Gari zinazotakiwa kubandika viakisi mwanga "reflectors"Kwa Mujibu wa Kanuni ya 3(1) na (2) ya Kanuni za Viakisi Mwanga za mwaka, 2014, GN.24, Gari zifuatazo zinatakiwa kubandika viakisi mwanga.

(a) Magari yote yaliyoundwa na kujenga mahususi kwaajili ya kubeba mizigo na yenye uzitowa chini wa tani 3.5;

(b) Magari makubwa ya mizigo (HDV);

(c) Magari ya abiria na Mitambo ya Kihandisi (Engineering Plant Vehicles);

Kwa Mujibu wa kanuni ya 3(2)

Kila la gari la mizigo, gari la kazi nyepesi (light duty), gari la abiria na mitambo litabandikwa viakisi mwanga upande wa nyuma (rear); Ubavuni (sides) na mbele (front).

Kwa mujibu wa kanuni ya 4 mtu yeyote atakayekiuka maelekezo ya kanuni hizi anatenda kosa, na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi laki moja na isiyozidi shilingi laki tatu au kufungwa jela miezi sita au vyote kwa pamoja.

[These Regulations shall apply to all vehicles designed and constructed for the carriage of goods and having a minimum weight of 3.5 tones, heavy duty vehicles, public service vehicles and
engineering plant vehicles.
(2) Every heavy duty vehicle, light duty vehicle, public service vehicle and engineering plant vehicle shall be affixed with retro reflective markings on the rear, on the sides and on front]UTATA NA SULUHISHO LAKE

Ukisoma vizuri kanuni ya 3(2) ukailinganisha na ya 3(1), utagundua kuwa light duty vehicles maarufu kama vi-carry, au kirikuu, havikukusudiwa kuwekewa reflekta ubavuni kwa mujibu wa kanuni ya 3(1) kwakuwa kwanza havizidi tani 3.5.

Hata hivyo kwakuwa maelezo ya kanuni ya 3(1) yanaanza na maneno gari lolote lililoundwa na kutengenezwa kwaajili ya kubeba mizigo.....tayari virikuu vyote vinaingia hapa.

Na kanuni ya 3(2) inakuja kukandamizia kwa kuvitaja kabisa. Kanuni ya 2 inatafsiri light duty vehicles kama gari iliyochini ya tani 3.5 lakini iliyoundwa kwaajilli ya kubeba mizigo. Kwa maana hii hadi mikokoteni na bajaji za kubeba mizigo zinaingia hapa.

Tafadhali mwelimishe na mwenzio, sambaza ujumbe huu

RSA TANZANIA, USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE.