Maagizo ya Waziri Prof. Muhongo alipozuru mabwawa ya Kihansi na Kidatu

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akimsikiliza Meneja wa Kituo cha Kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji, Mhandisi Pakaya Mtamakaya (kushoto) akizungumzia kuhusu uendeshaji wa mitambo ya kuzalisha umeme ya Kihansi.

Maombi ya siku za nyuma uunganishaji Umeme na Luku ukomo Januari 15


Mameneja wa Kanda wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) wametakiwa kuhakikisha kuwa ifikapo tarehe 15 Januari mwakani kazi ya kuwaunganishia umeme na LUKU waombaji wa muda mrefu iwe imekamilika.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwenye Kituo cha kuzalisha umeme cha Kihansi wakati alipokutana na Mameneja wote wa Kanda wa Shirika hilo.

Alionya kuwa Meneja yoyote atakaeshindwa kutimiza agizo hilo awe tayari kuacha ama kuachishwa kazi.

"Ikitokea Watanzania wakalalamika kucheleweshewa huduma kufikia tarehe 15 mwezi ujao, muwe tayari kuacha kazi," alisisitiza.

Profesa Muhongo alisema Watanzania wamechoshwa na utendaji duni wa Tanesco na kuagiza wahakikishe wanabadilika kwa kuwatumikia vyema wananchi.

Alisema kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi huku kubwa zaidi ikiwa ni kukatika kwa umeme mara kwa mara na kucheleweshewa huduma ya kuunganishiwa umeme na Luku.

Alisema kwa sasa anazungukia mitambo yote ya uzalishaji umeme nchini kufanya tathmini ili kuelewa hali halisi ya umeme na kuwataka kukomesha mara moja hali ya ukatikaji wa umeme mara kwa mara ambayo imekuwa kero kubwa kwa wananchi.

Vilevile Profesa Muhongo aliwaeleza Mameneja hao kuwa ifikapo siku ya Jumamosi ya tarehe 19 mwezi huu wawe na majibu ya kero mbalimbali za umeme nchini.

Alisema siku hiyo atakutana na Mameneja hao pamoja na watendaji wa taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya nishati nchini.

"Nimewaeleza hawa Mameneja kuwa siku ya jumamosi nitakuwa na kikao nao pamoja na watendaji wengine. Nataka waje na majibu ya kisayansi," alisema Profesa Muhongo.

Jambo jingine ambalo Waziri huyo anataka kutoka kwa Mameneja hao ni mkakati waliouandaa kuhakikisha bei ya umeme nchini inashuka.

"Watanzania wanauliza vipi tutafaidika na gesi yetu? Nataka mje na mkakati wa kupunguza bei ya umeme," alisema Muhongo.

Aidha, alizungumzia suala la kuongeza makusanyo ya mapato ya huduma ya umeme ambapo aliwaagiza Mameneja hao kuongeza mara mbili ya malengo ya ukusanyaji mapato waliyokuwa wamewekewa hapo awali.

Waziri Muhongo tayari amekwishatembelea vituo vya kuzalisha umeme vya Hale, Pangani, Nyumba ya Mungu, Mtera na Kihansi.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kushoto) akikagua Kituo cha Kuzalisha umeme cha Kihansi. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), Mhandisi Felchesmi Mramba. Waziri Muhongo alifanya ziara kituoni hapo kwa ajili ya kufanya tathmini ya hali ya uzalishaji wa umeme kituoni hapo.
Meneja wa Kituo cha Kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji cha Kihansi, Mhandisi Pakaya Mtamakaya (kulia) akimuelezea kwa mchoro muundo wa bwawa la Kihansi Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) wakati alipofanya ziara kwenye bwawa hilo ili kujionea hali ya maji. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini, Mhandisi Felchesmi Mramba.
Mtambo mmojawapo wa kuzalisha umeme wa kituo cha Kihansi ambao uwezo wake ni kuzalisha Megawati 60. Kituo hicho cha Kihansi kina jumla ya mitambo mitatu ya kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji ambapo kila mtambo inao uwezo wa kuzalisha kiasi cha Megawati 60 lakini kutokana na tatizo la maji mitambo hiyo inashindwa kuzalisha kiasi hicho.

Muhongo Aagiza kufungwa matoleo ya umwagiliaji


Serikali imeagiza matoleo ya maji ya kumwagilia mashamba yanayotumia maji ya mito inayotiririsha kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme ya Mtera na Kidatu yafungwe.

Agizo hilo limetolewa leo na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alipotembelea Bwawa la Kidatu na kujionea namna ambavyo kina cha maji kwenye bwawa hilo kilivyopungua.

Waziri Muhongo alisema tatizo kubwa la uzalishaji mdogo wa umeme wa maji nchini ni umwagiliaji usio zingatia taratibu za matumizi sahihi ya maji.

Alisema mfumo wa umwagiliaji unaotumika ni wa kienyeji sio wa kitaalamu. "Nimeshuhudia mtu anazuia maji kutiririka kwa kutumia mawe, magogo ama viroba vya mchanga; hii sio sahihi," alisema.

Akizungumzia umeme unaozalishwa kwa nguvu ya maji, Waziri Muhongo alisema kwa hivi sasa ni asilimia ishirini tu inayozalishwa kutoka kwenye vyanzo vya maji nchini.

Alisema jumla ya uwezo wa mitambo yote ya maji (installed capacity) ni Megawati 561.84 ambapo wastani wa uzalishaji kwa sasa kutoka kwenye mitambo hiyo ni Megawati 110 hiyo ni kuanzia tarehe 13 hadi tarehe 16 mwezi huu.

"Nimetembelea Nyumba ya Mungu, Hale, Pangani, Mtera, Kihansi na Kidatu na kugundua kwamba tatizo sugu ni umwagiliaji na siyo tabianchi," alisema.

Alisema mashamba ya umwagiliaji yanaongezeka Mikoani Mbeya, Iringa na Morogoro.

Aliongeza kuwa vibali vya umwagiliaji vimetolewa kienyeji bila kutafakari athari itakayotokea.

Profesa Muhongo alisema kipindi hiki ni cha mvua hivyo wenye mashamba ya umwagiliaji watumie maji ya mvua badala ya kuendelea kutumia mito.

Alisema wakati mazungumzo yanaendelea, Bodi ya Maji- Bonde la Rufiji wahakikishe wanakagua mifereji yote ya umwagiliaji inayoingiza maji kwenye Mto wa Ruaha mkuu na kuifunga ili kuruhusu bwawa la Mtera kupata maji.

Alieleza kwamba kwa kufunga mifereji hiyo ndani ya siku nne hadi tano maji yatakua yameingia kwenye bwawa la Mtera na hivyo kuweza kuendesha mitambo.

Awali akimueleza Waziri hali halisi ya uzalishaji umeme kwenye kituo hicho cha Kidatu, Meneja wa Kituo, Mhandisi Justus Mtolera alisema umeme unaozalishwa kituoni hapo kwa sasa ni megawati 50 wakati kituo hicho kinao uwezo wa kuzalisha jumla ya megawati 204.

Mhandisi Justus alisema kituo hicho kinayo mitambo minne ya kuzalisha umeme lakini kutokana na tatizo la maji, mitambo miwili tu inafanya kazi ambapo kila mmoja unazalisha kiasi cha Megawati 25.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza jambo wakati wa ziara yake kwenye kituo cha kuzalisha umeme cha Kidatu. Katikati ni Meneja wa Kituo hicho cha Kidatu, Mhandisi Justus Mtolera na anayemfuatia ni Meneja wa Kituo cha kuzalisha umeme cha Mtera, Mhandisi Abdallah Ikwasa.

Bwawa la maji la kuendeshea mitambo ya kuzalisha umeme la Kidatu likionekana katika hali ya kupungukiwa na maji

Barua ya Mbunge wa Malindi, Zanzibar, Ally Saleh kwa Rais Magufuli

Barua ya Wazi kwa Rais Magufuli. 

By Hon Ally Saleh. 
Member of the Union Parliament (Malindi Constituency)

Mheshimiwa

Amiri Jeshi Mkuu

Ikulu, Dar es salaam

Asssalam alaykum,

Natumai hujambo na familia na unaendelea na kazi kama msemo wako wa HAPA KAZI TU ulivyo. Inshallah Mungu atakupa afya na uzima uendelee. Pili nakupongeza kwa kuchagua Baraza la Mawaziri ambalo litafanya kazi na wewe, na sisi kama Wabunge kwa faida ya taifa.

Ingawaje hata hivyo, sikubaliani na wewe juu ya baadhi ya teuzi zako, kama vile kuwanyima fursa ya kutosha Wazanzibari na kuonekana Baraza lako kuwa ni la Tanzania Bara zaidi na kutufanya wadogo zaidi na wanyonge zaidi ndani ya Muungano.

Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu, hata hivyo nilotaka kukuandikia leo ni kuhusiana na hali ya usalama hapa kwetu Zanzibar na tishio la kutokuwepo Amani ambapo naamini wasaidizi wako watakuwa wamekuarifu, lakini nakuandikia nikiwa Mbunge wa Malindi kwa tukio lilotokea usiku wa juzi Jumamosi.

Tukio hilo la kuvunjwa vunjwa barza ya wana CUF katika eneo la Michenzani, Mjini Unguja kwa hakika ni muendelezo wa matukio mengi yanayofanywa na watu wanaoitwa wasiojulikana na ambayo yalishamiri sana wakati wa uchaguzi lakini hata baada ya uchaguzi yamekuwa yakiendelea.

Watu waliosemwa wakitumia magari rasmi ya Vikosi vya Zanzibar na wakiwa na silaha walifika eneo hilo usiku mkubwa na kufunga njia na kisha wakifanya ukhabithi huo, na Mheshimiwa Amiri Jeshi Mkuu sehemu hiyo ni mita mia tatu tu kutoka Kituo cha Polisi cha Madema.

Tunajiuliza kwa nini tukio hilo lifanywe usiku kama ni zoezi la kawaida la kusafisha mji? Na hilo tunajua kuwa lilitanguliwa na siku chache nyuma gari moja iliyopita na kutangaza kwa bomba kuwa sehemu hiyo ivunjwe, bila ya kuonyeshwa amri halali ya kufanya hivyo.

Mheshimiwa Amiri Jeshi Mkuu, sehemu hiyo maarufu huitwa Commonwealth na hadi leo haijaripotiwa kuwa na kitendo chochote kile cha ukosefu wa Amani tokea ilipoanzishwa.

Mita 100 tu upande wa pili kuna ile inayoitwa Maskani Mama ya Kisonge ambayo hiyo haiguswi wala haiulizwi na Polisi yoyote yule. Tokea kuanzishwa kwake hadi leo imekuwa na ubao unaoitwa Sauti ya Kisonge ambao umekuwa na matusi na kejeli kwa viongozi na hasa viongozi wa upinzani.
Ubao huo umekuwa ukichochea fujo, kutoa lugha ya kibaguzi na mara nyingi imekuwa ni chanzo cha kuzusha hamasa za kisiasa hapa Zanzibar, lakini inalindwa utafikiri ni taasisi rasmi ya kiserikali.

Siku chache nyuma, watu wasiojulikana wakiwa na silaha pia walivamia studio ya Hits FM wakati wa usiku na kuichoma moto na kutia hasara kubwa. Lakini hasara kubwa zaidi ni kuzima sauti za watu na kukaba uhuru wa maoni na kujieleza.

Wakati wa Kampeni makundi hayo pia yalitishia Amani ya wana habari kwa kumpiga mwana habari mmoja na kuvamia kituo cha radio cha Coconut FM mchana kweup wakiwa na silaha kama marungu, mapanga, msemeno wa kukatia miti na bunduki.

Mheshimiwa Amiri Jeshi Mkuu, sitaki nikuchoshe kwa mlolongo wa matukio ya makundi hayo katika kupiga watu, kuvunja na kuchoma sehemu kadhaa, lakini nataka nikuhakikishie kuwa hakuna sauti yoyote ya kukemea iliotoka kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kwa uhakika Rais wa Zanzibar wakati huo, Dk. Ali Muhammed Shein alisema “ hana habari”; Waziri wa Vikosi wakati huo Haji Omar Kheir alisema “ hakuna ukweli” na Polisi walisema “hawajawaona watu kama hao.”

Dhamana ya usalama wa nchi nzima ni yako wewe. Sitaki niamini kuwa tuna utawala ulioshindwa (failed state) kwa sababu ya Zanzibar ambapo makundi haramu yanafanya yanavyotaka na hakuna wa kuwauliza. Hakunonekani kuna nia ya kisiasa wala ya kiutendaji kwa wasaidizi wako wa Zanzibar kulikabili na kulimaliza jambo hili.

Hakuna nia hizo kwa sababu makundi hayo wameyaunda wao kwa faida zao za kisiasa. Ila naamini katika picha kubwa ya taifa makundi haya yanaharibu sifa yako na yanajuburi ( challenge) mamlaka yako.

Mheshimiwa Amiri Jeshi Mkuu, kuendelea kwa vitendo hivi hapana shaka kutashusha Imani ya wananchi kwa vyombo vyetu vya ulinzi vikiwemo Polisi na Jeshi la Wananchi na vikiwa chini yako. Na kushuka kwa imani hiyo kuna maana kuelekea kwenye fujo na vurugu (riot na anarchy).

Kanuni ya kuonewa inasema wazi kuwa anaeonewa hataonewa siku zote maana iko siku atasema basi na atajitetea hata katika hali yake ya udhaifu kuonesha msimamo wake na makundi haya yameonea sana watu wa Chama cha Wananchi CUF na nina hofu ya wanaononewa kusema wamechoka.
Wakati bado tumo kwenye kutafuta njia ya kutoka kwenye mkwamo ambao pia unatokana na ukweli kuwa Chama cha Mapinduzi hakina na hakijawahi kuwa na nia ya kutoa nchi kwa njia za kidemokrasia, matukio kama haya yana nia ya kuzidi kukwamisha kupatikana suluhu.

Haikubaliki kabisa, raia kuonewa, kunyanyaswa ndani ya mipaka yao, tena wafanye hao wa uonevu wakiwa ni wale waliopewa dhamana ya kuwalinda. Au kama wanaofanya hivyo sio wao, kufumba macho wenye nia hiyo chafu wakitekeleza dhamira mbovu.

Mheshimiwa Amiri Jeshi Mkuu, naamini si kuwa kadhia zote hizi hazijafika mezani huko Magogoni jumba kuu, lakini pengine ushauri ulitolewa kuwa hili ni jambo la kupita na dogo tu. Lakini napenda kusema kama cheche huzaa moto na dogo huzaa kubwa.

Sina haki ya kukushauri kama hujaniuliza ushauri wangu kwa heshima yako, lakini napenda kusema hili lisimamie mwenyewe utake kujua undani utandu na ukoko. Kisha ulishikia fimbo limalizwe na wanaohusika kuliwachia wachukuliwe hatua.

Zanzibar leo imekuwa eneo la khofu. Khofu ya mchana ambapo katika malindo yanayofanywa na askari wa JWTZ wananchi wamekuwa wakipigwa mchura wanafanya makossa na usiku makundi mengine yakifanya hujuma na kutishia maisha na Amani. Tushukuru Mungu kuwa mpaka leo hakuna maisha yaliopotea.

Mheshimiwa Amiri Jeshi Mkuu, ya Burundi, ya Burkina faso, ya Ivory Coast na kwengine tusiyaone yako mbali. Siku hizi tuna nafasi ya kujifunza mambo haraka na kuyazuia na naamini utalifanyia kazi hili ili nchi mshirika wa Muungano watu wake wafaidi uhuru wao wa kila kitu na isiwe kujikunyata.
Nashukuru na Mungu akubariki katika kazi na maisha yako.

Mwandishi wa Makala hii ni mshairi, mchambuzi wa siasa, mtunzi wa vitabu, mwanasheria na Mbunge wa Jimbo la Malindi.

Waziri Balozi Dk Mahiga kuzungumza na Katibu Mkuu EAC, Sezibera kuhusu hali nchini Burundi

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akijibu maswali kuhusu hali ya kisiasa nchini Burundi wakati wa mahojiano maalum na Mwandishi wa Habari kutoka Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) Bw. Mubali. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga akinukuu mahojiano hayo. Mahojiano hayo yatarushwa tarehe 18 Desemba, 2015 saa 3:00 usiku kupitia kipindi cha Dira ya Dunia kinachorushwa na Kituo cha Star TV


Mhe. Dkt. Mahiga akiagana na Bw. Mubali baada ya kumaliza mahojiano hayo.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

ZIARA YA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI, KIKANDA NA KIMATAIFA, MHE. DKT. AUGUSTINE MAHIGA
MKOANI ARUSHA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga atafanya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Arusha kuanzia kesho Jumamosi tarehe 19 Desemba 2015.

Atakapokuwa mkoani Arusha, Balozi Mahiga atafanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Dkt. Richard Sezibera. Mazungumzo yao yatahusu namna ya kutatua mgogoro wa kisiasa nchini Burundi.

Aidha, Mhe. Waziri atatembelea eneo la Lakilaki ambalo limetengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za taasisi za kimataifa. Ujenzi unaoendelea hivi sasa kwenye eneo hilo ni jengo la ofisi la taasisi yaMechanism for Crime Tribunals (MICT) inayorithi shughuli za Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) ambayo itakamilisha shughuli zake tarehe 31 Desemba 2015.

Mhe. Waziri pia atatembelea Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kuonana na uongozi wa Kituo hicho kwa madhumuni ya kufahamiana. AICC ni moja ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.

Mhe. Waziri atarejea jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili tarehe 20 Desemba 2015.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
18 Desemba, 2015Katuni: Hebu tuone...


Mhadhara 19.12.2015 UDSM kuhusu udhamini wa elimu ya juu Ughaibuni


MHADHARA - UDHAMINI WA ELIMU YA JUU UGHAIBUNI


Kutakuwa na mhadhara na majadiliano kuhusu udhamini/ufadhili wa Elimu ya juu ughaibuni (SCHOLARSHIP OPPORTUNITIES).

Mhadhara utakuwa siku ya Jumamosi Disemba 19, 2015 katika ukumbi wa ATB hapa chuoni UDSM Mlimani Main Campus.

Muda ni kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa nane mchana.

Presenters ni

Ernest B Makulilo
Francis Semwaza
Genuine Martin
Victoria B Makulilo, PhD
Mathew Agripinus, PhD

Tafadhali alika watu wengi zaidi. Ni BURE kushiriki fursa hii.

Ernest Boniface Makulilo

Kauli za Nassari, Dk Ndugulile kuhusu jitihada za Rais Magufuli

TZ ndo nyumbani kwangu, kwa watoto na watoto wa watoto wangu. MAMA TZ NI MUHIMU ZAIDI KWANGU
Kwa utaratibu huu wa kukusanya 1.3 Trillion kwa mwezi, tunaweza kuwa na Bajeti inayojitegemea kwa asilimia 100.
Thanks JPM, only if it's sustainable though!
Kama tunaweza kukusanya 1.3 Trillioni kwa mwezi kwenye kodi, basi tutaweza kuendesha Serikali na miradi ya maendeleo kwa kiasi kikubwa. Nakerwa sana na utegemezi wa wahisani. Mwanzo mzuri Mhe. Magufuli
  • Kauli ya Mbunge wa Kigamboni kwa tiketi ya CCM, Dk Faustine Ndugulile via Facebook

Waliochelewa kufika ofisini Wizara ya Afya watakiwa kuandika barua ya maelezoNaibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akiwaamrisha askari wa getini wizarani hapo kuweka kufuli na kutoruhusu mtumishi yoyote wa ofisi hiyo kuingia ndani ya ofisi za wizara ilipotimu saa 1:32 asubuhi mapema leo. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

Habaeri na Rabi Hume, Modewjiblog

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla amefanya ukaguzi wa kushtukiza katika ofisi za wizara hiyo kwa kusimama getini kuzuia wafanya kazi wote wa wizara ambao walikuwa wamefika ofisini baada ya saa 1:30 asubuhi muda ambao ndiyo mwisho wa wafanyakazi kuingia ofisini.

Awali Dkt. Kingwangalla alifika ofisini saa 1:05 asubuhi huku akiingia ofisini kwa kutembea mwenyewe bila kutumia usafiri wa gari na kwenda moja kwa moja ofisini kwake ambapo alitoka ilipofika saa 1:32 na kwenda kusimama getini na kisha kuwaamrisha askari wa geti la kuingia katika wizara hiyo kulifunga geti hilo na wasiruhusu mtu yeyote kuingia ndani.

“Fungeni geti na kila atakayefika msimruhusu kuingia ndani ninataka kuona wote ambao wanakuja wamechelewa,” alisikika Dkt. Kingwangalla akiwambia askari wa getini.

Baada ya kutoa amri hiyo alimtaka Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa wizara hiyo, Michael John kumpa vitabu vya kusaini kwa vitengo vyote ili aweke mstari wa kuonyesha kuwa muda wa kuingia ofisini umekwisha na akafanya hivyo kwa kuweka mstari kwenye vitabu vya mahudhurio kuwa muda wa kusaini kuingia umeisha.

Baada ya kukamilisha zoezi hilo Naibu Waziri alizungumza na wanahabari kuwa ameamua kufanya zoezi hilo katika ofisi za wizara kwa kutaka kuona ni jinsi gani watumishi wa ofisi hiyo wamekuwa na mwitikio wa kufanya kazi kwa kasi anayoitaka rais, Dkt. John Pombe Magufuli.

Alisema watumishi hao wameajiriwa na serikali ili kufanya kazi lakini wamekuwa wakichelewa kuingia ofisini na yeye kama Naibu Waziri ana wajibu wa kuwasimamia watumishi hao ili wafanye kazi ambayo serikali imewaagiza kufanya.

“Nina wiki moja tangu nimeingia hapa ofisini kuna mambo ambayo nimeyaona hayapo vizuri na sasa naanza na hili ili tujue kuwa ni kina nani huwa wanachelewa na zoezi hili litakuwa ni endelevu, kama mimi sitasimamia watumishi wa serikali basi sitakuwa na kazi wizarani tunataka watumishi ambao wanakuwa wanafanya kazi kwa kujitoa kwa ajili ya maslahi ya taifa,” alisema Dkt. Kingwangalla.

Aidha Naibu Waziri huyo alimtaka Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kuhakikisha watumishi wote waliochelewa kufika ofisini wanaandika barua ya kutoa maelezo kwanini wanachelewa kufika ofisini na baada ya hapo Mkurugenzi na yeye atoe maelezo kwanini muda wa kutoka watumishi wanakuwa hawasaini kuwa wametoka.

Pia alishauri uongozi wa wizara ufanye mabadiliko ya mfumo wa watumishi kuingia ofisini kwa kutumia mifumo ya kisasa ya kadi au kidole “Biometric” ili kuwa na taarifa katika mifumo ya mawasiliano kujua wanaochelewa ofisini na wanaowahi kutoka na baada ya hapo uongozi utajadili adhabu za kuwapa watumishi wote ambao wamekuwa wakichelewa kufika na kuwahi kutoka ofisini.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akisimamia zoezi la ufungwaji wa geti hilo, Kulia ni askari wa SUMA JKT akiweka kufuli katika lango kuu la kuingia katika ofisi za Wizara ya Afya.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akiwauliza askari wa getini kuhusu daftari la mahudhurio ya watumishi wa wizara baada ya kufungwa geti hilo, na kupewa maelezo kuwa watumishi huonyesha vitambulisho pekee na husaini katika vitengo vyao.


Mmoja wa wafanyakazi wa Wizara ya Afya akiwasili ofisini huku muda wa kuingia kazini ukiwa umepitiliza. Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akizungumza na mmoja watumishi wa wizara hiyo na kuagiza kuletewa vitabu vya mahudhurio kwa vitengo vyote vilivyopo wizarani hapo.


Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu katika Wizara ya Afya, Michael John akitoa maelezo kuhusu mahudhurio ya watumishi kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla.


Magari ya watumishi wa Wizara ya Afya yakiendelea kuwasili ofisini bila ya kutambua kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri, Dkt. Kigwangalla ametoa agizo la kuizuia watumishi wachelewaji.


Askari wa getini wakimpa maelezo mmoja wa watumishi wa wizara hiyo kuwa Mh. Naibu Waziri ameagiza watumishi wote waliochelewa kuzuiliwa kuingia ndani.


Mmoja wa wasaidi wa idara ya rasilimali watu akimkabidhi vitabu vya mahudhurio Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akipitia mahudhurio ya watumishi wa wizara kwa siku zilizopita.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akipitisha mstari wa kufunga mahudhurio kwa watumishi ambao wameripiti kabla ya saa 1:30 asubuhi ya leo.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akiendelea na zoezi hilo la kupitisha mstari kwa kila idara za wizara hiyo.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangalla akizungumza na waandishi wa habari kuhusu juu ukaguzi huo katika ofisi za wizara yake ya afya ili kuboresha utendaji wa wizara hiyo na vituo vyote vya sekta ya afya nchini kote.

Barua ya wazi ya Andrew Ndingo kwa Rais Magufuli

Ninayo heshima kubwa kukupongeza kwa kuwa Rais wetu wa awamu ya TANO. Ninayo mambo machache ya kukushauri kama Rais wangu na mimi kama mwananchi wako mpenda maendeleo kama kauli mbiu yako ya hapa kazi tu nayo ni kama ifuatavyo la kwanza ni usafirishaji wa abiria wakati wa usiku badala ya mchana kama ilivyo sasa mimi nakuomba na kushauri turudishe utaratibu wa miaka ya nyuma wa kuruhusu mabasi ya mikoani kusafiri usiku badala ya mchana, hii ni kwa sababu Serikali yetu inapoteza mamilioni ya shillingi kwa kuwafanya abiria wawe safarini mchana mathalani kila siku mabasi yanaondoka DAR yasiopungua 400 kila basi linabeba abiria wasiopungua 60 kwa wastani hii maana kutoka mikoani kuja DAR ni idadi ni idadi kama hiyo hii ina maana kuwa watu wasiopungua 48,000 wako barabarani wamekaa idle hawafanyi kazi, na kama wastani kila mtu anazalisha TSHS 50,000/= kwa siku akiwa kazini basi tunapoteza jumla ya shs 2.4 bilioni kila siku ambazo tungeziokoa kwa kuwasafirisha abiria hao usiku, maana kama nitaondoka Mbeya saa 12 jioni Dsm nitafika saa 12 alfajiri nitafikia kazi tu na jioni naondoka Dsm saa 12 jioni nafika Mbeya saa 12 alfajiri na kwenda kazini asubuhi hiyo hiyo hapa hakuna nguvu kazi iliyopotea maana nimepoteza usiku tu ambao hata hivyo ningekuwa nimelala nyumbani badala yake nitalala kwenye basi, hii itaokoa mamilioni ya shilingi ya watu na Taifa kwa ujumla.

- Sababu ya pili ni ajali zitapungua sana kwa sababu mchana kuna joto sana matairi yanapata moto na hatimaye kusababisha burst na vipuri vya gari kuharibika sana wakati wa mchana kuliko usiku maana injini wakati wa usiku inapoa nakupunguza burst za matairi inayosababisha ajali nyingi na hatimaye kupunguza vifo vingi vya watu wetu.

- Sababu ya tatu ni tutapunguza msongamano uliopo sasa hasa katika miji mikubwa nchini.

- Sambamba na hilo ili kupungusa ajali kabisa nashauri malori yapigwe marufuku kusafiri usiku ili yabaki mabasi tu

- Sababu ya nne ni kwamba nchi nyingi kama sio zote mabasi yanasafiri usiku na hasa ya masafa marefu ninaamini hawa wenzetu waliliona hilo kupoteza nguvu kazi ya watu kwa kuwafanya wasafiri mchana mfano ni Malawi, Zimbabwe, Mozambique, South Africa Namibia n.k najiuliza kwanini nchi yetu iwe kama kisiwa?

- Sababu ya tano mabasi yatapunguza speed maana atakimbilia wapi sharti afike Dsm asubuhi tu No way out

- Najua wengi wanafikiri kwamba mabasi yatatekwa hilo kwa sasa halipo kutokana na teknologia ilivyokua maana hayupo mtu anayetembea na hela mkononi tofauti za zamani na hili abiria wengi wanalipenda sana wanashindwa tu pa kusemea, na kutokana hilo abiria wanasafiri usiku na vikosta, Noa na IT ambavyo mara nyingi husababisha ajali ukiacha coasta ,NOA na IT havina balance vinaanguka sana. Ili kumaliza hilo nashauri serikali yako kuruhusu mabasi ya masafa marefu kusafiri usiku.

- Nitashukuru sana iwapo utalitazama hili kwa jicho la kiuchumi.

Jambo jingine ninaloshauri ni serikali kuhamia DODOMA Mh. Rais nitoe mfano wa nchi jirani ya Malawii ,Rais wa kwanza wa nchi hiyo Kamuzubanda alianzia makao makuu ya nchi yake kule ZOMBA baadaye akahamia BLANTYRE na baadaye akahamia LILONGWE kwa nini alifanya hivyo, ni kwa ajili ya kupanua maendeleo katika miji ya nchi hiyo ambapo mpaka leo kuna miji mikubwa Mitatu.

Mh Raisi kama wewe mwenyewe utahami DODOMA mkoa utakuwa kwa kasi na kupelekea mikoa ya jirani kukua kwa kasi kubwa sana

- Tutapunguziwa safari ndefu za kwenda DAR kufuata huduma za serikali kuu maana DODOMA ilo katikati ya nchi

- Foleni Dsm itapungua sana kama sio kwisha kabisa

- Sasa hivi uchumi wa Tanzaia kwa asilimia 80 unategemea Dsm hebu fikiria ikatokea tsunami kama ile ya INDONESIA je itakuwaje japo hatuombei hilo lakini linaweza kutokea (what if it happen) maana yake tutapoteza uchumi wa nchi kwa 80%.

- Sambamba na hilo viwanda vitajegwa sana DODOMA na mikoa mingine kuliko ilivyo sasa DSM ndo kila kitu.

- Mwisho nasema hayo ni mawazo yangu tu yananisumbua kwa muda mrefu sana nimeona kwa kuwa wewe umekuja kwa kauli mbiu ya hapa kazi tu pengine unaweza ukafanyia kazi haya tukasonga mbele.

Nakuombea kwa Muungu akupe hekima na busara katika kutekeleza majukumu Mazito ya kuingoza Tanzania.

Wako katika ujenzi wa Taifa.
Andrew Ndingo
0754447501
AMIN

Statement: Decision by MCC to defer vote on Tanzania compact eligibility

Millennium Challenge Corporation (MCC) Board Defers Vote on Tanzania Compact
December 18, 2015


Dar es Salaam, TANZANIA. The Board of the U.S. Government’s Millennium Challenge Corporation (MCC) met on December 16 and yesterday issued a statement available here. In the statement, the MCC Board said it chose to not vote on compact eligibility for Tanzania, pending resolution of ongoing governance concerns.

To request more information, please email Japhet Sanga ([email protected]), Senior Information Specialist at U.S. Embassy Dar es Salaam.

-----------------

Statement from Ambassador Mark B. Childress on decision by the Millennium Challenge Corporation to defer vote on Tanzania compact eligibility


December 18, 2015

On Wednesday, December 16, the Board of the Millennium Challenge Corporation (MCC) did not select Tanzania for a second compact. The Board deferred the vote on a second compact pending the resolution of governance concerns.

The Board may revisit Tanzania’s eligibility over the course of 2016. I remain hopeful that the Government of Tanzania will take steps to resolve MCC’s governance concerns in the near future. The Board could then vote to re-select Tanzania and approve compact development.

The Board’s governance concerns reflect longstanding MCC principles. The nullification of election results in Zanzibar halted an otherwise orderly and peaceful electoral process. The use of the Cybercrimes Act of 2015 during the elections to arrest individuals accredited by the National Electoral Commission inhibited fundamental freedoms of expression and association.

MCC has been encouraged by newly-elected President Magufuli’s recent steps to strengthen the fight against mismanagement and corruption, and hopes those efforts will continue and result in systemic change.

---
Statements source: tanzania.usembassy.gov, also available in Kiswahili.

Kikao cha kwanza cha Rais Magufuli na baraza lake la Mawaziri

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam Alhamisi tarehe 18, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na kushoto kwake ni Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa. Kikao hicho ni cha kwanza kufanyika tangu Rais Magufuli atangaze Baraza la Mawaziri la Serikali ya Awamu ya Tano wiki iliyopita.