Picha za kuapishwa kwa Baraza la Mawaziri la Rais Magufuli


Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi Ikulu leo.

Dj Bon Love katika Usiku wa Heart & Soul


Mkali wa magoma hapa nchini na nje, Dj Bon Love akifanya yake katika Usiku wa Heart & Soul uliofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye kiota kinachobamba zaidi hapa mjini cha Raphsody, ndani ya Jengo la Viva Towers katikati ya Jiji la Dar. Dj Bon Love na maDJ wengine wakali hukutana pamoja kwenye kiota hicho ili kukonga nyoyo za wapenda Burudani kutoka maeneo mbalimbali.

Baadhi ya Wadua wa Burudani wakiwepo DJ. Venture na Mwanalibeneke Haki Ngowi wakiwakilisha katika Usiku wa Heart & Soul.

Mmoja wa maDJ wanaopiga katika Usiku wa Heart & Soul akifanya mambo yake.

Furaha pindi wadau wanapokutana.Mdau Othman Michuzi (kulia) na marafiki wengine nao hawakutaka kukutukipwa ya Usiku wa Heart & Soul ndani ya kiota pendwa cha Raphsody, Jengo la Viva Towers katikati ya Jiji la Dar.

Jumapili kutakuwa na mjadala ukumbi wa Nkrumah kuhusu hotuba ya Rais MagufuliWaandaaji wa Mdajala kuhusu Hotuba ya Rais Dk. John Magufuli, aliyoitoa wakati wa kufungua Bunge mjini Dodoma, wakizungumza na waandishi wa habari leo, katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.