Loading...
Monday

Katibu Mkuu Kiongozi, Kijazi aapishwa na kukaribishwa ofisini


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Eng. John William Herbert Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu jijini Dar es Salaam. Balozi Kijazi anachukua nafasi ya Balozi Ombeni Sefue ambaye atapangiwa kazi nyingine.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi wakwanza kushoto na Wamwisho kulia ni aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue pamoja na viongozi Wakuu wa Ulinzi na Usalama nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali mara baada ya kuisha tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi pamoja na Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara mbalimbali mara baada ya kuisha tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.

PICHA NA IKULU.
--- RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Balozi Mhandisi John William Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Hafla ya kuapishwa Balozi Kijazi imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Makatibu wakuu na Naibu Katibu Wakuu.

Balozi Kijazi ambaye kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini India, anachukua nafasi ya Balozi Ombeni Sefue ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameagana na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) anayemaliza muda wake Bi. Joyce Mends-Cole Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine amemshukuru kwa kazi kubwa ya kuhudumia wakimbizi kwa kipindi chote alichokuwepo hapa nchini.

Kwa upande wake Bi. Joyce Mends-Cole amempongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri inayofanywa na Tanzania kuzisaidia nchi zenye matatizo, hususani migogoro ya kisiasa ambayo husababisha watu wake kuwa wakimbizi.

Pia amepongeza kuteuliwa kwa Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, kusaidia usuluhishi wa mgogoro wa Burundi ambao umesababisha idadi kubwa ya wakimbizi kukimbilia Tanzania.

Hata hivyo amesema idadi ya wakimbizi wanaokimbilia Tanzania imepungua kutoka wakimbizi 3,000 waliokuwa wakiingia hapa nchini kwa wiki, wakati Mgogoro wa Burundi ulipoanza hadi kufikia wakimbizi takribani 1,000 wanaingia hapa nchini kwa wiki hivi sasa.

Aidha, Bi. Joyce Mends-Cole amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano alioupata kwa kipindi cha miaka mitatu aliyofanya kazi hapa nchini, na ameahidi kuwa Balozi wa kuitangaza vyema Tanzania.

Gerson Msigwa.
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam

07 Machi, 2016

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Eng. John Kijazi, akisaini kitabu baada ya kuwasili Ikulu hii leo pamoja nae ni Katibu Mkuu Ikulu, Peter Ilomo

Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan, akimkaribisha Ofisini kwake, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Eng. John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es salaam leo.

Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan, akifanya mazungumzo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Eng. John Kijazi, Ofisini kwake, Ikulu Jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu Ikulu, Peter Ilomo

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Eng. John Kijazi, akitembezwa maeneo mbali mbali ya Ikulu Jijini Dar es salaam leo.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Eng. John Kijazi, akitembezwa maeneo mbali mbali ya Ikulu Jijini Dar es salaam leo.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Eng. John Kijazi, akitembezwa maeneo mbali mbali ya Ikulu Jijini Dar es salaam leo.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Eng. John Kijazi akizungumza na Baadhi ya Madereva wa Ikulu, wakati akiwa katika ziara ya kutembelea maeneo mbali mbali ya Ikulu, Jijini Dar es salaam leo.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Eng. John Kijazi, akitembezwa maeneo mbali mbali ya Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Eng. John Kijazi akiwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Eng. John Kijazi akifanya Mazungumzo na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Balozi Ombeni Sefue, Ikulu Jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu Ikulu, Peter Ilomo.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU WASIFU WA KATIBU MKUU KIONGOZI MTEULE BALOZI MHANDISI JOHN KIJAZI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Balozi Mhandisi John William Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi tarehe 6 Machi 2016, akichukua nafasi ya Balozi Ombeni Sefue.

Kabla ya uteuzi huo, Balozi Mhandisi Kijazi alikuwa mwakilishi wa Tanzania nchini India, Singapore, Sri Lanka, Bangladesh na Nepal mwenye makazi yake jijini New Delhi, India kuanzia mwaka 2007 na hivyo kumfanya kuwa Mkuu wa Mabalozi wote wanaowakilisha Tanzania nje ya nchi. Vilevile, hadi uteuzi wake, Balozi Kijazi amekuwa Mkuu wa Mabalozi wa Afrika nchini India ambaye amekuwa mtetezi mkuu wa wanafunzi wenye asili ya Kiafrika nchini India.

Kabla ya kuwa balozi, Mhandisi Kijazi alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na baadaye Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu kuanzia mwaka 2002 hadi 2006, baada ya kuteuliwa kuwa Balozi ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na hatimaye kupangiwa kituo cha New Delhi, India.

Kati ya mwaka 1996 hadi 2002, Mhandisi Kijazi alikuwa Mhandisi Mwandamizi wa Ujenzi wa Barabara ndani ya Wizara ya Ujenzi kabla ya kupandishwa cheo na kuwa Mkurugenzi wa Barabara za Mikoa ndani ya Wizara hiyo hiyo.

Balozi Mhandisi Kijazi alipata Shahada ya Sayansi ya Uhandisi wa Umma mwaka 1982 kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, na baadaye Shahada ya Uzamili katika Uhandisi wa Barabara Kuu kutoka Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza mwaka 1992.
Balozi Mhandisi John Kijazi amemuoa Fransiscar Kijazi na pamoja wamejaliwa watoto watatu, David, Emmanuel na Richard Kijazi.

Balozi Mhandisi John Kijazi ataapishwa leo tarehe 7 Machi 2016 na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu jijini Dar es salaam.

-MWISHO-

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa,
07 Machi 2016

 
Toggle Footer
TOP