Loading...
Wednesday

Dk Shein amjulia hali Maalim Seif


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amtembelea Makamu waKwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, kumjulia hali yake baada ya kupa ruhusa akiwa na Waziri Dkt. Mwinyihaji Makame, walipofika katika hoteli ya Serena Dar es Salaam. leo kumtembelea Maalim Seif kwa ajili ya kumjuilia hali. baada ya kuruhusiwa kurejea nyumbani kutoka katika hospitali ya Hindu Mandal Jijini Dar es Salaam, amesema afya yake inazidi kuimarika siku hadi siku. Dkt. Shein alifika hotelini hapo leo majira ya saa mbili usiku. (Picha na Salmin Said, OMKR)

_____________

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE

    Zanzibar                                                                                                   10 Machi, 2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amemjulia hali Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad.

Maalim Seif ambaye alikuwa amelazwa katika hospitali ya Hindu Mandal kwa siku kadhaa kwa ajili ya matibabu hivi sasa anapumzika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam baada kuruhusiwa kutoka hospitalini.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alifika hoteli ya Serena jana jioni na kumpa pole Maalim Seif na kumuomba Mwenyezi Mungu amponye haraka ili aweze kuendelea na shughuli zake kama kawaida.  

Kwa upande wake Makamu wa Kwanza wa Rais alimshukuru Dk. Shein kwa kufika kumjulia hali na kumuombea apone haraka.

Kuhusu hali yake Maalim Seif alimueleza kuwa hivi sasa anaendelea vizuri na kwamba ameshauriwa na madaktari wake apumzike kwa wiki nane.

Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822  
Toggle Footer
TOP