Comparing college rankings: The Top 10 Colleges in the US

Comparing College Rankings
Source: BestCollegeReviews.org

Katuni: Wimbo gani ulikukuna zaidi mwaka huu...NEMC yakataza hoteli kutoza fedha wananchi wanaobarizi 'beach'

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limewataka wawekezaji wa hoteli zilizopo pembezoni mwa bahari kuacha kuwatoza wananchi fedha za kiingilio wanapokwenda katika fukwe hizo kupunga upepo au kuogelea.

Tamko hilo limekuja kutokana na baadhi ya hoteli katika Jiji la Dar es Salaam kubainika kutoza fedha kuanzia Sh 10,000 hadi 40,000 kwa mtu mmoja kama gharama za kuogelea.

Uchunguzi uliofanywa na MTANZANIA umebaini kuwa wamiliki wa hoteli hizo wamekuwa wakifanya hivyo katika sikukuu mbalimbali na zile za mwisho wa mwaka, jambo ambalo limekuwa likileta kero kwa jamii.

Akizungumzia suala hilo Mwanasheria wa NEMC, Manchari Heche, alisema kwa mujibu wa sheria, fukwe zote ni mali ya umma, hivyo wananchi hawatakiwi kutozwa fedha wakati wanapokwenda kutembea au kuogelea.

“Kifungu cha 57 cha sheria ya mazingira kimeweka ukomo wa mpaka wa kila kiwanja kilichopo karibu na ufukwe.

“Beach (fukwe) zote ni mali ya umma kwa sababu kuna mipaka yake, hivyo kitendo cha kuwatoza wananchi fedha za kuingia katika fukwe hizo ni kosa kisheria na wanaofanya hivyo wanapaswa kuacha mara moja,”alisema Heche.

Kuhusu ujenzi karibu na fukwe hizo, Heche alisema wawekezaji wa hoteli wanapaswa kujenga umbali wa mita 60 kutoka katika ukingo wa bahari na kama kuna mwekezaji aliyezidisha umbali huo anapaswa kubomoa mwenyewe kabla hajachukuliwa hatua za kisheria.

“Wale waliokiuka na kujenga hadi katika eneo la bahari waanze sasa kuboboa wenyewe kwa kuwa zoezi la bomoabomoa nao litawahusu”, alisema.

Wiki iliyopita Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano na Mazingira), January Makamba alitoa taarifa ya Serikali kwamba sheria hiyo ya NEMC itatekelezwa kwa ukamilifu wake.

Alisema operesheni ya kuwaondoa watu wanaoishi na kufanya shughuli kwenye maeneo ya kingo za mito na maziwa, fukwe za bahari, maeneo oevu na maeneo ya wazi imeshaaanza.

Katika Jiji la Dar es Salaam, zoezi la kuwaondoa wananchi waliojenga mabondeni lilianza rasmi Desemba 17 mwaka huu na kusimama kwa muda ambapo litaendelea Januari 5 mwakani huku, zaidi ya nyumba 353 zikiwa tayari zimebolewa na nyingine zaidi ya 8,000 zinatarajiwa kubomolewa.

Polisi 6 wapandishwa kizimbani Dar kwa tuhuma za kuua wafanyabiashara Sinza

ASKARI sita waliokuwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kuhusishwa na mauaji ya wafanyabiashara, jana wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya kukusudia.

Washtakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Thomas Simba.

Mbele ya Hakimu Simba, Wakili wa Serikali Mkuu, Mutalemwa Kisheni, aliwataja washtakiwa kuwa ni Inspekta Bon Mbange mkazi wa Magomeni, F 919 Sajenti Filbert Nemes na Askari wa Kikosi cha Kuzuia Ujangili, Asubile Mwakyusa, Deogratius Mwageni na Joseph Jimmy.

Kisheni alidai washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa Desemba 19, mwaka huu maeneo ya Sinza, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, waliwaua Yasin Rashid na Samson Msigale.

Washtakiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Awali Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, alieleza kukamatwa kwa washtakiwa hao wakihusishwa na utata wa mauaji ya wafanyabiashara hao.

Kamanda Kova alidai taarifa zilidai kuwa Rashid na Samson wanaodaiwa kuwa ni majangili, waliuawa wakati wakirushiana risasi na askari hao wa kikosi maalumu cha kukabiliana na ujangili maeneo ya Sinza.

Pia alidai pamoja na askari hao sita kukamatwa mwingine aitwaye Issa Kazimoto anatafutwa na polisi baada ya kukimbilia kusikojulikana.

Walioiba mahindi ya msaada wahukumiwa kifungo miaka 5 jela

Watumishi wawili wa halmashauri ya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu wamefungwa jela miaka mitano kwa kosa la wizi wa mahindi ya msaada katika kijiji cha Masamwa tukio la wizi walikifanya Januari 7 na 8,2013.Mahindi hayo ni Tani 10.77 zenye thamani ya Sh 13275000.Waliokumbwa na adhabu hizo ni CHARLES KISENHA (VEO BUSHITALA) na ISACK GAMBISHI (AFISA KILIMO KATA YA BUSILILI).

Rais mstaafu Kikwete, Waziri Lwenge wakagua mitambo ya maji Wami, Chalinze


Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (katikati), akizungumza na Waziri wa Maji, Gerson Lwenge wakielekea kukagua mitambo ya kusafisha na kusafirisha maji Wami, katika Halmashauri ya Mji wa Chalinze, mkoani Pwani, Desemba 30, 2015.

Waziri wa Afya aahidi kutatua matatizo MSD


Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akitembelea moja ya ghala la kuhifadhia dawa iliyopo makao makuu ya MSD,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laureane Bwanakunu na watatu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya MSD Prof.. Idris Mtulia.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ametembelea Makao Makuu ya Bohari ya Dawa (MSD) na kuahidi kuwa balozi wa kuhakikisha deni la serikali linalipwa ili kuiwezesha MSD kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Waziri huyo ameeleza hayo baada ya Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu kueleza kuwa ukosefu wa fedha na deni la serikali ni changamoto kubwa inayoathiri utekelezaji mzuri wa majukumu ya MSD.

Mbali na hilo, Waziri wa Afya amesema mbali na deni hilo, hata kiasi cha fedha kinachotengwa na serikali kwaajili ya hospitali, vituo vya afya na zahanati na kununua dawa hakitoshelezi mahitaji, hivyo lazima suala hilo lifanyiwe kazi mapema, huku akisisitiza hata kiasi hicho kidogo kinachopatikana kitumike vizuri.

Katika hatua nyingine ameishauri Bohari ya Dawa kuanza utaratibu wa kununua dawa na vifaa tiba moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, kuhakikisha dawa muhimu zinapatikana wakati wote na kuiagiza MSD itangaze kwenye vyombo vya habari dawa zote ambazo zinapelekwa vituoni, zahanati na kwenye hospitali, ambapo Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu ameeleza kuwa tayari MSD imeshaanza kubandika kwenye mbao za matangazo za hospitali orodha ya dawa inazofikisha.

Waziri huyo ambaye alifuatana na Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Donald Mbando na watendaji wengine pia alitembelea maghala ya kuhifadhia dawa ya MSD, jengo la ofisi linalojengwa pamoja na kuwa na mkutano na menejimenti ya MSD, ambapo pamoja na mambo mengine ameipongeza MSD kwa hatua iliyofikia ya kuweka nembo ya GOT kwenye vidonge vyake ili kudhibiti upotevu wa dawa za serikali pamoja na kuanzisha maduka ya dawa Muhimbili, na mengine yanayotarajia kufunguliwa hivi karibuni mkoani Mbeya, Arusha na Mwanza.

Waziri Ummy Mwalimu alihitimisha kwa kusema kuwa ajenda yake kuu ni upatikanaji wa dawa kwa wakati, kama rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alivyoaainisha, hivyo MSD itekeleze majukumu yake ipasavyo kwani mafanikio ya MSD ni mafanikio kwake pia.

Waziri Ummy akiuliza jambo kwa wafanyakazi wa bohari hiyo.
Waziri huyo akiendelea na ukaguzi wa maghala hayo, kulia ni Mkurugenzi wa Ugavi Misanga Muja na kushoto ni mwenyekiti wa Bodi ya Bohari hiyo.

Baadhi ya watumishi wakiendelea na kazi ya kuhakiki dawa kwenye moja ya ghala mojawapo.

Waziri Ummy akielekea kwenye ujenzi wa jengo jipya linaloendelea kujengwa, ambapo linatarajiwa kumalizika kujengwa mwezi Juni, 2016 ,Kushoto ni Katibu mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Donnan Mmbando.

Mkurugenzi wa MSD Bwanakunu akieleza dira,malengo na majukumu ya Bohari hiyo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiangalia dawa zilizowekwa nembo ya serikali (GoT) ambayo itasaidia udhibiti wa upotevu wa dawa nchini.

Waziri huyo akionesha kopo la dawa la Bohari ya dawa.

Waziri Ummy akimuonesha ukurasa wa ugawaji fedha za bohari Mwenyekiti wa Bodi ya Bohari ya dawa Prof.Idris Mtuliya.
  • Picha zote kwa Niaba ya Wizara ya Afya

Wenyeviti wamchukulia hatua Mwenyekiti wa Kijiji

Wanafunzi katika shule ya msingi Shenda wakiwa wamekaa kwenye moja ya darasa lililosakafiwa
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na kilio toka kwa wananchi kuhusu ubadhirifu wa fedha za umma unaofanywa na viongozi waliowachagua pasipo kuchukua hatua zozote. Ukimya huu wa wananchi ndio unaosababisha kilio hicho kuendelea kukuwa kila siku. Ila vilio hivi huishaga pale tu wananchi wanapoamua kwa dhati kuchukua hatua, kama walivyofanya wananchi wa kijiji cha Shenda. Shenda ni moja kati ya vijiji zaidi ya 200 vinavyofanya kazi na programu ya Chukua Hatua mkoani Geita.

Kijiji hiki kinapatikana kata ya Masumbwe wilaya ya Mbogwe, mkoa wa Geita. Jumla ya wakazi 2,454 wanaishi katika kijiji hiki wakijishughulisha na shughuli za kilimo, uchuuzi na uchimbaji wa madini. Fredson Yaida ni mmoja kati ya waraghabishi wanaofanya kazi na program hii, kama walivyo waraghabishi wengine yeye pia alichaguliwa na wananchi na baadaye kuhudhuria mafunzo maalumu ya uraghabishi, “Baada ya kuchaguliwa basi tulienda kwenye mafunzo kule Ushirombo. Kule tulijifunza na kujengewa uwezo wa kufahamu mapato nmatumizi, kujua vyanzo vya mapato vya maeneo tunayotoka, haki na wajibu wetu katika kusimamia mali za umma lakini pia kuweza kuzihojia pale inapohitajika,” anaelezea Fredson Yaida. Kwa kuwa mraghabishi hana mamlaka ya kisheria ya kuitisha mikutano kwa ajili ya kuwashirikisha wananchi wote kile alichojifunza, badala yake amekuwa akitembelea vikundi mbalimbali kwa ajili ya uhamasishaji na kushirikishana. Vikundi hivyo ni pamoja na Mkombozi, Jiandae na Twende na Wakati; kila kikundi kina wastani wa wanachama 25 mpaka 30.

Akimuelezea jinsi anavyomuelewa mraghabishi, mwenyekiti mpya wa kijiji cha Shinde, Andrea Lubango anasema, “huyu bwana Fredson Yaida na kikundi chake wamekuwa mstari wa mbele katika ku- hamasisha wanakijiji kujua mambo ya mapato ya kijiji chao na kuwataka kuulizia ili kusudi waelewe zaidi.” Wakati wa majadiliano na wanachama wa vikundi hivyo na makundi mbalimbali ya jamii, suala lililojitokeza ni la mapato yanayotokana na malori yanayobeba mchanga wenye masalio ya dhahabu toka kijijini hapo. Akielezea jinsi alivyoitoa hoja hiyo kwa wenzake Mraghabishi Fredson anasema, “Niliwaambia jamani sasa hivi tuelimike sasa si mnaona magari hapa yanapakia mizigo, ushuru hatuupati, hata mapato hatusomewi imekuwaje nchi yetu hivi na tuna rasilimali na magari kila siku yanapakia mizigo, yapo magodown mengi tu yamejengwa hapa Shenda tulikuw hatupati hata shilingi.” Malori hayo huja kubeba mchanga unaokuwa umebakia kutoka mgodi wa Shenda kwenye mawe yaliyovunjwa na wenye makarasha. Mwenye lori huja kununua mchanga huo uliobakia na kuondoka nao pasipo kijiji kupata mapato tokana na mchanga mali huo.

Mgodi wa shenda hutegemewa kama njia ya kujipatia kipato hususani wakati wa hali mbaya ya kilimo baadhi ya wanavijiji huenda kuajiriwa na wamiliki wa mashimo hayo ya dhahabu. Wanakijiji huchimba udongo kisha huchekecha ili kupata dhahabu na baada ya kuchekecha mchanga huukusanya pembeni mwa mashimo ya dhahabu kwa ajili ya kuuza. Fredson anasema wengi wa vijana ndio hujishughulisha na shughuli za migodi ili kujipatia kipato. Fununu za kuwepo kwa wawekezaji katika mgodi wa Shenda wakawa wanajiuliza haya malori yanayopishana na shehena ya mchanga uliochanganyikana na dhahabu pasipo wao kupatiwa taarifa yoyote uliwapa shaka na hivyo kutaka kujua zaidi. Kupitia mraghabishi, vikundi na wanakijiji ukawekwa mkakati wa jinsi ya kufuatilia hivyo kupitia uhamashaji wananchi wakaanza kuongea kichinichini hatimaye wakaamua kuchukua hatua.
Mraghabishi Fredson Yaida (wa tatu toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi wa wanachama wa vikundi, Mwenyekiti wa kijiji (wa kwanza kulia) na baadhi ya wajumbe wa serikali ya kijiji cha Shinde wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya ofisi ya kijiji.
“Tukaanza kuhojiana sisi kwa sisi vipi mbona magari yanasomba tu, watu wakasema tuyasimamishe yasisombe, bahati nzuri serikali ya kijiji ikaliona hilo kwa haraka, wakawa wameitana mwenyekiti wa kijiji na wajumbe na mtendaji wa serikali ya kijiji. Wakaliwekea mkakati wa kulifuatilia,” anaelezea Fredson Yaida. Kamati ya serikali ikiwa tayari imeshanusa kilichopo mbele yao iliwalazimu kuchukua hatua za haraka kujinusuru na hasira za wananchi, kama anavyoelezea mjumbe wa kamati ya kijiji, Makemba Kubezia,“Tukaanza kujiuliza sisi wenyewe wa kamati ya kijiji, mh, mbona huu mchanga unatoka kwenye mashimo yetu pasipo sisi kujua, labda hapo mwenyekiti amefanya bila kutuhusisha serikali ya kijiji. Baadaye basi katika ufuatiliaji wananchi wakaanza kutuhoji ikabidi tuamke kweli na kuchukua Hatua stahili,”

Hivyo kamati ya serikali ya kijiji ikabidi imwite mwenyekiti wa kijiji ili kujua nini kinaendelea katika shughuli hiyo na kukubaliana kulifuatilia suala hilo ofisi ya kata na baadaye kwenda kwa mhusika (mwenye malori) ili kujua anasomba mchanga kwa kibali kipi. Lakini katika hali ya kushangaza aliyekuwa Mwenyekiti wa kijiji cha Shenda John Mapoli aliwachenga wenzake na kwenda peke yake kuonana na mtu anayeleta malori kijijini kuchota mchanga wenye masalio ya dhahabu. Baada ya kurudi hakuwaita wenzake wa serikali ya kijiji kuwapa mrejesho wa safari yake. Kukawa na maneno ya kichini chini kwamba mnunuzi humpa mwenyekiti bakshishi (rushwa) ili apate nafuu katika bishara yake ikiwa ni pamoja na kukwepa hiyo tozo.

Iligundulika baadae kuwa hakutaka wagundue kuwa alikuwa akipokea pesa kutoka kwa mnunuzi, kwani alikuwa hazifikishi katika ofisi yakijiji.Kutokana na kile kilichojitokeza ikabidi uitishwe mkutano mkuu wa kijiji uliosimamiwa na mtendaji wa kata. Ni dhahiri wananchi hawakuwa na imani na Mwenyekiti wao tena na hivyo kumtaka aachie madaraka na kisha kumteua mwenyekiti wa muda, Andrea Lubango atakaye kaimu kiti hicho mpaka uchaguzi ujao. “Hivyo baada ya wananchi kumuondoa tukambana na yule mwenye lori. Kwa kuanzia akatoa kiasi cha shilingi laki tano na miifuko 60 ya sementi kati ya hiyo, 30 imetumika kwa ajili ya ukarabati madarasa mawili na mi-fuko mingine 30 itatumika kwenye ujenzi wa zahanati, na kuna mtu kuwalazimisha. Tatizo ni watendaji wa vijiji,” Akitoa mfano wa hali hiyo ya watendaji wa vijiji Diwani wa kata ya Kishapu anasema, “Kijiji hiki hapa (Kishapu) kimemaliza karibu miezi tisa bila kusoma mapato na matumizi na nimekuwa nikimtumia mtendaji wangu wa kata kwamba waandikie wawe wanasoma mapato na matumizi. Lakini na yenyewe ikawa bla bla, mpaka nikalazimika kufika ofisi ya mkurugenzi badala yake akaandikiwa, ndio akasoma mapato na matumizi,”

Kwa upande wa Kata ya Mwakipoya mheshimwa Thabita anasema, “Watendaji wangu sio wazuri hawataki kualika mikutano, mambo yote yamekwama kwa ajili ya watendaji. Nimefanya mikutano miwilitu katika kijiji cha Mwangongo na hapa Mwakipoya. Changamoto kubwa ambayo alikumbabana nayo kwenye vile vijiji sana sana ni malalamiko kwa watendaji kwamba hawataki kusoma taarifa za mapato na matumizi. na hatua aliyochukua Mheshimiwa Thabita ni kupeleka taarifa hizi kwa mkurugenzi na mkuu wa wilaya kwa hatua zaidi. Lakini pamoja na changa- mwingine alichukua mchanga akatuletea mifuko 15,” anaeleza Mwenyekiti wa sasa wa kijiji cha Shande, Andrea Lubango. Kwa hakika wananchi ndio wamiliki wa kiti cha uenyekiti na wanapoamua kuchukua kiti chao wanaweza, kama wana Shenda wangeamua kukaa kimya na kundelea kuhuzunika na kulalamika tu pasipo kuchukua hatua hakuna ambacho kingAewezekana Na watoto wao wangeendelea kusoma kwenye madarasa yenye vumbi kutokana na kutokuwa na sakafu. Hatua zaidi zinatakiwa kuchukuliwa ili kuweza kuhakikisha Wanashenda wanapata mapato yenye thamani sawa na mchanga uliochanganyika na dhahabu.

[update] Waziri Mkuu Majaliwa atoa siku 2 apewe taarifa ya ufisadi KIGODECO


Januari 6, 2015...
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akijionea utayarishaji wa Samaki aina ya Dagaa katika Soko la Kisasa la Kibirizi mjini Kigoma. (Picha na Emmanuel Matinde).

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 

* Ni ubadhirifu wa fedha za umma, atoa siku mbili kukamilisha uchunguzi
* Ataka apewe taarifa ya maandishi Januari Mosi, 2016


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku mbili kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Eng. John Ndunguru kukamilisha uchunguzi wake na kumpatia taarifa ya maandishi juu ya tuhuma ubadhirifu wa fedha za umma unaohusisha uuzwaji wa jengo la KIGODECO na viwanja 12 vya Manispaa ya Kigoma/Ujiji ambao unadaiwa kukiuka taratibu.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumatano, Desemba 30, 2015) kwenye ukumbi wa NSSF, mjini Kigoma wakati akizungumza na viongozi na watendaji mbalimbali wa mkoa huo alipokuwa akifanya majumuisho ya ziara yake ya siku mbili mkonai humo.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema anazo taarifa kuwa jengo hilo liliuzwa kwa sh. milioni 370/- pamoja na jengo jingine la MIBOS kwa sh. milioni 50/- licha ya kupewa barua na Mkuu wa Mkoa huo kusitisha uuzwaji wa jengo pamoja viwanja hivyo, bado liliuzwa.

“Katibu Tawala wa Mkoa kaa na Mkurugenzi wa Manispaa, Mhandisi wa Manispaa na Mhasibu na unipatie taarifa kwa maandishi ifikapo Jumamosi hii,” alisema Waziri Mkuu huku akishangiliwa.
“Nataka kujua nani alifanya tathmini ya jengo, ni kwa nini jengo liliuzwa kwa thamani hiyo, je ndiyo thamani halisi ya jengo? Ni kwa nini RC alipozuia, utaratibu uliendelea? Je, utaratibu wa uuzaji ulifuatwa? Ni kwa nini viwanja viliuzwa chini ya thamani,? Katibu Tawala kaa na watu wako na uniletee hiyo taarifa kwa maandishi. Tukigundua kuna mianyamianya tutachukua hatua za kinidhamu,” alisema.

Viongozi walioagizwa kukutana na Katibu Tawala wa Mkoa ni Mkurugenzi wa Manispaa, Eng. Boniface Nyambele; Mhandisi wa Manispaa, Eng. Boniface William na Mhasibu wa Mapato wa Manispaa, Ndg. Bawili Mkoko.

Kuhusu uuzwaji wa jengo na viwanja, imebainika kuwa Mkuu wa Mkoa huo, Luteni Kanali (Mst), Issa Machibya alizuia uuzaji huo kwa barua ya tarehe 16 Juni 2015 akitaka viwanja hivyo vitumike kwa matumizi ya manispaa na mchakato huo usitishwe hadi mwakani lakini agizo lake lilipuuzwa na jengo likauzwa kwa sh. milioni 370 ambayo ni bei ya kiwanja pekee.

Tuhuma nyingine zinazopaswa kuchunguzwa ni pamoja na matumizi ya sh. milioni 809 kwa ajili ya ujenzi wa maabara. Kiasi hicho kilitolewa kutoka kwenye fedha za miradi ya maendeleo (Capital Development Grants-CDG), Mradi wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo na Mifugo (ASDP), Mradi wa Uendelezaji Miji (Tanzania Strategic Cities Programme –TSCP) na Miradi ya Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (SEDP).

Inadaiwa kwamba Mkurugenzi huyo kwa kushirikiana na baadhi ya watumishi wa idara ya mipango na fedha walitumia ujenzi wa maabara kama kigezo cha kuchota fedha hizo bila kutoa taarifa kwa wakuu wa idara husika ambao walikasimiwa fedha hizo.

Tuhuma nyingine ni manunuzi hewa ya vipuri (spare parts) vyenye thamani ya sh. milioni 8 na manunuzi hewa ya stationeries yenye thamani ya sh. milioni 4.6/-. Haya yanadaiwa kufanywa Julai 25, mwaka huu na Mkurugenzi huyo akishirikiana na Mhasibu Mkoko.

Waziri Mkuu amerejea jijini Dar es Salaam mchana huu.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, DESEMBA 30, 2015.

Wajasirimali katika Soko la Kibirizi wakitayarisha Samaki maarufu kwa wakazi wa mkoa wa Kigoma kwa jina la Mgebuka.

Agizo la TCRA kuhusu “spoofing” na adhabu kwa makampuni ya simu yaliyoshindwa kulinda wateja

JAMHURI YA YA MUUNGANO YA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

HATUA ZA KISHERIA NA KIUDHIBITI KWA MAKAMPUNI YA SIMU YALIYOSHINDWA KULINDA WATEJA WAKE KITEKNOLOJIA NA KISHERIA KUHAKIKISHA USALAMA WA MAWASILIANO YAO


1. Katika shughuili zake za udhibiti wa huduma za mawasiliano nchini, Mamlaka ya Mawasilaino Tanzania imepokea malalamiko kutoka kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano dhidi ya kuwepo mazingira yasiyo salama katika huduma za mawasiliano na hivyo kusababisha kufanyika kwa vitendo vya utapeli unaofanywa kwa kutuma jumbe za udanganyifu na kulaghai, hivyo kusababisha watu kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu. Kwa mfano kupokea ujumbe kutoka namba unayoifahamu ukikuagiza utume fedha au ujumbe wa kashfa au matusi wakati hautoki kwa mhusika mwenye namba. Mamlaka imepokea malalamiko mengi kutoka kwa wateja na malalamiko mengine hupelekwa Polisi. Kwa miezi miwili tu, matukio 42 yameripotiwa Polisi pamoja na TCRA ambayo tukio moja tu linakuwa na ulaghai wa takribani milioni 25 peke yake.

2. Tarehe 16 Oktoba, 2015 Mamlaka iliwakumbusha watoa huduma za simu nchini juu ya wajibu wao kuchukua hatua za kusheria na kitaalamu ili kulinda watumiaji dhidi ya utumaji wa jumbe za kilaghai na kuchukua hatua mara moja kuzuia mitandao yao kutumika kutuma jumbe za udanganyifu na kulaghai. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Mamlaka tarehe 16 Desemba, 2015 Mamlaka ilibaini kuwa kampuni za Benson Informatics Limited (inayojulikana kama Smart), MIC Tanzania Limited (inayojulikana kama Tigo), Airtel Tanzania Limited, Viettel Tanzania Limited (inayojulikana kama Halotel) and Zanzibar Telecom Limited inayojulikana kama Zantel) zimeshindwa, zimepuuzia na zimekataa kufuata maagizo ya Mamlaka kuchukua hatua mara moja kuzuia mitandao yao kutumika kutuma jumbe za kilaghai kinyume na Kanuni Na.8(a) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya mwaka 2011 [the Electronic and Postal Communications (Computer Emergency Response Team) Regulations, 2011].

3. Tarehe 18 Disemba, 2015 Mamlaka iliwaamuru watoa huduma za mawasiliano waliotajwa hapo juu kufika mbele ya Mamlaka na kujieleza kwa nini hatua za kisheria zisichukuliwe dhidi yao kwa kuvunja sheria na kanuni ya 8(a) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielectroniki na Postal ya Mwaka 2011 [the Electronic and Postal Communications (Computer Emergency Response Team) Regulations, 2011] kwa kushindwa kuweka mazingira salama kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano.

4. Watoa huduma walifika na kutoa maelezo ya utetezi kati ya tarehe 21 na 23 Desemba, 2015.

5. Baada ya kuwasikiliza na kutilia maanani utetezi wa watoa huduma na kwa mujibu wa uchunguzi na majaribio uliofanywa na Mamlaka, Mamlaka imejiridhisha kuwa mitandao ya watoa huduma waliotajwa hapo juu haikuwa salama na kuwa watoa huduma hao walishindwa kufuata maelekezo ya Mamlaka juu ya kuweka mazingira salama katika huduma wanazotoa. Hivyo Mamlaka imejiridhisha kuwa watoa huduma wamekiuka matakwa ya Kanuni ya 8(a) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielectroniki na Postal ya mwaka 2011 (The Electronic and Postal Communications (Computer Emergency Response Team) Regulations, 2011) inayowataka watoa huduma kuweka mazingira ya mitandao salama kwa kuchukua hatua za kusheria na kitaalamu ili kulinda watumiaji dhidi ya uhalifu ikiwa ni pamoja na utumaji wa jumbe za kilaghai kupitia mitandao yao.

6. Kwa mujibu wa Kifungu cha 17 cha Jedwali la Pili katika Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, Sura ya 306 ya Sheria za Nchi, kinachoipa Mamlaka uwezo wa kutoa adhabu kwa Wenye Leseni dhidi ya uvunjifu wa Sheria, Kanuni na Masharti ya Leseni, Mamlaka ya Mawasiliano imetoa:

A. Onyo kali kwa Kampuni za:
(i) Benson Informatics Limited (inayojulikana kama Smart),
(ii) MIC Tanzania Limited (inayojulikana kama Tigo),
(iii) Airtel Tanzania Limited,
(iv) Viettel Tanzania Limited (inayojulikana kama Halotel), na
(v) Zanzibar Telecom Limited (inayojulikana kama Zantel).

kwa kushindwa kutimiza matakwa ya Kanuni ya 8(a) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Postal ya mwaka 2011 [the Electronic and Postal Communications (Computer Emergency Response Team) Regulations, 2011] kwa kushindwa kuweza mazingira salama kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano.

B. Imeamuru Kila Kampuni husika:
(i) Kuhakikisha kuwa, kuanzia siku ya kutolewa kwa amri hii, inaweka mazingira salama katika mtandao wake yatakayozuia utumaji wa jumbe za kilaghai (yaani ‘spoofed messages’) na matishio mengine ya kiusalama;
(ii) Kulipa faini ya Shilingi za Kitanzania Milioni Ishirini na Tano (Shs 25,000,000.00) kwa Mamlaka ya Mawasiliano kabla ya tarehe 29 Januari, 2016; na
(iii) Endapo Makampuni haya yatashindwa kutimiza amri Na.2 hapo juu, Mamlaka itachukua hatua zaidi za kisheria na kiudhibiti dhidi ya Kampuni ya Simu husika.

7. Aidha, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inapeda kuchukua fursa hii kuwatahadharisha wananchi kuwa makini na jumbe za kuwataka kutuma fedha bila ya kuwa na uhakika. Inashauriwa kuhakiki ujumbe husika kwa kupiga simu na kuongea na mhusika kabla ya kufanya maamuzi ya kutuma fedha hata kama namba inayotumika unaijua. Vilevile wawe makini wanapopokea jumbe zinazoonesha zinatoka kwa mtu fulani wanayemjua kumbe ni matapeli wanaotumia ulaghai kwa njia hii ya “spoofing”.

IMETOLEWA NA

Dkt. Ally Y. Simba
MKURUGENZI MKUU
30 Desemba, 2015

Walioteuliwa na Rais Magufuli kuwa Makatibu Wakuu na Manaibu wa Wizara

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue Mara baada ya kumkabidhi orodha ya Makatibu na Manaibu Katibu Wakuu aliwateua leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Katuni: Maongezi ya kutatua mzozo Zenj...

Waziri Nnauye ampongeza Samata kwa kusajiliwa kucheza Ubelgiji


Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye (kushoto) akiongea na Mchezaji wa Timu ya TP Mazembe Mbwana Samatta (kulia) leo jijini Dar es salaam.Mbwana amemtembelea waziri Nape ofisini kwake na kuomba baraka za wizara katika kinyanganyiro cha kugombea uchezaji bora wa afrika anayechezea ligi za ndani na pia kumpa habari njema za yeye kutegemea kujiunga na timu ya Ubelgiji ya Genk.

Waziri wa Habari,Utamaduni,sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye (katikati )akiongea na waandishi wa Habari na kuwaomba watanzania kumwombea Mbwana Samatta ili ashinde katika kinyanganyiro cha kugombea uchezaji bora wa afrika anayechezea ligi za ndani kwani ni jambo la Taifa zima.Mhe Nape pia alimhakikishia kuwa Serikali ipo nyuma yake na ipo katika mkakati wa kuifanya michezo kuwa Shughuli Rasmi kwani itawafaidisha wanamichezo na Serikali kwa kupata kodi.

Mchezaji wa TP Mazembe Mbwana Samatta (wa kwanza kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) sababu za yeye kumtembelea Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika ofisi ya Wizara hiyo. Mbwana alisema kuwa amemtembelea waziri uyo kwa ajili ya kumfahamisha kuwa yumo katika kinyanganyiro cha kugombea uchezaji bora wa afrika anayechezea ligi za ndani na hivyo kuomba baraka za Wizara.Pia kumpongeza Mhe. Nape kwa kuchaguliwa kuwa waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.Mbwana anategemea kujiunga na klabu ya mpira ya Genk ya Ubelgiji kwa mkataba wa miaka minne.

  • Picha na Daudi Manongi-WHUSM

Waziri asimamisha kazi maafisa biashara 2 wa Halmashauri ya Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. George Simbachawene amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kuwasimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Dodoma Bw. Elias N. Kamara na Bibi Donatila D. Vedasto (Afisa Biashara) kuanzia leo tarehe 30/12/2015 kwa kosa la kusababisha urasimu katika utoaji wa leseni za biashara.

Kutokana na hali hiyo Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kumuondoa kwenye nafasi yake Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa na Msaidizi wake na nafasi zao kukaimishwa kwa watu wengine ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizotolewa dhidi yao.

Agizo hili limetolewa na Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wafanyabiashara ambayo yalionyesha kuwepo kwa mazingira ya rushwa.

Katika uchunguzi ambao umefanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imegundulika kuwa kulikuwa na maombi ya leseni 750 ambayo yalikuwa hayajashughulikiwa bila sababu za msingi na hali hiyo ilipelekea kuikosesha Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kiasi cha shilingi Milioni 75.

Aidha, Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI ameagiza Mamlaka za Serikali kote nchini kuhakikisha wanatoa leseni za biashara bila urasimu wowote na muombaji apate leseni ndani ya siku 2 au 3 anapoomba leseni.

Mhe. Simbachawene ametoa agizo kwa Maafisa biashara wote nchini kuacha urasimu katika kutoa leseni na kujiepusha na vitendo vya rushwa.

Imetolewa na:

Rebecca Kwandu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais - TAMISEMI

30 Desemba, 2015