Ati "sumenti" imemuishia?


Mahojiano: Kwanza Production na Hashim Kambi (mcheza filamu)

Hashim Kambi ni msanii wa filamu nchini Tanzania.

Alikuwa mkarimu sana kupita studio zetu za Kilimanjaro hapa Beltsville Maryland na kuzungumza nasi.

Watoto wa wahadhiri UDSM katika 'get together party'Watoto wa Chuo waliowahi kuishi chuoni hapo wakiwa kwenye picha ya pamoja hakika hii ilikuwa ni party ya nguvu.

Watoto wa chuo waliokuwa wakiishi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakati wazazi wao wakiwa ni wahadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ili kuweka ukaribu watoto hao wamekutana na kufanya party ya nguvu hivi karibuni katika viwanja vya UDSM hii ikiwa ni kurudisha ukaribu pamoja na kufahamiana kwa wale waliopotezana miaka kadhaa chuoni hapo.

Siku 50 za Rais Magufuli - Mahojiano ya AzamTv na Prof. Issa Shivji


Prof. Muhongo afanya ziara Bukoba: Kagera kuunganishwa na gridi ya Taifa

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto mbele) akimsikiliza Mhandisi wa kituo cha kufua umeme wa dharura cha Kibeta- Bukoba mjini, Mhandisi Filbert Mlaki wakati wa ziara yake kituoni hapo leo (27 Desemba, 2015). Kituo hicho chenye mitambo minne kinao uwezo wa kuzalisha megawati 2.1 ambacho hutumiwa pale umeme wa kutoka Uganda unapokatika.
Serikali imesema ifikapo mwaka 2018 Mfumo wa umeme katika Mkoa wa Kagera utakua umeingizwa kwenye Gridi ya Taifa.

Hayo yalisemwa jana tarehe 27 Desemba na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alipofanya ziara mjini Bukoba, Mkoani Kagera ili kukagua miundombinu ya umeme.

Ilielezwa kwamba Mkoa huo kwa sasa unapata umeme kutoka nchini Uganda ambao umekuwa ukikatika mara kwa mara na hivyo kulilazimu Shirika la TANESCO kutumia mitambo yake inayotumia mafuta ambayo hata hivyo haikidhi mahitaji ya umeme ya Mkoa.

Profesa Muhongo aliliagiza shirika hilo kuhakikisha linaharakisha taratibu za kuunganisha mkoa wa Kagera kwenye umeme wa Gridi ya Taifa.

"TANESCO ni lazima muharakishe mipango ya kuunganisha mkoa huu kwenye gridi ya taifa ili kuwapatia wananchi huduma ya umeme wa uhakika," aliagiza.

Aidha, Profesa Muhongo aliiagiza TANESCO kuhakikisha mafuta kwa ajili ya kuendeshea mitambo hiyo yanakuwepo yakutosha kwa muda wote.

Alisema ifikapo mwaka 2025, Tanzania itaingia kwenye uchumi wa kati ambao utatokana na uwekezaji mkubwa kwenye viwanda ambavyo vitahitaji umeme wa kutosha na uhakika.

Mbali na hilo, Profesa Muhongo aliliagiza Shirika la Tanesco mara baada ya mkataba uliopo wa kuuziana umeme kati ya Tanzania na Uganda kuisha, wahakikishe wanaingia mkataba wa muda mfupi mfupi lengo likiwa ni kuepusha kuwa ndani ya mkataba wakati tayari mkoa huo utakua kwenye gridi ya taifa.

Akielezea hali ya umeme mkoani humo, Meneja wa Tanesco Kanda ya Ziwa, Mhandisi Amos Maganga alisema kwa sasa Tanzania inanunua umeme kwa gharama ya senti za Marekani 8.4 kwa kila unit.

Alisema Tanzania inao mkataba wa kununua umeme kutoka Uganda kiasi cha megawati 10 ambao unahudumia wilaya za Bukoba Mjini na Vijijini, Karagwe, Muleba na Misenyi.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kushoto) akimsikiliza Mhandisi Filbert Mlaki.
Waziri wa nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akikagua moja ya mtambo wa kuzalisha umeme wa Kituo cha Kibeta
Moja ya mtambo wa kuzalisha umeme katika kituo cha kufua umeme wa dharura cha Kibeta- Bukoba Mjini.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongella kabla ya kuanza ziara ya kukagua miundombinu ya umeme mkoani humo.

Uchaguzi wa marudio hatutaki kusikia Zanzibar

Chama cha Wananchi CUF Zanzibar kimesema hakipo tayari kupokea maazimio ya mazungumzo ya kutafuta mwafaka wa Uchaguzi Mkuu kama yatakuwa yanakwenda kinyume na maamuzi waliofanya wananchi kupitia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 Mwaka huu.

Tamko hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mipango wa Chama hicho, Omar Ali Shehe katika mahojiano maalum na Nipashe Jumapili juu ya mazungumzo ya kutafuta mufaka wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar.

Mazungumzo hayo yanaogozwa na Rais wa Zanzibar DK. Ali Mohamed Shein na kuwashirikisha Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar na Mgombea urais kupitia CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi pamoja na marais wastaafu wa Zanzibar. Alisema CUF kiko tayari kupokea maamuzi na kuyaheshimu kutoka katika Kamati hiyo ya mazungumzo kama yatakuwa yamezingatia maamuzi ya wananchi waliyoyafanya kupitia Uchaguzi Mkuu huo.

Inaaminika kuwa matokeo yaliyofutwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yalikuwa yakimpa ushindi Hamad. 
“Sisi tunasubiri matokeo ya mazungumzo yao tukiamini kwamba mazungumzo hayo hayatokwenda kinyume na maamuzi waliyofanya wananchi kupitia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba Mwaka huu,” 
Shehe alisema kuwa Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum Jecha hakuwa na mamlaka ya kikatiba na kisheria kufuta matokeo ya uchaguzi huo ambao tayari ulikuwa umekamilika kwa asilimia 70 na matokeo ya majimbo 31 yakiwa yametangazwa katika uchaguzi huo.

Shehe alisema siri ya kufutwa kwa matokeo ni baada ya Mwenyekiti kuona CCM wapo katika hatari ya kuanguka katika uchaguzi huo na hakuna sababu nyigine. 
“Mchezo wa kufuta matokeo kwa sababu tu chama tawala kiko katika hatari ya kuanguka utaendelea kufanyika kama tukiacha hivi hivi,” “Huku ni kuvuruga demokrasia ya nchi yetu.” 
Alisema miezi miwili sasa imemalizika lakini hakuna mtu yoyote aliyefikishwa Mahakamani kwa kuharibu uchaguzi au Mwenyekiti kuweka vielelezo na ushahidi wa kuharibika kwa uchaguzi huo.

Aidha, alisema msimamo wa Baraza Kuu la CUF ndiyo muongozo wa chama kuwa Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar warudi kazini wakamilishe ujumlishaji wa matokeo ya uchaguzi wa awali na kumtangaza mshindi wa uchaguzi huo.

Alisema kuwa hali ya kisiasa ya Zanzibar ipo katika giza kutokana na wananchi kushindwa kufahamu lini watapata viongozi wa kidemokrasia huku wakiendelea kushuhudia kupanda kwa gharama za maisha Visiwani humo.

Hata hivyo alisema kuwa mazungumzo hayo yamesaidia kwa kiasi kikubwa kutuliza hali ya amani na kuondoa hofu wananchi lakini alitaka yakamilike kwa wakati ili wananchi wajue hatia yao ya kupata viongozi.

Aidha alisema kuwa CUF inatambua kuwepo kwa watu wanaotaka kupindisha uchaguzi uliyofanyika Oktoba 25 mwaka huu lakini alisema hawatafanikiwa kutokana na ripoti za waangalizi wa ndani na nje kuweka wazi kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki Zanzibar.
“Wakati Mwenyekjiti wa ZEC anatangaza kufuta matokeo tayari matokeo katika Majimbo 54 yalikuwa yamekamilika na kubandikwa matokeo na Wagombea kupewa vyeti vyao vya ushindi hoja ya kufuta matokeo Mwenyekiti katoa wapi?”
“Haiwezekani kufanyika uchaguzi wa marejeo kabla ya uchaguzi wa mwanzo kukamilika Zanzibar, sawa na kusherekea harusi kabla ya ndoa kufanyika.”
Alisema wakati Mwenyekiti Jecha anafuta matokeo hayo katika meza yake majimbo tisa yalikuwa yanamsubili kutangaza matokeo baada ya uhakiki kukamilika na kubakia Majimbo 14 ya Wilaya tatu za Kisiwani Pemba.

Aidha alisema kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo alivunja kanuni na sheria kutokana na kitendo cha ZEC kuhakiki matokeo ya Urais mara mbili wakati tayari kazi kama hiyo ilikuwa imefanyika katika Majimbo na kumalizika na kumalizika salama kabla ya kufutwa kwa matokeo hayo.
“Mwenyekiti arudi kazini atangaze marokeo na mshindi wa urais wa Zanzibar uchaguzi wa marudio hatutaki kusikia Zanzibar,” 
alisema Shehe.

Jecha alisema aliamua kufuta matokeo ya uchaguzi huo baada ya kutawaliwa na vitendo vya udaganyifu ikiwemo idadi ya wapiga kura kuzidi katika baadhi ya vituo kinyume na idadi ya watu waliosajiliwa katika daftari la wapiga kura Visiwani humo.

Mahojiano na Mkurugenzi TPDC: Aweka hadharani mapato ya gesi


WAKATI eneo la kujenga kiwanda cha kuchakata gesi itakayovunwa baharini likitangazwa kupatikana wiki hii, uvunaji utakapoanza Serikali itapata mapato makubwa kutokana na mikataba minono iliyoingiwa.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili wiki hii, Mkurugenzi wa Utafutaji na Uendelezaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Kelvin Komba, amesema mfumo wa sasa wa mikataba, unaihakikishia Serikali kupata mpaka asilimia 85 ya faida yote ya kitalu, baada ya kutoa gharama za uzalishaji na ukataji kodi.

Kwa mujibu wa Komba, mwekezaji akigundua gesi au mafuta, anatakiwa kurudisha gharama zake zilizotumika katika utafiti na baada ya hapo, faida hugawanywa kati ya Taifa na mwekezaji.

Taarifa zinaonesha kuwa mpaka sasa Tanzania kumefanyika ugunduzi wa gesi asilia katika eneo la bahari na nchi kavu, inayofikia takribani futi za ujazo trilioni 55.21. “Hata hivyo utajiri huu ili uwe na tija kwa Taifa ni lazima sheria, kanuni, sera na mikataba iwekwe katika namna ambayo inanufaisha Taifa,” alisema Komba.

Mgawanyo 

Akifafanua zaidi, Komba amesema Tanzania kwa sasa inatumia mfumo wa Mkataba wa Ugawanaji Mapato (Production Sharing Agreement-PSA), kati ya Taifa na mwekezaji, ambao mgawanyo wa mapato umewekwa kwa asilimia na hutofautiana kulingana na kiwango cha uzalishaji na maeneo ugunduzi ulipofanyika.

Kwa mujibu wa Komba, kama ugunduzi ni wa nchi kavu, basi Serikali itapata asilimia 70 hadi 85 ya faida baada ya kodi kwa mafuta na asilimia 60 hadi 80 ya faida hiyo kwa gesi asilia.

Kama ugunduzi umefanyika katika kina kirefu cha bahari, Komba alisema mgawanyo unakuwa asilimia 60 hadi 85 ya faida baada ya kodi, ambao huongezeka kwa upande wa Serikali kadri uzalishaji unavyoongezeka. Kwa maana hiyo, mwekezaji baada ya kufanya utafiti, kugundua gesi au mafuta, akianza kuzalisha tu na kurejesha gharama za utafiti, katika faida baada ya kodi ataambulia kati ya asilimia 40, kiwango cha juu na asilimia 15, kiwango cha chini.

Komba anasema kama uzalishaji ni mkubwa, basi mgao wa Taifa nao huongezeka na kama ugunduzi ni wa mafuta pia mgawanyo wa Taifa huwa mkubwa zaidi. “Taifa huchukua mgawanyo zaidi katika mafuta, kwa sababu mafuta yanauzika kirahisi zaidi duniani kuliko gesi na pia miundombinu ya kuendeleza mafuta, haihitaji mitaji mikubwa kama ilivyo kwa gesi asilia,” alisema Komba.

Aidha, alisema mpaka kufikia sasa mikataba ya PSA 35 imekwishaingiwa kati ya Serikali, TPDC na wawekezaji na kati ya hiyo, mikataba 22 bado inafanyiwa kazi na kampuni 19 ndizo zinazofanya kazi za utafiti na uendelezaji hapa nchini.

Faida za mkataba Kupitia mfumo huo wa PSA, Komba amesema kampuni au muwekezaji hutumia fedha zake kufanya shughuli zote za awali za utafiti, ikiwa ni pamoja na kukusanya data mtetemo (seismic), ambazo zingine huuzwa na TPDC, kuzifanyia tathmini na kuchimba kisima cha kwanza cha utafiti (exploration well), hatua ambazo ni za gharama kubwa.

Kwa mujibu wa Komba, kama itatokea hakuna ugunduzi katika kisima hicho, basi fedha yote ya mwekezaji iliyotumika katika uwekezaji hupotea na hasara huwa ni ya kwake. Lakini ikitokea ugunduzi umefanyika, Komba amesema muwekezaji atajirudishia sehemu ya gharama alizoingia wakati wa utafiti, baada ya kuanza kuingiza fedha kwa kuuza gesi au mafuta aliyogundua.

Faida nyingine, Komba amesema ni pamoja na rasilimali kubaki kuwa mali ya Taifa, huku kampuni au muwekezaji akibeba hatari ya kuwekeza fedha katika utafiti na kukosa rasilimali. Nyingine, mrabaha hulipwa kwa Serikali mwanzoni kabisa mwa uzalishaji, huku urejeshaji wa gharama za mwekezaji ukiwekewa kikomo cha asilimia 50.

“Mfumo huu hutoa fursa kwa Taifa kuanza kupata mapato yatokanayo na uzalishaji wa mafuta au gesi asilia mara tu uzalishaji unapoanza,” alisema Komba.

Urudishaji gharama

“Muwekezaji huruhusiwa kujirudishia gharama zake kwa mwaka bila kuzidi asilimia 50 ya gharama zote na faida hugawanywa kati ya muwekezaji na Taifa,” alisema Komba.

Kuhusu uwezekano wa Serikali kubambikiwa gharama ambazo hazikuwepo, ili mwekezaji atumie nafasi hiyo kujinufaisha wakati wa kujirudishia gharama, Komba amesema hiyo haiwezekani.

Akifafanua zaidi, Komba amesema Taifa kupitia TPDC, hupitia mpango kazi na bajeti ya kila mwaka ya muwekezaji na kutoa idhini ya mpango kazi na bajeti hiyo kutumika. Baada ya kuidhinisha bajeti ya mwekezaji, Komba amesema pia TPDC, hufanya ukaguzi wa gharama zote ambazo muwekezaji ametumia ambazo atahitaji kuzirejesha uzalishaji utakapoanza.

Naye Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa TPDC, Gabriel Mwero, alisema ukaguzi wa gharama anazotumia mwekezaji katika utafiti, hufanyika kwa kila kampuni iliyowekeza katika utafiti hapa nchini.

“Aina ya ukaguzi unaofanyika, ni ule wa asilimia 100 na hivyo kuhakikisha kwamba hakuna gharama ambayo haijaangaliwa. Hivyo kampuni hujirudishia zile gharama ambazo zimekaguliwa na TPDC na kuidhinishwa,” alisema.

Je uvunaji umeshaanza Mpaka sasa kwa mujibu wa taarifa za TPDC, kampuni zilizofanya ugunduzi mkubwa katika kina kirefu cha bahari za BG na Statoil, kiasi cha futi za ujazo zaidi ya trilioni 47.8, hazijaanza kuvuna gesi hiyo. Kwa mujibu wa taarifa hizo, uvunaji hauwezi kufanyika bila kujenga mtambo wa kugeuza gesi asilia kuwa kimiminika, ili ifae kusafirishwa ndani au nje ya nchi.

Wiki hii ndio TPDC imetangaza upatikanaji wa hati miliki ya ardhi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa mtambo huo wa kuchakata na kusindika gesi asilia (LNG), ili iwe kimiminika. Eneo la ardhi hiyo lipo katika kiwanja Na.1-Kitalu “A”, Likong’o katika Manispaa ya Lindi na lilipendekezwa na kuchaguliwa kwa pamoja kati ya TPDC na wawekezaji wa mradi huo.

Sheria kali Kuhusu udhibiti wa mapato, tayari Tanzania ina Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi wa Mwaka 2015, ambayo imeweka adhabu kwa watakaobainika kuchota fedha katika Mfuko wa Mafuta na Gesi utakaoanzishwa na sheria hiyo.

Miongoni mwa adhabu hizo ni pamoja na faini isiyopungua kiasi mtu alichochukua au kupoteza, kifungo cha miaka 30 jela na kufilisiwa mali zao.

Kwa mujibu wa Sheria hiyo, Mfuko huo wa Mafuta na Gesi utakuwa na akaunti mbili zitakazotunzwa na kusimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania. Akaunti hizo ni Akaunti ya Kupokea Mapato na Akaunti ya Kutunza Mapato.
  • via HabariLeo

Watanzania vijana 9 wachangishana milioni 500/= na kuanzisha kiwandaVIJANA tisa wenye vipato vya kawaida kutoka maeneo mbalimbali nchini, wametimiza ndoto ya umoja ni nguvu kwa kuanzisha kampuni ya kizalendo wanayotaka iongoze nchini kwa uzalishaji wa bidhaa zitokanazo na misitu zitakazo zingatia ubora wa kimataifa.

Vijana hao German Ibreck, Anael Samuel, Prosper Moshi, Edward Masuzya, Edwin John, Baraka Maduhu, Leevan Maro, Beatrice Masalu na Elisha Msengi wameanzisha kampuni ijulikanayo kama Agora Wood Products Ltd.

Kampuni hiyo iko katika hatua za awali za ujenzi wa kiwanda cha kutibu nguzo za umeme na bidhaa zingine zifananazo na hizo katika kijiji cha Igwachanya, kata ya Mseke, wilayani Iringa.

Jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda hicho kitakachokuwa na uwezo wa kutibu wastani wa nguzo za umeme 200 kwa siku, liliwekwa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza katika hafla iliyohudhuriwa na wananchi wa kijiji hicho, na viongozi wa serikali ya mkoa na wilaya ya Iringa.

Afisa Mtendaji wa kampuni hiyo, Elisha Msengi alisema kiwanda hicho kitatumia teknolojia mpya katika kuwezesha dawa kupenya vizuri ndani ya nguzo na bidhaa zingine zitokanazo na miti na hivyo kuongeza ubora na matumizi ya muda mrefu ya bidhaa hizo.

“Kitakapokamilika, kiwanda kitatoa ajira za moja kwa moja zaidi ya 50 na nyingine 200 zisizo za moja kwa moja,” alisema na kuongeza kwamba kiwanda hicho kitachangia kwa kiwango kikubwa mapato ya fedha za halmashauri na serikali kuu kwa njia ya kodi na tozo muhimu.

Alisema ujenzi wa majengo na miundombinu iliyopo katika kiwanda hicho ulianza Septemba, 2015 ukihusisha ununuzi wa mitambo, ardhi, malighafi za ujenzi na kazi kwa zaidi ya Sh Milioni 500 ambazo zimechangwa na vijana hao.

Alisema hadi kukamilika kwake, kiwanda hicho kitagharimu zaidi ya Sh Bilioni 2.5 na akashangaa mradi huo wenye manufaa makubwa kwa mkoa na Taifa ulivyokosa mkopo kutoka katika moja ya benki za hapa nchini pamoja na kusubiri kwa miezi tisa tangu mkopo huo uombwe.

Akiweka jiwe la msingi katika kiwanda hicho, Mkuu wa Mkoa wa Iringa alisema; “natiwa moyo na kufurahishwa sana kuona kwamba kiwanda hiki kimejengwa na kumilikiwa na wazawa kwa asilimia 100.”

Masenza alisema serikali ya awamu ya tano ya Dk John Magufuli imelenga kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda ili badala ya kuuza malighafi, ziuzwe bidhaa ambazo zimetengenezwa kwa ubora na zenye thamani katika soko la ndani na nje.

Alisema ili kufikia lengo hilo serikali hiyo imedhamiria kuondoa ukiritimba ambao umekuwa ukikatisha tamaa wawekezaji wa ndani na nje wenye nia ya kuwekeza katika sekta ya viwanda.

Ili kianze kufanya kazi kiwanda hicho ambacho mitambo yake ya kutibu bidhaa hizo za miti inaendelea kufungwa, kinahitaji kuunganishwa na umeme wa njia tatu na transfoma na ujenzi wa barabara ya mtaa kuelekea kiwandani.

“Tunawakaribisha Tanesco washirikiane nasi kupitia mpango wa Public Private Partnership, kifedha, kiutaalamu na kiushauri katika kuzalisha nguzo bora za umeme,” alisema Afisa Mtendaji wa kampuni hiyo.


Call for applications: Master of Bioethics

Application


To apply for the 2016-2017 academic year, you can do so as of 1 November 2015.
The deadline for applications for EEA students is 1 June 2016.
The deadline for applications for non-EEA students is 1 March 2016.

How to apply


1. Deadline for submission of applications:
  • March for non-EEA applicants.
  • June for EEA applicants and non-EEA applicants living in Belgium with a residence permit.
Late applications are allowed and considered on an individual basis. The candidates need to contact the programme coordinator ([email protected]) prior to submission of their application to request permission for a late application.

Please read carefully the admission criteria and the information for international students before starting your application.

2. Application procedure

Fill in the preregistration form for students (Winword). Send the preregistration form + a letter of motivation by e-mail to [email protected]

Fill in the online application form.

3. Selection procedure
  • The selection committee decides about acceptance of the applicants and in addition about the grant of the scholarships. Acceptance to the programme does not imply the grant of a scholarship.
  • It is possible that the selection committee invites you for an interview by telephone and/or webcam.
  • The selection procedure takes about 12 weeks.
  • You will receive the decision of the consortium by e-mail. After that the administrative procedure of admission will be started.