Loading...
Sunday

Balozi Kijazi ateuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Balozi Mhandisi John Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Kabla ya Uteuzi huo, Mhandisi Kijazi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini India.

Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue atapangiwa kazi nyingine.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
06 Machi, 2016. 
Toggle Footer
TOP