Loading...
Friday

Balozi Rwegasira aaga dunia

Joseph Rwegasira
Joseph Rwegasira
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa inasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuanzia mwaka 1993 hadi 1995, Balozi Joseph Rwegasira (Pichani) kilichotokea tarehe 04 Machi, 2016 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Jijini Dar es Salaam.

Msiba upo nyumbani kwa Marehemu Msasani Jijini Dar es Salaam ambapo tarehe 06 Machi, 2016 mwili wa Marehemu Balozi Rwegasira utaagwa katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Peter Mbuyuni saa 8.00 mchana.

Aidha, tarehe 07 Machi, 2016 mwili wa Marehemu utasafirishwa kulekea Bukoba, Kagera kwa mazishi.

Wizara inaendelea kuwasiliana na Familia ya Marehemu ili kupata ratiba kamili ya msiba huo.

Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina.

Imetolewa na: 
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, 
Dar es Salaam
04 Machi, 2016
________________Aliyekuwa Mwenyekiti wa vyama vya wafanyakazi JUWATA, Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Pwani na baadaye balozi wa Tanzania nchini Zambia halafu akawa Waziri wa viwanda na Biashara, na baadaye waziri wa Kazi na mwisho Waziri wa mambo ya nchi za nje, Ndugu Joseph Clemence Rwegasira amefariki dunia leo saa kumi alfajiri.

Mzee Rwegasira alizaliwa tarehe 21/03/1935.

0 comments :

Post a Comment

 
Toggle Footer
TOP