Kauli ya JWTZ kuhusu taarifa na picha zinazoonesha wanajeshi wake Zanzibar

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

Simu ya Upepo   : “N G O M E”                       Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM  22150463                  Sanduku la Posta 9203,
Telex                     : 41051                              DAR ES SALAAM,  16 Mar, 2016
Tele Fax                : 2153426
Barua pepe       : [email protected]
Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kwa Umma juu ya uvumi ulioenea katika mitandao ya kijamii kuwa, limepeleka Wanajeshi wengi visiwani Zanzibar kwa ajili ya kudhibiti Usalama wakati wa kipindi hiki cha uchaguzi marudio unaotarajia kufanyika tarehe 20 Machi, 2016

Habari hizo siyo za kweli na zina lengo la kupotosha Umma. Kimsingi JWTZ linao Wanajeshi visiwani Zanzibar wakati wote kwa majukumu yake ya msingi ya Ulinzi wa nchi yetu. Hivyo hakuna Mwanajeshi yeyote aliyeongezwa zaidi ya wale waliopo visiwani humo tangu awali. Taarifa hizo zipuuzwe, zisipewe nafasi yoyote ya kujenga hofu kwa Wananchi.

JWTZ linapenda kwa mara nyingine tena kuwahakikishia Wananchi kuwa wasiwe na wasiwasi wowote kuhusu ulinzi na usalama wa nchi yetu, kwani wakati wote Jeshi lao lipo imara kuwalinda.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0784-477638