Loading...
Tuesday

Magreth Mosha anashikiliwa na polisi kwa kkutwa na vipusa vya temboPOLISI Mkoani Morogoro inamshikilia mwanamke aliyatambuliwa kwa jina la Magreth Mosha (34) mkazi wa Kibaha, mkoani Pwani kwa tuhuma ya kukutwa na vipande saba vya vipusa vya ndovu katika nyumba ya kulala wageni iliyopo katika Manispaa ya Morogoro.

Vipande hivyo vilikutwa vimeviringishwa kwenye mfuko wa salfeti na kufichwa mvunguni mwa kitanda katika chumba aliyofikia.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema hayo leo kuwa tukio hilo lilitokea Machi 28, Mwaka huu majira ya saa nane mchana eneo la mtaa wa Kingo, Manispaa ya Morogoro katika nyumba ya kulala wageni ya Miami Beach chuma namba 2 alichokuwa amepanga Magreth Mosha (34) mkazi wa Kibaha.

Kamanda Matei alisema askari Polisi kwa kushirikiana na wenzao wa TANAPA wakiwa doria walipata taarifa kutoka kwa watu wema na walipofika katika eneo la nyumba hiyo walimkamata mwanamke huyo na baada ya kufanya upekuzi katika chumba alichokodi ndipo walipomkamata na uthibitisho huo.
 
Toggle Footer
TOP