Loading...
Monday

Lady Jaydee atarajiwa kufunga ndoa mwaka huu


Harusi tunayo hatunayo? Bila shaka kwa malkia wa muziki wa bongo, Lady Jaydee, jibu ni tunayo.

Mwanamuziki huyu anayefahamika kwa vibao kama vile Yahaya, anatarajiwa kufunga pingu za maisha na kiosha roho wake wa sasa, siku kadha baada ya kutalikiana rasmi na mumewe wa zamani.

Bado taarifa kuhusu kaka aliyejinasia binti huyu ni chache lakini kulingana na uvumi, alikutana na kaka huyo baada ya uamuzi wake wa kuhamia nchini Ujerumani kuendeleza muziki wake.

Kwa mujibu wa jarida la Risasi nchini Tanzania, inadaiwa kuwa alikutana na kaka huyu baada ya kuachana na mumewe huku akitarajiwa kuanza maisha mapya nchini Ujerumani huku ndoa hiyo ikitarajiwa kufanyika mwisho wa mwaka 2016.

Jaydee na aliyekuwa mumewe walitengana baada ya madai ya ya udanganyifu, na kutokana na sababu kuwa hawakuwa wamejaliwa mtoto, ilikuwa ngumu kusuluhisha tofauti zao.
 
Toggle Footer
TOP