Lawama kwa serikali Ruvuma kwa kutokumlipa mke wa mfanyakazi aliyetoweka 2005

Benedict Mlaponi
Benedict Mlaponi
Picnani ni Benedict Mlaponi aliyekuwa mfanyakazi wa hospitali ya mkoa wa Ruvuma aliyepotea tangu tarehe13/10/2005 na mpaka wa leo, haijulikani aliko.

Mara ya mwisho aliaga kuwa anasafiri kikazi kuelekea Dar es Salaam na alipata ruhusa kutoka kwa mkuu wake wa kazi (Dk Wella kwa wakati huo), na toka wakati huo mpaka leo (mwaka 2016) hajapatikana na haijulikani kama yuko hai au amekufa.

Benedict Mlaponi ameacha watoto 5 na mke, Angetruda Milinga.

Benedict Mlaponi kazini alikokua ameajiriwa bila kujua lililompata waliandika barua ya kumfukuza kazi.  Mkewe Angetruda Milinga alifungua kesi ya mirathi baada ya kutoa ripoti polisi. Mahakama iliamuru Angetruda Milinga alipwe fedha ya mirathi, lakini serikali ya mkoa wa Ruvuma haijafanya hivyo.

Swali la mke na familia kwa watanzania ni kuwa, Benedict Mlaponi alikuwa akifanya kazi serikalini, ni kwa nini asilipwe mafao ya mirathi wakati kesi ilishapitia na kuelezwa kuwa mumewe amefariki kwa mazingira ya kutatanisha?

Ombi la mke kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kumsaidia mjane huyu