![]() |
Pichani ni mkewe Seif Shariff Hamad, Bi Awena Sinani Masoud akiwa chumba cha VIP cha uwanja wa ndege na tiketi yake ya Oman Air, muda mfupi kabla ya kuondoka |
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Shariff Hamad ameondosha familia yake katika Kisiwa cha Unguja na kuipeleka Muscat, Oman.
Familia hiyo ya Maalim Seif Shariff Hamad wameondoka jana jioni kwa kutumia ndege ya Shirika la ndege la Oman (Omar Air). Familia hiyo ya Maalim Seif imeondoka katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 5:50 jioni.
Haikuweza kufahamika mara moja sababu hasa za Makamo wa Kwanza wa Rais kuiondoa familia yake Zanzibar ambaye kwa sasa yupo katika mapumziko ya kiafya kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
- via GSengo blog