Aliyekuwa mtangazaji mahiri RTD, Bi. Sarah Dumba aaga dunia

Sarah Dumba
Sarah Dumba
TAARIFA iliyotufijia hivi punde toka Wilaya ya Njombe mkoani Njombe zinaarifu kua Mkuu wa Wilaya ya Njombe bi Sarah Dumba amefariki dunia hii leo aada ya kuugua ghafla.

Imefagamika kua Bi Sarah Dumba ambaye kitaaluma ni Mwandishi wa habari aliyekua Mtangazaji wa iliyokua Redio Tanzania amefikwa na umauti wakati akipatiwa matibabu Hospitalini baada ya kufikishwa hapo akilalamika kifua kumbana ghafla.

Marehemu siku ya leo alikua kazini kama kawaida akitumikia taifa hadi.muda wa jioni alipotoka na kurejea nyumbani kwa mapumziko na akiwa nyumbani hapo ndipo alipoanza kuhisi afya yake kutetereka.

"Ni kweli Mheshimiwa Sarah Dumba ametutoka, ni majonzi mazito na hadi sasa siamini lakini huo ndio ukweli kua mwenzetu amefariki majira ya saa moja usiku wa leo," kilisema chanzo chetu.

Sara Dumba amepata kuwa Mkuu wa Wilaya katika maeneo tofauti Ikiwepo Wilaya ya Kilindi na Njombe alikofikwa na mauti.

Father Kidevu blog inatoa pole kwa familia yake, Wananchi wa Njombe, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Ofisi ya Waziri Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia msiba huo mzito.

Taarifa kamili itawajia wakati wowote juu ya mipango ya mazishi.

Sarah Dumba katika picha akipeana mkono na Waziri  Mkuu mstaafu, Mizengo K. P. Pinda