Mahakama yafuta kesi ya Dk Masaburi iliyopinga ubunge wa Kubenea


MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imefuta kesi ya madai ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Ubungo.

Kesi hiyo ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Didas Masaburi dhidi ya mbunge wa jimbo hilo, Saed Kubenea (CHADEMA).

Uamuzi wa maombi ya kufuta kesi hiyo uliwasilishwa mahakamani hapo jana na wakili wa Dk. Masaburi, Clement Kihoko mbele ya Jaji Lugano Mwandambo.

Wakili Kihoko alisema kuwa mteja wake hana nia ya kuendelea na usikilizwaji wa kesi hiyo ya kupinga matokeo.

Baada ya kuwasilisha maombi hayo, Jaji Mwandambo alisema mahakama imepokea maombi hayo ya kuifuta kesi hiyo.

GHARAMA

Baada ya jaji kukubali ombi hilo, Wakili Kihoko aliiomba mahakama kuwapunguzia gharama za uendeshwaji wa kesi ya msingi pamoja na fidia ya usumbufu.

Hata hivyo, Wakili wa Kubenea, Nyaronyo Kicheere, alisema licha ya upande wa utetezi kuomba punguzo hilo, lakini wanapaswa kulipa gharama hizo.

Kutokana na hali hiyo, kuliibuka mvutano wa sheria, jambo lililomlazimu Jaji Mwandambo kuahirisha kesi hiyo kwa muda mfupi, aweze kupitia hoja hizo kabla ya kurudi mahakamani.

Baada ya kurudi, Jaji Mwandambo alisema katika kesi ya msingi mdai anatakiwa kulipa asilimia 50 ya gharama zote za uendeshaji wa kesi hiyo.

Alisema katika maombi ya punguzo la uendeshaji wa kesi hiyo, kila upande utalipia gharama zake.

KUBENEA ANENA


Akizungumza baada ya kutoka mahakamani, Kubenea aliwashukuru wanachama wa Chadema kumsindikiza mahakamani wakati kesi hiyo ikiendelea.

Hata hivyo, alisema kitendo cha Dk. Masaburi kufuta kesi hiyo kinaonyesha wazi kuwa yeye ni mshindi na ataliongoza jimbo hilo katika miaka mitano.

“Wagombea wengine waliofungua kesi kama ya Dk. Masaburi wakati hawana uhakika wa kushinda wanapaswa kuzifuta ili waendelee na kazi nyingine,” alisema Kubenea.

Dk. Masaburi alifungua kesi hiyo namba 8 /2015 kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu kwa mbunge wa Ubungo, Kubenea akidai kuwa yeye na mawakala wake hawakuruhusiwa kuona vifaa vya kupigia kura kama ilivyofanyika kwa Kubenea na mawakala wake.

Vilevile alidai Kubenea alitoa rushwa ya jenereta katika Hospitali ya Mavurunza iliyopo Kimara, zawadi ya meza ya mchezo wa pool kwa vijana wa Makuburi na kujenga barabara ya Matete huko Kimara akiwashawishi kumchagua.

Dk. Masaburi pia alimlalamikia msimamizi kukataa kuhakiki kwa mara ya pili matokeo yake ikiwamo na watu kadhaa wa maeneo ya Mizizini, Mianzini, Kilimahewa, Mizambarauni, Shule ya Mugabe na Kanuni, kutokupiga kura.

Pamoja na Kubenea, washtakiwa wengine katika kesi hiyo walikuwa ni Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Ubungo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mawakili wengine kwa upande wa Kubenea walikuwa Tundu Lissu, Mabere Marando, Peter Kibatala, Method Kimomogolo na Frederick Kihwelo.

Maagizo ya Mawaziri tangu kuapishwa Desemba 12


Ni mwendo wa maagizo. Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na kila waziri anayefanya ziara katika idara au taasisi zilizoko chini yake kutoa maagizo kudhihirisha uwepo wao.

Mawaziri hao ambao waliapishwa Desemba 12, mwaka huu, wameanza kazi kwa kasi kama ilivyokuwa kwa Rais Dk. John Magufuli na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ambao walianza kazi kwa kuwasimamisha maofisa wa umma na wajumbe wa bodi zaidi ya 83 katika muda mfupi, kutokana na makosa mbalimbali.

Baada ya kuapishwa, siku hiyo hiyo baadhi ya mawaziri na manaibu wao walianza kazi kwa kutembelea idara zilizo chini ya wizara zao na wengine wakienda kuripoti wizarani, ikiwa ni kutimiza kaulimbiu ya Hapa Kazi Tu!

Muhongo atoa siku 30


Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alipotembelea kituo cha kuzalisha umeme cha Kihansi mkoani Iringa, alikutana na mameneja wa kanda wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na kuwataka kuhakikisha ifikapo Januari 15, mwakani kazi ya kuwaunganishia umeme waombaji wa siku nyingi iwe imekamilika.

Profesa Muhongo ambaye pia ni Mbunge wa Musoma Vijijini alisema meneja yeyote atakayeshindwa kutimiza agizo hilo aache kazi mwenyewe au ajiandae kufukuzwa.

“Ikitokea wananchi wakalalamika kucheleweshewa huduma kufikia tarehe 15 mwezi ujao, muwe tayari kuacha kazi wenyewe,” alisisitiza Profesa Muhongo.

Pia alisema kumekuwapo na malalamiko kutoka kwa wananchi, juu ya kukatika kwa umeme mara kwa mara na kucheleweshewa huduma ya kuunganishiwa umeme na mita za Luku.

“Mameneja wote ifikapo Jumamosi ya tarehe 19 mwezi huu, muwe na majibu ya kero mbalimbali zinazohusu umeme,” alisema.


Jafo atoa siku 26


Akizungumza na wafanyakazi na wakuu wa idara wa Halmashauri ya Bahi, Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jaffo, alitoa siku 26 kwa halmshauri zote nchini kukamilisha na kuanza kuutumia mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji wa mapato.

Jafo ambaye ni Mbunge wa Kisarawe, alisema atawawajibisha wakurugenzi watakaoshindwa kukamilisha mfumo huo wa ukusanyaji wa mapato ifikapo Januari 10 mwakani.

“Mkurugenzi atakayeshindwa kutimiza agizo hili aandike barua kwa Katibu Mkuu TAMISEMI kujieleza kwamba ameshindwa, kila mkurugenzi atawajibika katika hili kwa kushiriki ufisadi wa kuikosesha halmashauri mapato,” alisema.

“Mfumo huu ulitakiwa kuwepo kuanza kutumika tangu Julai mwaka huu, lakini hadi sasa zipo halmashauri hazijaanza kuutekeleza katika idara zake hali inayosababisha upotevu wa mapato.

“Wilaya ya Bahi ilitakiwa kuwa ya mfano kwa kuweka mfumo wa kielektroniki wa kukusanya mapato lakini kutokana na uzembe na inawezekana umecheleweshwa kwa makusudi ili kuendelea kutoa mianya ya watu kujipatia fedha,” alisema.

Mhagama atoa siku 26


Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, alitoa siku tano kwa Manispaa ya Ilala kuvunja mkataba na mkandarasi aliyepewa zabuni ya ujenzi wa mtaro uliopo Buguruni kwa Mnyamani, kutokana na kujenga chini ya kiwango.

Akitoa agizo hilo, Mhagama alisema ofisi yake haitatoa fedha za kumlipa mkandarasi huyo na kama manispaa imemlipa fedha zozote, wazirudishe na ikibidi waliozilipa wazitoe mifukoni mwao.

Kutokana na mafuriko katika eneo hilo, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, wakati wa uongozi wake alifika eneo hilo na kutaka baadhi ya nyumba zivunjwe na ujenzi uanze.

“Kama hamjamlipa mkandarasi serikali haitahusika na deni hilo na kama mmemlipa fedha hizo mkurugenzi na timu yako zitoke mifukoni mwenu, haiwezekani mkandarasi ajenge chini ya kiwango halafu mnamwangalia tu,” alisema Jenista.

Waziri huyo pia alitoa tangazo kwa vyombo vya habari, akiwapa siku saba waajiri wote nchini kuhakikisha wametoa mikataba ya ajira kwa wafanyakazi wao na kuruhusu wafanyakazi kujiunga na vyama vya wafanyakazi.

Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, aliwataka waajiri hao ndani ya muda huo wawe wameandikisha wafanyakazi wao katika mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na kupeleka michango yao kwa wakati.

Pia alitoa siku 14 waajiri ambao wana watumishi wasio raia wa Tanzania, wawe wamewachukulia vibali vya kufanya kazi kutoka kwa Kamishina wa Kazi kwa mujibu wa Sheria Namba 1 ya mwaka 2015.

Mbarawa na DAWASCO


Naye Waziri wa Maji, Makame Mbarawa alilitaka Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (Dawasco), kuhakikisha kuwa hadi kufikia Juni mwakani wateja milioni moja wawe wamepatiwa huduma ya maji.

Mbarawa alimtaka Mkurugenzi wa Dawasco, Cyprian Luhemeja, kuongeza kadirio la wateja walilokuwa wamejiwekea la wateja 148,000 hadi kufikia milioni moja.

“Naamini pindi tutakapofanya mazungumzo ya kina tutafikisha kiasi hicho cha wateja hiyo Juni na hilo mtalipima kwenye tathimini tutakapokutana Februari,” alisema Mbarawa.

Lukuvi atoa siku saba


Naye Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alitoa siku saba kwa wakuu wa idara za ofisi yake kuhakikisha wanaenda Kituo cha Uwekezaji (TIC), kukagua maeneo waliyopewa wakezaji kama yanaendelezwa kwa makusudi yaliyotarajiwa.

Lukuvi alisema, wapo wawekezaji ambao waliomba na kupewa maeneo ambayo wameyageuza matumizi bila taarifa, hivyo ni vyema wakafuatiliwa ili kuwabaini.

“ Tunafahamu wapo walioomba maeneo makubwa wakidai wanaendeleza miradi ya mifugo, viwanda wengine wameyatelekeza huku wakibadilisha matumizi wafuatiliwe tujue undani wake,” alisema.

Lukuvi ambaye pia ni Mbunge wa Isimani, alisema ana amini uendelezaji wa nyumba na makazi bora ya wananchi hauwezi kukamilika kwa kumtegemea mtu mmoja.

Kutokana na hali hiyo, amelitaka Shirika la Nyumba (NHC) kuja na mpango maalumu wa kuhakikisha wanawafanyia nini wananchi wenye hali za chini.

Kigwangalla atoa siku saba


Naibu Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangala, alitoa siku saba kwa wakuu wa mikoa, wilaya na halmashauri kuhakikisha wanasimamia zoezi la uondoaji taka zilizokusanywa Desemba 9, mwaka huu.

Kigwangala ambaye ni Mbunge wa Nzega Vijijini, alisema baada ya kupita kwa muda huo, atafuatilia na iwapo atagundua kuwapo kwa mtendaji aliyezembea agizo hilo, atamjulisha Rais Magufuli ili achukuliwe hatua.

“Hatutakuwa na utani katika hili kwa sababu hatutaki kuwa na wagonjwa wapya wa kipindupindu, tutakuwa vimbelembele kushtaki kwa rais na tutapendekeza hatua za kuwachukulia. Katika hili mtusamehe kwa sababu hatutakuwa tayari kufukuzwa,” alisema.

Mwigulu atoa siku tano


Akiwa mkoani Pwani, Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Mwigulu Nchemba, alitoa siku tano kwa Kampuni ya Sparkle Way lMT ya jijini Dar es salam ambayo ni mnunuzi wa zao la korosho, kulipa Sh bilion 3.4 ili wakulima wapewe fedha zao.

Alimtaka mnunuzi huyo kuhakikisha anaingiza fedha hizo katika akaunti ya Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Pwani (CORECU), ifikapo Jumatatu ya wiki ijayo.

“Nakuagiza kuanzia kesho (leo), hakikisha unaanza kuingiza fedha hizi kwenye akaunti ya chama cha ushirika kufikia Jumatatu wakulima waanze kulipwa,” alisema.

Kitwanga atoa siku mbili


Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ametoa siku mbili kwa Jeshi la Polisi kutoa ufafanuzi kuhusu changamoto mbalimbali zinazohusiana na uhalifu na usalama wa raia.

Kitwanga aliyasema hayo jijini Dar es salaam alipofanya ziara ya kutembelea kambi kuu ya polisi iliyopo barabara ya Kilwa maarufu kama Polisi Barracks pamoja na vituo vya polisi.

Miongoni mwa mambo ambayo waziri huyo alitaka apewe ufafanuzi ni suala zima la polisi kutokushiriki katika ulinzi wa Bandari na badala yake kuacha bandari ikilindwa na walinzi wa makampuni binafsi.

Pia alitaka ufafanuzi kuhusu kuendelea kushamiri kwa ugaidi unaoambatana na ongezeko la matumizi ya dawa za kulevya nchini, ambapo alitaka kupelekewa majibu ofisini kwake.

“Sote ni watu wazima, kama tulikosea kipindi cha nyuma hayo yameshapita lakini hatutavumiliana kama tutakosea huko tunapokwenda,” alisema Kitwanga.
 • via MTANZANIA

Your internet life to be reviewed during visa application to enter USA

WASHINGTON (AP) -- Lawmakers are working on legislation to ensure a person's online presence is reviewed as part of the vetting process for a visa to enter the United States.

The goal is to close security gaps that didn't pick up on one of the radicalized shooters in the San Bernardino, California, attack, who entered the country last year.

The Obama administration has directed the Homeland Security and State departments to review the process for screening people who apply for visas and to return with specific recommendations to close security gaps in the U.S. visa system, said White House spokesman Josh Earnest Monday.

Meanwhile, Rep. Bob Goodlatte, a Republican from Virginia who chairs the House Judiciary Committee, said the committee is working on legislation that would require online information, including social media accounts, be reviewed as part of the background check for visa applicants, including K-1 visas.

The Homeland Security Department said it is specifically reviewing policies on when authorities at U.S. Citizenship and Immigration Services can look at social media posts as part of the vetting process for would-be immigrants applying for certain visas.

"I think the president's top priority here is the national security and safety of the American people," Earnest said. "And that will continue to be the case with ensuring that this K-1 visa program is effectively implemented."

Tashfeen Malik, a Pakistani woman who the FBI says carried out the San Bernardino attack with her husband, came to the United States in 2014 on a K-1, or fianc, visa.

Earnest did not provide specifics of the security review for visas, but said one consideration going forward is resources.

The government approved more than 9.9 million visa applications during the 2014 budget year.

The Homeland Security Department said three pilot programs to specifically incorporate "appropriate" social media reviews into its vetting process were launched in the last year and the department is looking at other ways to use social media posts.

Malik's background check included at least one in-person interview in Pakistan and another after marrying Syed Farook, who was born in Illinois. She also had to provide fingerprints and a variety of background information. Authorities also vetted her, using intelligence and law enforcement databases.

The day after the attack, Facebook found a post on a page maintained by Malik pledging her and Farook's allegiance to the leader of the Islamic State group. The page was under an alias.

Authorities have said Malik and Farook exchanged messages about jihad and martyrdom online before they were married and while she was living in Pakistan.

The history of Malik's radicalization and her apparent online discussions about jihad have raised concerns about how she was able to pass a background check that the government has described as rigorous.

Sen. Richard Burr, a North Carolina Republican who heads the Senate Intelligence Committee, said on CBS' "Face the Nation" Sunday that Farook was radicalized as early as 2010 and Malik as far back as 2012, which would have been years before her visa was processed.

"We want to look at how our immigration process for a visa for a spouse broke down, that they didn't notice the radicalization," Burr said.

Certain DHS officials are currently allowed to look at social media posts as part of law enforcement investigations. The possible policy changes are being considered at USCIS, the DHS agency in charge of managing immigration benefits cases and interviewing green card applicants.

Malik was interviewed by USCIS after marrying Farook.

The FBI has said the couple was not on its radar until after the attacks and the shootout with police hours later that ended in their death.

"I don't think there are any indications that there was public use of social media that was missed, and we are looking into other questions about how they may have communicated to each other that avoided our detection," said Rep. Adam Schiff, D-Calif., after being briefed by law enforcement late last week.

Allowing people who vet visa applicants to review social media postings is no guarantee that a would-be immigrant who has radicalized views will be discovered. Facebook and Twitter users can make their pages private and aliases are routinely employed.

Sen. Dianne Feinstein, D-Calif., and Burr introduced legislation last week that would require social media companies to report to law enforcement any "terrorist activity" they became aware of - for example, attack planning, recruiting or the distribution of terrorist material.

But technology industry representatives say that would become a massive new liability for companies, chill free speech online and increase the number of reports funneled to law enforcement, making it difficult to find credible threats.

---

Follow Alicia A. Caldwell on Twitter at www.twitter.com/acaldwellap and Tami Abdollah atwww.twitter.com/latams

Implications of The Non-Citizen Atc, 2015 to Foreigners in Tanzania


Tamko la Wanasheria kuhusu hatua za baadhi ya Wakuu wa Wilaya


Wazanzibari nchini Marekani waandamana hadi ofisi za Umoja wa Mataifa


Wizara ya Afya yataka orodha ya watumishi wote waliosafiri nje baada ya agizo la Rais

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewaagiza wakuu wa vitengo vya wizara hiyo kuwasilisha taarifa za watumishi wake wote waliofanya safari za nje ya nchi baada ya katazo la Rais John Magufuli.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Donan Mmbando, ametoa siku tatu kwa wakuu hao wa idara kumfikishia taarifa hizo ofisini kwake na kuonya kwamba yeyote atakayethubutu kuficha ukweli atachukuliwa hatua.

Dokezo la Mmbando kwenda kwa wakuu wa idara linaeleza kuwa hadi Desemba 21 mwaka huu amri yake iwe imetekelezwa kwa ukamilifu.
“Naagiza wakuu wa Idara ya Rasilimali Watu (DHR), Meneja wa Ulinzi Data (DPM), Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Idara ya Habari, Teknolojia na Mawasiliano (H-ICT), Ofisa Ushirikiano (CO), Wakuu Ofisa Masoko (CMO), Usimamizi eneo la Rasilimali (DAHRM) na DPS wanipatie taarifa hiyo kabla ya Desemba 21, mwaka huu,” 
alisema Mmbando.

Dokezo hilo ambalo gazeti hili limeliona linaelekeza kuwa taarifa zitakazowasilishwa zionyesha nchi ambazo wahusika walikwenda, tarehe walizosafiri, madhumuni ya safari hizo, gharama ya usafiri, aliyezigharimia pamoja na kiasi cha fedha kilichotumika.

Sambamba na hayo, pia anaagiza kuwasilishwa kwa nakala ya kibali cha safari cha Katibu Mkuu kilichomruhusu mtumishi husika kusafiri safari ya nje.
“Taarifa hizo zitajumuisha pamoja na taasisi, hospitali zilizoko chini ya idara zenu,” 
aliagiza Mmbando.

Mbinu mpya: "Wahuni wa biashara wanavyowapiga chenga Majaliwa, Magufuli, Watanzania"

MTANDAO wa wafanyabiashara wasio waaminifu unaojihusisha na ukwepaji kodi wa bidhaa mbalimbali zinazoingizwa nchini kupitia bandari, umekimbia Dar es Salaam na kuhamishia shughuli zake kwenye mikoa ya Tanga na Mtwara.

Taarifa za uhakika zilizolifikia MTANZANIA Jumamosi zimeeleza kuwa wafanyabiashara hao na mawakala wao wameondoa maskani yao kwenye Bandari ya Dar es Salaam na kuyapeleka bandari za Tanga na Mtwara.

Imeelezwa kuwa kuhama kwa wakwepa kodi hao kumesababishwa na msako wa wakwepa kodi katika Bandari ya Dar es Salaam ulioanzishwa na Rais John Magufuli, ambaye amekwishawatia kitanzani baadhi ya maofisa wa Serikali wanaotuhumiwa kushirikiana na baadhi ya wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu kukwepa kulipa kodi halali ya Serikali.

Miongoni mwa maofisa wa Serikali waliosimamishwa kazi na wengine uteuzi wao kutenguliwa kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya kuikosesha Serikali mapato ni wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na Mamlaka ya Bandari (TPA).

Taarifa zimeeleza kuwa mbali na kuikimbia Dar es Salaam, mtandao huo wa wakwepa kodi pia umebadilisha mbinu za kupitisha mizigo isiyolipiwa kodi lengo likiwa kuwakwepa maofisa wa TRA.

Mmoja wa wafanyabiashara anayepitisha mizigo yake katika Bandari ya Dar es Salaam, ameliambia gazeti hili kuwa hivi sasa mawakala wa wakwepa kodi wanawahi makontena wanayoyalenga yanaposhushwa tu bandarini wanapakua mizigo yote na kuyaacha tupu hivyo wakifika maofisa wa TRA huyakuta yakiwa hayana mizigo.
“Wamemkimbia Rais Magufuli, wamemuacha Dar es Salaam wao wamepeleka maskani yao kwenye bandari za Tanga na Mtwara na hata mbinu za kufaulisha mizigo yao isiyolipiwa kodi nazo wamebadilisha.
“Sasa hivi wana mtindo mpya, wanavizia makontena yao yanapoingia tu bandarini wanapakua mizigo yote na kuyaacha tupu hivyo wanapokwenda maofisa wa TRA wanakuta hayana mizigo, yako tupu na wanapata hela nzuri kweli kwa sababu kufaulisha kontena moja siyo chini ya shilingi milioni tano,” 
alisema mfanyabiashara ambaye jina lake tunalihifadhi.

Mfanyabiashara huyo alieleza zaidi kuwa hivi sasa kazi ya kuvusha mizigo bila kulipiwa ushuru inafanywa kwa umakini mkubwa na mara nyingi imekuwa ikifanyika nyakati za usiku kwa msaada wa baadhi ya watumishi wa idara za Serikali.

Mfanyabiashara mwingine aliyezungumza na gazeti hili ambaye pia jina lake tunalihifadhi alieleza kuwa mtandao wa wafanyabiashara wakwepa kodi ni mkubwa na unawahusisha pia watumishi wa Serikali ambao wamekuwa katika ushirika huo kwa muda mrefu.

Alizitaja bidhaa zinazoongoza kupitishwa kwa magendo kuwa ni sukari inayotoka katika nchi za Brazil na India pamoja na makaa ya mawe yanayotolewa nchini Afrika Kusini.
“Wanaingiza sukari kutoka Brazil na India na ukichunguza sukari hiyo utabaini muda wake wa matumizi ya binadamu umekwisha. Wanapoipakuwa wanakwenda kuifunga katika mifuko mipya inayoonyesha kuwa ni sukari iliyozalishwa katika viwanda vya hapa nchini.
“Bandari ya Tanga hivi sasa ndiyo kichochoro cha wakwepa kodi na siku hizi kuna makaa ya mawe yanayotoka Afrika Kusini ambayo yanaingizwa kwa wingi hapa nchini ingawa hatujui yanapelekwa wapi.”
Alipoulizwa kuhusu ukweli wa taarifa hizo, Kaimu Meneja Mawasiliano wa TPA, Janeth Luzangi, hakukataa wala kukubali bali alionyesha mshangao huku akiahidi kufuatilia na kutoa tamko hivi karibuni.

Jitihada za kumpata Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Huduma kwa Walipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo, hazikuweza kufanikiwa na hata alipopigiwa simu yake ya kiganjani ilikuwa haipatikani.

Taarifa hizi zimepatikana ikiwa ni wiki kadhaa sasa baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kufanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam na TRA na kuibua upotevu wa makontena 329 ambayo pia hayakuwa yamelipiwa ushuru.

Kuibuliwa kwa kashfa hiyo ilifuatiwa na hatua za kutenguliwa kwa uteuzi wa aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade na kukamatwa kwa Kamishna wa Forodha, Tiagi Masamaki pamoja na maofisa wengine waliohusishwa nayo.

Sauti za Heri ya Krismasi / Merry Christmas - SpotLight Media


RC afuta posho za vikao kwa Watumishi na safari nje ya Wilaya, Mkoa


UPDATE: [video] Kifahamu kijiji cha Gamboshi, maarufu kwa "ushirikina"Raia wa India akamatwa kwa kutorosha Tanzanite ya shilingi bilioni 2.5/=Wakala wa Ukaguzi wa Madini nchini (TMAA) imetaifisha madini aina ya Tanzanite yenye thamani ya Sh2.5 bilioni yaliyokamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakati yakisafirishwa kwenda nje ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani alisema madini hayo yenye uzito wa gramu 2,871 yalikamatwa Desemba 15, wakati Jain Anarungi, raia wa India alipojaribu kuyatorosha kwenda nje ya nchi kinyume cha sheria.

“Madini yana thamani ya Sh 2.5 bilioni na tumeyataifisha kwa mujibu wa kifungu namba 6(4) cha sheria ya madini ya mwaka 2010, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2015 ” alisema Dk Kalemani.

Alisema katika kipindi cha kuanzia Julai 2012 hadi Novemba 2015, ukaguzi wa madini uliofanywa katika viwanja vya ndege kwa kushirikiana na vyombo vingine vya udhibiti, umebaini madini aina hiyo, dhahabu, fedha na madini mengine ya vito yenye uzito wa kilo 2,871 yenye thamani ya Sh16.4 bilioni katika matukio 87.

“Kuanzia Julai 2012 hadi Desemba mwaka huu thamani ya madini yaliyotoroshwa kwenda nje ya nchi kupitia viwanja vya ndege ni Sh 18.9 bilioni,” aliongeza.

Dk Kalemani alisema sekta ya madini nchini inachangia asilimia 3.5 ya uchumi na kwamba hadi kufikia mwaka 2025, uchumi wa sekta hiyo utakua kwa asilimia 10.

Staajabu kutoka Mwanza: Mtoto alelewa na mbwa "Tito" shauri ya ulevi wa wazazi


Free Online Course: Occupational Health in Developing Countries

Learn how occupational health can reduce illnesses or injuries caused by working conditions, with 
this free online course.

This free online course provides an introduction to occupational health – a part of public health that is neglected in many developing countries, where industrial activity is increasing, but the health and safety of workers is hardly discussed.
The course will teach you basic knowledge of occupational health and how to prevent the development of diseases and injuries, which are caused by working conditions in developing countries.
After the course, you will understand:
 • the basic concepts of occupational health;
 • the tasks and structure of occupational health services;
 • the most important risk factors for illness and injuries at workplaces globally;
 • the major occupational diseases;
 • the different steps in risk assessment at the workplace;
 • the association between workplace exposure and health effects;
 • and the main steps in preventing exposure to health hazards in the work environment.

Understand the role of different actors in occupational health

Through this course, you will be able to understand the interaction between the actors within occupational health, including employers, employees, health and safety personnel, occupational health services, occupational health clinics and the Labor Inspection.
You will also reflect on occupational health from a global perspective and know how to work on the issue in a low-income setting.
The course has been developed in association with:
 • Simon Mamuya, Gloria Sakwari, Vera Ngowi and Alexander Tungu of Muhimbili University of Health and Allied Sciences, Dar es Salaam, Tanzania
 • Wakgari Deressa of Addis Ababa University, Ethiopia
 • Akwilina Kayumba of the Occupational Safety and Health Authority, Dar es Salaam, Tanzania
 • Norwegian Agency for Development Cooperation (Norad)

REQUIREMENTS

This course is open to anyone, although previous degree-level study in medicine, dentistry, health sciences or natural sciences, and a good knowledge of English, will be helpful.

Wataalamu 6 wa ujenzi barabara Kinondoni wasimamishwa kazi


[video] Makazi katika bonde la Mkwajuni, Kinondoni yabomolewa


Moshi: Dawa za kulevya zateketezwa; Waathirika mtaa wa Njoro wazungumza


Maelezo ya Jaji Lubuva, NEC ya uchaguzi wa wabunge Ludewa na Masasi Mjini


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto) akifafanua kuhusu taarifa aliyoitoa iliyohusu Upigaji kura kwa Majimbo ya Masasi Mjini na Jimbo la Ludewa siku ya tarehe 20 Desemba, 2015 mara alipokutana na Waandishi wa Habari leo 19 Desemba, 2015 katika Ukumbi wa Tume uliopo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Uhcgauzi wa Tume hiyo BwanaKailima Ramadhani. (Picha: Benedict Liwenga-Maelezo)

Na Joseph Ishengoma, Maelezo

Majimbo ya Masasi Mjini mkoani Mtwara na Ludewa mkoani Njombe yanatarajia kufanya uchaguzi wa wabunge kesho (20.12.2015) ili kuwapata viongozi watakaoongoza majimbo hayo kwa kipindi cha miaka mitano.

Majimbo hayo hayakufanya uchaguzi tarehe 25.10.2015 kutokana na baadhi ya wagombea katika majimbo hayo kufariki dunia.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damiani Lubuva amewasihi wananchi kujitokeza na kupiga kura kwa amani na utulivu. Jaji Lubuva amesema hayo leo jijini Dar Es Salaam wakati akiongea na waandishi wa habari.

“Tume inawasihi na kuwashauri wananchi kujitokeza kupiga kura kwa amani. Hakuna sababu Masasi na Ludewa kuwa tofauti na majimbo mengine yaliyofanya uchaguzi kwa amani na utulivu,” alisema Lubuva.

Hata hivyo, Mwenyekiti huyo amewaonya Viongozi wa vyama vya siasa kutoingilia kazi ya tume katika uchaguzi huo.

“Viongozi wa vyama vya siasa wasiingilie kazi ya Tume ya Uchaguzi. Ulimwengu unatusifia kuwa uchaguzi uliopita ulifanyika kwa amani. Kila mwananchi, viongozi wa dini na vyama vya siasa tushirikiane wote kuhakikisha kuwa viashiria vya uvunjifu wa mani na utulivu vinaepukwa ili uchaguzi uwe huru, wazi na wa haki,” aliongeza Lubuva.

Jaji Lubuva alisisitiza kuwa watu wakisha piga kura waondoke vituoni ili kutowazuia wananchi wanaokuja kupiga kura isipokuwa Mawakala na wasimamizi wa uchaguzi wanaoruhusiwa kwa mujibu wa sheria.

Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Daftari la Wapiga Kura litakalotumika ndio lile lililotumika wakati wa uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25.10.2015.


Baada ya uchaguzi wa majimbo ya Ludewa na Masasi Mjini, litasalia jimbo la Kijitopele Zanzibar ambalo uchaguzi wake utategemea lini uchaguzi wa Zanzibar utakapofanyika.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva akitangaza taarifa ya Upigaji kura kwa Majimbo ya Masasi Mjini na Jimbo la Ludewa siku ya tarehe 20 Desemba, 2015 mara alipokutana na Waandishi wa Habari leo 19 Desemba, 2015 katika Ukumbi wa Tume uliopo Jijini Dar es Salaam.

Polisi: Yakana kufukuza askari wenye vyeti bandia; Inasaka waliosambaza uzushi


TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI


Katika siku za hivi karibuni, kumeibuka tabia ya baadhi ya watu kutoa taarifa za uzushi na uongo kutumia majina ya taasisi, mashirika ya umma na ofisi za Serikali na kueneza taarifa hizo katika mitandao ya kijamii kwa lengo la kupotosha wananchi.

Miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na taarifa kuhusu Jeshi la Polisi iliyosambazwa jana katika mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari ‘chujio Jesho la polisi, vyeti feki vyawaonndoa askari kazini’ Taarifa hiyo ni uzushi na hajatolewa na Jeshi la Polisi.

Kufutia hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini linapenda kukanusha taarifa hiyo ya uzushi ambayo haina ukweli wowote na inalengo la kuchafua taswira ya Jeshi la Polisi kwa jamii.

Jeshi la Polisi nchini limeanza upelelezi wa kuwatafuta watu wote waliohusika kueneza taarifa hiyo na kujifanya wao ni Jeshi la Polisi. Aidha, Tunatoa onyo kali kwa watu wote kuacha kutumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kufanya uposhaji na badala yake watumia mitandao hiyo kwa ajili ya ustawi wa jamii.

Imetolewa na:
Advera John Bulimba – SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.

----------- MWISHO -----------
 • Moja ya taarifa hiyo iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kama ambavyo wavuti.com iliuona kupitia WhatsApp inapatikana pia kwenye blogu kwa kubofya hapa.

Salam za rambirambi za Rais Magufuli kwa familia ya Rais mstaafu Kikwete

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye amepatwa na msiba mzito wa kufiwa na Dada yake Mpendwa Bi. Tausi Khalfan Kikwete kilichotokea jana tarehe 17 Desemba, 2015 huko nchini India.

Katika salamu hizo, Rais Magufuli amesema anaungana na familia ya Rais Mstaafu Kikwete katika kipindi hiki kigumu cha majonzi ya kuondokewa na mtu muhimu kwa familia."Kwa masikitiko makubwa nakupa pole nyingi Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete kwa kufiwa na dada yako ambaye alikua nguzo muhimu katika familia" Amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amemuomba Rais Mstaafu Kikwete kumfikishia salamu nyingi za pole kwa familia nzima na amewaomba wawe na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.Rais Magufuli amemuomba Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema aipumzishe roho ya marehemu Tausi Khalfan Kikwete mahali pema peponi, Amina.

Imetolewa na;
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

18 Desemba, 2015

Agizo la Waziri Kairuki kuhusu walioghushi na kutumia vyeti bandia kupata kazi Serikalini

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kushoto), akitoa maelekezo kwa Watumishi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri Kazi - UTUMISHI (picha: blog ya Wizara).

Kasi ya mawaziri wa Rais John Magufuli kufanya ziara za kushtukiza na kutoa maagizo kwa watendaji, imeanza kufumua ‘uozo’ baada ya jana kubainika kuwa watumishi 219 kati ya 704 wa Serikali wameajiriwa kwa vyeti vya kughushi.

Sakata hilo liliibuka baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki kutembelea idara, vitengo vya ofisi ya rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Kutokana na sakata hilo, Kairuki ameiagiza idara ya usimamizi wa rasilimali watu (Utumishi), kuwachukulia hatua watumishi hao waliotumia vyeti feki kupata ajira serikalini.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Rasilimali watu Utumishi, Leonard Mchau alisema Ofisi ya Rais, imehakiki watumishi 704, lakini 219 baada ya vyeti vyao kuhakikiwa na Baraza la Mitihani, NECTA, wamegundulika kuwa waliajiriwa kwa vyeti vya kughushi.

Mchau alisema baadhi ya watumishi waliobainika kujipatia ajira serikalini kwa vyeti vya kughushi wamekimbia vituo vyao vya kazi, kuwataka wananchi kuepuka mchezo huo wa kughushi vyeti.

“Ni kosa la jinai kughushi vyeti kwa lengo la kujipatia kazi. Endapo utagundulika utachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchi.” alisema Mchau.

Alisema ofisi hiyo inaendelea na uhakiki wa vyeti kwa watumishi wote wa umma nchini na matarajio ni kuwahakiki watumishi wote.

Akizungumzia suala hilo, Kairuki alisema, “Watumishi wote waliobainika kupitia HCMIS (Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara) wachukuliwe hatua stahiki.”

Waziri huyo alimtaka Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimali watu Utumishi, Emmanuel Mlay kutafuta ufumbuzi wa kumaliza tatizo la watumishi wanaotumia vyeti vya kughushi.

“Wasilisheni vyeti vyao baraza la mitihani kwa ajili ya uhakiki na baada ya uhakiki muwachukulie hatua stahiki watumishi wanaoonekana kutumia vyeti visivyo halali kwao” alisema Kairuki.

Itakumbukwa, Februari 24 mwaka huu, NECTA ilitangaza kuanza kuwasaka waajiriwa wote wanaotumia vyeti bandia katika ajira zao.

NECTA ilisema kuwa nchi kwa sasa inakabiliwa na tatizo la kuzagaa kwa vyeti bandia, hivyo limewataka waajiri nchini kote kushirikiana na baraza hilo kupeleka vyeti vya waajiriwa kwa ajili ya kukaguliwa.

Mkuu wa Idara ya Utawala na Fedha NECTA Daniel Matie alisema ili kufanikisha kupungua kwa tatizo la vyeti bandia nchini waajiri wanayo nafasi kubwa ya kushirikiana na NECTA katika ukaguzi wa vyeti ili kuchukua hatua za haraka kwa wale watakaobainika wanafanya kazi kwa njia ya kughushi vyeti.

Mei 21 mwaka jana, suala la vyeti bandia kwa watumishi wa umma na hata miongoni mwa wabunge, liliingia bungeni na kuzua mjadala mkali.

Vyeti feki bungeni

Wakati wa Bunge la Kumi, suala hilo lilileta mjadala mzito aliyekuwa Mbunge wa Ole, Rajabu Mohamed Mbarouk (CUF) alileta hoja ya kuitaka Serikali kueleza ni kwa nini NECTA inashindwa kudhibiti vyeti feki huku akisema kuna mchezo mchafu unaoathiri mfumo wa elimu nchini na uchumi wa Taifa.

Alisema kuzagaa kwa vyeti hivyo kunaifanya hadhi ya NECTA kushuka na kukosa imani hata katika jumuiya za kimataifa.

“Suala la vyeti feki ambalo Baraza la Mitihani la Taifa ndilo lenye dhamana na jukumu la kuhakikisha halitokei katika taifa limeonekana kama suala la kawaida,” alisema na kuongeza; “Vyeti feki ni vingi kiasi kwamba linasababisha kuajiriwa kwa watendaji ambao ni feki na mawaziri mizigo.”

Alisema kuzagaa kwa vyeti hivyo kunasababisha kupata makatibu wakuu na watendaji feki huku akisema katika Chuo cha Polisi cha Moshi walirejeshwa wadahiliwa 122 kwa sababu ya kukutwa na vyeti feki.

Akitoa ufafanuzi, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakati huo, Dk Shukuru Kawambwa alisema NECTA baada ya kugundua udanganyifu wa vyeti ilibadilisha namna ya kuchapa vyeti hivyo.

“Hivi sasa vyeti vinavyotolewa vina Serial number, jina la mhitimu katika cheti cha kuzaliwa na picha na kwamba siyo rahisi kughushi vyeti hivyo,” alisema.

Hata hivyo, Mbarouk alikataa ufafanuzi huo na kusema asilimia sita ya wanaoomba kazi nchini wana vyeti feki na kutaka kufahamu hatua zilizochukuliwa ikiwamo za kinidhamu katika kukabiliana na suala hilo.
 • via MWANANCHI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kushoto), akitoa maelekezo kwa Watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu-UTUMISHI. (picha: Blogu ya Wizara)

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, ameiagiza Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu (Utumishi) kuwachukulia hatua watumishi waliobainika kutumia vyeti visivyo vyao, kupata ajira serikalini.

Kairuki amesema hayo jana alipotembelea idara hiyo katika muendelezo wa ratiba yake ya kutembelea Idara/Vitengo vya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

“Watumishi wote waliobainika kupitia Mfumo Shirikishi wa Malipo ya Mishahara ya Watumishi wa Umma (Payroll), kwamba wametumia vyeti visivyo halali wachukuliwe hatua stahiki,” amesema Kairuki.

Amemtaka Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimali watu Utumishi, Emmanuel Mlay kutafuta ufumbuzi wa kumaliza tatizo la watumishi wanaotumia vyeti vya kughushi.

“Muwasilishe vyeti vyao Baraza la Mitihani kwa ajili ya uhakiki na baada ya uhakiki muwachukulie hatua stahiki watumishi wanaoonekana kutumia vyeti visivyo halali kwao,” alisisitiza.

Naye, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usimamizi wa RasilimaliwatuUtumishi, Leonard Mchau, alisema kuwa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, imehakiki watumishi 704 na kati ya hao, watumishi 219 baada ya vyeti vyao kuhakikiwa na Baraza la Mitihani, waligundulika waliajiriwa kwa vyeti vya kughushi.

Hata hivyo, Mchau aliongeza kuwa baadhi ya watumishi hao waliobainika kughushi vyeti ili kujipatia ajira serikalini, wamekimbia vituo vyao vya kazi. Mchau aliwaasa wananchi kuepuka mchezo wa kughushi vyeti, ili kujipatia ajira Serikalini.

“Ni kosa la jinai kughushi vyeti kwa lengo la kujipatia kazi, sasa endapo utagundulika umeghushi vyeti, utachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchi,” alifafanua Mchau. Kwa sasa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma inaendelea na uhakiki wa vyeti kwa watumishi wote wa umma nchini mpaka kila mmoja atakapohakikiwa.

Salamu za rambirambi za Rais Magufuli kwa ajali ya basi Iringa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza kufuatia ajali ya basi la kampuni ya New Force kugongana na lori, na kusababisha vifo vya watu 12, na wengine 15 kulazwa Hospitali.

Ajali hiyo imetokea tarehe 18 Desemba, 2015 Majira ya saa nane mchana katika Kijiji cha Mahenge, Wilaya ya Kilolo Mkoani IRINGA ambapo Basi la kampuni ya New Force lenye namba T 483 CTF lililokuwa limebeba abiria 49 limegongana na Lori la Kampuni ya Reign-ford Limited lenye namba T 616 BEF na Tela lake lenye namba T 320 DEF lililokuwa na shehena ya mbao.

Rais Magufuli amemuomba Mkuu huyo wa mkoa kufikisha salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote ambao wamepoteza ndugu zao katika ajali hiyo mbaya"Nimesikitishwa sana na kutokea kwa ajali hii, ninawapa pole nyingi wote waliopoteza ndugu zao na ninawaombea Majeruhi wote wapone haraka ili waungane na familia zao na kuendelea na shughuli zao za maendeleo" amesema Rais Magufuli.

Amewaombea marehemu wote kwa Mwenyezi Mungu ili azipumzishe roho zao mahali pema peponi, Amina.Aidha Dkt. Magufuli ametoa wito kwa watuaji wote wa barabara hususani madereva kuwa waangalifu waendeshapo vyombo vya usafiri na amewakumbusha wananchi wanaotumia barabara kwa kusafiri ama kusafirisha mizigo kutoa ushirikiano kwa vyombo husika pale wanapobaini kuwepo vitendo ambavyo ni chanzo cha ajali.

Imetolewa na; Gerson Msigwa,
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
18 Desemba, 2015

Taarifa: Mfumo rajisi wa TCRA - Simu kuorodheshwa katika makundi: Nyeupe, Kijivu, Nyeusi

UTANGULIZI:
Vifaa vya mawasiliano vya mkononi – hususan simu za kiganjani na vifaa vya mawasiliano vya kiganjani (tablets) – vina namba maalum inayovitambulisha. Namba hiyo inajulikana kama IMEI ambacho ni kifupi cha International Mobile Equipment Identity.

Kifungu cha 84 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya 2010 kinataka kuwepo kwa mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi. Rajisi hii inajulikana kwa kiingereza kama Central Equipment Identification Register, kwa kifupi CEIR. Sheria inataka rajisi hiyo ihifadhiwe na kuendeshwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

Aidha Kanuni za mwaka 2011 za EPOCA kuhusu mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi inawataka watoa huduma wa mawasiliano yanayotumia vifaa vya mkononi kuweka mfumo wa kudumu wa kumbukumbu za namba tambulishi (Equipment Identity Register – EIR) za vifaa vya mkononi vinavyotumika kwenye mitandao yao.

Mfumo huu wa kielektroniki ambao utahifadhi kumbukumbu za namba tambulishi za vifaa vya mawasiliano vya mkononi una lengo la kufuatilia namba tambulishi za vifaa vinavyoibiwa, kuharibika, kupotea au ambavyo havikidhi viwango vya matumizi katika soko la mawasiliano.

Vifaa vyote vya mawasiliano vya mkononi ambavyo vimeibiwa, vimeharibika, kupotea au visivyokidhi viwango vya matumizi katika soko la mawasiliano havitaweza kufanya kazi kwenye mitandao ya mawasiliano kutumia vifaa vya mkononi.

UFAFANUZI
Taarifa kwenye mfumo huu wa rajisi zitakuwa na aina tatu za kumbukumbu; ambazo ni orodha ya namba tambulishi ambazo vifaa vyake vinaruhusiwa, orodha ya namba tambulishi ambazo zimetolewa taarifa kuwa zimefungiwa na namba tambulishi ambazo zimefungiwa kwa muda au kuruhusiwa kwa muda.

Orodha Nyeupe:
Orodha ya vifaa vya mkononi vya mawasiliano vinavyoruhusiwa kutumika katika mitandao ya huduma za simu za kiganjani

Orodha Nyeusi:

Orodha hii ni ya namba tambulishi ambazo zimefungiwa na mtoa huduma kwenye mfumo wao wa EIR na kutumwa kwenye mfumo wa CEIR kwa ajili ya kufungiwa ili zisitumike kwenye mitandao mingine ya simu za kiganjani kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na kukubaliwa miongoni mwa watoa huduma. Simu zote za mkononi zilizoibiwa au kupotea zitafungiwa ndani ya saa 24 ili zisitumike kwenye mtandao wowote wa simu za mkononi Tanzania.

Ikitokea simu ya mtumiaji ikafungiwa kimakosa, anatakiwa kutoa taarifa mara moja kwa mtoa huduma wako kwa ajili ya kuifungua. Watoa huduma wanatakiwa wafungulie, ndani ya saa 24, simu zote zilizofungwa kimakosa.

Orodha ya kijivu:

Orodha hii ni ya namba tambulishi ambazo zimefungiwa au kufunguliwa kwa muda kwa lengo la kuanzisha mchakato wa kuzifuatilia.

FAIDA ZA MFUMO WA RAJISI YA NAMBA TAMBULISHI

Mfumo huu wa rajisi una faida zifuatazo:
1. Kuthibiti wizi wa simu. Iwapo mtu atapoteza au ameibiwa simu ya kiganjani na akatoa taarifa kwa mtoa huduma, simu hiyo itafungiwa isiweze kutumika kwenye mtandao mwingine wowote wa simu za kiganjani. Mteja anaponunua simu ni lazima adai risiti halali na halisi na pia garantiii ya angalau miezi 12. Mteja anatakiwa aihifadhi risiti hiyo angalau kwa miezi mitatu. Baada ya hapo, iwapo simu imekuwa inatumika, taarifa za matumizi zinaweza kutumika kama uthibitisho mbadala wa milki ya simu husika.

2. Kuhimiza utii wa sheria: Kifungu cha 128 cha EPOCA kinamtaka mtumiaji wa simu kutoa taarifa ya kupotea au kuibiwa kwa simu au laini ya simu. Kifungu cha 134 kinayataka makampuni ya simu kutokutoa huduma kwa simu ambayo imefungiwa kama ilivyoelezwa hapo juu. Mara tu mteja anapopoteza simu yake ya kiganjani anatakiwa kutoa taarifa kwa kituo cha Polisi cha karibu ambapo atapewa namba ya kumbukumbu ya taarifa ya tukio, maarufu kama RB.

Anatakiwa aende kwa mtoa huduma kutoa taarifa ya tukio akiwa na hiyo RB na uthibitisho wa umilki wa simu iliyopotea ( risiti aliyopewa wakati wa kununua iwapo itakuwepo). Mtoa huduma kwanza atahakiki umilki wa simu iliyopotea au kuibiwa na atampatia mteja namba ya kumbukumbu kwamba simu hiyo imefungiwa isutumike kwenye mitandao ya simu na hatimaye ataifungia simu hiyo ndani ya saa 24.

3. Kujenga misingi ya matumizi ya simu halisi, zisizo bandia. Mtumiaji ataweza kutambua iwapo simu aliyo nayo inakidhi viwango, ni halisi na sio bandia.

KUTAMBUA NAMBA TAMBULISHI
Ili kutambua namba tambulishi ya simu ya kiganjani au vifaa vya mawasiliano ya kiganjani, mtumiaji anatakiwa aandike tarakimu *#06# kwa kutumia kifaa chake. Baada ya kufanya hivyo, kutaonekana namba ndefu. Mtumiaji anatakiwa kuandika namba hiyo kama ilivyoonekana kwenye kifaa chakena kuihifadhi katika hali ya usalama kwa ajili ya rejea ya baadae.

Baada ya hapo mtumiaji atume ujumbe mfupi wenye hiyo namba tambulishi kwenda namba 15090. Atapokea meseji itakayomjulisha kuhusu hali halisi ya simu yake ya kiganjani. Mtumiaji atapokea ujumbe kuhusu uhalisia wa simu yake. Majibu yatakayokuja yatasomeka: Kama IMEI haioani na aina ya simu yako, wasiliana na aliyekuuzia. Usipoweza,ibadilishe kabla ya Juni 2016 kwani simu hiyo inaweza kuwa BANDIA.

HATUA ZA KUCHUKUA IWAPO SIMU ITAONEKANA HAIKIDHI VIWANGO, SI HALISI NA NI BANDIA

Mtu yeyote ambaye atatambua kwamba simu yake ya kiganjani si halisi,ni bandia na haikidhi viwango atapewa muda wa kuendelea kutumia simu hiyo. Baada ya muda huo kumalizika, simu hiyo itaingizwa katika orodha nyeusi na kufungiwa isitumike kwenye mitandao mingine yoyoye ya simu za kiganjani.

Watumiaji wote wenye simu za kiganjani ambazo namba tambulishi zao zinaonyesha kwamba simu hizo si halisi, ni feki na hazikidhi viwango watagharamia ununuzi wa simu nyingine.

Watumiaji wote ambao namba tambulishi za simu zao zinaonyesha kwamba vifaa hivyo si halisi, ni feki na havikidhi viwango watatakiwa kubadilisha simu hizo na kupata zinazokidhi viwango na halisi katika muda wa miezi sita kuanzia siku ya uzinduzi wa mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa simu za kiganjani.

Ni vyema ifahamike kwamba simu zote za kiganjani na vifaa vya mawasiliano vya kiganjani (tablets) ambazo zitakuwa na namba tambulishi bandia zitafungiwa kuanzia 16 Juni 2016.

HITIMISHO

Mfumo wa Rajisi ya Namba za Utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi una lengo la kuwahakikishia watumiaji usalama wakati wanapotumia vifaa hivyo vya mawasiliano, vikiwemo simu za kiganjani na vifaa vya mawasiliano vya kiganjani (tablets). Uanzishwaji wake ni sehemu ya kutekeleza matakwa ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya 2010. Ni vyema watumiaji wakazingatia maelekezo kuhusu utaratibu wa kuhakiki namba tambulishi, kutoa taarifa wanapopoteza au kuibiwa simu.

Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
18 December 2015

Waziri Prof. Muhongo afuta likizo TANESCO na kuagiza gharama ya umeme ishushwe


Bei ya umeme inatarajia kushuka wakati wowote kuanzia sasa baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuliagiza Shirika la Umeme (TANESCO), kushusha gharama za nishati hiyo.

Katika hatua nyingine, Waziri huyo amefuta likizo za wafanyakazi wa shirika hilo ili washughulikie tatizo la umeme nchini huku akisisitiza kuwa hataki kusikia kukatika katika kwa umeme.

Profesa Muhongo alitoa maagizo hayo jana jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika mtambo wa kuzalisha umeme wa Tegeta Gas Plant, ambapo alikwenda kwa ajili ya kukagua mitambo hiyo ili kuona kama yote inafanyakazi.

Akitoa maelezo ya mtambo huo, Meneja Mohamed Kisiwa alisema wana mitambo mitano na wana uwezo wa kuzalisha Megawati 42 kila saa.

Alisema gharama ya uzalishaji umeme kwa uniti moja ni Sh. 90 na wamekuwa wakiuza kwa Sh. 180 hadi 187.

Profesa Muhungo alisema kwa maelezo ya meneja huyo, inaonyesha umeme wanaozalisha wanapata faida mara mbili hivyo alisema kuna uwezekano mkubwa wa kushusha gharama za umeme.

Aliagiza maofisa wa wizara yake na wa shirika la Tanesco wakutane leo ili wajue umeme huo utashushwa kwa kiwango gani.

“Utauzaje umeme mara mbili ya gharama za uzalishaji, tunataka kuwapunguzia wananchi bei ya umeme na kwenye mkutano wetu wa kesho (leo) tutajadili kupunguza bei ya umeme..haya mahesabu hayajakaa sawa maana unazalisha uniti moja kwa Sh. 90 na kuuza kwa Sh. 180 tutajadiliana mpunguze,” alisema.

TANESCO yataja wadaiwa wakubwa na kusimamisha kazi maofisa 10 walioihujumuMkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme (TANESCO), Felchesmi Mramba, amewasimamisha kazi maofisa 10 wakiwamo wahasibu waandamizi na mafundi kwa kusababisha upotevu wa mapato zaidi ya Sh. milioni 100.

Hasara hiyo ilitokea katika mfumo wa mita kupitia minara ya simu za mkononi na faini Sh. milioni 198.1 za wateja waliobainika kuiba umeme kwa kuchakachua mita zao.

Hata hivyo, shirika hilo limefanikiwa kuokoa fedha hizo zilizotokana na umeme wenye thamani ya Sh. 100,248,386.42 uliotumika bila kulipiwa pamoja na faini kutoka kwa wateja waliojihusisha na wizi wa umeme Sh. 198,105,928.68.

Kadhalika, shirika baada ya kufanya msako mkali limefanikiwa kukamata taasisi binafsi na za serikali pamoja na watu binafsi wakijihusisha na kuhujumu shirika hilo,ikiwemo Shule ya Sekondari ya Jangwani (Sh. 11,023,238.00), Diwani wa Kata ya Sinza C, Joseph Marandu (Sh. 3,443,555.00), Royal Oven Bakery Kawe, (Sh. 4,112,614.00), Havan Hotel, Mbezi Beach (Sh.1,847,913.00) na Kampuni ya Simu ya Viettel Mtwara (Sh. 524,554.76).

Wengine ni, Kampuni ya Saffa Petroleum ya Mkoani Pwani (Sh. 16,105,235.00), Msanii wa Filamu Nchini, Wema Sepetu (Sh. 8,200,496.20) na Kampuni ya Leadcom (Sh. 13,694,632.81).

“Zoezi hili ni endelevu kwa nchi nzima na tutaendelea kuwakamata, kuwatangaza na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale watakaobainikiwa kulihujumu shirika hatutaogopa wadhifa wala umaarufu wa mtu ama taasisi” alisema Mramba katika mkutano wake na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.

Alisema mapema Desemba 6, mwaka huu alitoa taarifa kwa wale wote wanaojihusisha na wizi wa umeme ama wenye mita zenye matatizo, lakini walijisalimisha ni watu 30 na kati ya watu 2,156 waliokaguliwa 138 walikutwa na dosari mbalimbali katika mita zao na walilipishwa faini.

Akifafanua, alisema fedha zinazotakiwa kulipwa ni Sh. milioni 198.1 na zilizokwishalipwa ni Sh. milioni 44.9 wakati waliofikishwa kwenye vyombo vya sheria ni watu 37 kwa makosa mbalimbali. Akizungumzia kuhusu hatua atakazowachukulia watumishi 10 aliowasimamisha kazi, Mramba alisema uchunguzi unaendelea na fedha wanazodaiwa kuzifanyia udanganyifu zitalipwa na kampuni ya simu husika.

Mramba alisema ili kuhakikisha kero za huduma zinamalizika, katika kila ofisi ya kitengo cha dharula kutakuwa na Ofisa wa huduma kwa wateja na mhandisi ambao watasimamia muda na ubora wa huduma wanazopata wateja baada ya kutoa taarida za dharura.

“Kuanzia sasa kazi ya mafundi inapokamilika maofisa hawa niliowataja watawajibika kuwapigia simu wateja waliotoa taarifa kuhakiki kama kazi zimefanywa kwa wakati na mteja ameridhika … utaratibu huu utaanza leo (jana),” alisema Mramba.