Makonda aamuru Kubenea akamatwe na kutiwa ndani

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea (CHADEMA) amekamatwa na polisi eneo la viwanda (EPZA) Mabibo kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.

Tukio hilo limetokea kukiwa na mgomo wa wafanyakazi zaidi ya 1800 wa kiwanda cha nguo cha TZ TOOKU ambao walimpigia mbunge wao aende kutatua mgogoro huo.

Kubenea alifika katika eneo hilo saa 6 mchana, akakutana na wafanyakazi kusikiliza kero zao za muda mrefu.

Kisha aliamua kuondoka na viongozi wa wafanyakazi hao na kufanya kikao na menejimenti ya kiwanda hicho kuanzia saa 7 hadi saa 9.

Ilipofika saa 10:30 Makonda alikuja na kupata taarifa kwa muafaka uliofikiwa kati ya Kubenea, menejimenti na viongozi wa wafanyakazi.

Alitoa amri wafanyakazi wakusanyike, akaawaambia kesho atafika huko na Waziri wa Viwanda na Biashara, Waziri wa Kazi na Ajira, na Waziri wa Afya Wanawake, Jinsia na Watoto.

Baada ya kutoa maagizo hayo, Makonda alimzuia Mbunge asihutubie kuaga wananchi aliokuwa nao tangu mchana, kutokana na hali hiyo Kubenea alisema ni vema aseme neno, ndipo mvutano ulipoanza.

Makonda alimuru mkutano ufungwe lakini wafanyakazi hawakutawanyika eneo hilo, alipoona hivyo aliamrisha Polisi wamkamate Kubenea, kwa madai kuwa alimwita yeye ni kibaka.

Katika tukio hilo, Mwandishi wa habari wa Star Tv aliyekuwa anarekodi tukio hilo alinyang’anywa kamera na Polisi aliyejulikana kwa jina moja tu la Denis.

Mwandishi wa habari hii alijaribu kumsaidia mwenzake ili arejeshewe kamera lakini Polisi wa kituo cha Magomeni walimtisha, na kumtaka kuondoka haraka huku wakiondoka na aliyenyang’anywa kamera.

Baada ya Kubenea kushikiliwa na Polisi kwa zaidi ya saa tano na kuandika maelezo chini ya mwanasheria wake, Fred Kihwelo aliachiwa saa 4 usiku kwa dhamana.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda (mwenye fulana ya mistari) akimtaka Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea asiongee na wafanyakazi

Mandhari ya Tanzania ni nzuri sana!

A lone common waterbuck on a sand bar in the Luwegu River. (Robert J. Ross)
(Top) Stately Borassus palms rise from swamps between the Rufiji River and the northern lakes. (Bottom left) Hippos in the Selous often spend their entire day semi-submerged in pans where the water hyacinth helps to protect their thick but sensitive skin from the sun. (Bottom right) The Northern carmine bee-eater is a beautiful and gregarious seasonal visitor to the Selous. (Robert J. Ross)
A small breeding herd of elephants moves across a channel leading to the Rufiji River as the sun sets. (Robert J. Ross)
Photos from the article published at the NPR.org "The Rapidly Disappearing Elephants Of Tanzania"

Nape awaambia wanaoilalamikia TAHLISO "mwiba unapoingilia si ndipo unapotokea?"
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye jana alinusuru kuvunjika kwa mdahalo ulioandaliwa na Jumuiya ya Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO), baada ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuupinga.

Mdahalo huo ulilenga kujadili hotuba ya Rais Dk. John Magufuli aliyosoma bungeni Novemba 20, mwaka huu wakati akizindua Bunge la 11.

Dosari hiyo ilijitokeza mapema kabla ya Nape kuwasili katika ukumbi wa Nkurumah baadaya Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa chuo hicho (DARUSO), Kataponda Ahadi kusimama na kutoa hoja ya kuwataka wenzake wasusie mdahalo huo kwa sababu haukubeba ajenda na lengo la TAHLISO.

Hata hivyo, alikatishwa mazungumzo yake baada ya kuelezwa muda wa kujadili mada ulikuwa haujaanza, kwa sababu wakati huo mdhamini wa mdahalo huo ambao ni Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), alikuwa akielezea faida za mfuko huo.

Baada ya malumbano yaliyochukua muda kidogo, wanafunzi hao walikubaliana na hoja ya kuendelea kumsikiliza mwakailishi wa NSSF aliyekuwa akiwasilisha mada, hadi Nape alipowasili ukumbini hapo.

Katika hotuba yake, Nape aliusifia mdahalo huo na kusema utasaidia wabunge watakapo kwenda bungeni wawe na ajenda za wananchi, badala ya kwenda na ajenda zao ambazo pengine si matatizo wanayopata wananchi.

Alisema hotuba ya rais, imekuja kwa wakati na imeeleza changamoto nyingi, hivyo ni muhimu vijana wakawa sehemu ya mabadiliko yanayotakiwa kwa staha na uwazi.

Aliwataka wananchi waache utaratibu wa kusikiza na kushangilia tu, bali waichambue, waikosoe,washauri na kuwasisitiza kuwa wasiache suala la mabadiliko liwe la Rais Dk. Magufuli tu.

“Lazima tuhakikishe mabadiliko haya yanaingia kwenye mfumo na yasibaki kwa rais peke yake ili siku tukimpata mtu mwingine afuate mfumo huo. Inapaswa tuusukume mfumo ukubali mabadiliko hayo lakini mfumo ukigoma tutapata matatizo,” alisema Nape.
Baada ya hotuba hiyo, baadhi ya wanafunzi walinyoosha mikono kutaka kutoa hoja ambapo mshereheshaji aliwataka wasubiri mada zitakapowasilizwa wahusika ndiyo wapate muda wa kuzijadili.

Hata hivyo, wanafunzi hao hawakukubaliana na mwongozo huo na walisimama na kusema wana hoja ya kumweleza waziri kabla mada hazijawasilishwa na ndipo mmoja alipopewa nafasi.

Mwanafunzi huyo ambaye hakuweza kufahamika jina lake, alisimama na kuanza kutupa lawama kwa TAHLISO kuwa wameshindwa kusikiliza na kujadili matatizo yanayowakabili wanafunzi wa vyuo vikuu na badala yake wanajihusisha na mijadala ya kisiasa.

“Tunashangaa TAHLISO ambayo ni shirikisho la kuwatetea wanafunzi wa vyuo vikuu, wamekaa kimya kila tunapofikisha matatizo ya wanafunzi, sasa wameona bora wajadili hotuba ya Dk.Magufuli,” alisema mwanafunzi huyo ambaye kabla hata hajamaliza kutoa hoja yake aliamriwa kuketi.

Kitendo hicho kiliamsha hisia kwa wanafunzi wengine, ambao walisimama na kuanza kupaza sauti wakipinga mdahalo huo kwa madai kuwa hauna maslahi ya wanafunzi na kwamba ni wa kisiasa.

Hali hiyo ilimlazimu mshereheshaji kuwaomba askari kuingia ndani ili kuwatoa wanafunzi hao ambao hata hivyo waliamua kutoka wenyewe wakiongozwa na rais wao huku wakiendelea kuituhumu jumuiya hiyo.

Walipofika nje ya ukumbi waliendelea kupiga kelele ambapo iliwalazimu baadhi ya viongozi wa TAHLISO kutoka nje na kuwataka waondoke katika eneo hilo.

Yaliibuka mabishano baina ya viongozi wa pande hizo mbili na baadhi ya wanafunzi ambapo Waziri Nape aliamua kutoka nje na kuacha mdahalo ukiendelea na alipofika nje aliomba kusikiliza hoja zao.

Akielezea malalamiko yao, Rais wa DARUSO Ahadi alisema TAHLISO imeshindwa kusimamia maslahi ya wanafunzi hasa pale wanapoomba kukutana ili kujadili masuala ya wanafunzi wamekuwa hawajitokezi.

“Hawa kwenye mambo yanayohusu wanafunzi wanakaa kimya, mdahalo wameweza kuandaa kujadili hotuba ya Rais Magufuli, zaidi hata huu mdahalo unaofanyika hapa kwetu sisi viongozi wa DARUSO ambao pia ni wajumbe wake hatujapewa taarifa, ndio maana tumeamua kuupinga,” alisema Ahadi.

Kwa upande wake, Waziri wa Mikopo wa DARUSO, Shitindio Venance, alisema: “Kutokana na kitendo cha jumuiya hii kushindwa kutatua matatizo yetu tumeamua kuunda Kamati ya Taifa ya kufuatilia Mikopo ya wanafunzi nchi nzima na hivi tunapozungumza hapa kuna wanafunzi wapatao 80 ambao wanatakiwa wafungashe warudi nyumbani kwa kukosa mikopo na wengine wapo Chuo cha Bagamoyo lakini tunashangaa TAHLISO ipo kimya,”alisema.

Naye Makamu wa Rais wa DARUSO, Irene Ishengoma, alimweleza Nape kuwa pamoja na kusumbuliwa kwa kunyimwa mikopo, bado Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imekuwa ikiwatoza sh 20,000 za kuiendesha suala ambalo ilitakiwa yenyewe itafute mbinu za kujiendesha.

Akijibu hoja hizo Nape aliwataka viongozi hao kuitisha vikao ili kuwaondoa viongozi wa TAHLISO ambao wameonekana kushindwa kazi kwani wao ndio waliowaweka na hivyo wana mamlaka ya kuwaondoa.

“Unajua tatizo lenu ni dogo…hawa viongozi mmewaweka wenyewe na kwa kawaida mwiba unapoingilia ndipo unapotokea hivyo nyie ndio wakuwatoa, tumbueni majipu kama mnaona yapo,” alisema Nape.
Kuhusu matatizo ya mkopo, Nape aliwaambia tayari yanajulikana na kwamba licha ya kwamba yeye si waziri mwenye dhamana lakini ni kiongozi wa chama kilichopo madarakani hivyo atahakikisha leo watahakikisha, tatizo hilo linakoma.

“Naomba niwahakikishie kuwa ikifika kesho (leo) wanaohusika tutakwenda kuwashughulikia ili wakawajibike kwa sababu inaonekana kuna tatizo maana wanafunzi wakigoma fedha zipo lakini wakikaa kimya hawapewi,” alisea Nape.

Nape alifanikiwa kumaliza dosari hiyo iliyodumu kwa dakika 20 baada ya kuwaomba wanafunzi hao warudi ukumbini ili kuendelea na mdahalo kwasababu kama ni matatizo yao yamefika sehemu husika ambapo walikubali na kurudi ukumbini.

Ndani ya ukumbi huo mada zilikuwa zinaendelea ambapo akichambua hotuba ya Rais Magufuli, Mtaalamu wa Mambo ya Uchumi na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dk. Honest Ngowi alisema kiuchumi suala la elimu bure halipo kwani elimu hiyo inalipiwa kwa ruzuku ya serikali kwa asilimia 100.

Alisema ili kuweza kutekeleza hilo wananchi wanatakiwa kukubali kulipa kodi zilizowekwa kwasababu ndizo zitakazotumika kuendesha sekta hiyo.

Naye Mtaalamu wa Sayansi ya Siasa (UDSM), Dk. John Jingu alisema hotuba hiyo ilijikita katika dira ya maendeleo ya Taifa ifikapo mwaka 2025 ya kuwa na uchumi wa kati, kwani rais ameweza kuonesha njia na nia ya kutekeleza dira hiyo.

Kwa upande wake Mwanadiplomasia mkongwe, Balozi Christopher Liundi alisema hotuba ya Rais Magufuli imekuwa mfano kwa viongozi wa chini yake, kwani wanaonekana kutenda kwa kasi yake tangu aingie madarakani.

Madiwani washangaza watu walivyosoma kiapo "kwa taabu"


Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita juzi liligeuka kituko baada ya madiwani wanne kati ya 49 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushindwa kusoma kiapo kwa ufasaha.

Hali hiyo ilisababisha vicheko kutawala katika ukumbi wa halmashauri walimokuwa wanaapishwa madiwani hao.

Tukio hilo lilitokea saa 11:32 asubuhi muda mfupi baada ya mwenyekiti wa muda wa kikao hicho, Gaspar Kanyairita kufungua na hakimu mkazi, Joseph Wiliam kuanza zoezi la kuwaapisha madiwani hao.

Madiwani walioshindwa kusoma kiapo na kata zao kwenye mabano ni Heche Mathias (Nyakagomba), Khadija Joseph (Nyamigota), Daud Simeo (Nyamboge) na Sele Juma Isene (Nyamwilolelwa).

Mkuu wa wilaya ya Geita, Omari Mangochie na Mbunge wa Geita, Joseph Kasheku "Msukuma" hawakuweza kuvumilia hali hiyo na kujikuta wakiangua kicheko cha nguvu ambacho pia kilipokewa na wageni waalikwa na kusababisha ukumbi mzima kuzizima kwa kicheko wakati Diwani wa Kata ya Nyamboge akiapa kwa tabu mithili ya mwanafunzi wa shule ya awali.

Kutokana na hali hiyo, zoezi hilo la uapishwaji lilichukua muda mrefu kukamilika huku ukumbi mzima ukizidi kuzizima kwa vicheko.

Baadhi ya wananchi walishangazwa na hatua hiyo, ambapo mmoja wao alisikika akisema kutokana na baadhi ya madiwani kutokujua kusoma na kuandika kutazorotesha maendeleo yao.

“Kama diwani hajui kusoma hivi hapa wananchi waliomchagua watarajie maendeleo kweli au ndiyo wamejikaanga kwa mafuta yao…diwani kama huyu (anamtaja) anawezaje kukwepa kupitisha mikataba mibovu…hakika hii ni kali,’’ alisikika mwananchi mmoja aliyekuja kushuhudia viapo vya madiwani hao.

  • via MTANZANIA

Mwl. Mndeme: Kasi ya “HAPA NI KAZI TU” ni nzuri, ila itekelezwe kwa tahadhari kubwa


Tunamshukuru Mungu kwamba Rais kateua mawaziri na serikali imeanza kazi rasmi. Kila waziri kwa sehemu yake ameonesha kwamba ana hamasa na motisha ya kufanya kazi na kwa mara ya kwanza (huenda tangu nipate akili) tumeshuhudia mawaziri wakianza kazi lisaa limoja baada yakuapishwa huku kukiwa na habari kwamba hawakunya hata juice walizoandaliwa kwenye ukumbi wa kuapishwa. Hii ni njema sana na ni dalili nzuri katika kujenga Tanzania mpya inayothamini kazi na utumishi kwa wananchi badala ya wanaopewa uongozi kujiona ni miungu-watu, kuona nafasi zao ni za kula bata, na kujinufainya wenyewe na wanaowazunguka. Ninashawishika kwamba, kwa kiwango cha uwajibikaji walichokiweka Rais na Waziri Mkuu (high standard), hakuna waziri atakayelala wala kushindwa kazi kwa visingizio. Hata wale wanaodhaniwa kwamba “sio wazuri sana” katika nafasi walizopewa, nashawishika kwamba watafanya kazi tu hata kama ni kwa kujifunza upya.

Job opportunity: Data Manager - Agronomy

Organization: Columbia University
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 28 Dec 2015

Mtoto wa marehemu Abdallah Kigoda, Omari ashinda ubunge Handeni

Omari Abdallah Omari Kigoda
Omari Abdallah Omari Kigoda
Mgombea ubunge wa jimbo la Handeni mjini kupitia chama cha mapinduizi (CCM) Omari Abdallah Omari Kigoda ameibuka mshindi kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya kuwabwaga wapinzani wake wanne kutoka vyama vya siasa vya TLP, CUF, ADC na CHADEMA vilivyoshiriki uchaguzi huo.
Mteule huyo amewashinda wagombea wenzake kwa kupata kura 10, 315 Sawa na asilimia 75.90 kati ya kura 13,591 zilizopigwa.

Akitangaza matokeo hayo juzi (jana) saa 4.52 usiku Msimamizi wa uchaguzi huo mdogo, Keneth Haule alisema mchakato wote wa uchaguzi huo ulienda vizuri kama ilivyotarajiwa. 

"Kati ya kura zote zilizopigwa kura halali zilikuwa 13,591 ambapo 214 zilikataliwa.. Kwa sababu hiyo basi napenda kumtangaza Omari Abdala Kigoda mgombea kupitia CCM kwamba ndiye mbunge mteule wa jimbo hili la Handeni mjini ", alisema. 

Alisema wagombea wengine akiwemo Doyo Hasani wa ADC alipata kura 184 Sawa na asilimia 1.35, Kilo Daudi wa CHADEMA alipata kura 648 sawa na asilimia 4.77. 

Haule aliwataja wagombea wengine Remmy Shundi wa CUF alipata kura 2,419 sawa na asilimia 17.80 na Makame Bakari wa chama cha TLP aliyepata kura 19 sawa na asilimia 0.14.

Naye mbunge mteule akizungumza na waandishi mara baada ya kutangazwa mahindi aliwataka wananchi kummpa ushirikiano wa dhati katika majukumu yake hayo. 

"Nawashukuru sana wakazi wenzangu wa Handeni kwa kunichagua naomba tushirikiane kwa dhati katika kuondoa kero zinazowakabili wananchi kwasababu naamini peke yangu siwezi ila tukishirikiana kwa pamoja tunaweza", alisema Kigoda.

Mzanzibari aibusu picha ya Rais na kusema, "Nampenda huyu... Gufuli ameileta sheria ya Nyerere na Karume"


Godbless Lema arejeshwa Bungeni

Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amechaguliwa tena kwa mara ya pili kuongoza Jimbo la Arusha Mjini.

Akimtangaza Mbunge huyo, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arusha Mjini, Juma Idd alisema Lema ameshinda kwa kura 68,848 sawa na asilimia 65.7.

Alisema mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Philemon Mollel (Monban) amepata kura 35,607 sawa na asilimia 34 huku mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF) Zuberi (849),Navoi Mollel wa (ACT) 342 sawa na asilimia 0.3 huku chama cha NRA (43).

Alisema Idadi ya wapigakura ni 317,814 ,waliojitokeza ni 105,800 sawa na asilimia 32.83 huku kura halali zikiwa ni 104,353 na zilizoharibika 1447.
  • Imenukuliwa kutoka Lukwangule blog Ent.

Taarifa ya M/Kiti wa Jukwaa Huru la Wazalendo mkoa wa Kigoma

Ndugu Wanahabari

Poleni na majukumu ya kuelimisha na Kuhabarisha Taifa hili.
Tulio mbele yenu ni Viongozi wa Jukwaa Huru la Wazalendo kutoka Mkoa wa Kigoma.

Ndugu wanahabari

Sisi Wana Jukwaa Huru la Wazalendo tumekuwa tukifanya matamko mbali mbali katika mikoa tofauti tofauti hapa Nchini.Tumekuwa tukifanya hivi kwa lengo la Kuunga mkono Hotuba ya Mh.Rais Wa Jamhuri ya Muungano waTanzania alioitoa siku akifungua Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ndugu Wanahabari

Mnakumbuka Mh.Rais John Pombe Magufuli aliomba Watanzania wazalendo wamuunge mkono katika vita ya kutumbua majipu yaani vita dhidi ya Rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma.

Ndugu Wanahabari

Kwa leo tunafanya Mwendelezo ule ule wa kuunga mkono jitihada za Mh.Rais katika mapambano dhidi ya Rushwa.Lakini pia Tunampongeza Mh.Rais kwa kuunda Baraza dogo la mawaziri na lenye watu mahili na makini kwa maslahi mapana ya Umma.Pia tunawapongeza mawaziri walioteuliwa na Mh Rais John Joseph pombe magufuli .

Ndugu Wanahabari

Tunampongeza Mh.Rais kwa kuunda Baraza Dogo ikiwa ni ishara tosha kwamba Mh.Rais anapigana vita ya kubana matumizi ya serikali kwa vitendo na hii imedhihilika Mh.Rais alipotangaza baraza la wawaziri lenye wizara 18 na mawaziri 19 Tunampongeza sana Kwa kufanya mabadiliko kwa vitendo.

Jukwaa linaunga mkono Jitihada za Mh.Rais kwa kuteua mawaziri Makini, wazalendo, wawajibikaji na waadilifu kwa Taifa lao.

Jukwaa Tunapenda sana Kutoa shukrani za dhati kwa Mh.Rais kwa kumteua mh.Sospeter Muhongo kuwa Waziri wa Nishati na madini.WaTanzania tuna kero kubwa sana ya umeme, umeme limekuwa Tatizo kubwa sana hapa Nchini.

WaTanzania tumechoka kuimba wimbo wa Umeme kukatika katika lakini kwa sasa Tunaamini Mh.Rais ametutendea Haki kwa kumteua Mh.Muhongo kuwa waziri wa Nishati na Madini.

Watanzania tunajua uzalendo na uchapakazi wa Mh.Muhongo katika wizara hii na tunaamini Mh.Muhongo hata poteza imani yake kwetu Watanzania katika uchapakazi wake hasa juu ya kuondoa kero hii kubwa na upatikanaji wa umeme vijijini.

Ndugu Wanahabari.

Sote tunajua uwajibikaji wa Mh.Muhongo kwa maslahi ya umma ndio maana hata pale ilipotokea saga la Escrow Mh.Muhongo aliwajibika kwa Maslahi mapana ya Umma na tukumbuke Uwajibikaji wa pamoja haina maana kwamba Waliowajibika wote walikosea hio si tafiri sahihi ya uwajibikaji.

Sote Tunakumbuka hata Mh.Rais wa awamu ya pili Comrade Ally Hassan Mwinyi alishawahi wajibika kwa maslahi ya umma akiwa waziri kwa sababu kuna watendaji wake walio chini yake walifanya ndivyo sivyo kwa hio sio mara kwa kwanza kiongozi kuwajibika kw maslahi ya umma.

Ndugu Wanahabari Tunapenda kumtia nguvu na moyo Mh.Muhongo na kumwambia kwamba Watanzania tunaimani kubwa sana na utendaji wake na tunaamini hata Tuangusha na Tunamuombe kwa Mungu.

Ndugu Wanahabari.

Tunamwomba mh.Muhongo asikatishwe tamaa na baadhi ya Watu wasiolitakia Taifa hili mema kwa kutoa kauli za kukatisha Tamaa juu ya Mh.Muhongo na Jukwaa tunasikitishwa sana na baadhi ya Watu waliokuwa wanamuunga mkono Lowasa kwenye kampeni huku wakijua kwamba nae aliwajibika kwenye sakata la Richmond lakini leo wanambeza Mh.Muhongo kwa kuwajibika kwenye Sakata la Escrow.Tunaomba Watanzania kwenye maswala ya maslahi ya uma tuwe wamoja na tuondoe itikadi zetu za uchana.

Mwisho sisi Jukwaa Huru la wazalendo Tunasikitishwa sana na kitendo cha aliekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya kinondoni kuhamishwa kazi na kupelekwa Babati mkoa wa Manyara baada ya kuharibu katika manispaa ya kinondoni kwa kufanya njama za kuuza fukwe inayotumiwa na umma wa Watanzania wanyonge kwa Tajiri mmoja.

Tunamuomba Mh.Rais amfukuze kazi Mkurugenzi huyo ndugu Mussa Natty ili aendane na kauli yake ya hapa kazi tu maana kwa kitendo cha kumuhamisha kituo cha kazi ni sawa na kuhamisha Tatizo na tunaomba Watanzania walioko Babati wamkatae Ndugu Natty maana ni Tatizo kwa maslahi ya Umma.

Tunaamini Mh.Rais ataunga mkono jitihada za jukwaa kwa kumfukuza kazi Ndugu Natty kama alivyounga mkono Jukwaa lilipopiga kelele juu ya Ndugu Natty kwa jaribio la kuuza fukwe wa uma pale Coco Beach.
Mungu ibariki Tanzania.

IMETOLEWA NA
MWENYEKITI WA JUKWAA HURU LA WAZALENDO MKOA WA KIGOMA

MONALISA JOSEPH NDALA
0657299225

Balozi wa Iran amtambulisha msaidizi wake mdogo kwa Rais Mstaafu, Ali Mwinyi


Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kulia) akikabidhi picha kwa Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mhe. Mehdi Aghajafari, inayoonyesha sehemu ya utamaduni wa Tanzania, wakati alipomtembelea nyumbani kwake, Mikocheni, jijini Dar es Salaam leo Ddsemba 14, 2015.

Rais Mstaafu Mwinyi (kulia) akikabidhi picha yake rasmi kwa Balozi Aghajafari.

Rais Mwinyi akiwa katika mazungumzo na Balozi Aghajafari pamoja na msaidizi wake mpya, Bw. Ali Bagheni. Balozi huyo alifika nyumbani kwa Mzee Mwinyi kwa kumtambulisha msaidizi wake huyo.

Wazanzibari wanaoishi Sweden waandamanaAskari aangusha mtaroni Bajaj aliyoikamata akitaka kuipeleka kituoniAskari wa barabarani (Traffic Police) ameripotiwa kutumbukia mtaroni akiendesha bajaji ya mizigo aliyoikamata kutoka kwa dereva wa bodaboda. Imeelezwa kuwa, mara baada ya kumkamata mwendeshaji Hamis Omary kwa kosa la kupakia mzigo mkubwa wa mbao alimwamuru kulipa faini ya shilingi elfu 30. Hamisi akamwomba msamana na kwamba ni fedha nyingi sana ambayo hawezi kuilipa kwa hata kipato anachokipata toka kwa tajiri aliye mpa mzigo kuusafirisha toka eneo moja hadi jingine.

Traffic huyo akauliza kuhusu leseni, dereva huyo akaonesha Leseni ya biashara, akaonyesha….

Traffic huyo alipoona hakuna kosa jingine akarudi kwenye kosa la kwanza, akitumia kauli ya “Siwezi kukusamehe, nakulipua huku nacheka.”


Mwendeshaji Hamisi Omary akielezea kilichotokea.


Wananchi wakisaidiana kuitoa bajaj hiyo mtaroni mara baada ya mvutano wa mabishano kutaka michoro ya usalama barabarani ifanywe na maaskari waliokuwa zamu.

Kwa sasa mkoani Mwanza na maeneo mbalimbali nchini kuna baadhi ya sura mpya za wanausalama wa vyombo vya usafiri barabarani ambapo licha ya wale wakongwe waliohamishwa toka mkoa mmoja kwenda mwingine pia kuna wapya waliotoka vyuo vya jeshi nchini.


  • via kipindi cha KAZI NA NGOMA ya JEMBE FM Mwanza na GSengo blog.