraza la Mawaziri la Rais Magufuli

Baada ya Profesa Sospeter Muhongo kutangazwa kuwemo katika Baraza la Mawaziri la Serikali ya awamu ya Tano lililotangazwa na Rais Dk. John P Magufuli, kumezuka maneno mengi katika mitandao na vijiwe vya siasa kukosoa uteuzi huo kwa kile kinachotajwa kuwa ni tuhuma zake za kuhusika katika sakata la Escrow ambapo alilazimika kujiuzuru.
Aidha, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, aliyekuwa anagombea urais kwa tiketi ya CHADEMA kwa kuungwa mkono na UKAWA alijiuzuru mwaka 2008 baada ya kutuhumiwa kuhusika katika sakata la Richmond.
Je, uwezo wa kulitumikia Taifa hili wa wawili hawa unapimwa kwa kipimo kipi? .... ni ufisadi .... ni kuwajibika kisiasa .... au ........
via WhatsApp


Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu na aliyekuwa mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba wamepinga uteuzi wa Profesa Sospeter Muhongo kuwa Waziri wa Nishati na Madini wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Kwa nyakati tofauti, waliliambia gazeti hili jana kuwa msomi huyo hakupaswa kuteuliwa na Rais John Magufuli kushika wadhifa huo kutokana na kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow iliyomkuta kipindi alichokuwa akiongoza wizara hiyo.

Pamoja na kupongeza uteuzi wa baraza hilo, walieleza kushtushwa na uteuzi huo wa Prof Muhongo kuingia katika baraza lake la kwanza la Rais Magufuli.

Lissu, ambaye pia ni mwanasheria wa Chadema alisema baraza hilo halina jipya kwani asilimia kubwa ni sura ni zilezile zilizokuwa kwenye Serikali iliyopita.

Alisema Watanzania wasitarajie maendeleo katika baraza hilo kwa sababu miongoni mwa wateule hao walikumbwa na kashfa tofauti.

“Juzi, Rais Magufuli aliifumua uongozi wa Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kashfa, miongoni mwa waziri waliokuwa wakisimamia sekta hiyo ni Dk Harrison Mwakyembe, eti leo (jana), amemrudisha kundini?, “ alihoji.

Aliongeza kuwa kwa mtaji huo kuna haja ya kuanzia harakati alizoanzisha aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila kuhusu suala hilo.

“Baraza hili ni kama mvinyo ule ule na chupa ile ile kwa sababu karibu mawaziri wote kamili walikuwa wa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete,” alisema Lissu.

Kwa upande wake, Prof Lipumba alisema ameshangazwa na kitendo cha Rais Magufuli kumrejesha profesa mwenzake katika baraza lake hilo na wizara ile aliyopata kashfa ya Escrow iliyomsababisha ajiuzulu.

“Kwa kitendo kama hiki, Rais Magufuli amejiwekea dosari kutokana uteuzi huu. Maana yake ni kuwa katika kashfa ile Prof Muhongo hakuwa na hatia.

Hata hivyo, Prof Lipumba alisema Rais Magufuli ametimiza ahadi yake ya kuunda baraza dogo la mawaziri ili kubana matumizi ya Serikali.

Naye Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo, Anna Mghwira alisema mchanganyiko huo siyo wa zamani wala mpya katika baraza hilo jipya la mawaziri.

Alisema wote walioteuliwa wanaendana na taswira ya kiongozi wao, hivyo ni mapema kubashiri badala yake Watanzania wasubiri kuona utendaji wao.

“Tangu aingie madarakani Rais (Magufuli) ameonyesha utendaji wake, kikubwa kwa walioteuliwa kuendana na kasi hii ya kiongozi wao,” alisema Mghwira aliyekuwa mgombea urais katika uchaguzi uliopita.

Aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha TLP, Macmillan Lyimo alisema kwa sasa hawezi kuzungumza chochote badala yake anasubiri Rais Magufuli amalizie kuteua mawaziri wa wizara zilizobaki.

“Tumwache amalize wizara. Huwezi kujua utamu kauacha kwenye wizara hizo zilizobaki,” alisema Lyimo.

Gavana wa kwanza wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Edwin Mtei alimtaka Rais Magufuli kukamilisha mapema uteuzi wa mawaziri kwa wizara zilizosalia.

Mtei ambaye ni mwasisi wa Chadema alimpongeza Rais Magufuli kwa utendaji wake wa kazi na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisema ana imani mawaziri aliowateua watafanya kazi nzuri ya kupambana na ufisadi.

“Rais ameanza vizuri sasa na hao mawaziri lazima wamsaidie kufanya kazi ya kupambana na wala rushwa, mafisadi na wezi, “alisema.

Hata hivyo, alisema ni muhimu Rais akamaliza mapema uteuzi wa mawaziri wote ili kuepuka watendaji wengine wa Serikali, hasa makatibu wakuu kumhujumu.

“Sijamuelewa anaposema bado hajapata mawaziri wengine, Tanzania kuna watu milioni 45, haiwezekani kukosa nafasi za watu wachache, ila ni kweli lazima wawe waandilifu,” alisema Mtei.

via MWANANCHI


BAADHI ya wachambuzi na wanasiasa wamempongeza Rais, Dk. John Magufuli kwa kuteua baraza la mawaziri kwa kuwa na idadi ndogo, huku wakitoa kasoro mbalimbali.

Akizungumza na MTANZANIA baada ya kutangazwa kwa baraza hilo jana, Mtaalamu wa Uchumi ambaye pia alipata kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alikosoa uteuzi wa baraza hilo, ingawa alipongeza kuwapo kwa idadi ndogo ya mawaziri.

Profesa Lipumba alishangaa kitendo cha Rais Magufuli kumrudisha Profesa Sospeter Muhongo katika Wizara ya Nishati na Madini, wakati aliwahi kujiuzulu kwa kashfa ya Escrow.

“Watanzania hawajasahau kashfa ya Tegeta Escrow ambayo mawaziri na vigogo mbalimbali wa serikali walijiuzulu. Sasa nimeshangazwa kuona tena Profesa Muhongo akirudishwa alijiuzulu kwa tuhuma hizo za Escrow,”alisema Profesa Lipumba.

Mtaalamu huyo wa uchumi alisema ni wazi kwamba ile dhamira ya Rais Magufuli ya kupambana na rushwa na ufisadi itakuwa imepata doa kubwa kwa kumrudisha mtu ambaye alijiuzulu kwa kashfa ya ufisadi.

“Hili linafedhehesha sana kwa sababu suala la Profesa Muhongo kutuhumiwa kwa Escrow halina ubishi maana katika maazimio ya Bunge mawaziri waliotuhumiwa walitakiwa kujiuzulu na wakafanya hivyo sasa iweje leo Rais Magufuli aturudishie…inaleta picha gani?,” alihoji.

Alisema kwa upande wa uwakilishi wa Zanzibar, kwa kawaida Wizara ya Mambo ya Nje, waziri wake anatokea bara na naibu Zanzibar lakini safari hii wote wametokea Tanzania Bara.

LISSU

Kwa upande wake Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu alieleza kushangazwa kwa kitendo cha Rais Magufuli kurudisha majina ya mawaziri mzigo waliokuwa katika baraza lililopita la Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete.

“Nafikiri ameteua mawaziri kwa njia ya kushangaza sana, ni mwendelezo ule ule wa Kikwete. Mawaziri 13 kati ya 15 aliowateua ni wale wa JK, sasa yule rais wa hapa kazi tututamzamaje. Katika hili baraza lake sura mpya ni wawili tu sasa mtu kama Nape Nnauye huyu ana dili gani?

“Jingine lililonishangaza ni uteuzi wa Profesa Muhongo tulimfukuza bungeni kwa sababu ya kashfa ya Escrow, hii maana yake ni kwamba hajali Bunge lilisema nini na anawatukana wabunge na Watanzania…unamletaje mtu ambaye alihusika na kashfa hii?,” alihoji Lissu.

Lissu alisema kutokana na hilo, Bunge lijalo wataendeleza mjadala huo wa Escrow kwa kuwa hata mwaka haujaisha tangu Profesa Muhongo alipojiuzulu kwa kashfa hiyo kubwa.

Alisema tangu utawala wa Mwalimu Julius Nyerere hadi uongozi wa awamu ya nne, haijapata kutokea rais akakosa mtu wa kumteua kwenye baraza.

“Anatuambia ameshindwa kumpata mtu wa wizara fulani…Magufuli anatuambia kwamba wabunge wote wa CCM hajaona mtu anayefaa kuwa katika wizara ya ujenzi na maliasili,”alisema.

PROFESA MPANGALA

Kwa upande wake Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ruaha (RUCO), Profesa Gaudence Mpangala alisema Rais Magufuli ametimiza ahadi yake ya kuwa na baraza dogo kwa kuchanganya baadhi ya wizara pamoja ili kupunguza gharama za uendeshaji wa Serikali.

“Ametimiza ahadi yake kwa kuwa na wizara 18 ambazo ni chache ukilinganisha na serikali iliyopita, lakini ameonesha umakini katika uteuzi wa mawaziri wake kwani ametumia muda kuwatathimini na hadi sasa wizara nyeti kama vile Uchukuzi, Ujenzi na Miundombinu, Fedha na Mipango, Elimu, Sayansi na Ufundi na Wizara ya Utalii hajapata mawaziri, bado anaendelea kuwatafuta watakaomfaa,” alisema Mpangala.

PROFESA KITILA

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Kitila Mkumbo, alisema yalikuwa matarajio ya wengi kwamba ataunda baraza dogo, lakini ameunda baraza la kawaida.

“Katika historia ya Taifa hili ni Rais Jakaya Kikwete tu ndiye alikuwa na baraza kubwa la mawaziri, lakini kabla yake yalikuwa mabaraza madogo na ndicho alichofanya Rais Magufuli,” alisema Mkumbo nakuongeza.

“Kwa kadiri nilivyosikia majina ya mawaziri ni baraza la kawaida kwa sababu lina mawaziri wa zamani…kikubwa tumpe rais na mawaziri wake muda tuwaombee heri wafanye kazi nzuri tusonge mbele,” alisema.
BANA

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Benson Bana alisema baraza dogo aliloliteua Rais Magufuli imeondoa utitiri wa wizara.

“Pia ameteua wazoefu, wasomi na kuna mchanganyiko wa vijana na wazee. Pia alivyomrudisha Profesa Muhongo wakati tunafikiria kuisuka upya Tanesco ni jambo jema,”alisema Dk. Bana.

KIBANDA

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ambaye pia ni Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006), Absalom Kibanda alimpongeza Rais Magufuli kwa kumteua Nape Nnauye kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo.

“Nimepokea kwa furaha na matumaini makubwa ya kikazi, uteuzi wa Nape kuwa waziri mwenye dhamana ya habari. Namuhakikishia ushirikiano wa dhati wakati akitekeleza majukumu yake mapya,” alisema Kibanda.

WANANCHI

Baadhi ya wananchi waliozungumza na MTANZANIA baada ya Rais Dk. John Magufuli, kutangaza baraza hilo walisema wana imani kubwa na mawaziri na manaibu walioteuliwa.

Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) Mkoa wa Mwanza, Richard Rukambura, alisema ana imani kubwa na baraza hilo kwa kuwa limezingatia mahitaji ya Watanzania.

Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza, Mohamed Balla, alisema Rais Magufuli, amezingatia uwiano wa mikoa na ameteua mawaziri na manaibu wachapakazi na kuwataka wasimuangushe.
  • via MTANZANIA

None of us is free from this worry: What other people think

If someone tells you that they don’t care what other people think, they are fooling themselves.

None of us are free from this worry.

Everyone is trying to look good in the eyes of others. Everyone stresses out about how they look, how they’re perceived, whether people think they’re awesome or good people. It’s why Instagram, Facebook, Twitter, blogs and mirrors exist.

Unfortunately, this constant worry about how we’re perceived in the eyes of others can cause us to struggle. We worry about having the right clothes, about how our bodies look, how our hair looks (or the lack of hair, in my case), whether people will laugh at our writing, whether someone will “like” our photos or posts. This takes up so much mental energy.

We can’t just completely forget about it — it’s not in our human nature. We can tell ourselves that “other people’s opinions don’t matter” or “no one is really thinking about us” but it won’t stop our brains from worrying about it.

So what can we do?

We can be aware of these anxieties as they come up. We can realize that the anxieties aren’t a command but rather just something that arises, like clouds coming over a mountain. They’ll pass, float away, if we just watch them without too much attachment.

Then we can go below these anxieties and see our basic goodness underneath. We are good people, with good hearts, and we just want to be loved and appreciated. We worry about not being loved, we worry about being judged, and these are very human worries. We are good, underneath it all.

I encourage you to take a minute right now to contemplate this.

Get to know this goodness in yourself. It is always there, and you can tap into it when the worries come up.

Because no matter what other people think of you, you’ll know that this goodness is there.

Taarifa nzima ya habari ChannelTEN, Ijumaa, Desemba 11, 2015


[video] Magufuli kabla hajawa Rais akizungumzia mchanga unaosafirishwa ng'ambo


Job: Communications and Training Specialist - International Potato Center, Kenya, Tanzania

Organization: International Potato Center
Country: Kenya, United Republic of Tanzania
Closing date: 15 Jan 2016

Job: Director, Health Facility and Quality Improvement, MSH, Tanzania

Organization: Management Sciences for Health
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 31 Jan 2016

Job: M&E Director, MSH, Tanzania

Organization: Management Sciences for Health
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 31 Jan 2016

Job: Director, Health Systems Strengthening, MSH, Tanzania

Organization: Management Sciences for Health
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 31 Jan 2016

Job: Zonal Team Director, MSH, Tanzania

Organization: Management Sciences for Health
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 31 Jan 2016

Job: Deputy Chief of Party (DCOP/Technical Director), MSH, Tanzania

Organization: Management Sciences for Health
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 31 Jan 2016

Job: Director, Finance & Administration, MSH, Tanzania

Organization: Management Sciences for Health
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 31 Jan 2016

Job: Director, Community Based Health, MSH, Tanzania

Organization: Management Sciences for Health
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 31 Jan 2016

Bi Eliza Juma anaomba msaada wa kutibiwa uvimbe uliomo tumboni


Eliza Juma (30), mkazi wa Mtaa wa Mbwanga Manispaa ya Dodoma anaomba msaada wa hali na mali kutoka kwa yeyote ataeguswa ili aweze kufanyiwa upasuaji wa uvimbe tumboni ambao umekuwa ukiongezeka kila siku.

Akizunguma na waandishi wa habari mjini hapa Dodoma, alisema kuwa uvimbe huo ambao umekuwa ukiongezeka kila siku umekuwa kikwazo kwake katika kutekeleza majukumu yake ya kujipatia kipato.

Alisema kuwa uvumbe huo unaotokana na yeye kufanyiwa upasuaji wa utumbo aliofanyiwa miaka miwili iliyopita kutokana na utumbo wake kujikunja.

“Nilifanyiwa upasuaji wa utumbo miaka miwili iliyopita katika hospitali ya mkoa wa Dodoma ambapo utumbo wangu ulikuwa umejikunja lakini mara baada ya kufanyiwa upasujai huo kidonda kilianza kuwasha na mimi nikawa napakuna ndipo pakaanza kuvimba hadi kufikia ukubwa huu unaouona sasa” alisema Eliza.

Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo alikwenda hopitali ya mkoa ili kuweza kuonana na daktali ambaye alimweleza kuwa tatizo hilo linatokana na ngozi ya ndani kulika hivyo anatakiwa kufanyiwa upasuaji kwa mara nyingine.

Aidha alisema kuwa kutokanana hali yake ya kiuchumi na kiasi alicho ambiwa kulipia ili awze kufanyiwa upasuaji huo yeye hawezi kumudu kwakuwa hana msaada wowote anaoutegemea zaidi ya wasamailia wema.

“Kiasi kinacho hitajika ili niweze kufanyiwa upasuaji ni zaidi ya shilingi laki tatu na mie kama mnavyo hapa nilipo natunzwa na wasamilia wema sina mama wala baba hivyo nawaomba wasamalia wema kunisadia ili niweze kupata kiasi hicho kwaajili ya matibabu kabla tatizo halijawa kubwa zaidi”alisema Eliza.
Alisema kuwa kwa yeyote atakaye guswa anaweza kumchangia anaweza kuwasiliana naye kupitia namba ya simu ya mkononi 0678164633ili aweze kupata kiasi hicho cha pesa na kupatiwa matibabu.

Kodi iliyolipwa ndani ya siku 7 za msamaha wa Rais Magufuli

Diana Masalla
Diana Masalla

Meneja wa Huduma na elimu kwa mlipa kodi kutoka wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Diana Masalla akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, ambapo amesema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya jumla ya shilingi 10,075,979,462.08 kutoka kwa makampuni 22 ambayo yalihusika na uondoshwaji wa makontena bandarini kinyume cha sheria na taratibu za forodha hadi kufikia tarehe 10 Desemba 2015.

Amesema makampuni 6 kati ya hayo yamelipa kodi yote iliyokadiriwa pamoja na adhabu, huku makampuni 16 yakilipa sehemu ya kodi iliyokadiriwa pamoja na adhabu. Aidha amesema, makampuni 26 hayajalipa kodi kiasi cha shilingi 4,789,924,609.69 pamoja na kwamba zoezi la ukadiriaji limefanyika.

Hata hivyo amesema kuwa leo ni siku ya mwisho iliyotolewa na Mheshimiwa Rais kwa wafanyabiashara waliokwepakulipa kodi ya makontena.

Amewasisitiza wananchi wote watoe taarifa kuhusu vitendo vya ukwepaji kodi kutumia namba 0784210209. Pia taarifa za mwenendo wa wafanyakazi wa TRA Wasio waadilifu zitolewe kupitia simu namba 0689 122515 na ujumbe mfupi 0689 122516.

Baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhulia katika mkutano na Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova wakimsikiliza leo jijini Dar es Salaam.

Kamanda Kova aonesha picha ya anayetafutwa kwa kukwepa kodi ya makontena 329Pichani juu ni Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova akionyesha picha ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya REGIONAL CARGO SERVICES LTD, ABDULKADIR S/O KASSIM ABDI, miaka 38, Mkazi wa Temeke Mikoroshini ambaye anatuhumiwa kwa kutoa makontena 329 kwenye bandari kavu ya AZAM (AZAM ICD) bila kulipia kodi anayetafutwa na jeshi hilo pia ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni za “JAS EXPRESS FREIGHT LTD” na “XL CLEARING AND FOWARDING Co. LTD” ambazo zote zilitumika kutoa makontena hayo. 

Kova ameonyesha picha ya mtuhumiwa huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa 40 ambao wanahojiwa kwa tuhuma za kula njama na kuikosesha serikali mapato. Uchunguzi unafanywa kwa pamoja na maafisa wa Jeshi la Polisi na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kubaini jinsi ambavyo makontena 329 na mengine 2489 yalivyotolewa bandarini kinyume cha taratibu.

Kati ya hao, watuhumiwa 26 ni watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na watumishi 03 kutoka Bandari kavu (ICD) ya AZAM wanatuhumiwa kuhusika na upotevu wa makontena 329. Aidha, watuhumiwa 11 ambao ni watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa kuhusika na upotevu wa makontena 2489.

Uchunguzi unaoendelea pia unahusisha kupitia kumbukumbu mbalimbali na kadhia za forodha ili kubaini mtindo uliotumika na kuwabaini wote waliohusika katika mchakato huo. Makontena 329 yaligundulika kukosekana kwenye ICD ya AZAM kuanzia mwezi Julai hadi Novemba 2015, wakati makontena 2489 yaligundulika kutolewa Bandarini kuanzia Mwezi Machi mpaka Septemba, Mwaka 2014 kinyume cha taratibu kwa lengo la kukwepa kodi na ushuru.

Uchunguzi bado unaendelea ili kuwabaini wote wanaohusika na hatimaye majalada ya kesi yatapelekwa kwa mwanasheria wa serikali ili watuhumiwa watakaobainika kuhusika na makosa mbalimbali wafikishwe mahakamani.
  • via Michuzi Blog

Call for applications to Host the 7th MIM Pan-African Conference, October 2017

Call for Applications to Host the
7th MIM Pan-African Conference
October 1st – 6th, 2017
Open for applications: 11 December 2015
Letter of intent due date: 10 January 2016

This call for applications is for individual institution or group of Institutions (consortia) within a country in Africa to host the 7th MIM Pan-African Malaria conference.