International Project Manager & Advisor on Value Chain Development - TanzaniaOrganization: Belgian Development Agency
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 15 Jan 2016

International Technical Advisor on Strategic Marketing - Tanzania

Organization: Belgian Development Agency
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 15 Jan 2016

Volunteer Legal Advocate - Asylum Access Tanzania

Organization: Asylum Access
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 26 May 2016

Consultancy for profiling of in and out of school children & geographic mapping of schools

Organization: UN Children's Fund
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 07 Jan 2016

Consultancy for profiling of in and out of school children & geographic mapping of schools

Organization: UN Children's Fund
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 07 Jan 2016

Job opportunity: ADD International Country Director - Tanzania

Organization: ADD international
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 11 Jan 2016

Job opportunity: Programme Director

Organization: Children in Crossfire
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 18 Jan 2016

Job opportunity: Programme Development and Funding Manager

Organization: Voluntary Service Overseas
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 31 Dec 2015

Waziri Mahiga azungumza na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa waliopo Tanzania


Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Augustine Mahiga akizungumza kwa mara ya kwanza kwenye mkutano uliomkutanisha na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa yaliyopo hapa nchini. Mkutano huo ulikuwa na lengo la Waziri kujitambulisha ambapo pia alitoa taarifa mbalimbali ikiwemo umuhimu wa ushirikiano wa Tanzania na nchini mbalimbali; hali ya kisiasa huko Zanzibar baada ya uchaguzi na mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Burundi.


Sehemu ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini wakimsikiliza kwa makini Balozi Mahiga (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao, wa kwanza kushoto ni Balozi wa Rwanda nchini, Mhe. Eugene Segore Kayihura (wa kwanza kushoto), Balozi wa Marekani nchini, Mhe. Mark Children (wa pili kutoka kushoto), Balozi wa Oman nchini Mhe. Soud Al Mohammed Al-Ruqaish


Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini nao wakimsikiliza kwa makini Waziri Mahiga (hayupo pichani)


Sehemu nyingine ya Mabalozi na Makaimu Balozi waliohudhuria mkutano huo. Balozi wa China nchini Mhe. Lu Youqing (wa pili kutoka kulia kwenye mstari wa pili), Naibu Balozi wa Misri, Bw. Moataz Kareem Elbahnasawi (wa kwanza kulia mstari wa mbele).


Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Dkt. Suzan Kolimba naye alipata fursa ya kujitambulisha kwa Mabalozi na Wakuu hao wa Mashirika.


Sehemu nyingine ya Mabalozi wakimsikiliza Naibu Waziri Kolimba (hayupo pichani) alipokuwa akijitambulisha kwao.


Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Afrika Mashariki, Mhe. Joyce Mapunjo na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika nao wakimsikiliza kwa makini Waziri Mahiga (hayupo pichani).


Sehemu ya Wakurugenzi wa iliyokuwa Wizara ya Afrika Mashariki


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Bi. Amisa Mwakawago na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Bw. Abdallah Mtibora


Waziri Mahiga akiendelea kuzungumza


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Bi. Mindi Kasiga akizungumza


Sehemu ya Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka iliyokuwa Wizara ya Afrika Mashariki


Waziri Mahiga akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa, na Wakuu wa Mashariki ya Kimataifa nchini.


Waziri Mahiga (kushoto) akisalimiana na Naibu Balozi wa Misri, Bw. Moataz Kareem Elbahnasawi (katikati) na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Itifaki, Bw. James Bwana


Naibu Waziri akisalimiana na Balozi wa Demokrasia ya Kongo Mhe.Halfan Juma Mpango


Waziri Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa nchini


Picha ya pamoja

Taarifa: Ziara ya Waziri Mahiga nchini Burundi na Uganda

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

ZIARA YA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI, KIKANDA NA KIMATAIFA, MHE. DKT. AUGUSTINE MAHIGA NCHINI BURUNDI NA UGANDA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augistine Mahiga (Mb), atafanya ziara ya kikazi ya siku mbili katika nchi za Uganda na Burundi kuanzia tarehe 23 Desemba, 2015.

Ziara hiyo ya Mhe. Mahiga inafanyika kufuatia maelekezo ya Mhe. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ya kumtaka kwenda kufuatilia hali nchini humo ili kuiwezesha Jumuiya kushughulikia mgogoro wa kisiasa unaondelea nchini Burundi.

Akiwa Uganda, 2015, Mhe. Mahiga atakutana kwa mazungumzo na Mhe. Crispus Kiyonga, Waziri wa Ulinzi wa Uganda ambaye anaendelea na jukumu hilo la usuluhishi wa mgogoro wa kisiasa wa Burundi kwa niaba ya Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Uganda.

Aidha, Mhe. Waziri atakutana na Mshauri wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali nchini Burundi, Ndg. Jamal Benomar.

Mhe. Waziri atasafiri siku hiyo hiyo kuelekea Bujumbura, Burundi ambapo atakutana na wadau mbalimbali wa mgogoro huo kabla ya kukutana na Mhe. Pierre Nkurunziza, Rais wa Jamhuri ya Burundi. Mhe. Waziri atarejea Dar es Salaam tarehe 24 Desemba, 2015 baada ya kukamilika kwa ziara hiyo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam

23 Desemba, 2015

Wananchi wamtaka Mkurugenzi wa Halmashauri akazoe taka alizotupa kijijini kwao

Wananchi wa kijiji cha Shenda
Wananchi wa kijiji cha Shenda katika kata ya Masumbwe wilayani Mbogwe mkoani Geita Wameitaka ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbogwe, kuziondoa takataka zilizowekwa kijijini kwao kufuatia zoezi la usafi la December 9, mwaka huu Lililofanyika nchi nzima.

Wananchi hao wanakijiji hao wamesema kuwa wanashangazwa na kitendo cha halmashauri ya wilaya kutuma takataka katika kijiji chao licha ya kwamba hakuna dampo la uchafu eneo hilo.

Wameongeza kuwa taka hizo ni hatari kwa afya zao kwani zimetupwa karibu na eneo la shule ya msingi,Makazi ya watu na vibanda vya mama ntilie hali inayozua hofu ya kuzuka kwa magonjwa ya mripuko kwani taka hizo zimeanza kuoza na kusambaa katika makazi ya watu kipindi hiki cha masika.

Sambamba na hayo wameshangazwa na maamuzi ya ofisi ya mkurugenzi kutupa taka hizo katika kijiji chao licha ya kuwa yapo maeneo mengi ya wazi ambayo yangeweza kutumika kutupa taka hizo ambazo kwa sasa zimekuwa kero katika kijiji chao hasa kutoa harufu mbaya na funza.

Kwa mujibu wa kaimu mtendaji wa kijiji cha Shenda Joseph Jaseda, sehemu zilizotupwa taka hizo ni makazi ya watu na walipouliza kuhusu hatua hiyo waliambiwa kuwa gari la kuzoa taka liliharibika sehemu hiyo na ndipo walipoamua kutupa taka hizo.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Masumbwe Shimo Kiyuyu amesema kuwa alifikisha malalamiko ya wananchi kwa mkurugenzi na Mkurugenzi akatoa gari ili uchafu uzolewe lakini juhudi hizo ziligonga mwamba kutokana na gari hiyo kwenda eneo la uchafu bila wazoaji wa taka hizo.

Kwa upande wake Afisa Afya wa halmashauri ya wilaya ya Mbogwe Edward Lazaro amekiri uchafu huo kutupwa katika maeneo hayo na kusema kuwa baada ya wananchi kulalamika walienda kuweka dawa ya kuwa wadudu katika taka hizo na kwamba hawajazihamisha kutokana na taka hizo kutokuwa na madhara kwa wananchi.

Kauli ya Serikali kuhusu habari iliyochapishwa gazetini, "JPM kutolipa makocha Stars"

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inakanusha taarifa zilizoandikwa katika gazeti la Mwananchi la tarehe 24.12.2015 yenye kichwa cha habari “JPM kutolipa makocha Stars”.

Serikali kupitia Wizara inayohusika na michezo haijatoa tamko la kutowalipa makocha wanaofundisha timu ya Taifa Stars kama ilivyoripotiwa na gazeti hilo.

Suala la malipo ya makocha wa Taifa Stars linashughulikiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za Serikali, pindi maamuzi yatapofikiwa, serikali itatoa maelekezo kama itaendelea kuwalipa au la.

Serikali ya Awamu ya Tano inathamini michezo yote ikiwemo mpira na miguu , kwa hiyo itaendelea kushirikiana na Vyama vya vyote vya michezo na wadau wote wa michezo kwa ujumla katika kuhakikisha kuwa michezo inaimarika na kuwa chanzo cha ajira kwa vijana nchini.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI (MAELEZO)
24 DESEMBA, 2015

Waziri atoa maagizo kwa wanaoajiri wageni na wakala wwanaosaidia Watanzania kuajiriwa ng'ambo

WAZIRI  Jenista Mhagama (Mb), akisisitiza kutoa kipaumbele cha ajira kwa wataalam wa kitanzania wenye taaluma sawa na wataalamu wasio watanzania wakati alipokutana na Menejimenti ya Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TAESA), tarehe 23 Desemba, 2015, (katikati) ni Naibu Waziri, Anthony Mavunde (Mb), na Kaimu Mkuu mtendaji wa Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TAESA), Boniface Chandaruba. (Picha na Ofisi ya Waiziri Mkuu)
Na. Mwandishi Maalum.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, (Sera,Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), amewaagiza waajiri wote nchini kutoa kipaumbele cha ajira kwa watanzania wenye sifa za ajira ambazo ni sawa na zile walizonazo wataalamu wa kigeni kama sheria ya Kuratibu Huduma za Ajira kwa Wageni wa nchi za nje Na.1 ya mwaka 2015 inavyowaelekeza.

“Sheria hii ya Kuratibu Huduma za ajira inatoa mwongozo ambao inawataka wale wote wanaokuja hapa nchini kwa minajili kutafuta ajira lazima wawe na kibali cha Kamishina wa Kazi wa hapa nchini, lakini pia Kamishina wa kazi ili atoe kibali hicho lazima ajiridhishe kuwa kibali anachotaka kutoa kama kweli hakuna mtanzania mwenye sifa na uwezo wa kufanya kazi husika na ndiyo sasa atoe kibali, tukizingatia haya tutakuwa tunatoa kipaumbele cha ajira kwa watanzania katika sekta mbalimbali” Amesema.

Amesema hayo wakati akizungumza na Menejimenti ya Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TAESA), alipokutana nayo Jijini Dar es Salaam, Desemba 23, akiwa ameambatana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Anthony Mavunde (Mb), kama sehemu ya kujifunza majukumu na kuelewa changamoto zinazozikabili Taasisi na Idara zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Alibainisha kuwa kwa mwaka huu tayari watanzania wenye sifa za kuajirika 16,000 wamejisajili kwa Wakala huyo na watanzania 8,000 wameunganishwa na waajiri, lengo ikiwa ni kutoa kipaumbele kwa watanzania katika ajira hasa vijana katika soko la ajira la ndani na nje ya nchi.

Bibi Mhagama alisema: “Wakala wanalojukumu la kuwaunganisha Watanzania na hasa vijana katika soko la ajira la ndani na nje ya nchi. Hivyo jukumu hili linawalazimu wafanye utafiti wakuelewa ni sehemu gani kuna nafasi za ajira kwa waliosoma elimu ya juu na wale wenye elimu ya kati, lakini pia na kuwasaidia Watanzania hao wanaofika kwa Wakala huyo kuandaliwa ili waweze kuajirika” alisema.

Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TAESA) ilianzishwa kwa sheria ya Huduma za Ajira ya mwaka 2007 leno ikiwa ni kuwasaidia watanzania kupata kazi zenye staha na zenye mazingira rafiki kwa kazi husika ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanalipwa mishahara inayostahili kwa mujibu sheria za hapa nchini.

Prof. Muhongo aahidi milioni 100 kuanzisha mfuko wa elimu wa jimbo lake

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza jambo wakati wa kikao chake na wananchi wa jimbo hilo pamoja na wadau wa maendeleo.
Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameanza kwa kishindo kutekeleza ahadi zake kwa wananchi wa jimbo hilo na huku akiahidi maendeleo kwa kasi zaidi.

Profesa Muhongo alidhihirisha hayo juzi katika kijiji cha Murangi, Mkoani Mara katika kikao chake na baadhi ya wananchi wa jimbo hilo, watendaji wa Halmashauri ya Musoma Vijijini na madiwani huku lengo la kikao likiwa ni kujadili mipango na miradi ya uchumi na maendeleo ya jimbo hilo.

Katika kikao hicho, iliazimiwa kuanzishwe Mfuko wa Elimu wa Jimbo ambapo Profesa Muhongo aliahidi kutoa kiasi cha Shilingi Milioni mia moja ambazo atakopeshwa na Bunge kwa ajili ya kununulia gari.

Alisema badala ya kununulia gari, fedha hiyo ataiingiza kwenye Mfuko huo ili kuleta maendeleo kwenye jimbo hilo. “Dhamira yangu ni kuhakikisha jimbo letu linasongo mbele kiuchumi na kimaendeleo na siyo maneno bila mipango madhubuti,” alisema.

Katika maelezo yake ya mikakati ya maendeleo kwa jimbo hilo, Profesa Muhongo alisema kufikia Mwezi Januari mwanzoni, ataanzisha Ofisi tano za Mbunge jimboni humo ili kufikisha huduma kwa wananchi kiurahisi.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria Kikao cha Profesa Muhongo
Alisema Ofisi hizo zitakuwa na mtumishi mmoja ambaye ataajiriwa na Mbunge na atapatiwa vitendea kazi vya kuanzia ambavyo ni pikipiki ili kumuwezesha kuwafikia wananchi kirahisi na kompyuta mpakato (laptop) kwa ajili ya kutunza taarifa na mawasiliano.

Profesa Muhongo alitaja maeneo ambayo ofisi hizo zitaanzishwa kuwa ni kijiji cha Murangi ambapo ndio patakua makao makuu, Busekela, Sangana, Mugango na Nyegine na alitoa wito kwa vijana wa maeneo hayo kuomba kazi kwa nafasi husika na kwamba watakaofaulu watatakiwa kuwepo maeneo hayo ili kila watakapohitajika waweze kupatikana kiurahisi.

Alisema usaili wa kuwapata watumishi hao utafanyika tarehe 26 na 27 mwezi huu na watakaofaulu wataanza kazi tarehe 1 Januari, 2016 kwa uangalizi wa kipindi cha miezi mitatu (probation period) na alitaja vigezo vitakavyotumika kwenye kuwapata kuwa ni elimu kuanzia kidato cha nne na ujuzi wa kompyuta.

Mbali na hilo, katika kuimarisha elimu jimboni humo, Profesa Muhongo ametoa vitabu vya kujifunzia vipatavyo 20,000 (elfu ishirini) katika shule mbalimbali na huku kipaumbele kwa wakati huu ni kwa shule zilizofanya vibaya kwenye matokeo ya mwaka huu.

Alisema tayari ameagiza vitabu vingine 22,000 kutoka nchini Marekani na vitakapoingia nchini ameagiza Madiwani kuvisambaza kwenye shule ambazo hazina vitabu vya kutosha.

Mbunge huyo alisema kwa kutumia Mfuko huo wa Elimu wa Jimbo, pamoja na fedha za Halmashauri, kila shule itapatiwa huduma ya umeme, maji pamoja na kujenga na kukarabati shule hizo pamoja na nyumba za walimu.

Akizungumzia suala la miundombinu ya barabara, Mbunge huyo aliahidi kusimamia ujenzi wake ambapo alisema barabara kutoka Musoma mjini hadi makao makuu ya jimbo itajengwa kwa kiwango cha lami na alisema tayari tathmini imeanza na itakamilika mwishoni mwa mwezi huu.

Mbali na hilo, kwa barabara zilizo chini ya Halmashauri, Profesa Muhongo aliagiza madiwani wakae na kupitisha bajeti kwa ajili ya kukarabati barabara hizo na aliagiza kikao hicho kifanyike kabla mwezi huu haujamalizika.

Kuhusu suala la Afya, Profesa Muhongo alisema tayari ameagiza gari la wagonjwa ambalo linatarajiwa kuingia nchini ndani ya wiki mbili zijazo.

Kikao hicho cha maendeleo ya jimbo la Musoma vijijini kilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo kutoka ndani na nje ya nchi miongoni mwao kukiwa na wazawa wa jimboni humo ambao kwa sasa wanaishi nje ya jimbo hilo na wageni kutoka Ujerumani.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria Kikao cha Profesa Muhongo

Heri ya sikuu ya Maulid, Krismasi na Mwaka Mpya kutoka Kilimanjaro Studio

Nesi Wangu

Kilimanjaro Studio iliyopo Beltsville, Maryland inatoa salamu za kheri ya sikukuu ya Maulid, Christmas na mwaka mpya kwa wadau wote wa Vijimambo Blog, Kwanza Production na Nesi Wangu Blog. Sikukuu iwe ya upendo na amani na muweze kusherehekea kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka 2016.

Kama hukutimiza malengo mwaka 2015 usijali mwaka 2016 ni mwaka wa kujipanga upya na Kilimanjaro studio inakutakia kila la kheri kwa mwaka mpya 2016 uwe mwaka wa mafanikio makubwa kwako na kumwomba Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema palipokua na giza 2015 mwaka mpya apatie mwanga, palipokua na chuki 2015 mwaka mpya apaweke amani yote na tunaimani utafikia malengo na sisi kujipanga kwa mambo mapya kwa kuongeza vipindi kwenye Radio na kukuhabarisha kwenye blogs zetu.

SOTE KWA PAMOJA TUNASEMA KHERI YA SIKUKUU YA MAULID, CHRISTMAS NA MWAKA MPYA

Picha za maadhimisho ya sikukuu ya Maulid, Dar


Waumini wa Dini ya Kiislam wakiandamana jijini Dar es Salaam leo jioni, wakati wa kuadhimisha Sikukuu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.W.A).

Polisi Arusha wamkamata mtuhumiwa wa mauaji ya Kisamo, Afisa Intelijensia TANAPA

Pichani gari aina ya Nissan Mazda lenye namba za usajili T. 435 CSY lililokutwa na mwili wa marehemu Emily Kisamo ambaye ni Afisa wa Intelejensia TANAPA uliohifadhiwa kwenye buti mara baada ya kuuawa na Mfanyakazi wake wa ndani.
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha.

Jeshi la Polisi Mkoani hapa limefanikiwa kumkamata mtu mmoja aitwaye Ismail Swalehe Sang’wa (20) ambaye ni mwenyeji wa kijiji cha Sepuka wilayani Ikungi katika Mkoa wa Singida kwa tuhuma za kumuua Afisa wa Intelijensia wa TANAPA aitwaye Emily Kisamo (52).

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake asubuhi ya leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas alisema tukio hilo la mauaji ya Afisa huyo wa TANAPA lilitokea tarehe 18.12.2015 muda kati ya saa 2:30 asubuhi hadi saa 4:00 asubuhi mtaa uitwao Corridor Area Uzunguni jijini hapa.

Kamanda Sabas alisema kwamba, siku ya tukio hilo marehemu alikuwa nyumbani kwake sebuleni akiwa anakunywa uji ndipo mtuhumiwa ambaye ni mfanyakazi wake wa ndani na alimvizia na kumkata shingo na kitu kinachoaminika kuwa ni panga na kisha kuchukua mwili wake na kuuweka kwenye gari la marehemu aina ya Nissan Mazda lenye namba za usajili T. 435 CSY.

“Baada ya kuuweka mwili wa marehemu kwenye buti alilisafisha gari hilo kwa nje na kisha kuliendesha mpaka eneo la kikwakwaru “B” kata ya Lemara ambapo alilitelekeza hapo na kisha yeye kuondoka”. Alifafanua Kamanda Sabas.

“Mara baada ya gari hilo kukaa mpaka saa 2:00 usiku ndipo baadhi ya wananchi wa eneo hilo walitoa taarifa kwetu ambapo askari wa doria walikwenda na kulichukua gari hilo kwa kulivuta mpaka kituoni. Kwa kuwa mke wa marehemu aitwaye Caroline Lukumay (38) alikuwa anamtafuta mume wake kwa njia ya simu bila mafanikio ndipo alipoamua kuja kituoni kutoa taarifa ambapo tulimuonyesha gari lililotelekezwa ambalo alillitambua mara moja”. Alisema Kamanda Sabas.

Aliongeza kwa kusema kwamba askari walimuomba mke wa marehemu funguo za akiba za gari hilo ambapo baada ya kulifungua ndipo walipouona mwili wa marehemu kwenye buti akiwa na vitu mbalimbali kama vile simu mbili aina ya Sony na Panasonic, pesa taslimu Tsh 300,000, Laptop aina ya Asus na kadi za benki tofauti tofauti.

Mara baada ya mtuhumiwa huyo kukamatwa alikiri kuhusika na mauaji hayo na kusema siku hiyo walikuwa wawili tu yaani yeye na mrehemu na alifanya hivyo kwa kuwa alikuwa na tamaa za fedha alizokuwa nazo marehemu ndani ya nyumba hiyo kiasi cha Tsh. Mil.5.
Upekuzi zaidi wa Jeshi la Polisi ulibaini kuwepo kwa fedha taslimu Tsh. 4,294,000, simu tatu aina ya Sumsang na vocha za mtandao wa vodacom za sh. Elfu tano tano zenye thamani ya Tsh. 70,000 ambapo vyote vilifukiwa kwenye banda la kuku.

Mbali na vitu hivyo pia mtuhumiwa Ismail Swalehe Sang’wa aliweza kuonyesha panga lenye damu ambalo alilihifadhi stoo pamoja na taulo nne kubwa, kitambaa cha mezani na suruali yake ambazo zilikuwa na damu na alizitumia yeye mwenyewe kupigia deki sebuleni baada ya tukio na kisha kuzificha kwenye migomba karibu na mabanda ya kuku.

Kamanda Sabas alimalizia kwa kusema kwamba Jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa watatu wengine mbali na Ismail Swalehe Sang’wa akiwemo mke wa marehemu, rafiki wa mke wa marehemu ambaye ni mwanamke na dereva wa nyumbani wa marehemu kwa mahojiano zaidi.

Agizo la Wizara ya Afya kwa watoa huduma ya tiba mbadala

Taarifa kutoka Wizara ya Afya kuanzia tarehe 24 Desemba 2015 imepiga marufuku matangazo yote yanayohusu tiba asili na tiba mbadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Wale wote wenye vibali wanatakiwa kuviwasilisha vibali na matangazo yao kwenye Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ili vifanyiwe mapitio.

Utoaji wa elimu ya afya kwa umma unaofanywa na watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii umepigwa marufuku hadi hapo utaratibu mwingine utakapotangazwa.

Watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala nchini kote wanaagizwa wawasilishe kwenye Baraza nyaraka zote muhimu ndani ya wiki mbili kuanzia leo Desemba 2015. Baadhi ya nyaraka hizo ni zile zinazohusu kuuza dawa za asili na tiba mbadala, nyaraka za kumiliki mashine zinazotumika katika kufanya uchunguzi katika tiba asili na tiba mbadala

Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala linaagizwa katika kipindi cha siku 14 kuanzia leo 24 Desemba 2015, lipitie nyaraka zote zikapowasilishwa zinazohusu usajili wa watoa huduma, usajili wa vituo vyao, ikiwa ni pamoja na maduka ya dawa za asili na dawa za tiba mbadala, usajili wa dawa zote zinazotumika katika huduma hizo na usajili wa mashine zote zinazotumika katika huduma za tiba asili na tiba mbadala.

Taarifa hiyo imetolewa na Dismas Lyassa kwa niaba ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Hamis Kigwangala na kusainiwa na M.O John, Kaimu Katibu Mkuu.


Mawaziri, Manaibu wateule kuapishwa Jumatatu

Tarehe 23 Desemba, 2015 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliwateua Mawaziri wanne, Naibu Waziri mmoja na kumhamisha Wizara Waziri mmoja.

Walioteuliwa ni Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe, Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Dkt. Joyce Ndalichako na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Hamad Yusuf Masauni.

Rais Magufuli pia alifanya uhamisho wa Waziri mmoja ambaye ni Profesa Makame Mnyaa Mbarawa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Kufuatia uteuzi huu, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue anawaarifu Mawaziri wote na Naibu Waziri walioteuliwa kuwa wataapishwa Jumatatu tarehe 28 Desemba, 2015 Saa tatu asubuhi, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
24 Desemba, 2015