Job: Director of Finance

Organization: International Center for AIDS Care and Treatment Programs
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 31 Jan 2016

Job: Deputy Chief of Party

Organization: International Center for AIDS Care and Treatment Programs
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 31 Jan 2016

Job: Regional Change Manager

Organization: Oxfam
Country: Democratic Republic of the Congo, Kenya, Rwanda, Somalia, South Sudan, Uganda, United Republic of Tanzania
Closing date: 17 Jan 2016

Consultancy Opportunity: M&E and Research - ActionAid

Organization: ActionAid
Country: United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland
Closing date: 22 Jan 2016

Job: Deputy Chief of Party - Management Sciences for Health

Organization: Management Sciences for Health
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 23 Jan 2016

Job: Finance and Business Manager - Management Sciences for Health

Organization: Management Sciences for Health
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 23 Jan 2016

Job: Senior Monitoring and Evaluation Advisor - Management Sciences for Health

Organization: Management Sciences for Health
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 23 Jan 2016

Job: Chief of Party - Management Sciences for Health

Organization: Management Sciences for Health
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 23 Jan 2016

Rais Magufuli katika ibada ya sikukuu ya Krismas


Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwasili kushiriki Ibada ya Krismas misa ya kwanza katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es Salaam, Desemba 25, 2015.

Mchechu azungumzia tuhuma dhidi yake na malengo ya NHC


Nehemiah Mchechu, moja ya majina maarufu katika nyanja za uongozi wa mashirika nchini, jina lake limeteka mitandao ya kijamii kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.

Ukiachana na umaarufu wa Rais John Magufuli mtandaoni kwa kazi yake ya ‘kutumbua’ majipu, Mchechu ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Tanzania (NHC), anavuma kwa mema na ‘mabaya’.

Baadhi wanasifu mafanikio yake ya kuliimarisha shirika hilo kwa kipindi cha muda mfupi, lakini wengine wanamtuhumu kulitumia kujinufaisha ikiwamo kujilipa ‘mamilioni’ ya shilingi kama mshahara na posho za vikao.

Tuhuma zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii ni kwamba bosi huyo wa NHC, anajilipa mshahara Sh36 milioni kwa mwezi na kuhudhuria vikao vingi vya bodi vinampatia posho za kutisha.

“Kiwango hicho hakina ukweli,” anasema Mchechu, “mshahara wangu upo chini ya hapo,”anasema.

“Pia, huwezi kujilipa. Unalipwa kwa makubaliano maalumu tangu awali kabla ya kazi kulingana na kazi unayopewa,” anaongeza.

Mchechu anasema yupo NHC kulitumikia taifa kwa kuwa alipotoka sekta binafsi alikuwa akipata mshahara mkubwa, lakini alikubali kiwango kidogo serikalini kwa kuwa alikuwa akijua shirika hilo lilikuwa na hali mbaya kifedha na lilihitaji kuboreshwa.

Kuhusu vikao vya bodi na kamati mbalimbali anazotuhumiwa kushiriki na ‘kuvuna fedha’, Mchechu anasema kamati nyingi zinazorushwa mtandaoni siyo za kweli na hakuna fedha inayolipwa katika vikao hivyo.

“Watu wanapohoji mshahara wangu wanasahau kiwango ninachoingiza kwa Serikali. Jaribu kufikiri tumeirudisha ardhi ya Kawe Tanganyika Parkers yenye thamani ya zaidi ya Sh200 bilioni kutoka mikononi mwa aliyekuwa ameuziwa kipindi hicho, hivi ningekuwa mtu binafsi kwa kufanikisha majadiliano ya kurudisha kiwanja hicho, ningepata kiasi gani?” anasema.

Katika mahojiano maalumu yaliyofanyika hivi karibuni, Mchechu anaeleza kuwa Watanzania ni kigeugeu kwa kuwa wakati anaingia NHC mwaka 2010 akitokea Benki ya CBA, wengi walimuonea huruma wakieleza alikuwa anakwenda kupoteza weledi na mshahara, lakini sasa wanamzushia anapokea fedha nyingi zinazolifilisi shirika.

“Siku waajiri wangu wakigundua nalipwa mshahara mkubwa kuliko ninachofakifanya wataniondoa kwa sababu nawaletea hasara,” anasema.

Bosi huyo wa zamani wa Benki ya Standard Chartered alianza kazi mwaka 2010, wakati wa utawala wa Rais Jakaya Kikwete, kwa kupatiwa mkataba wa miaka minne kuboresha shirika hilo lililokuwa likichechemea.

Mkataba wa awali ulimalizika mwaka jana na kusaini mwingine wa miaka mitano ambao unatarajia kumalizika mwaka 2018/2019.

Kama yalivyokuwa malengo ya Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1962, Mchechu, alikabidhiwa kazi ya kuendeleza sera ya kujenga makazi ya bei nafuu kwa Watanzania.

Kama ilivyokuwa kwa mashirika mengine ya umma, NHC halikuwa likipata faida kubwa ya kuwezesha kuendeleza miradi mikubwa na kwa mujibu ripoti za fedha za shirika hilo, mwaka 2010 lilikuwa limepata faida ya Sh3.1 bilioni.

Ili kulifanyia mabadiliko Shirika hilo, Mchechu anasema, ilihitajika akili na nguvu ya kutosha kwa sababu mambo yalikuwa yakiendeshwa kienyeji na kwamba baadhi ya vigogo walikuwa wakihusika kulifilisi NHC.

Mikataba ya vigogo


Anasema kuwa kuna baadhi ya vigogo serikalini na watumishi wa shirika hilo waliokuwa wakiendesha ukodishaji wa nyumba kwa mikataba ya kilaghai na NHC kwa kulipatia fedha kidogo wakati wanatoza fedha nyingi kwa wapangaji.

Kuna baadhi ya ‘madalali’ walikuwa wakililipa shirika kodi ya Sh700, 000 katika baadhi ya nyumba za biashara kwa mwezi wakati wao wanakusanya zaidi ya Sh5 milioni lakini mikataba hiyo ilivunjwa.

“Tumekirejesha alichokuwa akikitaka Baba wa Taifa kwa sababu kwa sasa karibu kila mkoa una nyumba za bei nafuu zilizojengwa na shirika,” anasema Mchechu akieleza kuwa hadi sasa wamejenga nyumba zaidi ya 3,000 za bei ya chini.

Katika mtandao wa nyumba hizo, zilizokuwa zikiuzwa bei ya chini kuliko zote nchini ni zile zilizopo mkoani Katavi ambazo zilikuwa Sh32 milioni kwa sababu huduma za umeme na barabara zilikuwa zimesogezwa.

Anaeleza kuwa wastani wa bei ya makazi ya bei nafuu ni Sh34 milioni kwa nyumba ya vyumba viwili na Sh43 milioni kwa nyumba ya vyumba vitatu na bei hupanda kutokana na gharama za ujenzi zikiwamo kuandaa miundombinu na kodi ya ongezeko la thamani.

Pia, gharama hizo anasema zinatokana na riba kubwa ya mikopo iliyopo sokoni na kupanda kwa thamani ya Dola ya Marekani mara kwa mara.

Hata hivyo, baadhi ya wakosoaji wanasema nyumba hizo zinauzwa ghali na kununuliwa na mabepari pekee badala ya walengwa ambao ni watu wa kipato cha chini na sehemu kubwa zinadoda kwa kukosa wateja.

Kwa Mchechu, tuhuma hizo hazimnyimi usingizi. Na kabla ya kujibu hoja hiyo, anatasabasamu kidogo.

“Kila mradi tunaoufanya huwa tunalenga watu wa kundi fulani. Hatukurupuki. Tunaangalia wa kipato cha chini, kati na cha juu. Sina sababu ya kuficha.

“Lakini nyumba zetu ni za bei ya chini kulinganisha na kampuni binafsi hivyo naomba fananisha embe kwa embe na chungwa na chungwa na si vinginevyo,” anasema.

Mchechu anasema kuna baadhi ya miradi mikubwa kama ya Kawe na Morocco ni ya kibiashara zaidi na nyumba zake zinauzwa bei kubwa kwa kuwa zililenga kundi la watu ambao hukimbilia nje ya nchi kununua makazi lakini sasa wanataka wabaki nchini.

“Kama mtu ni wa malengo ya Sh50 milioni halafu anakosoa bei za mradi wa Kawe yupo sahihi kuona bei ile ni kichaa kwa sababu inaenda mara tatu hadi 10 ya kipato chake. Lakini mimi sikulenga kule,” anasema.

Nyumba za bei nafuu

Hata hivyo, anaeleza kwa kuwa NHC malengo yake ni kujenga nyumba za bei nafuu katika halmashauri zote nchini ambako tayari wamenunua ekari 5,600 huku nyingine 22,000 wapo kwenye mazungumzo ya kuuziana na wamiliki.

Kuhusu kudoda kwa nyumba, bosi huyo anapinga kidogo.

Anasema makazi mengi waliyoyajenga kwa bei nafuu yalinunuliwa yote na mengine kabla ya miradi yake kukamilika kupitia mikopo ambayo wananchi wanakopa benki za biashara kununua nyumba za NHC.

“Kibada, Kigamboni (Dar es Salaam) tuliuza ndani ya saa 48, mradi wa Eco Housing na Mchikichini zote zimeuzwa hata hizo za mikoani zina soko…hakuna zilizododa,” anasema Mchechu.

NHC inafahamika kwa muda mrefu kuwa na nyumba za kupangisha za bei nafuu nchini lakini kwa sasa miradi yake ya kupangisha haisikiki kwa kiasi kikubwa.

Hata hivyo, majibu ya kiongozi huyo yanashitua kidogo kwa wanasubiri kiwango kikubwa cha nyumba za kupangisha.

Anasema kuwa katika mikakati yao walipanga kujenga nyumba asilimia 70 kwa ajili ya kuuza na asilimia 30 ya kupangisha kwa watu wa hali ya chini.

Matangazo ya ukodishaji hayawi makubwa sana kama ilivyo katika uuzaji kwa kuwa wananchi wengi wanahitaji nyumba hizo, anaeleza.

“Tanzania ina upungufu mkubwa wa nyumba takriban 3.5 milioni hivyo iwapo nikisema nijenge nyumba moja kwa Sh100 milioni na kuikodisha ile fedha itasaidia familia moja tu lakini nikiuza nyumba mtaji ule nikauzungusha tunaweza kujenga zaidi ya nyumba nane za familia,” anasema Mchechu.

Tangu Rais John Magufuli aingie madarakani ameanza kubadilisha utendaji kwenye utumishi wa umma na moja ya njia ya kufanikisha hilo ni ziara za kushtukiza katika taasisi na mashirika ya umma.

Mchechu amejiandaje na ujio wa kushtukiza wa Rais?

“Sisi tayari tulikuwa tunaendesha mambo yetu kwa mwendokasi na baadaye tutaongeza zaidi kasi,” anasema.

Katika uongozi wake, anaeleza aliyoyapata NHC yakiwamo kuongeza uwekezaji wa ujenzi nyumba nchini na kukuza mapato ya shirika ambayo mwaka jana yalifikia Sh130 bilioni kutoka Sh36.6 bilioni mwaka 2010 baada ya kubana matumizi na kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi.

“Pesa tumeikuza lakini haitosheelezi miradi hata ukichanganya na mikopo hivyo tunaendelea kutafuta fedha zaidi ili kufanikisha malengo yetu.

“Na pia niwe muwazi kabisa kama nitashindwa kutimiza malengo kwa miaka tisa niliyokaa NHC sidhani kama nitaleta kipya nikipatiwa miaka 20 hivyo baada ya hapa nitarudi sekta binafsi,” anasema.
  • Imeandikwa na Nuzulack Dausen via Mwananchi

Rais Magufuli azungumza na Rais Dk Shein

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimlaki Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein Ikulu jijini Dar es Salaam leo Desemba 26, 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein Ikulu jijini Dar es Salaam leo Desemba 26, 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsindikiza Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein baada ya mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam leo Desemba 26, 2015


Various job opportunities at TBS

Tanzania Bureau of Standards (TBS) is Tanzania’s sole standards body, formerly established by the Standards Act No. 3 of 1975, which was repealed and replaced by the Standards Act No. 2 of 2009. It is a Parastatal Organization under the Ministry of Industry and Trade. The Bureau is looking for suitably, qualified, competent and committed Tanzanians to fill the following vacancies:

1.Standards Officer II (06 Posts)

2. Quality Assurance Officer II. (07 posts)

3 System Administrator II (01Post)

4. Inspection Technician II (02 Posts)

5. Inspector II (2 posts)

6. Personal Secretary I (5 posts)

Kindly click the following link for more details: RE-ADVERTISED_POSTS_(1).pdf

Askofu Sangu: Mataifa makubwa yanayohubiri amani ndiyo wana viwanda vya silaha, wanauza wapi?Askofu wa jimbo katoliki la Shinyanga mhashamu Liberatus Sangu (pichani) ameeleza kushangazwa na kusikitishwa na vitendo vya mataifa makubwa duniani kuhubiri amani duniani wakati wao ndiyo wana viwanda vikubwa vya kutengeneza silaha za kivita na kuuza ili watu waendelee kupigana matokeo yake kusababisha vifo,mateso na mahangaiko katika mataifa huku wahanga wakubwa wakiwa ni watoto,akina mama na wazee.

Askofu Sangau ameyasema hayo leo asubuhi katika adhimisho la misa takatifu ya Krismasi iliyofanyika katika kanisa kuu la Mama Mwenye Huruma la Ngokolo mjini Shinyanga Askofu Sangu.

Amesema wakati dunia inaadhimisha sikukuu ya Krismasi mataifa mengi hayana amani vita kutokana na baadhi watu kuwa na uchu wa madaraka na fedha.

“Mataifa makubwa yanayohubiri amani ndiyo wana viwanda vikubwa vya kutengeneza silaha, wanauza wapi? ili upate soko la silaha,lazima utengeneze vita, watu wapigane,ili bidhaa itoke, lakini ndiyo hao wanaokaa mezani na kusema wanataka amani, nadhani hawajanuia kuleta amani, uchu wa madaraka na fedha ndicho kinachosumbua",ameongeza askofu Sangu.

"Tuwaombee wenzetu katika nchi zenye vita, Mwenyezi Mungu apate kuwajalia amani na utulivu ili sote kama familia ya watoto wa mungu tufike kule kristo ametutangulia”, amesema Askofu Sangu.

Katika hatua nyingine Askofu Sangu amewataka kuwapuuza watu wanaosema nchi ya Tanzania haina amani na kusisitiza kuwa Tanzania ni nchi yenye amani huku akiwataka watanzania kumwombea rais John Pombe Magufuli aliyeonesha nia ya kuwatumikia wananchi bila upendeleo na ameonesha wazi wazi kuwa ana mtanguliza mwenyezi mungu katika maisha yake.

“Kuna baadhi ya watu wanataka kutusadikisha kuwa Tanzania hakuna amani kwa nia zao wenyewe,labda wakilinganisha Tanzania na mbinguni ni sawa, kwa sababu mbinguni kuna utumilifu wake wote, lakini ukilinganisha Tanzania na mataifa mengine,ndugu zangu tuna amani ambayo tunapaswa kuilinda kwa nguvu zetu zote”, ameeleza Sangu.

Katika hatua nyingine amewashangaa wazazi na walezi wanaoruhusu watoto wao kwenda kwenye kumbi za starehe na kusisitiza kuwa familia yoyote bora kamwe haiwezi kuruhusu mtoto kwenda disko.

CCM Iringa yatangaza M/Kiti na majina mengine 101 kuwa "wasaliti chama"

KAMATI ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa imetangaza majina ya makada wake 102, wakiwemo vigogo wa chama hicho mkoani hapa, wanaotuhumiwa kukisaliti na kukihujumu chama wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Wasaliti hao wametangazwa jana na Katibu Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Iringa, Dk Yahaya Msigwa ikiwa ni wiki moja tu tangu vijana wa chama hicho waifungie kwa zaidi ya saa mbili kamati hiyo, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza, katika ofisi za CCM mkoa wa Iringa, mjini Iringa.

Vijana hao zaidi ya 50 wanaotarajiwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Manispaa ya Iringa, Kaunda Mwaipyana, waliifungia kamati hiyo wakishinikiza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu ajiuzulu kwa madai ya kukisaliti chama hicho katika uchaguzi wa Jimbo la Iringa Mjini.

Msambatavangu mwenyewe amenukuliwa mara kadhaa akikanusha tuhuma hizo huku akidai kwamba zinasukwa na vigogo wenzake wa chama hicho mkoani hapo ili kulinda maslai yao na kuficha ukweli halisi wa sababu zilizopelekea wapoteze jimbo hilo na kata 14 kati ya 18 kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Akizungumza na wanahabari jana, Msambatavangu ambaye alikiri jina lake kuwemo katika orodha ya makada wa CCM wanaotuhumiwa kukisaliti chama hicho iliyopokelewa na kamati aliyoiongoza yeye mwenyewe alisema pamoja na kwamba tuhuma hizo dhidi yake hazina ukweli yupo tayari kuhojiwa na kutoa utetezi wake katika vikao vitakavyofanya kazi hiyo.

“Najua na wanajua kwamba tuhuma hizo dhidi yangu hazina ukweli wowote na ikithibitika ni za kweli nitajiuzulu vinginevyo niwahakikishie wana CCM mkoani hapa kwamba nitawania tena nafasi hii ya uenyekiti katika uchaguzi ujao kwasababu sifa ninazo,” alisema.

Akizungumza na wanahabari, Dk Msigwa alisema taarifa iliyopokelewa katika kamati hiyo inaonesha Iringa Mjini inaongoza kwa kuwa na wasaliti wengi, ikiwa na jumla ya wasaliti 32.

Pamoja na kukataa kutaja majina ya wasaliti hao kwa madai kwamba watajulikana watapoanza kuitwa kwenye vikao vya maadili vya ngazi mbalimbali za chama hicho mkoani hapa, alijikuta akilazimika kuwataja vigogo wawili waliohusishwa katika tuhuma hizo Iringa Mjini baada ya wanahabari kumbana kwa maswali.

Mbali na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa kutajwa rasmi katika orodha ya watuhumiwa hao, Dk Msigwa alimtaja kigogo mwingine aliyepo katika orodha hiyo kuwa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayewakilisha Manispaa ya Iringa, Mahamudu Madenge.

Katika mchakato wa chama hicho wa kumpata mgombea ubunge wa jimbo la Iringa Mjini uliofanyika Agosti mwaka huu, Msambatavangu na Madenge walikuwa ni miongoni mwa wana CCM 13 waliojitosa kuwania nafasi hiyo ambayo mshindi wake alikuwa Frederick Mwakalebela.

Wakati Mwakalebela alishinda kura hizo za maoni kwa kupata kura 4,388, Msambatavangu alikuwa mshindi wa pili kwa kupata kura 2,077 na Madenge alikuwa wa tano kwa kupata kura 423, nyuma ya Dk Yahaya Msigwa aliyepata kura 1,097 na Dk Augustine Mahiga ambaye Rais Dk John Magufuli amemteua kuwa mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje, aliyepata kura 745.

Kama tuhuma hizo zilivyokanushwa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa; Madenge naye amekanusha kuhusika na tuhuma hizo akisema; “Baada ya kushindwa kura za maoni nilirudi kijijini kwangu Image wilayani Kilolo na kufanya kampeni za kata ya Image na za jimbo la Kilolo ambako CCM na wagombea wake walipata ushindi mkubwa.”

Madenge alisema mbali na Kilolo, aliombwa pia kufanya kampeni katika majimbo ya uchaguzi ya wilaya ya Mufindi ambako pia CCM ilipata ushindi mnono.

“Naomba waniache kwasababu wanajua mimi nilishindwa vibaya kura za maoni kwa kupata kura 423 tu; kura ambazo hata kama ningewaambia walionipigia wakawapigie hao Chadema zisingeathiri matokeo hayo,” alisema.

Katika uchaguzi, huo Mchungaji Peter Msigwa wa Chadema alichaguliwa kuongoza jimbo hilo baada ya kupata kura 43,154 dhidi ya kura 32,406 za Frederick Mwakalebela wa CCM.

Akitaja orodha ya wasaliti wengine, Dk Msigwa alisema katika majimbo ya wilaya ya Mufindi kuna wasaliti 26 wakiwemo watumishi wanne halmashauri hiyo ambao hata hivyo hawakutajwa majina.

Kwa upande wa wilaya ya Kilolo, alisema taarifa waliyopokea inaonesha kuna wasaliti 23, huku Jimbo la Kalenga ikiwataja wasaliti saba na jimbo la Isimani wasaliti 14 wakiwemo watumishi wanne.

Alisema katika kuzishughulikia tuhuma hizo, watuhumiwa hao wataitwa kwenye vikao vya maadili vya ngazi mbalimbal ili wapate fursa ya kujitetea na watakaothibitika kutenda makosa hayo watachukuliwa hatua kwa kuzingatia kanuni, taratibu na Katiba ya chama.

“Wale ambao maamuzi dhidi yao hayawezi kufanywa na vikao vya ngazi ya kata, wilaya na mkoa, taarifa zao zitapelekwa taifani na tuombe vikao hivyo vya taifa vitende haki kwa kuzingatia ushahidi na mapendekezo yatakayotolewa na vikao vyetu ili kushughulikia tatizo hili la usaliti,” alisema.

Wakati huo huo, Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Elisha Mwampashi ambaye pia ni Katibu wa CCM Manispaa ya Iringa amekanusha uvumi unaonezwa na baadhi ya wa CCM kwamba chama hicho kilitumia zaidi ya Sh Milioni 600 kwa ajili ya uchaguzi wa jimbo la Iringa Mjini.

“Sio kweli hata kidogo, hatukuwa na fedha hizo, na nataka mjue CCM ilizingatia sana sheria ya gharama za uchaguzi wakati tukifanya kampeni. Niwashukuru CCM Makao Makuu, Mkoa na wana CCM na wapenzi wetu kwa jinsi walivyojitolea katika kampeni hizo,” alisema.

Diwani (CHADEMA) akataa posho za vikaoDiwani wa kata ya Gangilonga, Iringa Mjini kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Daddy Igogo amesema hatapokea posho za vikao vyote vya baraza la madiwani katika kipindi chake cha miaka mitano na badala yake ametaka zitumike kuwasaidia watoto wanaoshi katika mazingira magumu katika kata yake.

Diwani huyo mdogo kuliko madiwani wote wa halimashauri hiyo ambaye pia ni Mwalimu katika Chuo Kikuu cha Ruaha, Iringa anakuwa diwani wa kwanza nchini kukataa posho hizo huku baada ya Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu (CCM) naye kukataa kupokea posho kama hizo katika kipindi chote atakachokuwa mbunge wa jimbo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya kata ya Gangilonga Igogo alisema kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo ili kusaidia yatima na kuunga mkono ilani ya chama chake ya uchaguzi wa 2010 na 2015 ya kukataa posho ya vikao na kwamba ameshamuandikia mkurugenzi barua inayompa maelekezo ya wapi posho hizo zipelekwe.

Igogo alisema kuwa posho ya vikao ni ugonjwa wa ufisadi unaolitafuna taifa kila kukicha hususani kwa watendaji wa mashirika ya umma ,watendaji wa serekali kuu huu na kumpongeza Raisi John Magufuli kwa kubana matumizi yasiyo ya lazima kwa fedha nyingi zaidi zinaelekezwa katika miradi ya maendeleo.

Alisema posho za wabunge zinalingana na bajeti ya sensa ambapo Taifa lilikwenda kukopa baadhi ya fedha ili kuendeshea zoezi hilo huku wastani wa posho kwa za madiwani na watendaji katika manispaa ya Iringa kwa mwaka zinauwezo wa kusomesha zaidi ya wanafunzi 400 wa shule za sekondari kwa ada ya shilingi eflu 20,000 kwa kila mmoja na fedha zikabaki

Hata hivyo Igogo aliwaomba madiwani wa chama chake na mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Piter Msigwa na wabunge wote wa viti maalumu kuwa sehemu ya kupinga uendelezwaji wa posho zisizo za msingi ili kuonyesha dhamira ya dhati katika kuwatumikia watanzania

Katika vhatua nyingine Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Wilaya ya Iringa mjini ambaye pia ni diwani wa kata ya Mivinjeni Frank Nyalusi amesema uamuzi aliochukua diwani huyo ni mzuri na ni maamuzi yake ila yeye hana mpango wa kugomea kuchukua posho hizo.

Prof. Muhongo awatoa hofu wachimbaji wadogo

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza wakati wa kikao chake na wachimbaji wadogo wa madini, Mkoani Mara.
Serikali imedhamiria kuwaendeleza wachimbaji wadogo wa madini nchini ili kukuza uchumi wa Taifa.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alisema hayo kwenye kikao chake na wachimbaji wadogo wa madini kutoka mikoa ya Simiyu na Mara.

Profesa Muhongo alisema sekta ndogo ya madini nchini inao mchango mkubwa kwenye pato la Taifa wa kuondoa umasikini nchini na hivyo Serikali kwa jitihada mbalimbali itahakikisha wachimbaji wadogo wananufaika ipasavyo pamoja na kuchangia ukuaji wa uchumi.

“Tutawakaribisha wachimbaji wakubwa lakini tunataka na nyie wachimbaji wadogo mchangie ukuaji wa uchumi; mchangie upatikanaji wa ajira kwa vijana wetu,” alisema.

Aliongeza kuwa kwa kutambua umuhimu wa uchimbaji mdogo wa madini, Serikali imeamua na imedhamiria kuwaheshimu na kuwatambua wachimbaji wadogo.

Waziri Muhongo aliwataka wachimbaji hao kubadilika na sio kuendelea kulalamika badala yake wajitume na kufanya kazi kwa uadilifu huku wakitanguliza suala la uzalendo na pia kuamini kwamba Serikali inayo nia thabiti ya kuwasaidia.

Aliwatoa hofu na kuwahakikishia kuwa Serikali inaendelea na juhudi za kuwatafutia maeneo zaidi ya uchimbaji madini na vilevile soko la uhakika ili kuongeza kipato chao na wakati huo huo kuliingizia taifa mapato zaidi.

"Msiwe na wasiwasi, fanyeni uchimbaji wa uhakika; Serikali hii ni yenu; itawasaidia masuala mbalimbali pamoja na kuwatafutia ruzuku, masoko, mafunzo na pia kuwatafutia maeneo zaidi kwa ajili ya shughuli zenu," alisema.

Aliwataka kuachana na fikra potofu kuwa Serikali haiwajali badala yake waiamini Serikali yao kwamba ipo kwa ajili ya kuwasaidia na huku wakijituma kwa kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na uaminifu.

“Matatizo ya zamani ya uchimbaji mdogo tuachane nayo, lazima ulipende taifa lako; huwezi ukawa mchimbaji wa dhahabu ya Tanzania unaipeleka Kenya; halafu inauzwa kama imetoka humo hili ni kosa kubwa,” alisema.

Aliwaasa kuepuka kutorosha madini nje ya nchi; aliongeza kuwa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limepewa jukumu la kuwatafutia bei ya madini kusudi madini yanayopatikana nchini yauzwe nchini na yanunuliwe hapa hapa; iwe ni malighafi ya Tanzania.

Aidha, Profesa Muhongo alimuagiza Meneja wa TANESCO Kanda ya Ziwa, Mhandisi Amos Maganga kutembelea maeneo yote ya wachimbaji wadogo ili kujua mahitaji yao ya umeme pamoja na kutathmini namna ya kuwaunganisha na huduma ya umeme.

Aliagiza kuwa baada ya kutembelea maeneo hayo, masuala yanayoweza kutatuliwa hapo kwa hapo lazima yatatuliwe na yale ambayo yatakuwa yanahitaji fedha zaidi wahakikishe wanaweka kwenye mipango ya usambazaji umeme vijijini na iwe kwa ajili ya umeme mwingi wa kuendesha mitambo.

Kwa upande mwingine, wakizungumza kwa nyakati tofauti mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho, wachimbaji hao wadogo wa madini mikoa ya Mara na Simiyu walimpongeza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa juhudi zake katika kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.

Wachimbaji hao walisema uteuzi wa Profesa Muhongo kwenye nafasi hiyo ya Waziri wa Nishati na Madini ni neema kwa sekta hiyo kwani uwepo na umuhimu wake tayari umeonekana.

Akizungumza kwa niaba ya wachimbaji, Rais wa Wachimbaji Wadogo Tanzania, John Bina alisema changamoto zilizokuwa zikiikabili sekta ya madini nchini zimepata tiba.

"Mheshimiwa Rais hakufanya kosa kumteua Profesa Muhongo kwa nafasi hii; anafahamika kimataifa ni mchapakazi. Tulikwisha ona juhudi zake kipindi cha nyuma na sasa amerudi kututumikia," alisema Bina.

Alisema wachimbaji wadogo wa madini nchini wanamuamini Profesa Muhongo na vilevile wanaukubali utendaji wake ambao waliuelezea kuwa ni chachu ya maendeleo kwenye sekta hiyo.

Rais wa Wachimbaji wadogo wa Madini Tanzania, John Bina akizungumza wakati wa kikao na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wanne kutoka kushoto)

Anatafutwa na familia: Hemed Mzee Ibrahim "Njemba"

Hemed Mzee Ibrahim "Njemba"
Hemed Mzee Ibrahim "Njemba"
Ndugu na jamaa wanatarifiwa kwamba Bw. Hemed Mzee Ibrahim "Njemba" (pichani) ametoweka nyumbani kwake Magomeni Makuti mtaa wa Mchinga namba 22 jijini Dar es Salaam toka siku ya Alhamisi tarehe 24/12/2015.

Alionekana mara ya mwisho kwenye msikiti wa Magomeni Makuti muda wa alasiri alipokwenda kuswali, akiwa kavaa balaghashia (kama hiyo pichani), shati la light purple, suruali ya bluu na kandambili za bluu. Baada ya hapo hakurudi nyumbani kwake na hadi sasa hajulikani alipo. Mzee Njemba hupendelea kutembelea Magomeni Makuti.

Wanafamilia wanaomba mwananchi atayebahatika kumuona atoe tarifa kwa mkwewe Yusuf anayepatikana katika namba 0784 606 262.

Wanatanguliza shukurani za dhati kwa wote na kumuombea salama mzee wao.
Taarifa ya Ridhiwani Kikwete kwa umma kuhusu tuhuma kadha wa kadha


Enguserosambu warejeshewa msitu mikononi mwao

Mraghbishi Noorkiyengop Mbaima toka kijiji cha Enguserosambu akisimama mbele ya mifugo iliyokutwa msituni katika eneo lililoruhusiwa la msitu wa jamii wa Enguserosambu
Ilikuwa ni siku ya shangwe na furaha kwa wananchi wa kata ya Enguserosambu wilayani Ngorongoro. Hii ni baada ya serikali kukubali ombi lao la kusimamia rasilimali ya msitu wa Loliondo namba 2 unaopakana na vijiji vinne vinavyokadiriwa kuwa na idadi ya wakazi wapatao 20,000 wanaotegemea mahitaji yao toka katika huo msitu.

Huu ni msitu pekee ambao wananchi kwa kushirikiana na Mkuu wao wa wilaya, na mashirika rafiki, wamefanikiwa kuishawishi serikali kuukabidhi msitu huo kwao. Katika mchakato huo uliochukua miaka kadhaa wanawake toka katika vijiji vya Enguserosambu, Ng’arua, Orkiu na Naan wamekuwa mstari wa mbele katika kufanikisha azma hiyo ya kubakiza msitu wao wa enzi mikononi mwao. Akielezea furaha yake aliposikia msitu wa Loliondo namba 2 umekabidhiwa kwa wananchi, mraghbishi mwanamke Noorkiyengop Mbaima alisema.

“Mimi mwenyewe nimefurahia, kwa sababu sisi akina mama tunategemea sana msitu huu kwa mahitaji yetu. Huu msitu kama ungeondoka katika mikono ya jamii basi tungeathirika sana sisi kina mama.” Umuhimu wa msitu huu kwa kina mama ndio uliowapelekea wao kutunga na kuimba nyimbo za hamasa na kutumbuiza, kushiriki kwa wingi katika vikao mbalimbali vya maamuzi wakati wote wa mchakato huo. Kwa kuwa msitu huu ndio tegemeo lao katika kuendesha maisha ya kila siku. Hakuna chochote ambacho kiliamriwa bila ya wao kuchangia na kushirikishwa kuanzia utungaji wa sheria ndogongogo za usimamizi wa msitu hadi kukabidhiwa rasmi msitu huo. “Nikichukulia mfano katika mikutano yote ya vijiji. Kiukweli wanawake wamekuwa wanajitokeza kwa wingi, kuliko makundi mengine yoyote. Hata ile siku ya uzinduzi wa msitu walikuwa wengi zaidi,” anaelezea Jackson Nangiria.

Ushiriki huu wa wanawake unatokana na ukweli kwamba wana uhusiano wa karibu na msitu huo wa enzi wa Enguserosambu.Si kwa ajili yao tu pamoja na watoto wao pia. Ni watoto hawa wa kike wenye majukumu ya kujenga nyumba kwa kutumia miti inayotoka ndani ya msitu huu, ndio wanaotembea na punda wakiwabebesha maguduria ya maji kwa umbali mrefu wakitafuta maji ambayo chanzo chake kipo kwenye msitu huu. Wanapopata watoto wanahitaji dawa za kuwaogeshea na dawa za uzazi ambazo zinatoka kwenye msitu huu. Wao ndio wapishi katika familia zao hivyo wanahitaji kuni zinatokana na miti iliyoanguka na kukauka ambayo inapatikana kwenye msitu huu. “Kina mama wanafanya mitambiko ndani ya msitu huu wengine ambao hawakupata watoto wanapatia hapo baada ya kuomba ndani ya msitu huu. Si hivyo tu ndani ya msitu huu kuna dawa mbalimbali za asili kwa mfano mtoto akizaliwadawa ya kumwogesha na kumnawisha hupatikana humo humo na nyingine ni za kunywa kama maziwa na nyingine kwa ajili ya mama,” anaeleza mwanamama mraghbishi Noorkiyengop Mbaima. Uwepo wa wanawake hawa wa Kimasai katika kata ya Enguserosambu kiukweli unatokana na uwepo wa msitu huu. Huu ndio msitu wa enzi ambao serikali ilipendekeza uwe chini ya usimamizi wake kama ulivyokuwa msitnamba moja wa Loliondo.

Pendekezo hilo lilitolewa kupitia timu mbalimbali toka wizarani, ofisi za kanda na halmshauri ya wilaya, ambazo zilitembelea kijijini hapo kuomba kupatiwa muhtasari wa kikao cha kijiji kitakachopitisha ombi hilo la serikali.

Ombi hilo linakuja kwa kijiji kwa sababu msitu huo umekuwa chini ya usimamizi wa wananchi wa kata ya Enguserosambu kwa miaka mingi. Ni wananchi hao ndio ambao wameutunza msitu huo pasipo Kuombwa wala Kukabidhiwa na serikali. Na kwa kweli wameweza kuutunza kwa muda wote huo. Miti haijakatwa, wananchi wamejiwekea sheria ndogondogo na pia kuwakamata wale ambao wamekuwa wakiharibu msitu huo. Hivyo wananchi hawa wamewajibika katika kuhakikisha msitu unabaki katika hali yake ya asili pasipo kushurutishwa na mtu yeyote.

Kwa mantiki hiyo muhtsari uliokuwa unaombwa na serikali ya halmashauri yan wilaya ulihiitaji baraka za wananchi, ambao hawakuwa tayari kutoa sehemu ya uhai wao unaotegemea msitu huo. Hakuna mwanakijiji aliyekuwa tayari kukubali ombi hilo. Na jibu lilikuwa ni wazi kabisa kwamba ombi hilo lilitishia mustakabali wa jamii zinazozunguka msitu huo ambazo ni vijiji vya Enguserosambu, Ng’arua, Orkiu na Naan. Hivyo wakati serikali ikipendekeza kuusimamia

Msitu huo wananchi kwa upande mwingine wakaanza kuiomba serikali iwaruhusu kuusimamia. Ni kama kichekesho pande zote zinaombana kuusimamia msitu huo. Serikalikupitia halmashauri ya wilaya inasema tunahitaji kuusimamia, na wananchi wanaiomba serikali hiyo hiyo kuusimamia msitu huo. “Kwa kweli sisi kama wananchi wa Enguserosambu tumeona kwamba huu msitu ukiondoka chini ya usimamizi wetu tutaathirika. Kwa sababu msitu huu ni uhai wa wananchi wa hapa. Tukikosa huu msitu, hatupati maji wala mvua, tutakosa chakula. Kwa kifupi tutakosa kitu muhimu cha uhai wa jamii,” anaelezea mraghbishi Noorkiyengop Mbaima.

Ndani ya msitu huu kuna miti ambayo wazee wanaitumia kwa ajili ya shughuli za kimila pamoja na miti ya kiasili ambayo inatumika kwa shughuli mbalimbali. Baadhi ya miti hiyo ni pamoja na Oroilieni ambao unatumika kwenye shughuli za jadi, ujenzi na kiimani. Akifafanua kuhusu mti huo Robert Kamakia anaelezea, “Huwezi kuingia jando bila kuwa na mti Oroilieni. Kwa kuwa unatumika katika kufanya baadhi ya shughuli za kimila. Mti mwingine ni Orikienyi ambao unatumika kama dawa ya kutibia magonjwa ya aina mbalimbali kama homa, kifua, malaria na kadhalika. Mti mwingine ni Ostiani ambao hutumika kwa ajili ya kivuli na kutunza maji.” Hivyo msitu huu una maana kubwa sana kwa makundi mbalimbali yakiwemo ya wazee, wanawake na vijana. K wa upande wa vijana kwa mfano, mila na desturi

za kimasai zinawataka kujitenga hasa pale wanapoingia ngazi ya Morani. Ambapo hutakiwa kuweka kambi kwa ajili ya kuchinja ng’ombe na kula nyama. Tukio hili huchukua mpaka mwezi mmoja wakati vijana hao, wanapoazimisha sherehe hizo. Tukio hili linashirikisha matumizi ya miti mbalimbali kwa mujibu wa taratibu zao. Supu wanazokunywa huchanganywa na baadhi ya majani ya miti hiyo. Ni dhahiri ulaji wa nyama kwa mwezi mzima unahitaji pia matumizi ya dawa za asili. Na ndio maana wamasai hawasumbuliwi sana na magonjwa yanayotokana na ulaji mwingi wa nyamba. Si hivyo tu porini hamna vitanda hivyo baadhi ya majani hutumika kwa ajili ya zoezi hilo. “Kiukweli bila msitu vijana hawawezi kufanya chochote. Kwa kuwa kila kitu kinatoka katika huo msitu,” anafafanua Julius Long’oli. Lakini si hivyo tu, wakati wanaingizwa jando pia kuna miti inayotumika. Vivyo hivyo na katika sherehe za kumaliza jando. Hivyo msitu ni sehemu ya mila na utamaduni wa jamii hizi zinaouzunguka. Ni imani yao pia, ambayo kimsingi ni lazima iheshimiwe. Huu ni msitu wao wa enzi na enzi. “Huu ni msitu wa jamii kwa Kimasai unaitwa Elieteti yaani ndani ya jamii kwa maana ya jina hilo ni msitu unaosaidia jamii ya sasa na ya kizazi kijacho. Kwamba huu msitu unategemewa na kizazi cha sasa na kijacho,” anafafanua Yohana Tuluni mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya kusimamia msitu. Mtizamo huu wa wananchi wa kata hii, kwamba wao ndio wausimamie msitu huu, unatokana hali halisi ya msitu namba moja wa Loliondo unaosimamiwa na serikali kupitia halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro kuwa katika hali ya kutoridhisha. Miti mingi imekatwa kwa ajili ya matumizi ya ujenzi na hivyo kutishia uhai wa msitu huo. Kitu ambacho wana Enguserosambu hawakupenda kitokee kwa msitu namba mbili wa Loliondo ambao wanautegemea kwa mustakabali wa maisha yao. Msitu huu umekuwa ukitegemewa na jamii ya hapa kwa miaka mingi. Ni wao ndio ambao wamekuwa wakiutunza na kwa kweli wamefanikiwa kwa njia moja ama nyingine kuufanya uwe mzuri zaidi kuliko hata ule wa Liliondo moja unasimamiwa na serikali.

“Wazo la kutaka kumiliki msitu lilikuwa kama ndoto, ukiangalia na hali halisi ilivyokuwa. Ni maono ya mtu mmoja aliyewashirikisha wenzake. Mwishowe wazo likatolewa Kwa wanakijiji ambao waliungamkono wazo hilo. Na mwishowe tukamwandikia Mkuu wa Wilaya na kwa kweli alituunga mkono sana,” anafafanua mraghbishi na mjumbe wa Bodi ya Wadhamini Jackso Nangiria Mchakato wa kuomba hadi kukabidhiwa usimamizi wa msitu umewezesha wananchi wa Enguserosambu kuongeza ufahamu wa mambo mbalimbali juu ya usimamizi wa misitu lakini pia mahusiano baina ya wananchi na viongozi yameboreka zaidi. Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu, hivi ndivyo unavyoweza kusema Wanaenguserosambu wamekuwa wamoja zaidi. Mashirika rafiki yamesaidia sana katika kutoa elimu kwa wananchi na viongozi wao ambao maarifa hayo yamewezesha kujiwekea mikakati na hatimaye kufanikisha jamii kumiliki msitu wake wa enzi kwenye mikono yake. Wakati mchakato unaanza palikuwa na kijiji kimoja tu cha Enguserosambu kilichokuwa kinaundwa na vitongoji vinne vya Enguserosambu, Ng’arua, Orkiu na Naan ambavyo sasa vimepata hadhi ya kuwa vijiji. Kwa sasa sauti yao ni kubwa zaidi kuliko pale Mwanzo
Watendaji wa PALISEP wakiwa pamoja na wanajamii wakishikana mikono kuonesha ushirikiano baina yao. Kuanzia kushoto ni Sarah Saningo, Robert Kamakia, Jackson Nangiria, Norkiyengop Mbaima, Sunde Tutayo na Fredy Samberu
Hivyo Bodi ya Wadhamini ilichaguliwa na mkutano mkuu wa kijiji, ambacho sasa kina hadhi ya kata. Kwa hiyo usimamizi wa msitu huu kwa sasa umekabidhiwa kwa Kata ya Enguserosambu. Hivyo wananchi kutoka katika kila kijiji walichagua wawakilishi wao waliounda Bodi ya Wadhamini. Wawakilishi hawa jukumu lao kubwa ni kuratibu mchakato wote wa uombaji usimamizi wa msitu wa Loliondo 2. Baada ya kuchaguliwa wajumbe walipatiwa mafunzo na shirika la PALISEP ambao pia walisaidia uandikishwaji wa bodi tarehe 12/09/2012. Bodi hiyo imeundwa na wajumbe 10 kati ya hao wanawake ni 4. Bodi hii ilipata mafunzo ya sheria mbalimbali za misitu, usimamizi wa misitu na bodi yenyewe pia kupitia video ya hali ya msitu wa Loliondo 1. Walipata pia ziara za mafunzo kwa kutembelea misitu inayosimamiwa na jamii kwa mfano msitu wa Suledo uliopo Manyara wilaya ya Kiteto. Bila jamii kujitoa kwa hali na mali isingewezekana kufanikiwa kwenye hili. Kwani bodi ya wadhamini imefanya kazi kubwa. Jamii imeshiriki katika kuandika katiba ya bodi na sheria ndogondogo ambazo zimepitishwa katika mikutano ya vijiji.

“Baada ya kuchaguliwa jukumu letu ilikuwa ni kutembelea msitu ili kujua hali yake. Lakini pia tuliweza kutoa elimu kwa wale waliokuwa wanaishi na kufanya shughuli za kilimo ndani ya msitu. Ili waweze kuondoka. Si kazi rahisi,” mjumbe wa Kamati ya Bodi ya Wadhamini Sunde Tutayo.

Kwa sasa mpango ni kuboresha na kutunza vyanzo vya maji. Kupitia bodi hiyo, wananchi wamejiwekea malengo ya kuuongeza zaidi kwa kupanda miti zaidi. Hili linafanywa kwa uangalifu mkubwa kwa kuwa kuna baadhi ya miti si rafiki mzuri kwa vyanzo vya maji inayakausha. Lakini si hivyo tu Bodi ya Wadhamini inaangalia njia sahii ya kuhakikisha kwamba zinapatika fedha za kununulia miti mipya. Wazo lililopo ni kuwakilisha mtizamo huu kwa wanajamii ili waweze kutaarifiwa na kusikilizwa nini yatakuwa maamuzi yao kwenye uchangishaji huo wa fedha. Changamoto nyingine ni uboreshwaji wa sheria ndogondogo kwa kuwa hakuna mipaka ya majukumu baina ya Bodi ya Wadhamini na Halmashauri ya serikali za vijiji. Kuna umuhimu wa suala hili kuwekewa utaratibu mzuri wa kiuwajibikaji kwa sababu muda mwingine vyombo hivi vinaweza kugongana kimawazo na kiutendaji na nani anawajibika kwa nani.

“Hapo nje kuna mikaratusi tumeikamata sisi kama Bodi ya Wadhamini. Mtu ameangusha mti mbichi ambao haujakauka. Na ameiyangusha bila idhini. Tumefanya hivi kwa kushirikiana na Mheshimiwa Diwani. Tunachosubili tukae na serikali ya kijiji ili tujue tunafanya nini,” anafafanua mraghbishi na Kaimu Katibu wa Bodi ya Wadhamini Jackson Nangiria. Kwenye kukabidhiwa msitu mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Wilaya na Diwani wa Kata ya Enguserosambu walikuwepo wakati wa kukabidhiwa kwa msitu huo pamoja na wenyeviti wa vijiji vyote vinavyounda kata ya Enguserosambu. Kwa hakika wenzetu wa Enguserosambu wameweza kujipanga na kuhakikisha kwamba msitu wao wa enzi unabaki mikononi mwao.